Dawa asili na vyakula 20 vinavyotibu tatizo la msongo wa mawazo (stress)

Published by Fadhili Paulo on

Dawa asili na vyakula 20 vinavyotibu tatizo la msongo wa mawazo (stress)

Hali ya mfadhaiko inasemwa kutokea wakati ubongo unapokabiliana na tatizo la mvurugiko wa akili na kujikuta ukishindwa kuendana na hali zingine zinazohitaji umakini kwa wakati mmoja.

Jambo hili linaweza kuuteka ubongo na kudhoofisha uwezo wake.

Hatimaye hali hii ya ufadhaikaji katika ubongo inaweza kutengeneza dalili tofauti ambazo zimepachikwa majina mengi kwa mjibu wa sampuli tabia za nje anazozionesha mtu.

Idadi kubwa zaidi ya watu wanazidi kupatwa au wanategemewa kupatwa na aina fulani fulani za mifadhaiko.

Baadhi ya aina za mifadhaiko ni hali za asili katika hatua za maendeleo na kukua kwa mtu.

Kwa bahati mbaya, baadhi ya watu uwezo wao ni mdogo kushughurika na woga, wasiwasi na hamaki zinazohusiana na mifadhaiko.

Kwa bahati mbaya tena wanapotafuta msaada wa kitaaluma, wanapewa aina fulani za madawa.

Mfadhaiko huongeza utiririkaji wa asidi ndani ya tumbo.

Utafiti uliofanywa katika miaka ya hivi karibuni umeonyesha kuwa akili hutumia sehemu kubwa ya nguvu ya mwili.

Baadhi ya madaktari wamesema mfadhaiko huchangia sana katika kutokea kwa magonjwa mengi mwilini zaidi ya 50. !

Inaelezwa na wataalamu kwamba karibu asilimia 50 ya wafanyabiashara wote duniani wanasumbuliwa na maradhi ya kutoridhika, kufunga choo, vidonda vya tumbo na maradhi ya moyo.

Na wafanyabiashara ambao hawajui namna ya kupambana na wasiwasi au mashaka hufa wakiwa vijana.

Wasiwasi na hofu ya maisha humfanya yeyote kuwa mgonjwa.

Mvurugiko wa hisia una matokeo hasi katika afya ya mwili, pia wasiwasi na hofu ya maisha huweza kuleta magonjwa yanayoweza kuuwa kabisa sawa sawa na inavyotokea pia kwa magonjwa yale yatokanayo na lishe dhaifu.

Baridi yabisi, maradhi ya moyo, tezi, kisukari, vidonda vya tumbo, kansa, yote yanaweza kusababishwa na mvurugiko wa mawazo.

Utafiti wa kisayansi unasema hisia zetu na hali zetu na jinsi tunavyomudu kudhibiti mifadhaiko inaweza kutusaidia kuelewa ni kwa kiwango gani afya zetu zilivyo madhubuti au zilivyo dhaifu.

Ingawa utafiti katika uwanja huu ni mpya, lakini utendaji kazi wa mfumo wa kinga ya maradhi ya mwili unaweza kukandamizwa na mfadhaiko wa akili au mawazo yatokanayo na shida za maisha.

Majaribio yaliyofanywa kwa watu wenye mifadhaiko sana kama wajane, watu wanaosumbuliwa na maradhi kwa muda mrefu, watu waliopewa talaka na wale wenye kupambana na adui yalionesha kuwa watu hao huweza kupata maradhi mara kwa mara kutokana na mfumo wao wa kinga ya maradhi kugandamizwa.

Mfano katika kukabiliana na adui, akili hutambua hofu na ubongo hupata taarifa; neva zenye kujiendesha zenyewe hupanda juu ili kukutana na adui.

Hapo moyo huenda mbio, msukumo wa damu nao hupanda na damu huvimba kwenye misuli kwa ajili ya maandalizi ya mapigano au makabiliano na adui.

Oksijeni na virutubishi vingine hukimbilia kwenye ubongo vikimfanya mtu awe tayari zaidi kwa mapigano, na hapo mnyunyizo wa adrenalini, homoni inayohusika na uzalishwaji wa nguvu mwilini huongezeka.

Kadri mfadhaiko unavyokuwa ni wa muda mfupi, ndivyo pia athari zake zinavyokuwa ni fupi.

Lakini pindi mfadhaiko unapodumu kwa muda mrefu kama vile kipindi cha ndoa isiyo na amani au katika hali ya matatizo mengi kila mara, athari zake nazo hudumu kwa muda mrefu.

Dawa asili na vyakula 20 vinavyotibu tatizo la msongo wa mawazo (stress)

Katika kujidhibiti au kujitibu na mfadhaiko au stress jambo la kwanza ni kutambua nini chanzo cha huo mfadhaiko wako, ukishapata kujuwa chanzo ni rahisi kupata suluhisho kwa haraka.

Tambuwa kuwa kila mtu ana matatizo na kila mtu hufeli katika mipango yake na kila mtu hupata hasara.

Tofauti ni kwamba wakati baadhi ya watu wanaweza kumudu kudhibiti mvurugiko wa mawazo, wengine hawajui kabisa nini cha kufanya na matokeo yake hupatwa na mfadhaiko ambao huweza kusababisha maradhi mengi mwilini bila idadi.

Kama utakubali kuyapokea maisha kama yanavyokuja, ukaacha kuyakopa maisha ya jana na ukaacha kuhofu maisha ya kesho, ni hakika kabisa utaweza kujidhibiti kupatwa na mfadhaiko.

Kuna watu wakipatwa na matatizo huyaficha kimya na kuendelea kuumia ndani kwa ndani peke yao, hii ni tabia mbaya sana kiafya, unapopatwa na tatizo jaribu kutafuta mtu au watu unaowaamini na uwaeleze tatizo lako hata kama hawatakusaidia moja kwa moja lakini mawazo na ushauri wao tu vinaweza kuwa ni dawa tosha ya mfadhaiko au stress yako.

Pamoja na hilo dawa asili na vyakula vifuatavyo vitakusaidia kupunguza kama siyo kutibu kabisa hali hii mbaya inayoendelea kuwasumbuwa mamia ya watu kila siku.

1. Iliki

Iliki inao uwezo wa kuzirudishia nguvu mpya seli za mwili na kusafisha mwili jambo ambalo mwishowe linasaidia kuweka sawa akili yako.

Kunywa chai yenye iliki kila siku. Iliki inaweza pia kuongezwa kwenye vyakula na mboga nyingi jikoni.

Kazi ni kwako.

2. Kungumanga

Kungumanga hufanya kazi kama dawa ya kuchangamsha ubongo na kuondoa uchovu na mfadhaiko.

Kama matokeo yake matumizi ya tunda hili kutakufanya kuwa na akili yenye utulivu nah ii ni moja ya dawa rahisi kabisa za kutibu mfadhaiko.

Tumia nusu kijiko kidogo cha chai cha unga wa kungumanga ndani ya kikombe kimoja cha chai ya kijani kutwa mara 1 kila siku.

2. Korosho na maziwa ya moto

Korosho zina vitamini C kwa wingi ambayo inaweza kuuamsha mfumo wako wa neva za fahamu.

Vile vile korosho zina kitu kinaitwa kwa kitaalamu ‘riboflavin’ ambacho huongeza nguvu za mwili na hivyo ukajisikia ni mwenye furaha na mchangamfu.

Korosho pia zina magnesiamu, vitamini B6 na tryptophan ambavyo huhusika na afya ya akili moja kwa moja na hivyo kukusaidia kupigana na mfadhaiko.

Muunganiko wa korosho na maziwa ya moto unakuwa ndiyo dawa bora zaidi ya asili ya kutibu mfadhaiko wa akili.

Changanya unga wa korosho kijiko kidogo kimoja ndani ya kikombe kimoja cha maziwa ya moto na unywe yote kutwa mara 1 kila siku.

3. Baking Soda

Baking soda inaweza kusaidia kukupunguzia kiasi cha hamaki katika ubongo wako na hivyo kukuondolea msongo wa mawazo.

Sababu kubwa ni kuwa baking soda ina uwezo mkubwa wa kuondoa asidi ndani ya mwili wako.

Tumia nusu kijiko kidogo cha chai kutwa mara 1 ndani ya maji ya uvuguvugu kikombe kimoja kila siku.

4. Mafuta ya Samaki

Kwa mjibu wa tafiti mbalimbali watu wengi wanaosumbuliwa na mfadhaiko wa akili huwa wana upungufu wa omega 3 ndani ya miili yao.

Na mafuta ya samaki ni moja ya vyanzo vizuri vya mafuta yenye omega 3 ambayo huhitajika na ubongo wako kwa ajili ya ufanisi wa kazi zake kila siku.

Kunywa kijiko kidogo kimoja cha mafuta ya samaki kila siku au kula samaki wa maji baridi kwa wiki kila mara.

5. Figili

Figili (Celery) ina kiasi kingi cha ‘folic acid’ na potasiamu vitu viwili vinavyoweza kukusaidia usipatwe na mfadhaiko wa akili kirahisi.

Hakikisha kila mara haikosi kwenye mlo wako hii figili.

6. LOZI

Lozi (Almonds) zina vitamini B12 na madini ya zinki kwa wingi ambavyo ni mhimu katika kushusha mfadhaiko wa akili.

Tengeneza juisi yenye lozi 10, kipande cha tangawizi, kikombe kimoja cha maziwa na kiasi kidogo cha unga wa kungumanga kupata radha.

Kunywa juisi hii kila unapoenda kulala na stress yako itapotea yenyewe.

7. Tufaa

Tunda la tufaa (Apple) lina kingi cha potasiamu, phosphorus, na vitamini B.

Viinilishe hivi ni mhimu kwa ajili ya ubongo wako kujiripea na kuunda seli mpya jambo ambalo linaweza kusaidia kutuliza akili yako.

Kwenye mlo wako usikose kuwa na tunda hili kila siku.

8. Nyama ya kuku

Upungufu wa vitamini B6 hupelekea msongo wa mawazo kirahisi zaidi.

Mwili wako unahitaji vitamini B6 kwa ajili ya kutengeneza transmita nyurolojia zinazohusika na kuchangamka kwa akili na mwili wako ambazo ni ‘dopamine’ na ‘serotonin’.

Nyama ya kuku inayo kiasi cha kutosha cha vitamini B6.

Furaha iliyoje kuona kuwa kumbe kula kuku tu kunaweza kukupunguzia au kukuondolea kabisa msongo wa mawazo (stress)?.

Kula nyama ya kuku mara kwa mara.

Kwa kawaida asubuhi mi binafsi napendelea sana kula supu ya kuku.

Mhimu zingatia ni kuku wa kienyeji na siyo hawa wa kizungu ambao wanaweza kukuletea shida zaidi mwilini.

9. Spinach

Kwa mjibu wa utafiti moja ya sababu nyingine ya msongo wa mawazo ni kupungua ‘folic acid’ mwilini.

Ukweli ni kuwa wanasayansi wamegundua watu wengi wanaosumbuliwa na msongo wa mawazo wana kiasi kidogo cha folic acid ukilinganisha na wengine wenye utulivu katika akili zao.

Vile vile homoni mhimu inayojihusisha na udhibiti wa matendo ya akili ijulikanayo kama ‘serotonin’ kiwango chake hushuka chini sana inapotokea folic acid imeshuka mwilini jambo ambalo ndilo hupelekea kutokea kwa msongo wa mawazo au stress moja kwa moja.

Kwa bahati mbaya upungufu huu wa folic acid unawatokea zaidi wanawake kuliko wanaume.

Kikombe kimoja cha spinachi kwa siku kinatosha kukupa folic acid unayohitaji kila siku.

10. Masaji

Masaji ni njia nyingine rahisi ya kuondoa msongo ndani ya mwili wako isiyo na madhara yoyote.

Masaji ambayo inahusisha matumizi ya mafuta ni njia nzuri sana ya kuweka sawa akili yako na kuondoa sumu mwilini kirahisi.

Masaji ya mwili itakufanyia ujisikie vizuri kimwili na kiakili pia.

Kwa kazi hii unaweza kutumia mafuta ya nazi ua ya ufuta au ya karafuu kwa matokeo mazuri zaidi.

Mara moja moja katika wiki pata nafasi ya kupata huduma hii ili kuzuia na kukabiliana na tatizo la msongo wa mawazo (stress).

11. Kahawa

Kahawa inao uwezo pia wa kukufanya ujisikie vizuri na hivyo kuondoa msongo wa mawazo.

Kunywa kikombe kimoja cha kahawa asubuhi ikiwa unakabiliwa na tatizo la mfadhaiko wa akili.

Hata hivyo kuwa makini, kunywa kahawa kupita kiasi kunaweza kukupelekea ukapatwa na mfadhaiko zaidi sababu kahawa ina kaffeina ndani yake ambayo ni dawa ya kulevya kundi la madawa ya kulevya yanayosisimua akili (stimulants drugs).

12. Mafuta ya habbat soda

Tafiti zimeonyesha mafuta ya habbat soda kuwa msaada mkubwa katika kudhibiti tabia za kuhamaki na wasiwasi na hivyo kukuwezesha kujisikia vizuri kila mara. Na utaona matokeo haya baada ya matumizi ya habbat soda kwa siku 30 hivi.

Tafiti kadhaa zimeonyesha watu waliokuwa wakitumia mafuta ya habbat soda wanakuwa ni watu wenye furaha ya asili na kuwa si wepesi kuwa na huzuni au kufadhaika.

Kazi hii ya mafuta ya habbat soda ndiyo mhimu kuliko zote sababu mamilioni ya watu wanakabiliwa na tatizo la kuwa na huzuni au stress na mifadhaiko ya akili kitendo ambacho kinaweza kuharibu kinga zao za mwili na maisha kwa ujumla.

Ni vigumu sana kupata mtishamba ambao unaweza kutibu matatizo yanayohusiana na saikolojia moja kwa moja lakini mafuta ya habbat soda yanaweza kutumika kwa dhumuni hili la kutuliza, kupunguza na kutibu tatizo la huzuni au kufadhaika kwa akili.

Matumizi: Kunywa kijiko kidogo kimoja cha chai kutwa mara 1 kila siku

13. Chai ya Kijani

Watu wanaosumbuliwa na msongo wa mawazo mara nyingi wanapungukiwa na nguvu na ujasiri.

Na chai ya kijani inaweza kukurejeshea vyote hivi viwili yaani nguvu pamoja na ujasiri sababu ina kiinilishe mhimu kwa ajili kijulikanacho kama ‘L- Theanine’ ambacho hufanya kazi hii ya kuondoa mfadhaiko wa akili.

Hivyo kupunguza na kuondoa stress hakikisha hukosi kunywa chai hii mara 2 hata 3 kwa siku.

14. Chumvi

Unaweza ukashangaa kuona chumvi nayo imo kwenye orodha hii.

Ukweli ni kuwa watu wengi hawatumii chumvi ya kutosha kwenye vyakula vyao miaka ya sasa jambo linalopelekea wengi wao kupatwa na mfadhaiko wa akili na hata magonjwa kama shinikizo la juu la damu na kisukari.

Huwezi kuwa na afya bora kama hutumii ya kutosha kwenye vyakula vyako kila siku.

Chumvi ni mhimu mwilini kama ilivyo kwa maji ya kunywa.

Chumvi ninayoizungumzia hapa ni ile yam awe ya baharini ambayo haijapita kiwandani kwakuwa ndiyo huwa madini madogo madogo (trace minerals) mhimu zaidi kwa afya ya binadamu.

Najuwa umeambiwa chumvi ni mbaya na kuwa unatakiwa ule vyakula vyenye chumvi kidogo au visivyo na chumvi kabisa, hata hivyo madai haya hayana ukweli wowote na ndiyo sababu unaona hata kwenye dripu la maji lazima na chumvi iwekwe ndani yake.

Kila lita moja la dripu la maji ndani yake huwekwa chumvi gramu 9.

Chumvi inaweza kuwa mbaya ikiwa tu wewe si mtu unayependa kunywa maji mengi kila siku, ila kama unakunywa maji mengi kila siku basi unahitaji pia chumvi ya kutosha kwenye vyakula unavyokula kila siku.

Kama una msongo wa mawazo na unakula vyakula vyenye chumvi kwa mbali ni wakati sasa wa kubadili mtindo huo na hutakawia kuona mabadiliko mazuri.

15. LIMAU

Limau ni dawa nyingine ya asili rahisi ya kutibu msongo wa mawazo unayoweza kuiendea isiyo na madhara yoyote mabaya hapo baadaye kwenye afya ya mwili wako.

Ndiyo maana kila ukipewa supu asubuhi hawaachi kukuwekea na limau pembeni, kwakuwa limau huondoa uchovu na kujisikia vibaya kirahisi zaidi.

Tumia limau mara kwa mara kwenye kachumbali zako au unaweza kuchanganya vijiko vikubwa viwili vya maji ya limau ndani ya kikombe kimoja cha maji ya kawaida na unywe kila siku kutwa mara 1.

Usizidishe matumizi ya limau hata hivyo kwani kufanya hivyo kunaweza kupelekea kupungua kwa kiasi cha damu mwilini mwako.

16. KABEJI

Imethibitika pasipo na shaka kuwa kabeji ni chakula bora kabisa ambacho kinaweza kuulinda mwili wako dhidi ya aina mbalimbali za kansa, shinikizo la juu la damu, magonjwa ya moyo, maambukizi mbalimbali, na mhimu kuliko yote ni kuwa kabeji inao uwezo pia wa kuzuia usipatwe na hamaki na mfadhaiko wa akili.

Kabeji lina vitamini B6, vitamini K na vitamini C. Ukiacha hayo kabeji pia ni chanzo kizuri cha folate, vitamini B1, potasiamu, copper, nyuzinyuzi (fiber) na manganizi.

Viinilishe hivi ni mhimu sana katika kuichangamsha afya ya akili na mwili kwa ujumla.

Unaweza kutengeneza supu ya kabeji, juisi ya kabeji, kachumbali yenye kabeji ndani yake au ule tu mboga ya kabeji kila mara ili kupunguza stress yako bila gharama wala kutumia dawa yoyote yenye kemikali.

17. MAZOEZI YA VIUNGO

Mazoezi ya viungo ni dawa nyingine inayoweza kukuondoela msongo wa mawazo kirahisi zaidi bila gharama yoyote wala madhara yoyote katika afya yako.

Kuna watu mi nawaita kina chauvivu, kina chauvivu utawasikia ‘nakosa muda wa mazoezi’.

Unakosa muda wa mazoezi mbona muda wa kulala hukosi?

Huo ni uvivu tu ndiyo unakusumbuwa.

Hata katika kupungua uzito watu wengi hawapendi kusikia kuhusu mazoezi, wanahitaji dawa hata kupunguza uzito!

Unapopatwa na msongo wa mawazo au mfadhaiko nenda kawe bize na mazoezi na mazoezi na hutakawia kuona akili yako inarudi kwenye hali ya kawaida bila kukawia.

Mazoezi huongeza furaha, huongeza kujiamini na hukufanya ujisikie mwenye utulivu kwa haraka sana.

Haijalishi upo bize kiasi gani hakikisha unatenga muda wa lisaa limoja la mazoezi kila siku ili kujikinga au kujitibu na msongo wa mawazo.

18. KOROSHO

Unapokuwa unasumbuliwa na mfadhaiko kiasi chako cha madini ya zinki huwa kinashuka chini kwa kiasi kikubwa sana.

Kwahiyo namna nzuri ya kujitibu  tatizo hili ni kutumia vyakula vyenye madini ya kutosa ya zinki kila siku.

Korosho ni moja ya vyakula vyenye madini ya kutosha ya zinki.

Mhimu ni utambuwe kuwa miili yetu haijaundwa kuwa inahifadhi madini ya zink kila siku, hivyo unahitaji kuwa unatumia vyakula hivi siku zote kwa matokeo mazuri zaidi.

Kula kiganja kimoja cha mkono wako cha korosho kila siku na hutakawia kuona akili yako inapata utulivu unaohitajika.

19. MBEGU ZA MABOGA

Msongo wa mawazo au stress kama mlivyozoea wengi ni tatizo linaloendelea kuwasumbua watu wengi miaka ya sasa.

Mbaya zaidi wengi huwa hawaelewi nini madhara ya msongo wa mawazo kiafya.

Yaani stress au msongo wa mawazo unaweza kukuletea magonjwa mengine mwilini zaidi ya 50, hivyo utaona ni jinsi gani ilivyo mhimu kwako kuweka chini stress zako na uendelee na maisha kwani kuendelea kuwa na stress ni hatari zaidi kwa afya yako.

Moja ya sababu kuu ya watu wengi kuwa na stress ni usawa usio sawa wa homoni zao (hormonal imbalance).

Hivyo kama una tatizo la homoni kwenye mwili hebu weka mazoea ya kutafuna mbegu za maboga kila siku na hutakawia kuona tofauti.

Mbegu za maboga zina kimeng’enya mhimu sana kwa kutuliza mawazo kiitwacho ‘tryptophan’ na asidi amino zingine mhimu zinazohusika kutengenezwa kwa homoni nyingine ijulikanayo kama ‘ serotonin’.

Kama ulikuwa hujuwi ni kuwa serotonin ni homoni inayohusika na kazi mhimu sana ya kurekebisha matendo ya kitabia na kutoa matokeo chanya kwa mambo yanayohusu usingizi, hali ya mawazo kwa ujumla na mambo yanayohusu njaa.

Mbegu za maboga ni msaada mkubwa kwa kina mama waliofikia ukomo wa siku zao na huondoa matatizo ya kiafya yatokanayo na kukoma kwa hedhi.

Ni msaada kwa watu wenye saratani mbalimbali, huimarisha ukuaji na ustawi wa mifupa na meno, huondoa harufu mbaya ya kinywa na husaidia pia wenye tatizo la kufunga choo au kupata choo kigumu kila mara.

20. MPANGILIO WA CHAKULA

Chakula unachokula kila siku kinaweza kupelekea mfadhaiko zaidi kama hutakuwa makini.

Hivyo chakula bora kwa ajili ya kukulinda dhidi ya mfadhaiko lazima kijumuishe vitu vifuatavyo:

  • Kula zaidi vyakula vyenye omega 3.
  • Vyakula vyenye magnesium kwa wingi.
  • Vyakula vyenye vitamini C zaidi.
  • Vyakula vyenye vitamini kundi B
  • Unywe maji mengi kila siku lita 2 mpaka 3
  • Vyakula vyenye tryptophan kwa wingi kama nyama ya kuku, mbegu za maboga, maziwa nk
  • Punguza matumizi ya sukari na badala yake hamia kutumia asali
  • Acha vilevi vyote
  • Usikae mpweke hata mara moja
  • Shiriki tendo la ndoa mara kwa mara 
(Visited 27 times, 1 visits today)

0 Comments

Leave a Reply

Avatar placeholder

Your email address will not be published.

WhatsApp WhatsApp +255714800175