Chakula cha Mwanamke anayetafuta Ujauzito

Published by Fadhili Paulo on

Chakula cha Mwanamke anayetafuta Ujauzito

Chakula cha Mwanamke anayetafuta Ujauzito

Fanya mabadiliko haya kwenye mlo wako ili kuboresha afya yako ya uzazi.

Je unatafuta ujauzito? Unajuwa ni chakula kipi upendelee kula ili kuongeza uwezekano wa kupata ujauzito au kuimarisha afya ya ujauzito kwa ujumla?

Kwenye makala hii naeleza vyakula mhimu unavyotakiwa kupenda kula ili kujiongezea afya yako ya uzazi.

Kwa mwanamke anayetafuta ujauzito vyakula anavyopaswa kula ni vile vyenye folic kwa wingi. Chakula kina mchango mkubwa linapokuja suala la kupata ujauzito.

Unatakiwa ujuwe unakula nini na kwa ajili ya nini, usile tu bora ushibe.

Kula mafungu ya vyakula yafuatayo ili kuimarisha afya yako ya uzazi:

1. Mboga za Majani na Matunda

Chakula cha Mwanamke anayetafuta Ujauzito
Matunda

Ili kujiongezea nafasi ya kupata ujauzito, ili kuwa na mayai yenye ubora hakikisha sahani yako ya chakula imejaa matunda na mboga za majani.

Hakikisha nusu ya ujazo wa chakula unachokula imebeba matunda na mboga za majani.

Matunda matatu mhimu zaidi kwa ajili hii ni ndizi, parachichi na tikiti maji.

Matunda haya yanafanya utengeneze mayai bora kwa afya ya uzazi na yanasaidia pia kusafisha mwili wote ikiwemo mji wa uzazi.

Hakikisha matunda yote haya matatu unakula kila siku.

Unahimizwa pia kula mboga za majani nyingi na za kutosha kila siku. Unaweza pia kutengeneza juisi freshi ya mboga hizi za majani ili kupata viinilishe kwa kiwango cha juu kabisa.

2. Mafuta mazuri

Unahitaji mafuta ili kuwa na afya bora ya uzazi. Mafuta ninayohimiza hapa ni yale yatokanayo na mimea kama vile mafuta ya zeituni, mafuta ya parachichi, mafuta ya nazi, mafuta ya mbegu za maboga na mafuta ya karanga.

Mafuta haya yanaweza kukusaidia kutibu na kuzuia uvimbe, kuweka sawa mzunguko wa hedhi, kuweka sawa homoni na kuongeza afya ya uzazi kwa ujumla.

3. Wanga unaomeng’enywa pole pole

Chakula cha Mwanamke anayetafuta Ujauzito
Mkate wa Brown

Utahitaji pia kula vyakula vyenye wanga lakini wanga ule ambao humeng’enywa pole pole na mwili (complex carbs).

Mwili wako humeng’enya vyakula kama biskuti, keki, mkate mweupe na wali mweupe kwa haraka sana na kuvibadili kuwa glukozi (damu sukari).

Ili kuiondoa hii damu sukari kwenye damu kongosho huongeza insulin kwenye damu na tafiti zinaonyesha kiasi kingi cha insulin kwenye damu yako kinasababisha kutungwa ujauzito kuwa kibarua kizito.

Wanga mzuri ni ule wenye nyuzinyuzi nyingi (fiber) kama vile mkate ambao unga wake haujakobolewa (brown bread), ugali wa dona, maharage, matunda, mboga za majani.

Vyakula vya wanga vya namna hii vina matokeo mazuri kwa damu sukari (kisukari) na insulin.

Basi robo ya chakula chako unachokula kiwe ni aina hii ya vyakula vya wanga mzuri.

4. Protini

Samaki

Punguza sana kula nyama nyekundu na ule zaidi samaki hasa samaki wa baharini. Kula zaidi kuku wa kienyeji, mayai yakienyeji, bata na nguruwe (kama dini inakuruhusu).

Vyakula hivi ni vyanzo vizuri vya protini nzuri, madini ya zinki na madini ya chuma vitu ambavyo ni matofali ya kujengea ujauzito wenye afya.

Samaki anajulikana kama Samoni (salmon kwa kiingereza) ni samaki mkubwa mwenye mnofu mwekundu ambaye ni samaki wa maji baridi na dagaa ni samaki wazuri kula kwa mtu anayetafuta ujauzito.

Samaki wanasaidia kukupa mafuta mazuri (omega 3), wanatengeneza mfumo wa neva wa mtoto na kuzuia ujauzito usitoke kirahisi.

Samaki napendekeza wale wa hapa hapa kwetu Tanzania kwani ndiyo wanavuliwa kwa namna nzuri kiafya na hawana madawa mengine yanayotumika kuwahifadhi wasiharibike ambayo yanaweza kuwa na madhara kwa mtumiaji.

Mayai kumbe yanasaidia kuboresha ubongo wa mtoto.

Mayai mawili unaweza kula kila siku. Mayai hayaongezi uzito kama ambavyo wengine wanasema bali husaidia kukufanya ujisikie umeshiba kwa muda mrefu na hivyo kukusaidia usile mara kwa mara jambo linalopelekea usiwe na uzito mkubwa.

Kama upo bize kupata protini nzuri basi nakusihi vyanzo vyake zaidi viwe ni vile vinatokana na mimea kama maharage, choroko, dengu, karanga, mbegu za maboga na mbegu mbegu nyinginezo.

5. Maziwa na Bidhaa zake

Chakula cha Mwanamke anayetafuta Ujauzito
Maziwa na Bidhaa zake

Utahitaji pia kikombe kimoja cha maziwa fresh kwa siku au mtindi. Usizidishe kikombe kimoja kwa siku.

Pia haya maziwa au mtindi ni vizuri vikawa ni vya asili na siyo vya dukani au vya kwenye makopo na kudhibiti kiasi ni mhimu kwakuwa ukizidisha navyo vinaweza kupelekea kuzuia usipate ujauzito.

Na ikiwa kupata ujauzito kwako limekuwa ni jambo la shida kwa muda mrefu basi naweza kusema usitumie maziwa, mtindi wala bidhaa zitokanazo na maziwa.

Lakini kama si jambo kubwa kwako kikombe kimoja (robo lita) cha maziwa freshi au mtindi ni salama kwa afya yako ya uzazi.

Maziwa hata mtindi ukitumia kupita kiasi vinaweza kukuongezea sana uzito na kuharibu mfumo wako wa homoni.

Kama umekuwa ukitafuta ujauzito kwa kipindi kirefu bila mafanikio basi badili chakula unachokula na upendelee zaidi hivi nilivyoeleza hapa kwa kipindi kirefu.

Ikiwa unapata matokeo mazuri kupitia maelezo haya unaweza kunizawadia chochote kwenye tigo pesa 0714800175 (Fadhili Paulo).

Pia kama unahitaji dawa ya asili ya kupata ujauzito niachie ujumbe WhatsApp +255714800175

Tafadhari SHARE post hii kwa ajili ya wengine uwapendao

(Visited 874 times, 1 visits today)

0 Comments

Leave a Reply

Avatar placeholder

Your email address will not be published.

WhatsApp WhatsApp +255714800175