Chakula cha mama mjamzito

Published by Fadhili Paulo on

CHAKULA CHA MAMA MJAMZITO

Kwa ajili afya ya mama na mtoto ni muhimu sana, mwanamke anatakiwa apate chakula bora kilicho na madini yote kama vitamini na protini.

Mama mjamzito anatakiwa apate gramu 100 za protini kila siku.

Ifuatayo ni mlo kamili anaotakiwa apate mama mjamzito kila siku ya ujauzito wake kwa afya bora.

Nimeweza kukundalia vyakula 10 bora ambavyo mama mjamzito na mtoto wake wanastahili kula

1. Vyakula Jamii ya Kunde

Mbegu za makundekunde ni sehemu muhimu ya chakula kwa mama mjamzito kwa sababu huwa na kiwango kikubwa cha protini.

Kwa watu wasiokula nyama au wana uwezo mdogo tu kujipatia nyama mbegu za jamii kunde zinatosheleza mahitaji ya protini.

Hivi ni vyakula vya mimea kama Soya, Njegere, Karanga, Mikunde, maharage nk

2. Mayai

Mayai mawili kwa siku husaidia kuupa mwili protini, vitamini A na madini ambayo husaidia kuzuia kupatwa na maradhi mbali mbali.

Kumbuka ni mayai ya kuku wa kienyeji ndiyo mazuri kwako na siyo mayai mengine yoyote

3. Maziwa na vyakula vya jamii ya maziwa

Glasi nne au zaidi ya maziwa ya aina yoyote pamoja na/au vyakula vyenye jamii ya maziwa kama jibini, mtindi na siagi.

Maziwa ni muhimu kwa protini, calcium, vitamini na virutubisho vingi. Vitasaidia ukuaji wa mifupa na misuli,

Ni muhimu kwa damu yenye afya, kusaidia usingizi na kusawazisha mapigo ya moyo.

4. Viazi vitamu

Viazi vitamu vina vitamini A ambayo husaidia ukuaji wa macho ya mtoto, ngozi na mifupa

5. Nyama

Nyama ya nguruwe (kama dini yako inakuruhusu), kuku au ng’ombe huwa na protini nyingi sana na husaidia katika ukuaji wa mwili wa mtoto hasa kwa mama mjamzito wa miezi minne

6. Nafaka na vyakula vya wanga

Vyakula hivi huipa mwili nguvu ya kufanya kazi na pia ukuaji wa mtoto tumboni. Vyakula hivi ni kama mahindi, mtama, mihogo, vyakula vya ngano kama mkate n.k.

7. Parachichi

Ni matunda ambayo yana mafuta mengi maarufu kama fatty acid. Parachichi husaidia katika ukuaji wa ubongo, ngozi nyororo na ukuaji wa misuli ya mtoto tumboni.

8. Mboga za majani

Mboga za majani kama spinach, kabeji, mchicha na matembele. Mboga hizi zinafaa ziwe zenye rangi ya kijani iliyokolea kwa sababu hizi ndizo zenye virutubisho vya kutosha.

Mboga hizi zitampa mama na mtoto wake Vitamin A na B, pia virutubisho vitakavyosaidia mwili kupata protini ya kutosha, ukuaji wa mwili, na utengenezaji wa damu.

Kutopata mboga za kutosha kunaweza sababisha mama kupata ugonjwa wa Anemia.

9. Samaki

Mafuta yaliyomo kwenye samaki huwa na Omega fatty acids ambayo inasaidia ukuaji wa ubongo na macho ya mtoto.

10. Maji

Maji ni muhimu kwa mwili kwa sababu inasaidia kwenye mmenyenyo na unyonywaji chakula na pia husaidia kuzia choo ngumu Maji pia huzuia uvimbe wa mwili na maambukizi ya mfumo wa mkojo(UTI)

Kuna chakula kingine mhimu kwa mjamzito sijakiandika? nishirikishe hapo kwenye comment sasa hivi

Ikiwa unatafuta dawa ya asili ili kupata ujauzito nipigie simu au niachie tu ujumbe WhatsApp +255714800175

Chakula cha mama mjamzito 1

Usisahau juisi au chai ya rosella ina madini mengi mhimu kwa mjamzito na ni multivitamin mhimu kwa mjamzito

Tafadhali SHARE post hii kwa ajili ya wengine

Fadhili Paulo
Imesomwa mara 114

Fadhili Paulo

Naitwa Fadhili Paulo, ni Tabibu wa Tiba asili. Ofisi yangu inaitwa TUMAINI ALL NATURAL STORE, ipo Mwanagati Kitunda Ilala Dar Es Salaam. Kama unahitaji kuonana na mimi uso kwa uso weka miadi (appointment) kwa kubonyeza HAPA Pia napenda kukujulisha kuwa sina wakala au tawi mahali popote duniani.

0 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *