Haya ndiyo maajabu 24 ya asali yenye mdalasini ulikuwa huyajuwi bado

Haya ndiyo maajabu 24 ya asali yenye mdalasini ulikuwa huyajuwi bado
Haya ndiyo maajabu 24 ya asali yenye mdalasini ulikuwa huyajuwi bado

Asali ni tiba karibu kwa kila ugonjwa. Matumizi ya asali kama tiba kwa magonjwa mbalimbali ni kitu ambacho kinafahamika kwa karne nyingi zilizopita duniani kote. Vitabu vingi vya zamani vimeandika namna watu walivyotibiwa magonjwa mbalimbali kutokana na asali.

Inapotokea dawa za asili mbili zinachanganywa pamoja katika uwiano fulani, hutokea kuundwa dawa nyingine nzuri ambayo ni tiba kwa maradhi mengi sana. Moja kati ya muunganiko wa dawa hizo za kushangaza ni pale asali inapochanganywa na mdalasini.

Muunganiko huu umekuwa ukitumika kwa karne nyingi kutibu magonjwa mengi mwilini na kuimarisha afya ya mwili kwa ujumla. Watu wengi wanakiri maajabu yaliyomo kwenye hii dawa asili ASALI YENYE MDALASINI.

Dawa hii ya asili ni maarufu kwa maelfu ya miaka katika tiba asili za China (Traditional Chinese Medicine – TCM), Ugiriki (Unani Medicine), India (ayurvedic) na Mashariki ya kati (The science of medicines based on natural treatment in the East – Tibb).

Kwa mjibu wa wataalamu wa tiba asili nchini China, mdalasini huongeza joto mwilini. Mdalasini hutengeneza joto mwilini lijulikanalo kwa kichina kama “yang”. Yang hutibu “yin” (yin kwa kichina humaanisha baridi). Wakati asali yenyewe kwa asili huweka sawa usawa wa joto na baridi mwilini.

mbegu-za-maboga

Haya ndiyo maajabu 24 ya asali yenye mdalasini ulikuwa huyajuwi bado

1. Huua bakteria

Asali ina sifa ya kudhibiti bakteria. Nadharia hii inathibitishwa na tafiti nyingi kadhaa. Asali hupigana dhidi ya maambukizi ya ndani nay a nje.  Mdalasini pia una sifa ya kuondoa vivimbe pia huondoa sumu mwilini.  Vinapoungana vitu hivi viwili vya asili vinatengeneza muungano mmoja mhimu wa dawa dhidi ya maambukizi ya nje.

2. Nzuri kwa ugonjwa wa moyo

Chakula sahihi, mazoezi ya viungo, na kuepuka kukaa kwenye kiti masaa mengi ni mhimu kwa ajili ya kuwa na afya nzuri ya moyo.

Kunywa kinywaji chenye asali yenye mdalasini mara kwa mara kunaweza kusaidia kuepuka ugonjwa wa moyo kwa kuzuia kuzibika kwa ateri.

3. Inatibu maambukizi kwenye kibofu cha mkojo

Asali yenye mdalasini ni dawa bora sana kwa kutibu maambukizi kwenye kibofu cha mkojo na bacteria wowote wanaoweza kushambulia kibofu cha mkojo. Mchanganyiko huu unasafisha kibofu na kukiacha safi hivyo kukupa mazingira ya kutokuumwa lolote katika kibofu chako cha mkojo.

4. Tiba ya baridi yabisi (Arthritis)

Watu wengi wanaripoti matokeo mazuri baada ya siku chache tu za kutumia kinywaji hiki chenye mchanganyiko wa asali yenye mdasini kutwa mara 2. Ili kutibu baridi yabisi ongeza kijiko kidogo kimoja cha mdalasini ya unga na kijiko kikubwa kimoja cha asali mbichi ndani ya glasi 1 ya maji ya uvuguvugu na unywe nusu glasi kabla ya chakula cha asubuhi na nusu glasi nyingine kabla ya kwenda kulala.

Utafiti huo ulifanyika katika chuo kikuu cha Copenhagen ambako wanafunzi walipewa asali yenye mdalasini ili kutibu baridi yabisi. Baada ya wiki 1 iligundulika kuwa wanafunzi 73 kati ya 200 walikuwa hawaonyeshi dalili tena za ugonjwa huo. Baada ya mwezi mmoja kila mmoja alikuwa amepona na kuwa na uwezo wa kutembea na kufanya kazi.

5. Hutibu Fizi kutoa damu

Watafiti nchini New Zealand wamegundua kuwa asali mbichi ikichanganywa na mdalasini inaleta ufanisi mkubwa dhidi ya fizi kutokwa damu, kuuma fizi, ganzi kwenye meno na maambukizi mengine katika fizi.

Unaweza kupakaa kwenye mswaki na utumie kama dawa yako ya kusafisha meno ili kupata faida hii.

6. Inatibu meno yanayotoboka

Hii kidogo inashangaza. Watafiti katika jiji la New York nchini Marekani wanasema asali inaweza kusababisha meno kutoboka. Hata hivyo wanasayansi wengine nchini New Zealand wanasema asali inaweza kuwa msaada katika kuzuia meno kutoboka kutokana na sifa yake ya kuua bacteria mbalimbali.

Namna rahisi ni kutumia mchanganyika wa asali yenye mdalasini kama dawa yako ya meno utumie kusafisha meno yako ili kuepuka meno kutoboka na kuoza pia.

7. Husaidia mfumo wa mmeng’enyo wa chakula

Husafisha utumbo mpana kwa kuondoa sumu na taka nyingine. Husaidia uzalishwaji wa bacteria wazuri kwenye utumbo mpana na kama matokeo yake huusadia mfumo wa mmeng’enyo wa chakula.

8. Huondoa gesi tumboni

Asali yenye mdalasini husaidia kulinda tumbo kwa kufunika kuta za tumbo. Kwa kusafisha mfumo wa bakteria wabaya huwa imesaidia kutibu maambukizi yoyote na hivyo kusaidia kutibu tatizo la tumbo kujaa gesi na asidi.

9. Husaidia kupunguza uzito

Kuna shuhuda nyingi zisizotiliwa shaka juu ya ufanisi wa asali yenye mdalasini katika kupunguza uzito. Asali na mdalasini vinapotumika pamoja, mchanganyiko huo huchoma mafuta kwa haraka sana.

Wakati huo huo mchanganyiko huu hushusha njaa na hivyo kumfanya mtu kujisikia ameshiba muda mrefu.

Angalizo hata hivyo, asali ni tamu na ina nguvu (kalori), hivyo ili kupunguza uzito unashauriwa usitumie zaidi ya vijiko vikubwa vitatu vya mchanganyiko huu ndani ya glasi moja ya maji ya uvuguvugu kwa siku, Ukizidisha tu unaweza kuongezeka uzito tena.

10. Huongeza akili

Watu wengi wanaripoti kuwa asali yenye mdalasini inawaongezea uwezo wao wa kukumbuka vitu. Asali yenye mdalasini hongeza uwezo wa ubungo kufanya kazi na kuongeza uwezo wa kumbukumbu.

11. Hutibu kansa

Ingawa bado haijathibitishwa kisayansi ni jinsi gani asali yenye mdalasini inatibu kansa lakini uwezo wake wa kuondoa sumu na vimelea vingine vya magonjwa (free radicals) kunaifanya kuwa na sifa hiyo ya kutibu kansa.

Baadhi ya watu wameripoti kupona kansa ya titi na kansa ya utumbo mpanakwa kutumia asali yenye mdalasini.

12. Inaongeza nguvu ya mwili

Asali ina madini na vitamini nyingi ndani yake, wakati mdalasini wenyewe una kalsium, chuma, vitamini C, vitamini K, manganizi na nyuzinyuzi (fiber).

Vinapoungana vitu hivi viwili hufanya dawa moja mhimu sana ya kuongeza kinga ya mwili. Kunywa chai yenye asali na mdalasini mara kwa mara kunaongeza kinga ya mwili, nguvu ya mwili na nguvu ya ubongo kwa pamoja.

13. Hutibu chunusi

Kupakaa asali yenye mdalasini kwenye ngozi yako yenye chunusi kutaondoa chunusi hizo bila kuchelewa. Asali hudhibiti bacteria na mdalasini hudhibiti maambukizi na huondoa sumu.

Mchanganganyiko huu husaidia asali kubaki juu ya ngozi kwa muda mrefu na hivyo kufanya uponyaji unaohitajika.

14. Hutibu kikohozi

Kuinywa asali yenye mdalasini ndani ya glasi ya maji ya uvuguvugu hupunguzu vyote kikohozi na kikohozi kikavu. Husafisha msongamano kohoni na kutibu kikohozi cha kawaida na hata kile kikavu.

15. Huzuia madhara ya kung’atwa na wadudu

Ni nzuri kwa ajili ya uvimbe au kuondoa maumivu yatokanayo na kuumwa na wadudu. Chukua kijiko kidogo kimoja cha asali na uchanganye ndani ya vijiko vijigo viwili vya maji ongeza na mdalasini ya unga nusu kijiko cha chain a upake juu ya sehemu ulipong’atwa na mdudu.

Maumivu hayo yataondoka mara moja.

16. Husaidia kuotesha nywele

Changanya kijiko kidogo kimoja cha asali ndani ujazo sawa wa mafuta ya zeituni na uongeza kijiko kidogo cha chai tena cha mdalasini ya unga kwenye huo mchanganyiko.

Pakaa mchanganyiko huo kichwani sehemu ambako nywele zimeanza kupotea na uache kwa dakika 15 kisha jisafishe na maji ya uvuguvugu na shampoo ya asili.

17. Hutibu lehemu (Cholesterol)

Matumizi ya mara kwa mara ya asali yenye mdalasini husaidia kupunguza lehemu. Pia husaidia kushusha shinikizo la juu la damu na kusafisha ateri zinazoziba.

Pia kubadili matumizi ya mafuta mengine na kuamua kutumia mafuta ya zeituni kutarahisisha kuweka sawa kolesto yako kirahisi zaidi.

18. Hutibu maumivu ya jino

Changanya kijiko kidogo kimoja cha chai cha mdalasini ya unga na vijiko vikubwa viwili vya asali mbichi na upake kidogo kidogo juu ya jino linalouma mara kadhaa kwa siku mpaka maumivu yatakapopotea.

19. Harufu mbaya mdomoni

Changanya kijiko kikubwa kimoja cha asali na kiasi kingine sawa cha mdalasini ya unga ndani ya maji glasi moja ya uvuguvugu na unywe mara tu ukiamka asubuhi. Hii itakutibu tatizo la harufu mbaya mdomoni na utapumua vizuri bila shida yoyote.

20. Hutibu uanithi na kukosa hamu ya tendo la ndoa

Jaribu na uone tofauti! Changanya vijiko vikubwa vitatu vya asali yenye mdalasini ndani ya glasi moja ya maji ya uvuguvugu na uache mchanganyiko huo kwa dakika 15 hivi.

Kunywa nusu glasi asubuhi kabla ya chakula cha asubuhi na nusu nyingine kabla ya kwenda kulala kwa siku kadhaa hata wiki kadhaa.

21. Huongeza kinga ya mwili

Ongeza kinga yako ya mwili na magonjwa hayatakugusa. Vyote asali na mdalasini hupigana dhidi ya bakteria na virusi na hivyo kufanya dawa nzuri ya kupigana na kuua bakteria wabaya na virusi.

Asali pia ina madini na vitamini mhimu nyingi hivyo kuupa mwili viinilishe mhimu unaovihitaji.

22. Hutibu mafua

Tumia mchanganyiko wa kijiko 1 cha chakula cha asali yenye mdalasini ndani ya glasi moja ya maji ya uvuguvgugu kutwa mara moja kila siku kuondoa chafya na kuvimba koo.

23. Hutibu Ugumba

Asali inaaminika kuamsha hamu ya mapenzi. Wapenzi wa jinsia zote wanashauriwa kunywa walau vijiko 2 vya chakula kila siku kabla ya kwenda kulala kila siku.

Mdalasini umetumika miaka mingi katika dawa za kichina na kihindi kuongeza uwezo wa uzazi kwa akina mama wenye kuhitaji kuzaa.

24. Faida nyingine lukuki

Kumbuka asali ni dawa karibu kwa kila ugonjwa na watu wamekuwa wakiitumia kutibu magonjwa mengine mengi bila idadi ikiwemo matatizo ya kisukari, kukakamaa kwa miguu na mikono, udhaifu wa jumla wa mwili, kuongeza kumbukumbu, vidonda vya tumbo, kutibu majeraha nk nk

Hayo ndiyo maajabu 23 ya asali yenye mdalasini ambayo ulikuwa huyajuwi bado.

Namna ya kuandaa na kutumia Asali yenye Mdalasini?

Kwenye lita 1 ya asali ongeza vijiko vikubwa vitano vya mdalasini ya unga na ukoroge vizuri kabla ya kuutumia. Uhifadhi mchanganyiko huu kwenye bakuli kubwa ili iwe rahisi kuukoroga tena vizuri kila unapotaka kuutumia.

Unaweza kuutumia katika maji au wenyewe kama ulivyo ukipaka juu ya ngozi au ukitumia kwenye vyakula kama mkate na kadharika. Kama utakunywa basi vijiko vikubwa vitatu ndani ya maji ya uvuguvugu glasi moja kwa siku inatosha.

Angalizo kuhusu mdalasini feki:

Kabla sijakuacha, ni mhimu sana nikueleweshe juu ya mdalasini hasa ambao hutumika kama dawa. Siyo kila mdalasini unaouona unaweza kukupa maajabu haya, mwingine ni sumu kabisa mwilini. Na watu wengi hawajuwi hili jambo.

(a) Ceylon cinnamon

Ceylon cinnamon

Ceylon cinnamon

Mdalasini ambao hutumika kama dawa hujulikana kwa kitaalamu kama ‘Ceylon cinnamon’ na kwa kawaida wenyewe huuzwa gharama sana. Huwa na radha tamu na harufu ya kuvutia zaidi, unatoka katika nchi ya Sri Lanka katika mmea ujulikanao kama Cinnamon Zeylanicum. Hujulikana pia kama mdalasini wa India.

Huwa na rangi ya kahawia (light brown), mwembamba na mlaini.

(b) Cassia cinnamon

Cassia Cinnamon

Cassia Cinnamon

Wakati ule ambao ni feki na ni sumu pia hujulikana kama ‘Cassia cinnamon’ ni mdalasini huu ambao katika baadhi ya nchi umepigwa marufuku kutumika wala kuingizwa nchini mwao.  Hujulikana pia kama mdalasini wa China na wengine huuitwa Saigon.

Mdalasini huu unatoka katika nchi za China, Vietnam na Indonesia. Wenyewe huwa una joto zaidi na huwa na radha kali nay a kuwasha ukiutumia. Madhara yake ni pamoja na kudhuru Ini na figo ukitumika kwa kipindi kirefu.

Cassia cinnamon huuzwa bei rahisi sana na mwingi unaopatikana huko masokoni ni huu. Huwa na rangi inayokaribia na uweusi.

Kwa kawaida ni vigumu kutofautisha aina hizi mbili za mdalasini ukishakuwa tayari katika mfumo wa unga tofauti na ukiwa bado katika fimbo au magome. Mhimu tu ni ununuwe kutoka kwa mtu unayemuamini zaidi.

Angalizo kuhusu Asali feki:

Asali original

Asali original

Napenda kukufahamisha kuwa miaka ya karibuni kumejitokeza baadhi ya wafanyabiashara kutengeneza asali feki kwa kutumia maji ya miwa na sukari guru au kuongeza maji na vimiminika vingine ndani ya asali ili wajipatie faida kubwa, endapo utatumia asali ya namna hii basi utakuwa ukiihatarisha afya ya mwili zaidi badala ya kujitibu.

Zifuatazo ni mbinu za kuitambua asali ambayo ni salama kwa maana ya kwamba haijachakachuliwa:

 • Weka maji kwenye glasi na kisha mimina asali ndani yake na kwamba ikikaa chini ya glasi bila kuchanganyana na maji basi hiyo ni asali asilia na inakuwa haijachanganywa na chochote.
 • Njia ya pili ni kuiweka asali kwenye njiti ya kibiriti na kisha kuiwasha hiyo njiti ya kiberiti, ikiwa njiti hiyo itawaka basi asali haijachakachuliwa kwa kuchanganywa na chochote lakini njiti ya kiberiti isipowaka asali hiyo inakuwa ni feki.
 • Njia nyingine ni kuionja bidhaa hiyo na kwamba iliyochakachuliwa kwa kuchemshwa hutoa harufu ya moshi tofauti na ambayo ni halisi (original).

Ikiwa utahitaji asali iliyochanganywa tayari na mdalasini,  niachie ujumbe WhatsApp +255769142586.  Napatikana  Victoria Home Remedy ipo Buza Sigara Temeke, kwa Dar naweza pia kukuletea ulipo kama utataka unanilipa nauli ya daladala na natuma pia mikoani.

Umewahi kuitumia asali yenye mdalasini? Kama ndiyo nishirikishe juu ya ulivyoimarika afya yako au ni kipi ulifanikiwa kujitibu kwenye comment hapo chini.

Jiunge na ukurasa wangu wa facebook kwa kubonyeza hapa => facebook

Je Umeipenda makala hii? Ninakaribisha mchango wako wa mawazo au ikiwa una swali nitafurahi zaidi kwani ni faraja kwangu kuona nimekujibu vizuri.

mbegu-za-maboga

(Imesomwa mara 1,694, Leo peke yake imesomwa mara 138)

You may also like...

641 Responses

 1. Barikiwa sana doctar mikoani tutapateje???

 2. Kuvipata ni shingapi Dr.

 3. Mdalasini ndio ninao hiraji mm doc.

 4. Asante nitakutafuta

 5. Samahan Dr kama nataka kuchanganya kila cku kwnye glass naweka madalasin kiasi gan na asali kiasi can hapo nimeona ukichanganya kwenye liter ya asali

 6. Anisa Bai Anisa Bai says:

  Kwa kweli utatukomboa wengi Mimi nahitaji

 7. hbbnnn nnmmhgxgbvzxcvvvyhjjghjhhhhhjghhhhbhhhhhhhhhh67h8iiuipZY

 8. Geofrey Jeas Geofrey Jeas says:

  Ahsante dkt Fadhili. Kwa somo

 9. Kuvipata no shingapi dr

 10. Asante nitakutafuta

 11. Asante Ila Nina Swali Inaweza Kutibu Vidonda Vya Tumbo?

 12. Ubarikiwe doct,huu mdalasini wa muheza unafaa?

 13. Je mchanganyiko huo anaweza kutumia mtu mjamxito

 14. Sisi tuko arusha je tutaipataje ila nina dadaang mjamxito anasumbuliwa na tatizo la uti sana doctor ndio mana kila ck nakuuliza hili swali na mjb hujanipatia

 15. Rahma Kibumo Rahma Kibumo says:

  Nishingapi na nitawapataje

 16. Mdarasini wetu huu haufai?nijibu pliz

 17. Bei gani nikiitaka iliotengenezwa tayari

 18. Justin Aron Justin Aron says:

  Nauluza hivi mtu mwenye ugonjwa wa moyo hio dawa anaweza kuitumia? La pili mtu anae kuwa na tatizo lakuvimba miguu akitembea hio dawa inaweza kutumika? La tatu mdalasini nitaupataje na kuchanganya na asali mtu anachukua kama kiasi gani? Namatumizi kwa kila siku unatumiaje?. Kwakweli mimi sijui nisaidie kwamawasiliano pia niwekee namba yako yangu hii 0744466471, 0675348996.

 19. Kombo Mussa Kombo Mussa says:

  ni kweli kama ulivyoeleza mungu ndio mponyaji sisi kazi yetu ni kutumia.hongera lakini usiuze ghali usaidie zaidi watumiaji.

 20. Nasreen Ally Nasreen Ally says:

  Me ninatatizo lakushika mimba vp inaweza kunisaidia mana nishatumia sna dawa lkn akuna mafsaanikio

 21. Nasreen Ally Nasreen Ally says:

  naomba nijibu me ninamatatizo ya uzaji naweza kuitumia na ikanisaidi

 22. Votre commentaire…kwaj ?

 23. Xamahani wadau mdalasini upoje au unapatikana WAP?

 24. Naiwa Ismailly Naish Muheza Tanga Tz Je Kama Mikoani Unafanya Ku2ma Mim Nahtji Kujua Garama Zako Kua Nikihtji Unipostie Garama Ni Sh Ngp Na Pesa Yako Nitaku2mia Kwenye Akaut Yako 2 Dk. So Matatz Yte Ulioyataja Yana 2husu Cc Vjana Kwakutokan Na Makaz Ye2 Napia Matminz Ya Mavykula Ya Kileo 2napenda Kula Machps Mayai Ambyo Hayo Mayai Yenyew Yakisas Ni Sumu Ila Cc Hatjar Hko Nikula 2 So 2natengeneza Misumu Mwlin Na Mwsh Wa Cku 2nakuja Kufuga Mijitambi Icyokua Na Ubora Na Hatimae Hata Ndoa Zea Kutopungua Kelele Kwakutokana Na Kushndwa Kumfkisha Mke Wako So Mim Nahtji Hy Dawa Na Kama Utapenda Bs 2wacliane Kupitia Namb Yng Ambyo Ni 0654408926 Plz Nakuomb Dk Ninamatatz Zaid Na Zaid So Nisaidie Plz Elimu Nimeipata Hvyo Nasublia Tiba 2

 25. Mtui Mtui Mtui Mtui says:

  Upare nako unapatikana je huo ni feki?samahan

 26. kushukuru kwa tiba mzuri

 27. Ambayo iko tayari ni bei gani?

 28. Ni sh ngap asali iliyochanganywa na mdalasin kabsa

 29. Ruth Saiteru Ruth Saiteru says:

  Doctor tatizo langu mm kifua changu n cha usiku t kinanibana afu sikohoi ila kama kuna kitu kinanibn kwenye koo,,, afuu nikikohoa hakuna kitu ,,, afu asubuh wakt nikiwa naswaki kohoz linatoka kidogo afu linauchafu afu unanukaa kwann?? Nisaidie doctor

 30. doctor,me nahitj uo mvhanganyiko na npo kijitonyama,0679026781 namba yng iyo hapo

 31. Tunashukuru saana Mutumishi wa MUNGU kwa maerekezo pia ushauri mweema,, mwenyezi mungu akubariki na kukuongezea maisha marefu ,kwa faida ya wengi ,maerufu wanapona na kubarikiwa Haleluyaa

 32. Aisha Aboud Aisha Aboud says:

  Nami nahitaji 0717544344

 33. Tully Mabewa Tully Mabewa says:

  Asante kwa tiba yako.

 34. Grace Billa Grace Billa says:

  Tutaupataje mchanganyiko huo am a huo mdslasini halisi?

  • Ikiwa utahitaji asali iliyochanganywa tayari na mdalasini, niachie ujumbe WhatsApp +255769142586. Napatikana Victoria Home Remedy ipo Buza Sigara Temeke, kwa Dar naweza pia kukuletea ulipo kama utataka unanilipa nauli ya daladala na natuma pia mikoani.

 35. Alen Urio Alen Urio says:

  Mm npo tunduru naweza kuupata huo mchanganyiko .je nkwabei gan had nilpo

 36. mimi nina tatizo nikichunjumaa mdaa mrefuu au nikikaa nipaoamka tu lazima ni hisi kizunguzungu na kiza cha ghafla machoni mwangu je iyo dawa itanisaidia?

 37. Grace John Grace John says:

  mi nautumia sana na umenisaidia sana kwa maumivu ya tumbo ila naomba kùliza vipi mjamzito akitumia haudhuru?

 38. Hakika nimeshuhudia mafanikio ya mchanganyiko huo!

 39. Mungu akubariki sana kwa somo zuri la kutusaidia tulio wengi tuna uhitaji

 40. Alhajj Ally Alhajj Ally says:

  Poa nipe namb ya tgo

 41. Angel Juma Angel Juma says:

  Dr ntapata wapi huo mdalasini usio na sumu? mi nipo mwanza nisaidie kama supermarket unapatikana

 42. Dah somo zuri xana tuletee na huku mwanza

 43. Bahati Ntoki Bahati Ntoki says:

  Feki utaujuaje huyo mdalasini

 44. Vipi nikichanganya asali,mdalasini,tangawizi na magadi,haiwezi kuwa dawa nzuri ya kikohozi?Nilikuwa najua kuwa ukichanganya limao/ndimu,magadi na asali ni dawa ya kikohosi.Kisha nikajua kuwa asali na tangawizi ni dawa ya kikohozi.Nawe umenijuza kuwa asali na mdalasini ni dawa ya kikohozi.Je,nikichanganya vyote asali,ndimu/limao,mdalasini,tangawizi na magadi siwezi kutibu kifua,kikohozi,pumu na kifua kikuu? naomba majibu.

 45. Je,siwezi kuchanganya unga wa mbegu za mlonge,mdalasini na asali nikatibu matatizo ya ngozi kama madoa usoni,chunusi na mapele?

 46. Ubarikiwe nitakuja kuchukua dawa ya malaria sugu bei gani ?

 47. Asante Docta kwasomo zur samahan unaweza kunitumia picture ya huo mdalasin original kwenye watsup samahan lakin 0766621404 namba yangu

 48. Mimi nai mfugaji wa nyuki japo siyo kitaalamu. Na asali kweli ni dawa lakini wengine/ Mimi nikilamba nitaumwa kichwa, tumbo na kichefuchefu ya kutosha. Je tatizo ni nini na nifanyaje niondokane nalo ili niweze kutumia asali?

 49. Jalia Mbonde Jalia Mbonde says:

  Mdarasini wa maji haufai

 50. David Kija David Kija says:

  Kuotesha nywele inakueaje

 51. Ester Joseph Ester Joseph says:

  Ninaushuhuda nimesumbuliwa na vidonda vya tumbo sana nilipotumia asali na mdalasini nimepona kabisa.Mungu mwema…

 52. Este Surio Este Surio says:

  Nahitaji hivyo vitu ni shilingi ngapi? No. Yangu 0658683892

 53. Binafsi ndo dawa ninayotumia kwa watoto wangu hasa wanapoumwa na vikohozi, ni dawa nzuri sana asali sijawahi kutumia dawa za dukani kwahajiri ya fukohozi vya watoto wangu, kwahiyo always nakuwa nayo nyumbani na hata ninaposafiri asali mbichi ni muhimu sana na hata kama watoto wangu hawaugui huwa ninawapa kwenye kijiko walambe tu.

 54. Asante kwa elimu nzuri ubarikiwe sana

 55. Nimekuelewa doctor wangu

 56. Hawa Shabani Hawa Shabani says:

  Dokta naomba namba yangu ndo iyo ili nipate tiba 0657787490

 57. Nahitaji tafadhari wasiliana nami nijue gharama

 58. Uko vizuri asante sana sijawahi itabidi nikutafute ubarikiwe

 59. duh, inatibu kilaki2?

 60. duh, inatibu kilaki2?

 61. Km Mm Wa Bukoba Naeza Kuipat Vp

 62. Eddy Ngenzi Eddy Ngenzi says:

  Daa! Ngoja nitafte mdarasin mm mwenyewe natengeneza mzinga Asal hainisumbui! Ila madukan wanauza Asal halafu wanaandika Exp date mm sijaona Asal ina Exp aise

 63. Muniru Ayubu Muniru Ayubu says:

  Huo ulio changanywa bei yake ni sh ngap

 64. Doctor mm nina tatizo la chunusi namadoa natumia nn

 65. Tunashukuru Dr, mimi ninamiaka 3 sasa nasumbuliwa na vidonda vya tumbo nimetumia dawa za hospital hadi zimenikifu, na vinanitesa sana je..? nikitumia asali na mdalasini nitapona,niko Kitunda Nyantila Dar es salaam.

 66. Iliypchangnywa ni bei gani no za simu

 67. Nilishatumia asali iliyochanganywa na mdalasini, tangawizi na mlonge, yani ukitumia kwa week tu utaona mafanikio pia ukiwa unatumia ikiwa imechanganywa kama kulamba utumie kijiko cha chai kidogo asubuh na jioni pia baada ya kulamba kaa dakika kumi unywe na maji lita moja utaona maajabu jinsi itakavyotoa sumu mwilini nahata kama umezohofika utaona utakavyopata nguvu kwa haraka! ila asali iwe aijachakachuliwa.

  • Elinora Shoo Elinora Shoo says:

   Mohamedi tunaomba vipimo vya mchanganyiko huo

  • katika glass ya maziwa hakikisha papai ulioiponda iwe nusu glass hata ukizidisha kidogo sio mbaya pia haina madhara hata ukiinywa kilasiku…Dozi asubuh na jioni.

  • Katika chupa ya asali konyagi ndogo vijiko viwili vya mdalasini na tangawiz kavu iliyosagwa vijiko viwili na mlonge ukiosagwa kijiko kimoja. unaichanganya kwa asali unaikoroga vizuri.. doz kijiko kimoja cha chai asubuh na jioni hakikisha baada yakutumia kaa dakika kumi kunywa lita moja ya maji. inatoa sumu mwilini kwa haraka huweka ngozi kua nyororo, pia hata kama ulikua mchovu inakuweka vizuri pia hata kama ulikua unakojoa mkojo mchafu lazima utakojoa mkojo msafi.

 68. Haswaaa waingamkono kuruani ktk surat nahal nandiomana nawaambia wasilim msalimike na adhabu ya Allah

 69. Ahsante Dr mchanganyiko huo ni mzur sn, mm Binafsi naamini asilimia 100%, Pia husaidia hamu ya kufanya mapenzi sn, Pia ni dawa ya kiungulia sn na ulcers, ila mdarasini mzuri ni ule unatoka India ni mzuri sn, Pia mchanganyiko huo unarefusha uume, na kufanya mishipa kuwa na nguvu sn, Asali mdarasan na vitunguu swaumu ni matumizi yangu kila siku, Big time Dr,

 70. Mdalasini unaolimwa ndani ya nchi yetu unafaa au LA?

 71. Hivi ni kweli kwamba ukitumia kwa mda mrefu unaweza ukapata mapacha wakike? ()

 72. Safi nikiitaka naipataje

 73. Docta Naomba Unisaidie Dawa Ya Mafua Nasumbuliwa Sana Na Mafua Haipiti Wiki Bila Kuumwa Mafua Naomba Msaada Wako

 74. Asante Dr Mimi nauzito Mkubwa niutumiaje huko mdaradini Na asali

 75. Asanteeeeeeeeee kwa ujumbe

 76. Aza Mpinga Aza Mpinga says:

  Asee Mwenyezi mungu akulipe sana kwa wema huu kwa wanadamu hakika ww una huruma na mapenzi ufanikiwe sana ktkt maisha yako

 77. Asante sana kwa hidaya hii ya elimu ya asali na mdalasini

 78. Glory Msechu Glory Msechu says:

  Mi na vidonda kila nkila natapika Chakula chote na mwil unachoka je nitumie hii tiba na asali ni ya nyuki wadogo au

 79. Ahsante kwa kutuelimisha…. Mungu atakulipa inshaalah

 80. Mimi Nina asali ya nyuki wakubwa mbichi je inafaa

 81. Tumaini Tina Tumaini Tina says:

  Naomba maelekezo mdalasini orgnal naupatia wapi?

 82. Evodia Linus Evodia Linus says:

  Docter naomba samahani kwa kukusumbua kuna tatizo lingine linanisumbua. ninaumwa fangasi sehemu za siri zinsnisumbua sana.nakuomba unisaidie nifanyeje.

 83. Evodia Linus Evodia Linus says:

  Docter naomba samahani kwa kukusumbua kuna tatizo lingine linanisumbua. ninaumwa fangasi sehemu za siri zinsnisumbua sana.nakuomba unisaidie nifanyeje.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *