Dawa mbadala 10 zinazotibu kufunga choo au choo kigumu

DAWA MBADALA 10 ZINAZOTIBU KUFUNGA CHOO AU CHOO KIGUMU

Tatizo la kufunga choo au kupata choo kigumu ni jambo tunalolikwepa kwenye mazungumzo yetu ya kila siku. Hata hivyo ni tatizo kubwa katika jamii na mbaya zaidi wengi hawajuwi madhara yake ni nini ya kuendelea kulivumilia tatizo hili.

mbegu-za-maboga

Kupata choo kigumu au kufunga choo ni ishara ya tatizo lingine baya zaidi mwilini. Kama kuna jambo unapaswa uliepuke kwa nguvu zote basi ni hili. Kwa afya bora kabisa hakikisha unapata choo kila siku mara 2 hata mara 3. Choo kilaini siyo kigumu na chenye maumivu.

Wakati mwingine utakapopata tatizo hili naomba usiwe na aibu kulisema wazi hata kwa boss wako ili upate matibabu kwa haraka.

Kufunga choo au kupata choo kigumu ndiyo CHANZO KIKUU CHA UGONJWA WA BAWASIRI kwa waTanzania wengi na hii inachangiwa kwa sehemu kubwa kwa kula ugali wa sembe na kutokunywa maji mengi kila siku.

Pamoja na hayo, hakuna ugonjwa rahisi kutibika kama huu ikiwa utaamua kushughulisha kichwa chako kidogo hasa kwa kuangalia unakula na kunywa nini kila siku.

Dawa mbadala 10 zinazotibu kufunga choo au choo kigumu:

1. Mafuta ya Zeituni

Mafuta ya zeituni (olive oil) yanatosha kutibu hili tatizo. Yana radha nzuri mdomoni na ni dawa pia. Kama unaweza yafanye pia kama mafuta yako ya kupikia vyakula vyako mbalimbali, mafuta haya huweza kuliwa pia bila kupitishwa kwenye moto na hivyo ni mafuta mazuri kuweka kwenye kachumbari au saladi mbalimabali.

Matumizi: Chukua kijiko kikubwa kimoja cha mafuta ya zeituni changanya na kijiko kidogo kimoja cha chai cha maji maji ya limau na unywe asubuhi ukiamka tu tumbo likiwa bado tupu. Fanya hivi kila siku mpaka utakapopona.

2. Juisi ya Limau

Juisi ya limau inatumika kutibu tatizo la kupata choo kigumu au kufunga choo. Chukua maji maji ya limau kutoka katika limau kubwa 3 na uchanganye na juisi ya matunda kupata kikombe kimoja (ml 250) na unywe yote kutwa mara 1 kila siku kwa siku kadhaa mpaka umepona.

Ukiacha hilo la kutibu kufunga choo limau ina vitamini C nyingi na hivyo itakuongezea kinga yako ya mwili kwa haraka zaidi (usizidishe hata hivyo).

3. Mazoezi ya kutembea

Kama unataka kupata choo kilaini na cha kawaida basi jitahidi uwe mtu wa kutembeatembea na si kukaa tu kwenye kiti kutwa nzima. Maisha yetu ya kisasa na kazi za ofisini zinatulazimisha kuwa watu wa kukaa kwenye kiti masaa mengi wengine huamua tu kukaa kwenye kiti sebureni akiangalia TV asubuhi mpaka jioni!. Aina hii ya maisha ni hatari zaidi kwa afya zetu kuliko hata madawa ya kulevya.

Jitahidi kila siku uwe unapata muda wa kutembeatembea kwa miguu mpaka dakika 60 au zaidi. Hii itakusaidia kuondoa tatizo la kufunga choo au kupata choo kigumu sana.

4. Vyakula vya nyuzinyuzi (fiber)

Mara nyingi utasikia watu wakisisitiza juu ya umhimu wa kula vyakula vya asili na vyenye nyuzinyuzi. Chakula cha asili kina nafasi kubwa katika kuimarisha afya yako kwa ujumla.

Kinachonishangaza ni kuona watu bado wanaendelea kula ugali wa sembe ilihali inajulikana wazi ugali mweupe ndiyo chanzo kikuu cha kupata choo kigumu ikiwemo ugonjwa wa bawasiri. Ninakusihi sana uanze kula ugali wa dona kuanzia sasa na kuendelea.

Hakikisha pia asilimia 80 ya mlo wako kwa siku ni matunda na mboga za majani. Matunda kama ndizi na parachichi ni mhimu ule kila siku kadharika tumia unga au mbegu za maboga.

5. Mshubiri (Aloe Vera)

Mshubiri unajulikana wazi kwa kutibu tatizo hili la kufunga choo au kupata choo kigumu. Ni mhimu utumie mshubiri fresh kabisa kutoka kwenye mmea moja kwa moja kuliko kutumia za dukani au za kwenye makopo. Usitumie zaidi ya vijiko vikubwa viwili vya jeli ya shubiri kwa siku.

Matumizi: Changanya vijiko vikubwa viwili vya jeli ya aloe vera ndani ya kikombe kimoja cha juisi ya matunda uliyotengeneza mwenyewe nyumbani (hasa juisi ya parachichi) na unywe yote kutwa mara 1 hasa nyakati za usiku unapokaribia kwenda kulala kwa siku kadhaa au mpaka umepona.

6. Baking soda

Baking soda ni dawa nyingine ya asili nzuri kwa tatizo hili. Inafanya kazi vizuri kwa zaidi ya asilimia 95. Sababu ya bicarbonate iliyomo ndani yake itakusaidia kupumua nje vizuri gesi au hewa yoyote ilisongamana ndani ya tumbo pia inasaidia kupunguza asidi mwilini.

Baking soda ni ile wamama huitumia katika kupika maandazi au mikate inapatikana katika maduka ya kawaida hata hapo nje kwa Mangi ipo.

Matumizi:

-Changanya kijiko kidogo kimoja cha chai cha baking soda ndani ya nusu kikombe cha maji ya uvuguvugu (ml 125) na unywe yote kwa haraka kutwa mara 1 kwa siku 7 hivi au unaweza kuacha siku yoyote kabla kama tatizo litakuwa limeisha.

7. Mtindi

Unahitaji bakteria wazuri zaidi wakati huu unapokabiliwa na tatizo la kufunga choo au kupata choo kigumu. Utahitaji pia kuacha kula vyakula vya kwenye makopo (processed sugars and foods). Namna rahisi kabisa ya kuhakikisha mwili wako unapata bakteria wazuri ni kwa kutumia mtindi.

Tumia mtindi wowote ule uliotengeneza mwenyewe nyumbani au hata wa dukani (ila wa dukani usiwe umeongezwa vitu vingine ndani yake – sweetened yogurt).

Matumizi: Kunywa kikombe kimoja (robo lita) cha mtindi wakati wa chakula cha asubuhi na kikombe kingine usiku unapoenda kulala kwa wiki 1 hata 2.

8. Fanya mazoezi ya kusimama na kuchuchumaa (squat)

Fanya mazoezi ya kuchuchumaaa na kusimama (squatting). Hili ni zoezi mhimu kwa mtu anayesumbuliwa na tatizo la kufunga choo au kupata choo kigumu sana. Fanya kuchuchumaa na kusimama mara 25 na upumzike dakika 1 kisha unaendelea tena unachuchumaa na kusimaa hivyo hivyo mara 25 kwa mizunguko mitano (5 rounds) huku ukipumzika dakika 1 kila baada ya mzunguko mmoja.

Fanya zoezi hili kila siku mara 1 na usizidishe sana, ni mara 25 kwa mizunguko mitano inatosha na uzuri ni kuwa unaweza kufanya zoezi hili mahali popote.

Wakati huo huo unashauriwa kutumia choo cha kuchuchumaa yaani vile vyoo vya zamani na siyo hivi vya kisasa vya kukaa kama vile upo ofisini. Vyoo hivi vya kukaa ndiyo moja ya vitu vinavyochangia upate pia ugonjwa wa bawasiri (kuota kinyama sehemu ya haja kubwa na kupata maumivu wakati unajisaidia).

9. Matunda

Asilimia 80 ya chakula chacko kwa siku iwe ni matunda na mboga za majani. Unapoumwa na hili tatizo pendelea zaidi parachichi, papai na juisi ya ukwaju. Kula matunda siyo mpaka uumwe au ushauriwe na daktari, fanya kuwa ndiyo tabia yako kila siku na hutakawia kuona mabadiliko makubwa kwa afya yako kwa ujumla.

10. Maji ya Kunywa

Maji ni uhai. Asilimia 75 ya mwili wako ni maji. Asilimia 85 za ubongo wako ni maji. Asilimia 94 ya damu yako ni maji. Hakuna maisha bila maji. Inashangaza sana kuona mtu anamaliza siku nzima au hata siku 2 hajanywa maji!

Kama wewe si mpenzi wa kunywa maji ya kutosha kila siku SAHAU KUWA NA AFYA NZURI MAISHANI MWAKO. Hakikisha unakunywa maji kila siku lita 2 mpaka 3, kidogo kidogo kutwa nzima bila kusubiri kiu na hutaugua tatizo la kufunga choo au kupata choo kigumu.

Mambo mhimu:

-Acha vilevi VYOTE

-Acha vinywaji baridi na juisi zote za dukani

-Acha chai ya rangi na kahawa na vinywaji vingine vyote vyenye kaffeina

-Acha kula vyakula vilivyokobolewa

-Acha kula mkate mweupe

-Acha kula vyakula vigumu

Kama una swali zaidi liulize hapo chini kwenye comment nitakujibu

Share post hii kwa ajili ya uwapendao

mbegu-za-maboga

(Imesomwa mara 3,883, Leo peke yake imesomwa mara 96)

You may also like...

677 Responses

 1. Doctor fadhil mimi huwa nakunywa Lita na nusu kwa siku coz kwetu maji ni ya chumvi yananishinda nikinywa tumbo linajaa sasa naweza kupata hilo gonjwa?

 2. He kupata maumivu ya mogoti nahuwa ya moto inasababishwa na nini

 3. Du! Asante sana kwa somo, Swali langu napend kuuliza VP tatizo linaweza kuisha kwa mazoez tuu? Maan nimewai kupatw Na hili lkn naona Niko poa Now, Half cku hiz kila asubh nafany zoez LA kuchuchumaa kwel naona matunda japo cjwahi kufany kwa mda ulosema.

 4. Ubarikiwe kwa elimu nzuri Kama hii

 5. Dr mm ninandunguyangu ana tatizo hilo akienda kujisaidia anaza kutoka damu halafu ndio cho kinatoka na anasikia maumivo je nitatizo ngani

 6. Elina Zabron Elina Zabron says:

  Sawa dokt tinasubili majibu yako ili tuweze kupata elimu zaidi

 7. Asante kwa elimu nzuri Nauliza Mimi Nina vidonda vya umbo sasa itakuwaje wakati malimao pamoja na mkwaju havifai kwa mtu anaeumwa na vidonda vya gumbo?

 8. Furaha Macha Furaha Macha says:

  Doctor ubarikiwe ila mimi nina tatzo, niko na growth imejitokeza sehemu ya haja kubwa yan hko kwa ndani nimeambiwa nifanyiwe sajary naomba unisaidie kwa tiba asili.

 9. Dr mm nikiwa nyumbani naenda choo mara nne mpaka tano ila kilaini nn tatizo

 10. Salma Subet Salma Subet says:

  Dokta Nina mtoto anatatizo la kutapika nimeambiwa ni gesi na mtaalam jee ni dawa ipi hapa inamfaa Kwan ni mda sasa

 11. Asha Kinoge Asha Kinoge says:

  Mshauli nimekuelewa mambo mengi umeyazungumza swali langu kwenye hichi choo cha kukaa si kizuli inasababisha kuota kinyama sehem ya ajakubwa kama kunamtu anatatizo hilo Tiba yake inatibika na nini swali langu niilo kazi njema

 12. Anzisheni clinic huku mawilayani ili wananchi wenyekipato cha chini waweze kuzipata kwa karibu.

 13. Kwanini nikitumia kitunguu swaumu nasikia maumivu ndani ya viungo Kama pilipili naombajibu

 14. Naeli Joseph Naeli Joseph says:

  Je kwa MTU anaesikia kizunguzungu kila asubuhi anapoamka kitandani tu afanyaje ilikuondokana na hilo?

 15. Me nahitaji mafuta ya Habbat soda gred one mils 300 nayapataje ? Niweke ktk odar tafadhali

 16. Samahàni km tial Nina bawasil nitumie tu matunda na nisitumie vyakula vigumu nitapona.litaisha hill linyama

 17. Mimi na tatizo hili ni mwezi wa tatu sasa, napona ns kujirudia, hufunga choo, na kikitoka ni kigumu na maumivu makali na damu juu, nifanyeje ndugu, kuna dawa mbadaka za hospitali, kama zipo zinaitwaje?

 18. Ahsante kwa somo ila naomba unisaidie mm nikila chakula najickia kichefu chefu huwa hu7bidhwa na nn? Na 2mbo language linajaa gesi sana na kutoa hali ya hewa Kali sana naomba unisaidie nifanyaje?

 19. na mi pia kuna mdogo wangu anasumburiwa na tatizo hiro nimusha uli atumie dawa gani?

 20. Skyler Luoga Skyler Luoga says:

  Mung akubarik mi nataka kujua nini kinasababisha MTU anakonda siku ad siku na haum sorry doctor lakin au ale nin Ili mwil wake urud

 21. Ushauri mzuri Sana, anayesoma na kuzingatia, afya itakuwa njema.

 22. dk maji ya baridi yanamazara gani kwa mwanaume na je maji ya dukani nimazuri kwa kiafya.

 23. Joyce Evarst Joyce Evarst says:

  Nahitaji unga wa majani ya mlonge ntaupataje na kwa bei gan?

 24. Rey Sive Rey Sive says:

  Mm nimefanya mazoez ya kuchuchumaa na kukaa nilivyomaliza migugu imelegea ata kutembea vizuli cwez nifanyeje iludi katika hali yake ya kawaida

 25. vp anko “ushishi” nayo ni tiba ya kufunga choo?

 26. Nuru Ally Nuru Ally says:

  Shukrani sana doctor

 27. ahsant dk kwan nmejifunza meng kuptia kwako

 28. Zulfa Omani Zulfa Omani says:

  Assalam aleykom mpdwa dungu yagu mmi nina tatizo la vidonda vya tumbo jee naweza kutumia dawa gani mana nimetumia dawa za sipitali hamna

  • Aleykum msalam, tumia unga wa majani ya mlonge, mafuta ya habbat soda na Unga wa mbegu za maboga kwa mwezi mmoja hivi mpaka miwili MFULULIZO. Pia 80% ya chakula chako kwa siku iwe ni mboga majani na matunda. Kunywa maji mengi kila siku mpaka Lita 3. Kwa msaada zaidi tuwasiliane WhatsApp +255769142586

  • Zulfa Omani Zulfa Omani says:

   Asante sana kaka nitajitahidi baada ya mwezi nitakupa jibu kaka inshaallah jadhakalakhel

  • Zulfa Omani Zulfa Omani says:

   Assalamaleko kaka nakwabia hivi Sasa hizi dawa matumizi yake yanakuwaje nakunywa au vipi mana kuna mchaganyiko wa dawa UNGA WA MAJANI YA MLONGE NA UNGA WA MBENGU ZA MABOGA NA MAFUTA YA HABATI SODA

 29. Shekh Adam Shekh Adam says:

  Ndugu kama unafahamu juu ya tunda la stafeli umuhimu wake na kama unaweza kutolea ufafanuzi juu ya hilo naomba

 30. Lucy Bilingi Lucy Bilingi says:

  MBONA. MIM. NI KITUMIA. DONA. NA HALSHA. DAMU. TANGU. UTOTO

 31. Jimmy Mango Jimmy Mango says:

  thanx 4 this elimu,eliku c hadri darasani,ni maarifa yyte mazr kwan som hili hulipati drsan,be blessed

 32. linah says:

  Mungu akubariki.unatusaidia wengi

 33. Naomba maelekezo namna ya kutengeneza juic ya alovela na jeli yake asante

 34. Kiungulia knatokana na nn? Dct

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *