Dawa mbadala ya vidonda vya tumbo

Dawa  mbadala ya vidonda vya tumbo

Hapo kabla tumejifunza mengi kuhusu ugonjwa wa vidonda vya tumbo. Tuliona maana ya vidonda vya tumbo, dalili za vidonda vya tumbo na tuliongelea kwa kirefu ni vitu gani husababisha vidonda vya tumbo mwilini. Kama hukubahatika kusoma somo hilo unaweza kulipata kwa kubonyeza hapa => [Vidonda vya Tumbo]

Leo tutaangalia dawa mbadala 8 zinazotibu au kuzuia kabisa vidonda vya tumbo. Tafadhali wasiliana na daktari au mganga wako kabla ya kuanza kuzitumia hizi dawa ili akupe muongozo na maelezo mengine mhimu kulingana na hali na historia ya ugonjwa wako wa vidonda vya tumbo.

mbegu-za-maboga

Dawa mbadala ya vidonda vya tumbo

1. Kabeji

Kabeji

Kabeji

Kabeji ni moja ya dawa bora za asili zinazoweza kutibu vodonda vya tumbo. Kabeji inayo ‘lactic acid’ na husaidia kutengeneza amino asidi ambayo huhamasisha utiririkaji wa damu kwenda kwenye kuta za tumbo jambo linalosaidia kuuongezea nguvu ukuta wa tumbo na hatimaye kutibu vidonda vya tumbo.

Kabeji pia ina kiasi kingi cha vitamini C ambayo imethibitika kuwa na faida kubwa kwa watu wenye vidonda vya tumbo vilivyosababishwa na maambukizi ya bakteria aitwaye ‘H. pylori. Pia majaribio yamethibitisha kuwa juisi ya karoti freshi inayo vitamini U mhimu kwa ajili ya kudhibiti vidonda vya tumbo.

 1. Kata kabeji nzima mara mbili na uchukuwe nusu yake, chukuwa karoti mbili na ukatekate vipande vidogo vidogo na utumbukize vyote kabeji na karoti kwenye blenda na uvisage ili kupata juisi yake.
 2. Kunywa kikombe kimoja cha juisi hii kila nusu saa kabla ya chakula cha asubuhi, mchana na jioni na kikombe kimoja kabla hujaingia kulala.
 3. Rudia zoezi hili kila siku kwa wiki kadhaa na hakikisha unatumia juisi freshi pekee na siyo ukanunue juisi ya kabeji au karoti ya dukani.

 

2. Ndizi

Ndizi

Ndizi

Ndizi zilizoiva na hata ambazo hazijaiva zote ni nzuri kwa ajili ya kudhibiti vidonda vya tumbo. Kuna aina maalumu ya muunganiko wa vimeng’enya vilivyomo kwenye ndizi ambavyo huzuia kuongezeka au kuzaliana kwa bakteria wa vidonda vya tumbo ‘H. Pylori’.

Ndizi pia huulinda mfumo wa kuta za tumbo kwa kuiondoa asidi iliyozidi tumboni na hivyo kusaidia kuuondoa uvimbe au vidonda tumboni na pia kuuongezea nguvu ukuta wa tumbo.

 • Ili kutibu vidonda vya tumbo, kula walau ndizi zilizoiva 3 kwa siku.
 • Au menya ndizi 2 au 3 na uzikate katika vipande vidogo vyembamba (slices) na uanike juani mpaka zikauke kabisa. Kisha saga vipande hivyo ili kupata unga na uchanganye vijiko vikubwa viwili vya unga huu na kijiko kikubwa kimoja cha asali na ulambe mchanganyiko huu mara 3 kwa siku kwa wiki 2 hivi.

 

3. Nazi

mafuta ya nazi

mafuta ya nazi

Nazi ni nzuri sana katika kutibu vidonda vya tumbo sababu ya sifa yake na uwezo wa kuua bakteria. Nazi huziua bakteria zinazosababisha vidonda vya tumbo. Pia tui la nazi na maji ya nazi (dafu) vyote vina sifa na uwezo wa kutibu vidonda vya tumbo.

 • Kunywa vikombe kadhaa vya tui freshi la nazi au maji ya nazi kila siku. Pia unaweza kuitafuana nazi yenyewe mara kwa mara. Fuatisha mlolongo huu walau kwa wiki 2 ili kupata matokeo chanya.
 • Au kunywa kijiko kikubwa kimoja cha mafuta ya asili ya nazi asubuhi kabisa na kingine usiku kwa wiki 2 hivi.

 

 

4. Uwatu

Uwatu

Uwatu

Uwatu unajulikana sana kwa uwezo wake wa kutibu maradhi mengi mwilini. Unaweza pia kuutumia katika kutibu vidonda vya tumbo. Kwakuwa uwatu inayo gundi maalumu au ulimbo ambayo huulinda ukuta wa tumbo kwa kuufunga au kuufunika kama utando na hivyo kurahisisha hatua za kutibu vidonda vya tumbo.

 • Chemsha mbegu za uwatu kijiko kidogo cha chai ndani ya vikombe viwili vya maji, chuja na uongeze asali kidogo na unywe kwa pamoja kutwa mara 2 kwa wiki 2 au zaidi.
 • Unaweza pia kutumia kijiko kidogo kimoja cha chai cha unga wa mbegu za uwatu ukichanganya kwenye kikombe cha maziwa ya moto.
 • Au unaweza kuchemsha kikombe kimoja cha majani freshi ya uwatu, ongeza asali kidogo na unywe mara 2 kwa siku kwa wiki 2 au zaidi.
 • Ingawa maziwa hayashauriwi sana kutumika kwa mtu mwenye vidonda vya tumbo, hivyo unaweza kutumia maji ya uvuguvugu badala ya maziwa kama vidonda vyako vimeshakuwa sugu sana au ikiwa unahitaji upate nafuu ya haraka na hatimaye kupona.

 

5. Asali

dawa mbadala zinazotibu pumu

Asali

Asali mbichi, ile nzuri kabisa ambayo haijachakachuliwa inao uwezo mkubwa katika kutibu vidonda vya tumbo. Kama ujuavyo asali ni dawa karibu kwa kila ugonjwa. Kuna kimeng’enya kilichomo kwenye asali kijulikanacho kama ‘glucose oxidase’ ambacho huizalisha ‘hydrogen peroxide’ ambayo yenyewe inayo uwezo wa kuuwa bakteria wabaya mwilini ambao husababisha vidonda vya tumbo. Pia hii ‘glucose oxidase’ huulainisha ukuta wa tumbo na kupunguza muwako au vidonda tumboni.

Lamba vijiko vikubwa viwili kutwa mara tatu au vijiko vikubwa vitatu kutwa mara mbili. Itasaidia kusafisha tumbo, itaimarisha ukuta wa tumbo na kuzuia na kutibu vidonda vya tumbo. Fanya hivi kwa wiki 3 hadi 4. Hakikisha unapata asali mbichi salama ambayo haijachakachuliwa.

 

6. Kitunguu Swaumu

Kitunguu swaumu

Kitunguu swaumu

Kitunguu swaumu pia husaidia kutibu vidonda vya tumbo. Watafiti katika kituo cha utafiti wa kansa cha Fred Hutchinson Cancer Research Center in Seattle waligundua kuwa uwezo ambao kitunguu swaumu unacho katika kudhibiti na kuua bakteria mbalimbali mwilini unaweza kudhiti pia bakteria anayesababisha vidonda vya tumbo ajulikanaye kama Helicobacter Pylori (H. pylori).

Chukuwa punje 6 hadi 10 za kitunguu swaumu, menya na ukate vipande vidogo vidogo kisha umeze pamoja na maji vikombe viwili kutwa mara 2 kwa wiki 2 au 3. Soma makala hii kuhusu kitunguu swaumu => [Kitunguu Swaumu hutibu magonjwa 30].

 

7. Mkaa wa kifuu cha nazi

Vifuu vya Nazi

Vifuu vya Nazi

Mkaa pia hutibu vidonda vya tumbo hasa mkaa utokanao na vifuu vya nazi. Chukua vifuu vya nazi vitano au kumi vilivyokauka, viweke juu ya jiko la mkaa au popote na uvichome moto, mwishoni chukua mkaa wake usage kupata unga, kisha chota kijiko kikubwa kimoja na uweke ndani ya kikombe kimoja cha maji changanya vizuri na unywe kutwa mara 3 kwa wiki 2 au 3.

 

8. Unga wa majani ya Mlonge

mlonge

Mlonge ni mti mhimu sana katika utabibu kama tiba mbadala, majani, maua, mbegu na mizizi yake hutumika sana katika kutibu magonjwa mbalimbali. Mlonge una kiasi kingi cha vitamin C, Madini ya chuma, protini, Vitamini A na potasiamu.

Ongeza kijiko kimoja cha chakula kwenye bakuli ya mboga unapokula chakula cha mchana na jioni. Unaweza pia kunywa unga huu wa mlonge pamoja na juisi yoyote uliyotengeneza mwenyewe nyumbani au unaweza kuuchanganya kwenye chakula kama vile wali na hivyo ukajiongezea kinga zako dhidi ya vidonda vya tumbo. Tumia kwa wiki 3 hadi 4.

 

Chagua dawa mbili au tatu kati ya hizi na uzitumie kwa pamoja ili kupata matokeo mazuri zaidi. Na kwa hapa napendekeza zaidi dawa namba tatu, tano, sita na nane. Usisahahu pia kunywa maji ya kutosha kila siku na ili kutambua ni kiasi gani cha maji ya kunywa unahitaji kila siku tafadhari bonyeza => hapa

Pia sikiliza somo hili kuhusu vidonda vya tumbo kwa njia ya sauti (audio) kwa kubonyeza hapa

Kama una swali lolote au unahitaji ushauri wowote andika hapo kwenye comment sasa hivi nitakujibu.

Ikiwa utahitaji dozi kamili ya dawa za asili zilizoandaliwa tayari kwa ajili ya vidonda vya tumbo niachie ujumbe WhatsApp +255769142586

Jiunge na ukurasa wangu wa facebook kwa kubonyeza hapa => facebook

Je Umeipenda makala hii? Ninakaribisha mchango wako wa mawazo au ikiwa una swali nitafurahi zaidi kwani ni faraja kwangu kuona nimekujibu vizuri.

mbegu-za-maboga

(Imesomwa mara 44,908, Leo peke yake imesomwa mara 288)

You may also like...

1,680 Responses

 1. Asante sana Doct. hizo dalili zote ulizozitaja ninazo in shaa Allah nitaanza kutumia.shukrani kwa kutufumbua macho mana dawa tunazo kwenye mazingira yetu tena kwa gharama nafuu lkn hatuzijui .ubarikiwe sana

 2. Jamani ninashida hiyohiyo mimi kabra sijala najickia kichefu chefu alafu mwili huishiwa nguvu san na baada ya muda mfupi tu huwa napata kizunguzungu au same time nikiwa nimelala arafu mda nitakapo amka najisika kizunguzungu napia nashindwa kusimama nahiyo nidalili ya vidonda vya tumbo au dalili ya ugonjwa mwingine . nawtakia kazi njema

 3. Kuna mtu alikuwa na vidonda vya tumbo akawa anakula pili pili kwa wingi, anadai kuwa ni dawa yake. Je ni sahihi!??

 4. Samahan Docta umeandika chagua dawa 3 kati ya hz ili kupata matokeo mazur zaid swal langu ni je ukizitumia zote inamana utakunywa kwa kutwa mara moja kila dawa au utakunywaje kwa ambazo zinatakiwa unywe kutwa mara 2 au 3?

 5. Obadia asali ulikuwa unatumiaje au u achanganya na nini?

 6. Ibrahim mimi nilitumia mkia wa kondoo lakini niliharisha sana na kutapika hadi nikaishiwa nguvu

 7. Ukitoa 20000 utatakiwa kutoa lini tena au ndo basi?

 8. Zawadi Bihay Zawadi Bihay says:

  Me nahitaj kukata tumbo

 9. Nimejifunza sana kuhusu mateso yangu na vidonda tumbo asante Mungu akubariki sana

 10. Doctor nami ninasubuliwa na matatizo hayo hulivyo sema ukiaza hiyo tiba usitumie vidonge mimi nisipo kunywa dawa za maumivu siamki sasa nifanyeje?

 11. Asanteni nimependa ushauri wenu

 12. Nace Gideon Nace Gideon says:

  Acha nishare Kwakweli Maana watu wangi wanateseka Jmn.

 13. Adja Baruan Adja Baruan says:

  Jmn mm karbu dawa zote hapo nmetumia lkn wap nikianza kuumwa hadi xhida

 14. Adja Baruan Adja Baruan says:

  Jmn mm karbu dawa zote hapo nmetumia lkn wap nikianza kuumwa hadi xhida

 15. Tabu Abla Tabu Abla says:

  Mimi na sumbuliwa navidonda lhuwa nacheuwa kwa sauti kubwa saaingine nimekaa maji yanapanda machungu nayatema na chomwachomwa kwenye chamby ya moyo pana niuma mpaka mgongoni tumbo huwalinaja nashindwa kula saa ingine nahasira paspo tatizo inakuwepo tuu naweza kutumiwa dawa nizipate moshi au nimpalka nije daa naitaji matibabu

 16. Naomba niletee asali mbichi pure naona hiyo ndio dawa rahisi waubani Nyantuzu Mpo’rwe

 17. Judith Bippa Judith Bippa says:

  Asante kwa ushaur mzur

 18. Binti Abed Binti Abed says:

  Ubarikiwe,mi Mwenyewe Ninateseka Mno Na Vidonda Vya Tumbo Naanza Dozi,naimani Nitapona

 19. Elim zaid nmeipata juu ya faida ya maji mwilini

 20. Mi nasumbliw na kifua kinawaka moto sana sehem ya kichimba moyo hadi napata maumiv na mda mwingn nahis kama vile kiuno kizito,na joto Kali,je ni vdonda vya tumb

 21. Mi napata maumiv sana sehem ya kifuani juu hasa kweny kichimba moyo kama vile kinaungua na kiuno kama vile kimejaa vitu na joto Kali mda wote, je ni vdonda vya tumbo?na kama ni ivyo nitumie dawa gan?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *