Jinsi ya kuondoa au kupunguza mafuta tumboni kwa wanawake

Jinsi ya kuondoa au kupunguza mafuta tumboni kwa wanawake
Jinsi ya kuondoa au kupunguza mafuta tumboni kwa wanawake

Jinsi ya kuondoa au kupunguza mafuta tumboni kwa wanawake

mbegu-za-maboga

Wanawake wengi miaka ya karibuni wanakabiliwa na tatizo linalofanana na kitambi kwa upande wa wanaume. Hivyo ingekuwa ni wanaume tungesema ni kitambi ambalo nalo ni tatizo kubwa miongoni mwa wanaume wengi nyakati za sasa.

Kinachowasumbuwa wanawake siyo kitambi tunasema ni mlundikano wa mafuta sehemu ya chini ya tumbo na tumbo kwa ujumla kufikia hali kuonekana kama ana tumbo kubwa au kuhisi labda ni ujauzito kumbe ni mafuta tu mengi.

Kwa ujumla ni vigumu sana kupunguza tumbo la namna hii, hivyo kwenye post hii pamoja na mengine tutaona pia visababishi vya tatizo lenyewe, dawa za asili zinazoweza kuondoa tatizo hilo na aina ya maisha unayotakiwa kuishi ili ufanikiwe kirahisi zaidi bila kukuachia madhara mengine yoyote.

Nini kinasababisha tumbo kwa kina mama:

 • Vyakula feki (Junk food)
 • Kutumia vyakula vya wanga kupita kiasi
 • Kutokunywa maji ya kutosha kila siku
 • Kula chakula kizito muda mchache kabla ya kwenda kulala
 • Kukaa masaa mengi kwenye kiti
 • Kutokujishughulisha na mazoezi
 • Mfadhaiko (stress)
 • Kula wali kila siku
 • Ugali wa sembe
 • Kula vyakula vinavyopikwa katikati ya mafuta mengi (chipsi, maandazi, nk)

Vyakula vinavyoondoa mafuta kwenye tumbo kwa wanawake

mbegu-za-maboga

1. ASALI NA LIMAU

Chukua asali kijiko kikubwa kimoja cha chakula na majimaji ya limau vijiko vikubwa viwili, changanya hivi viwili ndani ya glasi moja (robo lita) ya maji ya uvuguvugu na unywe yote mara tu ukiamka asubuhi.

Tumia kwa wiki 3 hivi mpaka mwezi mmoja na hutachelewa kuona tofauti.

2. MAJI YA UVUGUVUGU

Kunywa maji ya uvuguvugu kama lita 1 hivi wakati tumbo likiwa tupu hasa asubuhi ukiamka tu. Hii inasaidia kusafisha mwili na kuondoa mafuta yasiyohitajika.

3. NYANYA

Kula nyanya ambazo hazijapikwa pia inasaidia kupunguza tumbo kwa kina mama, hivyo kula kachumbali ya kutosha kila siku ya nyanya peke yake na utaona mabadiliko.

4. TANGAWIZI

Chemsha chai ya tangawizi, ipua na usubiri ipowe kidogo, ongeza asali mbichi kidogo na pilipili manga kidogo ya unga. Pata kikombe kimoja cha chai hii kila siku asubuhi mapema ukiamka tu. Asali inasaidia kuyeyusha mafuta wakati pilipili itauongezea nguvu mfumo wa mmeng’enyo wa chakula.

5. SIKI YA TUFAA

Siki ya tufaa (apple cider vinegar) inasaidia kupunguza njaa na kukufanya ujisikie umeshiba kwa kipindi kirefu. Kunywa kijiko kikubwa kimoja cha siki ya tufaa mara 1 kwa siku kila siku wakati unakula chakula cha usiku. Kazi nyingine ya hii siki ni kuweka sawa damu sukari mwilini hivyo ni nzuri pia kwa wenye kisukari.

6. MAJANI YA BIZARI

Majani ya bizari husaidia kuondoa sumu na takataka nyingine mwilini kitu ambacho moja kwa moja hupelekea mlundikano mdogo wa mafuta katika tumbo. Kunywa chai ya majani ya bizari kila siku asubuhi, ukikosa majani unaweza kutumia hata unga wake.

8. ILIKI

Iliki hufanya kazi ya kuongeza nguvu katika mfumo wa mmeng’enyo wa chakula na ni dawa nzuri sana ya kuondoa sumu na takataka nyingine mwilini. Iliki pia hutumika katika kupunguza uzito. Tengeneza chai yenye iliki kila siku ndani yake, pia ni kiungo karibu kwa vyakula vingi hivyo hakikisha unaiweka katika kila chakula unachopika kwa matokeo mazuri zaidi.

9. MDALASINI 

Mdalasini hufanya kazi ya kuchoma mafuta mwilini. Chukua kijiko kidogo kimoja cha mdalasini ya unga na uweke ndani ya glasi 1 ya maji ya moto na uache kwa dakika 5 hivi. Ongeza kijiko kidogo kimoja cha asali mbichi ndani yake na ukoroge vizuri, kisha unywe huo mchanganyiko wote asubuhi ukiamka tu.

10. JUISI YA LIMAU 

Kunywa maji ya limau au juisi ya limau kila mara kutakusaidia kuondoa mafuta tumboni kwa haraka sana. Ongeza majimaji ya limau vijiko vikubwa viwili ndani ya glasi 1 ya maji na uongeze punje 1 ya chumvi ya mawe, koroga vizuri na unywe asubuhi ukiamka tu kila siku.

11. KITUNGUU SWAUMU

Ili kupunguza mafuta tumboni katakata vipande vidogo vidogo (chop) punje 3 mpaka 4 za kitunguu swaumu na unywe na maji vikombe viwili asubuhi tu na kisha shushia na glasi moja ya maji yenye limau kidogo kwa mbali. Hii ndiyo njia nzuri kabisa ya asili ya kuondoa mafuta tumboni kwa haraka zaidi.

12. TIKITI MAJI

Tikiti maji lina asilimia 82 za maji kitu kinachofanya tumbo lako kutokuwa na njaa ya kuhitaji chakula. Tikiti maji lina vitamini C ambayo ni mhimu kwa afya bora. Kula tikiti kila siku.

13. MAHARAGE

Kula maharage kila mara kunasaidia kupunguza mafuta katika tumbo. Maharage yana kiasi kingi cha nyuzinyuzi (faiba) kitu kinachosaidia tumbo lako kutojisikia njaa na hivyo itakuwezesha kula chakula kiasi kidogo. Kadri unavyokula chakula kichache ndivyo unavyokuwa mbali na uwezekano wa kuzalisha mafuta mengi tumboni.

Basi kula maharage kila siku.

14. TANGO

Tango lina asilimia 96 za maji na asilimia zinazobaki ni nishati. Tumia kachumbali yenye tango ndani yake kila siku au kula tu tango moja kila siku ili kupunguza mafuta tumboni kwa haraka.

15. PARACHICHI

Parachichi ni tunda lingine zuri sana kwa ajili ya kuchoma mafuta yaliyozidi mwilini. Parachichi ni chanzo kizuri cha nyuzinyuzi (faiba). Parachichi huikimbiza mbali njaa na wewe. Parachichi lina mafuta lakini ni mafuta mazuri (monounsaturated fatty acids) ambayo yenyewe husaidia kuchoma mafuta na hivyo kuondoa mafuta mabaya tumboni kirahisi zaidi.

Kula parachichi 1 kila siku.

16. TUFAA

Kula tufaa maarufu sana kama ‘apple’ (epo) kunaweza kusaidia kupigana na magonjwa mengi sana mwilini na inaweza pia kusaidia kuondoa mafuta kwenye tumbo lako. Tufaa hukufanya ujisikie umeshiba sana kwa masaa mengi sababu lina potasiamu na vitamini nyingi sana ndani yake.

Hivyo kula tunda hili 1 kila siku asubuhi kupunguza shauku yako ya kutaka kula zaidi ndani ya hiyo siku nzima.

17. MAFUTA YA SAMAKI

Mafuta ya samaki ni mbadala mzuri kabisa katika kuchoma mafuta ya tumboni. Mafuta ya samaki yenyewe hulenga kuyachoma moja kwa moja mafuta yanayozidi tumboni. Ukiweza unaweza kuamua yawe ndiyo mafuta yako ya kupikia, pia unaweza kunywa mafuta haya kijiko kikubwa kimoja kila siku unapoenda kulala.

18. SIAGI YA KARANGA

Siagi ya karanga hupunguza njaa na kuongeza nguvu katika mfumo wa mmeng’enyo wa chakula. Siagi ya karanga ina kiinilishe kijulikanacho kama ‘niacin’ ambacho chenyewe huzuia mafuta kujilundika tumboni. Hivyo kwenye mkate wako asubuhi ningekushauri utumie hii siagi ya karanga badala ya mafuta mengine ambayo si salama, pia unaweza kutumia hii siagi ya karanga kama mafuta yako ya kuunga katika mboga nyingi unazopika hata katika wali unaweza kutumia kama mafuta yako mbadala.

19. MAYAI

Mayai yana vitamini nyingi sana ndani yake (mayai ya kienyeji lakini) na yana madini pia kama kalsiamu, zinki, chuma, omega -3 nk. Viinilishe vyote hivyo katika mayai husaidia kuchoma mafuta yanayozidi tumboni. Hivyo kula mayai asubuhi kila siku ili kuondoa na kupunguza mafuta mwilini. Mayai pia ni moja ya vyakula vinavyomfanya mtu ajisikie kushiba kwa muda mrefu bila kuhitaji kula kula tena.

20. CHAI YA KIJANI

Chai ya kijani maarufu kama ‘Green tea’ hufanya kazi ya kuondoa sumu mwilini jambo linalosaidia pia kuchoma mafuta yaliyozidi mwilini. Kunywa chai hii ya kijani kila siku kutafanya ngozi yako kukua vivyo hivyo kufanya tumbo lako kukaa sawa bila kuwa na mafuta mengi.

21. MTINDI

Ingawa mtindi unaweza kupelekea kuongeza uzito zaidi, hata hivyo mtindi mtupu kabisa ule ambao haujaongezwa kingine chochote ndani yake unaweza kukusaidia kupunguza mafuta tumboni. Matumizi yake kwa siku yasizidi kikombe kimoja (robo lita). Pia mtindi ni moja ya vyakula vinavyoweza kukufanya ujisikie umeshiba na hivyo kukuondolea njaa ya kutaka kula.

22. JUISI YA KOTIMIRI 

Juisi ya kotimiri (Parsley juice) huondoa sumu na takataka nyingine zozote mwilini, pia huchoma mafuta na nishati. Kotimiri ni dawa nzuri kwa matatizo mbalimbali ya figo pia kwa kuchoma mafuta mwilini.

Pata kikombe kimoja cha juisi hii kila siku unapoenda kulala.

23. NDIZI

Kama lilivyo tufaa, ndizi pia zina kiasi kingi cha potasiamu na vitamini za aina mbalimbali ndani yake. Ukipenda kula ndizi kila mara zinachofanya mwilini mwako ni kuondoa ile hamu ya kutaka kula vyakula feki (fast food). Zaidi sana ndizi huuongezea nguvu mfumo wa mmeng’enyo wa chakula na hivyo kupelekea mafuta ya tumboni kuyeyuka kirahisi zaidi. Kula ndizi kila siku ukiweza ukiamka tu kula ndizi zilizoiva 3 mpaka 5 kila siku.

mbegu-za-maboga

24. MAJI YA KUNYWA

Kunywa maji ya kutosha kila siku kunasaidia pia kupunguza uzito. Kunywa maji lita 2 mpaka 3 kila siku iendayo kwa Mungu. Kunywa maji kidogo kidogo kutwa nzima. Hili halitafanya kazi ya kusafisha mwili tu bali pia litafanya ngozi yako kung’aa na kukuwa. Nywele zako pia zitaonekana ni zenye afya na mwili mzima utakuwa ni wenye kuvutia.

Kitu cha kwanza ukiamka tu ni kunywa maji glasi 2 na uendelee hivyo hivyo glasi moja moja kila baada ya lisaa limoja au mawili kutwa nzima. Maji ni uhai, bila kunywa maji kila siku ni sawa na kwenda dukani bila hela mfukoni.

Asilimia 94 ya damu yako ni maji, asilimia 85 ya ubongo wako ni maji, asilimia 27 ya mifupa yako ni maji, asilimia 75 ya mwili wako ni maji. Sehemu kubwa ya dunia hii imefunikwa na maji na sehemu yenye ardhi ni kipande kidogo sana. Haijalishi unaishi kwenye baridi au kwenye joto hakikisha unakunywa maji ya kutosha kila siku, huhitaji kusikia kiu au hamu ndipo unywe maji, hapana maji ni lazima uyanywe tu hata iweje.

25. MAZOEZI YA KUTEMBEA

Shida kubwa kwa kina mama wengi wa kiTanzania ni kuwa hawajishughulishi na mazoezi. Hapa Tanzania mazoezi inaonekana ni jambo la wanaume tu. Mazoezi ni jambo la lazima kwa mtu yeyote iwe unaumwa au huumwi.

Ili kuchoma mafuta mwilini kwa haraka zaidi tembea kwa miguu mwendo kasi kidogo lisaa limoja kila siku. Kumbuka nimesema lisaa limoja yaani dakika 60 bila kupumzika (none stop) kila siku. Kutembea kwa miguu lisaa limoja huamsha mwilini kimeng’enya kijulikanacho kama ‘lipase’ ambacho chenyewe huamka tu ikiwa utatembea bila kusimama kwa dakika 60 na kikishaamshwa (when it is activated) huendelea kuchoma mafuta mwilini kwa masaa 12 mfulululizo.

Usiseme nikitoka sehemu fulani kwenda sehemu fulani nitakuwa nimetembea vya kutosha, hapana, unahitaji uwe na saa mkononi kuhakikisha kweli dakika 60 zimeisha ukiendelea kutembea bila kusimama. Kama utaweza kukimbia kidogo kidogo (jogging) basi utachoma mafuta ya tumbo kwa haraka zaidi.

Ufanye zoezi hili kila siku kwa mwezi mmoja mpaka miwili mfululizo na mafuta kwenye tumbo lako yatapotea yenyewe bila kupenda.

Je una swali kuhusiana na hili somo letu la leo? liulize hapo chini kwenye comment nitakujibu.

Kwa mawasiliano zaidi; WhatsApp +255769142586

Tafadhari SHARE post hii kwa ajili ya wengine uwapendao.

Una ushuhuda wowote kama matokeo ya kutumia blog hii? Kama ndiyo toa ushuhuda wako ili uwe msaada kwa wengine, kutoa ushuhuda wako bonyeza hapa.

mbegu-za-maboga

(Imesomwa mara 7,576, Leo peke yake imesomwa mara 268)

You may also like...

844 Responses

 1. Vizuri, lakini umeweka vitu vingi na vyote ni tiba, pia unasisitiza vitumike kila siku asubuhi, swali je’ inawezekana kutumika vyote kwa pamoja?

 2. Asante kwa somo lako zuri nimekuelewa nitarifanyia kazi kuaaja ya kutumia njia zaidi ya moja au moja inatosha asante

 3. Mayai na parachichi na asali vitamu mno

 4. Nc kwa ushaur wko

  @ CHID GWAY @

  **** BORN 2 SHINE*****

 5. Joyce Marike Joyce Marike says:

  Mimi swali langu ni kweli kama ukitumia maji ya moto yanaharibu mapafu au

 6. Malago Jocha Malago Jocha says:

  Mi Nashangaa Wengine Tunavisaka Vitambi Wengne Wanavifukuza? Bac Mnaovitoa Naomba Mnigawie!!!!!!

 7. Mimi sajakuelewa umesema ni vigumu sana kuondoa Tumbo LA namna hii halafu unatoa DAWA za kupunguza !!!

 8. Leonard Malema says:

  je uweza kutoa huduma kwa waliombali nawe kwa kutuma anachohitaji kutoka kwako?

 9. Tedy Sukambi Tedy Sukambi says:

  Asante sana Dr kwa elimu boro

 10. jamani mm nakula sana matango maparachichi je nile kila nilapo chakula au??? je kitapungua kweli hiki kitambi

 11. Asante kwa somo zuri ila vitu naona ni orodha kubwa Sidhani kama mtumiaji ataweza vyote kwa pamoja maoni yangu ungeweka vichache ambavyo vyaweza kutumika kwa pamoja na kwa muda fulan ili kumfanya mtumiaji kutohamahama mfano Leo nikitumia juis ya limao kesho mazoezi siku inayofuata maji ya moto

 12. Asante ndg kwa somo,nitafanya hivyo,nilifanya ya mtindi na vitunguu swaum lkapungua kidogo,asante

 13. Tumekuelewa inawezekana kumaliza kitambi tatzo kutojali afya kwa walio weng wavivu

 14. Sifael Amos Sifael Amos says:

  Cjaelewa kuhusu kuchemsha tangawizi +asali & mdalasini vyote unaweza kutumia kwa wakati mmoja?

 15. Halafu doctor nimekumbuka kuna kitu nilikisoma kwenye ushauri wako inatuhusu wanaume , na ukataja dawa za kutumia sasa iyo dawa mbaka Leo kila nikiuliza hilo jina hawalijui(udishe) sijui kama kuna jina jingine?

 16. Shani Hamimu Shani Hamimu says:

  Asante kwa somo nzuri Mimi huwa nakunywa asali ndim na maji je naweza kuongeza mdalasini

 17. Asante xn kwa somo zuri nimelipenda mno

 18. Happy Kundy Happy Kundy says:

  Samahan naomba kuuliza kipi ni sumu ni tangawizi+asali au limao+ asali? Maana kuna watu wamenambia ni sum

 19. Duke Rwamara Duke Rwamara says:

  Naomba ufafanuz juu ya matumiz ya yai. Weng huxema ukzdisha kula mayai mwilin , utaxababisha cholestrol je ni kweli?

 20. Jesca Haven Jesca Haven says:

  Dr vp kuhusu juice ya Kabeji nmeckia nayo husaidia kupunguza kitambi nkweli

 21. Nitakutafuta kesho kwa namba Yako kwa wasap

 22. Hellen Chris Hellen Chris says:

  Vipi kuhusu kupunguza tumbo la uzazi(baada ya kujifungua)

 23. Ahasante kwa somo nzuri

 24. Rose Mmbuji Rose Mmbuji says:

  Nashukuru kwa elimu nzuri, naomba nikuulize dokta, hata kama ni tumbo la uzazi umejifungua kwa operation linaweza kwisha? Samahani naomba msaada wako.

  • Nashukuru kwa kushukuru, ndiyo tumbo lolote ukiweka nia na bidii na ukafuata maelezo haya utafanikiwa tu

  • Maggy Maggie Maggy Maggie says:

   Kabsa Linapungua, mimi nimejifungua kwa operation na nilikuwa na tumbo kubwa, nifanya mazoezi, nakunywa maji ya uvuguvugu na mdalasini na kitunguu saumu limepungua kabsa utafikiri sijawahi kuzaa, na tango pia nakula kila siku.

  • Kumbe Maggy kwa mtu wa oparesheni mazoezi pia hayana shida?

  • Maggy Maggie Maggy Maggie says:

   Ndio, Hayana shida yoyote unadownload mazoezi ya mtu aliyejifungua kwa operation. Me niko fit sana sifeel pain popote pale na mwili na tumbo vimepungua.

  • Maggy Maggie Maggy Maggie says:

   Wanawake tumejenga katabia kwa kujiendekeza, mama akishajifungua kwa operation ndo basi tena hataki kufanya kazi hata tu shughuli ndogondogo za nyumbani ni shida kisa operation. Hapana huko ni kujilemaza na ndo unakuta binti mdogo kale kashepu kako kazuri kanapotea, tumbo hlo. Wamama wenzangu hasa wale waliojaliwa watoto kwa njia ya operation na una mwaka 1, miaka 2 tuache kujiendekeza, operation sio ugonjwa kama hufeel maumivu yoyote fanya mazoezi, fanya shughuli zako kama kawaida jamani.

  • Sweya Othman Sweya Othman says:

   Maneno yakweli kbsa watu wamejiendekeza sn Kisa upareshen

  • Rose Mmbuji Rose Mmbuji says:

   Asante sana kaka fadhili na da Maggy kwa ushauri wenu mzuri mlionipa, nitajitahidi kufwata maelekezo na naamini nitafanikiwa.

  • Maggy Maggie Maggy Maggie says:

   Nina Imani utafanikiwa kabsa Rose kama mimi nilivyofanikiwa tena kwa kiasi kikubwa. Nitapiga Picha then nitakutumia nilivyosasa ili ikuhamasishe zaidi. usikate tamaa my dear.

  • Mimi pia nimepungua sana na tumbo sina kabisa ninafanya mazoezi na ninazingatia milo yangu
   Nilizaa kwa opareshion nilipofika miezi 4 nilianza gym na mazoezi ya nyumbani
   Sina mtumbo kabisa
   Nilikuwa na kilo 83 kwasasa nikilo 65 ndani ya miezi 9 ya kujifungua
   Kikubwa zingatia mlo sahihi
   Na mazoezi Hakika utafurahi mwenyewe Rose Mmbuji

  • Kitunguu punje kila siku nameza punje 6
   Hadi sasa
   Chai ya mchaichai na limao natumia hata sasa
   Mbogamboga na matunda ndio mlo wangu kwa sana
   Nakula na vyakula vingine kwa kiasi fulani na usiache kabisa utakosa nguvu
   Maji kila siku nakunywa lita 3 hadi 4 hii ni lazima kwangu
   Ukiniona utasema binti wa kidato cha 5 kumbe mama wa watoto 4
   #AFYAKWANZA ##

  • Rose Mmbuji Rose Mmbuji says:

   Asante sana kwa ushauri mzuri kwani tumbo limekuwa ni kero kwangu. Nitazingatia hayo naamini nitapungua.

  • Rose Mmbuji Rose Mmbuji says:

   Asante sana kwa ushauri mzuri kwani tumbo limekuwa ni kero kwangu. Nitazingatia hayo naamini nitapungua.

  • Rita David Rita David says:

   Maggy Maggie asante umeniamasisha ngoja na mm nijaribu.

 25. El’gael Bait Thout it myt help 😊

 26. Tatu Mpogo Tatu Mpogo says:

  Asantesana kwa elimu uliotupa insha Allah nitayafanyia kazi

 27. Ally Diwani Ally Diwani says:

  Shukran sana kwa elimu tiba. (Afya) Mola akuongoze kwa hili na jingine. Wa Tanzania wengi wameathirika na tatizo la matumbo. Wengine hadi kushindwa nyumba zao.

 28. Hope Peter Hope Peter says:

  Asante docta kwa somo nimekuelewa.lkn ninaswal binafs, napenda kutafuna mchele mbich nn madhara yake?

 29. Asante kwa somo nimechelewa kuelewa vyote hvyo vinafanywa sambamba au ni kimoja baada ya kingine na ni ndani ya muda gani?

 30. Kefa Jidoto Kefa Jidoto says:

  Me kuna kitu huwa kinajitokeza wakati nikiwa na njaa zaid ukiwa umelala utakiona kimeinuka upande wa kushoto ukibonyeza nikigumu mm ni mwembamba hilo itakuwa ni tatizo gani?

 31. Angela Eugen Angela Eugen says:

  nimeipenda sana hiyo ya limau asali na kitunguu saumu pamoja na maji yavugu vugu. ila nilikuwa naomba maelekezo zaidi jinsi ya kuchanganya na muda sahihi wa kunywa hiki kinywaji

 32. Kweli nimetumia juicy ya limao tgawizi na asali Siku tatu tu nimeona mabadiliko

 33. Nashukuru sana coz nijijaribu kula ninalo weza ss naona Tiba imenifata ubarikiwe

 34. Jaman ukitumia huo mchanganyiko unapungua tumbo tuuu au mail wote

 35. Nimekumanya nnatumbo linanikera sana naanza kesho

 36. Amina Saidy Amina Saidy says:

  Asante doctor kiukweli kitambi ni tatizo acha nifate muongozo wako

 37. Nimeipenda, ila watz waikuona unafanya hii wanakucheka wanasema kaonda siku hizi, anayembea kwa mguu

 38. Kwa Mahitaji ya Asali mbichi toka Mpanda Katavi wasiliana nasi 0766736782

 39. Kuvaa suruali zinazobana kwa mda mrefu zinanasababisha vitambi visivyo na mpango. Utakuta binti ana umbo namba 8 baana ya mda fulani utaona yupo kama gunia suruali umemkamua kuanzia miguuni analegegeza kiunoni

 40. Asante kwa ushauri mzuri

 41. Nashukulu kwa ushauli wako ila mimi ni mpenz sana wa limeo natumia San kwa juice na hata kwny mbga kachumbali je haiwezi kuniasili au niko sahihi na wakat mwngne nakula km chugwa.

 42. Asante doctar ila cjaelewa hvyo vitunguu swaum unavisaga au unameza punje zake namaji

  • 11. KITUNGUU SWAUMU

   Ili kupunguza mafuta tumboni katakata vipande vidogo vidogo (chop) punje 3 mpaka 4 za kitunguu swaumu na unywe na maji vikombe viwili asubuhi tu na kisha shushia na glasi moja ya maji yenye limau kidogo kwa mbali. Hii ndiyo njia nzuri kabisa ya asili ya kuondoa mafuta tumboni kwa haraka zaidi.

  • mimi ninatumia usiku, muda wa kulala,je ninakosea?

 43. Habari samahani apo umetaja zaidi ya vimiminika vinne ambavvyo vinatakiwa kunywewa asubuh pindi uamkapo je yapaswa kutumia vyite or kimoja kati yapo

 44. Trishaz Mtam Trishaz Mtam says:

  Naweza Nkanywa Juice Ya Limao Na Asali Asubuh Af Mchana Nkala Baadhi Ya Tunda Moja Ulotaja Au Nkitumia Juice Ya Limao Vngn Ctumii?

 45. Somo ni xuri sana,
  Mimi kwangu nswapa ushauri kwamba,point ys mwisho ktk maelezo ndio iwe ya kwanza,

  MAZOEZI,
  Ni muhimu sana kwa kutoa tumbo,waweza tumia hivyo lakini pasina mazoezi inakuwa ngumu sana kufikia malengo,
  Mi nafanya mazoezi na wengi kinadada wamekuja ktk chuo chetu,wakiwa wametimia muda mwingi sana kwa vitu km hivyo,
  Ila walipotumia na kujibidihisha na mazoezi, sasa wamekuwa sawa,hivyo Dr kasema mazoezi nayo muhimu,
  KUKATA TUMBO,NI KUJITOA HASA NI MCHEZO,

 46. Mimi siipendi kabisa asali hua nachukua mdalasini nachemsha baada ya kuepua yakipunguza umoto nasugulia tangawizi nakamulia limao mbili nachuja nakunywa niongeze au nipunguze nini?

 47. Asante docta kwa somo zuri wanasema kula asubuhi kama kawaida mchana km kawaida usiku kula matunda au juice tumbo linapungua kuna ukweli hapo???

 48. Nikiacha kufanya mazoezi Muda mfupi tu nanenepa kuliko mwanzo

 49. Glady Mwetta Glady Mwetta says:

  Kaka fadhili samahani naomba unitumie hii whatsup yani.umenipa.njia mbadala ya kupunguza huu mwili nataka nilete mrejesho hapa 0718191919

 50. Asante kwa somo zuri sana nafikiri wanawake wengi na wanaume wenye vitambi walifatilia somo hili

 51. Asali mbich na tango ukila kwa pamoja nilliwahi kusikia. inakuwa sumu kwa mlaji je ni kweli Dr?

 52. Mariam Kaisi Mariam Kaisi says:

  Yaani nafarijika Sana nakunufaika na mafunzo yako na ninaahidi kulifanyia kazi mungu akupe kheri daima uendelee kutusaidia

 53. Asante kwa somo zuru, saivi kitambi mwiko, ukiwa nacho umekipenda mwenyewe.

 54. Asante Doctor kwa somo nzuri lkn kikubwa zaidi ni mazoezi na kuwa na ratiba nzuri ya chakula haswa kupunguza wanga na sukari kula kwa kiasi kidogo na chakula cha Usk kiliwe mapema sana ukiweza hata saa kumi nambili au saa moja sio kula tu na kulala

 55. Ahsante sana kwa somo zuri maana wanawake wengi ni ttz kwetu.swal hivyo vitu ulivyovitaja hapo juu ni vyote kuvitumia au mtu unatizama kati yahivyo ulivyotaja urahis wa mtu kuvipata Dr????

 56. je kama nina vidonda vya tumbo, naweza kutumia,, rimao, au nyanya mbich, au piripiri,

 57. Jamani nishaurini mi vidonda vya tumbo kila ninachoweka tumboni kiungulia sasa ntatumia vipi hivo vitu nisaidieni nifanyeje

 58. Hakika hizi sasa ndio faida za Wasomi.
  Hakika Elimu yako itaikomboa jamii yetu.
  Ahsante sana kwa darasa lako murua.

 59. Qeeny Tunu Qeeny Tunu says:

  Asante docka KWA somo lako mungu akubari sana ila naomba kujua kitu kimoja umesema pamoja nakutumia vitu hivyoo mazoezi ni muhimu sasa nizoezi gani litaweza kutoa tumbo KWA haraka zaid plz nisaidie ili niepuke na tatizo LA kitambii?

  • Fanya zoezi la kutembea kwa miguu mwendokasi kidogo dakika 60 bila kupumzika kila siku kwa mwezi mmoja mpaka miwili mfululizo, ukiweza kukimbia kidogo kidogo (jogging) ni vizuri zaidi

 60. Tunashukulu kwasomo lako zuri ilanauliza hiv I ulisema tuchanganye asali na ndimu sinasikia asali nandimu nisumu tafadhari nifahamishe

 61. Asante kwa somo doctor vitunguu saum havina madhara kwa mama anaye nyonyesha

 62. Ahsante kwa ushauri, wadau tumieni kuondoa kero mwilini.

 63. Tumsifu Ngowi umesema limau,asali,kitunguu swaumu,na maji ya vuguvugu ni kiboko, nami nimeipenda sana hiyo,samahani naomba nielekeze ulivitumiaje hivyo vyote?

 64. Chai yang ni mdarasini.iriki na tangawizi hap vip siweki kituchochote hapo dokta vip

 65. Asante Dr kwa somo zuri kwetu wanawake.je hivi vyote ulivyosema vitumike asubuhi ni kwamba tutumie vyote au ni tunatakiwa tuchaguwe kitu kimojawapo?

 66. Dr hapa mada inahusu wanawake tu he wanaumw nao tunafanyaje kuondoa vitambi?

 67. Asante doctor kwaelimu nzuri sana

 68. Wandugu ,,nauliza ,nini imeongezeka maana miaka ya nyuma hakukuwa na hili la akina mama kuwa na vitambi kwa kasi kama ilivyo kwa sasa ,,

 69. Elimu uliyotupatia ni nzuri sana.wakinamama wenzangu tuondoe vitambi.Assumption kuwa kitambi ni utajiri huo ni umaskini wa kufikiri na kutokujitambua.

 70. Usher Bora Usher Bora says:

  Shukrani sana Dr nitaanza kutumia kimoja wapo maana nami ni muhanga wa tumbo ubarikiwe sana

 71. Hebu tujuze kuhusu limao na asali nisijekufa mie kisa kupunguza tumbo

 72. Nisikia watu wnasema ukila asli na limau sio nzuri je ni kweli eti unaweza ukafa?

 73. Somo zuri sana ila sasa kwa wale wenye vidonda vya tumbo je maji ya limao inakuaje apo

 74. Sasa mm Nina tumbo alafu Ni mnene je nikifuata haya maelekezo nitapunga na kitambi kitaisha

 75. Sanifa Shoo Sanifa Shoo says:

  Asante kwa hints zakupunguza Mafuta. Nitazingatia.

 76. Neyma Brown Neyma Brown says:

  Ahsante Sana kwa darasa

 77. Hajra Msangi Hajra Msangi says:

  Mimi nmejaribu vitu karibia vyote na bado tumbo kubwa nifanyej

 78. Nakubaliana na wewe kwa 100% hasa kwenye hichi kipengele cha hulaji wa wanga kwa kuwingi namna kinavyo ongeza mafuta tumboni labda kwa wasio jua ni kwamba ukila wanga na mafuta yoyote yanayo patikana kwenye mboga mbali mbali kama nyama kinacho tokea ni kwamba tumbo litamen’genya wanga na kuacha mafuta tumboni ambayo ndio mwanzo wa mafuta tumboni (bila kusahau sukari si ishu mwilini)

 79. Eva Katongo Eva Katongo says:

  Asante kwa somo,je kwa mm mwenye tumbo la uzaz la miez 11 litarudia hali yake

 80. Ndio ni dawa kibogo limao na maji ya uvuguvugu ila Siku za kwanza utaharisha sn ila baadaye unaendelea vema safi an dokita

 81. ahsante Dr kwa ushauri mzuri, tatizo upatikanaji wa hiyo aple cider vinegar nimejaribu kutafuta sehemu nyingi sipati nilipata ya Kenya ambayo ipo kahawia mpauko sikuichukua je nayo inafaa?

 82. Mariam Bata Mariam Bata says:

  Asant doctar nilkua mnene kupita kias nime2mia limao na maji ya moto na hasal ndan ya wk3 npo vzr nimepungua sn asant snaaa

 83. Tumbo la chini linapungua pia kwa mchanganyiko huu?! kile kitumbo cha uzazi.

 84. Asante kwa somo zuri saana,swali mm ni mwembamba hua ninafanya mazoezi hayo ya kutembea lakin nikimaliza nackia miguu inakufa ganzi pamoja na vidole vya mikono je nifanyeje?

 85. Inamaana vyote ulivyo vitaja vitumike vyote kwa kila siku au Kati ya ulivyo taja nikimoja wapo

 86. Inamaana vyote ulivyo vitaja vitumike vyote kwa kila siku au Kati ya ulivyo taja nikimoja wapo

 87. Eliza Molell Eliza Molell says:

  dokt me ninaxhida xn me naumwa na 2mbo upande mmoja wa 2mbo nikaenda hosptal nikaambiwa utiai na nimepewa dawa nime2mia nimemaliza je? nakulxa tafaxal je yutiai inawexa kuxababixha kutoxhika mimba? je dalil xa yutiai ni zipi? tafaxal naomba unixaidie kwn nimeumwa mda kwa xaxa nina mwaka naumwa 2 na nimexhindwa kuxhika mimba!

 88. Julieth Mtuy Julieth Mtuy says:

  Asante kwa somo zuri. Inabidi tujitahidi tutoe minyama uzembe

 89. asante sana nataman hata kunywa glass hata 3 kwa njinsi TUMBO linavyonikelaa

 90. Joyce Kileo Joyce Kileo says:

  Jaman mm mbona tumbo halipungui ? Vyote hivyo nishatumia mpk soda nimeachaa

 91. Irene Urasa Irene Urasa says:

  Mm tatiz lang nitumb linanium kil nilitk kufany mazoezi ss xijajuw ttizo nn doct

 92. mohd says:

  mafunzo ni mazuri sana nimo mbioni kutumia

 93. Haya wenye vitamb mmepata somoe mi mwezenu mazoez kama sala kwangu maj ndo usiseme hiyo chai ya kijan ndo kila SKU.lakin bado 2 jaman vingne ndo umbile lako lilivyo.asante doctor kwa somo zur.

 94. Asante sana kwakuona haya maelezo ya kupunguza tumbo. Nitaanza kesho.

 95. Asante sana kwakuona haya maelezo ya kupunguza tumbo. Nitaanza kesho.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *