Dawa asili 14 zinazotibu shinikizola juu la damu

Dawa asili 14 zinazotibu shinikizola juu la damu
Dawa asili 14 zinazotibu shinikizola juu la damu

DAWA ASILI 14 ZINAZOTIBU SHINIKIZO LA JUU LA DAMU:

mbegu-za-maboga

Shinikizo la juu la damu ni msukumo wa damu ulio juu kuliko inavyotakiwa kwa muda mrefu. Msukumo wa damu huhitajika mwilini ili kusambaza chakula, oksijeni na kutoa uchafu.

Shinikizo la juu la damu ni mojawapo ya magonjwa ambayo huitwa muuwaji wa taratibu (silent killer), magonjwa mengine ya namna hii ni pamoja na kisukari, ugonjwa wa moyo, kansa na virusi vya magonjwa ya ini.

Silent killers ni magonjwa ambayo wakati mwingine unaweza usione dalili zozote lakini yanaweza kupelekea kifo kama hutachukua hatua stahiki mapema.

Vitu vifuatavyo vinaweza kusababisha shinikizo la juu la damu:

• Uvutaji sigara
• Unene na uzito kupita kiasi
• Unywaji wa pombe
• Upungufu wa madini ya potassium
• Upungufu wa vitamin D
• Umri mkubwa
• Ongezeko la kemikali kwenye figo (renin)
• Kushindwa kufanyakazi kwa kichocheo kiitwacho insulin

Uanishaji wa shinikizo la damu

*Presha ya kawaida <120 <80
*Presha inayoelekea kupanda 120-139 80-89
*Presha hatua ya 1 140-159 90-99
*Presha hatua ya 2 160-179 100-109
*Presha hatua ya 3 ≥180 ≥110

Shinikizo la damu/BP ni ugonjwa unaosumbuwa watu wengi sana duniani na hii ni kutokana na kutokujuwa ni nini hasa husababisha ugonjwa huu mwilini.

Shinikizo la damu linaonekana kuwa ni ugonjwa wa kuishi kwa kufuata masharti.

Takwimu za Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) zinasema tayari watu bilioni moja duniani kote, wanaathiriwa na shinikizo la juu la damu huku likisababisha mshtuko wa moyo (Heart Attacks), kupooza na kiharusi (Strokes).

Takribani watu milioni nane hufa kila mwaka kutokana na ugonjwa huu wa kupanda kwa shinikizo la damu.

DALILI ZA SHINIKIZO LA JUU LA DAMU:

• Maumivu ya kichwa (Haswa nyuma ya kichwa mara nyingi nyakati za asubuhi)
• Kuchanganyikiwa
• Kizunguzungu
• Kelele sikioni (Mvumo au Mazomeo masikioni),
• Kutoweza kuona vizuri
• Matukio ya kuzirai
• Uchovu/kujisikia kuchokachoka
• Mapigo ya moyo kwenda haraka
• Kutokuweza kuona vizuri
• Damu kutoka puani

Uonapo dalili hizi unapaswa kuwahi hospitali kupata vipimo.

DAWA ASILI 14 ZINAZOTIBU SHINIKIZO LA JUU LA DAMU:

mbegu-za-maboga

1. MAJI YA KUNYWA

Maji ni uhai. Sababu ya kwanza ya watu wengi kupata shinikizo la juu la damu ni kutokana na ukweli kwamba hawanywi maji ya kutosha kila siku. Na wengi kama siyo wote wanasubiri kiu ndipo wanywe maji.

Kiu ni ishara ya mwili iliyochelewa kuhitaji maji, huhitaji usikie kiu ndiyo unywe maji.

Asilimia 85 za ubongo wa binadamu ni maji, wakati asilimia 94 za damu yako ni maji. Sasa kama asilimia 94 ya damu yako ni maji ina maana ubora wa damu yako unategemea unakunywa maji kiasi gani kila siku.

Hivyo ili kupona shinikizo la juu la damu kutegemea na uzito wako, hakikisha unakunywa maji kidogo kidogo kutwa nzima lita 2 mpaka 3 kila siku iendayo kwa Mungu.

Wakati huo huo utumie chumvi ya kutosha kwenye vyakula vyako hasa ile ya mawe ya baharini ambayo haijapita kiwandani. Najuwa umeambiwa chumvi ni mbaya na kuwa ni lazima ukae nayo mbali kujikinga na kupona shinikizo la juu la damu, hilo siyo kweli, ingekuwa ni kweli kwanini sasa madrip ya maji huwekwa chumvi ndani yake?.

Kama huna mazoea ya kunywa maji ya kutosha kila siku ndiyo hapo chumvi inaweza kuwa mbaya tofauti na hapo unahitaji chumvi ya kutosha kila siku.

Kwa maelezo zaidi soma post hizi zifuatazo:

*Shinikizo la juu la damu na upungufu wa maji mwilini hapa

*Maajabu ya chumvi hapa

2. KITUNGUU SWAUMU

Kitunguu swaumu kimeendelea kujipatia umaarufu katika kutibu shinikizo la juu la damu.

Kitunguu swaumu pia husaidia damu isigande mwilinini sifa ambayo ni nzuri sana kwa afya ya moyo.

Kitunguu swaumu pia ni kikojoshi cha asili (natural diuretic) na hivyo kinasaidia kuyalazimisha maji yaliyozidi mwilini pamoja na sodiamu kutoka nje ya mwili kwa kupitia mkojo ambao utauzalisha kama matokeo ya kutumia kitunguu swaumu.

Utaona unapata mkojo mara kwa mara ambao ni msafi mweupe, tendo hili husaidia kudhibiti shinikizo la juu la damu na wakati huo huo kuupa utulivu moyo wako kwa ujumla.

Jinsi ya kutumia:

1. Chukuwa kitunguu swaumu kimoja
2. Kigawanyishe katika punje punje
3. Chukua punje 6
4. Menya punje moja baada ya nyingine
5. Kisha vikatekate (chop) vipande vidogo vidogo sana na kisu na uache hivyo katika hewa kwa dakika 10
6. Meza kama unavyomeza dawa na maji nusu lita kila unapoenda kulala.

Namna nyingine nzuri zaidi ni kuviweka ndani ya kikombe kimoja (robo lita) cha mtindi freshi koroga vizuri na unywe na hii itakusaidia kupunguza harufu mbaya ya kitunguu swaumu huku ukipata faida nyingine nyingi mhimu zilizomo kwenye mtindi.

Soma magonjwa mengine zaidi ya 30 ambayo unaweza kujitibu kwa kutumia kitunguu swaumu kwa kubonyeza hapa

3. KAROTI

Karoti ina sifa kuu ya kuondoa sumu mwilini, pia ina vitamini A na vitamini C. Vitu hivi vya asili vinavyoondoa sumu mwilini hupunguza mwilini vitu vinavyosababisha kutokea kansa pia hulinda mishipa ya damu isidhurike na kupunguza kufa kwa seli.

Karoti pia zina kiasi kingi cha elektrolaiti na potasiamu. Potasiamu ni madini mhimu kwa ajili ya kuweka sawa usawa wa maji mwilini na hivyo kuweka sawa shinikizo la damu.

Potasiamu huziweka chini ya ulinzi hasara zinazoweza kuletwa na sodiamu mwilini.

Jinsi ya kutumia: Kunywa glasi 1 (robo lita) ya juisi ya karoti asubuhi na nyingine 1 jioni kila siku bila kuongeza sukari ndani yake.

mbegu-za-maboga

4. NYANYA

Nyanya zina beta-carotene, vitamini E, potasiam, na huondoa sumu pia mwilini, vitu vyote hivi ni mhimu katika kushusha shinikizo la juu la damu.

Nyanya pia zina kitu kinaitwa ‘lycopene’, hii ni kemikali ambayo huipa nyanya rangi nyekundu na ambayo ndiyo husaidia kuondoa kolesto mbaya mwilini na kuzuia mafuta kujijenga kwenye mishipa ya damu.

Mafuta haya yanayojijenga kwenye mishipa ndiyo pia husababisha magonjwa ya moyo.

Namna ya kutumia: Kula kikombe kimoja cha nyanya fresh kila siku, au tumia kikombe kimoja cha juisi ya nyanya kila siku.

Epuka juisi au nyanya za dukani.

Soma hii, Faida 7 za juisi ya nyanya hapa

5. KOMAMANGA (Pomegranate)

Komamanaga siyo tu zina viinilishe vingi mhimu bali pia zina kazi mhimu ya kuondoa sumu mwilini. Komamanga ni matunda yenye gamba gumu na juisi inayotokana na mbegu zake ndiyo hutumika kama dawa.

Komamanga zina vitu vitatu mhimu navyo ni ‘phytochemicals’ ambacho huondoa sumu mwilini na kuzuia seli zisizulike kirahisi, kitu cha pili na cha tatu vilivyomo kwenye komamanga ni ‘polyphenols’ na ‘punicalagin’ ambavyo hivi hupigana dhidi ya magonjwa ya moyo, kuweka sawa kolesto, kushusha shinikizo la juu la damu, kuzuia mishipa isizibe na kansa.

Komamanga zina uwezo mkubwa wa kuondoa sumu mwilini kuliko hata mvinyo mwekundu (red wine) au zaidi hata ya chai ya kijani (green tea).

Namna ya kutumia: Kunywa kikombe kimoja cha juisi ya mbegu za komamanga kutwa mara 2 asubuhi na jioni kila siku.

Au ongeza mbegu za komamanga kwenye kachumbari (salad) yako kila siku.

6. MAFUTA YA UFUTA (Sesame)

Mafuta yatokanayo na ufuta yana omega 6, vitamini E, na kiinilishe kingine kijulikanacho kama ‘sesamin’ ambacho chenyewe ndiyo huhusika moja kwa moja na kushusha shinikizo la juu la damu, magonjwa ya moyo na kisukari.

Namna ya kutumia: Fanya mafuta ya ufuta kuwa ndiyo mafuta ya kupikia vyakula vyako unavyokula kila siku na ndani ya mwezi mmoja mpaka miwili hivi utaona hata shinikizo lako la juu lipo sawa.

7. TANGAWIZI

Kwa karne nyingi tangawizi imetumika na watu wa India na bara la Asia kwa ujumla kama dawa ya kutibu shinikizo la juu la damu. Tangawizi pia hutumika kushusha kolesto na kuzuia damu isigande.

Shinikizo la juu la damu ni matokeo ya damu kutokupita kwa uhuru wote kwenye mishipa ya damu, kama tangawizi ina uwezo wa kuzuia damu isigande ni wazi ni nzuri kwa mtu mwenye shinikizo la damu.

Tangawizi pia huzuia mshtuko au kukamaa kwa mishipa na shambulio la moyo.

Namna ya kutumia: Tumia juisi ya tangawizi kikombe kimoja kutwa mara 2 asubuhi na jioni.

Namna inavyoandaliwa hii juisi; tangawizi mbichi za ukubwa wa kati nne, parachichi moja na asali mbichi vijiko vikubwa saba na na maji lita moja na nusu.

Unaweza kutengeneza nyingi zaidi na kuihifadhi katika friji, mhimu hapo ni tangawizi. Tumia blenda kutengeneza hi juisi.

Ongeza pia tangawizi kwenye vyakula vingi unavyopika kila siku.

8. MAJI YA NAZI (dafu)

Maji ya nazi yana potasiam na magnesium vitu viwili mhimu kwa mishipa ya moyo.

Maji ya nazi hufanya kazi kama vile dawa za kukojosha (diuretic) kwa kuyalazimisha maji yaliyozidi mwilini kutoka nje huku yakisaidia kushikilia ndani ya mwili madini mhimu ya potasiamu.

Maji ya nazi ni mazuri kama ni freshi na siyo yawe yametengenezwa na kuuzwa dukani tena.

Namna ya kutumia: Kunywa glasi moja (ml 250) za maji ya nazi kutwa mara 3. Ukiacha kushusha shinikizo la juu la damu maji haya husaidia pia kushusha uzito.

9. ILIKI (Cardamom)

Iliki ni kiungo (spice) ambacho kimekuwa kikitumika katika dawa za asili za kihindi kwa maelfu ya miaka mingi sasa. Inatumika zaidi kwa matatizo ya moyo, matatizo ya tumbo, matatizo ya kibofu cha mkojo, kiungulia na matatizo mengi katika mfumo wa upumuwaji.

Iliki ina sifa nyingi ikiwemo ya kuondoa sumu, kuondoa bakteria na kansa.

Iliki husaidia kutanuka kwa mishipa ya damu na hivyo kuruhusu damu kupita kirahisi zaidi na hivyo kupunguza shinikizo la juu la damu kwa asili kabisa bila madhara mengine mabaya.

Namna ya kutumia: Changanya kijiko kidogo kimoja cha chai cha iliki ya unga katika maji ya uvuguvugu glasi 1 ongeza asali kidogo kupata radha koroga vizuri na unywe yote.

Fanya hivi kutwa mara 2 asubuhi na jioni kila siku.

10. BIZARI (Turmeric)

Bizari ndiyo kiungo au dawa ya asili pekee ambayo inafuatiliwa na kusomwa na watu wengi zaidi duniani.

Inajulikana kwa uwezo wake wa kuondoa maambukizi karibu katika kila sehemu ya mwili. Kwa kuondoa maambukizi, bizari huuongezea nguvu msukumo wa damu na kazi za moyo kwa ujumla.

Bizari inaweza kusaidia pia kuondoa takataka zinazojijenga kwenye kuta za mishipa, pia ni dawa ya asili ya kufanya damu isigande mwilini kama matokeo yake huweka sawa shinikizo la juu la damu.

Namna ya kutumia: Ongeza kijiko kidogo kimoja cha bizari ya unga kwenye glasi 1 ya maji ya uvuguvugu, ongeza tangawizi kidogo na asali kidogo kupata radha, koroga vizuri na unywe yote kutwa mara 2 kila siku. Ongeza pia bizari kwenye vyakula vyako vingi unavyopika.

11. VYAKULA VYENYE OMEGA 3

Vyakula au kingine chochote chenye Omega 3 husaidia sana kuweka sawa shinikizo la juu la damu na kolesto pia. Unahitaji kutumia vyakula vyenye omega 3 kila siku iendayo kwa Mungu kama unasumbuliwa na shinikizo la juu la damu.

Vyanzo vizuri vya omega 3 ni mafuta ya samaki au samaki wenyewe, mayai (mayai ya kienyeji), parachichi, spinachi, mbegu za maboga au mafuta yake, pia mafuta ya asili ya nazi.

Kunywa kijiko kikubwa kimoja cha mafuta ya asili ya nazi kutwa mara 2 kila siku ili kuweka sawa shinikizo lako la damu.

Tafuta pia vyakula vingine vyenye omega 3 na upendelee kuvitumia hivyo kila mara.

12. VITAMINI D

Vitamini D hupatikana kirahisi katika miale ya jua, na hii ndiyo vitamini inayohusika na udhibiti wa jeni (genes) zaidi ya 200 mwilini.

Vitamini hii pia inahusika na usitawi na ukuwaji sahihi wa seli za mwili.

Kwa kawaida asilimia 50 mpaka 90 za vitamini D hupatikana kwa mwili kutoka kwenye jua moja kwa moja.

Pamoja na jua tunatakiwa pia kutumia vyakula vyenye vitamini D kwa wingi tunaposhambuliwa na shinikizo la juu la damu.

Viatmini D inapatikana kirahisi katika mayai, samaki, na katika nyama pia.

Maisha ya kisasa yanapelekea watu wengi kuwa ndani ya ofisi karibu kutwa nzima na hivyo kuwapelekea kukosa mwanga wa jua moja kwa moja.

Upungufu wa vitamini D mwilini ni tatizo linaloendelea kuongezeka kila siku duniani.

Upungufu wa vitamini D unaweza kusababisha matatizo kama shinikizo la juu la damu na magonjwa mengine kadhaa ikiwemo matatizo ya akili, kansa, kushuka kinga ya mwili na matatizo mengine yanayohusiana na uzazi.

Katika utafiti mmoja mwaka 2014 iligundulika kuwa vitamini D husaidia kushusha shinikizo la juu la damu. Vitamini D huidhibiti homoni ya ‘renin’ na kuleta matokeo sawa na yanayoletwa na homoni nyingine ya ‘angiotensini’.

Dawa sawa zinazodhibiti kazi za rennin na angiotensin hutolewa kwa wagonjwa wenye shinikizo la juu la damu.

Tembea kwenye jua lisaa limoja kila siku iendayo kwa Mungu ukiwa hujavaa nguo nyingi ili jua liweze kukufikia kila sehemu ya mwili wako.

13. PUMZIKA (Relax) na USIKILIZE MUZIKI UUPENDAO

Jambo moja la kushangaza ni kuwa kuna uhusiano wa moja kwa moja wa msongo wa mawazo (stress) na shinikizo la juu la damu.

Na mara nyingi nimesema stress inaweza kukuletea magonjwa mengine mwilini zaidi ya 50 ikiwemo shinikizo la juu la damu.

Muziki unao matokeo ya kukupa pumziko na kukuletea utulivu wa akili na nafsi.

Sikiliza muziki uupendao kama ni wa kidunia au wa kiMungu ni sawa mhimu ukuletee utulivu unaohitaji.

Aina ya muziki ni jambo la mhimu pia, usiwe muziki wa kukuongezea mawazo au shida nyingine tena bali ni ule mzuri mtulivu wenye kuiweka akili yako sawa na siyo wa kukuletea hamasa ya mipasho mingine tena.

Kusikiliza muziki mzuri kwa dakika 30 tu kwa siku kunaweza kusaidia kushusha shinikizo lako la damu, kushusha mapigo ya moyo na kupunguza hamaki (panic).

Muziki unaosemwa kusaidia kushusha shinikizo la juu la damu ni ule unajulikana kwa kiingereza kama ‘slower tempo classical music’, utafute kwenye google au youtube.

Miziki hii ifuatayo inaongeza presha nayo ni rap (ya kufokafoka), pop, jazz, na rock .

Tenga muda kila siku usikilize muziki uupendao.

14. MAZOEZI YA VIUNGO

Uzito wako unapokuwa juu unaongeza shida zingine kwenye kuta zako za mishipa ya damu na kuulazimisha moyo wako kufanya kazi kwa shida masaa 24 siku 7 za wiki.

Uzito uliozidi pia unakuweka katika hatari ya kupatwa na magonjwa mengine kama matatizo mbalimbali ya mishipa ambayo yanaweza kupelekea shinikizo la juu la damu, shambulio la moyo na kiharusi (stroke).

Maisha ya kukaa tu kwenye kiti masaa yote yanapelekea hatari ya kupatwa na shinikizo la juu la damu kwa zaidi ya asilimia 30. Kutembea kwa miguu mwendo kasi kidogo lisaa limoja kila siku ndiyo zoezi mhimu kuliko yote unaloweza kulifanya kwa ajili ya afya ya mwili wako.

Tafiti zinaonyesha kutembea kwa miguu saa moja kila siku bila kupumzika (none stop) au kukimbia mdogo mdogo (jogging) kila siku kunasaidia sana kuweka sawa shinikizo la juu la damu pia husaidia kupata usingizi mzuri na mtulivu.

MHIMU SANA:

Ni mhimu kuhakikisha kuwa unaliweka katika hali ya usawa shinikizo lako la damu. Kwa bahati mbaya hakuna njia ya mkato ya kulitekeleza hilo wala hakuna dawa ya kukuponya ndani ya siku 2.

Elewa kuwa dawa hizi za asili haziwezi kukuletea maajabu yoyote kama haubadili mfumo wako wa kuishi ikiwemo vyakula au vinywaji au jinsi unavyouweka mwili wako kila siku.

Lishe bora na mazoezi ya nguvu ya kila siku ni mhimu katika kutibu shinikizo la juu la damu.

Mambo 11 mhimu ya kuzingatia unapokuwa na shinikizo la juu la damu:

mbegu-za-maboga

1. Ongeza kiasi cha unywaji maji na chumvi kila siku
2. Kula nyama isiyo na mafuta mengi
3. Ongeza kula vyakula visivyokobolewa
4. Kula zaidi matunda, mboga za majani, karanga na maharage
5. Punguza vyakula vya viwandani vinavyoongezwa sukari nyingi
6. Punguza vyakula vyenye lehemu au kolesteroli nyingi
7. Acha kuvuta sigara na tumbaku za aina zote
8. Acha kunywa pombe
9. Dhibiti uzito wako, hakikisha una uzito unaopaswa kuwa nao kwa mjibu wa urefu wako
10. Punguza mfadhaiko au stress
11. Fanya mazoezi ya viungo hasa mazoezi ya kukimbia kila siku na kama kukimbia kimbia huwezi basi kutembea kwa miguu masaa mawili kwa siku inatosha kabisa.

Ikiwa utahitaji dawa za asili au dawa lishe za asili kwa ajili ya shinikizo la juu la damu, niachie tu ujumbe kwenye WhatsApp +255769142586.

Tafadhali SHARE post hii kwa ajili ya uwapendao.

Una ushuhuda wowote kama matokeo ya kutumia blog hii? Kama ndiyo toa ushuhuda wako ili uwe msaada kwa wengine, kutoa ushuhuda wako bonyeza hapa.

mbegu-za-maboga

(Imesomwa mara 2,415, Leo peke yake imesomwa mara 36)

You may also like...

243 Responses

 1. Doctor samahani Najua nitakua nimetoka nje ya mada kuna madhala gani kwa mama mjazito kukosa chooo kwa Mda mrefu

 2. Aksante Saaana Mtaalam!! Mungu Akupe Moyo Wa Huruma Zaidi!!

 3. tumekupata Doctor wetu unatuokoa kwenye mambo meng sana mung akujaalie afya njema

 4. Glory Thomas Glory Thomas says:

  Asant san kwa somo zuri Mungu azidi kukubariki

 5. Tunashukuru sana kwa kujitoa kwetu

 6. Melcl Coltd Melcl Coltd says:

  Ok dr je? Kabeji na kitunguu maji na limao haizadii pia?

 7. Doctor ubarikiwe kwa huu ujumbe

 8. Juma Shabani Juma Shabani says:

  Samahan Dkt Ivi Mama Mjamzito Inafaa Kufanya Ata Mazoz Ya Kutembea Au Kupumzikaa 2 Kuuliza Si Ujinga

  • Ni lazima afanye mazoezi, kukaa tu ni haraei hata kwa afya ya mtoto tumboni. Anaweza kutembea kwa miguu dakika 30 mpaka 40 kila siku na mengine ya viungo ya kumnyooshanyoosha unaweza kumsaidia

 9. Chards Mmari Chards Mmari says:

  Ahsante sana kiongozi

 10. doctor nina tatizo, huwa nasikia kelele masikioni lakini nimepima shinikizo la damu daktari nipo sawa, nifanyeje ili kelele ziishe?

 11. NOndo zako huwa zimejaa kisawasawa! big up…

 12. Joan John Joan John says:

  Asante sana mtumishi kwa helimu unayotupa kila leo. Ila naomba unisaidie nina tatizo la kupata ganzi na sina pressure ila nna vidonda vya tumbo je naweza tumia kitu gani mbali na dawa za hospital kuondoa ganzi? Ntashukuru Mtumishi

  • Pole sana ndugu yangu, ganzi mara nyingi ni ishara ya sumu kujijenga mwilini. Hapo nakushauri ujitibie kwanza vidonda vya tumbo. Tuwasiliane WhatsApp +255769142586

 13. Mungu akupe maisha marefu

 14. Mungu Akuongeze Elimu Ya Kuwasaidia Wanyonge

 15. Maria Joseph Maria Joseph says:

  Ubarikiwe dr nimejifunza mengi na baadhi ya dalili huwa nazihisi

 16. Doctor asante kwa post yako! Swali: mwanaume/mwanamke mwenye shininiko la juu la damu (hy blood pressure) inawezekana akashindwa kushiriki tendo la ndoa kwa ufasaha? Au hakuna uhusiano wowote kati ya ugonjwa huo na ushiriki wa tendo la ndoa!!?

 17. Mi nitaipata wap hiyo dawa dockta

 18. Ubarikiwe kwa kuokoa afya zetu

 19. Sesilia Kiza Sesilia Kiza says:

  As ante kwakutuelimisha mungu akubariki


 20. Wani lavu♥
  (Add mee)🆗

  #No_swagger_Team
  By :Take 👊

 21. Muddy Mdoe Muddy Mdoe says:

  Habar za kazi kiongozi, me nna tatizo la kupata maumivu kwenye moyo lakini hapo awali nlikua nimesumbuliwa sana na tatzo la mkojo wa njano na tumbo kupata joto kali lakini kwa sasa tumbo limeacha ila mkojo bado kidogo naomba msaada kwa hilo maana huu moyo ndo unanipa wakati mgumu?

 22. nafanyaje ili nijue uzito wangu na urefu uko sawa?

 23. Docta mim Nina tatizo siwezi kuangalia juani zaidi ya dakika tano!kichwakinauma !!napia kilanikimaliza kula nabanja!!je!hilinitatizo gani?

 24. Nashkru ndg yangu kwa jarida lako zuri mungu akujarie sana.

 25. Omadwa MJ Omadwa MJ says:

  Kwa kweli unatusaidia sana kutuelimisha juu ya utumiaji wa mahitaji ya mwili na pia jinsi ya kujikinga na maradhi yanayo sumbua kila kukicha miongoni mwetu sisi Binadamu ast sana, Barikiwa

 26. Joyce Hamisi Joyce Hamisi says:

  Mi nampenda cna dk @fadhil paulo anaweka maelezo ya ugonjwa ya kutosha, Anatoa tiba asili na maelekezo yake vizuri cna labda ukitaka kujua zaid ndio atakuambia umtafute na anajibu coment vizuri sio wengine wako ki biashara zaid ukiuliza unajibiwa fika kituoni kwetu Big up kaka unasaidia sana Mungu azidi kukupa hekima na maisha marefu

 27. Asante doctor huwa nakuelewa sana ;be blessed

 28. Daa Ahsante Kwa Sana Kwa Kutujuza Mambo Makubwa Sanaaa.

 29. Mipia nahitaji dawa tatizo ninalo miaka miaka mingi nitazipataje

 30. Ubarikiwe sana .Mungu azidi kukuongezea maarifa ili uwasaidie na wengine

 31. Dr Samahani Mimi Huwa Miguu Yangu Inakuwa Ya Baridi Sana Je Tatizo Ni Nn Na Tiba Yake Ni Ipi?

 32. Asante doctor.Sina tatizo lkn nimefurahi kwa elimu yako unayotupa.Mungu akubariki.

 33. Rehema Saidi Rehema Saidi says:

  Ahsant kwa matibabu na ushauri

 34. Leo nimeshiba haswa ila kinachonipa shida maelezo ni mengi pia ni marefu sana nami nataka nifuatilie kwa umakini utanisaidiaje haswa juisi ya komamanga

 35. Asante kwa somo zur dkt bt naomba kuuliza inatakiwa kutumia vtu vyote Au kimoja wapo ? Mfano kwa siku unatumia juice ya tangawizi na ya bizar ?

 36. Jamani mimi nataka tu kupungua nifanyaje docta

 37. Asant sana Dk.lkn nlikuj inbo ujanjib

 38. Neema Tarimo Neema Tarimo says:

  Dr.ile juice ya tangawizi bado mwanangu anaendelea nayo hivi anatakiwa anywe kwa muda gani

 39. Ahsante sn Dr,unatusaidia na kutuokoa sana kwa post zk.Mungu akujalie maisha marefu!

 40. Aseee uko vizur Dr nimekubar

 41. SAWA,NAOMBA KUJUA DAWA YA KUONDOA UVIMBE WENYE MAUMIVU MAKALI ULIOTOKANA NA KAMA VIJIPELE VIDOGOVIDOGO VINATOKEA MUDA MWINGINE VINAWEZA KUWA VINNE AU VITATU ,ALAFU VINASAMBAA VINATENGENEZA NUNDU MOJA YENYE MAUMIVU MAKALI ,JE NAWEZA KUPATA DAWA YA KUONDOA HIYO SUMU MWILINI??

 42. UNANITAMANISHA KINIMA

 43. UNANITAMANISHA KINOMA

 44. Rabia Luongo Rabia Luongo says:

  Asante kwa elimu

 45. Mary Patel Mary Patel says:

  Asante sana Mungu akubariki

 46. Brian Didas Brian Didas says:

  Nashukuru sana ndugu kwa elimu ya bure ya afya unayotupa

 47. Sangu DS Sangu DS says:

  hii ni dawa zaidi ya mwa-arobaini kwa kuwa imeandikwa zaidi kuliko nyinginezo ktk vitabu vitakatifu

 48. Happy Naiman Happy Naiman says:

  Asante kwa darasa,ubarikiwe

 49. Barikiwa doctor kwa elimu nzuri na muhimu

 50. Martin Yuda Martin Yuda says:

  Asant sana best kwa elim ulio nipa nimepata tiba tosha

 51. Asante ninatatizo LA bp ya juu nifanyaje iliiishe kabisa

 52. Asante sana ndugu yangu nimeelimika vya kutosha

 53. Prisca Siame Prisca Siame says:

  Asante doctor kwa kutupa elimu nzr

 54. Edith Hiza Edith Hiza says:

  Asantee sana umeniokoa

 55. Lucy Mapunda Lucy Mapunda says:

  Je Dawa za shinikizo la chini la damu nazo zipo.

 56. Asante sn nimekuelewa

 57. Hongera kwa kutujuza Tiba rafiki

 58. Dr ubarikiwe sana kwani tatizo hill ninalo nimesoma maelekezo yako nimefarijika sana

 59. Nashukru sana dr Mungu axidi kukupa hekima ya kutusaidia waja wake mimi nina bp ya kupanda na kisukari cha kupanda umenisaidia sana ka mafunfisho yako ya kutumia tiba asilia. Asante sana

 60. asante docter Mimi Nina tatizo la seli seli zangu za kinga hazina nguvu za kuzuwiya marazi kuwa naumwa sana na mwili na modular inauma sana naomba ushauri docter tafazali

 61. Asante sana kwakutukumbusha jinsi ya kujiweka sawa

 62. doctor mm nina tatizo la moyo kwenda mbio sana ni miez sita sasa hata kaz nashindwa kufanya nisaidie plz

 63. vilevile kuna shida ya shinikizo la chini la damu na shida nyingine ni kutanuka kwa moyo ( MOYO KUWA MKUBWA) je tiba hizi ulizo elekeza zinaweza kutibu maradhi yote hayo na pia kuna mafuta kujaa ktk moyo

 64. Dr mm ttz langu kubwa sn inafikia kipindi moyo uwa unanienda mbio km vl mtu nilie amshwa usingizini kwa kushituriwa sasa sijajua ttz nn na moyo unakua unanivuta sn mpaka inafikia macho kutoona vzr Dr

 65. Eva John Eva John says:

  asante sana,doc!

 66. Ukiwa na shinikizo la damu je unaweza kunywa red wine white wine au bia?

 67. Mungu akulinde xana

 68. Jack Mremi Jack Mremi says:

  Yaani mpaka rahaaa, hata aliye jua atajua, ubarikiwe mnoo dk, umejitahidi kuandika kiswahili ili aliyesoma na asiye soma aweze kujua, Mungu zaidi kukupatia maisha marefu ili ukoe maisha ya watu wake kwa wingi, AMENIIIIIIIIIIIIIIIIIIII

 69. Zai Rajabu Zai Rajabu says:

  Asante sana dk yn hapo umeshanitib tayar

 70. Mwenyezi Mungu akubariki Doctor wetu ili uendelee kutuelimisha ubarikiwe sana

 71. Asante sana Dr. Ila mimi ni tatizo la mapigo ya moyo kupanda na kushuka unaweza kuamka asubuhi mapigo yako juu baada ya muda mfupi ukipima tena yako chini kabisa na bila kumeza dawa je nifanyeje Dr.?

 72. Saidi Juma Saidi Juma says:

  Asante kwa elimu hii

 73. Asante sana.Mimi nina vidonda vya tumbo na nimesikia kitunguu saumu na mtindi ni dawa je ni kweli? Ni mtu alinishauri lkn sijatumia bado

 74. Daa Nikweli Hiz Zoteni Dawaa Maana Hiz Zote Siko Na Watu Wanakula Kama Kukumanga,nanyingnez Nying Porin Zimejazana .

 75. kabla sijalala mm huwa nameza vitunguu swaumu kweli vinasaidia mno na nilishazoea mno pia vinatibu kikohozi na mafua

 76. Daudi Msangi Daudi Msangi says:

  Shukrani kwa tiba mbadala

 77. Editha Deus Editha Deus says:

  Mungu akubariki sana, ata siku nyingine hutufundishe zaid

 78. Barikiwa Sana Dokta

 79. Recho Fanuel Recho Fanuel says:

  Mamaangu. Anasumburewa xna na presha

 80. Asante sana kwa ushauri wako

 81. Doctor Nina tatizo nikilala chali na sikia chini ya kitovu tumbo linauma hata nikiinama alafu mguu inaisha nguvu halafu vitu kama vinachomachoma

 82. Onorata Mdee Onorata Mdee says:

  Ubarikiwe na Mbariki wa wote

 83. Naomi Msama Naomi Msama says:

  Asante sana nitafanya hivi Dr

 84. Kassi Amnaay Kassi Amnaay says:

  Hakika mimea na maji ni dawa

 85. du axante dk koz nami nmeanza iyo k2 mwaka jana

 86. Nimekuwa nikiishiwa nguvu nakuchokasana, naninasikia njaa kilamda,namiguu inaniwamoto. Nikipima naambiwa vidonda vyatumbo. Naomba kujua docta vidonda vinaweza kunisababishia hali hii. Nachanganyikiwa.

 87. Bnjh.jkkmkmmnbkllkklllkmnn vjh

 88. Asante sana Mungu akubariki sana

 89. Rose Kiwale Rose Kiwale says:

  Asante kwa somo zuri.

 90. Samahani mama yangu ana matatizo moyo umetanuka bandama limevimba pia pressure na vidonda vya tumbo nifanyeje? Nipo mbeya

 91. Debora Msuya Debora Msuya says:

  Asante doctor,ila samahan naomba msaada wa jinsi ya kutibu vidonda vya tumbo

 92. Mung akubariki endelea kutujuza zaidi kuhusu shinikizo la juu la damu maana wengi tumeshakumbwa

 93. Naomi Msama Naomi Msama says:

  Naomba kujua hii ya tangawizi inachujwa au unapiga na machicha yake?

 94. Enezael Urio Enezael Urio says:

  Asante sana dor Mungu akubariki

 95. Muheshimiwa mtarajiwa ninashukuru kwatiba,mimi nimiongo ni mwa wahanga wakubwa wa shinikizo ladamu yani presha yakupanda

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *