Dawa ya jino ya asili

Dawa ya jino ya asili

Dawa ya jino ya asili

Maumivu ya jino ni moja ya maumivu mabaya sana kuyapata, maumivu mengine mabaya zaidi ni maumivu ya sikio. Jino linaweza kupatwa na maumivu ambayo yanaweza kupelekea jino kutoboka na hata kuong’olewa kabisa.

Maumivu haya yanaweza kuletwa na maambukizi ya bakteria kutokana na vyakula tunavyokula au kutokusafisha kinywa vizuri kila siku, jino kupata jeraha, magonjwa ya fizi, na udhaifu wa mifupa mwilini mwako kwa ujumla.

Maumivu mengi ya jino ni ishara kuwa huna chumvi ya kutosha mwilini, huna maji ya kutosha mwilini na hujishughulishi na mazoezi ya viungo kila mara.

Dawa zifuatazo zinaweza kutuliza maumivu ya jino na hata kuliziba kabisa iwapo tayari limeanza kutoboka.

1. Asali yenye mdalasini

dawa ya jino

Asali yenye mdalasini

Changanya kijiko kidogo kimoja cha chai cha mdalasini ya unga na vijiko vikubwa viwili vya asali mbichi na upake kidogo kidogo juu ya jino linalouma mara kadhaa kwa siku mpaka maumivu yatakapopotea.

2. Aloe vera (mshubiri)

dawa ya jino

Aloe Vera (mshubiri)

Pata aloe vera fresh na uchane kupata maji maji yake (utomvu) na unyunyize juu ya hilo jino linalouma kidogo kidogo kutwa mara 2

3. Mafuta ya nazi na karafuu

Dawa ya Jino

Mafuta ya nazi

Chukua karafuu 3 zitwangwe kwenye kinu, changanya na mafuta ya asili ya nazi kijiko kidogo kimoja  uliyotengeneza mwenyewe nyumbani. Pasha kwenye moto kama dakika tatu, ipua na usubiri mchanganyiko wako upoe.

Paka mchanganyiko huu juu ya jino linalouma na uache kwa dakika 7 kisha jisukutue kinywa na maji.

Dawa ya Jino

Karafuu

4. Majani ya mpera

Dawa ya Jino

Majani ya Mpera

Majani freshi ya mti wa mpera yanatibu pia jino linalouma sababu ya sifa yake ya kutibu maambukizi na huua pia bakteria wabaya wanaoshambulia jino.

Tafuna tu jani au mawili ya mti huu mpaka mara mbili kwa siku kwa siku kadhaa na jino litaaacha kuuma.

Unaweza pia kuchemsha katika moto majani kadhaa ya mti huu kisha ipua chuja na uongeze chumvi kidogo ya mawe ya baharini na utumie kusafishia kinywa chako ukitumia mswaki mara 2 kwa siku kwa siku kadhaa.

5. Maji ya uvuguvugu na chumvi

Mchanganyiko rahisi wa maji ya uvuguvugu na chumvi unaweza kusaidia kutibu maumivu ya jino.

Changanya nusu kijiko cha chai cha chumvi ya mawe ya baharini na maji ya uvuvugu glasi moja na utumie kusafisha kinywa chako ukitumia mswaki mra 2 kwa siku kwa siku kadhaa.

Mchanganyiko huu husaidia kutibu bakteria, maambukizi na uvimbe katika fizi.

6. Kitunguu maji

 

Dawa ya Jino

Silesi za kitunguu maji

Kitunguu maji kina sifa ya kuzuia vijidudu nyemelezi ndani ya mwili na kinaweza kutumika pia kutibu maumivu ya jino kwa kuviua vijidudu vinavyosababisha kuoza kwa meno.

Tafuna silesi kadhaa cha kitunguu maji freshi ili kupunguza maumivu ya jino. Au kama huwezi kukitafuna basi weka tu kipande cha silesi cha kitunguu maji juu ya jino linalouma kwa dakika 10 hivi mara kadhaa kwa siku ili kuondoa hayo maumivu.

7. Kitunguu swaumu

Dawa ya Jino

Kitunguu Swaumu

Kutumia kitunguu swaumu pia kunaweza kurahisha kwa haraka kuondoa maumivu ya jino. Kitunguu swaumu huua bakteria, huua virusi pia ni antibiotiki ya asili isiyo na madhara kama antibiotiki za viwandani.

Tafuna punje 1 au 2 za kitunguu swaumu kila siku. Au katakata vipande vidogo vidogo vya punje 2 au 3 za kitunguu swaumu uchanganya na chumvi kidogo ya baharini kwa mbali na uweke mchanganyiko huo moja kwa moja juu ya jino linalouma na uache kwa dakika 5 au 7 hivi mara 2 kwa siku kwa siku kadhaa.

8. Pilipili na chumvi

Dawa ya Jino

Pilipili Manga

Pilipili na chumvi unaweza kuwa mchanganyiko mzuri sana wa dawa za asili kwa kutibu maumivu ya jino sababu vyote viwili chumvi na pilipili hudhibiti bakteria na maambukizi mbalimbali.

Pata pilipili manga nyeupe au nyeusi ya unga na uchanganye kiasi sawa cha pilipili na chumvi ya mawe ya baharini kisha ongeza kiasi kidogo cha maji kupata uji mzito kidogo na uuweke juu ya jino linalouma kwa dakika kadhaa kila siku kwa siku kadhaa.

Ni mhimu pia kuonana na daktari wa meno kwa uchunguzi zaidi kwani wakati mwingine dawa hizi zinaweza zisikuponye tatizo la jino kuuma au kutoboka kama unavyotarajia.

Sehemu nyingi mijini zipo kliniki maalumu kwa ajili ya meno tu, waone madaktari hao kwa uchunguzi juu ya matatizo yako ya meno mara kwa mara.

*Zingatia sana kutumia chumvi ya kutosha kila siku na mazoezi ya viungo.

Soma hii makala => maajabu ya chumvi

*Epuka vyakula vitamu sana vya madukani, ice cream, pipi, na soda zote na vingine vya jamii hiyo

Soma na hii => faida 50 za mazoezi

Kama unahitaji dawa hizi za asili zilizoandaliwa tayari kutoka kwangu, niachie ujumbe WhatsApp +255769142586

Tafadhari SHARE post hii kwa ajili ya wengine uwapendao.

Una ushuhuda wowote kama matokeo ya kutumia blog hii? Kama ndiyo toa ushuhuda wako ili uwe msaada kwa wengine, kutoa ushuhuda wako bonyeza hapa.

(Imesomwa mara 6,545, Leo peke yake imesomwa mara 159)

You may also like...

288 Responses

 1. Asante sana.
  Na hili ni janga kwa wengi

 2. Bob Chipe Bob Chipe says:

  Shukrani sana dokta, vipi kuhusu dawa ya maumivu ya sikio maana mimi ndio ugonjwa wangu mkubwa huo.

 3. Asante sana mungu akubaliki

 4. Girec John Girec John says:

  Docta kuna mdogo wangu anayatizo LA maskio hasikii sass anamwaka 1 unamsaidiaje

 5. Ahsante Mr Fadhili ,endelea kufanya uponyaji thawabu yako iko kwa baba,barikiwa sana

 6. hizo kiliniki za meno zinapatikana wapi dokta

 7. Membe Membe Membe Membe says:

  Ubarikiwe kwa kutuwezesha kupata elimu bora kwa afya zetu

 8. Sawa nahii nko pmja nayo tuko sambamba

 9. Ana Mtambo Ana Mtambo says:

  Asante sana,naanza sasa hivi.

 10. Zaina Musa Zaina Musa says:

  Assante kwakutuelewesha

 11. Glory Godson Glory Godson says:

  Dr jino langu alijatomboka ila linauma

 12. Angel Lucas Angel Lucas says:

  Ahsante kwa ku2elimisha

 13. Amen Mutumishi wa MUNGU pauro kuw atakia mema watu ,pia kuwatanguriza ni ibada,,na ni zaidi ya upendo kwa hiyo mamirioni ya watu wanaopona na Ku barikiwa wanakuombea BARAKA TELE PIA MAISHA ,marefu pokea kwa jina ra MWENYEZI MUNGU ,MUUMBA MBINGU NA inchi

 14. Tauc Said Tauc Said says:

  MUNGU akubariki Dr fsdhili

 15. John Malapwa John Malapwa says:

  Asante sana,Dk…!!

 16. Yuda Mwidete Yuda Mwidete says:

  Asante sn docta kwa elim yako nzur na mimi jino langu linaniuma ngoja nijaribu

 17. Ahsante sana Dr. Fadhili una thawabu zisizo kifani kwa Mwenyezi Mungu kwa kutusaidia sisi watu wake
  Mungu akuzidishie maarifa zaidi na moyo wa kuendelea kutufundisha

 18. dawa ya kuzibua masikio dkt ipi nisaidie

 19. Asante kwa elimu mungu akubarik

 20. Ally Abdul Ally Abdul says:

  Kwaiyo mwalim mtu akiwa na maji na chuvi ya kutosha mwilin maumivu ya jino kwake yatakua hayapo

 21. Rashid Ubabu Rashid Ubabu says:

  Inaleta raga kudumisha mira

 22. Asante kwa dawa, japo dawa ya jino hata kama limetoboka inapatikana na hakutakuwa na jino jingine la kuuma ikitumiwa

 23. Juma Hory Juma Hory says:

  Dawa njyengine unga wakarafiuu

 24. daah nishang’oa ma3 ndo najua

 25. Asante Doctor
  Kama utapata muda tudaidie na dawa ya sikio

 26. Asanteni sana maana haya meno duh

 27. Betty Powl Betty Powl says:

  As ante kwa somo zur

 28. Faudhia Ally Faudhia Ally says:

  Mungu akubariki dk

 29. Mufti Muft Mufti Muft says:

  Pilipili na chumvi hayo masihara pilipili uaniweka kwenye jino itulie tu mdomoni itawasha kwa dakika ngapi

 30. Mercy Denic Mercy Denic says:

  Ahsante kwa elmu yako

 31. Asha Abdalah Asha Abdalah says:

  Amina mungu akupe afya kila siku uweze kuelimisha mamii

 32. DAWA NYINGINE YA JINO NI UTOMVU WA MPAPAI UNAWEKA KWENYE JINO LINALOUMA

 33. DAWA NYINGINE YA JINO NI UTOMVU WA MPAPAI UNAWEKA KWENYE JINO LINALOUMA

 34. Ahsante mungu akubaliki sana

 35. Ubarikiwe na bwana kwa elimu yako nzur

 36. Ubarikiwe na bwana kwa elimu yako nzur

 37. Mmmmhahaha sijui Ila kwaneno zima naona kama kung’oa ndo,suluhu,

 38. Mmmmhahaha sijui Ila kwaneno zima naona kama kung’oa ndo,suluhu,

 39. Barikiwa mungu akuongezee ufahamu

 40. Barikiwa mungu akuongezee ufahamu

 41. Shinta Nzuki Shinta Nzuki says:

  doctor vp kwa jino lilokatka

 42. Shinta Nzuki Shinta Nzuki says:

  doctor vp kwa jino lilokatka

 43. Asante kwamaan Ninasumbuliwa najin ntaufata ushauliwako

 44. Samahn, hiv kwa wenye tatizo la kutosikia vizur upande mmoja, Dawa yakutumia nzur kama ni ipi ila sikio haliumi??

 45. Mariam Komba Mariam Komba says:

  Asante mana uwanaumwa sana meno

 46. Barikiwa kwa tiba, chumvi ya baharini ni sawa na za madukani?

 47. Lucy Mlowe Lucy Mlowe says:

  Asante sana kwa kutimiza kila wakat.

 48. Ubarikiwe sana kwa matibabu unayotupatia kila wakati

 49. Weeee jino halina dawa, hii unatuliza tu………

 50. Mwanangu meno yake yameanza kutoboka na fizi zinatoa usaha na kuvimba je nitumie dawa ipi?

 51. Asante sana Ubarikiwe

 52. Ahsante.Mungu akulipe kwa hili

 53. Anna Utou Anna Utou says:

  Asante sana docta kwa Ushauri wako

 54. Asante sana doctor kwani mada umeileta muda muafaka naumwa sana na jina na nilikua sijui dawa.

 55. Mke wangu linamsumbuaga kweli

 56. Merry Kundy Merry Kundy says:

  asante,kwa ushaur

 57. Glory Msechu Glory Msechu says:

  Dah mi ndo tangu nimengoa now yanauma yote at a nkinywa maji yanauma Chakula cha moto yanauma sina raha kabisa yapo kama yamekufa ganzi

 58. Amina Adam Amina Adam says:

  Asante nasumburiwa sana najino

 59. Anna Laulent Anna Laulent says:

  Asante kwa elimu hiyo itatusaidia

 60. Na meno kama hayajatoboka ila ukitafuna kitu yanauma unaweza kutumia dawa hizo?

 61. Tunakuthamini na kukuombea kwa Mungu maana unatusaidia mnooo

 62. Mimi nasumbuliwa na jino

 63. Weston Mbuba Weston Mbuba says:

  Naongezea dawa nyingine. Majani ya mpingo.

 64. Asante dokta kwa somo

 65. Hope Malaki Hope Malaki says:

  Stella Severine Shayo

 66. Magnus Frank Magnus Frank says:

  Asante maana mimi ni mmoja wa shida ya me no

 67. barikiwa doctor kwa elimu

 68. Juma Said Juma Said says:

  du hizi dawa bana

 69. Haji Gora Haji Gora says:

  Hongera kwa kutupa dawa

 70. Anna Mozess Anna Mozess says:

  Çhunvi yabahari niipi

 71. Ubarikiwe sana MTU wa Mungu

 72. Asante dokta kwasomo maana mimi meno manne amna mdomoni

 73. Hawa Rajab Hawa Rajab says:

  Asante na shukrani kwa kutupa maarifa

 74. Asante Sana Mungu akuvariki

 75. Shukurani kwa elimu uliyotupatia

 76. Mungu akuongoze asant kwa tiba

 77. Asia Musa Asia Musa says:

  Na kwajino lilotoboka pia dawa hizi zasaidia?

 78. Asante 0764 854639

 79. Temba Agness Temba Agness says:

  Asante sana doctor,mungu aendelee kukutia nguvu na maarifa yakutusaidia

 80. Temba Agness Temba Agness says:

  Asante doctor navipi kuhusu tatizo la kiungulia maana mimi ndougonjwa wangu sidhubutu kula chakula chamafuta mengi au Vitu vichachu

 81. Asante kwa somo zuri nimejifunza mengi.

 82. Prisca Jombe Prisca Jombe says:

  Ubarikiwe sana kwa kuwafundisha watu

 83. Asante ubarikiw xana?

 84. Mimi ugonjwa wa meno unapona maramoja ndani wiki nipo mtwara masasi pigA 0716829416 naitwa dk.Rajabu ni docta wamagonjwa sugu

 85. JuCha Enzi JuCha Enzi says:

  Dawa ya jino kung’oa tu

 86. Asante kwa kutujuza

 87. Ester Msangi Ester Msangi says:

  Jamani dawa za asili bwana naziaminia hebu tuzitumie

 88. aksante doctor umetuhabarisha.

 89. Neema Markob Neema Markob says:

  Thnks For Your Idea

 90. Ahsante Xan Doctor Kwa Uelimishaj Wako Man Na Ndugu Yangu Hapa Yey Kila Cku Ni Kuumwa Jino 2 Had Huruma Ameshamez Dawa Zote Za Maumivu Had Hazmsaidii Ten Xa Hvi.

 91. Shukrani kwa elimu

 92. Muu nitatumia mwanangu meno yote nimabovu alikunywa sana dawa za hosptal

 93. Asante Dokta Kwa Elimu Vip Dawa Ya Vidonda Vya Tumbo

 94. Na Majani ya mpapai

 95. Kwa tiba hii hatung’oi meno teeena!!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *