Kukaa muda mrefu kwenye kiti husababisha kufa mapema

Kukaa muda mrefu kwenye kiti husababisha kufa mapema
Kukaa muda mrefu kwenye kiti husababisha kufa mapema

Pengine tayari unafahamu kuwa kutokujishughulisha na mazoezi ya viungo mara kwa mara ni hatari kwa afya yako. Ndiyo hilo ni jambo ambalo kila mtu analijuwa (common sense).

Vipi lakini ikiwa ni kweli unajitahidi kila siku kutimiza jukumu hilo la kufanya mazoezi dakika 30 hadi lisaa limoja na wakati huo huo unatumia masaa mengi ukiwa umekaa kwenye kiti, ukiangalia TV masaa mengi, masaa mengi umekaa na una kazi katika Kompyuta?.

Ndiyo wewe unadhani kwakuwa unaenda kufanya mazoezi kila siku basi hiyo inatosha, si ndiyo?.

Ukweli ni kuwa hata kama wewe ni mtu wa kutembeatembea hapa na hapa lakini kama masaa mengine mengi yanatumika ukiwa umekaa kwenye kiti, mwili wako unakuwa karibu na magonjwa mengi bila mwenyewe kutambua.

Haya ndiyo madhara 7 ya kiafya utakayoyapata ukiwa ni mtu wa kupenda kukaa masaa mengi kwenye kiti au chini kila siku:

Kukaa muda mrefu kwenye kiti husababisha kufa mapema

1. Kunakosesha kupata oksijeni ya kutosha

Mara nyingi ukiwa umekaa unapenda kuegemea mgongo na siyo kukaa wima umenyooka, matokeo ya mkao huu ni kuzuia oksijeni kutembea kwa uhuru wote ndani ya mwili na mapafuni kwa ujumla.

Kisayansi tunapumua kwa uhuru wote tukiwa tumesimama na siyo tukiwa tumekaa.

Ukiwa umesimamaa ndipo mapafu hupata uwezo wa kujitanua mpaka mwisho na hivyo kuweza kutoa hewa chafu na kuingiza hewa safi ndani kiurahisi zaidi. Hali hii ya kukosa oksijeni ya kutosha mwilini hujulikana kwa kitaalamu kama ‘hypoxia’.

Wanasema kukaa kwenye kiti masaa matatu tu ni sawa na mtu aliyevuta sigara 6. Bila kupata oksijeni ya kutosha mwilini mwako kunapelekea magonjwa mengi mwilini bila idadi.

2. Unapata kirahisi kansa ya titi na kansa ya tumbo

Kansa ya titi na kansa ya utumbo mpana mara nyingi imeonekana kujitokeza kwa watu wa kula kulala yaani wale wasiopenda kujishughulisha na mazoezi ya viungo.

Kituo cha kudhibiti magonjwa cha Marekani (CDC) kimesema maisha ya kula kulala yanaweza kukuweka kuwa karibu karibu na kansa kwa zaidi ya 40%.

Hii ndiyo sababu wanawake wengi wanapatwa na kansa ya matiti miaka hivi karibuni sababu wengi wao ni watu wa kukaa tu nyumbani masaa mengi tofauti na wanaume ambao hutembea huku na huko kutafuta riziki ya kila siku.

Kuepuka kansa ya matiti na kansa ya utumbo mpana epuka kukaa kwenye kiti masaa mengi.

3. Una uwezekano mara 147 zaidi wa kupatwa na maradhi ya moyo

Matatizo katika mfumo wa upumuwaji ndiyo moja ya matokeo makubwa unaweza kuyapata ukiwa ni mtu wa kupenda kukaa kwenye kiti masaa mengi.

Ni matokeo ya kutokupata oksijeni ya kutosha kama matokeo ya kukaa kwenye kiti masaa mengi. Kwenye utafiti mmoja uliohusisha watu 800,000, wale waliokuwa wakikaa kwenye kiti masaa 10 kila siku walikuwa na uwezekano mara 147 zaidi wa kupatwa na magonjwa ya moyo kuliko wale waliokaa kwenye kiti masaa machache au mara moja moja.

Kuna tafiti nyingi zinazokubaliana na nadharia hii na inatokana na ukweli kwamba ukiwa umekaa ni rahisi mafuta mengi kujilundika mwilini mwako kuliko ukiwa umesimama.

Kadri unavyokaa masaa mengi kwenye kiti ndivyo vimeng’enya vinavyofanya kazi ya kuchoma mafuta mwilini vinavyokuwa na nguvu chache kuchoma hayo mafuta. Na tatizo la unene au uzito kupita kiasi lina uhusiano wa moja kwa moja na matatizo mbalimbali ya moyo.

4. Itakuwa vigumu kitambi na uzito kukuisha

Madhara ya kukaa muda mrefu kwenye kiti

Madhara ya kukaa muda mrefu kwenye kiti

Umewahi kujaribu kufanya mazoezi, kubadili chakula au hata kufunga na bado ukawa unasumbuliwa na kitambi au uzito kuwa mkubwa? Basi jibu la tatizo lako ni kukaa kwenye kiti masaa mengi.

Utafiti unaonyesha kukaa tu kwenye kiti hata kama hauli chakula kingi bado utaendelea kuongezeka uzito.

Kwahiyo kama unataka kuondoa kitambi au tumbo au kupungua uzito kwa haraka acha kukaa masaa mengi kwenye kiti, hata kama kazi yako ni ya ofisini jaribu namna unaweza kupata meza ya kusimama huku unaendelea na kazi yako.

5. Ni rahisi kupatwa na ugonjwa wa Kisukari

Unataka kupona au kuepukana na Kisukari aina ya pili? Basi acha kukaa kwenye kiti muda mrefu.

Moja ya hatari zaidi za kukaa kwenye kiti masaa mengi ni kuwa mwili unakuwa hauitiki vema kwa insulin jambo ambalo ni matokeo ya kukaa masaa mengi kwenye kiti na hii ni matokeo ya kuzalishwa kwa wingi kwa kongosho kupita inavyohitajika kama matokeo ya kukaa muda mrefu.

Wakati ukiwa umekaa tu kwenye kiti kongosho linaendelea kutengeneza insulin lakini katika mwili huo uliokaa tu, insulin inakuwa haitumiki vema na mwili jambo linalomaanisha kuwa damu sukari (glucose) haiondolewi kwenye mzunguko wa damu kwa haraka.

Hivyo uwezekano wa kupata Kisukari unaongezeka kwa zaidi ya asilimia 14 kwa Yule mwenye tabia ya kukaa masaa mengi kwenye kiti kuliko mtu mwingine yoyote.

6. Utapatwa na maumivu ya nyuma ya mgongo

Ukiwa ni mtu wa kupenda kukaa kwenye kiti masaa mengi kuna uwezekano ukawa haukai hata mkao mzuri kiasi cha kuwa karibu na maumivu ya mgongo kila mara. Watu wa namna hii pia huwa na maumivu ya kwenye uti wa mgongo kila mara.

Kwa mjibu wa utafiti wa Taasisi ya ‘DNA India’ wagonjwa wengi wenye matatizo ya uti wa mgongo ni wale wenye miaka 20 na 30 na wengi wao ni wale hufanya kazi wakiwa wamekaa kwenye kiti masaa mengi.

Miaka ya sasa ni rahisi kukutana na watu wanaolalamika kupatwa na maumivu ya mgongo na wengi wao ukiwachunguza ni wale wanaotumia masaa mengi kukaa kwenye kiti.

madhara ya kukaa muda mrefu kwenye kiti

madhara ya kukaa muda mrefu kwenye kiti

7. Utakufa ukiwa bado kijana

Shirika la afya duniani limesema mtindo wa kukaa masaa mengi kwenye kiti ndiyo unaohusika na kuongezeka kwa uzito na unene kupita kiasi katika nchi nyingi zilizoendelea.

Na uzito kupita kiasi ni moja ya tatizo kubwa la afya kwa mtu mzima yoyote kuwa nalo ingawa wengi hawaelewi hilo, wengi hasa waAfrika wakiwa wanene au wenye uzito mkubwa ndiyo hudhani hiyo ni afya.

Uzito na unene kupita kiasi huja na matatizo mengine makubwa ikiwa ni pamoja na matatizo katika mfumo wa upumuwaji, kisukari, stroke, kukosa usingizi nk na haya yote yanaweza kupelekea wewe kufa ukiwa bado kijana.

Utafiti uliofanywa na chuo kikuu cha Harvard mwaka 2014 ulitoa hitimisho kwamba kukaa kwenye kiti masaa mengi ni moja ya sababu ya vifo vya mapema kwa watu wengi.

Mtandao wa Huffington ulienda mbali zaidi na kusema kukaa kwenye kiti masaa matatu tu kwa siku ni sawa na mtu aliyevuta sigara 6 na kuwa kukaa kwenye kiti masaa mengi kunaua watu wengi zaidi duniani kote kuliko hata UKIMWI.

Mara ya kwanza niliposoma habari hizi nilishikwa na mshangao wa ajabu maana mimi mwenyewe nimekuwa mtu wa kukaa kwenye kiti kwa miaka mingi sasa kwani kazi zangu nyingi huzifanya nikiwa kwenye computer.

Yaani haikuchukuwa muda nikabadili mkao tayari ninafanya kazi zangu nikiwa nimesimama, na tayari nimeona mabadiliko makubwa kwenye afya yangu kwa ujumla.

Pamoja na kuwa kusimama ni bora zaidi kuliko kukaa, bado unatakiwa utumie muda fulani kukaa pia, usisimame masaa yote kutwa nzima, ukisimama masaa matatu tumia nusu saa nyingine kukaa hivyo hivyo mpaka siku yako inaisha.

Nini maoni yako? umekaa muda mrefu kwenye kiti na unapata mojawapo ya madhara yaliyoandikwa hapa? nipe uzoefu wako.

Kama una swali uliza hapo chini sasa hivi.

Umesoma hii? Soma maajabu ya mbegu za maboga, bonyeza => hapa

screenshot-www-fadhilipaulo-com-2016-11-17-23-16-10

 

 

 

TAFADHARI SHARE POST HII KWA AJILI YA WENGINE

(Imesomwa mara 1,130, Leo peke yake imesomwa mara 12)

You may also like...

338 Responses

 1. Asante kwa elimu kaka. Niko na wewe

 2. Aisee Hatamimi Nlikuwa Cjajua Hii Xaxa Kwamlemavu Anayetumia Kiti Mda Wote Cjui Inakuaje Hapa

 3. Annie Isdory Annie Isdory says:

  Ubarikiwe sana Dr, kwa elimu nzuri unayo tupatia.

 4. Suzan Mosha Suzan Mosha says:

  Ahsante kwa ujumbe wako mzur

 5. Grace John Grace John says:

  mi pia nilikuwa sijui na tena napenda sana kukaa na maumivu ya mgongo,na kiuno inaweza ikawa inachangia na kukaa xana.nimejifunza

 6. Kukaa mda mrefu kunasababisha mgongo kuuma na ni hatari hata miguu kuvimba

 7. Yamenikuta ss nala dawa za presha kwa kukaa muda mwingi

 8. David Mollel David Mollel says:

  Na wanafunzi je, wanaosoma si wako hatarin na wao?
  Maan wao ni kukaa tu darasani kila mara!

 9. Hata mimi sikufahamu kukaa muda mrefu kuwa kuna madhara.

 10. Thanks doctor ubarikiwe elimisha jamii tuleteee na nyengine

 11. Ahsante sana tumejifunza

 12. Ndio maana wengine oficn hakukaliki kutwa kuzurura,ahsante kutukumbusha.

 13. Mmm Hilo ckuungi mkono hata kidogo maana mungu kashampangia kila MTU cku yake ya kufa na haibadiliki

 14. Bakari Juma Bakari Juma says:

  Mimi nataka kujua vipi kwa sisi madereva tunaokaa muda mrefu Kwenye usukani?

 15. Kweri cha msingi nikufanya mazoezi

 16. axante kwa ujembe mzr!

 17. mh vp kwa madereva? mbona ndo wapo kwenye hatar kubwa sana maana wao ndo siku nzima wanashinda wamekaa ! nini ushauri wako kwao?

 18. Ase sasa nimepona kwakuwa somo nidawa tosha

 19. Magreth Leo Magreth Leo says:

  Asante sana kwa kutuelimisha.

 20. Na madereva je inakuwaje kwa upande wao

 21. Nimejifunza itabd nifanye mazoezi

 22. Asante kwa elimu yako kaka

 23. Mmetuelimisha so kidog

 24. Beni Magaya Beni Magaya says:

  Tunakushukuru kwa kutupa ELIMU ELIMU ELIMU Ubarikiwe

 25. Hapo ndo nimeelewa mwixho leo kukaaa!…

 26. Ni kweli doctor.. nina matatizo ya mgongo mara nyingi huwa yanazidi nikikaa sana.. lakini siku nikiwa bize kusimama na kulala, mgongo hauumi kabisa..

 27. Umesomeka Vilivyo

 28. Ukikaa kwenye usukani hakuna shida shida ipo kukaa kwenye kiti.

 29. Props Camara Props Camara says:

  Ni kweli ila MUNGU akiamua kukuvuna atauwe na mazoez hayasaidii.

 30. N nzur hyoo nimeipenda

 31. Frank Mtui Frank Mtui says:

  Asant san kwaushaur wen

 32. Msani Best Msani Best says:

  Kuna wengine anashinda maofisini mda wote wamkaa kwa hiyo wanajihatalishia afya

 33. Naza Mjewa Naza Mjewa says:

  Tigo nimekosea no nihyo 0718507433

 34. Fabian Jumbe Fabian Jumbe says:

  Nashukuru sana kwa utafiti wenu nimejifunza mambo mengi sana na tatizo nimeshaanza kuliona la kuumwa kwa mgogo

 35. Prisca Saidi Prisca Saidi says:

  Duuuuh! asante kwakunifungua masikio.

 36. Aneth Kajuna Aneth Kajuna says:

  Huko xawa kaka…

 37. Na vp kwa abiria wanaotumia vyombo mbalimbali vya usafiri?

 38. Juma Pembr Juma Pembr says:

  Masikini mwee,mimi dereva daradara,muda mwingi nimekaa,ndio basi tena

 39. Pia kuna hatari ya kupata ugonjwa wa kiharusi.

 40. Hajara Seif Hajara Seif says:

  Nikweli kabisaa maana loohh!! me nakaa kwenye kiti zaid ya masaa 9 kweli dalili nyingi zilizo tajwa nilikua nazo ila cjui tatizo nn?? Daah!!! Mungu akubariki

 41. daaah nimejifunza sana asante kws somo.

 42. Nashukuru Kwa Darasa Nzuri Nimekuelewa Tena Sana, Asante

 43. Juma Lupembe Juma Lupembe says:

  karibuni. tiba.m,badala.na tiba.asilia.0677556237

 44. Hiyo ni elimu tosha,asante

 45. Namba 6 inanihusu mimi tayari dalili zote ninayo

 46. Asante kwa kutuelewesha

 47. Hannah Sulle Hannah Sulle says:

  Tangawiz inasaidia nini mwililn

 48. Asante kwa somo allah akuzidishie kila zito liwe jepesi kwako.

 49. Maswala ya kifo ni mwenyenzi mungu mwenyewe anae jua mbona marubani na madereva awafi mapema na wanakaa 24hours

 50. Asante Dr kwa kutujulisha, sasa wale wanaopenda kulala sana inakuaje? Na hii imo miongoni mwa kukaa sana?

 51. kwani mungu alipangalo hakika lazima limfikie awe na mazoezi asiwe na mazoezi mungu ana sababu za msingi

 52. Nimekuelewa vizuri sana

 53. Mary Mlai Mary Mlai says:

  Mm siliamini hilo hata kidogo kwani asilimia kubwa duniani kazi zao nikukaa kwamuda mrefu Mbona wanaishi kifo nimipango ya mungu hakuna binadam kuishi Muda mrefu nimipango ya mungu

 54. Waambieni matajiri maskini hakai wala halali

 55. Docta Nisaidie Hili, Huwa Nasumbuliwa Na Miguu Kuwaka Moto, Kifua Pia Kinanisumbua Hivyo Naomba Ushauri Wako..

 56. Asante sana kwa kunijuza bro

 57. Kwel nyie Walimu wenu wa chekechea walikua wanapenda kipindi cha mapumzko ndomana ata hamuelew et.

 58. Nikweli mm nimeamin,kwa kutwa mzima yaan kuanzia sa 1 mpka sa12 masaa8 ninayatumia kukaa au kulala na ma 4 tu nasimama,na ndomana juz tu nimepma nina kilo nying sana sasa cjui kip nifanye ili nipungue jaman loooh asante dictor nilikuwa cjajua kwann ninaongezeka kilo hivyo wakat cli vyakula vya fat

 59. Asante dr.Mungu akubariki sana.

 60. Hellen Mushi Hellen Mushi says:

  Na ambao ni bedrest sindio hatari sana hao

 61. Sasa jaman wale wabenki au ofisi ambzo ziko bize masaa 24 wafanye kaz kwa kusimama?

 62. Siku hizi kila kitu kibaya! Mnaufanya ulimwengu mgumu

 63. Asante mangi kwa kutuelimisha

 64. kwaiy wanafunz 2po matatan?

 65. nini ushauli wako kwa wabunge,wanafunzi!wanatumia mda mlefu kukaa

 66. vp kuhusu madereva wa magari ya abiria au mizigo ya toka dar to songea wafanyaje maana kazi zao ni kukaa tu. pia kuna mafundi kushona, madereva yebo au bajaji au taxi nao wafanyaje kwa kuwasaidia?

 67. Ochu Kunambi Ochu Kunambi says:

  Fundisha watu lkn usiongee habar za kifo, unaingilia kazi ya Mungu, na hata usipokaa miaka 20 na ukasimama miaka 100 utakufa tu, babu yangu alikua dereva wa Malory sasa hv kaacha na ana miaka 59 sasa bado yuko hai hadi leo, hapo sikuungi mkono

 68. Baraka Mbura Baraka Mbura says:

  Somo zuri doctor, inabidi kubadili mfumo wa maisha kabisa

 69. Abdul Seif Abdul Seif says:

  Darasa ni tamu sana!

 70. Ahsante kwa ushauri mzr

 71. Deus Jackson Deus Jackson says:

  Hiyo Kali VIP kwa madereva

 72. Du! Hiyo naikubari kabisa je inakuwaje kwa madereva wa masafa marefu?

 73. Mi natatizo la kuvimba miguu,inavimba,nikitembea mda mrefu au nikikaa chini mda mrefu,na ninapata maumivu makali,awali niliambiwa labda kwa sababu ya ujauzito niliokuwa nao kipindi hicho BP,lkn baada ya kujifungua tatizo hill bado lipo.nisaidie kwa hill.

 74. Chamsingi mizigoyako itue kwa Yesu ,Mungu ndie atakupanjia pasipo na njia,aukamaukikaa ni matatizo basi kaaukikimbia usiku namchana utapona,si mnawanasayansi!!! hapo chamsingi imaniyako iweke kwa Muumba wako ajakuwacha , mbarikiwe AMINA

 75. fact! ila ukitaka kuona wabongo wanapenda kukaa angalia wanavogombania dalala akati job alikaa tangu asbh….

 76. Wema Mwasi Wema Mwasi says:

  Ushauri mzuri sana.

 77. Pamoja xaana fadhilipaul,God bless u

 78. Tumpare Musa Tumpare Musa says:

  Samahan mi nasumbuliwa sana na kizunguzung ntapata dawa

 79. swali.mi sifanyagi kaz za kukaa sana ofsini vile. lakini nnatatzo la kuuma mgongo pale tu ntakapo kuwa nmekaa sana kwa kiti mpaka natamani nilale ndipo mgongo unapoa tatzo ninin?

 80. Yani kila tunachofanya ni madhara tuu kwa mwli cjui tufanyaje au tufanye kazi ofisini tumesimama.

 81. Mh mm fund cherehan itakuaje jaman

 82. Agnes Nziku Agnes Nziku says:

  Asante kwa kutuelimisha dokta

 83. Duh Kwa staili hiyo wangu tuuwagonjwa

 84. hiv wanafunz c waathirika wakubwa?

 85. Peter Malema Peter Malema says:

  Ni mekuelewaaaaaaaaaaaaaaaaa

 86. Ezena Ally Ezena Ally says:

  kwel me mgongo unaniuma sana inabidi nianze mazoezi

 87. asiye ckia la mkuu………,doctor umemalza kaz wanaobixha achana nao uxhanawa mikono so lzm ukpnda kukaa we kaa tu hakuna mwenye anakuzuia

 88. Me nikikaa kuna mawil kwaz kiuno tafadhli bwan siinuk mpk nikae kwaz chin ndio ninuk alaf nyay pia nishid

 89. doctor tatizo langu mimi navuta sigara nying sana kwa siku

 90. kwel Kabisa mazoezi ni muhimu saaana

 91. Mweeee Ochu Kunambi…(nimeshangaa kikwetu kirug……)

 92. Mimi naitwa Elia chalamila. Mpaka sasa naumwa mgongo na maumivu ni mpaka kwenye mguu wa kushoto. Kitaalamu uti wa mgongo hasa chini nina tatizo la bulging of cartilage that acts as a cushion. Hii imepelekea hadi usiku nikilala mgongo kuuma saaana. Doctor na Physiotherapist wameniambia nina tatizo la sciatica. Nipo naendelea na matibabu na mazoezi ya mgongo. Historia ni kwasababu nilikuwa na depression na kukaa ktk kiti muda mrefu sana. Upo sahihi mwezeshaji, hata mimi ni muuguzi wa afya

  • John Meshack John Meshack says:

   Nami pia nina tatizo kama hilo, hapa nina clinick katika taasisi ya mifupa moi !! Lakini huwa nikitembea kwa muda mrefu napata maumivu makali sana!! Lakini kulinganana na kazi zangu ni ngumu sina budi nakomaa na maumivu na kutumia dawa!!

 93. Nimekupata Mkuu, Lakini Ningeomba Sku 1 Uandike Madhala Ya Kuwa Na Was Was Au Mshi2ko Mm Ninakua Na Hilo Tatizo Najarbu Kujiami Lakini Naona Bado Tu

 94. Salum Njene Salum Njene says:

  si kweli kufa kunatokana na kuisha kwa miaka aliopanga mungu kuishi duniani.

 95. Kukaa masaa mengi ndo masaa mangap maana cjaona sehem umeshaur watu wakae kwa muda usiozid masaa kadhaa. Na hata huko kucmama unakosema watu wasimame kwa muda gan maana kwa elimu yangu ndogo ya form two biology mtu anaposimama kwa muda mrefu damu nyingi inakimbilia sehemu za chin za mwili hivyo kuufanya ubongo kupata oxygen kidogo inayosambazwa na damu na huweza kumfanya mtu aanguke na kupoteza faham. Ujumbe wako una mapungufu mengi hebu urekebishe

 96. dah hal sasa n tete kwene kukaa apo mh masaa manne kawaida duh

 97. Kiufupi ni ushaur wa kufanya mazoez ya viungo mara kwa mara japo mda mfupi sio kushinda siku nzima umekaa kama umetiwa gundi,,,hio inadumaza afya ,uwezo na ukuwaji wa cell za mwili,,,wanafunzi wana break

 98. Jackson John Jackson John says:

  Meza ya kusimama ukifanya kazi? Mhhhh!!!! By the way hata usimame bado utaondoka tu

 99. Asante lkn dunia ya Leo kila kitu kinaleta magonjwa mpk tunashindwa tukimbilie wapi,maana kufanya kaxi huku umesimama daaah Mungu atusaidie

 100. kweli bro uko sawa kabisa

 101. Anna Mlawa Anna Mlawa says:

  Axante kwanakala hii mm nina kilo 90 ulefu cjapima umli 34 ninakitambi namanyama uzembe yaliyobebana nimeanza kufanya mazoez nakupunguza vyakula vyawanga lakini bado mda mwing nautumia kwakukaa chin kupitia msada huu nianze kuzoea kucmama’

 102. Ismail Wemba Ismail Wemba says:

  Ujumbe uko vzr kwangu nimepata changamoto kubwa ubarikiwe br

 103. Jishughulishe sio kula kulala kwanza hiyo dhambi uishi miaka mingi uwe na afya njema.

 104. asante kwa somo hapo ndyo nimeelewa mwisho leo kukaa kwenye kiti muda mrefu

 105. Jacob Muney Jacob Muney says:

  Thanks very much.

 106. Uongo utafiti wa siku hizi umejaa vitisho binadam wanakufa ssb ya kujengewa hofu IPO siku watakuja na utafit wa kushaur tusivae nguo

 107. Asante.Hivyo ni elimu umetoa kwa wengi kwani wengi hawana uelewa huo wa kutokukaa muda wote kwa kuhofia maumivu ya mgongo,na madhara yote uliyotaja.

 108. Babu Ally Babu Ally says:

  Mi nina shida ya usingizi.sijui tatizo nn

 109. Sasa jaman ss madreva na mameneja robotatu ya muda wetu wa kazi ni kukaa kama sio ofisini ni kwenye gari tufanyeje????

 110. Uongo huo inamaana tafiti hiyo ni kwa mwaka huu hao walioishi zamani vipi.

 111. Hongera sana Dr kwakutupa semina ya afya kwani imetujenga Kwa namna moja au nyingine

 112. Nimekuewa mkuu kwamaelezoyako!

 113. Sara Ngimba Sara Ngimba says:

  Mikoan tunawapataje

 114. Ndio maana mwalimu aliyenifundisha primary hazeeki labda inaweza ikawa ni sababu mojawapo.

 115. Said Mtutuma Said Mtutuma says:

  Ikiwa Mimi Kazi Yangu Ni Dereva Nasafiri Masafa Marefu Je Pia Nahusika Na Hili? Na Kama Nahusika Je Nifanyeje Ili Kuepuka Hayo Madhara

 116. Dr upo sahihi ila nahisi inadepend na mwili wa mtu Mimi binafsi ni mtu was mazoezi ila nature ya kazi yangu nakaa mda mrefu kwenye kiti na mpaka mdaa huu nnao comment nna maumivu kiuno kwenye joint ya goti kwa pembeni na sometime mgongo hasa nikisimama au kutembea kwa mda mrefu nilishakwenda hospital wakaniambi tatizo limeanzia kwenye uti wa mgongo maana nilikuwa mahisa labda fluid zimeisha kwenye joint, hospital walinipatia dawa pamoja na ratiba ya physiotherapy lakini tatizo bado na kuna wafanyakazi wenzangu wanamda mrefu kuliko mimi lakini hawana hilo tatizo naomba solution yako nifanyaje maana hospital nshaenda

 117. Sa tutafanyaje na ndo kazi za kila siku

 118. Duuhhh,mbonaaa!!!!! Enviolatha Magesa Mary Shayo

 119. Rukia Masaka Rukia Masaka says:

  Uko sahihi kabisa

 120. Joan John Joan John says:

  Hapo ndo nakumbuka lile andiko lisemalo hivi. Siku za kuishi mwanadamu ni chache nazo zimejaa tabu . Barikiwa mtumwa wa Bwana kwa somo

 121. John Malapwa John Malapwa says:

  Duuh hatar kweli Dk …!!

 122. Nahitaji kupungua tumbo pia mwili lkn sina muda wa mazoezi pls niaambie nifanyeje??

 123. Nasumbuliwa na kuumwa na magoti, nifanyeje?

 124. Neema Mongi Neema Mongi says:

  Kwahiyo kama Mimi hivo nikitembee kidogo nahema Nikila chakula bada ya dk 2 moyo unaenda mbio je inawezekana ni sababu hiyo Dr

 125. Binti Abed Binti Abed says:

  Mimi nasumbuliwa sana na kiuno docta nini sababu,hata kama sipo kwenye hedhi yani ni muda wote

 126. shukran ila hapo kwenye kufa ni mipango ya Mungu.

 127. Dr na kama unalala sana je unaweza pata mazara kama hayo?

 128. Kwan kisukari cha pili kikoje. nachakwaza?jee ukikaa chini. Kabisa. Kwa muda mrefu inakuwaje hasa sisi wamama tunapika kuosha. Vyomba,kufua nk

 129. Mke Wang anasumbuliwa na tatzo LA tumbo kuuma chini ya kitovu upandea wa kushoto pengne tatzo ni nn dokta?

 130. Dr.Mungu wa mbinguni akubari kwa elimu unayowapa watu hyo ni karama ulopewa na mungu

 131. Nafanya kaz ya kukaa Masaa 11-12. Nafanya mazoez ya kukimbia dk 20-30. Nakosa usingz Na MgongoN Maumiv kias. Dr tba Pliz

 132. Tutegemee kuwaona machinga wakiishi muda mrefumaana mtu anatoka kkoo mpaka mbezi halafu anakata boda mpaka kinyerezi to tabata barakuda huyooo vingunguti hiyo anaambaa ambaa na nyerere road mpaka tazara toa mandela road to sokota mambo temeke hapo home mbagala majimatitu.

 133. Mazoezi yenyewe yanazeesha. Uktaka kuamin mazoez yanazeesha we angalia wacheza mpira hasa wa miguu. Mtu ana miaka chini ya 30 lkn anaonekana km anamiaka 45. Lkn watu wa mazoezi asilimia kubwa wamepalalaizi uzeeni.
  Mazoez mazuri ni kuacha ngono za aina zote na kuacha matumizi ya vileo na ule lishe bora icyo na kemikali na ukila chakula chenye kemikali iondoe kwa kula kitunguu maji au swaumu, chunga, mlonge n.k. Usisahau kunywa maji mengi ambayo ni safi na salama. Chakula cha asili na maji salama ni dawa namba 1 dunian.

 134. Na wanafunzi watasoma wima? Na madereva wanaoendesha masaa nane?

 135. Mm nikikaa sehem nimening,iniza miguu hua naskia maumivu chini ya kisigino ni dalili ya ugonjwa gani?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *