Chakula cha mgonjwa mwenye Kisukari aina ya kwanza

Published by Fadhili Paulo on

CHAKULA CHA MGONJWA MWENYE KISUKARI AINA YA KWANZA

Kisukari ni ugonjwa wa kongosho, wakati uzarishaji wa Insulini au utolewaji wake haufanyi kazi vizuri, na ikiwa hali hii haitadhibitiwa, inaweza kusababisha matatizo makubwa kwenye macho, figo, neva, mishipa ya damu, Ini na moyo.

Kisukari aina ya kwanza, ambapo Insulini inakuwa tegemezi (insulin-dependent); hapa kongosho halitengenezi kabisa insulini au linaitengeneza kwa kiasi kidogo sana kiasi kwamba mgonjwa analazimika kuchomwa sindano ya insulini au kutumia pampu za insulini.

Aina ya kwanza ya kisukari inaweza kutokea kwa watu kuanzia utotoni mpaka kwa watu wa umri wa miaka 30. Aina hii ya kisukari hushambulia kwa haraka sana, kwa kawaida ndani ya majuma mpaka miezi kadhaa.

Kwakuwa kongosho halifanyi kazi vizuri, usawa wa damu sukari lazima upewe uangalizi wa karibu. Watu wenye kisukari aina hii ya kwanza pia huwa na uzito pungufu (underweight).

Ni mhimu kula vyakula vyenye afya unapokuwa na kisukari aina ya kwanza. Hata hivyo hii haina maana kwamba unalazimika kuacha kila chakula ukipendacho sababu tu una kisukari.

Aina ya kwanza ya kisukari inaweza kutokea kwa watu kuanzia utotoni mpaka kwa watu wa umri wa miaka 30. Aina hii ya kisukari hushambulia kwa haraka sana, kwa kawaida ndani ya majuma mpaka miezi kadhaa.

Kwakuwa kongosho halifanyi kazi vizuri, usawa wa damu sukari lazima upewe uangalizi wa karibu. Watu wenye kisukari aina hii ya kwanza pia huwa na uzito pungufu (underweight).

Ni mhimu kula vyakula vyenye afya unapokuwa na kisukari aina ya kwanza. Hata hivyo hii haina maana kwamba unalazimika kuacha kila chakula ukipendacho sababu tu una kisukari.

KWANINI NI MHIMU KUZINGATIA CHAKULA

Unapokuwa na kisukari aina ya kwanza mwili wako unaacha kutengeneza insulini. Hivyo unalazimika kuchomwa sindano za insulini kila siku.

Ni mhimu pia kufuatilia kiasi cha damu sukari katika mwili wako kila siku.

Insulini ni sehemu tu ya mambo mhimu ya kuzingatia.

Mlo sahihi na kamili pia mazoezi ya viungo vina umhimu mkubwa kwa mtu mwenye kisukari aina ya kwanza.

Unapochagua kula vyakula vyenye afya kila siku vinaweza kukusaidia kuweka sukari katika kiwango kinachotakiwa.

Kula mlo sahihi kunaweza pia kukusaidia kuepuka na matatizo mengine yahusianayo na kisukari kama ugonjwa wa moyo, magonjwa ya ini, na kudhurika kwa neva.

Chakula cha mgonjwa mwenye Kisukari aina ya kwanza

Baadhi ya wataalamu wamekuwa wakifikiri kwamba kuna lishe au chakula maalumu kwa ajili ya mtu mwenye kisukari.

Wamekuwa wakidhani kwamba mtu mwenye kisukari hatakiwi kabisa kutumia vyakula au vinywaji vyenye sukari na baadhi ya vyakula.

Lakini unapokuwa na kisukari aina ya kwanza unaweza kula vyakula vyovyote vyenye afya kama mtu mwingine yoyote.

Fuata huu muongozo wa jumla:

1. Punguza kutumia mafuta yasiyo na afya (saturated fats).

Haya ni mafuta yatokanayo na wanyama, maziwa, siagi ya wanyama, nk. Mafuta yasiyo na afya yanaongeza uwezekano kwako wa kupatwa na ugonjwa wa moyo.

Unapokuwa na kisukari hatari ya kupata ugonjwa wa moyo inakuwa kubwa zaidi. Hivyo kuwa makini na chaguo la chakula chako ili kupunguza hatari hiyo.

2. Kula vyakula vingi vyenye nyuzinyuzi.

Vyakula vyenye nyuzinyuzi vinaweza kukusaidia kudhibiti sukari yako.

Unaweza kupata nyuzinyuzi toka katika vyakula ambavyo havijakobolewa, maharage, matunda na mboga za majani. Jitahidi upate gramu 25 mpaka 30 kila siku za nyuzinyuzi.

Vyakula hivyo vyenye nyuzinyuzi kwa wingi ni bora zaidi kwa mgonjwa wa kisukari aina ya kwanza kuliko vile vyenye nyuzinyuzi chache kama vile vilivyokobolewa na vile vyenye sukari nyingi vya dukani.

KUTAMBUA KIASI CHA WANGA UNACHOKULA

Vyakula vya wanga ndiyo vyakula pekee ambavyo ni chanzo kikuu cha nguvu cha mwili. Unavipata hivyo katika vyakula vingi unavyokula kama mikate, tambi, mboga za majani, matunda, maziwa, viazi, ugali, wali, sukari nk

Vyakula vya wanga vinapandisha sukari yako kuliko vyakula vingine vyovyote.

Kiasi gani na ni vyakula aina gani hasa hivyo vyenye wanga unavyokula vinaweza kuathiri jinsi gani unadhibiti kisukari chako.

Kujua ni kiasi gani cha wanga unakula ni namna nzuri ya kudhibiti kisukari.

Unaweza kushirikiana na daktari wako au na mtaalamu yoyote wa lishe kufanya hesabu kujua ni kiasi gani cha wanga mwili wako unahitaji kila siku.

MBADALA WA SUKARI

Baadhi ya watu hudhani kuwa sukari husababisha kisukari na hivyo mtu mwenye kisukari eti asitumie kabisa sukari.

Lakini kisukari aina ya kwanza husababishwa na sababu za kijenetiki na mambo mengine yasiyohusu sukari moja kwa moja.

Hata hivyo vyakula vingi vitamu vina wanga mwingi ambao unaweza kuathiri sukari katika damu yako.

Ukiambiwa chakula au kinywaji hakina sukari ndani yake hasa hivyo vya kwenye makopo haina mana kwamba havina wanga au nishati .

Soma vizuri maelezo kwenye vifungashio ya kila unachonunua na kula au kunywa ili ujuwe ni wanga kiasi gani unatumia kila siku.

Pamoja na hayo bado nashauri upendelee kutumia vyakula au vinywaji vyenye nishati kidogo na visiwe vimeongezwa sukari ya kutengenezwa (artificial sweeteners).

VYAKULA VIZURI ZAIDI KWA MWENYE KISUKARI AINA YA KWANZA

Vyakula vifuatavyo vina wanga mchache na vina viinilishe mhimu kama kalsiamu, potasiamu, nyuzinyuzi, magnesiamu na vitamini zingine mhimu. Navyo ni pamoja na:

  1. Maharage
  2. Mboga za majani zenye rangi ya kijani
  3. Matunda jamii ya machungwa
  4. Viazi vitamu
  5. Nyanya
  6. Samaki
  7. Vyakula ambavyo havijakobolewa
  8. Mbegu za maboga
  9. Mtindi usio na mafuta ndani yake
  10. Maziwa yasiyo na mafuta ndani yake

Kama unatafuta dawa ya asili kwa ajili ya kutibu kisukari niachie tu ujumbe WhatsApp +255714800175

Je Umeipenda makala hii?

Share post hii kwa ajili ya wengine

Fadhili Paulo
Imesomwa mara 146
Categories: Kisukari

Fadhili Paulo

Naitwa Fadhili Paulo, ni Tabibu wa Tiba asili. Ofisi yangu inaitwa TUMAINI ALL NATURAL STORE, ipo Mwanagati Kitunda Ilala Dar Es Salaam. Kama unahitaji kuonana na mimi uso kwa uso weka miadi (appointment) kwa kubonyeza HAPA Pia napenda kukujulisha kuwa sina wakala au tawi mahali popote duniani.

0 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *