Hii ndiyo tiba kwa kutumia masaji ambayo wengi hawaifahamu

Tiba kwa mazoezi
Hii ndiyo tiba kwa kutumia masaji ambayo wengi hawaifahamu

HII NDIYO TIBA KWA KUTUMIA MASAJI AMBAYO WENGI HAWAIFAHAMU

Wakati tunakabiliwa na mfadhaiko mkubwa kiakili na kimwili wa muda mrefu wengi wetu huwa tunatafuta msaada.

Hata hivyo moja ya tiba ya matatizo haya ambayo wengi hawaijuwi ni tiba kwa kutumia masaji, tiba ambayo ina uhakika wa uponyaji kwa karibu ya asilimia 100 bila kutumia dawa yoyote na bila madhara yoyote.

Masaji ni njia nzuri sana ya kuondoa stress na kupigana na maradhi mengi mwilini ukitumia nguvu ya mwili wenyewe kujitibu bila dawa yoyote zaidi ya mazoezi maalumu kwa kutumia mikono.

Shuhudia faida na uponyaji kupitia masaji kutoka katika kuongeza kinga ya mwili, kuondoa tatizo la kukosa usingizi, kupona baridi yabisi (stroke), kifafa na magonjwa mengine mengi yahusianayo na mishipa.

Masaji ni tiba inayofanywa kwa kutumia mikono tu huku mtoa masaji akikugusagusa na kukusugua juu ya mwili wako kwa namna maalumu ambayo ndiyo huamsha na kufungua mishipa na kuondoa sumu na stress mbalimbali na hivyo kuongeza kinga ya mwili kupambana na maradhi mbalimbali bila kutumia dawa yoyote.

Ni tiba maarufu kidogo maeneo ya mijini kuliko vijijini.

Pia ni huduma inayopatikana kwenye mahoteli makubwa ya kifahari Dar Es Salaam na Zanzibar wenyewe huita SPA’s ingawa hizo za kwenye mahoteli lengo kubwa huwa ni kwa ajili ya kukufanya u-relax na kupata utulivu baada ya uchovu wa shughuli za kila siku.

Hii masaji ya tiba (physiotherapy message) ni masaji maalumu kwa ajili ya wagonjwa.

Unaweza kujitibu hali hizi 6 zifuatazo kwa kutumia masaji tu:

1. Kuongeza kinga ya mwili

Kufanya masaji hakukufanyi ujisikie ni mtulivu peke yake, bali pia kunaweza kukuongezea kinga yako ya mwili.

Masaji ya dakika 45 kwa siku imethibitika kuongeza uwingi wa seli nyeupe za damu (lymphocytes) ambazo ndizo hupigana dhidi ya vijidudu nyemelezi vya magonjwa mbalimbali mwilini.

Faida nyingine za kiafya ni pamoja na kushuka kwa homoni inayohusika na kupunguza maambukizi mbalimbali homoni ijulikanayo kama ‘cytokines’ vile vile masaji inashusha homoni inayohusika na matendo ya mashari homoni ijulikanayo kama ‘cortisol’.

Kipindi kimoja cha masaji kinatosha kuzalisha matokeo yanayoonekana ya kuongezeka kwa kinga ya mwili.

2. Kuondoa tatizo la kukosa usingizi

Mamia ya watu wanapatwa na tatizo hili la kukosa usingizi jambo linaloharibu ufanisi wa kazi zao kila siku.

Tatizo la kukosa usingizi linaweza kutibika kwa kufanya masaji tu kwakuwa masaji husaidia kupunguza uchovu na kuongeza uwezo wa kupata usingizi mtulivu kwa watu wa rika zote yaani watoto wadogo mpaka wazee ikihusisha wale wenye matatizo ya akili, kansa na magonjwa ya moyo, machache kati ya magonjwa mengi yawezayo kutibika kwa masaji tu.

Tafiti nyingi zinasema masaji inao uwezo wa kuamsha mawimbi ndani ya ubongo yanayohusiana na kutengenezwa kwa usingizi mzito (delta waves) na hii ndiyo sababu kwanini wengine hupitiwa na usingizi mzito mara tu baada ya mazoezi ya masaji.

3. Kuondoa mfadhaiko wa akili (Stress)

Zaidi ya asilimia 32 ya watu waliojaribu tiba hii wanathibitisha kupungukiwa na kiasi kikubwa cha mfadhaiko wa akili katika miili yao huku tafiti zaidi zikiendelea kutoa ushuhuda wa aina moja.

Utafiti uliofanywa na chuo kikuu cha Afya cha chuo kikuu cha Harvard umethibitisha kuwa masaji huondoa hamaki na maumivu huku yakiongeza uwezo wa kupata usingizi mzuri na wa uhakika.

Chuo kikuu cha afya cha Boston Uingereza kiliona matokeo yaliyo sawa kati ya wagonjwa 60 wenye kansa ambao walifanya tiba ya masaji dakika 20 kabla ya mionzi kuliwapunguzia kiwango cha hamaki na mfadhaiko wa akili.

Watafiti kutoka Australia wameripoti kwenye jarida la afya liitwalo ‘The Journal of Thoracic and Cardiovascular Surgery’ kuwa masaji hupunguza maumivu, hamaki na mshtuko wa mishipa baada ya upasuwaji wa moyo.

Utafiti mwingine kutoka chuo kikuu cha Toho cha Japan umethibitisha masaji inayohusisha mafuta maalumu ambayo huwa na harufu ya kunukia (ya kuvutia) na ambayo ni dawa husaidia kupunguza mfadhaiko wa kisaikolojia katika wazee wagonjwa wanaotibiwa majumbani.

4. Kuondoa huzuni

Tafiti kutoka chuo cha afya cha Nashville’s Meharry Medical College wagonjwa 43 wa ukimwi walionyesha kuondokewa na hali zao za huzuni baada ya kufanya masaji ya mwili mzima kwa majuma matatu tu.

Profesa maarufu na mtafiti Russell Poland, Ph.D. ambaye ni Profesa wa magonjwa ya akili na sayansi ya akili amesema: “Wakati tunaanza huu utafiti hatukutegemea kuona matokeo mazuri kiasi hiki kwa tiba hii ya masaji. Sote tulibaki na mshangao tu’’.

Faida hizi zilirudiwa pia na chuo kikuu cha Los Angeles Calfornia Marekani ambapo watu 95 waliojitolea kwa utafiti wa tiba hii ya masaji walionyesha kuongezeka homoni ijulikanayo kama ‘oxytocin’ na kupungua kwa homoni nyingine iitwayo ‘adrenocorticotropin’.

Oxytocin inahusika na matendo ya huruma, maono, upendo na ushirikiano wa kijamii. Wakati adrenocorticotropin yenyewe huhusika na kupungua kwa mfadhaiko (stress) moja kwa moja.

5. Kuondoa maumivu mbalimbali mwilini

Watafiti kutoka kitengo cha jinakolojia (uuguzi) cha chuo kikuu cha Sao Paulo Brazil walitafiti wanawake 46 wajawazito waliofanyiwa masaji ya mgongo walipunguza kiasi cha maumivu wakiwa leba kwa zaidi ya asilimiaa 27.

Katika utafiti mwingine uliofanyika hospitali kuu ya Beijing nchini China masaji nzito ilisaidia kuondoa maumivu ya mgongo kwa wagonjwa. Kupungua kwa maumivu haya kuliripotiwa na robo tatu kati ya wagonjwa 110 waliofanyiwa utafiti huo.

Maumivu mengine yaliyoripotiwa kuondoka kwa kutumia tiba ya masaji ni pamoja na maumivu ya kichwa na maumivu ya kwenye mishipa.

6. Kuongeza uwezo wa kujiamini

Watu wengi zaidi kila kukicha wanaendelea kuitafuta huduma hii ya tiba kwa njia ya masaji wakiwa na maradhi mabalimbali katika miili yao. Madaktari wengi nao wameendelea kuwashauri wagonjwa wao kujaribu tiba hii.

Utafiti unaendelea kuwaeleimisha watoa tiba hii jinsi ya kuifanya ili kupata matokeo mazuri katika kutibu matatizo kama maumivu sugu ya misuli, matatizo yanayotokea wakati wa matibabu ya kansa, wakati wa mabadiliko yaletwayo na ujauzito, na maradhi mengine mengi.

Matatizo mengine yanayoweza kutibika kwa kutumia masaji ni pamoja na saratani ya matiti, tatizo la kufunga choo, ukichaa, maumivu, maumivu ya kichwa, maumivu ya mifupa, baridi yabisi (stroke) nk.

Bila shaka mpaka hapo umepata kuzijuwa faida za masaji na magonjwa inayoweza kuyatibu.

Bahati nzuri kwa wenyeji wa Dar huduma hii ya masaji inapatikana kwenye kituo chetu cha tiba asili cha Victoria Home Remedy kilichopo Buza Sigara Temeke tena kwa gharama nafuu kabisa.

Pia kwa wale wenye matatizo ya uzazi tunazo dawa nzuri za asili zinazotibu matatizo mengi ya uzazi kwa pamoja ikiwemo uvimbe, homoni, uchafu, mirija kuziba, mayai kutopevuka nk nk

Kama unahitaji huduma hizi tupigie 0714755582

Tafadhali SHARE kwa ajili ya uwapendao.

(Imesomwa mara 183, Leo peke yake imesomwa mara 91)

You may also like...

241 Responses

 1. Agnes Tala Agnes Tala says:

  Ubarikiwe dokta

 2. Rukia Masaka Rukia Masaka says:

  Safii ubarikiwe sana

 3. Shani Sella Shani Sella says:

  Asamte kwakutujulisha

 4. Mungu akubariki kwa somo zuri

 5. Ahmad Ali Ahmad Ali says:

  iko powa sana, ila ni wachache sana wanaofahamu umuhimu wa jambo hilo, lkn bila shaka somo limefika. kwa hivo Ahsante Dokta.

 6. Anna Mgimba Anna Mgimba says:

  Hiyo tiba ni bila kutumia mafuta au na Mafuta??

 7. Asante Kwa Elimu hii. Mungu akubariki

 8. Mafuta yapi sasa dct

 9. Tutapata vp ujuzi wa vitendo kwa hii tiba ya kutumia masaji,kwani bils ujuzi yaweza kuleta madhara au nimekosea Dr.?

 10. Ahsant mpndwa unatumia mafuta gani???

 11. nilikuwa na siku ngumu sana wakat flan had kichwa kiliuma nikaenda kufanyiwa masaji ya kichwa ukweli nilipona kabisa ,tatizo la huduma hiz ni ghali na jamii inaona masaji kama kitu kinachoshawishi kuchepuka badala ya kuona kama tiba .

 12. Asante kwa elimu lkni wengine hatujajuwa hyo mafuta

 13. Unatumia mafuta gan

 14. Nashindwa elewa kiasi Fulani inaleta mfaiko ebu fikilia utakuta mwanamke anamfanyia mwanaume wakati kavua nguo zote uku akimkandanda wanaume wenye roho zaifu itakuaje ili kuepusha matatizo katika ndoa inabidi mwanake afanyie mwanake na Mme afanyie mwenzie masaji nyingi washugulikaji waschana docta unategea kutakua na nini ndio maana wanawake wanaogopa peleka waume zao binafsi nilishaona ugovi kuhusu masaji

  • Upo sahihi ndugu, nakushauri uwe unaongozana na mwenza wako akienda kupata huduma kama hizi

  • Ushauri nzuri sana lakini unaweza kujifunza wewe na Mumeo anajifunza pia mnakua mnanunua vifaa mnafanyiana wenyewe hata nyumbani kikubwa ni kujifunza my dear Ashura na uwe na vitendea kazi u can do it at home anytime

  • Ndio maana baadhi ya watu Wa Pwani huwafundisha msichana na mvulana wanaotarajia kufunga ndoa jinsi ya kufanya masaji tendo hili huitwa singo kwa wale Wa Pwani watanielewa ili kuondoa utata Wa kwenda salun mnanunua tu vifaa mnafanyiana wenyewe nawapongeza wahenga Wa Pwani walilijua hili

 15. Wanaofanya hiyo huduma ni jinsia gani?

 16. Mery Wiliam Mery Wiliam says:

  Mafuta gn nabei gan

 17. Ng Ng'unda Jmo says:

  Naomba uwe unanipostia kwa whatsap yangu plz, 0712883012

 18. Hiyo masaji unafanyiwa eneo lenye tatizo au kuna sehemu maalum tu?

 19. Aluhya Ally Aluhya Ally says:

  Mm nataka nijifunze masag nimfanyie mwenyewe Mme wangu unatoa huduma ya kujifunza?

 20. Eddy Hega Eddy Hega says:

  Doctar kwani huwezi fanyia home?

 21. Asante kwa elimu nzuri

 22. Ahsante sana. Mungu akubariki Kwa kazi yako njema Kwa watu.

 23. John Laiza John Laiza says:

  Ok thank you doctor

 24. James Brown James Brown says:

  Asante kua ripoti

 25. Asante. Ubarikiwe.

 26. Mikono inatakiwa iwe laini au migumu Kama ya mkulima?

 27. Vitendea kazi gan vnatakiwa kukamilisha hiyo tiba

 28. Masaji Noma

  😂😂😂
  Lazima abdala Kichwa wazi asimame😂😂

 29. Naweza kuyapata hayo mafutah!?

 30. Kuna mafuta maalum yakufanyia masaji au mafuta yoyote?

 31. Frida Peter Frida Peter says:

  Mafuta gani haswa yanafaa kwa kazi hiyo?

 32. Asante dokt, hiy tiba wapi hinapatika

 33. Lucy Jengela Lucy Jengela says:

  Jamani ,mungu akulinde miaka mingming 2 u

 34. iv MTU anaweza fanyiwa masaji ya maskio msaada pls

 35. Teddy Lymo Teddy Lymo says:

  Mm huwa natumia mafuta ya Nazi cjui kama ni sahihi?

 36. Asnte sana dokta mungu akibari sana

 37. Othman Chimo Othman Chimo says:

  Doctor hbr hv doc na tatizo la maumivu ya mifupa ya kifuani inaweza tibika na hiyo massage therapy? ahsante.

 38. Irene Kilang Irene Kilang says:

  Asante doctar nazan umewasaidia kujibu wasichana wengi wanaofanya hizo huduma na si wasichana tu hata wavulana. Unajua muudumu wa massage anakuwa anakuhudumia kwa lengo moja tu la uduma basi lakini anaefanyiwa ndo anaeanzisha vishawishi kwa asilimia kubwa sana kwaiyo embu watu wajirekebishe na waone ni sehemu ya tiba tu na sio vituvingine

 39. eneo la mwili linalofanyiwa meseji mfano mgongo n.k unamfanyia mtu meseji kwa dakika ngapi? Fadhili Paulo

 40. Tiba safi na salama kwa afya. Nimeipenda.

 41. Asante sana je ni aina gani ya mafuta

 42. Khadija Ali Khadija Ali says:

  Asante kwa kutupa elimu

 43. MA Jack Solo MA Jack Solo says:

  Asante doctor, kwa elimu nzur.ubarikiwe

 44. Trk Kibona Trk Kibona says:

  Mafuta gani doctor.

 45. docta niendelee kuomba ile post ya kuongeza maumbile kwa njia ya mazoez plz docta

 46. Asante kwa elimu naanza kesho Mungu akubariki Doctar

 47. Rehema Ramadhani si umeona hee MTU wangu

 48. Hawa Mbiaji Hawa Mbiaji says:

  Asante sana nimekuelewa mkuu

 49. Analizo,wengine wanaitumia ndivyo sivyo

 50. samahani docter kunasomo nimesoma google kuhusiana na INFECTION nimepewa maelezo yote kuhusiana na dawa nimepewa nimeona dawa nyingi pale nwaza kutumia je niazitua zote kwa pamoja ao nachakuwa ninayo itaka ?

 51. Mariam Kaisi Mariam Kaisi says:

  Nimejifunza kitu asante dokta

 52. Ukijifanyia masaji mwenyew Na akukufanyia MTU kuna tofauti au zote sawa?

 53. Leah Maimu Leah Maimu says:

  Asante kwa elim nzuri ya Afya zetu

 54. Hiyo massaji inakuwaje mwanamke anamchua mwanaume au inakuwaje!!!

 55. Rahaa ya masege kufanyiana

 56. dokta mimi ninashida yauzazi nina miaka mitano sasa sijapata ujauzito namtoto ana miaka nane sasa nasitumii kinga yeyote nifanyaje mimi nipo arusha naomba ushauri wako natamani sana kupata mtoto mwingine.

 57. Dr_samahani.Kwanza_ahsante_kwa_mafunzo.Na_mimi_nahitaji_ile_post_ya_jinsi_ya_kuongeza_maumbile/uume_kwa_kufanya_mazoezi,please_nisaidie.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *