Chanzo cha uzito na unene kupita kiasi

Published by Fadhili Paulo on

Chanzo cha uzito na unene kupita kiasi

Last Updated on 22/05/2021 by Fadhili Paulo

CHANZO CHA UZITO NA UNENE KUPITA KIASI

Kuna watu hudhani ukiwa mnene au mwenye uzito mkubwa ndiyo kuwa na afya na ndiyo maana wengine wakikonda basi huchanganyikiwa kabisa.

Lakini uzito au unene uliozidi ni ugonjwa tena ugonjwa mubaya kabisa ambao unapaswa kuwa makini nao sana kwani ni chanzo cha magonjwa mengine mengi kama vile kisukari, kolesteroli, shinikizo la juu la damu na orodha inaendelea.

Kila mmoja anapaswa kuwa na uzito unaomstahili kulingana na urefu wake.

Na je uzito na unene kupita kiasi hutokeaje mwilini?

Mfumo mkuu wa fahamu katika ubongo hutambua kushuka kwa kiasi cha nguvu kinachopatikana kwa ajili ya matumizi yake.

Hisia za kiu au njaa pia hutokea kunapotokea kupungua kwa nguvu mwilini.

Pengine ulikuwa bado hujuwi ni kwa jinsi gani njaa au kiu hutokea mwilini au ni nini kinacholeta njaa au kiu mwilini.

Hivyo Hisia za kiu au njaa hutokea kunapotokea kupungua kwa nguvu mwilini.

Ili kuiamsha nguvu toka katika mafuta yaliyohifadhiwa, kunahitajika mwingilio maalumu wa ki-homoni.

Zoezi hili huchukuwa muda mrefu zaidi na pengine mazoezi zaidi kwa mishipa huhitajika kuliko udharura wa uhitaji wa nguvu unavyohitajika na ubongo.

Sehemu ya mbele ya ubongo hupata nguvu ama kutoka katika nguvu inayozarishwa kwa nguvu za maji au kutoka katika sukari kwenye mzunguko wa damu.

Nguvu zitokanazo na maji huhitajiwa kwa dharura zaidi siyo katika kuzarisha nguvu tu, bali hata katika mifumo yake ya usafirishaji ambayo hutegemea maji zaidi.

Kwa hiyo hisia za kiu na njaa huja kwa pamoja kuonesha mahitaji ya ubongo. Hatuzitambui hisia za kiu, na tunazichukulia hisia zote kuwa ni hitaji la kula.

Tunakula chakula hata wakati mwili unapotakiwa upokee maji.

Watu waliopunguza uzito wao kwa kunywa maji kabla ya kula, wamefanikiwa kuzitofautisha hisia hizi mbili.

Hawakula kuzidi ya kipimo kuituliza kiu ya mwili kwa maji.

Hata hivyo, watu wengi sana kote duniani huwa hawafuatilii lolote kuhusu uzito wao.

Uzito uliozidi ni ugonjwa na ni hatua ya kwanza katika kuporomoka kwa mwili wa binadamu. Kila mmoja anapaswa kujua kama uzito alionao unafaa kwa mwili wake au la.

Soma pia na hii > Jinsi ya kupungua uzito huku unacheka

KWANINI WATU WANAKULA SANA?

Moja ya sababu ya kuongezeka kwa uzito au unene ni hulka ya watu kupenda kula chakula kingi na hili kwa wengine ni shida.

Yaani kuna mtu ukimkuta anakula chakula kilichopo kwenye sahani ni kile wanaweza kula watu wawili mpaka watatu lakini yeye anakimaliza peke yake na bado ataongeza na soda juu amalizapo hicho chakula!

Ni nini hasa kimepelekea tatizo hili la kuongezeka kwa njaa kwa baadhi ya watu?:

Ubongo wa binadamu una ukubwa kama 1/50 ya uzito wa mwili. Inasemwa, ubongo una seli neva kama tilioni 9, inasemwa, zaidi ya asilimia 85 ya seli za ubongo, ni maji.

Asilimia 20 ya damu yote mwilini imeelekezwa na inapatikana kwa ajili ya ubongo.

Hii inamaanisha ubongo unahitajika kuchukua kila unachokihitaji kwa ajili ya kazi zake toka katika mzunguko wa damu.

Ubongo ni moja kati ya ogani pekee za mwili ambazo hufanya kazi muda wote hata katika usingizi mzito, huzishughurikia taarifa zote toka katika maeneo mbalimbali ya mwili na zile zinazouingia toka katika mazingira, jamii na hata zile toka mazingira ya ki-usumaku.

Katika kushughurikia kazi zote hizo, ubongo hutumia kiasi kikubwa sana cha nguvu.

Wakati huo huo ubongo hutumia nguvu katika kutengeneza mahitaji ya mwanzo na jumbe kemikali (chemical messengers) ambazo zimetengenezwa toka seli za ubongo na ambazo zinatakiwa kusafirishwa kwenda miishio ya neva kuzunguka mwili.

Mfumo wa usafirishaji mwilini hutumia pia kiasi kikubwa cha nguvu.

Kiasi hiki kikubwa cha matumizi makubwa ya nguvu yanayofanywa na ubongo ndiyo sababu ya ubongo kutengewa asilimia 20 ya mzunguko wa damu.

Seli za ubongo huhifadhi nguvu zake katika mifumo miwili. Stoo yake ya kwanza inaitwa Adenosine Triphosphate (ATP), na ya pili inaitwa Guanosine Triphosphate (GTP).

Baadhi ya maswali maalumu hujibiwa na nguvu zilizohifadhiwa toka stoo ya kwanza (ATP) ambayo inapatikana katika maeneo mbalimbali ya seli hasa katika kuta zake.

Kwenye ukuta wa seli (cell membranes) ndiko ambako taarifa huingilia na ndiko ambako majibu huanzishwa.

Kuna mfumo wa mgawo wa ‘nguvu’ ambao hufanya kazi muda wote katika seli. Siyo madokezo yote ya maswali yanaweza kufanikiwa kupata majibu toka katika stoo ya nguvu ya kwanza (ATP).

Kuna vikwazo katika uelekezwaji wa nguvu kwa baadhi ya maswali. Ubongo unakokotoa na kukielewa kipi ni cha mhimu na kipi si cha mhimu katika bajeti yake ya nguvu.

Soma na hii pia > Mbinu 11 za kupunguza uzito na unene bila mazoezi wala kufunga kula

Wakati inapopungukiwa nguvu stoo ya kwanza, baadhi ya madokezo hayapati majibu.

Kupunguwa huku kwa nguvu toka stoo ya kwanza kwa baadhi ya seli za ubongo, kunatokea kujionesha kama hali ya uchovu katika baadhi ya kazi zinazosimamiwa na seli hizo.

Vivyo hivyo, matendo hayo hutokea pia kwa stoo ya pili ya nguvu (GTP).

Katika baadhi ya matendo maalumu ya dharura, baadhi ya nguvu toka stoo ya pili inaweza kuelekezwa kuiongezea nguvu stoo ya kwanza kwa madokezo maalumu kushughurikiwa.

Hifadhi ya nguvu katika maghala ya nguvu za ubongo, inaonekana kutegemea zaidi upatikanaji wa sukari mwilini.

Muda wote ubongo unachukuwa sukari toka katika damu ili kuyajaza maghala yake (ATP na GTP).

Hivi karibuni imegundurika kuwa, mwili unao uwezo wa kutengeneza nguvu kwa kutumia maji (hydroelectric energy), wakati maji peke yake yanapoingia kupitia kuta za seli na kuwasha pampu maalumu za majenereta ya kuzarishia nguvu yaitwayo kwa kitaalamu, ‘cation pumps’, ni kama vile bwawa la umeme linapojengwa karibu na mto mkubwa.

Kwa hiyo ubongo hutumia mifumo miwili kwa ajili ya mahitaji yake ya nguvu, wa kwanza ni ule wa kiumetaboli (umeng’enyaji) wa chakula na kuunda sukari, na wa pili unahusisha matumizi ya maji kuzariha nguvu umeme zitokanazo na maji (hydroelectric energy).

Inajionyesha wazi sasa kwamba ubongo unategemea zaidi nguvu zitokanazo na umeme wa maji hasa katika mifumo yake ya usafirishaji kwenye neva zake kwenda sehemu mbalimbali za mwili.

Ili kuhimili mahitaji ya ubongo, mwili umekuza mfumo maalumu ili kutunza kiasi cha kawaida cha sukari katika mzunguko wa damu.

Hufanya hivyo kwa njia mbili, ya kwanza ni ile ya kusisimua ulaji wa vyakula vyenye protini na wanga ambavyo vitabadilishwa kuwa sukari ikijumuisha pia sukari yenyewe katika mlo, njia ya pili ni ya kubadili wanga na protini toka katika hifadhi ya mwili na kuwa sukari.

Njia hii ya pili huitwa kwa kitaalamu kama ‘Gluconeogenesis’, yaani utengenezwaji wa sukari toka katika malighafi zilizohifadhiwa.

Utengenezaji wa aina hii ya sukari hufanyika katika Ini.

Utegemezi wa sukari kwa kazi nyingi zifanywazo na ubongo, kumepelekea mapenzi kwa vyakula vyenye radha ya utamu.

Mwili umekuza mfumo kanuni maalumu, uunganikaji wa kazi na ogani zingine hasa Ini wakati radha ya utamu inaposikika katika ulimi.

Inapotokea hakuna sukari ya kutosha katika mzunguko, Ini huanza kuitengeneza na kuijaza kwenye usawa wa damu.

Mwanzoni litaanza na wanga uliokuwa umehifadhiwa ukifuatiwa na protini na kiasi kidogo cha mafuta.

Ubadilikaji wa mafuta kuwa sukari huchukuwa muda mrefu zaidi.

Mwili unahitaji kubaki bila chakula (kufunga kula) kwa muda fulani kabla kiasi kikubwa cha umetaboli (umeng’enywaji) wa mafuta hakijaanzishwa.

Protini hupatikana kiurahisi zaidi na umetaboli wake ni mrahisi zaidi kuliko mafuta.

Dipositi za mafuta zimetengenezwa kutokana na yuniti nyingi mbalimbali za asidi mafuta ambazo zimeungana pamoja.

Asidi mafuta za mtu ndizo huvunjwa (humeng’enywa) kwa ajili ya thamani yake kwa nguvu ya mwili.

Kila gramu 1 ya mafuta hutoa kalori 9 za nishati, kila gramu 1 ya protini au sukari hutoa kalori 4 za nishati.

Hii ndiyo sababu mafuta yanapotumika kuzarisha nguvu, mtu hajisikii sana njaa.

Mafuta yatatumika kuzarisha nguvu iwapo tu utakuwa umefanya mazoezi ya viungo au umefunga kula kwa masaa kadhaa, kinyume na hivi mafuta yataendelea kujirundika.

Kwa watoto wadogo, stoo za mafuta zina rangi ya kahawia na zina mzunguko zaidi wa damu.

Kwenye mafuta ya rangi ya kahawia, mafuta yanameng’enywa moja kwa moja na nguvu hutengenezwa.

Baada ya miaka kadhaa baadaye, stoo za mafuta huwa na mizunguko michache ya damu na uwezekano mdogo wa kuvifikia vimeng’enya vinavyozihamasisha asidi mafuta kwa mabadiliko yake kwenye ini na mishipa.

Wakati mwili unapokuwa legelege yaani unapokuwa ni mtu wa kula kulala bila kujishughulisha na mazoezi, mishipa hushambuliwa kirahisi zaidi na protini yake humeng’enywa na kufanywa sukari.

Ingawa, ikiwa mishipa inashuhulishwa, itaanza kumeng’enya baadhi ya mafuta yake yaliyohifadhiwa na kuyatumia kama chaguo la chanzo chake cha nguvu katika kufanya kazi na kuutunza au kuuongeza ujazo wake.

Ili kufanya hivyo, mishipa hukiamsha kimeng’enya chake cha mafuta, homoni iitwayo kwa kitaalamu ‘lipase‘ (tamka lipesi).

Imedhihirika katika majaribio ya kujirudia huko nchini Sweden kwamba kimeng’enya hiki cha kuchoma mafuta huamka baada ya mwendo wa miguu wa saa moja MFULULIZO, na huendelea kumeng’enya mafuta kwa muda wa masaa 12.

Kwa hiyo ikiwa mtu atatembea kwa muda wa saa moja mara mbili kwa siku, atakuwa amekiamsha kimeng’enya (enzyme) hiki kufanya kazi kwa masaa 24 (yaani siku nzima)!.

Kutembea zaidi, ndivyo kimeng’enya hiki kinavyoendelea kujitokeza zaidi, kwa hiyo fungu lolote la mpango wa mlo lazima liegemee zaidi upande wa mahitaji ya mishipa kwa ajili ya matokeo ya muda mrefu ya moja kwa moja ya kifiziolojia katika kumeng’enywa kwa mafuta.

Ni kimeng’enya hiki hiki (lipase) kwenye mzunguko wa damu ambacho huisafisha mishipa dhidi ya mabaki ya mafuta, cholesteroli na dipositi zake.

Hivi ndivyo ilivyo rahisi kupunguza uzito na unene bila nguvu wala gharama yeyote!.

Anza leo, tembea saa moja kutoka kituo A mpaka kituo B bila kupumzika asubuhi na jioni, baada ya wiki mbili pima tena uzito wako kuona namna ulivyofanikiwa kwa muda huo na muda gani uwekeze tena kumaliza tatizo hili linalosumbuwa watu wengi kote duniani. Itabidi uwe na saa kabisa mkononi na siyo unakisia tu, kuhakikisha kweli umemaliza dakika 60 ukitembea kwa kasi pasipo kusimama.

Kama hali yako siyo nzuri sana, unaweza kuanza na dakika 15 siku ya kwanza, dakika 20 siku ya pili, dakika 25 siku ya tatu … hivyo hivyo ukiongeza dakika kadhaa kila siku hadi utakapoweza kwenda lisaa lizima bila kupumzika.

Kumbuka pia kunywa maji kila nusu saa kabla ya kula.

Kazi zinazofanywa kwa kukaa (maofisini) katika maisha yetu ya kisasa, ni kipindi cha mabadiliko ya kiutamaduni.

Fiziolojia ya miili yetu bado haijabadilishwa vya kutosha kuwezesha matumizi yasiyo ya kawaida ya mwili wa binadamu.

Mwili bado unahitaji kushughulishwa kwa mishipa ili kuhimili hali ya kawaida ya kazi zake.

Ikiwa mwili unaendesha kazi zake katika hali yake ya kawaida, utaelewa ni muda gani wa kula na kwa kiasi gani bila kuizidisha hifadhi ya mafuta.

Kila sehemu ya mwili itatumia kiasi chake cha nguvu iliyotengewa kwa ufanisi na kazi zinazoendeshwa vizuri zaidi.

Hivi ndivyo mwili ulivyosanifiwa.

Ingawa, ikiwa ubongo umetumika zaidi (wakati wa mfadhaiko kwa mfano) na mwili haujatumika kwa uwiano huo huo kuusambazia ubongo mahitaji yake ya sukari, mtu mwenye uelewa mdogo ataangukia kwenye kula zaidi mara nyingi na kwa kiasi kikubwa.

Inashangaza zaidi inapotokea tunashindwa kuzielewa ishara za mwili unapoyahitaji maji kwa ajili ya mahitaji yake ya kusambaziwa nguvu, na badala ya kunywa maji, tunakimbilia kula zaidi.

Katika mfadhaiko (stress), mwili unakuwa umepungukiwa maji (dehydrated).

Sababu ya kwanini inatutokea kuongezeka uzito ni rahisi kuielewa sasa. Tunakula ili kuusambazia ubongo mahitaji yake ya nguvu kwa ajili ya kazi zake masaa 24.

Kama ilivyofafanuliwa, mwili una vyanzo vitatu vya nguvu: Sukari, Mafuta na Maji/chumvi.

Hata hivyo, wakati chakula kimeliwa, ni karibu asilimia 20 tu za chakula ndizo hutumika na ubongo, sehemu inayobaki huhifadhiwa taratibu ikiwa shughuli za mishipa (mazoezi) hazitumiki kutumia kiasi chake cha chakula iliyotengewa.

Maji yanapotumika kama chanzo cha nguvu yaani unapokuwa na mazoea ya kunywa maji ya kutosha kila siku, stoo hii ya kuhifadhia sehemu iliyobaki ya chakula, haitokei, maji yanayozidi hutolewa nje kupitia mfumo wa mkojo.

Wakati mwingine utakaposikia njaa kati ya chakula cha asubuhi, cha mchana au cha jioni, badala ya kukimbilia kula chakula, chukua maji kunywa nusu yake kisha tafuna chumvi (hasa chumvi ya mawe) na umalizie maji yaliyokuwa yamebaki na kisha usubiri kwa muda wa dakika 20 na uone kama utaendelea kujisikia njaa.

Zaidi ya asilimia 90 ya njaa yako itakuwa imepotea, hii ilikuwa ni namna ya ubongo wako kukuambia kuwa unahitaji maji.

Ubongo hauwezi kutuma ishara tofauti za njaa na kiu, ishara zote hutumwa kwa pamoja, hatuzitambui ishara za kutaka kunywa maji na badala yake tunakimbilia kula hata wakati mwili unahitaji maji.

Mambo mhimu ya kufanya unapokuwa una tatizo la uzito au unene kupita kiasi:

1. Hakikisha unakunywa maji kila nusu saa kabla ya kula chakula

2. Fanya mazoezi hasa mazoezi ya kutembea kwa miguu mwendo kasi lisaa limoja mara 2 kwa siku kwa mwezi 1 mpaka miwili

3. Punguza vyakula vyenye wanga

4. Punguza vyakula vinavyopikwa katikati ya mafuta mengi kama vile zinavyopikwa chipsi au maandazi

5. Acha kabisa soda na juisi za viwandani

6. Usikae kwenye kiti au usikae tu kwa masaa mengi katika siku

7. Unaweza kufunga mara moja moja katika wiki

Ukiwa na swali zaidi kuhusu makala hii liulize hapo chini kwenye comment nitakujibu tena hapa hapa na wala huhitaji hata kuandika jina lako ili kuuliza swali lako.

Soma na hii pia > Dawa ya asili ya kupunguza uzito, unene na kitambi

Tafadhali SHARE post hii na wengine uwapendao

Chanzo cha uzito na unene kupita kiasi Click To Tweet

Bonyeza kengele ili kujiunga kupokea kidokezo kila mara makala mpya inapoandikwa hapa.

Fadhili Paulo
(Visited 16 times, 1 visits today)

Fadhili Paulo

Naitwa Fadhili Paulo, ni Tabibu wa Tiba asili. Ninayo ofisi yangu binafsi Jijini Dar Es Salaam. lakini nafanya pia kazi kwa njia ya mtandao. Ofisi yangu inaitwa TUMAINI HERBAL LIFE, Ipo Kibugumo Mji Mwema Kigamboni Kama unahitaji kuonana na mimi uso kwa uso weka miadi (appointment) kupitia WhatsApp +255714800175 Nifuate kwenye > Twitter

0 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published.

WhatsApp WhatsApp +255714800175