Dawa asili 10 zinazotibu kikohozi

Dawa asili 10 zinazotibu kikohozi
Dawa asili 10 zinazotibu kikohozi

DAWA ASILI 10 ZINAZOTIBU KIKOHOZI

Kikohozi ni moja ya ugonjwa ambao huwapata watu karibu wote.

Kunapotokea kuzibika au muwasho kwenye koo lako ubongo hutambua kuwa kuna wavamizi kutoka nje na hivyo huuamrisha mwili wako kukohoa ili kuondoa hao wavamizi.

Kukohoa pia kunaweza kuwa ni matokeo ya maambukizi ya virusi, homa, kuvuta sigara au matatizo ya kiafya kama pumu, kifua kikuu na kansa ya mapafu.

Baadhi ya dalili za kikohozi ni muwasho kooni, maumivu ya kifua na msongamano mapafuni.

Badala ya kutumia dawa za viwandani kutibu kikohozi unaweza kujaribu mojawapo ya hizi dawa za asili za kikohozi ambazo zinapatikana kirahisi jikoni kwako.

Dawa asili 10 zinazotibu kikohozi:

1. BINZARI (Turmeric)

Dawa hii ya asili inao uwezo wa kutibu kikohozi hasa kikohozi kikavu.

Ongeza kijiko kidogo kimoja cha unga wa binzari ndani ya kikombe kimoja (robo lita) cha maji ya moto, ongeza ndani yake tena kijiko kidogo cha pilipili manga ya unga, nusu kijiko cha chai cha unga wa mdalasini na kijiko kidogo kimoja cha asali mbichi, koroga vizuri na unywe mchanganyiko huu wote kutwa mara moja kila siku mpaka umepona.

2. TANGAWIZI

Tangawizi ni moja ya dawa maarufu kwa kutibu kikohozi.

Tengeneza chai ukitumia tangawizi mbichi na ndani yake utumie asali na siyo sukari kwenye hii chai yako. Kunywa kikombe kimoja kutwa mara 3 kila siku mpaka umepona.

Angalizo usitumie dawa hii kama una ujauzito mchanga chini ya miezi minne na hata ukiwa na ujauzito zaidi ya miezi minne basi tumia kikombe kimoja tu kwa siku.

Unaweza pia kutengeneza juisi ya tangawizi freshi ukiongeza parachichi ndani yake na unywe kwa mtindo huo huo wa chai hapo juu.

3. LIMAU

Limau inaweza kutumika kwa namna nyingi katika kutibu kikohozi. Limau zina sifa za kuondoa maambukizi na pia limau lina vitamini mhimu ambayo hupigana na maambukizi na kukuongezea kinga ya mwili vitamini mhimu sana vitamini C.

Changanya vijiko vikubwa viwili vya maji maji ya limau na kijiko kikubwa kimoja cha asali mbichi na unywe mchanganyiko huu mara 2 kwa siku kwa siku kadhaa.

4. KITUNGUU SWAUMU

Kitunguu swaumu kina sifa ya kuua bakteria na virusi mwilini sifa ambayo inakifanya kuwa dawa bora ya kutibu kikohozi.

Menya punje 6 za kitunguu swaumu, kata vipande vidogo vidogo (chop) na uchanganye kwenye kikombe kimoja (robo lita) cha asali na uuache mchanganyiko huu kwa usiku mzima.

Kuanzia kesho yake asubuhi chukua kijiko kidogo kimoja cha mchanganyiko huu na ulambe mara 2 kwa siku mpaka upone.

5. KITUNGUU MAJI

Moja ya dawa nyingine rahisi ya kutibu kikohozi ni kitunguu maji. Unaweza kunusa tu mara kadhaa harufu ya kitunguu na ukaona mabadiliko.

Changanya kijiko kidogo kimoja cha juisi ya kitunguu maji na kijiko kidogo kimoja cha asali mbichi na unywe mara 2 kwa siku mchanganyiko huu kwa siku kadhaa.

6. MAZIWA YA MOTO NA ASALI

Maziwa ya moto na asali vinaweza kusaidia kutibu kikohozi kikavu na kupunguza maumivu ya kifua ambayo hutokeo kama matokeo ya kukohoa mfululizo kwa kipindi kirefu.

Kwa matokeo mazuri kunywa dawa hii kabla ya kwenda kulala. Changanya kijiko kikubwa kimoja cha asali mbichi ndani ya nusu kikombe (ml 125) cha maziwa ya moto na unywe kabla ya kwenda kulala kila siku.

Hii itasaidia kusafisha na kulainisha koo lako haraka.

7. PILIPILI KICHAA (Cayenne)

Pilipili kichaa (zile ndogo ndogo sana huwa kali kweli kweli) zinasaidia kupunguza maumivu ya kifua yatokanayo na kikohozi cha mfululizo kwa muda mrefu. Pia huuamsha na kuuchangamsha mwili.

Changanya robo ya kijiko cha chai cha unga wa pilipili kichaa, robo kijiko kidogo nyingine ya tangawizi ya unga, kijiko kidogo kimoja cha siki ya tufaa, kijiko kikubwa kimoja cha asali na vijiko vikubwa viwili vya maji.

Kunywa mchanganyiko huu mara 2 kwa siku kila siku mpaka umepona.

8. JUISI YA KAROTI

Karoti zina vitamini na viinilishe vingi mhimu ambavyo vinaweza kusaidia kutibu kikohozi.

Tengeneza jusi freshi ya karoti, isiwe nzito sana wala nyepesi sana, tumia asali katika juisi hii na unywe kikombe kimoja kutwa mara 2 kila siku kwa siku kadhaa mpaka umepona.

9. ZABIBU

Zabibu zinazo kazi na sifa kuu ya kuondoa makohozi na uchafu mwingine kwenye mfumo wako wa upumuwaji wa mwili. Kadri unavyoondoa haya makohozi kwenye mfumo wako ndivyo unavyopona kwa haraka kikohozi.

Unaweza kula tu zabibu kadhaa kila siku au tengeneza juisi freshi ya zabibu na unywe kikombe kimoja kutwa mara 2 kwa siku kadhaa mpaka umepona.

10. LOZI (Almonds)

Lozi zina viinilishe mhimu ambavyo husaidia kutuliza dalili za kikohozi.

Loweka lozi 6 ndani ya maji kikombe kimoja (ml 250) kwa masaa 8 mpaka 10.

Kisha zichuje na uzisage na urudishie ndani ya maji yake na uongeze kijiko kidogo kimoja cha siagi na ule mchanganyiko huu kijiko kidogo kimoja kutwa mara 3 kila siku mpaka dalili za kikohozi zimepotea.

Dawa asili hizi zinaweza kukutibu na kuondoa dalili za kikohozi bila kukuachia madhara kama ambavyo ungetumia vidonge au dawa za kizungu.

Kama dalili na ugonjwa utaendelea zaidi ya wiki 2 hata baada ya kutumia dawa hizi tafadhari muone daktari kwa uchunguzi na msaada zaidi.

Kama utahitaji hizi dawa zikiwa zimeandaliwa tayari niachie ujumbe WhatsApp +255769142586

Tafadhari SHARE post hii kwa ajili ya wengine uwapendao.

Una ushuhuda wowote kama matokeo ya kutumia blog hii? Kama ndiyo toa ushuhuda wako ili uwe msaada kwa wengine, kutoa ushuhuda wako bonyeza hapa.

Kama utahitaji hizi dawa zikiwa zimeandaliwa tayari niachie ujumbe WhatsApp +255769142586

(Imesomwa mara 1,885, Leo peke yake imesomwa mara 145)

You may also like...

523 Responses

 1. Asante dr kumbe tangawizi haifai kabisa kwa mjamzito

 2. Ahsante dr kwa tiba unazotupatia ila mm nina tatizo la mafua linanisumbua mda mrefu sana yaan haipiti wiki lazima niumwe naomba unisaidie dawa yk kuondoa hili tatizo maana sina rahafadhilipaulo.com

 3. Nurdin Cash Nurdin Cash says:

  Kwahyo dr tangawaz mm mjamzito hatkiwi kutumia

 4. Naje nikiwekaa limau na magadi nayo pia nidawa ya kikohozi???

 5. HD Mrindoko HD Mrindoko says:

  Shukrani sana kwa elimu

 6. Makame Omar Makame Omar says:

  Huduma zenu au clinic yenu inapatika sehemu gani doctor

 7. Mjamzito anaweza kutumia tangawizi?

 8. DTK mfumo wa hewa ipi inatibu hapa

 9. Asante doctor kwa dawa zisizo na gharama

 10. Neema Mongi Neema Mongi says:

  Asante sana sana mwanangu amepata dawa sasa kifua chake kinamsumbua sana has a kipindi hichi cha baridi na mtoto vipimo hivi hivi

 11. Ahsante sana doctor

 12. Mi nina rafiki yangu ana vuta sana sigara kw sk ana wez vuta ht pakti tatu katumia dawa nyingi za kujizuia kashindwa kafanyiw hd maombi nchi za nje India ya kusini kule lakin ime sindikan na amesha anza kukohoa mt kam huyu uta msaidi aje ???????

 13. Yassin Said Yassin Said says:

  Asante Allah akulipe

 14. Amen. God bless you. Haleluyaa

 15. Rifa Jafari Rifa Jafari says:

  nimeshuku docta,mungu azidikupa mawazo mingi

 16. Ally Abdul Ally Abdul says:

  Et Dr. Nilishawai kusikia ukichangaya asali na limau unaweza kuzurika nahata kupelekea kifo

 17. Tina Linusy Tina Linusy says:

  Doctor mm ninatatizo hapa kwenye kifua kunakuwa kama panawaka moto na pia shingoni kunakwangua ila sikohoi nn tatizo

 18. Ahsante dr ,ubarikiwe.

 19. Salma Laswai Salma Laswai says:

  Namba 3 umesema limao na asali mbona nasikia ukichanganya asali na limao ni sumu unakufa?

 20. Tyson Mrope Tyson Mrope says:

  Ahsante kwa somo doctor Mimi nasumbuliwa na kikohozi Mara kwa mara nilienda hospital walisema ni dalili za pumu sasa unawezaje kunisaidia

 21. tunashukuru kwa dawa leta dawa jino

 22. Asante mpendwa kwa msaada

 23. Mwenyezi Mungu na aendelee kukutunza daima

 24. Martha John Martha John says:

  asante doctor Kwa somo ila docta mi nakohowa pindi kiubaridi kinipigapo au nikisikia harufu ya jiko lamchin zilee tambi ziizimwapo naaza kukohowa .doctor waweza nisaidia tafadhar

 25. Maria Maingu Maria Maingu says:

  Da umetuelisha ubalikiwe

 26. Rajabu Ndaro Rajabu Ndaro says:

  na kuusu mafua vp Dr?

 27. Maziwa yaunga yanafaa?

 28. Viungo asilia ni muhimu na maarufu kwa afya zetu kwa kinga na tiba wala si maagizo ya wachawi wanaojiita waganga wa kienyeji wenye kuagua na kukupa masharti ya kichawi pokea maelezo kama haya

 29. Dawa hizi unaweza kupa mtoto wa mwaka mmoja?

 30. Tina Yaled Tina Yaled says:

  Mwanangu ameambiwa Ana kifua cha aleji anaweza kutumia tangawizi akapata nafuu

 31. Welldone mtaalamu hakika ya hili somo nimelipenda nami nimechukua nukuu kwa kuongeza elimu zaid kwan nimekua mwenye kujifunza hii kitu so nawezaje soma zaid toka kwako mtaalam!?

 32. hiyo dawa ni shilingi ngapi?

 33. Asante sana doctor me ndo ugonjwa unao nisumbua huo nitazitumia mojawapo

 34. Agnes Mlay Agnes Mlay says:

  Dr hizi tiba anaweza kutumia MTU anayesumbuliwa na pumu?

 35. Nipe mchanganyiko wote

 36. Hilda Twaha Hilda Twaha says:

  Asante kwa somo zuri

 37. Asante,unatusaidia sana.

 38. Lozi ni kitu gani jmn nisaidieni

 39. Ahsante kwa Kutuelimisha

 40. Je kama mtu anakichomi atumie nn

 41. Dr.mimi ninasumbuliewa sana na gesi tumboni, sikusikii kula , kiungilia kikali na kutapika. Vp matibabu yanapatika? na hii gesi husababishwa na nini?

 42. Dafaa Ali Dafaa Ali says:

  Ahsante. Ila naomba unisaidie tafazal ina maana ukiwa mja mzito matumiz ya mara kw mara yana athari

 43. Mayd Deus Mayd Deus says:

  Limau Na asali ni sumu

 44. Asante kwa ushauri wako mzuri
  Mimi nikitumia maji hasa ya baridi huwaga ninabanwa sana nakikogizi sasa je nifanyaje dct au niache kabisa kunywa maji baridi.

 45. Asantee..kwa somo Nzuri

 46. Nancy Sumary Nancy Sumary says:

  iko pw mm apo nime pend iyo ya maziw

 47. Shukran sana. Kuna siku nimebanwa na kifua usiku huku nakohoa. Nikakumbuka kitunguu maji ni dawa. Nilitafuna nikajisikia vizuri mno na usingizi nikapata.

 48. Je wenyepumu dawa Ni ipi? please (Asma)

 49. Barikiwa ndugu yangu kwa somo zuri

 50. Besta Sam Besta Sam says:

  Asante sana mpendwa

 51. Naitj sawa ilio changanywa fulu napataje 0767024677 jibu kwan nabaiy

 52. Ahsante Dr kwa ushauri bora, tena kwa bidhaa za kawaida na zinazopatikana kila pahala hapa Tz.

 53. Neema Shio Neema Shio says:

  barikiwa kwa ushauri mnzuri

 54. Hasant kwa hudum hii ya kipekee

 55. Asante kwa kutokuwa mchoyo wa Tiba . Ubarikiwe sana. Mimi huwa nakohoa km napaliwa

 56. Je inakuwaje kwa mtot WA miaka mitano doctor

 57. Shaibu Ally Shaibu Ally says:

  Mimi nnapumu na kifua nn dawayake dct

 58. Betty Msofe Betty Msofe says:

  Asante kwa elimu nzur

 59. Samahan doctor Lozi n nni?

 60. Ubarkiwe Na Mungu,mm Ninatatzo La Macho Kutokuona Mbal,ntmie Daw Gan Ya Asil Ambay Inawza Kunisaidia?

 61. Napia Asali na limao haina madhara ee!

 62. Barikiwa sana Doctor.

 63. Fadhil Ahmad Fadhil Ahmad says:

  Shukran kwa elimu.

 64. John Uisso John Uisso says:

  Asante sana Dr. Ila kuna ukwel wowote kuhusu asali na ndimu zina madhara kwenye mwili!?

 65. kazi kwako mgonjwa

 66. Amina James Amina James says:

  Je dawa ya mtu alievunjika nyoga haswa mzee ni ipi?

 67. Shuran kwa darasa la tiba

 68. Aisha Salehe Aisha Salehe says:

  Zawad kubwa umetupa asante

 69. Vizuri sana nimoja yaelimu

 70. shukran kwa darasa saafi

 71. Asante kwa elimu nzuri

 72. Kwa kweli umetupa faida jamani nikiumwa na kikoozi ni nishindwe hata dawa moja hapa uliyo tufundisha aaa jamani watu wengine hawana roho mbaya umetupa faida mungu akubariki sana amen

 73. Angel Chriss Angel Chriss says:

  Kumbe tiba tunazo wenyewe xafi xana

 74. Hapo kwenye pilipili kichaa, sijapaelewa vizur

  • 7. PILIPILI KICHAA (Cayenne)

   Pilipili kichaa (zile ndogo ndogo sana huwa kali kweli kweli) zinasaidia kupunguza maumivu ya kifua yatokanayo na kikohozi cha mfululizo kwa muda mrefu. Pia huuamsha na kuuchangamsha mwili.

   Changanya robo ya kijiko cha chai cha unga wa pilipili kichaa, robo kijiko kidogo nyingine ya tangawizi ya unga, kijiko kidogo kimoja cha siki ya tufaa, kijiko kikubwa kimoja cha asali na vijiko vikubwa viwili vya maji.

   Kunywa mchanganyiko huu mara 2 kwa siku kila siku mpaka umepona.

 75. Geofrey Jeas Geofrey Jeas says:

  Ahsante sana dokt kwa somo zuri

 76. Tangawizi +asali nidawa moja nzuri sana ndani ya siku 3 upo cool…nilijaribu nikaona matokeo.

 77. Naomba nitumie wtsp jamn hii sms,0625840360

 78. Me nimetumia lakini kokohozi kipo

 79. Dr fadhiri me kifua kinabana nitumie nini. Kama ya hivo

 80. Allah akulipe kwa hili

 81. Maria Sadiki Maria Sadiki says:

  Nimeelewa docta.ila naomba nisaidie kitu.nliwahi kuona mtu amechemsha mafuta ya kula kidogo na magadi kwa pamoja katika kijiko na kumpatia mtoto aliekuwa anakohoa.je ikoje hapo?naomba kueleweshwa kuhusu dawa hiyo.

 82. Mm huwa nakohoa sana nakoo huwsha xana na kifua kubana nyakati za jioni na asubuhi

 83. Asante umenisaidia sana

 84. Amina Juma Amina Juma says:

  YAAN MIM KUWASHWA KWENY KOO KILA SIKU NAMEZA DAWA WAPI KINAPUNGUA KINARUD TEN NAWSHWA MPAK KERO MPAK NITATUMIA

 85. Me mwanangu anakohoa sana usiku nitumie ipi ita mfaa

 86. Faudhia Ally Faudhia Ally says:

  Asante dokta kwa elimu yako

 87. Mi naitajikupunguza mwili dkt naomba nisaidi

 88. Minde Mbya Minde Mbya says:

  Ofisi iikowapi?

 89. Ney Wa Momy Ney Wa Momy says:

  Ubarikiwe sn doctr

 90. Amina James Amina James says:

  Yenyewe nimeipenda hiii,asante sana dr

 91. Dr f na mafua he Mbona yanasumbua Sana help us

 92. Edwin Mmary Edwin Mmary says:

  Aise limao na tangawizi mbichi saluti sana ni dawa za ukweli mno hazina uwongo nazikubali mno.

 93. Je na dawa ya malaria doct iko vip❓ barikiwa sana doct

 94. Mm nina tatz la kifua kinauma na mda mwingine kinaziba kinatulia na nikifanya kazi ngumu ndio maumivu yanazidi nimeenda hospital Mara kwenda sijapata Tiba ya kupona sasa nifanyaje

 95. Asante kwa kutupa somo maana kikohoz ni inshu nyumbani kwangu

 96. Asante kwa tiba za asili.

 97. Anna Kiwia Anna Kiwia says:

  Dr thanx sana matuta ya habati soda nachanganya afu nakunywa au

 98. Peter Bwire Peter Bwire says:

  Ahsante kwakutuelekeza dawa maana kikoozi niugonjwa usioepukika kwa kila mtu

 99. Eva John Eva John says:

  Asante kwa somo

 100. Dr mim na vidonda kooni nitumie nn?

 101. Ahsante doctor kwa somo Mimi nasumbuliwa sana na kifua kinakua kikavu na kina toa sauti kama ya paka alalavyo ni cha miaka mingi nme2mia dawa nyingi lakni amna afadhal tafadhal nahtaj msaada wko dk

 102. Na ngozi kuwa na MBA kali

 103. Asante kwa utalamu wako.

 104. Vicky Kweka Vicky Kweka says:

  Swaffi sana doctor

 105. Mungu akubariki kwa masomo yako tushindwe wenyewe

 106. Ubalikiwe na bwana kwa ushauri wako mzr.

 107. Asante sana doctor

 108. Shey Jonas Shey Jonas says:

  Asante kwa somo zuri

 109. Umefanya vizuri kuwapa watu elimu

 110. Hussein Mnjonjo, Tukumbukege Jasson, Tukumbukege Jasson

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *