Dalili kuu 3 za mwanzo za kisukari kwa wanaume

Published by Fadhili Paulo on

 

Dalili kuu 3 za mwanzo za kisukari kwa wanaume

1. Upungufu wa nguvu za kiume

Upungufu wa nguvu za kiume ni kitendo cha kukosa uwezo wa uume kusimama na kufanya kazi ipasavyo.

Upungufu wa nguvu za kiume unaweza kuwa ni dalili za matatizo mengine ya kiafya ikiwemo shinikizo la juu la damu, magonjwa ya figo na matatizo mengine kwenye mfumo wa upumuwaji.

Upungufu wa nguvu za kiume unaweza kuletwa pia na msongo wa mawazo (stress), baadhi ya dawa za hospitali, kuvuta sigara nk

Jifunze mengi zaidi kuhusu nguvu za kiume kwa kubonyeza hapa.

Wanaume wanoumwa kisukari wana hatari zaidi ya kupatwa na tatizo la upungufu wa nguvu za kiume kuliko wanaume wengine.

Kwa mjibu wa tafiti mbalimbali, karibu asilimia 50 ya wanaume wote wenye kisukari wanakabiriwa pia na tatizo la upungufu wa nguvu za kiume.

Wanaume wenye kisukari hupatwa na upungufu wa nguvu za kiume mwanzoni kabisa wakiwa bado vijana au umri wa kati.

Ikiwa upungufu wa nguvu za kiume limekuwa ni tatizo likikunyemelea na kutishia afya yako ya kitandani kuna uwezekano mkubwa ukawa na kisukari.

2. Kushuka kwa homoni ya testosterone

Wanaume wanaosumbuliwa na kisukari hasa kisukari aina ya pili wana uwezekano wa mara mbili zaidi wa kupungukiwa na homoni mhimu sana kwa mwanaume ijulikanayo kama testosterone.

Testosterone ni homoni mhimu sana kwa afya ya mwanaume na inahusika na afya ya mwanaume kwa ujumla kuanzia kwenye afya yake ya kitandani, afya ya uzazi, wingi wa misuli, mgawanyo wa mafuta mwilini, na uzalishaji wa seli nyekundu za damu.

Kwa sababu ya kuwa na kiasi kidogo cha homoni hii wanaume wenye kisukari wanaweza kuwa na dalili zingine mbaya zaidi za kiafya kuliko dalili hizo zinavyojitokeza kwa wanawake.

Kushuka kwa homoni ya testosterone kunaweza kupelekea matatizo kwa wanaume kama

 • Kushuka kwa hamu ya kutaka kushiriki tendo la ndoa
 • Msongo wa mawazo (stress)
 • Kushuka kwa nguvu ya jumla ya mwili
 • Kupungua kwa wingi wa misuli
 • Kushindwa kuhimili mkojo
 • U.T.I
 • Kushindwa kutungisha mimba na
 • Matatizo mengine kwenye kibofu cha mkojo

3. Kufika kileleni bila mbegu kutoka

Dalili kuu 3 za mwanzo za kisukari kwa wanaume 1

Lipo tatizo lingine ambalo ni ishara za kuja kwa kisukari kwa mwanaume nalo ni kitendo cha mwanaume kushiriki tendo la ndoa na asitowe mbegu au mbegu zinatoka lakini ni chache sana karibu na hakuna.

Kwa kitaalamu tatizo hili hujulikana kama ‘retrograde ejaculation’.

Hujulikana pia kama kilele kikavu.

Kinachotokea ni kuwa mwanaume anaweza kushiriki tendo la ndoa vizuri na akasikia kabisa ile raha ya kufika kileleni kama kawaida lakini akiangalia haoni mbegu zikitoka.

Hapa mbegu zinakuwa zipo ila badala ya kutoka nje kupitia mrija wa kwenye uume (urethra) zenyewe zinaenda moja kwa moja kwenye kibofu cha mkojo.

Ni matokeo ya madhara ya kisukari kwenye mishipa ya damu inayodhibiti kibofu cha mkojo na mrija wa mkojo.

Tatizo hili lenyewe kwa ujumla halina madhara makubwa bali linaweza kupelekea ugumba au hali ya mwanaume kushindwa kutungisha mimba.

Sababu zingine zinazoweza kuleta tatizo hili ni pamoja na upasuaji wa tezidume au kibofu cha mkojo, baadhi ya dawa za shinikizo la juu la damu na dawa za msongo wa mawazo pia majeraha katika uti wa mgongo.

Soma pia hii > Dawa ya kuongeza mbegu za kiume

Vitu vinavyosababisha kisukari kwa wanaume

 • Uvutaji sigara, tumbaku, bangi
 • Unywaji wa pombe kupita kiasi
 • Uzito kupita kiasi
 • Kutokujishughulisha na mazoezi ya viungo
 • Kolesto
 • Shinikizo la juu la damu
 • Ukiwa na umri kuanzia miaka 45 na kuendelea

Mjulishe raiki yako kwenye Twitter naye asome makala hii kwa kubonyeza maneno yafuatayo;

Dalili kuu 3 za mwanzo za kisukari kwa wanaume Click To Tweet

Kama unahitaji dawa ya asili inayotibu kabisa kisukari hasa kisukari aina ya pili nipigie simu au niachie ujumbe WhatsApp +255714800175

Tafadhali SHARE post hii na wengine uwapendao

Fadhili Paulo
Imesomwa mara 1,047
Categories: Kisukari

Fadhili Paulo

Naitwa Fadhili Paulo, ni Tabibu wa Tiba asili. Ofisi yangu inaitwa TUMAINI ALL NATURAL STORE, ipo Mwanagati Kitunda Ilala Dar Es Salaam. Kama unahitaji kuonana na mimi uso kwa uso weka miadi (appointment) kwa kubonyeza HAPA Pia napenda kukujulisha kuwa sina wakala au tawi mahali popote duniani.

0 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *