Kachumbari/fresh mixed salad

Kachumbari
Kachumbari

Kachumbari/fresh mixed salad

Mahitaji:

Utahitaji mboga mboga fresh zifuatazo, si lazima uwe nazo zote lakini walau zifikie 5;

 • Nyanya fresh
 • Vitunguu maji
 • Pilipili hoho
 • Kabeji
 • Lettuce (tamka letusi)
 • Maharage machanga (greenbeans (tamka; grinibinzi))
 • Kaloti
 • Tango
 • Rocket/ruccolla (tamka; roketi au rukola, kama inapatikana eneo ulipo)
 • Ndimu/limau fresh
 • Chumvi
 • Mafuta ya zaituni (Olive oil) vijiko 2 au 3.

INAVYOANDALIWA HATUA KWA HATUA:

1. Osha vizuri mboga mboga zote katika maji mengi yanayotiririka.

2. Kwenye mahitaji yetu kuna mboga mboga inaitwa maharage machanga/greenbeans, haya ni vigumu kidogo kuyala moja kwa moja mabichi; utatakiwa kisha kuyaosha ondoa miishio yake pande zote mbili huku na huku na ukate katikati kila harage kupata vipande viwili na uyachemshe kidogo katika maji au unaweza kuchemsha maji vya kutosha kisha zima moto na utumbukize hayo maharage ndani yake kwa dakika kama 5 hivi kisha yachuje toka katika maji, hii inafanyika ili tuweze kula bila shida na kupunguza ukakasi au ule uchungu wake kidogo. Unapopasha au kuzichemsha hizi green beans unaweza kuongeza kiasi kidooogo cha baking powder (tamka; beking’i poouda) ndani ya maji ili kuyafanya maharage haya yasipoteze ile rangi yake nzuri ya ukijani kibichi cha kupendeza.

3. Kata pilipili hoho mara mbili na uondoe zile mbegu mbegu zake za ndani na sehemu zingine zisizohitajika, menya vitunguu na kaloti. Tafadhari, usimenye nyanya wala usitoe mbegu mbegu zake za ndani.

4. Sasa kata kata mboga mboga zako zote katika mkato wa aina moja unaoupenda, kuna mikato ya aina nyingi; unaweza kukata katika duara (rings), pembe nne, pembe tatu, kyubu, na kadharika. Kwa pishi hili mimi napenda zaidi kukata mboga mboga zangu katika julliene (unakata nyembamba ndefu kama fimbo hivi).

5. Kisha kukatakata mboga mboga zako zote sasa zichanganye pamoja katika bakuli kubwa.

6. Mwisho kabisa iunge salad yako na chumvi, maji/jusi ya ndimu na vijiko 2 u 3 vya mafuta ya zeituni. Tafadhari iunge salad yako (yaani iongeze chumvi, ndimu na mafuta) dakika 1 kabla ya kuandaa mezani hivyo kama umemaliza kuitengeneza na unadhani utahitaji kusubiri robo saa au nusu sasa ndipo ukae ule basi si vema kuiunga papo hapo kwakuwa chumvi itaongeza limchumzi lisilohitajika kwenye salad yetu pia mafuta yataifanya ilainike kiasi inaweza kukera machoni mwa anayekula.

7. Waweza kula sasa/Enjoy.

MHIMU:
a. Tumia mafuta ya zeituni (olive oil) tu na si mafuta mengine kwakuwa chakula hiki hakipikwi katika moto na ni mafuta haya tu yanaweza kuliwa bila kupikwa katika moto bila shida yoyote. Kama mahali ulipo huwezi kupata mafuta ya zeituni unaweza kuwasiliana na mimi.
b. Baada ya kukatakata vitunguu, usivioshe au usivisuguwe katika chumvi, kufanya hivyo ni kupunguza thamani ya kitunguu mwilini.
c. Kuna wanaoshikilia dhana kuwa nyanya ziondolewe mbegu mbegu zake katika kachumbari, bali mi nakushauri usiondoe mbegu za nyanya kwani unaondoa lishe mhimu mwilini ndiyo maana utalazimika kuwa na nyanya ambazo hazijaiva sana ili usikereke na hali hiyo.

Utaila na nini hii kachumbari/ fresh mixed salad?
Kachumbari/Fresh mixed salad ni chakula cha pembeni (side dish) kinachosindikiza chakula kingine kama vile samaki wa kukaangwa (fried fish), nyama choma, au kuku wa kukaangwa (fried chicken) na kufanya mlo kamili ama wa mchana au jioni. Pia wengine hupenda kuitumia katika pilau.

kachumbari

Hakikisha haipiti siku hujapata hii kitu japo katika mlo mmojawapo iwe ni mchana au usiku.

 

Makala nyingine zinazohusiana na hii:

 

Kwa maswali na ushauri zaidi: WhatsApp +255769142586

Jiunge na ukurasa wangu wa facebook kwa kubonyeza hapa => facebook

Je Umeipenda makala hii? Ninakaribisha mchango wako wa mawazo au ikiwa una swali nitafurahi zaidi kwani ni faraja kwangu kuona nimekujibu vizuri.

(Imesomwa mara 13,215, Leo peke yake imesomwa mara 45)

You may also like...

12 Responses

 1. helena mbonde says:

  Nimefaidika sana na maelezo.

 2. helena mbonde says:

  Ubarikiwe sana,

 3. paul says:

  asante kwa elimu hii

 4. pamela mziray says:

  Tunashukuru mno kwa kutuelimisha kaka maana tulikuwa hatufahamu mengi hasa kwa manufaa ya maisha yetu

 5. Hasheem says:

  Nina tatizo la nguvu za kiume,

 6. Hasheem says:

  Nina tatizo la nguvu za kiume, niliwahi kujichua nikiwa sec, naomba maelekezo, tiba, na bei

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *