Dawa mbadala 9 zinazotibu U.T.I

Dawa za U.T.I

U.T.I ni kifupi cha maneno ya kiingereza: ‘Urinary tract infections’, ni maambukizi ya bakteria katika njia ya mkojo. Ni moja ya ugonjwa unaowakumba sana wanawake kwa sehemu kubwa ingawa hata wanaume pia wanapatwa na ugonjwa huu.

Zaidi ya wanawake milioni 8 wanauguwa ugonjwa huu kila mwaka nchini Marekani peke yake.

Kama ulishawahi kupatwa na U.T.I basi hutazisahau dalili zake ambazo mara nyingi huanza kwa hitaji la ghafla la kutaka kwenda kupata haja ndogo na unapofika bafuni mara baada ya kutoa kiasi kidogo cha mkojo utaanza kusikia maumivu kwenye kibofu cha mkojo na hata kwenye urethra.

Katika dalili kubwa zaidi utaishia kujisikia homa, baridi kali, maumivu nyuma ya mgongo na hata damu kutoka pamoja na mkojo.

Habari njema ni kuwa kuna dawa mbadala za nyumbani unazoweza kuzitumia na ukajikinga na hata kujitibu na ugonjwa huu. Endelea kusoma.

mbegu-za-maboga

Kinachosababisha U.T.I:

 • Kisukari
 • Maumivu ya mishipa
 • Ajari katika uti wa mgongo
 • Ushoga (kwa wanaume)
 • Usafi duni
 • Upungufu wa maji mwilini
 • Kushikilia mkojo muda mrefu
 • Kurithi
 • Kuongezeka ukubwa kwa kibofu cha mkojo au mawe kwenye figo.

Baadhi ya dalili za kawaida na zisizo za kawaida za U.T.I

 • Kusikia maumivu wakati wa haja ndogo
 • Kukojoa mara kwa mara
 • Kupatwa ghafla na hitaji la kutaka kukojoa
 • Maumivu kwenye kibofu cha mkojo
 • Mikojo kukutoka pasipo kutaka
 • Hali ya kusikia kuungua wakati wa kukojoa
 • Kukojoa damu
 • Harufu nzito au mbaya ya mkojo
 • Homa
 • Kusikia baridi
 • Kutokujisikia vizuri
 • Kujisikia uchovu

Dawa mbadala 9 zinazotibu U.T.I

1. Baking Soda

Dawa mbadala 7 zinazotibu U.T.I

U.T.I ambayo imedumu zaidi ya siku mbili inahitaji kuripotiwa kwa daktari. U.T.I isiyotibiwa mapema inaweza kupelekea matatizo zaidi kwenye figo na kuleta matatizo mengine makubwa zaidi.

Ili kuzuia U.T.I isijiimarishe zaidi jaribu kuongeza kijiko kimoja cha chai cha baking soda kwenye glasi ya maji na unywe na hivyo kusaidia kupunguza makali au kuendela kwa maambukizi ya U.T.I.

Baking soda itapunguza hali ya uasidi katika mkojo wako na kupelekea nafuu haraka.

Baking soda ni ile kinamama wanatumia wakati wanapika maandazi. Siri iliyopo hapa ni huko kupunguza asidi kwenye mkojo na mwilini kwa ujumla na hivyo kuongeza hali ya ualikalini mwilini.

2. Zabibu nyeusi (Blueberries) na zabibu nyekundu (cranberries):

Dawa mbadala 7 zinazotibu U.T.I

Dawa mbadala 7 zinazotibu U.T.I

Zabibu nyeusi (Blueberries) na zabibu nyekundu (cranberries) zote zinatoka katika mti wa aina moja na zina sifa sawa ya kudhibiti bakteria. Katika utafiti mmoja, juisi ya zabibu nyeusi iligundulika kuwa na uwezo wa kudhibiti U.T.I.

Pendelea kutumia juisi ya matunda haya glasi 2 mpaka 4 kwa siku mara kwa mara ili kujikinga na hata kujitibu na ugonjwa huu.

­3. Nanasi

Dawa mbadala 7 zinazotibu U.T.I

Kula Nanasi mara kwa mara ni mbinu nzuri kabisa katika kudhibiti maambukizi katika njia ya mkojo. Kwenye nanasi kuna kimeng’enya mhimu sana kijulikanacho kwa kitaalamu kama ‘Bromelain

Katika utafiti mmoja, watu wenye U.T.I waliopewa hii bromelain sambamba na antibiotic zao walifanikiwa kuondokewa na maambukizi ya U.T.I.

Kula vipande vitatu mpaka vitano vya nanasi kila siku kutakuweka mbali na ugonjwa huu.

4. Maji

Dawa mbadala 7 zinazotibu U.T.I

Kama unasumbuliwa na U.T.I au inakutokea unapatwa na ugonjwa huu mara kwa mara, basi hakikisha unakunywa maji ya kutosha kila siku walau glasi 8 mpaka 10 kwa siku, maji yenye joto la kawaida yaani yale ambayo hayajawekwa kwenye friji.

Mara nyingi mtu mwenye U.T.I huwa ana upungufu wa maji mwilini na ikiwa utauchunguza mkojo wake utaona ni wa rangi ya njano.

Kunywa maji ya kutosha kila siku na kama matokeo yake bakteria wote wanaokupelekea upatwe na U.T.I watalazimishwa kutoka nje ya mwili kupitia mkojo utakaoupata kutokana na kukojoa mara kwa mara kama matokeo ya kunywa maji mengi na utaona baada ya siku 4 mpaka 7 hata rangi ya mkojo inabadilika na kuwa mweupe kabisa.

Kujifunza zaidi kuhusu tiba kwa kutumia maji bonyeza hapa.

5. Vitamini C

 

Dawa mbadala 7 zinazotibu U.T.I

Baadhi ya madaktari wanashauri mtu atumie mpaka mg 5,000 za vitamin C kwa siku kwa mgonjwa anayesumbuliwa na maambukizi ya mara kwa mara kwenye njia ya mkojo.

Vitamini C hukifanya kibofu cha mkojo kubaki na afya kutokana na asidi yake safi kwenye mkojo kitendo ambacho ni mhimu katika kuwazuia bakteria wabaya kufanya makazi kwenye kibofu cha mkojo. Ukiacha machungwa, Vitamini C inapatikana pia kwa wingi katika juisi ya ubuyu na kwenye unga wa majani ya mlonge.

Hakikisha unapata kiasi cha kutosha cha Vitamini C kila siku ili kujikinga na hata kujitibu na U.T.I.

6. Kitunguu swaumu:

Dawa mbadala 7 zinazotibu U.T.I

Kitunguu swaumu ni mojawapo ya tiba mbadala ya nguvu katika kutibu maambukizi kwenye njia ya mkojo. Ni dawa nzuri dhidi ya bakteria na virusi na hivyo moja kwa moja kuwa mhimu katika kutibu U.T.I ya jumla na hata ile ya kibofu cha mkojo.

Kwakuwa moja ya kazi ya kitunguu swaumu ni kusafisha mkojo basi ni dhahiri inafaa sana katika kutibu U.T.I.

Namna ya kukitumia; Chukuwa kitunguu swaumu kimoja na ukigawe na uchukuwe punje 6, menya punje moja baada ya nyingine na kisha kikatekate (chop) vipande vidogo vidogo na kisu kisha meza kama unavyomeza dawa nyingine yoyote na maji vikombe 2 (nusu lita) kila unapoenda kulala kwa siku 7 hivi au zaidi.

7. Limau/ndimu:

Dawa mbadala 7 zinazotibu U.T.I

Weka vijiko vikubwa vitatu vya juisi ya limau au ndimu ndani ya glasi moja ya maji (robo lita) na unywe yote. Fanya zoezi hili kutwa mara tatu.

Pia unaweza kuongeza asali vijiko vikubwa vitatu ndani yake. Mchanganyiko huu wa limau na maji ya uvuguvugu utakuondolea maumivu yatokanayo na U.T.I na hata kuzuia kutokwa na damu kama matokeo ya maambukizi ya U.T.I hasa kwenye kibofu cha mkojo.

8. Unga wa majani ya Mlonge

mlonge

Tumia kijiko kidogo kimoja cha chai ndani ya uji,  au ndani ya juisi  ya matunda kikombe kimoja (robo lita) juisi uliyotengeneza mwenyewe nyumbani, au katika maji ya uvuguvugu kutwa mara 1. Tumia kwa wiki 3 mpaka mwezi mmoja.

9. Mshubiri (Aloe-Vera):

Mshubiri/Aloe Vera

Chukua jeli ya mshubiri (aloe-vera) vijiko vikubwa viwili, changanya na maji ya kawaida ili kupata kikombe kimoja (ml 250) au robo lita, changanya vizuri mchanganyiko huu na unywe kutwa mara 1 kwa siku 3 hadi wiki 2 au hadi utakapopona.

Unaweza kuongeza asali ndani yake vijiko vikubwa vitatu ili kupunguza ukali wa dawa hii.

Vitu vya kufanya kujikinga usipatwe na U.T.I

 • Ongeza unywaji maji kila siku au juisi za matunda, juisi uliyotengeneza mwenyewe nyumbani.
 • Epuka vinywaji baridi, pombe, chai ya rangi na kahawa.
 • Penda kuwa msafi.
 • Mara zote jitawaze kutoka mbele kurudi nyuma (hasa kwa wanawake) na uepuke kuchangia na wengine vifaa vya bafuni.
 • Jisafishe vizuri mara baada ya tendo la ndoa.
 • Usiushikilie mkojo muda mrefu, mara usikiapo kutaka kupata haja ndogo mara moja nenda
 • Vaa nguo za ndani zilizotengenezwa kutokana na pamba.
 • Epuka kaffeina.
 • Epuka tendo la ndoa kinyume na maumbile.

Dawa mbadala hizi 9 zinaweza kukusaidia kujikinga usipatwe na U.T.I au kujitibu ingawa bado inashauriwa kwenda kumuona daktari iwapo maumivu au dalili zinadumu kwa muda mrefu.

Kama utahitaji dozi kamili ya hizi dawa za U.T.I niachie ujumbe WhatsApp +255769142586. Ofisi yangu inaitwa Victoria Home Remedy ipo Buza Sigara temeke unaingia kupitia jet corner (uwanja wa ndege) au tandika.

Kama una swali liulize hapo chini kwenye comment sasa hivi.

mbegu-za-maboga

(Imesomwa mara 86,387, Leo peke yake imesomwa mara 449)

You may also like...

12,273 Responses

 1. NISAIDIE DAWA YA MENO PLS YAMETOBOKA NA YANAUMA SANA

 2. mjamzito anatumia kipi ili imsaidie kwa tatzo ilo la U.T.I???

 3. Asante sana dokta

 4. Dah!Nashukuru Kwa Tiba

 5. god bless you much for that

 6. Asante doctor lkn nasikia asali na limao au ndimu nisumu iyo nayo vipi nikweli au maneno tu

 7. Mungu akupe maisha marefu

 8. Neyma Brown Neyma Brown says:

  Mungu akubariki maradufu tunajufunza mengi mnoo

 9. Asante sana mtumishi Wa Mungu je kwa mama mjamzito anaruhusiwa kutumia huo mlonge ?

 10. Fatma Eliasa Fatma Eliasa says:

  Samahan doctor na vitunguu swaum pia naweza tumia kama dawa ya uti na ninakunywa punje ngapi na kwa siku ngapi

 11. Neema Kz Neema Kz says:

  Asante kwa somo

 12. Asante doctor unatuokoa

 13. Asante kwa somo zur

 14. Jessica Ab Jessica Ab says:

  Eeh asante kwa matibabu

 15. Leah Charles Leah Charles says:

  He bicarbonate inaponesha kbs!

 16. Dawa iliyotengenezwa kbx ni sh ngap?

 17. Asante kwa ushauri

 18. Asante kakutufunguwa ufahamu hakika kwa tiba hizi tutapona

 19. Subira Ame Subira Ame says:

  Dr fadhili mm nna swali……..iwapo mtu hana hili tatizo je anaweza kutumia hizi dawa km ni kinga kiupande wake?

 20. Grace Mgaza Grace Mgaza says:

  Asamte sana Dr ubarikiwe

 21. Somo zuri,imeeleweka

 22. Me nahitaji doz hy maana doctor nmechoma mpk sindano lkn inard mpk nachoka yan 0679 020277 no yng

 23. Anna Kilian Anna Kilian says:

  Nashukuru sana doct,je hiz dawa zinafaa kwa mwanamke mjamzito?

 24. Ndugu zangu wana fb na mitandao mingine ya kijamii tuzingatieni tiba hii hili tuweze kuutokomoza ugonjwa huu wa U T I

 25. Mungu akubariki sana doctor wangu

 26. Asante sana Docta

 27. Asante sana docta nitafanya zoezi hili,mungu akujaliye na akuongoze uzidi kutusaidia asante

 28. Anna Ntima Anna Ntima says:

  Asante kwa tiba ya uti

 29. Paul Jonh Paul Jonh says:

  Unapatikana wapi doctor

 30. Asante sana doct nitazingatia hayo

 31. Asante kwa ushauri wako

 32. Dr hauna vtabu,ushaur wangu,haya mambo mazuri sana yaweke kwenye vitabu,ili tununue kwa kumbukumbu zaidi.

 33. Siah Mtenga Siah Mtenga says:

  Ahsante docta ila hapo kwenye vitunguu swaum sijaelewa,unakunywa vyote sita baada ya kuvikata

 34. Nuru Chotta Nuru Chotta says:

  Ubarikiwe sana doctor.

 35. Asante Kwa Darasa Doct Kuazia Leo Nitaongeza Juhudi Kutumia Hzo Dawa

 36. Adam David Adam David says:

  sawa kabisa asante drct

 37. Doctor mie Nina tatizo la kupenda kula udongo kama mjamzito kwa Siku hata 8 nisaidie niache mwenzenu

 38. Mary Beatriz Mary Beatriz says:

  Samahan dokta io ya kitunguu swaum unaweza kutumia ata km mjamzito

 39. Lucy Swetu Lucy Swetu says:

  Barikiwa sana kwakutujuza

 40. Jovin Gitta Jovin Gitta says:

  dokta baba yangu anasumbuliwa sana na u.t.I je?Nikupateje mm nipo ukerewe bwiro ksiwan pia nahtaj dawa kwa uharaka zaid ila cjajiunga watsup d

 41. Asante sana dr me nauliza kwasisi wenye vidonda vyatumbo hizo dawa zinatuwafaa?

 42. Anna Carlos Anna Carlos says:

  Asante endelea na moyououo.

 43. Mbona nasikia limao na asali ukichanganya ni sumu

 44. Asante sana docta nashukuru kwani tunateseka sana wanawake na u t l

 45. Asante Thana Dr Na Hz Dawa Za U.T.I Znaitwaje

 46. Joseph Mdemu Joseph Mdemu says:

  Nimeipenda sana maandarizi inakuwaje sasa mkuu

 47. Scola John Scola John says:

  Mm nahitaji sana hizo dawa zote ninafanga huku sehemu za siri nitazipataje mm napatika mkoa wa manyara wilaya ya mbulu

 48. Asante kwa ushauri ubarikiwe sana

 49. ubarikiwe sana kwa tiba na ushaur wako doctor

 50. Sawa mtaalamu wangu,,ni,mekupata

 51. Mimi naumwa kinenani apa pia ndani ya uke kunavuta sana nimeenda ospitar nimeambiwa fangasi na sio u. T. I sasa nifanyeje nisaidieni

 52. Kitunguu swaum unatumia mara moja kwa siku yani usiku tu mara moja kwa siku saba

 53. Shuklani tatiz hil limenipelekea had maumiv makali mgongonj na nikilala nikja amka maumiv chin ya ktv mpaka uanz kutembea tembea ndo uwe shwar xx dr ni ip dawa nianze nayo itakayo nifaa nahangaika kwel.

 54. Huo ni mfano wa kuigwa na madoctor wote ili kuwasaidi wale wasiojua. Mungu akubariki sana kwa kuwagawia watu kile kidogo ulichojaaliwa na mungu akuzidishie zaidi.

 55. Zanura Swai Zanura Swai says:

  Asante Kwa somo zuri

 56. Huyo nyie acheni hizo Nanasi toka ln likatibu U.T. I.

 57. Asack Sesack Asack Sesack says:

  Asante docta nimejifunza mengi nashukulu

 58. Ata zabibu zadukani juice yakeinafaa

 59. Umeeleza vzr umeeleka

 60. Ahsante & ubarikiwe xna

 61. Sheri Salum Sheri Salum says:

  Asante doctor mungu akupe barak nying utufunze na mengine

 62. Nimeipenda imenifungua.

 63. ASANTE KWA USHAULI WENU

 64. Ves John Ves John says:

  Asante darasa nzuri

 65. Asante Sana kwa kupata Dawa,me huwa inanisumbua Sana.

 66. Jafeth Fue Jafeth Fue says:

  Mungu akubariki kwa somo zuri

 67. Ivan Mosses Ivan Mosses says:

  Mbona kimya sana VP umeongea na mzeee lini

 68. Lucy Liymo Lucy Liymo says:

  Asante Dokita mm naitaji Daw hiyo

 69. Ubarikiwe mtu wa Baba.

 70. Mainaz Ally Mainaz Ally says:

  Jaman mm cjaelewa doctor je unashemsha au nafanyaje

 71. thx kwa darasa saf ujaaliwe miaka mng uish

 72. Asante sana doctor

 73. Mimi nielekeze dawa yakupunguza mwili na tumbo

 74. Samia Burton Samia Burton says:

  Asante sana kwa somo muhimu km hili ubarikiwe sssaaaaaana.

 75. Rose Saimon Rose Saimon says:

  Asant san ubarkiw

 76. Salma Salum Salma Salum says:

  Somo lipo vzur linaeleweka

 77. Tausi Ally Tausi Ally says:

  Mimnaitaji
  Hiyotiba
  Ntaipataje?

 78. Tausi Ally Tausi Ally says:

  Namba
  Yangu
  0712130615

 79. Fesali Salum Fesali Salum says:

  Nimekuelewa docta

 80. Asante kwa ushauri mzuri binafsi ndajitahidi kufanya hivyo

 81. Asante sana barikiwa sana

 82. Mercy Jakson Mercy Jakson says:

  Asante kwa somo dr

 83. Asante sana kwa ujumbe huu ila mm cjaelewa maana ya baking soda au ni paking poda

 84. Nahitaji Sana hiyo dawa

 85. Dah Ahsante sana maana

 86. Mimi mke wangu anatokwa na uchafu sehemu za Siri uchafu mzito ka mtindi nifanyeje ili apone

 87. Mi naitaji dawa mkuu

 88. Nashukuru Doctor Kwa muongozo mzuri wa dawa hivi sasa naanza asante sana

 89. Ester Nteko Ester Nteko says:

  Asante sana kwa ujumbe

 90. Mimi MNA tatizo LA kifua na mgongo kuuma kichwa kuuma na mapigo ya moyo yanaenda mbio dalili ya nini

 91. Mamuu Haji Mamuu Haji says:

  Asante kwa kutisakusaidia hasa ss wanawake

 92. Emanuel Jeremia says:

  juna uhusiano wa kuwa na magojwa ya zinaa ukiwa na UTI

 93. Emanuel Jeremia says:

  kuna uhusiano wa kuwa na magonjwa ya zinaa ukiwa na UTI

  • fadhili says:

   Ndiyo upo, ukiwa na U.T.I ni tayari una maambukizi kwenye njia yako ya mkojo hivyo ni rahisi kupata maambukizi mengine zaidi

 94. Marry Patric Marry Patric says:

  Shukran doctor’ kama Nina vidonda vya tumbo ‘ na Nina utiai ‘ nikitumia hizo dawa’ vidonda vya tumbo havitasumbua ?

 95. Endesh Nicol Endesh Nicol says:

  Doctor tunashukuru kwa ushauri wako nimetoka nje ya mada Dawa ya jino Na Vidonda Vya Tumbo ni nini .samahani sana kwa usumbufu

 96. Shule tosha kwangu asante

 97. Asante Doctor,Mimi nimefurahi sana somo hili,nimejifunza sana.nitajilinda dhidi ya UTI kwakutmia njia hizi.barikiwa sana

 98. Angel Mganga Angel Mganga says:

  Mosi,pongez zangu za dhati kwako dr.stay blessed.Other people bna! huo ndo mchango wake kwa jamii, ikiwa ni kwa kesi ya baking soda ni namna ya mtazamo na application,mbona chinese mnakula na ni sawa na baking soda kwa cases?ungeuliza tu kwanza na c vinginevyo,ikiwa lengo kubwa kuiokoa jamii yetu.potofu,mbona hukuchangia chochote ukakaa na karama yako hiyo!afu kwa jeur na kibur kikubwa unacomment she/he is wrong!vyote alivyooelekeza dr ni applicable nami shuhuda na c mnafiki,ewe na yeye nan chaka ss.Busara kwanza plz.

 99. Asanteni sana mbarikiwe

 100. Mudy Daudi Mudy Daudi says:

  Mungu akubaliki sana kwa kuwasaidia wa2 kwa dawa zako au ushaur wako

 101. mycrtoh santoh says:

  dr.mimi kwa sasa nackia maumiv chini ya kitovu,nakunywa maji mengi pia ila nikienda kukojoa hali haibadilik mkojo n kama mwekundu ila xo sana nseme pale-red,,,kwahiyo ndo UTI au??

 102. Nimehamasika na dawa lakini naomba unuelekeze nijaribu kutengeneza nimeipenda.

 103. Mimi nasumbuliwa sana na miwasho sehem zangu za siri je vitunguu swaum vtansaidia?

 104. Naima Yusuph Naima Yusuph says:

  Asante doct mie nimeshaenda hospital zaidi ya mala 5 kwa tatizo la u’ t, i nifanyaje

 105. MARIAMU MROPE says:

  tunashukuru

 106. Unaweza kutumia vitunguu hata asubuhi au ni usiku tuu

 107. Unaweza kutumia vitunguu hata asubuhi au ni usiku tuu

 108. Unaweza kutumia vitunguu hata asubuhi au ni usiku tuu

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *