Kitunguu Swaumu hutibu magonjwa 30

Kitunguu swaumu
Kitunguu swaumu

Mungu anaposema watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa hamaanishi maarifa ya kutengeneza au kuendesha ndege, ni maarifa ya kawaida tu katika maisha yetu ya kila siku ambayo yanaweza kubadilisha afya na ustawi wetu. Moja ya mmea ambao umependelewa sana na Mungu kwakuwa na viinilishe vingi na mhimu sana kwa afya ya binadamu ni kitunguu swaumu. Kitunguu swaumu ni dawa karibu kwa kila ugonjwa.

Kitunguu swaumu ni jamii ya vitunguu ambayo kwa kitaalamu huitwa Allium sativum. Jamii hii ilianza kutumika katika mabara mbalimbali duniani hususani Asia, Afrika na Ulaya takribani miaka 6000 iliyopita. Matumizi makuu nyakati hizo yakiwa viungo katika mboga na tiba.

Kitunguu swaumu kimetajwa kwenye vitabu mbalimbali vya dini vikielezea faida zake katika kutibu maradhi mbalimbali yasababishwayo na bakteria, matatizo katika mapafu, matatizo katika mfumo wa umen’genyaji chakula, na matatizo ya kuishiwa nguvu.

Historia inaonyesha kuwa, vitunguu swaumu vilianza kutumika nchini China mwaka 510 kabla ya Kristo na pia vilitumiwa na wanajeshi wa Ugiriki na Warumi. Aidha wasafiri wa vyombo vya baharini na vijijini pamoja na wakulima barani Afrika walivitumia sana. Kuna baadhi ya imani watu wanaamini kitunguu swaumu kina uwezo wa kufukuza hadi wachawi! hivyo kama unatokewa unapata usingizi wa usioeleweka au unakabwa kabwa na wachawi hebu jaribu kitunguu swaumu na utuletee mrejesho

Mwaka 1858, mtafiti na mwanasayansi wa nyakati hizo, Louis Pasteur aligundua uwezo wa kitunguu swaumu katika kuua vimelea mbalimbali vinavyosababisha magonjwa, na hivyo vikaanza kutumika kama dawa ya kusafishia vidonda na kuzuia kidonda ndugu hasa zama za vita ya kwanza na pili ya dunia. Isitoshe, mpaka sasa zipo dawa kadhaa zilizotengenewa kwa kutumia jamii hii ya vitunguu swaumu ikiwemo dawa ya kusafisha mdomo (mouth wash).

Huko sokoni tayari nimeviona vitunguu swaumu kutoka China na Afrika kusini ambavyo vyenyewe huwa vina punje kubwa nene na huwa rahisi kuvimenya, hata hivyo ili upate faida hizi zote hapa chini naendelea kukushauri utumie vitunguu swaumu vyetu vinavyolimwa hapa Tanzania kwani hivyo vya kutoka nje pamoja na kuwa ni rahisi kuvimenya lakini ubora wake si kama ule wa vitunguu vyetu.

Hakikisha kila mboga unayopika haikosi kitunguu swaumu ndani yake na ikibidi ukiweke mwishoni mwishoni unapokaribia kuipuwa mboga yako toka katika moto kwamba kisiive sana hata kupoteza viinilishe vyake. Kama una friza au friji ya kawaida unaweza kumenya vitunguu swaumu hata kilo nzima na kuvitwanga kidogo katika kinu, vifunge vizuri katika bakuli au mfuko wa plastiki na uvihifadhi katika friza au friji na hivyo kila unapopika unachukuwa tu na kukitumia ili kuepuka usumbufu wa kukimenya kila siku.

Lakini ili upate faida zaidi za kitunguu swaumu utatakiwa ukimeze katika maji au ukichanganye na mtindi kikiwa kibichi, yaani bila kupitishwa katika moto au kuwa kimepikwa.

Chukuwa kitunguu swaumu kimoja

kitunguu swaumu

kitunguu swaumu

 

Kigawanyishe katika punje punje

kitunguu swaumu

kitunguu swaumu

 

chukua punje 6

kitunguu swaumu

kitunguu swaumu

 

Menya punje moja baada ya nyingine

kitunguu swaumu

kitunguu swaumu

 

Kisha vikatekate (chop) vipande vidogo vidogo sana na kisu na uache hivyo katika hewa kwa dakika 10

kitunguu swaumu

kitunguu swaumu

Meza kama unavyomeza dawa na maji nusu lita kila unapoenda kulala. Namna nyingine nzuri zaidi ni kuviweka ndani ya kikombe kimoja (robo lita) cha mtindi freshi koroga vizuri na unywe na hii itakusaidia kupunguza harufu mbaya ya kitunguu swaumu huku ukipata faida nyingine mhimu zilizomo kwenye mtindi.

Katika zoezi hili nimetumia mtindi wa Tanga freshi na nimeona matokeo mazuri sana ikiwemo ngozi kuendelea kung’aa na kitambi ni kama kimeisha kabisa kwa siku 7, hivyo siyo lazima uwe mtindi uliotengeneza nyumbani bali hata huo wa dukani wa Tanga fresh bado ni mzuri pia (bila shaka Tanga fresh watanipa hela ya soda kwa kuwapigia promo)!

Fanya hivi kila siku au kila mara unapopata nafasi na hivyo utakuwa mbali na kuuguwauguwa. Mama mjamzito chini ya miezi 4 ni vema asitumie, kwa ujumla tu mjamzito uwe makini utakapotumia kitunguu swaumu kwa namna hii kama wewe ni mjamzito.

kitunguu swaumu

Kitunguu swaumu kilichokatwakatwa/chopped

Kitunguu swaumu hutibu magonjwa 30

mbegu-za-maboga

Haya ni baadhi ya magonjwa yaliyothibitika kutibika na yanatibika au kukingika na kitunguu swaumu:

 1. Huondoa sumu mwilini
 2. Husafisha tumbo
 3. Huyeyusha mafuta mwilini (kolestro)
 4. Husafisha njia ya mkojo na kutibu U.T.I
 5. Hutibu amoeba, minyoo na Bakteria wengine
 6. Huzuia kuhara damu (Dysentery)
 7. Huondoa Gesi tumboni
 8. Hutibu msokoto wa tumbo
 9. Hutibu Typhoid
 10. Huondoa mabaka mabaka kwenye ngozi
 11. Hutibu mafua na malaria
 12. Hutibu kifua kikuu (ukitumia kitunguu swaumu kesho yake unaweza kutokwa na makohozi mengi tu ambayo ni ishara kwamba kweli kinatibu kifua kikuu (TB)
 13. Hutibu kipindupindu
 14. Hutibu upele
 15. Huvunjavunja mawe katika figo
 16. Hutibu mba kichwani
 17. Huupa nguvu ubongo. Kazi nzuri niliyopenda zaidi katika kitunguu swaumu.
 18. Huzuia meno kung’ooka na kutuliza maumivu
 19. Huongeza SANA nguvu za kiume pia hutibu uanithi (kushindwa kusimama kabisa uume)
 20. Hutibu maumivu ya kichwa
 21. Hutibu kizunguzungu
 22. Hutibu shinikizo la juu la damu
 23. Huzuia saratani/kansa
 24. Hutibu maumivu ya jongo/gout
 25. Huuongezea nguvu mfumo wa mmeng’enyo wa chakula
 26. Huongeza hamu ya kula
 27. Huzuia damu kuganda
 28. Husaidia kutibu kisukari
 29. Husaidia kutibu tatizo la kukosa usingizi (ni kweli, na ni moja ya kazi nyingine ya kitunguu swaumu iliyonishangaza zaidi) pia kinaondoa msongo wa mawazo/stress na kukufanya uishi miaka mingi
 30. Huongeza SANA kinga ya mwili na kwa muda mfupi, kijaribu na ulete majibu

Sifa kuu zinazokifanya kitunguu swaumu kuwa na uwezo na faida zilizoainishwa hapo juu ni kule kuwa kwake na viasili kadhaa (ingredients) ambavyo vinafanya kazi tofauti tofauti. Uwezo wake wa kiutendaji unatokana na mambo yafuatayo;

 • Vina uwezo wa kusababisha kutanuka kwa mishipa ya damu (vasodilation) kwa kubadilisha polysulfides zilizopo ndani yake kuwa hydrogen sulfides kwenye seli nyekundu za damu.
 • Husaidia uthibiti wa kiwango cha sukari mwilini kwa kushusha kiwango cha kemikali ya homocystine na kupunguza madhara ya kisukari.
 • Iwapo vitapondwa pondwa vizuri, vitunguu swaumu hutoa kemikali iitwayo Allicin ambayo ni dawa dhidi ya bateria, na phytoncide ambayo huua fangasi wa aina mbalimbali.
 • Harufu mbaya ya kitunguuu swaumu hutokana na gesi aina ya hydrogen sulfide ambayo hutolewa baada ya kuvila.

Nini madhara ya vitunguu swaumu?

Ukiacha faida zake, vitunguu swaumu pia vina hasara na madhara mbalimbali kwa mtumiaji. Madhara hayo ni pamoja na;

 • Harufu mbaya mdomoni ambayo hutokana na kemikali ya AMS (allyl methyl sulfide). Harufu mbaya hii, hata hivyo, yaweza kupunguzwa kwa kunywa maziwa, kunywa maji mengi au kutafuna karafuu. Na nimeshuhudia nikinywa kwenye mtindi hii harufu ni kama haipo kabisa na hata ukijamba haikutokei ile harufu mbaya sana kama ukinywa vitunguu swaumu katika maji
 • Kwa baadhi ya watumiaji, vinaweza kuwaletea mzio au mcharuko mwili (allergies au inflammatory reactions)
 • Kichefuchefu, Kutapika na kuharisha. Ikikutokea kuharisha siku mbili tatu furahi kwani ni njia mojawapo ya mwili kujisafisha
 • Huweza kusababisha hatari ya kuvuja damu, kwa sababu huzuia kazi ya seli sahani (platelets) zenye kusaidia kuganda kwa damu kushindwa kufanya kazi yake vizuri, na hususani kwa mama wajawazito, baada ya upasuaji au mara baada ya kujifungua.
 • Huingiliana katika utendaji kazi wake na dawa kadhaa kama vile warfarin, antiplatelets, saquinavir, dawa za shinikizo la damu kwa ujumla hasa calcium channel blockers, na antibiotiki za jamii ya quinolone kama vile ciproflaxacillin.
 • Aidha, vinaelezwa pia kuwa na madhara kwa wanyama jamii ya paka na mbwa.

Kumbuka kitunguu swaumu kinaweza kuwa na faida nyingi zaidi ya hizi lakini bado nakushauri utumie kiasi kidogo (punje 6 tu) kila siku kwa kipindi kirefu wiki 2 au 3 hata mwezi ili uone faida zake zaidi. Ikikutokea tangu umeanza kutumia kitunguu swaumu kichwa kinauma zaidi unaweza kupumzika siku mbili hivi na baadaye unaendelea hivyo hivyo.

Tafadhari SHARE post hii kwa manufaa ya wengine.

Jiunge na ukurasa wangu wa facebook kwa kubonyeza hapa => facebook

Je Umeipenda makala hii? Ninakaribisha mchango wako wa mawazo au ikiwa una swali nitafurahi zaidi kwani ni faraja kwangu kuona nimekujibu vizuri.

mbegu-za-maboga

(Imesomwa mara 154,269, Leo peke yake imesomwa mara 828)

You may also like...

1,995 Responses

 1. Nashukuru sana kwa hakili hii njema ya kuwasaidia watanzania wengi mungu hakubariki ndugu

 2. Duuu,saaafi kweli,hiii ndo matumizi halali ya mitandao,inaelimisha,inafundisha na kutoa faida kwa msomaji.

 3. Cesilia Kway Cesilia Kway says:

  Nashuru kwa elimu Mungu akubariki ungeweka na namb yako napia kama unaelimu zaidi endelea kutuelimisha

 4. Nilikuwa sijui nanilidhani porojo tu kumbe ndio kilivyo

 5. iyo kuusu wachaw mkuu mimi nikilaga kitunguu swaumu au nikanukia kitunguu swaumu wachaw nawaona live ktk macho yangu nyakat za usiku na nilikuwa natumia kitungu swaumu kama dawa mkuu kwaiyo nilikuwa cj gundua kip knacho sababisha mm kuwaona wachaw na sibitisha iyo nikwel mkuu kitunguu swaum kina fukuza wachaw na ikiwezekana kuwaona pia walau hii ya kuwaona wachaw uwainanitokea mala kwa mara pindi nilipo kuwa mtoto lakin hi ya kitunguu swaum nime fluliza kuwaona wachw na kwuwafukuza kabisa walau bado ili swala nalifanyia udadc vzur

 6. Asmin Salum Asmin Salum says:

  Hakika nimetumia kitunguu swaum duu! Kimenisaidia sanaaa yani sanaaa asante kk yangu mungu akubariki sanaaaa

 7. Na je nikitafuna inakuaje

 8. Hii ndiyo maana halisi ya mitandao ya jamii. Asante kwa elimu hii nzuri ubarikiwe.

 9. Ally Said Ally Said says:

  Vp kwa mwanamke ambae hashiki uja uzito na anahitaji sana kuzaa kitunguu swaumu kinamsaidiaje?

 10. Je, waweza changanya na asali?

 11. Kweli kinapunguza kitambi,nitumieje mpendwa ili kinisaidie kupunguz mafuta/ kitambi

 12. Ndama Korofi Ndama Korofi says:

  Kama mimi ni mchawi nikitumia itaaribu mamboyang ya kichawi na ninaumwa

 13. Mbona docter watu wengi umewajibu maswali yao mimi mwezi sasa hujanijibu au swali langu halieleweki swali kinasema hivi mimi nina vidonda vya tumbo zaid ya miaka 7 na pia nilikua naitaji kuanza tiba ya vitunguu saum ili kuweka mwili sawa ila je kuna mathara yoyote endapo nikitumia au vp

 14. Kwa mwenye vidonda vya tumbo vp kuhusu mtind maana hua nikitumiaga mtindi tumbo linaujaa gess pia maumivu nayapata unashaurije kuhusu hilo

  • Mtindi usizidishe, ni kikombe kimoja tu (robo lita) ikibidi hata chini ya hapo kwa siku la sivyo tumbo litasongamana na utaongezeka uzito. pia ongeza kiasi cha unywaji maji kila siku

 15. kuondoa mabaka una2miaje?

 16. Husna Chris Husna Chris says:

  Ubarikiwe sana kaka

 17. Sasa wajawazito hawaruhusiw KBS.. au ipite miez hyo minne

 18. Rama Irunde Rama Irunde says:

  Asant xana banah kw kuniongezea maarfa

 19. Ninasumbuliwa na chembe ya moyo naweza kutumia hii

 20. Mbona nikitumia punje 6 nalewa nitaweza wiki2 nina tatizo lashindikizo ladam kichwa taifodi naomba ushauli zaidi pia nikitumia muke ananihama kwa arufu

 21. Asante sana nimekuelewa vizuri sana nitatumia nizione faidazake

 22. Pritty Macha Pritty Macha says:

  Kitinguu saumu ni Dawa sana Mungu akubariki kwa kuelimisha jamiii ujaficha uweza wako. Uliojaliwa na Mungu hujaitadi pesa kama hawa doctors wengine

 23. vp kuhusu dawa ya kuondoa harufu mdononi

 24. Safi sana ahsant.

 25. Neymah Mbowe Neymah Mbowe says:

  Asante ndugu leo siku ya tatu, namalizia nami nipate ushuhuda, ila mimi nameza na maji tuu

 26. Umenielimisha sana bigup bro

 27. Kepha Festo Kepha Festo says:

  Inapozuia damu kuganda huoni kuwa ni hatari kwan mtu atapoteza damu nyingi na hata kupelekea kifo kwa mtumiaji

 28. mim mwenyewe nimebobea ktk matumizi yake.natumia kwa miaka 13 SASA,NPO POA BALAA

 29. Mimi huwa natafuna viwili ASB na viwili jioni kumbe Ni sita alafu nakunywa na maji

 30. Nimebarikiwa Sana tena Saana hapa nikutumia tu japo awali nilikuwa nachanganya vitunguu swaaumu tangawizi robo au nusu navitwanga vyote nachanganya na konyagi km Maji au mbadala wa Maji unaviloweka wiki mbili baada ya hapo unaanza kutumia km robo glas asubuhi na jioni hiyo vipi ulisha wahi kuisikia? Au umechukuliaje huu mchanganyiko wa swaaumu tangawizi na konyagi?

 31. Shukulani kaka kwa kutujuzaa mungu

 32. mungu akujaliee mengine utujuzee tenaa kaka

 33. Neymah Mbowe Neymah Mbowe says:

  Mimi nataka kupunguza tumbo, nitumie kwa wiki moja au niendelee

 34. Kweli ni dawa tosha

 35. Rose Sollo Rose Sollo says:

  Samahanii naomba nkuulize mm nasumbuliwa na tones nmeambiwa imepatwa na infenction, nkapewa dawa ntumia lkn bado haijaisha, saivii nmeandikiwa nyingine dawa natumia, je naweza kutumia kitunguu saumu tatizo likaishaaa

 36. Kharid Ahmed Kharid Ahmed says:

  Kaka kwelikabisa Mimi nikimeza pune 6 kichwa kinauma Kwambali nameza 3 asubui 3 jion kuna ubaya wwt

 37. Sky Walcker Sky Walcker says:

  Asante Kwa Elimu Nzuri Mimi Niliwai Kutumia Nilikuwa Namenya Punje Moja Asubuhi Na Kuimeza Kama Kidonge Mala 2 Kwa Siku Kumbe Zilikuwa Punje Chache ?

 38. Kweli kabisa kitunguu swaumu ni dawa hata mm nilikuwa nasumbuliwa na tatizo la tumbo la amoeba ila tokea nimeanza kukitumia nimepona kabisa

 39. je kwa wanaonyonyesha hakina madhara!! na kinaweza kupunguza tumbo kwa waliojifungua kwa operation??

  • Kwa anayenyonyesha anaweza kukitumia. Chenyewe kinaondoa mafuta mwilini ikiwemo cholesto pia. Kwahiyo yeyote anayetaka kupunguza unene au uzito au mafuta mwilini anaweza kujaribu kukitumia huku ukiambatanisha na mbinu zingine ikiwemo kubadili mtindo wa vyakula vyako na mtindo wako wa maisha kwa ujumla. Kuongezeka uzito ni rahisi lakini kupungua sasa unahitaji ujirekebishe vitu vingi kwa pamoja ili kupata mattokeo mazuri

  • Nicka Micka Nicka Micka says:

   Kaka fadhili ukivisaga na kuwek kweny maziwa napo unaezkutmia

  • Nicka Micka unaweza ndugu ila napendekeza kwenye mtindi na siyo maziwa na nina sababu za kupendelea mtindi zaidi kuliko maziwa

  • Mery Pima Mery Pima says:

   mtindi niip tena namtindi wamua au

 40. Fatma Masudi Fatma Masudi says:

  Punje moja unaikata mara sita?

  • Lakini ili upate faida zaidi za kitunguu swaumu utatakiwa ukimeze katika maji au ukichanganye na mtindi kikiwa kibichi, yaani bila kupitishwa katika moto au kuwa kimepikwa.

   1. Chukuwa kitunguu swaumu kimoja
   2. Kigawanyishe katika punje punje
   3. Chukua punje 6
   4. Menya punje moja baada ya nyingine
   5. Kisha vikatekate (chop) vipande vidogo vidogo sana na kisu na uache hivyo katika hewa kwa dakika 10
   6. Meza kama unavyomeza dawa na maji nusu lita kila unapoenda kulala. Namna nyingine nzuri zaidi ni kuviweka ndani ya kikombe kimoja (robo lita) cha mtindi freshi koroga vizuri na unywe na hii itakusaidia kupenguza harufu mbaya ya kitunguu swaumu huku ukipata faida nyingine mhimu zilizomo kwenye mtindi.

   Katika zoezi hili nimetumia mtindi wa Tanga freshi na nimeona matokeo mazuri sana ikiwemo ngozi kuendelea kung’aa na kitambi ni kama kimeisha kabisa kwa siku 7, hivyo siyo lazima uwe mtindi uliotengeneza nyumbani bali hata huo wa dukani wa Tanga fresh bado ni mzuri pia

 41. Poa poa nimewaelewa sana

 42. kaka fazili mm sijaelewa kidogo kwamba ukisha chambua pingili sita sawa unavikata katikati vinatoka 12 kwahiyo unakunywa vyote na mtindi au unakunywa 6 tu

  • Lakini ili upate faida zaidi za kitunguu swaumu utatakiwa ukimeze katika maji au ukichanganye na mtindi kikiwa kibichi, yaani bila kupitishwa katika moto au kuwa kimepikwa.

   1. Chukuwa kitunguu swaumu kimoja
   2. Kigawanyishe katika punje punje
   3. Chukua punje 6
   4. Menya punje moja baada ya nyingine
   5. Kisha vikatekate (chop) vipande vidogo vidogo sana na kisu na uache hivyo katika hewa kwa dakika 10
   6. Meza kama unavyomeza dawa na maji nusu lita kila unapoenda kulala. Namna nyingine nzuri zaidi ni kuviweka ndani ya kikombe kimoja (robo lita) cha mtindi freshi koroga vizuri na unywe na hii itakusaidia kupenguza harufu mbaya ya kitunguu swaumu huku ukipata faida nyingine mhimu zilizomo kwenye mtindi.

   Katika zoezi hili nimetumia mtindi wa Tanga freshi na nimeona matokeo mazuri sana ikiwemo ngozi kuendelea kung’aa na kitambi ni kama kimeisha kabisa kwa siku 7, hivyo siyo lazima uwe mtindi uliotengeneza nyumbani bali hata huo wa dukani wa Tanga fresh bado ni mzuri pia

  • Emma Mlowe Emma Mlowe says:

   Mimi huwa nakitwanga harafu nachanganya kwenye maji nakunywa kila siku.yaani nimepata faida sana.pia inapunguza hata hasira.

 43. Na inakuwaje kw mama mjamzito??? Inamadhara??

 44. Naomba kuuliza navichanganya na mtindi ktk kikombe mana nimeona umesema making wa kama ninavyokunywa dawa na maji nieleweshe apo ndungu nichanganye na mtindi au nivimeze kwa kutumia maji kama navokunywa dawa za kawaida

  • Kuna machaguzi mawili hapo kama umesoma vizuri maelezo ya hii post, ama unakunywa kama unavyomeza dawa za kawaida (panadol) na maji nusu lita (hautafuni kitunguu swaumu) au unachanganya kwenye mtindi. Karibu

 45. Mungu akubariki sana bro !

 46. Rose Ikela Rose Ikela says:

  Mungu akubariki uzidi kutujuza mambo mengi zaidi

 47. Ubarikiwe kwa kutuelimisha,mm nipo kwenye dozi ya maleria natumia alu je nikimeza k saumu aitaleta shida

 48. Big up sana kwa somo zuri ambalo binafsi nitalitendea haki. MUNGU a bariki kazi za mikono yako. Ni lazima kunywa usiku tu!

  • Amina. Ndiyo usiku ndiyo vizuri zaidi labda kwa sababu huendi kazini muda huo au hukutani na watu wengi tena baada ya hapo ili kuepuka usumbufu wa harufu yake, halafu ni vema kifanye kazi tumboni ukiwa usingizini nk nk

 49. Joseph Aman Joseph Aman says:

  Nimependa kuelimishwa!

 50. Amini Em Amini Em says:

  Huwa natafuna tu,je nile punje ngapi kwa CKU na kuna madhara yoyote kwa mgonjwa wa unlcers

  • Ukitumia kwa style hii nimeelezea kwenye post hii hakika utaona matokeo mazuri mapema. Ukishakikatakata (chop) kiache kwenye hewa kwa dakika 10 kabla ya kukichanganya na mtindi. Ni dawa pia ya vdonda vya tumbo sababu kinaondoa gesi, kinaua virusi na bakteria mbalimbali mwilini. Kama una vidonda vya tumbo unaweza kuanza na kiasi kidogo kwanza cha punje za vitunguu swaumu kama punje 3 hivi badala ya 6. Amini Em

 51. Matius Urio Matius Urio says:

  NIHAKIKAA MUNGU MWEMA KWAKILA JAMBO AMETUZAWADIA KILA KITU KTK HII DUNIA KWAHVYO TUMSHUKURU KTK YOTE

 52. Matius Urio Matius Urio says:

  MIMI KWANGU NIKAMA SHERIA MAANA NATAMBUA UMUHIMU WA VITU HIVYOO TUSHIRIKIANE KWA PAKOJAA

 53. Anna Mlawa Anna Mlawa says:

  Asante ubarikiwe sana fadhilipaulo.com

 54. Asante sana kwa elimu yako Mungu akubariki

 55. Anna Utou Anna Utou says:

  Asante kwa ujumbe mzuri

 56. Zena Masasi Zena Masasi says:

  Kama UnaTB naumeshaanza kutumia dawa za TB Je unaluhusiwa kutumia dozi hii

 57. Kuanzia wiki ijayo naanza dozi rasmi. Punje sita kila siku kwa mwezi mzima.

 58. Nywele Miudu Nywele Miudu says:

  samahani ndugu naomba niambi kwa typhod unatumiaje?

 59. Petro Bahha Petro Bahha says:

  Samahani Kaka Kuhusu Upungufu Wa Nguvu Za Kiume,utatumia Maisha Au Vipi?

 60. Candy Stima Candy Stima says:

  Nimekukuba na Mimi naanza dozi leo

 61. Sia Peter Sia Peter says:

  Amina ubarikiwe kwakutupa elimu ya kitunguu

 62. Amoce Mbotwa Amoce Mbotwa says:

  Uko wapi tutakupata

 63. umetaja punje6 je unameza zote kwa pamoja au kama palacetamol yan2x3 au 6kwa pamoja?

 64. Rahma Hashim Rahma Hashim says:

  Kitunguswaumu.kinatibu.magonjwa.gani

 65. Sefu Mazoya Sefu Mazoya says:

  Nakushukulu sana leo nimepata faida ya kitunguu swaumu je kwamfano nikivitafuna bilayakuvitwanga nitakuwa nimekose

 66. Safi Sana Watu Wengi Wanakosa Akili Kuweka Pst Za Kufundisha Jamii ,.Wanaweka Post Za Ajabu ,.Hii Post Ni Nzuli Sana

 67. Juma Rajabu Juma Rajabu says:

  nimekuelewa jekwamtotomwenye umri wamika10kushasha jeanatumije? nauyo mtoto anatatizo lakifua kukoowa nakukoromama kwakubanwa napumzi

 68. Wadi Mtwana Wadi Mtwana says:

  Safi sana kaka na hii sio kwa mgonjwa tu hata kwa walio wazima k.

 69. Asente Sana Nimefarijika Kwamagonjwa Madogo

 70. Edna Mghase Edna Mghase says:

  Asante sana nimeipenda

 71. Emma Pol Emma Pol says:

  Nashukuru Kwa mafunzo yako

 72. Adam Daggaa Adam Daggaa says:

  Ahsante sana kwa Elimu sana barikiwa !!!

 73. Ahsante kwa mafunzo

 74. Je kama unatumia dawa unaruhusiwa kuvitumia?

 75. Kaka asante nimesoma hii dawa kwa kweli nimeamasika mm ni muanga waugonjwa wa vidonda vya tumbo naanza leo hii tumbo linauma nakuchoma sana ngoja nianze doz ubarkiwe

 76. Asante sana doctor #Fadhilipaulo_com MUNGU na akubariki kwa kutufundasha, sababu wengi we2 tulkuwa hatujui ata kama tulkuwa tunajuwa lkn n vchache.

 77. He kama unamimba mwezi mmoja huwezi kutumia?

 78. Sasa ukitaka kutumia ni lazima uviponde au kusaga

 79. Lucy Komanya Lucy Komanya says:

  Asante kwa somo zuri, mwenyezi mungu akupe maarifa zaid uzid kutufahamisha, ubarikiwe saaanaa

 80. Tina Ludo Tina Ludo says:

  Je watot wadogo wanafaa kutumia

 81. Nakili uliyofundisha, kwa ushuhuda , mi tangu nianze kutumia, nimejizui kutumia dawa yoyote ya madukani, wala sijawahi kuugua UGONJWA WA KUNIACHISHA KAZI kwa miaka tisa sasa. Nasema mbele ya Mungu. Namshukuru Mungu .

 82. Nakubali bila kupinga

 83. Ata Mtot Anawza Ktumia Au

 84. Rajabu Saidi Rajabu Saidi says:

  Nmeelewa sana juu ya ktunguu swaumu kuanzia leo ntafanya kama ulivosema bwana #Fadhili asantee sana kwa ushauri wako

 85. ndugu jitibu bila kinga

 86. jitibu bila gharama yoyote chukua tahadhari mapema

 87. Isack John Isack John says:

  Mm huwa natumia punche moja moja asubuhi nchana na jioni je nakosea au

 88. habari yako kaka fadhili mm sijaelewa kidogo nikisha chambua punje 6 navimenya sasahapa ndio sipaelewi navikata katikati vitakuwa 12 sasa ndio nachukuwa sita natafuna na mtindi au inakuwaje

 89. Umesema kuwa ukikosa Usingizi na kukabwa na wachawi unakitumiaje plse nifafanulie!

 90. John Elias John Elias says:

  Nakama unavidonda vya tumbo kunatatizo

 91. Kama hauna uwezo wa maziwa

 92. Abuu Mrope Abuu Mrope says:

  sasa nauliza swali moja kwa upande wangu huwa natafuna kawaida tu kitunguu swaumu, je kinamazala gani ukitafuna normal na faida gani ukitafuna kawaida tu………..???

 93. kuhusiana na nguvu za kiume una2miaje me zangu zimepungua 2

 94. mm naomba namba yako 2 2weze kuwasiliana kk

 95. Sia Mtema Sia Mtema says:

  Xamahan me nipo njee ya mada, mafuta ya nazi yanaxaidia nn kwa mt mzima anapotumia kujipaka,

 96. vp ukitumia kwenye maji unatafuna ?

 97. Asalaam Aleykum. Mm nataka kujua jinsi ya kupunguza kitambi( tumbo) natakiwa nitumie punje ngapi na nichanganye na nn na kwa siku ngapi?

 98. Jovin Maijo Jovin Maijo says:

  Nimewahi kuambiwa na ndugu yangu mmoja kua kitunguu swaumu punje zake ukichanganya na pesa zako huwezi ibiwa na wezi Wa mfukoni,hahahahaha ila kuhusu mchawi inawezekana kumzuia

 99. Saleh Saleh Saleh Saleh says:

  Vizuri kwa elimu yk imesaidia ,tujuze namegine yenye faida nasi.

 100. ninatafuna au ninasaga nichanganye nakitu au chenyewe tu naomba nisaidie

 101. Tunashukuru kwa kutupa elimu nzuri ya afya.

 102. Unakunywa kutwa Mara ngpi

 103. Tunashukuru kwa kutupa elimu nzuri ya afya.

 104. Hogera kwa ushauli wako

 105. Asante sana kwa ushauri. M. Mungu akujaalie

 106. Kiongoz vp mbona nimetumia kitunguu swaumu kwa mda wa wiki moja nikasikia kichwa kinauma ni dawa au kuna tatizo?

 107. Hamisi Salum Hamisi Salum says:

  fanyeni mazoezi aya mengine asaidii chochote

 108. Mm niko na ulcers nkitumia kitunguu saumu Naeza kupona?

 109. Lawi Lunoba Lawi Lunoba says:

  Vp kuhusu tatzo la giri inasaidia na tatzo la mabaka meusi mwilini

 110. Vip kuhucana na maradhi ya pumu! Maana nilielekezwa juu ya moja wapo ya dawa ya pumu ni kwamba, unachukua haba soda na tangawizi unachanganya pamoja na asali safi, swali lipo hapa jee ktk mchanganyo huo ukihucsha na hicho kitunguu swaumu!

 111. Je kwa wenye shinikizo la chini la damu

  • Wenye presha ya kushuka ni vema wasitumie. pia nitafute WhatsApp +255769142586 kama una presha ya kushuka kama upo tayari kuna dawa ya mtishamba nahitaji watu wafanyie majaribio

 112. Yusuf Mtui Yusuf Mtui says:

  ni kweli na nina imani hiyo

 113. Abali mwalim jee izo punje unazikatakata au nnzima ivyoivyo

 114. Hizo punje sita ni kwa siku

 115. Salum Salum Salum Salum says:

  Kaka fadhilipaulo mm nipo kwenyekuongeza nguvu za kiume ukishakichambua na kukikata unatumia hivyohivyo tu au

 116. Said Zitto Said Zitto says:

  sasa kama mimi situmii mtindi je?,na je siwez kutafuna tu kikawaida na ni lazma iwe usiku?

 117. Elia Shoo Elia Shoo says:

  Samahn kaka angu..naomba unisaidie kidg….kama mtu mwwnye kansa ya kibofu cha mkojo…je kitamsaidia?

 118. Norah Wilson Norah Wilson says:

  Asante sana, barikiwa sana

 119. Mungu akubariki sana kwakutuelimisha

 120. Saleh Sahal says:

  Me nahitaji kutumia kitunguu saumu lakini nataka kujua hili tatizo la kuvuja damu linaweza kujitokeza mpaka kwa wanaume au ni wanawake tu?

  • fadhili says:

   Tatizo la kuvuja damu haliwezi kutokea kirahisi hivyo, ni siku nyingi mimi natumia kitunguu swaumu na sijapata hilo. Unaweza kuamua kutumia siku 1 siku inayofuata unapumzika, kesho unatumia tena hivyo hivyo. #Saleh

 121. Math john says:

  Nimeelewa vizur mi awali nilikua natafuna vitinguu swaum kisha nakunywa maji

  • fadhili says:

   Safi kabisa ndugu. Kutafuna inataka moyo na inaweza kukuletea majeraha yasiyo ya lazima mdomoni. Tumia tu hkama hivi nilivyoeleza. #Math

 122. Iddah karuga says:

  Mimi Niko Kenya I thank you for your help.my child is 9ys Ako Na shosh ya kifua Wakati wa baridi Na kufungana mapua nifanye nini

 123. Thomas Gibson says:

  asante kwa kutuelimisha dokta

 124. Goodhope says:

  Shukrani sana Mkuu kwa taarifa muhimu, AMANI iwe nawe

 125. Goodhope says:

  Ningependa kuona taarifa nyingi kama hizi ni msaada wa kweli kwa jamii zetu usio na gharama na unaosaidia wote watakaofatilia.

 126. Philipo Makungu says:

  Aisee nimeanza dose jumapili tarehe 23/10/2016 nimeanza kuharisha tangu jana nadhani ndio uchafu unatoka hivyo. Jumapili nitatoa matokeo. Asante sana

 127. jesca mwendwa says:

  hivi vitunguu unameza usiku baada ya kula au kabla ya kula?

 128. jesca mwendwa says:

  hivi vitunguu dwaumu nameza kabla ya kula usiku au baada ya kula

 129. jesca mwendwa says:

  mm nina kawaida ya kunywa maji zaid ya lita 3 kila siku je nikitumia hivi vitunguu vitafanya kazi au nitskapotumia vitunguu nipunguze kunywa maji?

 130. Asante kwa taarifa

 131. Hans Brice Hans Brice says:

  BRO SAMAHANI NAOMBA NAMBA YAKO

 132. Kwahiyo kwa magonjwa yote hayo utumiaji wake huo wa maji au kunywa na mtindi?

 133. Asante kk nimekuelewa mwenyezi mungu akulinde akupe afya njema zaidi ya zaidi Amin

 134. Na dozi ya mtoto anatumiya vitungu vingapi mtoto wa miaka 2 na mwingine 5 mngne 7 naomba unieleweahe

 135. Asantee nimielewa haswaa

 136. Mimi numefanyiwa upasuaji wa appendix iliyopasukia tumboni in sahihi kutumia kitunguu swaumu

 137. Daniel Yohana says:

  Ndugu Fadhili mm nasumbuliwa na tatizo la kutokwa na vipele usoni na baadhi Ya sehemu kwenye mwili wangu ikiwemo kichwa nimejaribu sana dawa za hospital vipele vinapungua na kurudi baada ya mda nakosa amani ya kutoka out na marafiki sbb kila mtu ananiuliza nn tatizo..sina tena amani na mwili wangu sbb mda mwingine vinaniwasha sana hasa nikitokwa na jasho je kituunguu saum kinaweza nisaidia au kuna tiba nyngne Ya asili inayoweza kunisaidia sbb nimechoka kupoteza pesa zangu pasipo mafanikio ntashukuru sana ukinisaidia katika hili ndugu yangu

  • fadhili says:

   NIPE PIA UZITO NA UREFU WAKO PIA UMRI WAKO. kITUNGUU SWAUMU, MAFUTA YA HABBAT SODA NA MAFUTA YA ASILI YA NAZI VITAKUSAIDIA HAYO. Angalia pia ikiwa unakunywa maji ya kutosha kila siku au la

 138. Juma rashid says:

  Mm ninmgongwa wa vidonda vya tumbo je nini nifanye niweze kupona “

 139. Athumani Ruvuly says:

  Habari kaka Nina swali hapa ila samahani lakini kwako na kwa wanaosoma comments hizi. Swali ni je kujichua kunasababisha ugumba kwa mwanaume ?

  • fadhili says:

   Habari nzuri kabisa ndugu. Ndiyo kama utazidisha kunaweza kusababisha ugumba na mengine mengi bila idadi. Hata hivyo hakuna sababu ya kujichua, tafuta mke au mchumba uwe naye karibu

 140. Bigritha says:

  Asante kwa ujumbe mzuri Ndugu, ila naomba juju a kwa mama mjamzito kama wa miezi 2-3 je hafai kutumia dawa hii ya kitunguu saumu? na kama ametumia bila kujua mara moja au mbili unamshauri nini ili mimba isitoke?

 141. lazaro says:

  pia hata mimi nina tatizo la kuwai kufika kileleni na pia nina uti ila nimeanza kunywa mtindi nakitunguu swahumu ongera kwa kujitolea Mungu akuxidishie ufanishi zaid

 142. Mzuzu masaga says:

  Natumia vitunguu swaumu na nayaona matokeo vinanisaidia sana pale presha inapokuwa juu

 143. Haroun says:

  Nimekubali kama kitunguu swaum ni kiboko ya dawa na maradhi sugu hapa ndio yanapata dawa hasa.

 144. moses says:

  kaka  naweza kuvimeza bila ya kuvikatakata? je utendaji kaz utakuwa ni sawa na vikiwa vimekatwa katwa?

 145. Danny says:

  Nimejaribu kula leo siku ya pili naharisha bro mpaka nikaogopa ila nimesoma nikaona kuwa hiyo hali inaweza kutokea barikiwa sana ndugu yangu.

 146. Benson Godson says:

  Asante kwa ushauri na elimu yako nzuri “lakini kuna watu wengine wanasema vitunguu swaumu sio vizuri kwa mtu mwenye vidinda vya tumbo mfano mi nilikua natumia sana lakin kuna mtu akaja kuniambiia niache kutumia” je! ni kweli?

 147. pol sijora says:

  bado sijaelewa juu ya matumizi ya hivi vitunguu,he!nikisha vikatakat nivinywe vyote au kidogokidgo?na je nivinywe wakat wa kulala tu au hata mchana?na je ninywe mara moja kwa siku au inakuaj!sijaelew apo naomba unisaidie maana vidonda vya tumbo vinansumbua sana

 148. Julius says:

  Asante sana Dr. Fadhili nimekuelewa vizuri. Napenda kuuliza ni kwa nini tuache vitunguu swaumu vikae dakika 10 kabla ya kunywa na maji au mtindi?

  • fadhili says:

   Kuna kitu mhimu sana kinaitwa ALICIN kwenye kitunguu swaumu ambacho ndiyo dawa, cha ajabu ni kuwa hii ALICIN haitokei isipokuwa tu umeacha kitunguu swaumu hewani kwa dakika 10 baada ya kukikatakata, inahitajika pia kiwe crushed au chopped ndiyo hiyo ALICIN itokee. Ni maajabu kwakweli

 149. Khamis Ali says:

  Tunakushkur sana doctor wetu kwa kutuzindua hili ni jambo muhimu sana katika maisha yetu. Ila nataka nikulize swali doctor me na mke wangu ni watumizi wazur san wa kitunguu swaumu kama ulivo elekeza katika nakala yako ila mke wangu ni mjamzito wa miezi 2 je aache kutumia kwanz mpaka atimize miezi 4? na je kuna madhara yoyote yanaweza kumtokea kwa vile aliwah kula kitunguu thom hali ya kua yeye ni mjamzito chini ya miezi 4?.

 150. Viola says:

  Ahsante sana kaka.. sijui kama huku Kenya naeza pata hizo swaumu za kutoka tanga ?lakini meanwhile wacha tu ntumie hizi zetu za whites.Baraka tele bro.

 151. ton says:

  Nimenunua vitunguu swaumu vya kusagwa vimewekwa na chumvi,je vitafaa?
  nimetumia kijiko kimoja cha chakula je ni sahihi?

 152. Dennis says:

  samahani kaka, me nimeanza kutumia kama ulivyo eleza lakini naona kama imeniletea vipele flani kama vya aleji je unanishaurije kaka

 153. daudi says:

  Aisee sasa nimepata somo safi sana nependa

 154. Victor mwanzendo says:

  Daah asante sana kaka kwa kunifungua macho kitunguu tunalima sana kwetu mbeya vijijini kata ya ilungu ila watu hatujui kama ni dawa moja nzuri namna hii

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *