Chanzo cha kufunga au kupata choo kigumu wakati wa ujauzito

Published by Fadhili Paulo on

CHANZO CHA KUFUNGA AU KUPATA CHOO KIGUMU WAKATI WA UJAUZITO

Kipindi cha ujauzito ni kipindi cha furaha kubwa kwa mwanamke yoyote.

Hata hivyo kuna baadhi ya mabadiliko ya kiafya yanayoweza kukutokea unapokuwa na ujauzito ambayo yanaweza kukuondolea furaha hiyo ikiwemo tatizo la kupata choo kigumu sana au kufunga choo kabisa na kupelekea tatizo la ugonjwa wa bawasiri.

Kwa afya nzuri kabisa kila mtu anahitaji kupata choo walau mara moja mpaka mara tatu kwa siku.

Baadhi ya wanawake wanapokuwa katika kipindi cha ujauzito wanatokewa kupata tatizo la kufunga choo au kupata choo kigumu na chenye maumivu.

Wanawake wengi wanaoumwa ugonjwa wa bawasiri ninapowasiliana nao huniambia walipata ugonjwa huo wakati wakiwa wajawazito au mara tu baada ya kujifungua.

Bawasiri ni matokeo ya kupata choo kigumu kwa muda mrefu na mwishoni hukuletea maumivu wakati unajisaidia haja kubwa, kutoa damu wakati unajisaidia na kukuletea vinyama kwenye njia ya haja kubwa ambavyo vinaweza kukuletea maumivu zaidi wakati unajisaidia.

Soma hii pia 👇

Tiba ya bawasiri bila upasuwaji

Nini chanzo cha kufunga au kupata choo kigumu wakati wa ujauzito?

Kufunga choo au kupata choo kigumu ni tatizo linalowatokea wajawazito wengi.

Ni moja kati ya matatizo makuu yanayolalamikiwa na wanawake wengi wawapo wajawazito.

Karibu asilimia 38 ya wanawake wote wanaopata ujauzito hupatwa na tatizo hili wakati wa ujauzito au baada ya kujifungua.

Chanzo cha kufunga au kupata choo kigumu wakati wa ujauzito

Zipo sababu nyingi za kutokea kwa tatizo hili kwa wamama wajawazito ambazo ni pamoja na zifuatazo:

  1. Mabadiliko ya homoni wakati wa ujauzito – Mabadiliko haya hupelekea misuli ya kwenye mfumo wa mmeng’enyo wa chakula kulegea na kusababisha mwendo wa pole pole wa chakula tumboni na kuleta kufunga choo au kupata choo kigumu.
  2. Kupungua kwa kazi za mwili – Wakati wa ujauzito wanawake wengi hutumia muda mwingi kupumzika.

Hawajishughulishi na mazoezi wala shughuli nyingine za kuuchosha mwili kama vile mazoezi ya viungo.

Mara nyingi kufunga choo au kupata choo kigumu ni matokeo ya kupenda kukaa tu chini au kwenye kiti masaa mengi jambo ambalo ni kawaida kwa wanawake wengi wanapokuwa wajawazito.

  1. Baadhi ya dawa wanazotumia wakati wa ujauzito – Wakati wa ujauzito wanawake huanza kutumia dawa na vidonge mbalimbali ili kujilinda na kumlinda mtoto.

Dawa hizo kwa ajili ya madini na vitamini mbalimbali anazotumia zinaweza pia kumsababishia tatizo la kukosa choo au kupata choo kigumu.

Vitu unavyoweza kufanya ili kuzuia na kutibu tatizo:

Nyingi ya njia zinazotumika kuzuia usipate choo kigumu au kufunga choo ndiyo hizo hizo unaweza kuzitumia kutibu tatizo kama tayari unalo.

Matatizo ya kufunga choo

Matunda

Baadhi ya njia zinazotumika kushughulika na tatizo la kufunga choo au kupata choo kigumu kwa mama mjamzito ni pamoja na;

1. Kula zaidi vyakula vyenye nyuzinyuzi (fiber) – Mboga za majani na matunda uwe ndiyo mlo wako mkuu.

Asilimia 80 ya chakula chako kwa siku iwe ni matunda na mboga za majani. Matunda kama parachichi na ndizi ni mhimu sana kwa mama mjamzito.

Chagua mlo wako mmoja katika milo yako mitatu ya siku uwe ni matunda pekee. Unaweza kuamua chakula cha asubuhi au cha usiku kuwa ni matunda pekee mpaka utakaposhiba.

2. Kunywa maji ya kutosha kila siku: Mama mjamzito au unayenyonyesha unahitaji kuongeza kiasi cha maji unachokunywa kila siku.

Unahitaji maji glasi 8 mpaka 10 za majai kila siku na pengine zaidi ya hapo kama unaishi maeneo yenye joto.

Unaweza pia kunywa juisi ya matunda uliyotengeneza mwenyewe nyumbani. Ni vizuri kutumia asali kidogo katika hiyo juisi badala ya sukari.

3. Punguza au acha kabisa vinywaji vyenye kaffeina – Soda, energy soda, kahawa, chai ya rangi, chokoleti nyeusi, cocoa, nk. Punguza sana matumizi ya sukari na vyakula vigumu kama vile mikate, chapati, viazi vitamu, wali na vingine kama hivyo.

4. Fanya mazoezi – Unaweza kutumia muda mwingi kupumzika hasa miezi miwili mpaka mitatu ya mwanzo ya ujauzito ili kuzuia mimba isitoke kirahisi au kizembe.

Lakini kuanzia mwezi wa nne wa ujauzito unahimizwa kuwa bize na mazoezi ya viungo hasa ya kutembea tembea kwa miguu na kusimama hapa na hapa na siyo kukaa tu chini au kwenye kiti masaa yote.

Huhitaji mazoezi mazito au ya kukimbia riadha, mazoezi tu ya kutembea tembea hapa na pale, kuogelea, kucheza muziki wa pole pole na mmeo, kufagia uwanja, kumtembelea jirani yako na mazoezi mengine madogo madogo.

5. Usitumie simu uwapo chooni – Ukiwa chooni usitumie simu na ni vizuri usitumie choo cha kukaa badala yake utumie cha kuchuchumaa.

Kwenda chooni na kukaa tu muda mrefu huku unachat na mtu kwenye simu kunaweza kukupotezea hitaji la kupata choo na kukuletea kufunga au kupata choo kigumu.

6. Kuwa makini na baadhi ya dawa unazotumia – Baadhi ya dawa unazotumia unapokuwa mjamzito kama vile multivitamins, dawa za kuondoa maumivu, dawa za kuondoa gesi au kiungulia, dawa za kuongeza madini chuma na kalsiamu zinaweza kukuongezea uwezekano wa wewe kupata choo kigumu au kukufunga kabisa usipate choo uwapo mjamzito.

Kubadili aina ya hizo dawa au namna zinavyotumika kunaweza kusaidia kuzuia tatizo la kufunga choo.

Ni mhimu kwamba unawasiliana na kuonana na daktari wako wa karibu uso kwa uso kwa msaada na maelekezo zaidi juu ya tatizo lako na siyo kuishia facebook.

Usitumie dawa yoyote unapokuwa mjamzito bila ushauri na uangalizi wa karibu wa daktari.

Je umekuwa ukitafuta ujauzito bila mafanikio? Kama jibu lako ni ndiyo pata suluhisho la tatizo lako kwa kubonyeza hapa.

Mjulishe rafiki yako kwenye twitter naye asome post hii kwa kubonyeza ujumbe ufuatao:

Chanzo cha kufunga au kupata choo kigumu wakati wa ujauzito Click To Tweet

SHARE post hii na wengine uwapendao

Fadhili Paulo
Imesomwa mara 63

Fadhili Paulo

Naitwa Fadhili Paulo, ni Tabibu wa Tiba asili. Ofisi yangu inaitwa TUMAINI ALL NATURAL STORE, ipo Mwanagati Kitunda Ilala Dar Es Salaam. Kama unahitaji kuonana na mimi uso kwa uso weka miadi (appointment) kwa kubonyeza HAPA Pia napenda kukujulisha kuwa sina wakala au tawi mahali popote duniani.

0 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *