Dalili 18 zinazoashiria una ujauzito wa mtoto wa kiume

Published by Fadhili Paulo on

Jinsi ya kujua jinsia (gender) ya mtoto tumboni bila ultrasound

Dalili 18 zinazoashiria una ujauzito wa mtoto wa kiume

Awali ya yote nitoe pongezi kwa mama K na Baba K wote popote walipo kwa kazi nzuri na baraka ambayo wanaisubiri kutoka kwa Mungu (mtoto).

Mojawapo ya mambo ambayo yanatia furaha katika maisha ya ndoa ni pale wanandoa wanapokuwa wapo kwenye kipindi cha kutegemea mtoto.

Mambo mengi huwa yanaleta hamasa na ushawishi kuhusiana na huyo mtoto. Mambo kama jinsia yake kama ni wa kiume au wa kike nk.

Maandalizi kadhaa huanza kufanywa kabla hata ya mtoto kuzaliwa, hii ikijumuisha manunuzi ya vitu kwa ajili ya mtoto na majina wakati atakapo zaliwa.

Madaktari wana uwezo wa kujua jinsia ya mtoto ambaye hajazaliwa kwa kutumia kipimo cha ULTRASOUND.

Watu wengi hawajuwi kuwa wanaweza kufahamu jinsia ya mtoto kutokana na dalili ambazo mama mjamzito anazionyesha, kuanzia mabadiliko ya kimwili, kulala na mpaka upendo wa vyakula fulani.

Soma hii pia > Dawa ya asili ya kupata mimba haraka

Utastaajabu kujua kuna uwezekano wa viashiria kuhusiana na jinsia ya mtoto anaetegemewa, bila kwenda hospitali na kutumia ULTRASOUND.

Kuna ishara kadhaa ambazo zinaweza kukujulisha kuhusiana na jinsia ya mtoto hata kabla hajazaliwa.

Kwa mjibu wa tafiti mbalimbali, yafutayo yanaweza kutumika kama viashiria vya kujua kama mama K ana mtoto wa kiume.

Dalili za mimba ya mtoto wa kiume

1) Chakula

Tabia ya mama K kupendelea vyakula vyenye chumvi au vyakula vyenye ukali au uchachu basi ni dalili ya kupata jinsia ya kiume.

Kama mama mjamzito atapendelea kula vyakula vyenye sukari hii ni dalili ya mtoto wa kike kuja.

2) Tumbo la uzazi kuwa juu ama chini

Kama tumbo la mama mjamzito linakua juu ni dalili mtoto wa kike atazaliwa.

Kama tumbo la uzazi la mama mjamzito litakuwa chini hii ni dalili mojawapo ya kuzaliwa mtoto wa kiume.

3) Umachachari wa mama

Kwa kila jinsia mwili au tumbo la mjamzito linavyokua lazima umachachari uwepo, hata hivyo jambo hili linapozidi kuliko kawaida kuna uwezekano mkubwa wa mwanamke kuwa atajifungua mtoto wa kiume.

4) Kukua kwa matiti

Kwenye kila hatua ya kukua ujauzito, mama mjamzito huwa anatambuwa ni jinsi gani matiti yake hubadilika kwa kukua.

Hata hivyo ikitokea titi lake la upande wa kulia kuwa kubwa kuliko la kushoto huwa ni dalili mwanamke huyo ana ujauzito wa mtoto wa jinsia ya kiume.

5) Rangi ya chuchu

Rangi ya chuchu wakati mama akiwa mjamzito zaweza kubashiri jinsia ya mtoto.

Rangi inapokua ni ya kiza kuliko kawaida ni dalili ya kujifungua mtoto wa jinsia ya kiume.

6) Namna anavyolala

Ikiwa mjamzito anapendelea kulalia ubavu wa kulia mara nyingi huwa ni dalili ana ujauzito wa mtoto wa kiume.

7) Maumivu ya kichwa

Ikiwa mama kijacho (mjamzito) anatokewa kupatwa na matatizo ya kuumwa kichwa mara kwa mara ni ishara ya wazi mtoto wa kiume yupo njiani kuja.

8) Uzito wa Baba K

Kama mzazi wa kiume akiongezeka kilo ghafla mara tu ya mkewe kuwa mjamzito ni mojawapo ya dalili za mama mjamzito kujifungua mtoto wa kike.

Kumbe ikitokea mzazi wa kiume hajaongezeka uzito ni dalili za mama K kuwa na mimba ya mtoto wa kiume.

Soma hii pia > Jinsi ya kupata mtoto wa jinsia ya kiume

9) Kuvimba miguu

Ikiwa miguu ya mama mjamzito haivimbi wakati wote wa ujauzito hii inaashiria atajifunguwa mtoto wa kike.

Kwa kawaida mtoto wa kiume ana uwezo wa kumwongezea mjamzito uvimbaji wa miguu hata mara mbili ya ukubwa wake wa kawaida wa miguu ya huyo mjamzito.

Kwahiyo ukiona inatokea miguu inavimba mara kwa mara pengine hata mwanzoni tu miezi miwili au mitatu ya ujauzito ujuwe kuna uwezekano wa kuzaliwa kwa mtoto wa kiume.

10) Mabadiliko katika ngozi

Kama ngozi ya mjamzito ikibadilika na kua yenye mafuta (oily skin) ni dalili za kuashiria mtoto ajae ni wa kike.

Kama ngozi ikibakia kuwa kavu (dry skin) ni dalili za ujio wa mtoto wa kiume.

11) Joto katika nyayo za miguu

Ikitokea mama K anakuwa na nyayo za baridi muda mwingi hata akiwa sehemu za joto ni dalili ya kujifungua mtoto wa kiume.

Kumbe ikitokea nyayo hazijabadilika joto lake halisi ni dalili za mtoto wa kike kuja.

12) Mgawanyo wa uzito katika mwili

Ikiwa mjamzito baada ya kupata ujauzito miezi ya mwanzo anaongezeka uzito (kilo) mwili mzima, ni dalili atajifungua mtoto wa kike.

Kama mama K ataongezeka uzito sehemu ya tumbo tu ni ishara mtoto wa kiume yupo njiani.

13) Vinyweleo

Kama mama mjamzito atatokewa na hali ya nywele za mwili (vinyweleo) kukua kwa haraka na kua imara, ni dalili mtoto wa kiume atazaliwa.

Kumbe ikitokea nywele hazioti mwilini wakati wa ujauzito ni dalili mama ana ujauzito wa mtoto wa kike.

14) Kunawiri kwa nywele kichwani

Ikiwa mama K anatokewa kuwa na nywele nzito nzuri na zenye mafuta (zimenawiri) ni ishara zaa kujifungua mtoto wa kiume.

Na akitokewa na nywele kavu, mbovu, za kukatikakatika au zinakosa mvuto ni dalili ya kujifugua mtoto wa kike.

15) Mstari tumboni

Huu ni msitari ambao hutokea pole pole katika tumbo la mjamzito baada ya kupata ujauzito.

Mstari huu ukitokea na kuishia chini ya kitovu ni dalili ujio wa mtoto wa kike, na kama ukipitiliza mpaka juu ya kitovu ni dalili za kuja kwa mtoto wa kiume.

16) Kiwango cha furaha

Ni ujauzito wa mtoto wa kiume tu ndiyo ambao humpa mama K muwako au sura ya furaha na kunawiri.

Kumbe mimba ya mtoto wa kike humchosha sura mama yake muda wote.

17) Chunusi

Kubeba mimba ya mtoto wa kike huwaletea wajawazito chunusi usoni muda mwingi wakati wa ujauzito.

Kama mama hasumbuliwi na chunusi ni dalili atajifunguwa mtoto wa kiume.

18) Kipimo cha baking soda

Chukua vijiko vikubwa viwili viwili vya baking soda (hujulikana pia kama bicarbonate of soda) na uchanganye na mkojo wa mjamzito.

Kama baking soda itatoa mapovu ya gesi na mliokama wa kuchemka (fizzes), ni dalili mtoto wa kiume anakuja. Kinyume na hapo basi atakuwa ni wa jinsia ya kike.

Mwisho wa siku usiache kumuomba Mungu kwani yeye ndiye muweza wa yote.

Hizi ni dalili tu, ili kupata uhakika zaidi utatakiwa ufanye kipimo cha ULTRASOUND.

Vile vile mtoto ni mtoto tu haijalishi ni wa jinsia gani mhimu ni apewe matunzo mazuri na maandalizi bora kwa maisha yake ya baadaye.

Mimi binafsi kwa mama na baba tulizaliwa watoto 8, wakiume sita na wakike wawili, lakini ni mtoto wa kike ndiye alifanikiwa kuja kuwajengea nyumba wazazi sisi wakiume 6 hatukuweza.

Kama unatafuta dawa ya asili kwa ajili ya kupata ujauzito, niachie tu ujumbe WhatsApp +255714800175

Pokea dondoo nyingine za afya kama hii kupitia facebook BURE. Jiunge na mimi na watu wengine zaidi ya 98000 kwenye ukurasa wangu wa facebook kwa kubonyeza hapa .

Tafadhali SHARE post hii kwa ajili ya wengine.

Soma hii pia > Mimba huanza kuonekana baada ya siku ngapi

Mjulishe rafiki yako kwenye twitter naye asome post hii kwa kubonyeza ujumbe ufuatao:

Dalili 18 zinazoashiria una ujauzito wa mtoto wa kiume Click To Tweet
(Visited 6,243 times, 1 visits today)

0 Comments

Leave a Reply

Avatar placeholder

Your email address will not be published.

WhatsApp WhatsApp +255714800175