Aina za vidonda vya tumbo

Published by Fadhili Paulo on

Vidonda vya tumbo vimegawanyika katika makundi matatu makuu na leo nitajadili kwa kina aina hizo za magonjwa haya ya tumbo kama ifuatavyo:

1. Vidonda vya tumbo kubwa (Gastric Ulcers):

Aina hii ya vidonda vya tumbo hutokea kwenye mfuko wa kuhifadhia chakula yaani tumbo.

Vidonda hivi hutokea katika utumbo kwa sababu mbalimbali kama vile mtu kupata maambukizi ya bakteria aina ya Helicobacter pylori.

Imegundulika kuwa zaidi ya asilimia 50 ya watu duniani wana vimelea hivi katika utumbo na huwa ni vigumu kuonesha dalili yoyote ya kuugua maradhi haya.

Aina hii ya vimelea vya bakteria husababisha karibu asilimia 60 ya vidonda vinavyotokea kwenye tumbo na huitwa kitaalam Gastric Ulcers.

2. Vidonda vya sehemu ya juu ya tumbo (Duodenal Ulcers):

Hivi ni vidonda ambavyo hutokea kwenye utumbo mdogo.

Aina hii huwapata watu kutokana na kushindwa kwa mfumo wa kinga mwilini ambao huua na kuondoa kabisa vimelea vya kinga ndani ya mwili.

Matokeo ya kushindikana huko kunasababisha kuwepo kwa uambukizi wa kudumu katika kuta za tumbo ambao kitaalam huitwa Chronic Active Gastritis, hivyo kuharibu mfumo na uwezo wa kuta za tumbo kutunza homoni ya Gastrin ambayo kazi yake ni kuhakikisha tumbo linakuwa na tindikali (acid) inayotakiwa tumboni.

Acid hii iitwayo Gastric Acid, ikizalishwa kwa wingi tumboni husababisha kuchubuka kwa ukuta wa tumbo na mtu huyo kuambiwa ana vidonda vya tumbo.

Lakini ukuta wa utumbo hujilinda na madhara yatokanayo na tindikali ya utumbo yaani Gastric Acid kwa kuwa na utando laini (mucus) ambao hutolewa na vichocheo vijulikavyo kama Prostaglandins.

Hata hivyo, kuna dawa ambazo huharibu mfumo wa kutengeza vichocheo hivi yaani Prostaglandins na hivyo kufanya kuta za tumbo kukosa mucus za kuzilinda na mashambulizi ya tindikali, hali ambayo hufanya vidonda vya tumbo kuibuka.

3. Vidonda vya utumbo mdogo (Ulcers in small intestine):

Kundi hili ni wale wagonjwa wanaougua ugonjwa wa vidonda kwenye sehemu ya kwanza ya utumbo mdogo yaani Small Intestine na maumivu yao makali husikia wanapokuwa na njaa na hupata nafuu pindi anapokula.

Soma zaidi kuhusu vidonda vya tumbo kwa kubonyeza hapa.

Fadhili Paulo
Imesomwa mara 143

Fadhili Paulo

Naitwa Fadhili Paulo, ni Tabibu wa Tiba asili. Ofisi yangu inaitwa TUMAINI ALL NATURAL STORE, ipo Mwanagati Kitunda Ilala Dar Es Salaam. Kama unahitaji kuonana na mimi uso kwa uso weka miadi (appointment) kwa kubonyeza HAPA Pia napenda kukujulisha kuwa sina wakala au tawi mahali popote duniani.

0 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *