Kuhusu Mimi

fadhili paulo

Naitwa Fadhili Paulo, Ni Tabibu wa Tiba Asilia. Ninaishi Dar Es Salaam na ni Mtanzania. Kwa sasa nasoma Sayansi ya Kompyuta kwa njia ya mtandao.

Ninayo ofisi yangu binafsi Dar Es Salaam lakini pia bado nafanya kazi kwa njia ya mtandao, kwa tatizo lolote kuhusiana na tovuti hii au kama unahitaji kuniona, wasiliana na mimi kwenye WhatsApp +255769142586.

Nahisi upo katika kurasa hii ili kujuwa kidogo kuhusu mimi?!!. Bahati mbaya si mjuzi sana katika kujielezea binafsi, kumbe ukitaka nikuelezee wewe naweza tumia hata kurasa 10, hata hivyo usinihukumu. Bali nitajaribu kidogo. Nahusudu Afya,  Kompyuta na Teknolojia. Napendelea Kujisomea, Kuandika, Kupika, Kusafiri na kuukomboa ulimwengu dhidi ya ujinga na uongo.

Masharti na Vigezo vya matumizi ya tovuti hii:

  • Mtumiaji wa tovuti hii awe na umri usiopungua miaka 13. Udhibiti zaidi waweza kuongezwa itakapobidi.
  • Nyaraka zozote zinazoambatanishwa humu kama zipo, haki zake zinabaki kwa wamiliki wa nyaraka hizo.
  • Unaruhusiwa kubeba chochote hapa kwa matumizi yako binafsi tu.
  • Tovuti hii inahaririwa (edited) kila siku.
  • Ukurasa wowote waweza kuhaririwa au kuondolewa muda wowote itakapohitajika bila taarifa yoyote kwa msomaji.

 

www.fadhilipaulo.com

13310407_1348490351834253_4979532465422137324_n-300x300

 

Sambaza Upendo. Usisambaze Chuki.

(Imesomwa mara 8,903, Leo peke yake imesomwa mara 32)