Mazoezi yanayoongeza nguvu za Kiume

Zingatia sana umhimu wa mazoezi ya viungo. Bila kujishughulisha na mazoezi ya viungo kila siku itakuwa ni vigumu sana kwako kupona tatizo la upungufu wa nguvu za kiume.

Kutengeneza mishipa na kupunguza uzito isiwe ndiyo sababu pekee ya kwenda gym.

Kama unahitaji nguvu za kiume na uume wenye afya, unahitaji kujishughulisha na mazoezi ya viungo mara kwa mara ili kusafisha mishipa ya damu na hivyo kuongeza kiasi cha utiririkaji wa damu kwenda kwenye uume.

Makala hii ni maalumu kwa ajili ya wanandoa tu na si vinginevyo au kama elimu kwa wanandoa watarajiwa.

Katika kilele cha juu kabisa cha furaha katika ndoa, kama inavyojulikana, ni sherehe inayopatikana katika tendo lenyewe la ndoa. Ingawa, ili furaha hiyo ipatikane ni lazima tendo hilo liwe limefanyika katika hali ya afya kwa wanandoa wote wawili.

Nguvu za kiume ni neno linalotumika mara nyingi kumaanisha ‘Uwezo wa mwanaume kufanya tendo la ndoa’. Na inapokuwa tofauti na hivi, tunaita ni ‘kupungua au kukosa nguvu za kiume’.

Kupungukiwa kwa nguvu za kiume hutofautiana toka mtu mmoja hadi mwingine.

Inaweza kuwa ni hali ya kutokuwa na uwezo wa kusimamisha uume, au hali ya kutokuwa na uwezo wa kufika kileleni kwa muda mzuri wa kutosha.

Nguvu za kiume pia siyo idadi ya mabao. Hilo ni mhimu kwanza ulielewe. Unaweza kwenda mabao hata manne na bado ukaonekana huna nguvu za kiume. Nguvu za kiume ni muda gani umetumia kubaki hapo mchezoni ndiyo jambo la mhimu.

Kama unafika mpaka magoli manne na kila goli unatumia dakika 3 au 4 kufika kileleni basi tunaweza kusema wewe huna nguvu za kiume.

Ila kama utaweza kwenda goli moja tu na likachukua dakika 10 au 15 au 20 hivi na kuendelea hakika tunasema wewe una nguvu za kiume. Tunaamini muda huo umetosha kuweza kumfikisha mwenza wako kileleni.

Mwanaume pia utahitaji kujua dalili au ishara za mwanamke anapofika kileleleni. Bila kujua dalili au ishara za mwanamke anayefika kileleleni kazi bure.

Kufahamu dalili na ishara za mwanamke anayefika kileleni bonyeza hapa.

Kumbuka pia tendo la ndoa siyo ugomvi. Wapo baadhi ya wanaume wanadhani ili umfikishe mwanamke basi unatakiwa umfanye kwa nguvu au kwa fujo sana utadhani ni ugomvi fulani hivi!, mapenzi siyo hivyo. Ndiyo hutakiwi ufanye kilegelege sana lakini pia huhitaji kufanya kwa nguvu kama vile ni ugomvi!

Tatizo ni hizo video feki mnazotazama mnadhani mapenzi ndiyo huwa hivyo jambo ambalo si kweli. Kila mwaka wasichana na wanawake wengi hutekwa na watu wasiojulikana sehemu mbalimbali duniani na baadhi yao hufanyiwa vitendo vya kikatili ikiwemo vya kingono na hurekodiwa.

Sasa wewe unapoangalia picha kama hizo unadhani mapenzi ndiyo hufanywa hivyo kumbe si kweli.

Kuna wanaume wakianza kazi hiyo ni kama vile mashine inakoboa mahindi yaani ni ugomvi mwanamke anabaki akiumia tu na kama hajuwi naye anabaki kuumia tu hata siku nyingine ukimhitaji atakataa kwa visingizio  vingi sababu unamuumiza bila wewe kujua.

Pole pole, kwa nguvu kidogo inapochanganya lakini siyo kwa fujo kama vile ugomvi. Umeipata hiyo bila shaka kazi inabaki kuwa kwako!.

Kumbuka mwanaume lazima utafika kileleni hata iweje, hivyo ni jukumu lako kuhakikisha kabla hujawa na uwezo tena wa kuendelea na tendo la ndoa uwe umeona na una uhakika mke wako naye amefika kileleleni.

Hivyo nguvu za kiume siyo idadi ya mabao, ni muda unaotumia kubaki hapo kifuani ndiyo mhimu na si idadi ya mabao.

Pamoja na hayo yote, elimu mhimu ambayo mwanaume anatakiwa kuwa nayo, ni kuwa nguvu za kiume hazipatikani kwa kutumia madawa ya kemikali au mahala pengine; bali zinatokana na vyakula tunavyokula kila siku.

Sababu za Wanaume kuishiwa nguvu za kiume:

Kuishiwa nguvu za kiume ni jambo la kawaida kwa wanaume wengi. Ni kushindwa kwa uume kudumu kusimama barabara kwa ajili ya tendo la ndoa, au kuwahi kufika kileleni.

Tatizo la kupungukiwa nguvu za kiume huongezeka sababu ya umri. Tafiti mbalimbali zinasema wanaume wa umri kuanzia miaka 61 na kuendelea ndiyo wanapatwa na tatizo hili zaidi kuliko wanaume wenye umri wa miaka 41 Kushuka chini.

Wanaume wenye elimu ndogo juu ya utendaji kazi wa mwili na afya ndio wanaokabiliwa sana na tatizo hili.

Hii ni kutokana na kwamba wengi wao wanakuwa hawaelewi aina ya vyakula vinavyoongeza nguvu za kiume na za mwili kwa ujumla, namna wanavyotakiwa kuishi ili kupunguza janga hilo, wanakunywa pombe na hawajishughulishi na mazoezi ya viungo.

Mazoezi ya viungo hupunguza tatizo la kuishiwa nguvu za kiume kwa asilimia kubwa sana.

Soma zaidi kuhusu mazoezi kwa kubonyeza hapa => Hizi ndizo faida 50 za Mazoezi.

Kupungukiwa nguvu za kiume kunaweza pia kuwa kumetokana na mambo ya kihisia, kwa kiingereza ‘emotional causes’. Vitu vingine vinavyoweza kusababisha kupungua kwa nguvu za kiume ni pamoja na magonjwa kama vile ugonjwa wa Kisukari na Shinikizo la juu la damu.

Asilimia 51 mpaka 61 ya wanaume wanaosumbuliwa na kisukari wanapatwa na tatizo la uume kushindwa kusimama vizuri. Kadharika wagonjwa wa kiharusi na wale waliotekwa na ulevi nao ni miongoni mwa watu wanaoweza kupatwa kirahisi na tatizo la upungufu wa nguvu za kiume.

Walevi wengi wa pombe kwa mfano wanakabiliwa na tatizo la uzalishaji mchache wa mbegu za kiume (manii).

Wengine wenye hatari ya kupatwa na tatizo la kupungukiwa nguvu za kiume ni pamoja na wanaume wenye shinikizo la juu la damu, wenye matatizo ya tezi, waliowahi kufanya upasuaji katika viungo vya uzazi wakabaki na majeraha, watu wanaotumia dawa zenye kemikali kiholela bila kushauriwa na wataalamu na wale wanaougua maradhi yanayodhoofisha msukumo wa damu kwenda katika mishipa ya uume.

Pamoja na hayo, tatizo la upungufu wa nguvu za kiume linaweza kutibika kwa watu wa rika zote.

Kabla dakatari hajaanza kukutibu tatizo kupungukiwa nguvu za kiume, atataka kujuwa:

 1. Umri wako
 2. Utendaji wa tendo la ndoa kabla na baada ya kuugua
 3. Afya yako kwa ujumla
 4. Matatizo katika ndoa ikiwa kuna ugomvi wowote n.k
 5. Nini sababu ya wewe kutaka kupona

Kuwa na mtaalamu mzuri ni njia ya kwanza katika kupata uponyaji sahihi. Ni mhimu wewe kujisikia vizuri na kuwa na imani na daktari wako. Kwa kufanya hivi utakuwa umepiga hatua nzuri kelekea kwenye ufumbuzi wa tatizo lako.

Nini Sababu ya uume kushindwa kusimama?

Kushindwa kwa uume kusimama pia hutambulika kama kuishiwa nguvu za kiume. Ni kitendo cha mtu kushindwa kusimamisha uume au kudumisha usimamaji wa uume kwa muda wa kutosha kufanya tendo la tendo na mwenza wake.

Pamoja na ukweli kuwa mara zote Mwanaume lazima atafika kileleni, hali huweza kuwa tofauti kwa upande wa pili kwani mwanamke anahitaji mwanaume akawie zaidi ili na yeye (mwanamke) aweze kutosheka.

Mkeo hupendelea ukawie na ikiwezekana ukawie zaidi. Kama utakuwa unawahi kumaliza, basi mkeo anakuwa hapati raha kamili.

Hata hivyo tambua pia kuchelewa sana kufika kileleni inaweza kuwa kero kwa mwenza wako. Kwa kawaida wanawake wengi wanaweza kufika kileleni kuanzia dakika ya 8 kwenda juu tangu tendo la ndoa lianze.

Muda mzuri wa kutumia katika kushiriki tendo la ndoa bila kuleta kero zingine ni kati ya dakika 15 mpaka dakika 30 hivi. Ikiwa mwanaume ataendelea bila kufika kileleni hata baada ya dakika 35 au 40 na zaidi basi hiyo sasa ni kero na si tendo la ndoa tena.

Ingawa, kama una tatizo la kuwahi kufika kileleni hauko peke yako. Asilimia 30 hadi 40 ya wanaume wa rika zote wanakabiliwa na tatizo la kuwahi kufika kileleni au kupungukiwa kwa nguvu za kiume.

Hata hivyo kutambuwa tu kwamba wanaume wengine pia wana tatizo kama lako siyo sababu ya wewe kukaa tu bila kutafuta suluhisho la tatizo lako.

Habari njema ni kuwa zipo njia zinazoweza kuleta matokeo mazuri na hatimaye kulimaliza tatizo hili bila madhara mabaya hapo baadaye.

Wakati mwingine uume kushindwa kusimama inaweza kuwa si tatizo, lakiini jambo hilo linapojitokeza kila mara na kwa kipindi kirefu inaweza kuleta msongo wa mawazo kwa mume na hata kwa mke.

Sababu nyingine ambazo zinaweza kupelekea uume usisimame vizuri ni pamoja na matatizo ya mhemko kama;

 1. Wasiwasi
 2. Hasira
 3. Msongo wa mawazo (Stress)
 4. Huzuni
 5. Hofu na mashaka
 6. Kukosa hamu ya tendo la ndoa n.k

Ili uume usimame vizuri ni lazima:

 • Mfumo wako wa neva uwe  na afya nzuri inayopelekea mpwito neva (nerve impulses) katika ubongo, uti wa mgongo na uume.
 • Mishipa ya ateri iliyo na afya ya ndani na iliyo karibu na corpora cavernosa
 • Misuli laini yenye afya na tishu za ufumwele (fibrous tissues) ndani ya corpora cavernosa
 • Kiwango sahihi cha oksidi nitriki (nitric oxide) ndani ya uume.

Uume kushindwa kusimama vizuri kunaweza kusababishwa pia kama kipengele kimojawapo hapo juu hakifanyi kazi vizuri.

Mambo mengine yanayopelekea kupunguwa kwa nguvu za kiume, uume kushindwa kusimama vizuri na kuwahi kufika kileleni ni:

 1. Uzee
 2. Kisukari
 3. Kujichua/Punyeto
 4. Uzinzi
 5. Kukosa Elimu ya vyakula
 6. Kutokujishughulisha na mazoezi
 7. Shinikizo la juu la damu
 8. Ugonjwa wa moyo
 9. Uvutaji sigara/tumbaku
 10. Utumiaji uliozidi wa kafeina
 11. Kudhurika kwa neva au uti wa mgongo
 12. Madawa ya kulevya
 13. Kupungua kwa homoni ya testerone
 14. Athari kutoka kwa baadhi ya dawa
 15. Pombe
 16. Kutazama picha za X mara kwa mara

Nguvu za kiume na mzunguko wa damu:

Kitu gani husababisha uume usimame?

Unaweza kujibu ni msisimko. Ni kweli, Jibu lako linaweza kuwa sahihi. Hata hivyo msisimko ni matokeo. Kipo kinachosababisha kutokea huo msisimko. Bila hicho, hakuna msisimko unaoweza kutokea.

Kila mwanaume anatakiwa kujuwa jibu sahihi la swali hili ili atakapopatwa na tatizo atambuwe wapi pa kuanzia na pa kuishia. Siyo lazima uwe daktari, Elimu ya kutambua  mfumo wako wa mwili unavyofanya kazi ni mhimu sana kwa kila mtu na si kwa madaktari pekee kama watu wengi mnavyodhani.

Kutokusoma soma lolote kuhusu miili yetu inavyofanya kazi ndiyo sababu kubwa inayotufanya kuparamia dawa kiholela na hivyo kujikuta tunapata madhara zaidi badala ya kujitibu.

Mzunguko wa damu ndicho kitu kinachofanya uume USIMAME. Na kabla hujaendelea kusoma tambua jambo moja mhimu; ‘’Asilimia 94 ya damu ni maji’’. Hii ni kusema katika kila lita 10 za damu, lita 9 kati ya hizo 10 ni maji. Kwa kifupi maji ndiyo kila kitu mwilini, nakushauri upendelee Kunywa maji bila KUSUBIRI KIU.

Mzunguko wa damu unaofanya kazi vizuri kama inavyotakiwa na usio na hitilafu yeyote ni kipengele mhimu sana katika afya ya mwili, mishipa na kusimama kwa uume wako.

Soma hii => [Jitibu kwa kutumia maji mp3].

Kwanini mzunguko wa damu ni mhimu?

Mzunguko wa damu wenye afya bora husambaza damu ya kutosha katika viungo vyote vya mwili ikijumuisha pia damu iliyo katika mishipa ya uume. Hivyo, hata kama utagusana na mwanamke hautaweza kufanya lolote ikiwa damu haizunguki katika viungo vyako kama inavyotakiwa.

Mtazame mtu aliyekufa, damu yake haizunguki, je anaweza kufanya lolote? Hata hivyo huo ni mfano mkubwa sana.

Hii ni kusema kuwa, chochote ambacho kinazuia mtiririko wa damu kwenda kwenye uume kinaweza kuzuia kusimama kwa uume. Kama mishipa ya vena na ateri imeziba, mwili wako hautaweza kusimamisha uume vizuri. Hii ni kutokana na kwamba uume hautapata damu ya kutosha.

Mara nyingi vena zilizoziba kutokana na mzunguko dhaifu wa damu ni sababu ya kushindwa kusimama uume kwa wanaume wengi wenye miaka 60 kwenda juu, wanaume wenye kisukari na pia wanaume wenye hali ya kukauka kwa vijiateri vya ateri, na wenye maradhi ya moyo.

Baadhi ya wanaume wanapatwa na tatizo la kuishiwa nguvu za kiume kama matokeo ya kula vyakula vyenye mafuta mengi ambayo yanaweza kuzuia mtiririko mzuri wa damu kwenye uume. Inashauriwa pia kuepuka vinywaji na vyakula ambavyo husindikwa viwandani.

Katika tendo la ndoa kwa mwanaume, mishipa ya damu ya ateri ina nafasi kubwa sana sababu ya kazi yake ya usafirishaji wa damu kwenda sehemu mbalimbali za mwili, hivyo unashauriwa kujifunza namna ya kutunza ateri za mwili wako ili kuruhusu mtiririko mzuri wa damu mwilini mwako.

Pia ni mhimu sana kuwaona wataalamu wa tiba kuhusu unavyojisikia na jinsi unavyohisi kuwa pengine unaweza kuwa na tatizo katika mishipa yako ya ateri. Jaribu kujiwekea utaratibu wa kujichunguza afya yako mara kwa mara kama utahisi kunyemelewa na tatizo hili.

Baadhi ya watu hufanya maradhi kuwa sugu kwa sababu ya kuacha kujichunguza mara kwa mara hadi wauguwe, huku ni kukosa kuelewa na kushindwa kujithamini na kujipenda mwenyewe.

Hapa nimekuelezea yale mazoezi ambayo kazi yake hasa ni kuongeza msukumo wa damu mwilini pia homoni mhimu na hivyo kuongeza nguvu za kiume moja kwa moja kila siku mwilini mwako.

Nimekuwekea picha, video na maelezo mengi kwa ajili hiyo.

Soma pia hii > Njia 14 za kuondoa tatizo la kuwahi kufika kileleni

Mazoezi yanayoongeza nguvu za Kiume

1. Kutembea kwa miguu

Mazoezi yanayoongeza nguvu za Kiume

Kutembea ni moja ya zoezi zuri kabisa unaweza kufanya na ambalo mtu mwingine yeyote anaweza kufanya pia. Ni zoezi unaweza kufanya mahali popote, wakati wowote na haligharimu chochote.

Sehemu nzuri kutembea ni nje au uwanjani au karibu na msitu ambako unaweza kupata hewa safi ya asili ya kutosha. Unaweza kufanya ndiyo zoezi lako la kwanza asubuhi au jioni vilevile mchana wakati wa jua kali ni muda mzuri kufanya zoezi hili au wakati mwingine wowote utakapojisikia kufanya basi fanya kuliko kuleta visingizio.

Kama una lengo la kupunguza pia uzito basi tembea mwendokasi kidogo dakika 60 bila kusimama mara moja mpaka mbili kila siku. Huhitaji kusema nitoke hapa mpaka pale, unahitaji uwe na saa mkononi kukuonyesha kwamba kweli dakika 60 zimeisha ukitembea pasipo kusimama.

Kama afya yako siyo nzuri unaweza kuanza hata na dakika 15 siku ya kwanza huku ukiongeza dakika 5 zaidi kila siku mpaka utakapozoea kwenda dakika 60 pasipo kusmama basi uendelee hivyo kila siku.

Wanasayansi huko Sweeden wamegundua kama utatembea kwa miguu mwendokasi kidogo bila kusimama kwa dakika 60, mwilini mwako kuna kimeng’enya kinaitwa kwa kitaalamu ‘LIPASE’ ambacho baada ya mwendo huo wa saa moja huamshwa (activated) kuanza kuchoma mafuta mwilini kwa masaa 12 mfululizo.

Hivyo kama utatembea lisaa limoja asubuhi na lisa linguine jioni ina maana mwili wako utabaki unachoma mafuta kwa masaa yote 24 katika siku! Na matokeo yake ni kuwa hatutasikia tatizo la kitambi au unene kupita kwako tena.

Kama huna uzito uliozidi basi napendekeza dakika 30 mpaka 40 za zoezi hili kwako zinakutosha.

Ukiacha kuchoma mafuta zoezi hili pia linaongeza msukumo wa damu kwenda mishipa karibu yote katika mwili wako na hivyo moja kwa moja kuhusika na kukuongezea nguvu za kiume na kukuwezesha kuhimili tendo la ndoa kwa muda mrefu zaidi.

Soma pia hii > Faida 20 za mazoezi ya kutembea kwa miguu

2. Kuchuchumaa na Kusimama

Mazoezi yanayoongeza nguvu za Kiume

Zoezi hili la pili ndiyo zoezi ninalolikubali zaidi kuliko mazoezi mengine yote yanayoongeza nguvu za kiume. Ni zoezi gumu kulifanya lakini ukilizoea na kulifanya mara kwa mara basi hutachelewa kuona faida zake na utakuja kuniletea ushuhuda wewe mwenyewe.

Hili ni zoezi linalotengeneza na kuimarisha misuli katika eneo lako lote la chini ya mwili kuanzia misuli ya tumbo (sixpacks), mgongoni mpaka misuli ya kwenye visigino miguuni.

Ukizoea kufanya zoezi hili sahau kusumbuliwa na kitambi na unaweza kutengeneza misuli ya tumboni maarufu kama ‘sixpack’ kirahisi zaidi. Zoezi hili pia husadia kuchoma mafuta mwilini ingawa siyo sana kama vile kukimbia au kutembea mwendokasi lisaa lizima.

Unaweza kuanza na mwili wako pekee bila kubeba kingine chochote. Unachohitaji ni kuchuchumaa na kusimama, kuchuchumaa na kusimama mara 15 au mpaka 25 huku ukipumzika sekunde 30 au dakika 1 kisha unaendelea tena kwa mizunguko mitano.

Kama ni ngumu sana wakati unaanza unaweza kuanza na kuchuchumaa na kusimama mara 5 au 7 kisha pumzika huku ukiendelea kuongeza idadi hivyo hivyo kidogo kidogo mapak uatakapozoea kwenda mara 25 bila kupumzika. Unaweza kufanya zoezi hili mahali popote iwe ni chumbani, jikoni, ofisini na mahali pengine popote. Unaweza kufanya mara 3 au 2 kwa siku. Ukiona unapungua zaidi uzito punguza mpaka mara 1 tu kwa siku.

Utahitaji usikie maumivu kiasi fulani na upumuwe kwa shida lakini isiwe maumivu kuzidi sana ndiyo utaona faida zake zaidi.

Zoezi hili linaongeza msukumo wa damu katika sehemu zote za mwili na wakati wote. Faida nzuri zaidi ya zoezi kuliko mengine yote ni kuwa inaifanya damu iliyokuwa imeenda miguuni kurudi tena juu katika moyo na mwili kwa aujumla jambo ambalo ni mhimu katika kusafisha damu na itembee kwa uhuru wote kila sehemu.

Kama wewe ni mtu unayefanya kazi za ofisini na unakuwa umekaa kwenye kiti masaa mengi basi ujuwe damu yako inajilundika miguuni na haipati nafasi ya kurudi juu isafishike na kuongeza mzunguko. Matokeo yake utaanza kuona miguu au nyayo zako zinaanza kuwaka moto au miguu inavimba au miguu tu inauma kutokana na hiyo damu ambayo imejilundika na kutengeneza taka za asidi ambazo mwisho wake kabisa hutokea kuwa kansa.

Hili ndilo zoezi pekee ambalo linaifanya miguu kutumika kama moyo wa pili wa mwili wako kwa kuiwezesha damu kusukumwa kurudi juu tena kwenye mfumo wa mwili faida ambayo wengi hawaifahamu. Ukifanya zoezi hili unakuwa na mioyo miwili ndani ya mwili wako!

Zoezi hili hujulikana pia kama ‘squatting’ kwa Kiingereza siyo tu linaongeza msukumo wa damu mwilini lakini pia linaongeza na kuweka sawa homoni mhimu sana ya kiume ijulikanayo kama ‘testosterone’ na matokeo yake utaongezeka nguvu zako za kiume kwa haraka zaidi ndani ya siku kadhaa tu na utajisikia raha sana unapofika kileleni tofauti na siku zingine kama utaanza kufanya zoezi hili.

Siri nyingine nataka nikupe hapa ndugu msomaji wangu ni kuwa nguvu za kiume zinatengenenezwa kwenye magoti na kwenye enka karibu na visigino chini. Hivyo zoezi lolote litakalozifanya sehemu hizi mbili zishughulishwe lazima moja kwa moja litapelekea kuongezeka kwa nguvu za kiume. Kuthibitisha hili mwanagalie magotini mtu aliyezoea kupiga punyeto utaona waziwazi eneo hilo linang’aa na ni dhaifu kwa macho tu!

Kama nilivyosema ni zoezi gumu kulifanya hasa kama wewe ni mtu mvivu na usiyekosa kuwa na visingizio. Baadaye kadri unavyolizoea unaweza kubeba vitu katika kila mkono au begani kuongeza uzito na ufanisi zaidi. Ingawa hii siyo lazima kwani uzito wa mwili wako wenyewe unatosha.

Namna ya kufanya zoezi hili > Unaweza kuweka mikono yako shingoni au kusika kiuno au kuinyoosha yote miwili mbele na ushuke chini yaani uchuchumae mpaka karibu na visigino huku sehemu ya juu ya mwili ikiwa imenyooka na kisha urudi juu tena yaani usimame na ufanye hivyo hivyo kuchuchumaa na kusimama mfululizo mara 20 mpaka 25 kwa mzunguko mmoja.

Unatakiwa uwe mbunifu zaidi wakati unaendelea na zoezi mfano kuna wakati unaweza kuchuchumaa bila kushuka chini kabisa kwenye visigino ukaishia nusu na kusimama tena, unaweza kuongeza uzito mikononi au begani kama nilivyoeleza pale juu nk.

Soma pia hii => Hizi ndizo faida 50 za mazoezi

3. Push-Ups (pushiapu)

Mazoezi yanayoongeza nguvu za Kiume

Nashindwa kupata neon sahihi la Kiswahili la zoezi hili lakini natumaini picha itakusaidia kujua nazungumzia zoezi gani. Hili ni zoezi ambalo mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli alilifanya jukwaani wakati ule akifanya kampeni za kugombea urais 2015 na kuzua gumzo kila mahali.

Hili ni zoezi jingine gumu kulifanya lakini lenye uwezo mkubwa wa kuongeza msukumo wa damu mwilini na hivyo kuimarisha nguvu zako za kiume kwa ujumla.

Siyo hivyo tu zoezi hili pia linaimarisha misuli yako ya mikono, misuli ya kifua, msiuli ya mabega, na misuli ya tumboni.

Kama kawaida anza pole pole mara 3 au 5 hivyo hivyo ukiongeza idadi pole pole mpaka utakapozoea kwenda mara nyingi zaidi. Mhimu tu usilale usingizi moja kwa moja hapo chini.

Pia nitowe angalizo kuwa huhitaji kujiumiza vidole vyako ukiwa umekunja ngumi eti ili kupata faida zaidi, maaana kuna mwingine anaweza kukushauri fanya push up kwenye kokote au sakafuni moja kwa moja ndiyo zoezi liingie, hili siyo kweli unaweza kufanya zoezi hili hata juu ya zulia la manyoya nab ado ukapata faida zake vizuri.

Unachohitaji ni kama unalala chini miguu imenyooka na mikono yako ikiwa wazi au umefunga ngumi na ushuke chini siyo kugusa ardhi kisha upandishe tena juu mwili wako. Ni mikono yako itakuwa kama inapinda kutoka nje unaposhuka chini na kunyooka tena unaporudi juu huku mwili na kichwa vimenyooka kusindikiza mwili.

Zoezi hili pia unaweza kufanya popote iwe ni chumbani, sebureni au kiwanjani mhimu tu usiwe na haraka ufanyako zoezi hili. Ni zoezi gumu lakini pia ukijitahidi ukaliweza na kulizoea basi hutachelwa kuona faida zake.

.

4. Kukimbia mwendo wa pole pole (Jogging)

Mazoezi yanayoongeza nguvu za Kiume

Hili ni zoezi jingine zuri zaidi katika kuongeza mzunguko wa damu mwilini na hivyo kukuongezea nguvu za kiume na stamina kwa ujumla katika tendo la ndoa. Hili ni zoezi maalumu zaidi kwa Yule anayetaka kupunguza unene na uzito kirahisi zaidi na kwa haraka.

Ni zoezi linalohitaji moyo zaidi kulifanya kwani linachosha lakini kwa mtu asiye mvivu au asiye na visingizio basi hataona ugumu wowote kulifanya kila siku. Kama ilivyo kwa zoezi la kutembea zoezi hili pia kama lengo lako ni kupunguza uzito basi ni vizuri likifanywa kwa muda usio chini ya dakika 60 kwa matokeo mazuri kama niliyoeleza pale katika zoezi la kutembea.

Zoezi hili linajenga na kuimarisha misuli katika miguu na mwili wote kwa ujumla. Na kama ulikuwa hujuwi misuli ya miguuni ndiyo mhimu zaidi linapokuja suala la kuwa na mzunguko mzuri wa damu na nguvu za mwili kwa ujumla.

Watu wengi miaka hii wanahangaika na vitambi au na tatizo la kupunguza uzito wengine wananunua mpaka dawa lakini namna rahisi ya kutatua hilo ni kufanya zoezi hili la kukimbia mwendo wa pole pole maarufu kama ‘jogging’ ambalo hupunguza uzito haraka bila kukuacha na maumivu mengine na halina gharama yoyote kulifanya.

Mhimu kwenye zoezi hili ni kuwa liwe ni jambo la kila siku na siyo siku za mwisho wa wiki tu (weekend). Hapa ndiyo wanapokosea watu wengi. Yaani  jumatatu mpaka ijumaa amekaa tu halafu anakuja kukurupuka jumamosi na jumapili kufanya mazoezi na kutegemea miujiza. Mazoezi ni kila siku siyo weekend tu.

Kama unapunguza uzito na unene fanya lisaa limoja kila siku bali kama uzito wako upo sawa basi dakika 30 za zoezi hili kwa siku zinatosha.

.
.

.

NJIA ZINGINE ZA KUONGEZA NGUVU ZA KIUME AMBAZO SIYO MAZOEZI

1. Acha mawazo

Mawazo na mfadhaiko huondoa mtiririko mzuri wa damu kwenda kwenye uume na kusababisha nguvu kupungua nguvu za kiume na hata uume wenyewe.

Ikiwa unasumbuliwa na mfadhaiko au stress uangalifu mkubwa unahitajika kabla ya kuamua kutumia dawa yoyote. Katika hali ya mfadhaiko wa akili utokanao na hali ya kushuka kwa uchumi kwa mfano, wanandoa wanapaswa kuwa ni wenye umoja na kujaliana zaidi, shida ni pale kama mke akili yake ni ndogo kwani badala ya kufunga na kuomba kwa Mungu huenda akaenda kukutangaza kwa majirani!.

Kama una mfadhaiko wa akili (stress) ni vigumu sana wewe kuwa na nguvu za kiume. Hilo haliwezekani. Ili uwe na nguvu za kiume unatakiwa usiwe na mawazo mawazo yoyote. Uwe mtu uliyetulia kimwili, kiakili na kiroho (cool).

Jipekuwe na ujitambuwe ni kitu gani hasa kinakufanya uwe na mawazo mawazo kila mara na ufanye kila uwezalo kukiondoa hicho kinachokuletea stress kwenye maisha yako kila mara.

Stress nyingi kwa wanaume wa KiTanzania zinatokana na ugumu wa maisha, magomvi ya mara kwa mara kwenye mahusiano, magonjwa ambayo hayatibiki nk.

Haijalishi nini chanzo cha mawazo mawazo upande wako, ukiamua hakuna stress isiyo na tiba. Chimba tu inawezekana. Kuwa bize na mazoezi ya viungo kila siku ni namna nzuri ya kuondoa msongo wa mawazo.

Kama stress yako ni matokeo ya maisha magumu basi jipe moyo pia jipe muda hakuna usiku usio na mchana kuna siku tu utatoka kama hutakata tamaa. Pigana na upambane mpaka kieleweke kuna siku utaishi maisha bila stress ya umasikini.

Kuwa karibu na Mungu kila mara. Usiache kutafuta msaada wa kimawazo toka kwa wataalamu au watu wengine wenye uzoefu juu ya hali unayopitia. Pia jikubali na umshukuru Mungu kwa kila jambo. Wakati mwingine unajiona una matatizo sababu hujakutana na wenye matatizo zaidi yako. Kuwa na moyo wa kuridhika kwa mambo madogo Mungu anayokupa. Hata kuamka salama tu ni baraka tosha unahitaji kushukuru Mungu.

Ridhika na hali na usonge mbele.

Soma hii pia >  Dalili na Ishara 50 za Mfadhaiko

2. Jitibu magonjwa yafuatayo

Kama tatizo limesababishwa na magonjwa kama kisukari, vidonda vya tumbo, shinikizo la juu la damu au uzito kupita kiasi ni vema ukajitibu kwanza maradhi haya. Tatizo ni kuwa watu wameaminishwa kwamba maradhi haya hayana dawa jambo ambalo si kweli.

Kisukari, shinikizo la juu la damu, vidonda vya tumbo na hata uzito kupita kiasi ni magonjwa yanayotibika kabisa hasa kwa kutumia dawa mbadala na kufuata muongozo sahihi katika kula na kunywa kwa kipindi cha majuma kadhaa.

3. Acha vilevi

Vilevi

Kama tatizo linatokana na matumizi ya vilevi, hatua ya kwanza ni kuviacha kwanza hivyo vilevi. Ndiyo kuviacha kwanza, unatakiwa ujiulize mwenyewe kipi ni mhimu kwako ndoa yako au hivyo vilevi? Mtu anayejali vilevi kuliko hata afya yake hafai.

Kuna watu wanajidanganya kwamba ukitumia sijuwi kilevi fulani nguvu zinaongezeka, ni kweli zitaongezeka hapo mwanzoni mwa matumizi ya hicho kilevi lakini kadri siku zinavyoenda ndivyo utakavyoendelea kuwa mtegemezi wa hicho kilevi na itafika siku hata hicho kilevi hakitasaidia kitu na hapo ndipo hatari zaidi ya kutotibika tatizo lako itakapojitokeza.

4. Tumia Unga wa Msamitu

Msamitu

Unga wa msamitu (mtishamba wa porini) ni mzuri sana katika kutibu tatizo la nguvu za kiume na pia unasaidia sana kwa wanaume wenye tatizo la nguvu za kiume hasa lililosababishwa na kujichua au kupiga punyeto kwa muda mrefu kwani unaimarisha sana mishipa ya uume.

Pia unaweza kuutumia hata kama unasumbuliwa na tatizo la kisukari. Msamitu unao uwezo mkubwa katika kuongeza hamu ya tendo la ndoa hata kwa kina mama pia.

Msamitu pia unatibu magonjwa yafuatayo bila shida yoyote; pumu, chango la uzazi, kupooza mwili, unaondoa kabisa gesi tumboni na kuongeza nuru ya macho kuona.

Msamitu unao uwezo pia wa kuongeza ukubwa wa uume wako. Labda utauliza kwa namna gani?, kwa sababu moja ya kazi zake mwilini ni kuponya mwili uliokuwa umepooza, mwili unapokuwa umepooza ina maana hata damu yako pia inakuwa haitiririki vizuri kama inavyotakiwa na mzunguko mzuri wa damu una umhimu katika nguzu za kiume.

Kwa kuwa mwili ulikuwa umepooza, Msamitu unapokuja kukutibu unakufanya kuwa mtu uliyechangamka na damu yako itaanza kuwa inatiririka kwa mtiririko mzuri zaidi na kama matokeo yake utaanza kuona hata ukubwa wa mheshimiwa unaanza kuongezeka kidogo kidogo.

Na hii ni hasa kwa wale ambao walizaliwa na uume wa kawaida lakini sababu ya punyeto, lishe duni au stress walijikuta maumbile yao yanaanza kusinyaa au kupungua badala ya kuongezeka.

Soma pia hii >Vidonda vya Tumbo husababisha upungufu wa Nguvu za Kiume

5. Mafuta ya habbat soda

Vyakula vya kuongeza nguvu za kiume haraka

Ukiacha uwezo wake katika kuongeza stamina na nguvu kwa wanaume na kuongeza hamu ya tendo la ndoa kwa wanawake, mafuta haya pia hutumika kutibu tatizo la afya dhaifu la mbegu za kiume na kuongeza wingi wake kwa ujumla (semen count).

Kwa mjibu wa tafiti mbalimbali, mbegu za kiume zinaonekana kuimarika na kuwa nyingi za kutosha baada ya kutumia dawa hii kwa miezi miwili kila siku.

Matumizi: Kunywa kijiko kidogo kimoja cha chai kutwa mara 1 kila siku

Soma hii pia > Mafuta ya habbat soda ni dawa kwa kila ugonjwa isipokuwa kifo

Kama utahitaji mchanganyiko wa Unga wa msamitu, unga wa mbegu za maboga, asali, kitunguu swaumu na mdalasini niachie tu ujumbe kwenye WhatsApp +255769142586.

Ofisi yangu inaitwa Victoria Home Remedy ipo Buza Sigara temeke Dar Es Salaam Karibu na ofisi ya TANESCO wilaya ya Yombo, unaingia kupitia jet corner (Uwanja wa Ndege) au Tandika.

Naweza pia kukuletea ulipo unanilipa nauli ya daladala na natuma pia mikoani.

Jiunge na watu wengine zaidi ya 94000 kwenye ukurasa wangu wa facebook kwa kubonyeza hapa

Una ushuhuda wowote kama matokeo ya kutumia blog hii? Soma shuhuda za wengine kwa kubonyeza hapa.

Jiunge na Group langu la Afya Kila Siku kwenye WhatsApp na utakuwa karibu na mimi masaa 24, Ili kujiunga bonyeza hapa

Soma hii pia > Vyakula Vinavyoongeza Nguvu za Kiume

(Imesomwa mara 12,901, Leo peke yake imesomwa mara 758)

91 Comments

Peter Musa

Peter Musa · 17/01/2018 at 9:27 am

saf

Faraja Muna

Faraja Muna · 17/01/2018 at 10:43 am

Pamoja doctor

Essau Alfredy

Essau Alfredy · 17/01/2018 at 11:08 am

Nice

Yohana Buyobe

Yohana Buyobe · 17/01/2018 at 12:20 pm

Je, mwanamke ambae alishawah kujifungua kwa oporeshen analuhusiwa kufanya mazoez ya kukata tumbo. @fadhilipaulo.com

  fadhilipaulo.com

  fadhilipaulo.com · 17/01/2018 at 2:22 pm

  Hapana haruhusiwi kufanya zoezi hilo

  Yohana Buyobe

  Yohana Buyobe · 17/01/2018 at 2:24 pm

  Asante sana, je kuna njia yoyote ya kufanya ili tumbo lake lipungue?

  fadhilipaulo.com

  fadhilipaulo.com · 18/01/2018 at 6:29 am

  Yohana Buyobe Ndiyo njia ipo. Tuwasiliane, WhatsApp +255769142586

  Grace Saimoni

  Grace Saimoni · 18/01/2018 at 3:20 pm

  Duh hilo janga hta mm linanihusu

  Grace Saimoni

  Grace Saimoni · 18/01/2018 at 9:21 pm

  Ila mm nashukuru kwa ushaur wako mzur wa tiba ya asili ya fangasi yani nimepona na cku c nyingi ntareta mrejesho Wang

Kaamil Said

Kaamil Said · 17/01/2018 at 1:46 pm

Gud daktar

Gardy Diego Costa

Gardy Diego Costa · 17/01/2018 at 3:30 pm

Je Mazoez ya kuruka kamba badala ya kukimbia ni sawa.?

Njalimbo Omary

Njalimbo Omary · 17/01/2018 at 5:01 pm

One love doctor Fadhili

Jonathan Salim

Jonathan Salim · 17/01/2018 at 5:19 pm

Je? Mwanaume aliye fanyiwa upasuaji wa tezi dume anaruhusiwa kufanya mazoezi ya kukata tumbo

Mikidadi Juma Mdakia

Mikidadi Juma Mdakia · 17/01/2018 at 6:22 pm

Nikiweka mb ntafungua

Marvel Roshan

Marvel Roshan · 17/01/2018 at 6:45 pm

wale wenye data ni mazoezi gan ayoo

Minzi Stanley

Minzi Stanley · 17/01/2018 at 6:57 pm

Kazi nzuri

Paul Mollel

Paul Mollel · 17/01/2018 at 7:33 pm

Asante

Prosper Mmalungo Mmole

Prosper Mmalungo Mmole · 17/01/2018 at 7:33 pm

Naweza kuzalisha ikiwa nguvu za kiume zimepungua? Naenda bao moja na la fasta sana ndani ya sec kadhaa tu sina wazungu. Msaada tafadhali

  fadhilipaulo.com

  fadhilipaulo.com · 17/01/2018 at 9:39 pm

  tiba ipo niachie tu ujumbe WhatsApp +255769142586, mimi napatikana Victoria Home Remedy ipo Buza Sigara temeke karibu na ofisi ya TANESCO.

  fadhilipaulo.com

  fadhilipaulo.com · 18/01/2018 at 6:31 am

  Ndiyo unaweza, ingekuwa wanaozalisha ni wale wenye nguvu za kiume tu mbona ingekuwa balaa!

  Prosper Mmalungo Mmole

  Prosper Mmalungo Mmole · 18/01/2018 at 7:15 am

  Ahsante sana,mana hii hali imekuja ghafla sana mpk nahisi nimerogwa na mwanamke flani kwa sababu nilikuwa napiga mechi ngumu na nafunga bao nyingi km hamna beki wala kipa,lakini duh najisikitikia sana

  Exavery Anthony

  Exavery Anthony · 18/01/2018 at 1:26 pm

  Hahahahaha duh!!

  Tottimaumbi Maumbi

  Tottimaumbi Maumbi · 18/01/2018 at 3:17 pm

  Poa docta

  D-k Mdashi

  D-k Mdashi · 18/01/2018 at 8:31 pm

  Tafuna njugu kwa wingi kula sana tende kwa maziwa

  Shomari Athuman

  Shomari Athuman · 18/01/2018 at 8:51 pm

  tende zipi izo

  Prosper Mmalungo Mmole

  Prosper Mmalungo Mmole · 19/01/2018 at 8:08 am

  Huku kwetu tende hadimu sana hazipatikani kbs,njugu zipo.

  Paul Mc Donald B

  Paul Mc Donald B · 19/01/2018 at 10:34 am

  Lamba asali

  James John

  James John · 23/01/2018 at 6:25 pm

  Tehtehhh,,,, kunywa mkuyatiiiii

  D-k Mdashi

  D-k Mdashi · 23/01/2018 at 10:27 pm

  Kula mboga mboga kwa wingi

  Laurian Kinyaiya

  Laurian Kinyaiya · 28/01/2018 at 3:11 pm

  Mkuu tafuta unga wa msamitu hyo ndyo funga kaz yan ukiupata wew mwenyewe utanipa matokeo au ukikosa uwo tumia asali mbichi changanya na mdalasin piah hyo babu kubwa

Joseph Yohana

Joseph Yohana · 17/01/2018 at 8:05 pm

Mmh

Joseph Yohana

Joseph Yohana · 17/01/2018 at 8:06 pm

Sisi ambao hatuna m b hatujaona chochote

Robert Lazaro

Robert Lazaro · 17/01/2018 at 9:28 pm

Nimependa sana hii kaka ipo vizuri mazoezi ndio mpango mzima kula vizuri kunywa maji mengi mno

Maxmilian Makoto

Maxmilian Makoto · 18/01/2018 at 6:53 am

Tumekusoma

Ahmed Ally

Ahmed Ally · 18/01/2018 at 6:58 am

Nice

Nerey Msangi

Nerey Msangi · 18/01/2018 at 8:15 am

Pamoja

Kidbway Juma

Kidbway Juma · 18/01/2018 at 9:27 am

Nmekukubali sanaa brother

Makene raphael · 18/01/2018 at 10:38 am

Gud, VP kuruka kamba napenyewe ni Sawa dokta

  fadhili · 22/01/2018 at 8:18 am

  Ni zoezi zuri pia ndugu. Unaweza kufanya

Jackisony Zakaria Mawese

Jackisony Zakaria Mawese · 18/01/2018 at 1:21 pm

Dokta Tunashukuru Sana Kwamafundisho Yako Ira Tunaomba Namba Ambayo Si Yamasap Wengine Tunauwezo Mdogo

Pâsçäl M. Jôhñ

Pâsçäl M. Jôhñ · 18/01/2018 at 1:36 pm

Asante doctor kwa Elimu

Juma Mukhaimar

Juma Mukhaimar · 18/01/2018 at 2:40 pm

PAMOJA

Simon Pyuza

Simon Pyuza · 18/01/2018 at 3:25 pm

Kwl

George Wallece

George Wallece · 18/01/2018 at 3:27 pm

Good

Paul Kennedy Machungwa

Paul Kennedy Machungwa · 18/01/2018 at 4:50 pm

Hilo zoez la squatting limenkumbusha maisha ya ukuruti jkt.Ktk mazngira ya jeshin linaitwa zoez la kunywa viroba.Kiukweli hayo mazoezi yote uliyoyaorodhesha huwa nayafanya sio siri kiafya nipo fit

Bakary Gunda

Bakary Gunda · 18/01/2018 at 5:02 pm

Nilipo litambua hilo mazoezi kwangu ni kama chakula.

Rohamukh Chidy

Rohamukh Chidy · 18/01/2018 at 6:01 pm

sawa kaka

Aman Mdulingwa

Aman Mdulingwa · 18/01/2018 at 7:09 pm

Mazoezi ni afyaa

Timothy · 18/01/2018 at 10:37 pm

Sawa dokta

Timothy Mubuga · 18/01/2018 at 10:48 pm

Sawa dokta kwa ushauri

Joseph Komba

Joseph Komba · 22/01/2018 at 8:41 pm

doctor me huwa na chchumaa na kuinuka nilianza mala 25 mpaka mala90 lakn saiv naenda mpaka mala 200 bila kupumzika je? kuna madhala yoyote?

Ibrahiim Makonovic

Ibrahiim Makonovic · 23/01/2018 at 2:22 pm

doctar unaptikan sehem gani

Davido Moses

Davido Moses · 23/01/2018 at 2:38 pm

nimekusoma doct,yote yako poa xna.

Casian Baranzize

Casian Baranzize · 23/01/2018 at 7:40 pm

Dawa ya mafua ni ipi mtaalamu wetu?

Masongo Japhary Karino

Masongo Japhary Karino · 23/01/2018 at 8:50 pm

Dr upo sawa! Ulivyoelekeza ndivyo ilivyo. Safi sanaaaa

  Benhusein Mhina

  Benhusein Mhina · 19/02/2018 at 8:57 am

  Safi mkuu ata mm ni ivyo ivyo yani tangu nianze haya mazoez nmejikuta mwili una change mwanzo nlikua nawah sana ila saivi kimoja kinakuja dakika 30 hadi 40 hadi nimejiogopa

Innocent Proches

Innocent Proches · 24/01/2018 at 10:02 am

Namba za whatsap vp

Saleh Seif

Saleh Seif · 28/01/2018 at 11:10 am

Shukran
Ilahuounga wamsamitu wapatikana wapi na matumizi yake yakoje

Michael Elikunda

Michael Elikunda · 28/01/2018 at 11:13 am

Docta vp kuhusu unga wa mlonge?

Mussa Pande

Mussa Pande · 28/01/2018 at 12:06 pm

Squatting ime nipa matokeo bora mno

Richbanks Yohana Mshigati

Richbanks Yohana Mshigati · 28/01/2018 at 1:38 pm

Je dokta kuna ukweli kwamba kuendesha baskeli mara kwa mara au kila siku kwa muda wa saa moja kuna athari ktk mfumo unaohusu nguvu za kiume? Na je uendeshaji huo wa baskeli kwa muda wa lisaa kila siku ni mojawapo ya mazoezi??

Hashym Harun

Hashym Harun · 28/01/2018 at 5:02 pm

Safi doctor

Robert Magige

Robert Magige · 29/01/2018 at 9:33 pm

Safi sana

Zungu Black

Zungu Black · 03/02/2018 at 5:12 pm

kwahiyo hatakuinua vyuma fresh tu docta

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *