Dawa ya Uchafu Ukeni

Dawa ya Uchafu Ukeni

Kwa kawaida mwanamke hutokwa na majimaji mepesi (vaginal fluids) yenye rangi nyeupe au ya njano.

Inapotokea anatokwa na majimaji yenye ute mzito wenye rangi nyeupe au kahawia na yanatoa harufu kali na muwasho, hiyo huwa ni ishara ya ugonjwa uitwao wa kutokwa uchafu ukeni ujulikanao kwa kitaalamu kama ‘Vaginosis’.

Mwanamke mwenye tatizo hili hujisikia vibaya na anaweza akaacha kushiriki tendo la ndoa ama kwa kuhofia maumivu au kwa kuona aibu kwani mwanaume ni vigumu kuvumilia harufu hiyo au hata kuuona tu huo ute ute kwani humjengea hisia kwamba mwenza wake atakuwa na magonjwa ya zinaa au si mwaminifu kwa ujumla.

Kinachosababisha kutokwa na uchafu ukeni:

• Kuwa na wapenzi wengi
• Baadhi ya dawa za uzazi wa mpango
• Kusafisha uke kwa kutumia dawa zenye kemikali
• Uchafu
• Uvutaji sigara
• Pombe
• Maambukizi ya Bakteria au bakteria wabaya wanapozidi ukeni

Dalili

• Kutokwa na uchafu usio wa kawaida
• Kutokwa na uchafu wenye harufu kali kama shombo ya samaki au kitu kilichooza
• Kuwashwa sehemu za siri na ndani ya uke
• Uke unaweza kubadilika na kuwa na rangi nyekundu
• Maumivu sehemu za siri wakati wa kukojoa
• Maumivu makali chini ya kitovu
• Kutokwa uchafu uliochanganyika na damu

Matibabu

Mara uonapo dalili hizo unashauriwa kwenda kumuona daktari haraka iwezekanavyo kwa vipimo zaidi na dawa zaweza kuwa ni za kunywa au za kupaka.

Pia unaweza kutumia dawa za asili zifuatazo:

1. Kitunguu Swaumu

Dawa ya Uchafu Ukeni

Kitunguu swaumu ndiyo dawa ya asili nzuri kuliko zote kwa ajili ya maambukizi ya maambukizi ya bakteria kwa wanawake. Kitunguu swaumu ni antibiotiki ya asili na hufanya kazi ya kuua bakteria wasababishao huu uchafu ukeni bila shida yoyote.

Menya punje 3 au 5 za kitunguu swaumu, zipondeponde kidogo na uzifunge vizuri ndani ya kitambaa laini na ingiza ndani ya uke wako kwa masaa 6 hivi kisha ukitoe.

Pia menye punje 6 za kitunguu swaumu na uzikate vipande vidogo vidogo (chop) na unywe na maji nusu lita asubuhi ukiamka au usiku unapoenda kulala kwa wiki mbili mpaka tatu.

2. Mtindi

Dawa ya Uchafu Ukeni

Chukua mtindi ujazo wa kijiko kidogo cha chain a utumbukize ndani ya uke wako na uache huko usiku mzima. Mtindi una bakteria wazuri wanaohitajika ukeni kuweka sawa usawa wa PH (alikalini na asidi) na hivyo kuondoa maambukizi.

Pia unashauriwa kula tu huu mtindi mara mbili kwa siku kuongeza kinga ya mwili wako kwa ujumla dhidi ya magonjwa mbalimbali

3. Siki ya tufaa

Dawa ya Uchafu Ukeni

Chovya pamba ndani ya siki ya tufaa (apple cider vinegar) na uweke ndani ya uke kwa dakika 15 hadi 20 kila siku na bakteria wabaya wote watakufa.

4. Uwatu

Dawa ya Uchafu Ukeni

Loweka kijiko kidogo cha mbegu za uwatu (fenugreek seeds) ndani ya maji glasi moja na uache kwa usiku mzima. Kesho yake asubuhi maji haya yaliyolowekwa mbegu za uwatu kabla ya kula au kunywa chochote.

Uwatu husaidia kuweka sawa homoni za mwili na kuweka sawa mzunguko wa hedhi.

5. Maziwa na binzari

Dawa ya Uchafu Ukeni

Changanya kijiko kimoja cha chai cha binzari (manjano) ya unga na kikombe kimoja cha maziwa ya moto na unywe yote. Fanya hivi mara mbili kila siku mpaka tatizo litakapoisha.

6. Lemonade

Dawa ya Uchafu Ukeni

Lemonade inaandaliwa kwa kutumia limau na asali na mdalasini ya unga kidogo, nayo inaandaliwa hivi:

*Chukua asali mbichi nusu Lita

*Chukua limau kubwa 12 au zaidi, zikate katikati kila moja. Zikamuwe moja baada ya nyingine kupata maji maji ya limau mpaka umepata ujazo wa nusu lita.

*Kwenye sufuria nyingine kubwa changanya mdalasini ya unga vijiko vikubwa 10 na maji lita 2 na nusu na uchemshe kama chai kisha ipua na uchuje na usubiri ipowe iwe ya uvuguvugu kidogo.

*Sasa changanya pamoja asali nusu lita, juisi au maji maji ya limau nusu lita, maji ya uvuguvugu ya mdalasini lita 2 na nusu ongeza na ya maji ya kawaida lita 1 kupata lita 5, chuja vizuri. Ihifadhi katika friji isiharibike.

Kunywa robo lita (ml 250) kutwa mara 2 kwa siku 10 kwa mtu mzima na glasi ndogo moja kwa siku kwa mtoto wa miaka miwili mpaka kumi.

Unaweza pia kuongeza majani kidogo ya mnanaa (mint) na mbegu za shamari (fennel seeds) ili kuongezea radha na harufu nzuri. Kunywa juisi hii kila unapokuwa umepata chakula cha mchana cha nguvu au cha jioni.

7. Jeli ya mshubiri (aloe vera jel)

Dawa ya Uchafu Ukeni

Ingawa jeli fresh ya mshubiri haitibu moja kwa moja tatizo la kutokwa na uchafu ukeni inaweza kuwa msaada mkubwa katika kupunguza maumivu na muwasho ukeni.

Chana kipande kidogo cha jani la mmea huu na ukamue kidogo kupata maji maji yake na upake vizuri taratibu ndani ya uke mara mbili kwa siku kwa majuma kadhaa hadi muwasho utakapoisha.

8. Bamia

Dawa ya Uchafu Ukeni

Bamia husaidia kuondoa maji maji na makohozi kwenye mfumo wako wa mwili.

*Chukua bamia gramu 100
*Zikatekate vipande vidogo vidogo
*Weka kwenye sufuria ongeza maji nusu lita na uchemshe mpaka maji yamebaki robo ndani ya sufuria
*Ipua na uchuje
*Gawanya hayo maji uliyochuja katika sehemu mbili na unywe sehemu moja asubuhi na nyingine jioni kila siku mpaka umepona

9. Komamanga

Dawa ya Uchafu Ukeni

Komamanga ina sifa ya kuwa dawa na inaweza kutumika kama dawa ya kutibu uchafu ukeni. Vyote majani yake au mbegu zake vinaweza kutumika kwa ajili hii.

Kunywa glasi moja ya juisi ya komamanga kutwa mara moja kwa mwezi mmoja hivi mpaka umepona.

MAMBO MHIMU YA KUZINGATIA:

Zingatia dawa peke yake hazitofaa kitu bila kuzingatia ushauri au masharti mhimu yafuatayo:

1. Kunywa maji mengi kila siku kuanzia glasi 8 hadi 10
2. Tumia zaidi vyenye vitamini B, C, D na E
3. Tumia sana matunda hasa machungwa, limau, ndizi na vitunguu
4. Punguza vyakula vyenye wanga
5. Acha kutumia vidonge vya uzazi wa mpango, hii ni kwa sababu vidonge hivi vinasemwa huwa vinasababisha kushuka kwa kinga ya mwili na kukufanya mrahisi kupata maambukizi ya fangasi.
6. Epuka mapenzi kinyume na maumbile
7. Acha kutumia sukari na badala yake tumia asali
8. Usitumie chokoleti na vitu vingine vya namna hiyo
9. Kuwa na mpenzi mmoja tu
10. Pendelea kujiweka msafi muda wote
11. Oga maji ya moto
12. Acha vinywaji baridi, acha pia chai ya rangi na kahawa
13. Acha vilevi
14. Acha matumizi ya pafyumu hasa maeneo ya huko

Mhimu: Kama una swali au unahitaji ushauri zaidi comment hapo chini nitakujibu.

Je umewahi kuugua ugonjwa huu na ukapona? kama ndiyo ulitumia dawa gani? nitashukuru ukiniambia dawa uliyotumia mpaka ukapona ili nisaidie na wenzako wengine.

Kama unahitaji dawa za asili zilizoandaliwa tayari kwa ajili ya kutibu uchafu ukeni au fangasi ukeni niachie tu ujumbe WhatsApp +255769142586. Ofisi yangu inaitwa Victoria Home Remedy ipo Buza Sigara Temeke Dar Es Salaam, unaingia kupitia jet corner (uwanja wa ndege) au tandika.

Una ushuhuda wowote kama matokeo ya kutumia blog hii? Kama ndiyo toa ushuhuda wako ili uwe msaada kwa wengine, kutoa ushuhuda wako bonyeza hapa.

Tafadhari SHARE post hii kwa ajili ya wengine uwapendao.

(Imesomwa mara 17,972, Leo peke yake imesomwa mara 343)

You may also like...

1,409 Responses

 1. 0716930331whatsap

 2. Ever Mollel Ever Mollel says:

  na hicho kitunguu swaumu naweka kwa cku ngapi

 3. Mariam Saidy Mariam Saidy says:

  Hzo dawa zote ulizoorodhesha hazina madhara kwa mjamzito??

 4. Focas Neema Focas Neema says:

  Asante sana umetusaidia wanawake

 5. Tino Bea Tino Bea says:

  Dk niunge whsp 0765278758

 6. Janeth Mzoma Janeth Mzoma says:

  Somo zuri Dr barkiwa

 7. Aisha Chande Aisha Chande says:

  0714937352 whatsapp

 8. Rose Jackson Rose Jackson says:

  Asante kwa somo janga la wengi

 9. Asante sana doctor kwa elimu nzuri nimeielewa naenda kuitumia Barikiwa sana japo nikishindwa nitakucall whatsap

 10. Pendo Daudi Pendo Daudi says:

  Izo punje za kitunguu swaum unazoponda unaziwek kweny maji afu unakunywa au naomb mnielewesh jamn sijaelew hapo

 11. Rose Bahati Rose Bahati says:

  Mi naomba kuuliza mtindi huwo upi au inayouzwa madukani

 12. Alice Peter Alice Peter says:

  Doctor naomba kuuliza mm narafiki yangu anasumbulowa sn tumbo sn akifanya mapenzi anaumia upande wa kushoto na dawa katumia hadi kachoka ss afanyanye doctor

 13. Wasaidie Dada zetu ndugu yangu, wengi wanateseka sanaa

 14. Dr mm natatizo nikimaliza kufanya mapenzi natokwa na majimaji chin ya uke

 15. Maria Mdege Maria Mdege says:

  Niko tanga nitapataje dawa hizo

 16. Somo zur tunashukulu

 17. Johari Moshi Johari Moshi says:

  Dr mi nna tatzo lingne nnje ya hko nna kuna mtu wngu wa karb ana tatzo LA kupiga chafya sna lkn ni kwa baaz ya maeneo akikaa sna ndo hpiga chafya ila ndo hatujajua tatizo ni ñn

 18. Dokta Mimi nashika mimba lakini zikikaribia mwezi zina toka tatizo nini

 19. Yusuph Saidi Yusuph Saidi says:

  Mungu akubariki brother uwenamoyohuohuo

 20. Mm nikiingia kwenye sikuzangu huniuma sana tumbo utanisaidia vp

 21. Asante somo limeeleweka sana

 22. Uwatu ndiyo tunda gani naomba nifahamishwe cfaham

 23. Maryam Salum Maryam Salum says:

  Ahsante kwa ushaur

 24. Betty Powl Betty Powl says:

  Asante kwa somo zuri Dr, ubarikiwe

 25. Duh tutengenezeeni vizuri hizo sehemu mana ndio starehe zetu wengine hatunywi pombe wara sio washabiki wa mpira!!

 26. Asante kwa dawa dr. Mungu akubariki. Hii ya ki2nguu swaumu mama mjamzito anaruhusiwa ku2mia dr?

 27. Fetty Frida Fetty Frida says:

  Asante kwa ushauli wako nzuri Dk

 28. Hyo ya mafuta ya nazi ya uwasho haiathiri kw mja mzito?

 29. dada mm nili2mia jaman nljuta kuzaliwa k ilibana af ikavimba nkitaka kwnd kukojoa yan hd nalia kutembea unatembea kama vle una kaswend nd nlkuwa napona au maana nliweka xk mja 2 lakn mmh

 30. Hawa Numbi Hawa Numbi says:

  Asante sana Dr kwa kutugaiya elimu mung akufanyie wepes ktk kira jamb

 31. Katika vitu vinavyo changia kusababisha fangasi kwa bibi ni pamoja na kujisafisha na kidole mpaka huko ndani kabisa nakumbuka kuna kipindi tatizo hili lilinipata siku moja nilipata ushauri kwa docta mmoja nikaacha kujisafisha kwa kutumia kidole mpaka Leo ni mwaka wa saba sijawahi kupatwa na tatizo hili tena alisema sehemu za ndani zinajisafisha zenyewe

 32. Happy Temu Happy Temu says:

  Dr asante ,naomba kuuliza kutumia vitungu swaumu kwa kunywa vinatibu au mpaka utumbukize tena ukeni? Asante

 33. Docter mm nmechomasindanoya uzaziwampango ya miezimitatu tu lakn nilikuwanaendasawa kwenye siku zangu sasa hv miezimitatu umeishia lakn nmenda kwenye sikuzangumwezimzm nifanyenn doctailiikate

 34. Saumu Swai Saumu Swai says:

  Jamani hili tatizo lipate ufumbuzi limekua sugu mno kwa wanawake
  Kuna baadhi ya Dawa sijui inapatikana kwa wote nitaipiga picha niirushe ukichemsha utakunywa na kitawadhia inasaidia kama si kutibu
  Kwa wale wa Kilimanjaro inaitwa kingili inayoharufu na ni chungu

 35. Asante kwa somo Dr

 36. Farida Fredy Farida Fredy says:

  M nasumbuliwa na hlo tatzo na nmetumia vdonge lakn cjaoona dalili ya kupona

 37. Hongera Doctor kwa somo zuri nikweli usione wanawake tunatembea matatizo nimengi.

 38. Ndina Bula Ndina Bula says:

  Asante dokta napenda kujua kama husumbuliwi na matatizo hayo unaweza kutumia kama kinga ?

 39. Princess Mam Princess Mam says:

  Asantye doctor kwa somo zuri

 40. Editha Mkude Editha Mkude says:

  Pole na kazi, asante kwa ushauli. Naomba kujua endapo utatumia uwatu bila kipimo unaweza kupata madhara?

 41. Dk mimi nina tatizo la uti, nimetumia dawa za hospital mpaka nimechoka lkn cjapona, nimepima magonjwa ya zinaa yote sina, unaweza kunixhauri nitumie dawa gan ya asili

 42. Na je? Kwa mtu mwenye mimba anaruhusiwa kuthmia kitunguu swaumu docter

 43. Hyo alovera kwa mja mzito inafaa kueka huko chini??kwa wenye uwasho tu?

 44. Sia Mangia Sia Mangia says:

  Watu wanasema eti mwanamke akishafunga siku zake za hedhi yaani kufikia ukomo wa hedhi hatakiwi kutokwa na uchafu wowote ukeni ni kweli?

 45. Gerald Emma Gerald Emma says:

  Dr asante sana kwa somo zuri kwa maana nimesha pata mkombozi kwa tatizo langu

 46. Ahsante sana doctor

 47. Leilah Wila Leilah Wila says:

  0746045538 watxap

 48. Naima Juma Naima Juma says:

  Samahan docta m nmjifungua nnamiez 4sasa lkn mgongo waniuma sana siwez kuinama jaman nahitaji msaada naumia sana kiuno na mgongo tafadhal nisaidien

 49. Nothing to add. Thank you so much doctor

 50. Saumu Swai Saumu Swai says:

  Doct naomba utupe uhakika nilipata elimu kwa wataalam wa Dawa za asili kua hili tatizo Hakuna tiba za hospital ila wakasema chukua majani ya kiasi ya mlonge na alovera au shubiri majani 3 saga kwenye blender utapata juice unywe vijiko 3 × 3 kwa siku utumie kwa siku 3 au 5

  • Siyo kweli kwamba hakuna tiba hospitali huyo mtaalamu alikudanganya, dawa hizi nimeziandika hapa zinatibu hilo ila kila mmoja ana historia ya dawa fulani iliyomponya. Kuna wengine wanapona na dawa za hospitali wengine za asili, hivyo hivyo tuendelee kutafuta dawa nyingine maana ni tatizo sana kwa sasa

 51. Asante doctor nitakutaft

 52. Tumy Nnko Tumy Nnko says:

  Shukran kwa somo dr

 53. Mossy Lamar Mossy Lamar says:

  Jaman nna swal v2nguu swaum ukishaviponda na kuvifunga kwenye ktambaa lain na kukiingiza uken hakiwez kuzama kwel na unakitoaje

 54. Mimi ninajisafisha na kidole hata nikiwa kwenye siku

 55. Habiba Daudi Habiba Daudi says:

  jee njiti nayo inamadhara kama vidonge?

 56. Rebeka Jonas Rebeka Jonas says:

  Mungu akubariki Dr. kwa kutujuza mengi.ubarikiwe.

 57. Mary Anthony Mary Anthony says:

  je vitunguuo sahumu na weka kweny uke kvp yan cjaeelewa na nkwamuda wa cku ngap niweke

 58. Fau Abdallah Fau Abdallah says:

  Hahahaaa paskazia umenifurahisha

 59. Hizi punje sita za kunywa na maji unavitia kwenye maji unakunywa kwa wakati mmoja vyote au kidogokidogo?

 60. aisee wanawake tuna matatizo mengi jaman!!hv vitu mbona haviwapati wanaume??mungu tusaidie asante dr ubarikiwe mm nauliza tu hicho kitunguu swaumu ukikiweka na kikazama kabisa hafi kwenye cervics itakuaje????

 61. Docta me naomba kuuliza,
  Nikikaribu period nawasha nikishaingia na kumaliza tatizo LA kuwazha halipo tena je ni khali ya kawaida! Au in tatizo

 62. doctar MUNGU azidi kuku bariki maana msaada wako elimu yako juu ya dada zetu inawasaidia sana mana wengi wanateseka sana na hivi hali

 63. Nana Reshy Nana Reshy says:

  Nimependa somo lako doctar mm tatizo langu ni michubuko kwenye mapaja yanakuwa kama mapunye yanawasha sana nimetumia dawa bado nisaidie doctar

 64. Saidi Msangi Saidi Msangi says:

  Tuwekee na makala ya tiba mbadala ya Malaria mana ni tatizo kweli .

 65. Kisa Gorge Kisa Gorge says:

  Mungu akubarik kwa kutusaidia hasa sisi wanawake

 66. Teddy Kimath Teddy Kimath says:

  Asante docter kwa somo zuri….

 67. Ni vizuri pia ukisema na madhara take

 68. Abel Martin Abel Martin says:

  Asanteni mb,&mabwn swali na ulizaje ? Mwanaume atapata madhara gani atapo jamiana na mwanamke mwenye vaginal fluids

 69. Wini Pati Wini Pati says:

  Nimeelewa somo vizuri hiyo dawa inafanya kazi kwa muda gani na madhara yake ni yapi unapoitumia pia inauzwa bei gani

  • Kama unahitaji dawa za asili zilizoandaliwa tayari kwa ajili ya kutibu uchafu ukeni au fangasi ukeni niachie tu ujumbe WhatsApp +255769142586. Ofisi yangu inaitwa Victoria Home Remedy ipo Buza Sigara Temeke Dar Es Salaam, unaingia kupitia jet corner (uwanja wa ndege) au tandika.

   Mhimu: Kama una swali tu au unahitaji ushauri zaidi comment hapo chini nitakujibu. Nitafute WhatsApp ikiwa tu unahitaji dawa toka kwangu tofauti na hapo uliza hapa hapa nitakujibu.

 70. Mamuu Muddy Mamuu Muddy says:

  Je ukitumia punje za vitunguu swaum kila cku kwa kunjwa na maji bila kuweka kwenye uke je inasaidia

 71. Asante dr,najifunza

 72. Happy Shayo Happy Shayo says:

  Hiyo dawa inapatikanaje na inagharimu sh ngapi?

  • Kama unahitaji dawa za asili zilizoandaliwa tayari kwa ajili ya kutibu uchafu ukeni au fangasi ukeni niachie tu ujumbe WhatsApp +255769142586. Ofisi yangu inaitwa Victoria Home Remedy ipo Buza Sigara Temeke Dar Es Salaam, unaingia kupitia jet corner (uwanja wa ndege) au tandika.

   Mhimu: Kama una swali tu au unahitaji ushauri zaidi comment hapo chini nitakujibu. Nitafute WhatsApp ikiwa tu unahitaji dawa toka kwangu tofauti na hapo uliza hapa hapa nitakujibu.

 73. Zulfa Sigato Zulfa Sigato says:

  Samahan docta, hiko kitambaa baadae kitatoka chenyewe au inakuaje………

 74. Linah Fredy Linah Fredy says:

  Jamani hakuna dawa nzuri kama vitunguu saum tutimie

 75. Ndungu yangu Ana mpangilio mzuli wa hedhi na umtoka wa kati wowote, naaki shiliki sana tendo Otokwa na damu naimba msaidie jamani

 76. Asante DK,wiki yatufaa inapatikana wapi?

 77. Rehema Nkini Rehema Nkini says:

  Deto ya maj kwa kunawia huko ina tatizo?

 78. Mimi shidayangu ni ukeni kujisikia maumivu muda watendo la ndoa kuota ndoto mbaya pindi ninapo kalibia hedhi kujihisi kama mwenye ujauzito kutopenda tendo la ndoa

 79. Ahsante sana Mungu akujalie; nimekuelewa.

 80. Ni bonge la somo kwakweli kwa kina mama na wadada na lipo kwa asilimia zake

 81. Docta ukwaju unatibu nn

 82. Samahan mm nataka kjua hzo aina za dawa zlizoolozeshwa hapo unatmia zote au unatmia moja kat ya hzo?

 83. Pia wakati tunapoenda haja kubwa kwa wanawake, jitahidi wakati wa kutawaza uanze kusafisha mbele kwanza ndo umalizie na kusafisha nyuma!! Maana kuna bakteria wa nyuma ambao hawatakiwi kuingia mbele wakiingia wanashambulia wale bakteria wa mbele na kuharibu kinga ya eneo hilo!! Ukizingatia usafi na kunywa maji mengi sana tatizo la uti halitakusumbua au hata ukiwa nalo litaisha!! Tunywe maji mengi sana!!

 84. Frida Peter Frida Peter says:

  Nahitaji hiyo sawa ya uwatu

 85. Mohd Juma Mohd Juma says:

  kwa wale wanaonyonya uke kama huu watapata madhara gani?

 86. Hili limekuwa no tatizo sugu kwetu wanawake

 87. Rose Johari Rose Johari says:

  Pia axante toka nmezaliwa ckuwai kujua ni vibaya kunawia sabuni uken

 88. Waziri Munga Waziri Munga says:

  Je kama nipo mukoani ntapataje huduma yenu naomba kuelekenzwa

 89. Mimi nimjamzito hali kama hii hua inatokea mara kwa mara. Maji mazto kama mtindi na muwasho. Clinic walisema uti. Nikapewa amoxlyne ila bado linajitokeza.

  • Kuna sindano nenda onana na dr bingwa uchome maana ikikolea inaleta uchungu wa uongo unaona kabisa kama unaenda leba kumbe ni hiyo.mimi ilinitokea nikatibiwa ikaishaa.

 90. Maria Kimaro Maria Kimaro says:

  Asante, ila mm naomba kuuliza au naomba utusaidie kutuelezea vitu vya asili vinavyo weza kuzuia uzazi mbali na kalenda pamoja na kuangalia ute. Asante

 91. duh ukiwaon wanatembea km malaik vile lkn ndan yao ni hatr tupu…..poln dad zang

 92. asante dockta bora umenifungua kwani tatizo hili limenitesa kwa muda mrefu nasikupata jibu la tatizo langu ila leo nimelipata ntaanza kutumia kwani huwa napata maumivu makli mno wakati wa tendo la ndoa nakutokwa uchafu ukeni

 93. nahitaji pia hiyo ya uwatu na kinga ya uzazi kienyeji km inapatikana

 94. Mm nauliza hiza tiba unachagua rahisi na ww au hayo yote yafuatane?

 95. Ashura Sige Ashura Sige says:

  Ikiwa mtu hanahamu yatendo landoa inakunn

 96. Kama uko mbali unapataje Dawa?

 97. Jully Ken Jully Ken says:

  Mtindi ndo mgani in English?pia komamanga in English ndo nini?

 98. Jully Ken Jully Ken says:

  Doc haki naomba unizaidie ama yeyote anayeelewa haya majina nin English pls;BAmIA,KOMAMANGA,Na MTINDI plzzzzz

 99. Juma Hamis Juma Hamis says:

  Nashukuru Doctor kwa msaada wako

 100. Rehema Mpapa Rehema Mpapa says:

  doctor asante kw ushauri,naomba kuuliza kama unakua na tatizo la kuwa na maji meng wakat wa tendo la ndoa kuna dawa ya kusaidia kupunguza hiyo ali? wengne wanasema kuna vidonge vya kukausha je ni kwel vipo?samahan kw gazet doctor!

 101. Wasaidie wenye jasho kali

 102. Jaman Dr hivi madhara gani naweza kupata maana nina miaka 4sasa sifanyi mapenzi yaan hata wazo sina niliachana na mwenzangu kwa tabia zake,

 103. Wengi hawafuatilii mambo yamcngi kama haya mitandaon zaid ya umbea,Dr uko vzr xana

 104. Upendo Lwena Upendo Lwena says:

  Mm ninarafiki yangu alitumia dawa za uzazi WA mpango na hajaingia hezi anamiezi miwili naomba ushauli

 105. Neema Simo Neema Simo says:

  Mbona hizo namba zako hazitumiki. WhatsApp

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *