Chanzo na suluhisho la ugumba kwa wanaume

Chanzo na suluhisho la ugumba kwa wanaume
Chanzo na suluhisho la ugumba kwa wanaume

CHANZO NA SULUHISHO LA UGUMBA KWA WANAUME

Watu wengi hudhani kama mwanamke hapati ujauzito basi tatizo na lawama zote zitakuwa ni upande wa mwanamke, lakini hilo si lazima mara zote liwe hivyo. Kuna uwezekano mkubwa kuwa tatizo la kutopata mtoto katika familia likawa linatokana na ugumba upande wa mwanaume.

Visababishi vya ugumba kwa mwanaume:

Kuna sababu kuu 2 za ugumba kwa mwanaume, nazo ni mbegu chache na homoni kutokuwa sawa.

1. MBEGU CHACHE (low sperm count):

Ni moja ya kisababishi kikubwa cha ugumba kwa wanaume wengi. Ni mhimu wenza wote kufanya vipimo inapobainika wamekaa muda mrefu bila kupata mtoto. Wakati wanawake wanahitaji vipimo vingi kujua chanzo cha ugumba wao, wanaume wao wanahitaji kipimo kimoja tu nacho ni cha kujua uwingi wa mbegu na afya ya mbegu kwa ujumla (sperm analysis).

Vipo vipimo vidogo vya kawaida kwa ajili ya kupimia uwingi wa mbegu unavyoweza kuvitumia hata mwenyewe binafsi ukiwa nyumbani au unaweza kumuona daktari kwa vipimo vya jumla zaidi.

Mwanaume mwenye uwezo wa kuzalisha anahitaji kuwa na mbegu zisizopungua milioni 20, chochote chini ya hapa kinaweza kuwa sababu ya kutokutungisha ujauzito.

Ikitokea umegundulika kuwa na mbegu chache, ni nyepesi sana na hazina nguvu za kukimbia vya kutosha basi makala hii itakupa maelezo juu ya dawa za asili zinazoweza kukusaidia hilo.

Visababishi vya mbegu kuwa chache

Kuna vitu vingi vinavyoweza kusababisha tatizo la mbegu chache na ugumba kwa ujumla kwa wanaume, kwa bahati nzuri vingi ya vitu hivyo tunao uwezo wa kuvidhibiti kwa kupunguza matumizi yake.

mbegu-za-maboga

Vitu hivyo ni pamoja na:

• Vifaa vya kieletroniki – Tafiti zimeonyesha vifaa vingi vya kisasa vya kieletroniki vinasababisha kushuka kwa wingi na ubora wa mbegu kwa wanaume wengi miaka ya sasa kwani mionzi yake hupelekea joto lisilohitajika katika mifuko ya mbegu za kiume. Vifaa hivi ni pamoja na simu na Kompyuta.

Unashauriwa kutokuweka simu ndani ya mfuko wako wa suruali kwa kipindi kirefu na kutokuweka kompyuta mpakato (laptop) kwenye mapaja yako wakati wote ukiitumia. Ni mhimu pia kutokutumia masaa mengi kutwa nzima ukiwa kwenye kompyuta.

• Vifaa vya Intaneti visivyotumia waya – Siku hizi tofauti na zamani, kuna teknolojia mpya imeingia ya kuunganisha intaneti kwa kutumia vifaa visivyotumia waya (wireless internet) au kwa lugha nyepesi hujulikana kama Wi-Fi.

Vifaa hivi vinapunguza wingi wa mbegu, uwezo wa mbegu kukimbia na kuharibu muundo asili wa mbegu kwa ujumla (DNA fragmentation). Wanaume wenye tatizo la uzazi wanashauriwa kutotumia aina hii ya vifaa vya kuunganishia intaneti kwenye kompyuta zao na vile vile kutokuweka simu kwenye mifuko yao ya mbele ya suruali.

• Uvutaji wa Sigara – Uvutaji sigara, bangi na bidhaa nyingine za tumbaku huharibu ubora wa mbegu za kiume. Hilo halihitaji majadiliano. Habari njema ni kuwa madhara yaliyosababishwa na uvutaji sigara yanaweza kurekebishika ikiwa tu utaamua kuacha kuvuta. Huhitaji dawa kuacha kuvuta sigara, unahitaji kuamua tu kwamba sasa basi na hakuna lisilowezekana kwa mtu mwenye maamuzi na mwenye ndoto za maisha mazuri ya kiafya.

• Viuavijasumu na homoni katika vyakula – Viuavijasumu (pesticides) vinavyotumika katika mazao mbalimbali mashambani miaka ya sasa ni sababu mojawapo ya tatizo la homoni kutokuwa sawa kwa wanaume wengi.

Kwenye bidhaa nyingi za maziwa za viwandani sasa huongezwa homoni kama vile homoni ya estrogeni ambazo hazihitajiki katika mwili wako. Vyote hivi vina madhara katika afya ya mwanaume.

• Vyakula vyenye soya – Vyakula vyenye soya ndani yake hasa vile vya viwandani kama vile maziwa ya soya, burger za soya nk si vizuri kwa afya ya uzazi ya mwanaume. Vinasemwa moja kwa moja kuathiri ubora wa homoni ya testosterone homoni mhimu sana kwa afya ya uzazi wa mwanaume
.
• Unywaji pombe – Katika moja ya utafiti kwa wanaume wenye mbegu zenye ubora wa chini, matumizi ya kupitiliza ya unywaji pombe yalionyesha kuhusika na kupungua kwa mbegu za kawaida yaani mbegu nzuri zinazofaa kwa ajili ya uzazi.

• Matumizi ya vifaa vya plastiki – Wakati kifaa cha plastiki kinapowekewa chakula cha moto hutoa kitu kijulikanacho kama ‘xenohormones’ ambacho huigiza kama ni ‘estrogen’ ndani ya mwili na hivyo kupelekea matatizo kwenye mfumo wa uzazi wa mwanaume.

• Joto kupita kiasi (Hyperthermia) – Mifuko ya mbegu za uzazi ya mwanaume inahitaji joto la chini kidogo ya lile joto la mwili kwa ujumla ili mbegu zibaki na afya. Inasemekana kuwa hii ndiyo moja ya sababu viungo vya uzazi vya mwanaume vipo karibu nje kabisa ya mwili wake.

Joto linajulikana wazi kuharibu ubora wa mbegu na hivyo itakuwa vizuri kuepuka mazingira ambayo yanaweza kusabbaisha joto la moja kwa moja kwenye viungo vya uzazi vya mwanaume ikiwemo kuepuka kuvaa nguo za ndani zinazobana sana.

• Mfadhaiko (Stress) – Mfadhaiko au stress inaweza kuleta majanga makubwa katika homoni na kupelekea kushuka kwa uzalishaji wa mbegu za kiume.

Stress inahusika sana na tatizo la ugumba kwa wanaume wengi, na moja ya sababu ya stress hii ni ile hamu yenyewe ya kuwa na mtoto inapokujia kila mara kichwani.

Vile vile kuna presha kutoka kwa wazazi, ndugu jamaa na marafiki kwamba kwanini huzai. Hivi vyote ukiviweka kichwani na kuviwaza kila mara ni rahisi kwako kupatwa na tatizo la kupungua kwa mbegu na uzazi kwa ujumla.

Kuwa na amani, mwamini Mungu kwamba siku yako ipo, just relax kila kitu kina muda wake.

• Aina ya chakula unachokula – Chanzo kingine cha kuwa na mbegu chache au zisizokuwa na afya ni kutokula chakula sahihi na cha kutosha kila siku. Kwa afya bora kabisa ya uzazi mwanaume anahitaji vyakula vyenye madini ya zinki (zinc) kwa wingi, selenium, Vitamin E, folic acids, Vitamini B12, Vitamini C na vyakula mbalimbali vinavyoondoa sumu mwilini (antioxidants).

• Kujichua (punyeto) – Hili ni janga kubwa miongoni mwa wanaume wengi wengi karibu kote duniani. Tabia hii ukiianza huwa ni vigumu kuiacha na ni rahisi sana kugeuka kuwa teja wa punyeto. Madhara makubwa ya kujichua ni pamoja na kupungua kwa kasi kwa uwingi wa mbegu kwa mwanaume pia nguvu zake kwa ujumla na hivyo kutokuwa na uwezo wa kumpa mwanamke ujauzito.

2. USAWA WA HOMONI USIO SAWA (Hormone Imbalance):

Tatizo la homoni kutokuwa sawa si jambo linalowapata wanawake peke yao, ni jambo linalojitokeza pia kwa wanaume ingawa wengi wao huwa hawana muda wa kufikiri kuwa nalo. Homoni zina umhimu mkubwa katika kazi ya uzalishaji wa mbegu na katika afya ya uzazi wa mwanaume kwa ujumla.

Moja ya homoni kuu inayohusika na uzazi kwa mwanaume ni homoni ya testosterone. Kutokana na maisha yetu ya kisasa na baadhi ya matatizo yaliyoelezwa hapo juu upande wa uwingi wa mbegu, wanaume wengi wanajikuta katika hali hii ya kuwa na tatizo la homoni zao kutokuwa katika usawa unaohitajika kwa afya bora ya uzazi.

Vipo vitu vinavyoweza kuharibu homoni ya testerone na huanza kwa kuigiza au kijifanya vyenyewe ni estrogens (xenohormones). Estrogen ikizidi katika mwili wa mwanaume hupelekea uhanithi (uume kushindwa kusimama), kukosa hamu ya tendo la ndoa, kupungua kwa mbegu na kupungua kwa maji maji ya mbegu kwa ujumla.

Visababishi hasa vya kuharibika kwa testeroni ni pamoja na

• Vyakula vyenye soya
• Madawa yanayotumika katika mazao mashambani
• Homoni zinazoongezwa katika bidhaa za maziwa na nyama
• Vifaa au vyombo vya plastiki

BAADHI YA MITISHAMBA NA MIMEA INAYOWEZA KUTUMIKA KUTIBU TATIZO LA UGUMBA KWA WANAUME:

mbegu-za-maboga

Hii ni mitishamba na mimea ambayo imetumika na mababu na jamii nyingi duniani hata sasa katika kutibu tatizo la ugumba kwa wanaume.

Unaweza kuipata ikiwa katika mfumo wa unga au katika mfumo wa maji. Hakikisha unaipata kutoka kwa mtaalamu wa tiba asili unayemwamini kwa maelezo sahihi juu ya matumizi.

Kwa matokeo mazuri nakushauri uzitumie kwa muda wa mwezi mmoja mpaka mitatu kutegemea na hali yako ilikuwa imeshakuwa mbaya tayari kwa kiwango gani.

Mitishamba na mimea hiyo ambayo karibu yote majina yake kwa Kiswahili hakuna, ni pamoja na American Ginseng, Ashwagandha root (Withania somnifera), Epimedium ( goat weed), Fo-ti (Ho Shou Wu), Ginkgo, Goji berry, Maca root, Saw Palmetto berries Schisandra, Tribulus na Yohimbe bark.

Tafadhari usitumie dawa yoyote bila ruhusa au uangalizi wa karibu wa tabibu. Kufanya hivyo unaweza kujiongezea matatizo mengine zaidi bila mwenyewe kujua.

Kama una swali zaidi liulize hapo kwenye comment nitakujibu. Kama unahitaji hizi dawa au dozi kamili pamoja na ushauri mwingine wa kina nitafute WhatsApp +255769142586. Mimi napatikana Dar Es Salaam, ofisi yangu inaitwa VICTORIA HOME REMEDY ipo maeneo ya Buza Sigara Temeke.

Share post hii na wengine uwapendao.

Una ushuhuda wowote kama matokeo ya kutumia blog hii? Kama ndiyo toa ushuhuda wako ili uwe msaada kwa wengine, kutoa ushuhuda wako bonyeza hapa.

mbegu-za-maboga

(Imesomwa mara 3,325, Leo peke yake imesomwa mara 20)

You may also like...

783 Responses

 1. Kwani tatizo la ugumba linatibika kwa jinsia zote mbili ? Naomba jibu plz

  • fred mwafyela says:

   linatibika sabab visababishi vyake ni vyake ni vya kawaid tu mfan,uchache wa mbeg kwa mwanaume huwez kutatuliw kwa kula vyakul vinavyoongez kiwango cha mbegu

 2. Pasto Tarimo Pasto Tarimo says:

  Asanteni wote kwa aliepost na walio coment kwani nimejifunza mengi ambayoo nilikuwa siyaju nasematena asanteni sana na muwe na uscku mwema

 3. Eebwanaee! Hilo Ni bonge La Darasa! Mwenye Masikio Na asikie,,,

 4. kwahyo docta kama unaupungufu huo unatakiwa kula vya aina gani?

 5. Doctor mtu akifanya mastabation kwa mda mrefu,ikafika mahali hawezi tutenda tendo la ndoa kwa kipindi kirefu,hali hii inasaidiwaje manake ni kero!

 6. Paulo Ngomba Paulo Ngomba says:

  Asante,nimejifunza K2.

 7. Eben says:

  Ninashkuru kwa hilo pia ninaomba kujua jinsi ya kuandaa hizo mbegu za maboga.

 8. allen mkwavi says:

  asante mkuu somo zuri

 9. Farida Abasi Farida Abasi says:

  Matatizo ya ganzi kutohisi ladha ya tendo hapo vipi

 10. Mm nna mdogo wangu anatokwa maziwa (yaan chuchu zinatoa maziwa) na ana mimba na pia ana mtoto na amepimwa amekutwa ana homon nyingi lkn aktumia dawa hapon na tba mbadala ametumia kwa doctor mwaka lkn hajapona je kuna dawa tofaut ili atumie?

 11. Mm nna mdogo wangu anatokwa maziwa (yaan chuchu zinatoa maziwa) na ana mimba na pia ana mtoto na amepimwa amekutwa ana homon nyingi lkn aktumia dawa hapon na tba mbadala ametumia kwa doctor mwaka lkn hajapona je kuna dawa tofaut ili atumie?

 12. Mm nna mdogo wangu anatokwa maziwa (yaan chuchu zinatoa maziwa) na ana mimba na pia ana mtoto na amepimwa amekutwa ana homon nyingi lkn aktumia dawa hapon na tba mbadala ametumia kwa doctor mwaka lkn hajapona je kuna dawa tofaut ili atumie?

 13. Je , mke kuwa anashika ujauzito kisha baada ya wiki tatu au mwezi 1 , 2 ujauzito unaharibika ! Je , ktk Hali kama hiyo inawezekana tatizo likawa linamchango toka kwa mwanaume pia !?

  • Hapana ndugu mwanaume hahusiki katika hilo, hata hivyo zipo dawa za asili zinazoweza kuzuia ujauzito kutoka kirahisirahisi, Tuwasiliane, WhatsApp +255769142586

 14. Kwa mikoani kama arusha tutapataje huduma yako

 15. Kwa mikoani kama arusha tutapataje huduma yako

 16. Kwa mikoani kama arusha tutapataje huduma yako

 17. Kwa mikoani kama arusha tutapataje huduma yako

 18. Ni vyakula gani hutumika ili kuongeza nguvu za kiume ili kuproduce sperms kwa wingi

 19. Bei ya tiba hizo ni bei gani?

 20. Geofrey Kato Geofrey Kato says:

  Kwa wale tulioko mkoani mfano Mpanda Katavi tunaweza kupataje huduma yako?

 21. Ni dawa tosha hii

 22. Nilikutania tu…asante Joni,njema

 23. OK poaa tupoo pamoja

 24. Hamisi Mkali Hamisi Mkali says:

  Utajipimaje mwenyewe kujua mbegu zako ni ndogo

 25. Usikate tamaa kuelimisha

 26. Soya unayoiongelea ni soya beans inayouzwa soloing? Unatushauri vp wakinamama tusiwasagie watoto wa kiume soya

 27. Barikiwa Sana Docter

 28. Kweli jasiri haachi asili

 29. Marco John Marco John says:

  Je kiongozi hii dawa ukiitumia nusu ukabakisha huwezi kuja kuendelea mbeleni kama baada ya miezi 6 au 7?

 30. UTI sugu nayo aichangii tatizo hilo,?

 31. Silas Silas Silas Silas says:

  je bada ya kuacha kupiga punyeto ita chukua mda gan il kurud katka ali yko yq kawaida?

 32. Silas Silas Silas Silas says:

  je bada ya kuacha kupiga punyeto ita chukua mda gan il kurud katka ali yko yq kawaida?

 33. ivi kaka , kuna wanaume wanatokwa na vitu kama mauvimbe kwenye kwenye mapumbu ( hernie ama msipa) je mtu wa ugojwa huyo anaweza pata uwezo wa kumpa mwana mke mimba? tu saidie kaka.

 34. ivi kaka , kuna wanaume wanatokwa na vitu kama mauvimbe kwenye kwenye mapumbu ( hernie ama msipa) je mtu wa ugojwa huyo anaweza pata uwezo wa kumpa mwana mke mimba? tu saidie kaka.

 35. Umetaja mno miti ya kizungu na hali sisi tu waafrika.Mungu ameiwekea kila jamii magonjwa na miti inayowazunguka iwe tiba kwao.
  Kwa hiyo kwa Watanzania hatunabudi kutumia miti shamba kama, muhogo wa bonde,
  kilume hagona,
  pilipili dume,
  nyanya chungu,
  kasamba,
  Muungu,
  maziwa na tende,
  asali na muungu na yai.
  na dawa zingine za ngiri dume/chango.
  Pia dawa za kutoa sumu mwilini kama alovera au shibirimwitu na zingine.Tafadhali usizidishe dozi.

 36. Ninatatizo la uzaz nikupataje’

 37. Doctor nna ndugu yng ana tatizo la kutoona siku xske huu mwaka wa pill sasa utamsaidiaje

 38. Peter Mwita Peter Mwita says:

  Kweli hata huyu jamaa kakata tamaa kweli,pole sana.

 39. Peter Mwita Peter Mwita says:

  Kweli hata huyu jamaa kakata tamaa kweli,pole sana.

 40. vyakula venye soya!,ufahamu wangu mim soya ni moja ya chakula kizuri kwa afya ya mwanadam,inana protin na inadaiwa protin ya soya yazid ya ilyopo kwenye nyama..

 41. vyakula venye soya!,ufahamu wangu mim soya ni moja ya chakula kizuri kwa afya ya mwanadam,inana protin na inadaiwa protin ya soya yazid ya ilyopo kwenye nyama..

 42. vyakula venye soya!,ufahamu wangu mim soya ni moja ya chakula kizuri kwa afya ya mwanadam,inana protin na inadaiwa protin ya soya yazid ya ilyopo kwenye nyama..

 43. Mi nakufata WhatsApp Brother

 44. Mi nakufata WhatsApp Brother

 45. mmm mungu atusaidie kuepusha majanga haya amina

 46. Naskia fangas ikidum mda mref pia husababisha ugumba. Ni kwel?

 47. Naskia fangas ikidum mda mref pia husababisha ugumba. Ni kwel?

 48. Mim nnatatzo la kutokwa na jasho jingi sana ila kwa kufanya kazi ngumu au kutembea hata juani kwa mda mrefu je? huenda nitatizo kwangu

 49. Mim nnatatzo la kutokwa na jasho jingi sana ila kwa kufanya kazi ngumu au kutembea hata juani kwa mda mrefu je? huenda nitatizo kwangu

 50. Mim nnatatzo la kutokwa na jasho jingi sana ila kwa kufanya kazi ngumu au kutembea hata juani kwa mda mrefu je? huenda nitatizo kwangu

 51. Mimi nilikuwa Nina uvimbe nikayeyusha je nitajuaje kama umeisha na nitaweza kupata mtoto docta

 52. Mimi nilikuwa Nina uvimbe nikayeyusha je nitajuaje kama umeisha na nitaweza kupata mtoto docta

 53. Mimi nilikuwa Nina uvimbe nikayeyusha je nitajuaje kama umeisha na nitaweza kupata mtoto docta

  • Kama uvimbe umeisha na hospitali uliambiwa kizuizi ni uvimbe tu basi unatakiwa upate ujauzito sasa, nakushauri mfanye vipimo upya wote wawili na mme wako

 54. Hiyo Dawa ni sh, ngapi

 55. Hiyo Dawa ni sh, ngapi

 56. Anna Lingo Anna Lingo says:

  Kaka uko sehemu gani mm nipo kigambon

 57. Anna Lingo Anna Lingo says:

  Kaka uko sehemu gani mm nipo kigambon

 58. Ahsante dr uko vizuri sana ila sasa kuhusu umri wa kubeba mimba uwe gani ukiwa mdogo ni shida na ukivuka ni tabu pia mzurii ni upi?

 59. Ahsante dr uko vizuri sana ila sasa kuhusu umri wa kubeba mimba uwe gani ukiwa mdogo ni shida na ukivuka ni tabu pia mzurii ni upi?

 60. Ahsante dr uko vizuri sana ila sasa kuhusu umri wa kubeba mimba uwe gani ukiwa mdogo ni shida na ukivuka ni tabu pia mzurii ni upi?

 61. Kwahyo Dokta Kama Hutokuwa Na Stress Utakuwa Na Uwezo Wa Kutungisha Ujauzto?

 62. Kwahyo Dokta Kama Hutokuwa Na Stress Utakuwa Na Uwezo Wa Kutungisha Ujauzto?

 63. Kwahyo Dokta Kama Hutokuwa Na Stress Utakuwa Na Uwezo Wa Kutungisha Ujauzto?

 64. je Unapo Fanya Tendo Landoa Ukimalizatu Zinayeyuka Zinatoka ,JE? Tatizo liko wapi kwamwanamke au kwamwanaume kama zipo naitaji na nitazipata wapi niko nzega tabora

 65. je Unapo Fanya Tendo Landoa Ukimalizatu Zinayeyuka Zinatoka ,JE? Tatizo liko wapi kwamwanamke au kwamwanaume kama zipo naitaji na nitazipata wapi niko nzega tabora

 66. Fina Henry Fina Henry says:

  Dr sorry me niko nje ya mada et vipele fulan vyeus vinatokaga kuzunguka macho. Vipo kama sunzua tatizo au dalili za ugonjwa gan .

 67. ikopoa xana wape habar vijana wajielewe

 68. ni kwel weng wanaamin wanawake ndo huwa wanashda tu

 69. na vp kwa mwanamke km unatatizo la uvimbe kwenye mlija wa uzazi ambao unasababisha usipate mtoto. waweza kupata tiba yake?

 70. Mwanaume akiwa inapiga bao moja kisha anachoka na hawezi rudia ten mpaka baada ya siku mbili au zaidi , pia huyo siatakuwa na upungufu wa nguvu za kiume?

 71. kaka umetisha sana kwa somo lako umefundisha vizur xana kaka mung akuzidishe ufunuo zaid na maarifa zaid hongera xana

 72. Vp manii kuwa mazito xn ni kawaida au tatizo

 73. Vipi ponyeto mtu aliefanya kwa muda gani atapata hayo madhara! Na kwa nin ni ngumu kuacha!

 74. Vipi ponyeto mtu aliefanya kwa muda gani atapata hayo madhara! Na kwa nin ni ngumu kuacha!

 75. Vipi ponyeto mtu aliefanya kwa muda gani atapata hayo madhara! Na kwa nin ni ngumu kuacha!

 76. kwel unaweza kulma shamb mwaka amna mavuno

 77. asante kwa ushaur

 78. sawa ,kwan musturbation ukifanya @ mara/siku ndo inaleta madhara hayo au ?

 79. sawa ,kwan musturbation ukifanya @ mara/siku ndo inaleta madhara hayo au ?

 80. Dokta kuna ndgu yngu ana tatzo amepga punyeto zaid za miaka 7 saiv anaxma anajihc amepungukiw na nguvu afanyje

 81. Docta ee ebunielekeze jinsi ya kulefusha uume

 82. Sijaelewa swala la bangi na upungufu wa mbegu za kiume ? Pia kutumia wireless na upungufu wa mbegu za kiume

 83. Sijaelewa swala la bangi na upungufu wa mbegu za kiume ? Pia kutumia wireless na upungufu wa mbegu za kiume

 84. Je Uboo Kukosa Nguvu Inasababishwa Na Nin? Na Kuchelewa Kuanza Mapenz Kuna Madhara Gan?

 85. Je Uboo Kukosa Nguvu Inasababishwa Na Nin? Na Kuchelewa Kuanza Mapenz Kuna Madhara Gan?

 86. Asante kwa ushauri wako Dr

 87. Rrain Meena Rrain Meena says:

  Naomba Unitajie Iyo Dawa Zamiti Shamba Kwakiswahili Znaitwaje?

 88. Musa Mvungi says:

  Ni lazima mbegu za maboga ziwe zimekaushwa au hata mbich zinafaa

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *