Chakula cha mgonjwa wa kisukari aina ya pili

Published by Fadhili Paulo on

Chakula cha mgonjwa wa kisukari

Chakula cha mgonjwa wa kisukari aina ya pili

Chakula bora kabisa kwa mgonjwa wa kisukari ni kile ambacho ni chakula cha asili na si kile ambacho kimetengenezwa kiwandani.

Unahitaji chakula ambacho hakijakobolewa, unahitaji zaidi matunda na mboga za majani.

Kutumia vyakula hivi naenda kukueleza kwenye hii makala kutakusaidia kupata mahitaji ya viinilishe unavyohitaji wakati huo huo ukipunguza matatizo yanayoweza kuletwa na kisukari ikiwemo hatari ya kupatwa na magonjwa ya moyo.

Ndiyo, si vyakula hivi tu kwenye hii orodha ndivyo unavyopaswa kuwa unakula, bali kuvijumuisha vyakula hivi kwenye mlo wako kila siku kutakusaidia kuimarika kwa afya yako kwa ujumla.

Kama tayari unafuata mlo wenye afya wenye matunda, mboga za majani na kula vyakula ambavyo havijakobolewa naomba nikupe hongera mapema. Upo njiani kuelekea kwenye maisha ya afya bora na marefu na unaelekea kwenye hatua za kudhibiti uzito wako na kiasi cha sukari kwenye damu yako.

Vyakula hivi naenda kuvijadili siyo tu vina nyuzinyuzi za kutosha, madini, vitamini na viuavijasumu tu, lakini pia vyakula hivi vinapatikana kirahisi kwenye mazingira yetu na vinapatikana kwa bei rahisi.

Kula ugali wa dona na uachane na ugali wa sembe na ugali mzuri kabisa kwa mtu mwenye kisuakri aina ya pili ni ugali wa mtama, kama ni mkate tumia mkate wa ngano ambayo haijakobolewa (brown bread), kunywa maji mengi bila kusahau kujishughulisha na mazoezi ya viungo kila siku.

Kisukari ni ugonjwa wa tabia, ni matokeo ya kile unachokula na kunywa kila siku.

Wapo watu hawaamini kama unaweza kupona Kisukari lakini kama utaamua kula chakula sahihi kwa muda mrefu, ukawa bize na mazoezi kila siku, ukinywa maji ya kutosha kila siku na kutumia chumvi ya kutosha kwenye vyakula vyako kila siku kupona inakuwa ni jambo la kawaida.

Kuna kila aina ya upotoshwaji na maelezo yasiyo sahihi kuhusu ugonjwa wa kisukari, hata hivyo ni ugonjwa wa kawaida ambao hautakiwi kuwa kitendawili kwako kama utakuwa tayari kujifunza ukweli na mambo mapya kupata uelewa mpya na wa kweli.

Kisukari si ugonjwa wa kuendelea kuteseka nao miaka na miaka wala hivi vyakula sijaviandika ili ndiyo iwe lishe yako kwa miaka yote, la hasha hii ni kwa muda mfupi tu wakati ukiwa na kisukari na huku ukipambana kuhakikisha unapona na kutokuwa mtumwa wa kuchagua kula hiki au hiki.

Kisukari aina ya pili ni wakati ambapo insulini inakuwa huru (insulin-independent) au inapatikana lakini kongosho haliitoi na hivyo dawa (kemikali) lazima itumike kulilazimisha kongosho kutoa insulini.

Aina ya pili ya kisukari huanza kujitokeza kuanzia umri wa miaka 40 na kinachosababisha ni miaka mingi ya kula chakula kisicho sahihi, kutofanya mazoezi au sababu za kurithi (genetics).

Kwa bahati mbaya, nyakati hizi tunashuhudia hata watoto wadogo wakipatwa na aina hii ya kisukari. Watu wenye kisukari cha aina hii ya pili pia huwa na uzito uliozidi (overweight).

Chakula cha mgonjwa wa kisukari aina ya pili

Kama unasumbuliwa na Kisukari aina ya pili basi mlo wako wa kila uwe unajumuisha vyakula hivi vifuatavyo:

1. Tufaa (Apple)

chakula cha mgonjwa wa kisukari

Kuna msemo wa kizungu unasema: ‘An apple a day keeps the doctor away’, inamaanisha kula tunda moja la tufaa kwa siku kunaondoa uhitaji wa daktari hasa daktari wa matatizo ya moyo.

Kula tufaa moja tu kwa siku kwa wiki 4 kunaweza kupunguza kolesto mbaya mpaka asilimia 40.

Kuna aina ya viondoa sumu vilivyomo kwenye tufaa ambavyo huwezi kuvipata sehemu nyingine yoyote na ndiyo vinalifanya tunda hili kuwa tunda mhimu zaidi kutumika na mtu mwenye kisukari kila siku.

Tunda hili tamu limeonekana kutoa ulinzi mkubwa kwa watu wenye kisukari hasa kisukari aina ya pili. Tufaa moja dogo la kawaida lina gramu 3 za nyuzinyuzi (fiber), nyuzinyuzi ni kitu kingine mhimu kwa mgonjwa wa kisukari.

Kumbuka pia lakini tufaa moja lina wanga gramu 15 hivyo usile zaidi ya moja kwa siku.

2. Parachichi

Chakula cha mgonjwa wa kisukari aina ya pili 1

Parachichi linajulikana kwa kuwa na mafuta mazuri kwa ajili ya moyo (monounsaturated fat).

Mafuta ya namna hii kama yanayopatikana kwenye tunda la parachichi yanaweza kuweka sawa usawa wa kolesto mwilini, yanaweza kupunguza hatari ya kupatwa na magonjwa ya moyo na hivyo kuwa tunda zuri kwa mtu mwenye kisukari.

Parachichi ni tunda zuri sana kwa mtu anayesumbuliwa na kisukari aina ya pili.

Parachichi ni tunda ambalo sababu ya mafuta yake mazuri, sababu parachihchi moja laweza kuwa na mpaka gramu 16 za mafuta linatakiwa lichukuliwe kama mafuta.

Wakati huo huo parachichi moja lina nyuzinyuzi gramu 2 na wanga gramu 2.

Unaweza kula parachichi lenyewe kama lilivyo, unaweza kuongeza kwenye kachumbali mbalimbali au ukanywa juisi yake kila siku.

3. Maharage

Chakula cha mgonjwa wa kisukari aina ya pili 2

Maharage ni moja ya matunda au mboga za ajabu sana watu wengi hawajuwi.

Kile nataka nikujulishe kupitia makala hii ni kuwa maharage yana nyuzinyuzi (faiba) ya kutosha kwa mahitaji yako ya kila siku na si hivyo tu maharage yana protini bora kabisa kuliko zote isiyo na madhara kama ile ya kwenye wanyama na hizi ndizo sababu maharage ni chakula kizuri sana kwa mtu mwenye kisukari na mwenye shinikizo la juu la damu pia.

Vile vile kutumia vyakula vyenye nyuzinyuzi zaidi kunakuondolea hatari ya kupatwa na mishtuko ya moyo (stroke).

Inasisitizwa upate walau gramu 25 za faiba kila siku. Kikombe kimoja cha maharage yaliyopikwa kina mpaka gramu 9 za faiba.

Inashauriwa kwa watu wenye kisukari kula gramu 25 mpaka 30 za maharage machanga ya kijani kibichi au njegere (green beans), siagi halisi na chumvi dakika 15 kabla ya kwenda kulala, hii itasaidia kushusha damu sukari waamkapo asubuhi.

Maharage haya yana kiasi kidogo cha wanga (carbs), na kiasi kingi cha protini, magnesiamu na asidi amino iitwayo ‘tryptophan’ ili kuubeba mwili usiku mzima.

Jaribu kutumia maharage kama chanzo kikuu cha protini kila siku na vizuri zaidi ni kuwa yanapatikana kwa bei rahisi zaidi ukilinganisha na nyama au samaki.

4. Karoti

Chakula cha mgonjwa wa kisukari aina ya pili 3

Zilizopikwa au zikiwa freshi ni mboga nzuri kuongezwa kwenye chakula chochote. Karoti zina kiasi kingi cha vitamini A, viuavijasumu mhimu zaidi ‘beta-carotene’.

Vitamini A ni mhimu sana kwa matatizo ya macho, kuzuia kansa na kinga ya mwili vitu viwili mhimu sana kwa mtu anayesumbuliwa na Kisukari.

Kwa mjibu wa tafiti mbalimbali hii beta-carotene inao uwezo wa kuzuia usipatwe pia na kisukari hasa kisukari aina ya pili.

Pendelea kutafuna karoti mbichi zaidi na siyo zilizopikwa kwa matokeo mazuri.

5. Samaki

Chakula cha mgonjwa wa kisukari aina ya pili 4

Samaki ni chakula bora kwa mgonjwa wa kisukari. Samaki wana omega 3 ambayo ni nzuri kwa mtu anayetaka kuepuka kolesto na kisukari kwa ujumla.

Omega 3 pia ni nzuri kwa mtu mwenye presha ya kupanda na hupunguza uwezekano wa kutokea tatizo la kupoteza kumbukumbu na ukichaa.

Pamoja na hayo nakushauri utumie samaki wa hapa hapa kwetu Tanzania na siyo wale kutoka nje kwani wengine wanavuliwa kwa namna ambayo si salama kwa afya.

Kula samaki kila mara kama unasumbuliwa na kisukari.

6. Kitunguu swaumu

Chakula cha mgonjwa wa kisukari aina ya pili 5

Kitunguu swaumu ni kiungo kizuri kwa chakula sababu ya harufu yake nzuri ya kupendeza na wakati huo huo ni dawa nzuri sana kwa magonjwa mbalimbali mwilini ikiwemo kisukari.

Kitunguu swaumu kwa miaka mingi kimetumika kutibu kolesto, magonjwa ya moyo, shinikizo la juu la damu na kansa. Hizi ndizo sababu zinazokifanya kitunguu swaumu kuwa chakula bora kwa mtu mwenye kisukari

Hata hivyo ili kitunguu swaumu kiwe kizuri kama tiba ni vizuri kitumike kibichi yaani bila kupikwa katika moto.

Katakata punje 3 za kitunguu swaumu na unywe na maji vikombe viwili kama unavyokunywa dawa nyingine za kawaida kila unapoenda kulala.

Ukishakuwa umevikatakata inashauriwa uviache kwanza katika hewa kwa dakika 10 ndipo umeze kwa matokeo mazuri zaidi.

7. Tikiti maji

Chakula cha mgonjwa wa kisukari aina ya pili 6

Ukipata hamu ya kutaka kula au kunywa chochote kitamu hasa hivi vya dukani basi wewe kimbilia kula tikiti maji au hata juisi yake.

Kama ilivyo kwa nyanya, tikiti maji pia lina viuavijasumu mhimu sana (lycopene) ambavyo vinaweza kusaidia kukukinga dhidi ya baadhi ya kansa na kudhurika kwa seli kunakohusiana na magonjwa ya moyo.

Tikiti maji pia ni zuri pia kwa mtu mwenye kolesto.

8. Unga wa Mbegu za maboga

Chakula cha mgonjwa wa kisukari aina ya pili 7

Unga wa mbegu za maboga ndiyo chakula bora zaidi kwa mtu mwenye Kisukari.

Unga wa mbegu za maboga una mafuta ya omega 3, nyuzinyuzi (faiba), na vitamin E. Vitu Hivi ni mhimu kwa mtu mwenye kisukari hasa kisukari aina ya pili.

Sababu unga wa mbegu za maboga hauhitaji friji ni rahisi kuubeba popote unapokuwa.

Pamoja na hayo nakukumbusha usizidishe sana kula unga huu kwani unao uwezo wa kuongeza uzito na unene kama utatumika kupita kiasi. Kwa kawaida kijiko kikubwa kimoja au viwili kwa siku vinatosha.

Kama utahitaji unga wa mbegu za maboga niachie tu ujumbe WhatsApp +255714800175.

Unga wangu ni mzuri kuliko mwingine wowote umewahi kuuona au kuutumia.

Wakati nasaga nasafisha tu mbegu na kuzikausha, nakaanga kidogo sana katika moto na kuongeza kidogo chumvi ya mawe ya baharini.

9. Vitunguu maji vyekundu

Chakula cha mgonjwa wa kisukari aina ya pili 8

Vitunguu maji ni chanzo kizuri cha viuavijasumu (antioxidants), nyuzinyuzi, na folate vitu vizuri sana kwa afya ya moyo.

Vitunguu maji vina kiondoa sumu mhimu sana kiitwacho ‘flavonoid’ ambacho ndicho hupigana dhidi ya kansa na magonjwa mengine kwenye mfumo wa upumuwaji kama vile pumu.

Ukiweza kula vitunguu maji katika kachumbali kila mara na usivioshe na chumvi, ule ukali wake ndiyo dawa yake yenyewe.

Na vitunguu maji ninavyoongelea hapa zaidi ni vile vyekundu.

10. Pilipili hoho nyekundu

Chakula cha mgonjwa wa kisukari aina ya pili 9

Pilipili hoho nyekundu ni pilipili hoho za kawaida ila tu zinakuwa zimeachwa shambani zikomae kwa muda mrefu zaidi. Pilipili hoho nyekundu zina viiinilishe mhimu ikiwemo kiuakijasumu vitamin C, lycopene na beta-carotene.

Pia zina vitamini A na C ambazo kwa pamoja zinahamasisha afya bora na kupunguza hatari ya kupata magonjwa ya moyo, kisukari na baadhi ya saratani.

Unaweza kuwa upo bize na vidonge vya multivitamins lakini tafiti zinaonyesha vidonge hivyo haviwezi kufanya vizuri kama vile ukila vyakula kamili kama hivi ninavyoelezea kwenye hii makala.

11. Ugali wa Mtama

Chakula cha mgonjwa wa kisukari aina ya pili 10

Kwa sababu ugonjwa wa kisukari unaathiri usawa wa sukari katika damu wapo baadhi ya watu ambao wameaminishwa na wakaamini kwamba mgonjwa wa kisukari hatakiwi kutumia sukari au vyakula vya wanga kama vile ugali wa mtama.

Huwezi kuishi bila kuwa na sukari au chumvi kwenye mwili wako. Kila chakula unachokula ukiacha sukari yenyewe hubadilishwa na kuwa damu sukari (glucose) ndipo kitumike na mwili kutengeneza nguvu.

Ni kweli ulio wazi kwamba mgonjwa wa kisukari anapaswa kuwa makini na vyakula vya wanga ili kudhibiti sukari yao, lakini kile ulikuwa hujuwi ni kuwa kuna aina mbili za wanga ambazo ni wanga mzuri (good carbohydrates) na wanga mbaya.

Wanga mzuri hujulikana pia kwa Kiingereza kama ‘complex carbohydrates’. Huu ni aina ya wanga ambao mgonjwa wa kisukari anaweza kula na bado asipatwe na tatizo lolote. Ni aina ya wanga ambao unapatikana katika ugali wa mtama na tafiti zinasema wanga huu unaweza kukusaidia kudhibiti ugonjwa wa kisukari.

Kwahiyo akitokea mtu anakuambia kwa vile wewe una kisukari basi hutakiwi kutumia wanga wowote uwe na uhakika kwamba anakupoteza na pengine hajuwi wanga ni nini hasa.

Unga wa mtama una kiasi kingi cha nyuzinyuzi (fiber), madini na vitamini mbalimbali mhimu kwa mtu mwenye kisukari. Vitu hivi mhimu vinapaswa kujumuishwa kwenye milo yako ya kila siku.

Kwahiyo ukiulizwa JE MGONJWA WA KISUKARI anaruhusiwa kula ugali wa mtama? Jibu NDIYO ANAWEZA.

Mtama ni nafaka kamili. Hutambuliwa kama wanga mzuri hivyo humeng’enywa kirahisi tumboni. Mtama una viinilishe vizuri kwa ajili ya mgonjwa wa kisukari.

Kikombe kimoja cha unga wa mtama kina:

 • Gramu 6.11 za protini
 • Gramu 2.26 za nyuzinyuzi
 • Ml  76.6 za magnesium
 • Ml  108 za potassium

Ni ugali mzuri na unaongeza sana nguvu mwilini wasukuma na watu wa kanda ya ziwa wanaufahamu kwa hili. Hauongezi mwili na utakufanya ukae muda mrefu bila kusikia njaa tena baada ya kuwa umeula.

Inashauriwa ugali huu uliwe na mboga nyingi za majani na uwe ni mpenzi wa kunywa maji utumiapo ugali huu.

Ingawa mtu yoyote anaweza kupata faida nyingi za kiafya kwa kula ugali wa mtama bado imegundulika ni ugali wenye faida kubwa kwa watu wanaoishi na Kisukari na unatambulika kama moja ya wanga bora zaidi katika kudhibiti damu sukari.

Mtama ni chaguo bora kwa mtu mwenye kisukari sababu ya kuwa na kiasi kingi cha nyuzi nyuzi ndani yake.

Nyuzi nyuzi au faiba husaidia mmeng’enyo wa chakula kwenda pole pole na akama matokeo yake sukari ya kwenye mtama huiingia mishipa ya damu yako pole pole na hivyo kuzuia uwezekano wa damu sukari kuongezeka sana mara baada ya kula kama inavyotokea kwa aina nyingine ya wanga.

Tafiti zinathibitisha kuwa mtama ni chakula kizuri kwa mtu mwenye kisukari. Soma utafiti huu HAPA ambao ulishirikisha watu 300.

Jambo la mhimu kwa mtu mwenye kisukari ni kujitahidi kula vizuri, kula mlo sahihi na kula vyakula vyenye afya. Na hili siyo kwa mtu mwenye kisukari tu bali linapaswa kuwa ni mazoea kwetu sisi sote hata ambao hatuna kisukari.

Kama unahitaji unga wa mtama kwa ajili ya ugali niachie ujumbe WhatsApp +255714800175

12. Spinachi

Chakula cha mgonjwa wa kisukari aina ya pili 11

Spinachi ni chakula kizuri kwako. Pengine tayari unafahamu kwamba spinachi ina vitamini nyingi na madini mbalimbali.

Spinachi ina vitamini C, A, folate na beta-carotene. Bakuli moja ya spinachi kwa siku inakutosha. Spinachi ni nzuri pia kwa kuzilinda seli dhidi ya vijidudu nyemelezi ambavyo vinapelekea magonjwa sugu na kuzeeka mapema.

Watu wanaokula mboga za majani zenye rangi ya kijani wanapata kinga dhidi ya kisukari kwa zaidi ya asilimia 14 hasa wenye kisukari aina ya pili.

Spinachi inapatikana kirahisi karibu kila sehemu hapa Tanzania na kwa bei nafuu kabisa.

13. Nyanya

Chakula cha mgonjwa wa kisukari aina ya pili 12

Nyanya ni chanzo kizuri cha vitamini C na A, pia zina kiondoa sumu mhimu sana kiitwacho ‘lycopene’. Nyanya ni chakula kizuri dhidi ya kansa mbalimbali hasa tezi dume.

Habari njema ni kuwa kiondoa sumu ‘lycopene’ kinahusika moja kwa moja na udhibiti wa ugonjwa wa moyo.

Nyanya zimethibitika kuwa dawa nzuri dhidi ya maambukizi sababu ya kuwa na viinilishe mhimu viwili vijulikanavyo kama ‘carotenoids’ na ‘bioflavonoids’ ambavyo vinahusika pia na kupunguza hatari ya kupatwa na magonjwa ya moyo ugonjwa ambao unatesa watu miaka ya sasa.

Kwenye hili, nyanya nzuri ni ile iliyopikwa ndiyo inayo hii ‘lycopene’ kwa wingi kuliko nyanya freshi.

Bado nakushauri usitumie nyanya za kwenye makopo au za dukani zilizotengenezwa viwandani.

14. Mtindi

Chakula cha mgonjwa wa kisukari aina ya pili 13

Mtindi ni chakula kingine kizuri kwa ajili yako. Ni chanzo kizuri cha kalsiamu ambayo husaidia kuimarisha afya ya mifupa yako na meno pia kujenga na kuimarisha kazi za misuli na mishipa ya damu.

Ni chanzo kizuri pia cha vitamini B2 (riboflavin) na protini.

Mtindi huwa na bakteria wazuri kwa afya yako hasa kwa ajili ya kuongeza nguvu katika mfumo wa mmeng’enyo wa chakula na kuimarisha kinga ya mwili.

Mtindi ni mzuri kwa mtu anayetaka kujikinga hata kujitibu na kisukari aina ya pili.

Mtindi hushusha kolesto na kutengeneza vitamini maalumu ambazo husaidia kudhibiti kisukari. Vitamini D, madini ya kalsiamu na magnesiamu katika mtindi ndivyo vitu vinavyoufanya mtindi kuwa chakula kizuri kwa mtu mwenye kisukari aina ya pili.

Mhimu, pamoja na kuwa mtindi ni chakula kizuri kwako bado unatakiwa usitumie zaidi ya kikombe kimoja kwa siku (robo lita), pia ni mhimu upate mtindi uliouandaa nyumbani kuliko wa dukani na wakati huo huo kama utanunua dukani hakikisha usiwe umeongezwa kitu kingine chochote ndani yake na uwe na mafuta machache au usio na mafuta kabisa.

15. Viazi Vitamu

Chakula cha mgonjwa wa kisukari aina ya pili 14

Viazi vitamu ni chanzo cha madini ya chuma, potasiamu na kalsiamu.

Viazi vitamu vina nyuzinyuzi ambazo husaidia kupunguza kasi ya ufyonzwaji wa sukari kwenye damu. Hii husaidia kudhibiti kiwango cha sukari kwenye damu, kuukinga mwili na kuboresha umeng’enyaji wa chakula.

Kwa sababu ugonjwa wa Kisukari unaathiri usawa wa sukari katika damu kuna baadhi ya watu wamekalilishwa kwamba mgonjwa wa Kisukari hatakiwi kutumia kabisa sukari au vyakula vya wanga kama viazi vitamu.

Hata hivyo kuna wanga wa aina mbili, kuna wanga mzuri na wanga mbaya kama ilivyo kwa mafuta kwamba kuna mafuta mazuri na mafuta mabaya.

Hivyo wanga mzuri kama wanga wa kwenye ugali wa dona, ugali wa mtama na wa kwenye viazi vitamu unaweza kutumiwa na mgonjwa na mgonjwa wa kisukari bila shida yoyote.

Kama unahitaji unga wa dona kwa ajili ya ugali niachie ujumbe WhatsApp +255714800175. Unga wangu wa dona ni mlaini, mzuri na mtamu na ukiutumia hutanunua sehemu nyingine tena zaidi ya kwangu milele kwani ni mzuri hakuna mwingine unaoweza kufanana nao.

Ukweli ni kuwa huwezi kuwa na afya bora bila kula vyakula vyenye wanga. Hata hivyo kuna vyakula vya wanga vyenye afya au vizuri kwa ajili ya mgonjwa wa kisukari.

Kula chakula chenye wanga kidogo au kisicho na wanga kabisa siyo lishe kamili na kunaweza kupelekea mwili kupungukiwa vitu mhimu kama madini, nyuzinyuzi na vitamini.

Kula vyakula vya wanga hata kama una kisukari kunasaidia kupunguza njaa, kupunguza damu sukari na kupunguza kolesto.

Kama unahitaji dawa ya asili inayotibu kisukari aina ya pili, niachie tu ujumbe WhatsApp +255714800175.

Mambo mengine ya kuzingatia:

1. Mgonjwa wa Kisukari usiache kula chakula cha asubuhi

Chakula cha mgonjwa wa kisukari aina ya pili 15

Kuruka kula chakula hasa chakula cha asubuhi kunaweza kusababisha sukari kuongezeka zaidi katika damu.

Unapokaa masaa mengi bila kula sababu ya kuwa ulikuwa umelala au kwa sababu nyingine yoyote mwili huwa unajitafuna wenyewe ili kupata damu sukari toka katika ini.

Watu wengi wenye kisukari aina ya pili ini huwa linashindwa kuona kama kuna sukari nyingi tayari kwenye damu na hivyo lenyewe litaendelea kuongeza damu sukari (glucose) kwenye mfumo wako wa mwili.

Kuruka kula chakula cha asubuhi pia kunaweza kusababisha kuongezezeka kwa njaa na hivyo ukala chakula kingi zaidi mlo unaofuata kuliko kawaida yako na hivyo kupelekea kuongezeka uzito.

Mgonjwa wa kisukari usiache kula chakula cha asubuhi wala kuruka kula mlo wowote katika siku

2. Mgonjwa wa Kisukari mazoezi ni mhimu kwako

Chakula cha mgonjwa wa kisukari aina ya pili 16

Mazoezi ni mhimu sana kwa mgonjwa wa kisukari. Kukaa tu kwenye kwenye kiti masaa yote kunaongeza kisukari zaidi.

Mazoezi pamoja na faida zingine pia yatakusaidia kukuwezesha unapata usingizi wa kutosha na wenye utulivu usiku.

Na unapopata usingizi wa kutosha ina maana hata nafasi ya kufanya mazoezi utaipata kumbe kama hupati usingizi wa kutosha utaona hata muda wa kufanya mazoezi hauna.

Mazoezi yanasaidia pia kuweka sawa insulini na kufanya kazi zake kwa ufasaha zaidi.

Fanya mazoezi kila siku si chini ya nusu saa, kama una uzito umezidi fanya dakika 60 kila siku.

Usiingie kwenye kundi la kina chauvivu eti unakosa muda wa kufanya mazoezi sababu upo bize sana! HAPANA hata iweje hakikisha unatenga muda kwa ajili ya mazoezi kila siku.

Mazoezi mazuri ni pamoja na kutembea kwa miguu, kukimbia, kuogelea, kudansi, kuendesha baiskeli nk.

Mgonjwa wa kisukari kama unataka kupona HAKIKISHA UNAFANYA MAZOEZI KILA SIKU.

3. Mgonjwa wa Kisukari pata usingizi wa kutosha kila siku

Chakula cha mgonjwa wa kisukari aina ya pili 17

Kama haupati usingizi wa kutosha kila siku inaweza kupelekea kuvurugika kwa homoni zako kunakopelekea kuongezeka kwa njaa na kuongezeka kwa damu sukari.

Utafiti unaonyesha kuwa kutokupata usingizi mzuri kwa usiku mmoja tu kunaweza kupelekea insulini kutofanya kazi zake vizuri kwa zaidi ya asilimia 25.

Tafuta ratiba nzuri ya kulala inayokufaa. Kama unapata tatizo la kutopata usingizi kila mara tafadhari ongea na daktari wako haraka iwezekanavyo.

Wakati huo huo sikushauri utumie dawa yoyote ya kemikali kwa lengo la kulazimisha kupata usingizi. Unatakiwa pia ukilala usiku basi ulale usingizi mtulivu mpaka asubuhi na siyo kuamka tena kwenda kwenda kukojoa mara kwa mara kwani hii huharibu ubora wa usingizi wako.

Kuamka kila mara usiku kwenda kukojoa ni ishara una sukari nyingi kwenye damu yako, jitahidi unywe maji mengi nyakati za mchana. Pia kuota ndoto za kutishatisha kila mara usiku inaweza kuwa ni ishara ya kuwa na sukari chache kwenye damu yako.

Vyovyote itakavyokuwa zungumza mara nyingi na daktari wako na upime sukari yako mara kwa mara.

Ushauri : Ni vema kuonana na daktari kabla ya kutaka kufanya mabadiliko yoyote katika utaratibu wako wa kula kama ni mgonjwa wa kisukari na unatumia dawa.

Kuna chakula kingine mhimu unahisi nimesahau kukiandika hapa? kitaje hapo kwenye comment.

Makala hii inaendelea kuboreshwa kwa kuongeza picha na maelezo zaidi, endelea kuja …

Tafadhali SHARE kwa ajili ya wengine uwapendao.

Fadhili Paulo
Imesomwa mara 2,735
Categories: Kisukari

Fadhili Paulo

Naitwa Fadhili Paulo, ni Tabibu wa Tiba asili. Ofisi yangu inaitwa TUMAINI ALL NATURAL STORE, ipo Mwanagati Kitunda Ilala Dar Es Salaam. Kama unahitaji kuonana na mimi uso kwa uso weka miadi (appointment) kwa kubonyeza HAPA Pia napenda kukujulisha kuwa sina wakala au tawi mahali popote duniani.

4 Comments

Costa Ruheta · 03/28/2020 at 7:06 am

Nimependa sana asante Mungu akubariki.

  Fadhili Paulo · 03/30/2020 at 2:56 am

  Amina. Karibu sana

Fatuma Mwacha · 06/20/2020 at 1:45 pm

Nimefurahishwa sana kwa maelezo haya. Nimepata mwanga wa kutosha. Mimi ni mgonjwa mpya ( nimegunduliwa mwezi mmoja uliopita) wa kisukari. Najitahidi sana kufuata masharti na maelekezo ya madaktari.
Mungu akuzidishie. Nipo Kibosho Moshi.

  Fadhili Paulo · 06/22/2020 at 3:51 am

  Amina. Karibu tena na tena hapa

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *