Katika makala hii nitakueleza kiundani juu ya dawa ya asili ya vidonda vya tumbo. Vidonda vya tumbo ni majeraha au vidonda ndani ya kuta za tumbo.

Seli ndani ya mwili lazima zibaki katika kiasi kidogo cha alkalini kutoka 7.2 mpaka 7.4, wakati 7.0 ni ya kati au husemwa sifuri katika kipimo cha PH yaani potential hydrogen. Chini ya 7.0 ni asidi na juu ya 7.0 ni alkalini.

Unaweza kukinunua kipimo cha PH na kupima Ph ya mate yako au ya mkojo wako kila mara ili kupata mwelekeo wa namna gani ufanye alkalini katika mwili wako ibaki kuwa ya 7.2 mpaka 7.4 kwenye seli ndani ya mwili wako.

Ikiwa mate yanasoma 6.0 au 6.5 ni kiashiria kuwa una asidi iliyozidi kwenye seli zako.

Kila mtu anapaswa kula zaidi vyakula vyenye alkalini yaani matunda na mboga za majani na kunywa vinywaji vyenye asidi chache na ikibidi basi atumie vinywaji vyenye alkalini nyingi kama juisi ya limau, juisi ya chungwa, ya zabibu na maji halisi.

Kwa maneno mengine, hali ya uasidi ndani ya mwili ndiyo hupelekea kusikia maumivu yatokanayo na vidonda vya tumbo.

Vidonda vya tumbo pia vinaweza kuletwa na bakteria ajulikanaye kama H.Pyrol.

Kutokana na tafiti za hivi karibuni, takribani mtu mmoja katika kila watu kumi anasumbuliwa na vidonda vya tumbo.

Jina langu naitwa Fadhili Paulo. Endelea kusoma ….

Dalili za vidonda vya tumbo

Dalili zitakazokufanya ujihisi una vidonda vya tumbo ni pamoja na

 1. Kuchoka choka sana bila sababu maalum
 2. Kuuma mgongo au kiuno
 3. Kupungukiwa au kupoteza kabisa nguvu za kijinsia
 4. Kizunguzungu
 5. Kukosa usingizi
 6. Usingizi wa mara kwa mara
 7. Maumivu makali sehemu ya mwili
 8. Kifua kwa ndani kana kwamba unachomwa na kitu cha moto au chenye ncha kali
 9. Kichefuchefu
 10. Kiungulia
 11. Tumbo kujaa gesi
 12. Tumbo kuwaka moto
 13. Maumivu makali sehemu kilipo kidonda
 14. Kukosa choo au kupata choo kwa shida tena kikiwa kigumu na chenye kukatika kama cha mbuzi
 15. Kukosa hamu ya kula
 16. Kula kupita kiasi
 17. Kusahahu sahau na hasira

Maumivu hayo wakati mwingine hutokeza mgongoni na huchoma kama sindano yenye sumu na kuacha maumivu makali.

Kwa kweli ni vigumu kueleza maumivu yote apatayo mgonjwa wa vidonda vya tumbo hasa kwa mwenye vidonda sugu kwani hakuna hata kiungo kimoja mwilini atakachokuambia ni kizima.

Vidonda vya tumbo husababishwa na nini?

Linapokuja suala la nini husababisha vidonda vya tumbo unaweza ukapata stori nyingi bila idadi, lakini kwa kifupi kabisa; vidonda vya tumbo ni ishara za mwili kupungukiwa maji na kama matokeo ya asidi kuzidi mwilini kuliko alkaline.

1. Asidi iliyozidi mwilini

Unapokaribia kutaka kula chakula chochote, au ukiwaza kutaka kula au ukiuona tu msosi kwa macho, TUMBONI MWAKO HUZARISHWA haidrokloriki asidi ili kuuandaa na kuusaidia mfumo wa mmeng’enyo wa chakula.

Kadri unavyoendelea kuishi haidrokloriki ASIDI HIYO HUENDA KUTOBOA KUTA ZA TUMBO na hatimaye taratibu baadaye hukusababishia VIDONDA VYA TUMBO.

Aina zote mbili za vidonda vya tumbo hutokea kutokana na kutolingana nguvu kati ya nguvu ya mnyunyizo wa asidi ya tumbo katika kushambulia na uwezo wa kuta za tumbo katika kuzuia mashambulizi.

Utokeaji wa vidonda vya tumbo hutegemea zaidi juu ya vipengele viwili.

Kwanza, vitu ambavyo huongeza mnyunyizo wa asidi katika tumbo, mfano vyakula vya kusisimua, vyakula vya mafuta, uvutaji wa sigara, utumiaji pombe, chai, kahawa, baadhi ya dawa tunazotumia kujitibu maradhi mbalimbali mwilini, n.k.

2. Mfadhaiko wa akili utokanao na shida za maisha

Mfadhaiko wa akili utokanao na shida za maisha ni moja ya vipengele vikuu vinavyosababisha vidonda vya tumbo.

Mfadhaiko huongeza utiririkaji wa asidi ndani ya tumbo. Hii asidi ya ziada ambayo hutiririka ndani ya tumbo kama matokeo ya mfadhaiko na hakuna chakula cha kufanyiwa kazi au kumeng’enywa humomonyoa kuta za tumbo na hivyo kusababisha vidonda.

Utafiti uliofanywa katika miaka ya hivi karibuni umeonyesha kuwa akili hutumia sehemu kubwa ya nguvu ya mwili.

Baadhi ya madaktari wamesema mfadhaiko huchangia sana katika kutokea kwa magonjwa mengi mwilini zaidi ya 50. !

Utafiti wa kisayansi unasema hisia zetu na hali zetu na jinsi tunavyomudu kudhibiti mifadhaiko inaweza kutusaidia kuelewa ni kwa kiwango gani afya zetu zilivyo madhubuti au zilivyo dhaifu.

Ingawa utafiti katika uwanja huu ni mpya, lakini utendaji kazi wa mfumo wa kinga ya maradhi ya mwili unaweza kukandamizwa na mfadhaiko wa akili au mawazo yatokanayo na shida za maisha.

Majaribio yaliyofanywa kwa watu wenye mifadhaiko sana kama wajane, watu waliopewa talaka na wale wenye kupambana na adui yalionesha kuwa watu hao huweza kupata maradhi mara kwa mara kutokana mfumo wao wa kinga ya maradhi kugandamizwa.

Mfano katika kukabiliana na adui, akili hutambua hofu na ubongo hupata taarifa; neva zenye kujiendesha zenyewe hupanda juu ili kukutana na adui.

Hapo moyo huenda mbio, msukumo wa damu nao hupanda na damu huvimba kwenye misuli kwa ajili ya maandalizi ya mapigano au makabiliano na adui.

Oksijeni na virutubishi vingine hukimbilia kwenye ubongo vikimfanya mtu awe tayari zaidi kwa mapigano, na hapo myunyizo wa adrenalini, homoni inayohusika na uzalishwaji wa nguvu mwilini huongezeka.

Kadiri mfadhaiko unavyokuwa ni wa muda mfupi, ndivyo pia athari zake zinavyokuwa ni fupi.

Lakini pindi mfadhaiko unapodumu kwa muda mrefu kama vile kipindi cha ndoa isiyo na amani au katika hali ya matatizo mengi kila mara, athari zake nazo hudumu kwa muda mrefu.

Dalili za mtu mwenye mfadhaiko

Ikiwa bila ya sababu yoyote, zaidi ya dalili sita katika hizi zifuatazo zitatokea, basi mtu amwone daktari kuhusiana na mfadhaiko. Dalili hizo ni:

 • Kujisikia huzuni sana kiwango cha kutokuwa na matumaini yoyote,
 • kupoteza kabisa uwezo wa akili kufurahi,
 • kupoteza kabisa hamu ya tendo la ndoa
 • Kupoteza hamu ya chakula
 • Kukosa usingizi
 • Wasiwasi unaosababisha hali ya kutotulia kwa ujumla
 • Kupoteza kumbukumbu au hali ya kusahausahau na kushindwa kuamua
 • Kughadhibishwa na vitu vidogo, yaani mtu kitu kidogo tu ameshachukia
 • Kujiona huna thamani na kujitenga na marafiki na ndugu.

3. Sababu ya tatu inayosababisha vidonda vya tumbo ni Haraka haraka

Maisha ya kisasa yanataka haraka katika kazi nyingi tuzifanyazo kila siku, ni lazima tufike mahala haraka na turudi haraka! Haraka hizi husababisha vidonda vya tumbo. Mbanano wa ratiba katika shughuli zako za kila siku pia husababisha matumbo nayo kubanana.

Malalamishi makubwa leo ya wagonjwa kwa madaktari wao ni: “Tumbo langu linanisokota na kuniletea matatizo, au nasikia kiungulia baada ya kula”. Haraka haraka na wasiwasi ni baadhi ya sababu ya matatizo haya.

Tumbo ni kama kioo cha akili. Akili ikihangaishwa, basi wasiwasi na msukosuko wa hisia hufungia breki kwenye viungo vya ndani.

Akili iliyohangaishwa na kukimbizwa mbio mbio hupeleka hisia kwenye tumbo na kusababisha mkazo wa ghafla wa misuli na hapo husababisha kiungulia na maumivu.

Ili kuepuka kufanya kazi zako kwa hali ya uharakaharaka unashauriwa kupanga kabla ni kazi gani na gani utaenda kuzifanya siku inayofuatia kwa kuziandika kabisa katika karatasi au kitabu maalumu kiitwacho kiingereza diary au kumbukumbu za kila siku kwa Kiswahili na mhimu ni uwe na kiasi kwa kila jambo kwani si lazima umalize kazi zote leo.

4. Sababu ya nne ya kutokea vidonda vya tumbo ni ulaji wa Vyakula vya kusisimua

Vyakula vya kusisimua ni hatari kwa neva za tumbo. Uchunguzi wa kitabibu unabainisha kuwa vyakula vya kusisimua kama vile ketchup, chill sauce, achali, pilipili na vingine vingi vya jamii hii huchangia kwa kiwango fulani kudhuru neva za tumbo na havitakiwi kuliwa hasa kwa mtu mwenye vidonda vya tumbo na mwenye tatizo la kutosagika chakula tumboni.

Sababu ni kuwa, visisimuaji hivi huzichoma pia kuta za tumbo.

5. Vinywaji na vyakula vyenye kaffeina na asidi nyingi

Vinywaji vyenye kaffeina na asidi nyingi kama vile chai ya rangi, kahawa, soya sauce, mayonnaise, jibini, Vyakula jamii ya Mkate, samaki wa kwenye makopo, pombe, soda na juisi za viwandani pia huchangia kwa kiasi kikubwa katika kutokea kwa vidonda vya tumbo.

Utambuzi wa vidonda vya tumbo

Utambuzi wa kubainisha vidonda vya tumbo hufanyika hospitalini kwa kutumia mionzi au X-Ray kwa lugha ya kikoloni.

Upimaji wa tumbo na vilivyomo ndani yake unaweza pia kufanywa na njia inayojulikana kama ‘endoskopi’ au ‘biopsi’, ambayo huyakinisha hali halisi.

Matibabu ya vidonda vya tumbo

Katika kutibu vidonda vya tumbo, mara nyingi ni lazima kupunguza uzalishaji wa asidi tumboni au mwilini kwa ujumla.

Matibabu ya vidonda vya tumbo hujumuisha lishe na kubadilisha mitindo ya maisha na kutumia dawa maalumu.

Ikiwa matatizo kama kuvuja damu au vitobo sehemu ya kidonda yatatokea, basi hapo upasuaji huwa ni muhimu.

Vidonda vya tumbo kwa ujumla hupona ndani ya wiki 4 mpaka 6 za matibabu.

Dawa mbadala ya vidonda vya tumbo > Mafuta ya mbegu za mlonge

Dawa ya asil ya vidonda vya tumbo
Mafuta ya Mbegu za Mlonge

Unapotaka kutibu vidonda vya tumbo ni mhimu kutambua kwanza nini kinaweza kuwa ndiyo chanzo hasa cha tatizo kwa upande wako.

Watu wengi wanaugua vidonda vya tumbo kama matokeo ya kushuka kwa kinga zao za mwili jambo linalosababisha bakteria mbalimbali kushambulia na kutoboa tumbo.

Kadri hawa bakteria mbalimbali wanavyozidi kuongezeka tumboni wanaharibu mfumo wa kawaida wa uundwaji wa asidi mwilini na kupelekea asidi nyingi zaidi kuzalishwa zaidi ya inavyohitajika na mwili.

Asilimia 98 ya watu wengi wanaougua vidonda vya tumbo ni matokeo ya asidi nyingi kuzidi mwilini.

Mafuta ya mbegu za mlonge ni dawa nzuri ya asili inayoweza;

 • Kuongeza mara dufu kinga yako ya mwili
 • Kuua bakteria mbalimbali tumboni akiwemo bakteria wa vidonda vya tumbo H.Pyrol
 • Kuweka sawa usawa wa asidi na alkalini mwilini
 • Kurahisisha kutibu vidonda sehemu mbalimbali mwilini (yana vitamini C ya kutosha)
 • Kuondoa gesi tumboni
 • Kusafisha na kuondoa sumu mbalimbali mwilini
 • Kuondoa msongo wa mawazo (stress)
 • Kudhibiti virusi (anti-virus)
 • Kuuongezea nguvu na ufanisi mmeng’enyo wa chakula
 • Kuondoa uchomvu sugu na kuongeza nguvu za mwili kwa ujumla
 • Kutibu maumivu na matatizo karibu yote ya tumbo

Kama umeumwa vidonda vya tumbo kwa kipindi kirefu na umejaribu kila dawa bila mafanikio basi mafuta ya mbegu za mlonge ni suluhisho pekee la uhakika kwa tatizo lako.

Ni dawa ya uhakika kwa kutibu vidonda vya tumbo isiyo na madhara yoyote mabaya hapo baadaye.

Siyo vidonda vya tumbo tu utapona ukitumia dawa hii bali pia utaona afya yako ya mwili kwa ujumla imeimarika, utaona tu afya yako ni tofauti kabisa na ilivyokuwa hapo kabla hujaanza kutumia dawa hii.

Matumizi: Kunywa kijiko kidogo kimoja cha chai kutwa mara 2 asubuhi na usiku baada ya chakula. Unaweza kunywa dawa yenyewe moja kwa moja kama ilivyo au unaweza pia kuchanganya kwenye kikombe kimoja cha juisi ya matunda uliyotengeneza mwenyewe nyumbani hasa juisi ya parachichi na uongeze asali vijiko vikubwa viwili ili kupata radha.

Dawa hii isitumike na mama mjamzito na mtu yeyote mwenye shinikizo la chini la damu.

Wakati umeanza kutumia dawa siku 3 au 4 za mwanzo unaweza kupatwa na tatizo la kuharisha lakini baadaye hali hutulia kadri unavyoendelea kutumia dawa hivyo usishtuke. Kama tatizo linaendelea hata zaidi ya siku 7 punguza kiasi cha dozi au sitisha kwanza dawa kwa siku mbili tatu.

Unaweza kuhitaji kutumia dawa hii kwa siku 30 mpaka 60 ili kupona kabisa vidonda vya tumbo. Unaweza pia kuitumia muda wowote hata kama huumwi ili kujiongezea kinga dhidi ya vidonda vya tumbo.

Usitumie dawa yoyote bila uangalizi wa karibu wa Tabibu.

Ikiwa utahitaji dozi ya dawa kwa ajili ya vidonda vya tumbo niachie ujumbe WhatsApp+255714800175

Nitakuwa bega kwa bega na wewe mpaka unapona, nipo online WhatsApp nyakati zote za mchana kila siku.

Naweza pia kukuletea ulipo kama utataka BURE ndani ya Dar, Natuma pia popote ulipo nje ya Dar kwa nauli yangu.

Naitwa Fadhili Paulo, ni Tabibu wa Tiba Asili na ni mTanzania.

Ofisi yangu inaitwa Victoria Home Remedy ipo Sigara Yombo Vituka Temeke Dar Es Salaam.

Jiunge na mimi na watu wengine zaidi ya 94000 kwenye ukurasa wangu wa facebook kwa kubonyeza hapa

Imesomwa mara 1,387

Imehaririwa


Niulize swali hapo kwenye comment nikujibu
WhatsApp Chat na mimi kwenye WhatsApp