Chakula cha mwanaume anayetafuta ujauzito

Published by Fadhili Paulo on

Chakula cha mwanaume anayetafuta ujauzito

Chakula cha mwanaume anayetafuta ujauzito

Wakati uliopita tulisoma vyakula hivyo upande wa mwanamke na msisitizo ilikuwa ni vyakula vyenye folate au folic acid.

Kumbe kwa upande wa mwanaume msisitizo ni vyakula vinavyotoa sumu mwilini.

Tutaona vyanzo vya sumu kwenye miili yetu wanaume na namna ya kuidhibiti.

Hakuna namna unaweza kuepuka sumu lakini tutaona vyakula vinavyoweza kupunguza hali hiyo na hivyo uwe na afya nzuri kwa ajili ya uzazi

Kuna namna 2 sumu huingia mwilini. Namna ya kwanza ni kupitia vyakula tunavyokula na namna ya pili ni matumizi ya vilevi mbalimbali.

Wakati tumekula chakula mwili hukimeng’enya ili kitumike kama nguvu ya mwili. Wakati wa mchakato huu wa umeng’enyaji wa chakula mwishoni hutengenezwa taka za sumu, unaweza pia kuziita asidi

Tunapokula vyakula vya asidi vilivyoongezwa utamu kama kemikali na kemikali vihifadhio, jumlisha vinywaji ambavyo ni asidi na vimeongezwa utamu kama kemikali; vitakuwa vikiuandaa mwili kupata asidi zaidi

Moja ya sababu kuu ya mtu kutakiwa kula matunda na mbogamboga ni kuwa vyakula hivi ni alkalini, wakati nyama, kuku, samaki, nyama ya nguruwe, pasta na mayai ni asidi.

Wengi wetu siku hizi tunakula vyakula ambavyo vimekwisha andaliwa (fast food) na hatutumii vyakula vyenye alkalini ya kutosha. Kumbuka kuwa kabonidayoksaidi ni asidi pia kama ilivyo kwa kahawa, chai na pombe ambavyo huathiri PH ya damu na tishu.

Seli ndani ya mwili lazima zibaki katika kiasi kidogo cha alkalini kutoka 7.2 mpaka 7.4, wakati 7.0 ni ya kati au husemwa sifuri katika kipimo cha PH (potential hydrogen). Chini ya 7.0 ni asidi na juu ya 7.0 ni alkalini.

Unaweza kukinunua kipimo cha PH na kupima Ph ya mate na mkojo, hii itakupa mwelekeo wa namna gani unafanya kuitunza 7.2 mpaka 7.4 kwenye seli ndani ya mwili wako.

Ikiwa mate yanasoma 6.0 au 6.5 ni kiashiria kuwa una asidi iliyozidi kwenye seli zako.

Kwahiyo kwa mwanaume kuwa na afya nzuri ya uzazi awe bize kuhakikisha anabaki bila kuwa na sumu mwilini.

Vitu vitatu tu vina msaada mkubwa wa kuondoa sumu mwilini navyo ni maji ya kunywa, matunda na mboga za majani.

Hivyo asilimia 80 ya chakula chako kwa siku kama mwanaume unayetafuta ujauzito iwe ni matunda na mboga za majani na maji ya kunywa.

Teua mlo wako mmoja au miwili iwe ni matunda pekee. Mimi napendekeza mlo wa asubuhi au wa jioni uwe ni matunda tu. Sahani nzima ijae matunda tu mbalimbali, ndizi, peazi, tikitimaji, parachichi, embe, papai nk sahani nzima ijae matunda tu mpaka ushibe.

Ninaposema mboga za majani namaanisha nyingi siyo kiasi kidogo pembeni kwenye kibakuli. Mboga za majani nyingi zijae kwenye sahani kubwa na hii ni vizuri kama utakula mchana au hata usiku siyo mbaya.

Hakikisha unakunywa maji mengi kila siku iendayo kwa Mungu glasi 8 mpaka 10 (lita 2 na nusu mpaka 3) bila kujali upo wapi yaani uwe mikoa ya baridi au ya joto ni lazima unywe maji mengi kila siku.

Vingine vyote vinaongeza sumu mwilini iwe ni nyama, samaki, mkate, soda, juisi, ugali, wali, mayai nk. Vyakula hivi mara nyingi vinaongeza sumu kama matokeo ya mmeng’enyo wa chakula.

Unapokuwa ni mwanaume na una tatizo la kupata mtoto nashauri usinywe soda yoyote, juisi yoyote ya dukani, kinywaji chochote cha dukani isipokuwa maji, usinywe pia chai ya rangi na kahawa. Kumbuka nimesema kama una tatizo la kutopata mtoto ila kama huna tatizo hilo unaweza kuvitumia bila shida yoyote.

Vifuatavyo vinaleta sumu au asidi moja kwa moja mwilini navyo ni sigara, tumbaku, bangi, madawa ya kulevya aina zote, pombe, na vilevi vingine vyote unavyovifahamu. Pia usitumie soya na bidhaa zake na kama uzito wako wa mwili upo juu sana nao itafaa upunguwe ili kubaki na afya bora kwa ajili ya uzazi.

Pombe moja tu nayo ni mvinyo mwekundu (red wine) unaweza kunywa glasi moja au mbili tu kwa siku na isikuletee madhara yoyote kama una tatizo la kutopata mtoto.

Unahitaji pia madini ya zinki kwa wingi na utayapata katika unga wa mbegu za maboga ujazo wa kijiko kikubwa cha chakula kutwa mara 1. Madini ya zinki ni mhimu ili kuongeza wingi wa mbegu (sperm volume) na ubora wa mbegu (sperm quality).

Wanaume wengi wenye tatizo la kutungisha mimba huwa na upungufu wa madini ya zinki pia.

Chakula cha mwanaume anayetafuta ujauzito
Unga wa Mbegu za Maboga

Utahitaji pia kuhakikisha homoni yako ya testosterone ipo juu na kwa kiasi kinachotakiwa ili kutungisha ujauzito.

Soma hii pia > Jinsi ya kuongeza uume bila dawa

SHARE Post hii na wengine uwapendao

Jiunge na mimi na watu wengine zaidi ya 94000 kwenye ukurasa wangu wa facebook kwa kubonyeza hapa

Fadhili Paulo
Imesomwa mara 2,201

Fadhili Paulo

Naitwa Fadhili Paulo, ni Tabibu wa Tiba asili. Ofisi yangu inaitwa TUMAINI ALL NATURAL STORE, ipo Mwanagati Kitunda Ilala Dar Es Salaam. Kama unahitaji kuonana na mimi uso kwa uso weka miadi (appointment) kwa kubonyeza HAPA Pia napenda kukujulisha kuwa sina wakala au tawi mahali popote duniani.

0 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *