Rekebisha homoni zako sasa upate ujauzito

Rekebisha homoni zako sasa upate ujauzito
Rekebisha homoni zako sasa upate ujauzito

REKEBISHA HOMONI ZAKO SASA NA UPATE UJAUZITO

Homoni zina mchango mkubwa katika afya kwa ujumla katika mwili wa mwanamke hasa linapokuja suala la uzazi. Mara nyingi usawa usio sawa wa homoni husababishwa na mabadiliko katika homoni ya ‘estrogen’.

Mabadiliko haya mara nyingi hutokea wakati wa kuvunja ungo, wakati wa hedhi, wakati wa ujauzito na wakati wa ukomo wa hedhi (menopause).

Vitu vingine vinavyopelekea mabadiliko ya homoni ni pamoja na kuongezeka umri, lishe duni, kutokujishughulisha na mazoezi, kupungua kwa ogani ya adreno, mfadhaiko au stress, kukosa usingizi, dawa za uzazi wa mpango, sumu na kemikali mbalimbali nk.

mbegu-za-maboga

Dalili zitakazokuonyesha homoni zako hazipo sawa ni pamoja na:

1. Kuwa na tabia ya hamaki (kukosa utulivu)
2. Uchovu sugu
3. Kuongezeka uzito
4. Kupungua kwa nywele
5. Maumivu ya kichwa ya mara kwa mara
6. Kukosa hamu ya tendo la ndoa
7. Chunusi
8. Kuwa na hamu na vyakula au vinywaji vya viwandani kila mara
9. Kushindwa kushika ujauzito
10. Kutokujisikia vizuri kila mara bila sababu maalumu
11. Kukosa usingizi
12. Hasira zisizo na sababu maalumu nk

Zipo dawa za asili zinazoweza kukusaidia kurekebisha na hatimaye kuweka sawa usawa wa homoni mwilini mwako.

Ni mhimu uonane na daktari kabla kwa uchunguzi, vipimo na ushauri zaidi kabla ya kuamua kutumia hivi vinavyopendekezwa kwenye makala hii hasa kama una matatizo kama ya uvimbe katika kizazi, saratani ya matiti, saratani ya kizazi au una saratani katika mirija ya uzazi.

Njia mbadala 6 za kurekebisha homoni zako na hatimaye upate ujauzito:

1. TUMIA OMEGA 3 KILA SIKU

Asidi mafuta yenye Omega-3 yana umhimu mkubwa katika kuweka sawa homoni zako.

Kwa wanawake yana umhimu mkubwa kwani husaidia kurekebisha mzunguko wa hedhi usiosawa na kupunguza dalili za kukoma kwa hedhi (menopausal symptoms). Omega-3 husaidia kuondoa sumu mwilini na vivimbe sehemu mbalimbali za mwili.

• Vitu vyenye omega 3 kwa wingi ni pamoja na mafuta ya samaki (yasiyo na mercury), walnuts, maharage ya soya, mafuta ya nazi, mafuta ya zeituni, mafuta ya mawese na mbegu za maboga. Tumia hivi vitu kila siku katika kuishi kwako ili kuweka sawa homoni zako.

2. VITAMINI D

Vitamini D ni mhimu kwa ajili ya tezi ya pituitari (pituitary gland) iweze kufanya kazi zake vizuri na ni tezi inayotengeneza homoni zingine nyingi mhimu.

Vitamini D pia husaidia kuondoa dalili zinazohusiana na usawa mdogo wa homoni ya ‘estrogen’. Vitamini D pia ina uhusiano na kiwango cha njaa ulichonacho na uzito pia.

Upungufu wa vitamini D unaweza pia kupelekea utolewaji usiosawa wa homoni nyingine ijulikanayo kama ‘parathyroid’.

• Tembea juani wakati wa jua kali dakika 20 hadi 30 kila siku huku ukiwa wazi sehemu kubwa ya mwili wako.

• Kula vyakula kama mafuta ya samaki, maziwa na mayai ya kuku wa kienyeji kila siku.

3. JISHUGHULISHE NA MAZOEZI YA VIUNGO

Kujishughulisha na mazoezi ya viungo ndiyo njia rahisi ya kurekebisha homoni zako kwani mazoezi yanahusika katika uzalishaji wa hizo homoni. Mazoezi huipunguza nguvu homoni inayohusika na mfadhaiko (stresss) ijulikanayo kwa kitaalamu kama ‘cortisol’.

Hii homoni ya Cortisol huidhibiti homoni nyingine mhimu ijulikanayo kama ‘estrogen’ ambayo kama itazidi basi inaweza kuleta madhara kwa afya yako yote kwa ujumla.

Mazoezi ya mara kwa mara huusaidia ubongo kutoa kemikali ambazo huongeza hali ya kujisikia vizuri (improves your mood). Jambo hili la kupelekea ujisikie vizuri husaidia kuweka sawa homoni zako.

Siyo hilo tu mazoezi yatakusaidia pia kuwa na uzito sahihi kwani uzito uliozidi ni sababu mojawapo inayopelekea homoni zako kutokuwa sawa.

Nusu saa ya mazoezi kwa siku inatosha. Tatizo wanawake wengi hawana habari na kitu kinaitwa mazoezi!

• Nenda kaogelee, katembee kwa miguu lisaa limoja, au kimbia taratibu (jogging) mara 3 mpaka 4 kwa wiki.

4. TUMIA MAFUTA YA NAZI

Mafuta ya nazi yale ya asili yaliyotengenezwa nyumbani bila kupita kiwandani ni dawa nyingine nzuri ya asili ya kurekebisha na kuweka sawa homoni zako. Mafuta haya huiwezesha tezi ya koromeo (thyroid) kufanya kazi zake vizuri.

Mafuta ya nazi pia husaidia kuweka sawa sukari katika damu, huongeza kinga ya mwili, huuongezea nguvu mfumo wa mmeng’enyo wa chakula na kusaidia pia kupunguza uzito. Mafuta haya ni mazuri kwa afya ya moyo wako na hayana kolesto yoyote mbaya.

Kunywa vijiko vikubwa viwili kila siku kwa mwezi mmoja hata miwili au hata mitatu kwa uhakika wa matokeo mazuri zaidi. Unaweza pia kuyaweka kwenye kachumbali. Pia nakushauri kila upikapo wali tumia tui zito la nazi na siyo wali tu hata katika mapishi mengine unaweza kutumia tui la nazi, kazi ni kwako.

5. UWATU PIA HUREKEBISHA HOMONI

Madaktari wengi wa tiba asili duniani hushauri kutumia uwatu (kwa Kiingereza huitwa ‘fenugreeek’) kwa ajili ya kuongeza maziwa kwa mama anayenyonyesha. Uwatu hutumika pia kama dawa ya asili ya kuongeza ukubwa wa matiti (natural breast enlargement).

Uwatu husaidia umeng’enywaji wa sukari mwilini na hivyo kuwa msaada mkubwa kwa watu wanaosumbuliwa na ugonjwa wa kisukari na uzito kupita kiasi (obesity).

• Chukua kijiko kikubwa kimoja cha unga wa mbegu za uwatu na uweke ndani ya glasi moja ya maji ya uvuguvugu, koroga vizuri na unywe yote. Fanya hivi kutwa mara 2 kwa mwezi mmoja mpaka miwili.

Unaweza kuongeza asali kidogo kupata radha. Unaweza kutumia pia ndani ya maziwa ya moto hasa kama huna vidonda vya tumbo au kisukari.

6. TUMIA MREHANI (Basil)

Mrehani hutumika pia kama dawa ya asili ya kurekebisha homoni. Huiweka sawa homoni ya ‘cortisol’ ambayo kama itazidi kuwa nyingi inaweza kuleta shida kwenye homoni koromeo (thyroid gland), Mirija ya uzazi na Kongosho. Wakati huo huo mrehani husaidia kuweka sawa akili yako na hivyo huleta hali ya kujisikia vizuri (good mood).

Unaweza kupata Mrehani ukiwa Dar kwenye soko la kisutu au hata kariakoo pia Zanzibar. Ni kiungo mhimu katika mahoteli mengi ya kitalii.

• Tengeneza chai ukitumia majani fresh ya mmea huu na unywe kikombe kimoja kutwa mara 3 kwa miezi miwili hadi mitatu.

MAMBO YA MHIMU KUZINGATIA:

Pamoja na dawa, zingatia haya yafuatayo kwa matokeo mazuri zaidi:

• Kula parachichi 1 kila siku
• Tumia vyakula asili zaidi kuliko vya kwenye makopo na migahawani (fast foods)
• Tumia vyakula vyenye nyuzinyuzi (fiber) nyingi kwenye chakula chako
• Epuka kahawa, chai ya rangi, soda nyeusi na vinywaji vingine vyote vyenye kafeina ndani yake
• Achana na msongo wa mawazo (stress) na upate usingizi wa kutosha kila siku
• Usitumie dawa za uzazi wa mpango kama unahitaji kuweka sawa homoni zako
• Epuka vilevi vyote
• Kunywa maji mengi kila siku lita 2 hadi 3
• Usitumie vyakula vya moto kwenye vyombo vya plastiki

Kama unahitaji dawa zilizoandaliwa tayari za kurekebisha homoni zako kutoka kwangu tuwasiliane WhatsApp +255769142586, zinagharimu 45000.

Kama unahitaji dozi kamili kwa ajili ya matatizo ya uzazi kama mirija kuziba, uchafu katika kizazi, uvimbe kwenye kizazi, homoni, mayai kutopevuka, kutokuona siku zako nk tuwasiliane WhatsApp +255769142586, zinagharimu 90000.

Kama unahitaji kuonana na mimi weka miadi (appointment) kwenye WhatsApp +255769142586, nipo Buza Sigara Temeke Dar Es Salaam, unaingia kupitia Jet Corner (Uwanja wa ndege) au Tandika. Ofisi yangu inaitwa *VICTORIA HOME REMEDY* ipo Sigara karibu na ofisi ya TANESCO wilaya ya Yombo

Kama hupati ujauzito na hujuwi sababu hasa ni nini tafadhari fika hospitali yoyote kwa uchunguzi na vipimo zaidi.

Kama una swali au unahitaji ushauri uliza hapo kwenye comment nitakujibu.

Like ukurasa huu wangu kwa makala nyingine zijazo kama hii.

Nisaidie ku-SHARE post hii kwa ajili ya rafiki zako wengine

mbegu-za-maboga

(Imesomwa mara 2,808, Leo peke yake imesomwa mara 68)

You may also like...

583 Responses

 1. Mimi nimetumia sindano ya uzazi wa mpango na now meacha kwa muda wa miezi sita sasa na not nahitaji kupata ujauzito nifanyeje?

 2. Niko Arusha uduma hiyo nitaipataje

 3. Ujumbe,,mzuri,SNA!!

 4. Johary Senga Johary Senga says:

  Km mwanamke mirija imeziba inakuaje

 5. Anna Moris Anna Moris says:

  Doctor mm nikiwa kwenye cku zangu nakuwa na hasra xna tatizo nini?

 6. Hongera kwa kaz mungu akubariki. Nna Shida ya muzunguko wa hedhi naweza kaa hata miezi 6 sijaona na nikija kuaza na bleed hata miez miwili. Je kwa hili tatizo linaweza sababisha kukosa mtoto hapo badae na nlivo Pima wananiambia kizazi kipo sawa na sina uvimbe wowote

 7. Stella Lorry Stella Lorry says:

  Tunashukuru kwa Elimu docta *God bless you*

 8. Vickie Rhino Vickie Rhino says:

  Mimi nna shida y kuto kushka ujauzito na cku zangu huwa npta kwa shda sana mauniv mkli zntka kidogo nmefnya chkapu nmeambiwa nna vijiuvumbe pia homni hz balance nmtumia dawa bdo cjaona unafuu,je dawa zko n zamiti shmba au

 9. mini ninatatizo la upungufu wa homon ya oestrogen kwan nina miaka 20 sioni hedhi wala matiti sina pia huwa nakonda sana na kuonekana kama binti mdogo nifanyeje naomba ushauli

 10. Dr mimi kubeba mimba imekuwa shida sana nina mtoto miaka 12 paka leo cjabeba mimba kwenye siku zangu naumwa tumbo sana nikitoka nakuwa poa nini tatizo litakuwa

 11. Mimi nashida ya kutokwenda bled naomba msaaada Dr.

 12. Mm mke Wang anauvimbe ndan ya tumbo mkono WA kushoto atumie dawa ngan

 13. Tatizo langu nimetumy njiti kamuda wamiaka8 sasa nimetoa sasa nina mwaka nanus cijaona ckuzangu nina itaji mtoto naweza pata

 14. Docta unapatikana wap tuje mana Nina tamani mtoto siwezi kupata tatizo kubwa ni homon

 15. Naomba kufaham matumizi ya Mafuta ya zaitun.

 16. Mery Mgimwa Mery Mgimwa says:

  asante kwa ujumbe wako

 17. Shao Nelson Shao Nelson says:

  Hongera sana Dkt Paul,
  Kwa kweli mtu ukipitia comments ndo unajua waTz wanashida kiasi gani ktk matatizo ys uzazi. Daktar wa hospitali hawatoshi kabisa kuhudumia hili kundi.
  Mm naiomba Serikali iangalie Dkt kama nyie sababu mnasaidia sana jamii kwa kweli.
  Nafahamu changamoto yenu, wapo wanaoingia ktk fani iyo kwa nia ya kibiashara ila nimekuwa nafuatilia makala zako naona una hofu ya Mungu na unatoa huduma kwa kwelii.
  Kujibu comments za watu bila kuchoka, i real appreciate.

 18. Happy Victor Happy Victor says:

  Mimi na mwaka na nusu xaxa katika ndoa cjapata mtoto na tatzo cjui na cku zangu hazina mpangilio. nifanye nini na

 19. ASANTE KWA MAFUNZO, JE MNAFANYA NA VIPIMO HAPO HAPO OFISIN KWENU?

 20. Jane Mussa Jane Mussa says:

  Asante kwa somo

 21. Nasra Haji Nasra Haji says:

  Docta: Mbegu Za Kiume Kutoka Nje Ya Uke Baada Ya Tendo Nalo Ni Tatizo

 22. asante kwa elimu yako,naomba kuuliza docta eti mtu napojifungua alafu asipoona cku zake na hajawah kufanya tendo la ndoa je nitatizo,

 23. asante dk kwa somo zur kumbe kutokua na ham ya mapenz n tatizo la homon

 24. Ubarikiwe kwa somo zuri,

 25. Aisha Hamis Aisha Hamis says:

  Ahsante kwa Tiba

 26. Docter mimi nina tatizo la kutokupata hedhi je nitumie nini au nidawa qani nitumie itakayo nisaidia

 27. Naomba namba zako tuwasiliane ili nijue qarama zako na wapi unapatikana

 28. Hellen Moshi Hellen Moshi says:

  Nashukuru Sana kwamsaada wako kwawanawake mm Tatizo langu nikutokwa maziwa tangu nimwachishe mtt wangu mwaka wa Risa we Sasa na pia sioni siku zangu

 29. Lucy Henly Lucy Henly says:

  mm tatizo kuharibikaminba zimetokanne

 30. Chidi Mwaga Chidi Mwaga says:

  Ata mm mke wangu ana kila kitu ulicho elezea docta dah nimepata jibu lake ahsante

 31. Asante sana kwa elimu nzuri kwan hats Mimi kupitia utafiti wako nimesaidia weng sana mungu akubark

 32. Farida Juma Farida Juma says:

  Dk minasumbuliwa na tumbo maumivu makali mno na kuona sioni takirbani mwaka wa6 huu tulio nao ila hapo mwanzo nilikua natumia uzazi wa mpango ila tangu nimeacha ndio Nina miaka 6 sioni

 33. Celina Limbe Celina Limbe says:

  Asante sana kwa elimu bure

 34. Farida Kondo Farida Kondo says:

  Asante kwa elimu

 35. Mary Mtambo Mary Mtambo says:

  Asante sa na doctor kwa ushauri wako mimi natafuta dáwa ya kunisaidia kutokupata ujauzito kwa muda huu na dawa za hospitali huwa zinaniletea madhara je hiyo naweza kupatá??

 36. Asante kwa ushaur wako kesho ntaanza kuufanyiapo kaz,coz 90% ya ulosema apo yananihusu

 37. Mm docta nna kizazi nshazaa watoto wawil ila huwa nachukuwa muda kupata mimba kwa sasa nahitaj kuzaa nifanyeje na cjawahi kutumia uzazi wa mpango toka nianze kuzaa

 38. Glory Nkya Glory Nkya says:

  Asante kwa somo zuri, barikiwa

 39. Aisy Kimaro Aisy Kimaro says:

  Dr ahsante kwa elimu nzur, Mungu akubarik sana kwan watu wengi wana shida mno na ukiangalia hospital ni gharama kumuona specialist ahsant kwa kujitolea

 40. Geofrey Jeas Geofrey Jeas says:

  Doctor fadhiri naomba kunisaidia dawa mbadala ya pumu

 41. Zakia Shaban Zakia Shaban says:

  asante nitakutafuta

 42. Eddy Ngenzi Eddy Ngenzi says:

  Hapo kwenye mambo muhmu ya kuzngatia ndo kuna kasheshe,

 43. Asante kwa darasa naomba ushauri nilishampata mtoto miaka mingi iliyopita nikatumia uzazi wa mpango ndani ya

 44. Zawadi Juma Zawadi Juma says:

  Mm nilikuwa natumia njia zauzazi wampango sindano ilanimeacha mdamlefu sana naitaji ujauzito ijapata hadi Leo nisaidie nifanye nn

 45. Amina Rashid Amina Rashid says:

  Mimi huwa napata maumivu makali sana wakati wa hedhi, tumbo ,kiuno huwa kinauma sana mpaka nikimeza panado maumivu yanapungua ila zamani ilikuwa kila tar.na mwezi zinalingana ila sasa hivi kila mwexi tarehe zinatofautiana.Tatizo ni nini hasa?? Doctor ushauri wako tafadhali

 46. Abby Habby Abby Habby says:

  Doctor naomba kuuliza je kwa wale wa mama waliotumia kufunga mirija ya uzazi kisha mda Wa kukoma hedhi hapati tena he kwa dawa hizi akitumia haitaleta madhara?

 47. Judy Obed Judy Obed says:

  Sante sana doctar kwa ushaur mungu akubarik

 48. Mke anadai hsjisikii Kafanya tendo la ndoa Hata kula denda hataki je ni tatizo linaloishaje?

 49. Mm nina ndugu yangu haoni period vizur kaaenda hospital kaambiwa damu zimeganda plz kuna dawa ya kumsaidia huyo mtu maana anatakiwa ableed hizo uchafu plz doctor help us

 50. Me nina muda mrefu dokta bila kushika ujauzito nifanyeje?

 51. Idd Salim Idd Salim says:

  doctor mm mke wngu anapoingia ktk siku zake huwa kiuno kinamuuma sna ttzo nn? halafu nilipomuowa mwanzo alikuwa anaingia ktkt sku zake kila mwezi lakin doctor alibeba ujauzito ukahabika kutoka hapo mfumo wa siku zke ukabadilika baada ya mwezi ss mpk miezi miwili ai zaid hili doctor husababishwa na nini

 52. Anna Kimaro Anna Kimaro says:

  Asante kwa somo zur doctor. Ndugu yangu anamaumiv makali upande wa kushoto na kulia na damu kutoka kidogo kidogo ameshaenda hosp wakamwambi ni homon imbalance akaambiwa atumie vidonge vya uzaz wa mpango ametumia KwaZulu mwez mmoja na siku kumi ila vikawa vinamletea shida.na baada ya kuviacha amerudia hali ile ile ya kutoka damu kidogokidogo na maumiv makali. Naomba masada wako .na kwa sasa anahitaji kupata uzao wa pili.

 53. Geofrey Jeas Geofrey Jeas says:

  Hivi dkt fadhiri,ofic zako zinapatikana wapi nataka nije kuonana na ww

 54. Atu says:

  Asante docter, tatizo language ni mzunguko was hedhi usioeleweka je nitumie dawa gani?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *