Jinsi ya kurekebisha mzunguko wa hedhi

Jinsi ya kurekebisha mzunguko wa hedhi
Jinsi ya kurekebisha mzunguko wa hedhi

Jinsi ya kurekebisha mzunguko wa hedhi

mbegu-za-maboga

Hili ni tatizo linalowatokea karibu wanawake katika safari yao ya kuishi hapa chini ya jua.

Tatizo la kuvurugika kwa mzunguko wa hedhi huanza ghafla au polepole ambapo mwanzo mwanamke alikuwa akipata siku zake katika utaratibu unaoeleweka lakini mara haelewi au hajielewi namna mzunguko wake unavyoenda.

Kuvurugika kwa hedhi ni kitendo cha mwanamke kuanza kuona siku zake bila tarehe au mzunguko maalumu na matokeo yake ni kuwa mwanamke atashindwa kutimiza malengo yake kwa kutumia mzunguko huo sababu ni haueleweki.

Unaweza kutokewa ghafla tu unapata hedhi mahali usipotarajia jambo linakufanya ubaki na woga na huelewi nini cha kufanya kwani hukuwa umejiandaa kwa tukio hilo kama matokeo ya siku zako kutokuwa mzunguko maalumu. Wakati mwingine unaweza kupitiliza mwezi hata miezi kadhaa bila kuona kabisa siku zako na hata ukipima ujauzito unakutwa huna ujauzito wala dalili huna.

Madhara ya kuvurugika kwa mzunguko ni pamoja na;  kushindwa kupata ujauzito, maambukizi katika kizazi na kuziba kwa mirija ya uzazi.

Kwanini unahitaji mzunguko wa hedhi ulio sawa?

Faida za kuwa na mzunguko wa hedhi ulio sawa:

 1. Utakusaidia kupata ujaouzito ulioupangilia
 2. Utakuepusha kupata ujauzito ambao hukuupangilia
 3. Utaweza kuamua jinsia ya mtoto unayemtaka

Nini husababisha kuvurugika kwa mzunguko wa hedhi

Ni rahisi kugundua kama mzunguko wako umevurugika ikiwa tu unauafahamu vizuri mzunguko wako ulio sahihi. Kufahamu mzunguko unahitaji uifahamu siku ambayo ulianza kuona damu hadi siku utakapoona tena katika mzunguko unaofuata. Karibu kila mwanamke huwa na mzunguko wake usiofanana na wa mwingine.

Tatizo linaweza kuanza kwa kurukaruka siku, mwanamke pia anaweza kupoteza siku yaani mwezi mwingine anaona na mwezi mwingine haoni, au anaingia mara mbili kwa mwezi au anaona damu ya hedhi kwa siku nyingi hata zaidi ya siku arobaini mfululizo. Damu yake inaweza kutokea kidogo kidogo kila siku au nyingi huku ikiambatana na mabongemabonge na maumivu pia. Maumivu haya ya wakati wa hedhi huenea chini ya tumbo mpaka miguuni na kiunoni.

Kuvurugika kwa hedhi kunaweza kutokea kutokana na sababu zifuatazo:

 1. Mabadiliko ya mazingira ambayo hupelekea mfumo wa mwili hubadilika pia hasa mwanamke akitoka sehemu ya joto kwenda mikoa ya baridi au toka mikoa ya baridi kwenda mikoa ya joto.
 2. Msongo wa mawazo (stress)
 3. Hofu
 4. Woga
 5. Mabadiliko ya kisikolojia
 6. Uvimbe kwenye kizazi
 7. Matatizo kwenye mfumo wa homoni
 8. Matatizo kwenye vifuko vya mayai
 9. Mimba kuharibika
 10. Maambukizi sugu ya kizazi pia ni mojawapo ya sababu.
 11. Maumivu ya tumbo chini ya kitovu ya mara kwa mara na kila ukipima unaambiwa ni ugonjwa wa U.T.I kumbe siyo yutiai
 12. Kutokwa na uchafu ukeni
 13. Maumivu wakati wa tendo la ndoa.

Jinsi ya kurekebisha mzunguko wa hedhi

mbegu-za-maboga

Kabla ya yote unapopatwa na tatizo hili kwa muda mrefu ni vizuri ukaonana na daktari uweze kupata uchunguzi wa kutosha kubaini nini hasa inaweza kuwa ndiyo sababu hasa ya tatizo kwa upande wako.

Zifuatazo ni dawa mbadala 6 unazoweza kuzitumia ukiwa nyumbani ili kurekebisha tatizo hili

1. Papai

Papai

Papai

Papai ni moja ya dawa nzuri sana katika kutibu tatizo la kuvurugika kwa hedhi. Ina viinilishe mhimu kama carotene, chuma ( iron), Kalsiamu (calcium) na vitamini A na C ambavyo husaidia kulainisha na kunywea kirahisi kwa kuta za mji wa uzazi.
Siku 2 au 3 kabla ya kuanza kula papai kila siku nusu papai papai zima kutegemea na ukubwa wake au uwezo wako.

Kwa mtu mwelevu sababu ameshagundua papai laweza kumsaidia hivyo basi atalifanya papai kuwa sehemu ya chakula chake kila siku na si mpaka aumwe tu.

2. Mdalasini

mdalasini

Mdalasini

Mdalasini unayo sifa ya kuondoa tatizo la damu kuganda sifa inayoweza kusaidia kuondoa tatizo la maumivu wakati wa hedhi.
Mdalasini ni chanzo kizuri cha nyuzinyuzi (fiber), kalsiamu (calcium), chuma (iron) manganizi (manganese).

• Tengeneza chai ya tangawizi kwa kutumia kijiko kidogo cha mdalasini ya unga na maji kikombe kimoja (robo lita), ipua na uache ipowe kidogo, ongeza asali kijiko kikubwa kimoja ndani yake na unywe. Fanya zoezi hili mara 2 mpaka mara tatu siku 2 au 3 kabla ya kuanza siku zako.

• Au changanya kijiko kidogo kimoja cha mdalasini ya unga na kijiko kidogo kimoja cha asali katika glasi moja ya maji ya uvuguvugu na unywe kutwa mara 2 siku za mwanzoni unapoanza au kukaribia kuingia katika siku zako.

3. Tangawizi

Tangawizi

Tangawizi

Tangawizi ni dawa ya asili yenye maajabu katika kutibu tatizo la mvurugiko wa hedhi. Tangawizi hufanya kazi mhimu kabisa katika kushusha kiwango cha homoni inayosababisha maumivu ijulikanayo kwa kitaalamu kama ‘prostaglandins’. Tangawizi husaidia pia katika kupigana na uchovu uletwao na mzunguko wa hedhi katika siku zile za mwanzo au siku 2 hivi kabla ya kuanza siku zako na huweza pia kufanya mzunguko usio sawa wa hedhi kuwa sawa

• Tengeneza chai ya tangawizi ukitumia tangawizi mbichi, kunywa kikombe kimoja kutwa mara 3 wakati wa siku zako au siku yoyote tu kama kinga. Kamulia ndimu kidogo ndani yake na utumie asali kupata radha badala ya sukari.

• Unaweza pia kuongeza tangawizi kwenye vyakula na mboga mboga nyingi unazopika kila siku.

4. KOTIMIRI (Parsley):

Kotimiri

Kotimiri

Tengeneza juisi ya kotimiri, viazi pori (Beet Root), karoti au matango. Tumia asali mbichi ukitengeneza juisi hii. Hii kotimiri inapatikana kirahisi Dar na Zanzibar ni mboga mboga inayotumika zaidi kwenye mahoteli ya kitalii. Mboga hii inacho kitu mhimu sana kijulikanacho kama ‘Apiol’ amabcho kazi yake kuu ni kurekebisha na kuweka sawa homoni za kike.

Changanya kwa ujazo sawa yaani kama juisi ya kotimiri ni kikombe kimoja basi ya kiazi pori nayo kikombe kimoja kadharika kwa matango. Juisi hii ni dawa tosha ya maumivu wakati wa siku za hedhi, hurekebisha mzunguko wa hedhi na imethibitika kuwa bora kuliko dawa nyingi za kizungu.

Kunywa glasi moja ya juisi hii kutwa mara 2.

5. MREHANI

Mrehani

Mrehani

Mrehani au Basil kwa Kiingereza ni mmea mwingine mzuri sana katika kuondoa maumivu wakati wa hedhi na kurekebisha mzunguko wa hedhi kwa ujumla. Mmea huu unatumika sana jikoni kwenye mahotel ya kitalii Dar na Zanzibar. Unao sifa kuu ya kuzuia au kuondoa maumivu mwilini.

• Ongeza kijiko kikubwa kimoja cha majani freshi ya mrehani yaliyokatwakatwa na kisu (chop) kwenye kikombe kimoja cha maji ya moto, funika vizuri na usubiri ipowe. Kunywa yote ikishapoa na ufanye zoezi hili kutwa mara 3 kwa wiki 3 mpaka 4 au mpaka tatizo lako limeisha.

• Au tengeneza juisi ya majani haya. Yatwange kwenye kinu au kwenye blenda ya umee kupata majimaji yake kisha chota vijiko vya chai viwili uweke ndani ya kikombe kimoja cha maji ya moto na unywe yote. Fanya zoezi hili kutwa mara 3.

• Unaweza pia kuongeza majani freshi ya mrehani kwenye vyakula vingi unavyokula kila siku.

6. MAJI YA KUNYWA

Maji ya kunywa

Maji ya kunywa

Matatizo karibu yote mwilini chanzo chake ni mwili kutokuwa na maji ya kutosha. Maji ni uhai. Unachohitaji hapa ni kutokusubiri kiu. Kiu ni ishara ya mwili iliyochelewa kuhitaji maji.

Matatizo mengi ya kiafya tumeyaona kwa watu wasiopenda kunywa maji ya kutosha kila siku.

Jitahidi hata iweje iwe unaumwa au huumwi chochote unywe maji lita mbili mpaka tatu kila siku iendayo kwa Mungu na utaniletea mrejesho hapa hapa.

Kama una swali au unahitaji ushauri wowote liulize hapo kwenye comment nitakujibu.

Kama utahitaji hizi dawa tuwasiliane WhatsApp +255769142586

Tafadhali SHARE kwa ajili ya wengine.

mbegu-za-maboga

(Imesomwa mara 2,705, Leo peke yake imesomwa mara 99)

You may also like...

788 Responses

 1. Oriver Nkuba Oriver Nkuba says:

  Asante doct kwa elimu uliyo itoa ,mm tatizo langu kwenye uke wangu nimevimba upele kwa ndani kwaiyo nilikua. Naomba ushauli

 2. Hafsa Ismail Hafsa Ismail says:

  Asalam alaykum warahmatullahi wabarakatu km napima kila Mara naambiwa ni uti inanisumbua kumbe sio je nipime vpimo gn zaid ili nijue nn tatizo naombnijulishe

 3. MIMI NINATATIZO LA KUTOKWA NA UCHAFU UNAOTOA HARUFU NA MZUNGUKO WANGU WAHEDHI HAUELEWEKI LAKINI KILA MWEZi NAINGIA KWENYE CK JE NN sababu za kutokwa na uchafu huo na hata mimba zinaingia hazikai zinatoka nn tatizo?naomba unisaidie docta

 4. Asante Sana kwa kutuelimisha mungu aendelee kukupa uwezo zaidi wa kutuelimisha

 5. Doct asate kwa hilo somo mm nasumbuliwa na hezi nikikalibia tu tumbo linaniuma sana Naomba ushauli wako nifanyeje asante kwa huduma

 6. Mm one week before kupata period huwa naumwa sana nakosa nguvu, nikipata period ndio naumwa kabisa mm ni kulala tu,siku ya 1 na ya 2 huwa nakoma najuta kuwa mwanamke mpaka zipite siku 5 hv ndio naweza kujickia vizuri kuchefuchefu na mda wote huo Wa period huwa sihitaji chakula zaidi ya chai tu,chai ya Tangawizi au mdalasini hunisaidia ila najiuliza kwa nn uwa naumwa sana dr?? Naomba jibu dr 0714-29 76 70

 7. Dija Kipingu Dija Kipingu says:

  Docta asante ila docta mimi ninashida nanaomba unisaidie yaani mimi hedh napata bali tarehe hazieleweki

 8. asante doct mm nina tatizo naziona sik zang xiku mbil au tatu af kidogo xan vp nina tatizo gan nixaidie

 9. Asante Docta mm tatizo langu kubwa linalonisumbua kwa mwezi naweza nikapata hedh mara 2 kwa mwezi hili nitatizo gan au nifanyeje naimenichukua muda mref kweli

 10. Axante xana doctar kwa uxhali wako na anzakulifanyia kaz 2tawaxiliana

 11. mm matatizohayo mnayo yote kumwachin yakitov kilacku kuckia maumivuwakat watendo landoa napia kama miaka 4ilopta nilikuwa natumia majila lakn toaka niache mpakasasa cjashka mimba docta naomc ushaul nifanyeje?

 12. Siku ya kwanza ya hedhi ndo huwa naumwa na tumbo na maumivu makali chini ya kitovu nifanyeje na husababishwa na nn

 13. Docta tatizo la kukauka ukeni wakati na maumivu ya tumbo chini ya kitovu na uke kuvuta au kuma kama kuchomachoma. Docta tatizo linatokana na nini na dawa yake nini?nisaidie docta

 14. Lucy Mtui Lucy Mtui says:

  Doctari naomba unisaidi mzunguko wangu naweza nikaenda mwezi huu na mwezi ujao nikapitiliza mwezi mwengine nikaingia tarehe tofauti na ninahitaji mtoto

 15. asante doctor mm ninadada yangu alkuwa anatumia njia zauzazi wa mpango sindano 5na vidonge vyamajila sasahivi anamwaka mzma bila hata mimba nampaka sasa hajabeba hata mimba nakwenye siku zake anapitilza mpaka mwez nanusu naoba ushaul wako doctor

 16. Anna Vicent Anna Vicent says:

  Doctor mm ninatatito nilikuwa mimba ya mwez I ikatoka baada ya kutoka nikawa nakumia sindan kama baada ya apo nikaacha sasa ninashida ya mtt arafu mimba sipat nifanyeja

 17. Hallia Defao Hallia Defao says:

  Asante kwa tiba yako mm nanyonyesha tangia nijifungue nilikaabila kupata ck mwaka na miezi 2 nikapata mwezi wa11mpaka leo cjaona tena na cna dalili yoyote.ya mimba je nitumie ilo papai

 18. Ninaitwa amina ninaumwa na kiuno, uti wamgongo na pia naskia maumivu Chin ya kitovu, nanina miaka2sijaona sijaona damu

 19. Aksante docta mmnaomba kuulizaswali tamgia naanza kuingia kwenye siku zangu adi Leo cku zangu azilingani talehe adi as ninamiaka 5 nabado azijawaikuwa talehe moja eti tatizo litakuwa ni nn?

 20. Mungu akupe Maisha marefu amina

 21. Mbegu za mboga mboga gan asante kama utanisaidia kulijua hilo na nimefurahia sana elim ulio tupa

 22. Mbona mm nimetumia papai abdasini kabla ya siku 2 ndio nimeumwa kuliko siku zote?

 23. ASANTE MTAALAM KWA KUGUNDUA HILO MUNGU AKUBARIKI SANA TUTASOMA VIZURI NA KUYATENDEA KAZI BE BLESSED

 24. dokta kuna dada mmoja hajaona siku zake imepita miez mitatu sasa na hana mimba nn tatizo na tiba ake

 25. Asante mjomba kwa somo lako zur ni kwel hali hii uwatokea wanawake walio weng at na mm ilinitokea ila nilisaidiwa na matunda, yalinísaidia sana tupende kutumia matunda

 26. Doris Sengo Doris Sengo says:

  dokta mi ninatatizo lakufunga kuingia brid au wakati mwingine naingia lakn natokwa dam isiyo kua ya kawaida unakuta dam sio nyekundu afu inaku na mabonge kama vile nyamanyama alafu nikiwa bridi tumbo huwa linauma sana tena kwa maumivu makali sana halafu Sina taree maalum ya kuingia bridi pliz naomba unisaidie dokta

 27. Asante doct mimi litaka kujua jinsi yakupata mtoto wa kike tafadhali docta,

 28. Aisha Hashim Aisha Hashim says:

  Mimi nataka mtoto ila mirija yangu imebana msaada wako nitumie kitu gani ili itanuke vizuri ipitishe uchafu vizuri na mimba ingie

 29. Asante doct kwa ushauri wako.in swali ninahitaji Mtoto Wa kike nifanyeje?

 30. Asante doct kwa ushauri wako.in swali ninahitaji Mtoto Wa kike nifanyeje?

 31. Nifanyeje ili kupata aina ya mtoto kike au kiume_

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *