Dawa ya asili inayoongeza kinga ya mwili

Published by Fadhili Paulo on

Dawa ya asili inayoongeza kinga ya mwili

Dawa ya asili inayoongeza kinga ya mwili

Kumbuka, ile hali ya kuonekana umezeeka au mwili wako kuonekana umechoka mara zote huwa kuna uhusiano wa moja kwa moja na kushuka kwa kinga yako ya mwili hali ambayo inauacha mwili wako kushambuliwa kirahisi na vijidudu nyemelezi na magonjwa mbalimbali.

Kama unataka kuishi vizuri kila siku basi jifunze namna kinga yako ya mwili inavyoweza kuongezwa kila siku kadri unavyoendelea kuishi.

Kinga ya mwili ni kile unachokula kila siku kimwili na kiroho.

Kile unachokula kila siku ndicho kitakachoamua aina ya kinga ya mwili utakayokuwa nayo.

Na ndiyo maana mara zote unatakiwa ule chakula kinachokufanya uishi na siyo kinachokufanya ushibe!

Dalili za kupungua kinga ya mwili

JE, NITAJUAJE KAMA KINGA YA MWILI WANGU IMESHUKA?

Watu wengi huwa wamekariri kuwa mtu ambaye kinga ya mwili wake imeshuka ni muathirika wa UKIMWI, Hii dhana siyo ya kweli kabisa, sasa leo kupitia makala hii utajua mtu ambaye kinga yake ya mwili imeshuka anakuwaje.

Kwa kifupi ni watu wengi sana ambao kinga yao ya mwili imeshuka ila hawajitambui lakini wanaishia kulalamika kuwa wanaumwa matatizo mbalimbali.

Sasa ukiwa na matatizo au dalili zifuatazo basi tambua kabisa kuwa kinga yako ya mwili imeshuka na unaweza kuchukua tahadhari mapema.

1. Ukiwa unaugua mara kwa mara hata kama ni mafua au homa yoyote basi jua kuwa kinga yako ya mwili ipo chini.

2. Mwili kuwa na uchovu au kujisikia kuchoka mara kwa mara

3. Maumivu ya kiuno na mgongo mara kwa mara.

4. Kukosa usingizi hadi kufikia hatua ya kumeza vidonge vya usingizi ndipo unalala.

5. Kuwa na Ugonjwa wa Kisukari. Mgonjwa yeyote wa Kisukari kinga yake ya mwili huwa ipo chini na ndiyo maana mtu yeyote mwenye tatizo hili huweza kuandamwa na magonjwa mengi sana.

6. Kwenda Hospitali ukiwa unaumwa lakini ukifanyiwa vipimo unaambiwa huna ugonjwa wowote japo wewe unajisikia kuumwa.

Dawa ya asili inayoongeza kinga ya mwili

Dawa ya asili inayoongeza kinga ya mwili > Unga wa Majani ya Mlonge

Mlonge au Moringa oleifera kwa kiingereza umekuwa ukijulikana kama mti wa miujiza kwa karne nyingi katika baadhi ya nchi za Afrika, Asia na katika nchi za Caribbean.

Mti huu umeripotiwa kuwa dawa nzuri kwa ajili ya kuongeza kinga ya mwili.

Karibu kila sehemu ya mti huu hutumika kama dawa bali kwenye majani yake ndiko kuna viinilishe vingi mara dufu zaidi hasa yanapoandaliwa na kuwa katika mfumo wa unga.

Sasa unaweza kuwa unajiuliza ni nini kinachoufanya mti wa mlonge mti huu wa ajabu kuwa kitu cha thamani SANA katika kuimarisha kinga yako ya mwili na hivyo kujikinga na vijidudu nyemelezi, homa na magonjwa mbalimbali?

Kwanza kabisa mlonge umebarikiwa kuwa na viinilishe vingi zaidi kuliko mti mwingine wowote chini ya jua ukiwa na viinilishe 92 ndani yake, una vitamini nyingi, madini na viondoa sumu mwilini tofauti tofauti 46! Huu ndiyo ukweli wa kustaajabisha wa mti huu unaoleta afya na maisha.

Kwahiyo nipe nafasi nikueleze kiundani kidogo kuhusu hivi viinilishe katika mti wa mlonge vinavyoufanya kuwa silaha kubwa katika vita yako ya kulinda kinga ya mwili wako na utaona ni kwanini habari hii uisomayo ni dhahabu katika maisha yako.

Sehemu ya mti wa mlonge yenye viinilishe vingi sana kuliko sehemu zote za mti huu ni sehemu ya majani ya mlonge

Hata hivyo majani haya yakikaushwa na kutengenezwa unga ndivyo viinilishe vyake vinavyoongezeka zaidi kuliko yakiwa freshi

Tofauti ni kwenye vitamini C.

Majani mabichi (fresh) yana vitamini C nyingi kuliko katika unga wake lakini bado hata kwenye unga kuna vitamini C nusu ya ile ya kwenye chungwa.

Majani mabichi (fresh) ya mlonge yanaweza kutafunwa mabichi yenyewe kama yalivyo au unaweza kuyachanganya kwenye kachumbari, unaweza kuchanganya na matunda na kuyasaga pamoja kama juisi.

Unaweza kuchanganya majani mabichi (fresh) ya mlonge na kuyapika sambamba na mboga zingine za majani na kuliwa kama mboga nyingine yoyote ya majani ingawa yakipikwa hivi kwenye moto vitamini C yake hupungua kwa kiasi kikubwa sana.

Majani freshi ya mlonge yana:

1. Vitamini A mara 4 zaidi ya ile ya kwenye karoti
2. Vitamini C mara 7 zaidi ya ile ya kwenye chungwa
3. Madini ya kalsiamu mara 4 zaidi ya yale ya kwenye maziwa
4. Madini ya Potasiamu mara 3 zaidi ya yale ya kwenye ndizi
5. Protini mara 2 zaidi ya ile ya kwenye mtindi
6. Madini ya chuma mara robo tatu zaidi ya ile ya kwenye spinachi

Kwahiyo kama unao mti wa mlonge nyumbani au karibu na unapoishi hakikisha unapata kutumia pia majani mabichi ya mlonge ili kupata vitamini C kwa wingi na si unga peke yake.

Na kama mahali ulipo huwezi kupata mti wa mlonge karibu basi hakikisha unapata unga wa majani ya mlonge.

Unga wa majani ya mlonge una:

1. Vitamini A mara 10 zaidi ya ile ya kwenye karoti
2. Vitamini C nusu ya ile ya kwenye chungwa
3. Madini ya kalsiamu mara 17 zaidi ya yale ya kwenye maziwa
4. Madini ya Potasiamu mara 15 zaidi ya yale ya kwenye ndizi
5. Protini mara 9 zaidi ya ile ya kwenye mtindi
6. Madini ya chuma mara 25 zaidi ya ile ya kwenye spinachi

Watu wengi ukiwaambia kinga yangu inashuka lazima hawaataacha kukushauri upendelee kula machungwa,

si ndiyo?

Hili siyo jipya kwako.

Habari mpya kwako ni kuwa unga wa majani ya mlonge una vitamini C nusu ya YA ILE INAYOPATIKANA KATIKA MACHUNGWA!

Na hivyo mlonge unabaki kuwa ndicho kitu pekee chenye nguvu ya kuondoa sumu mwilini kuwahi kutokea katika historia.

Vitamini C kama wote tujuavyo ni kitu mhimu katika kurejesha kinga ya mwili kwa sababu ni vitamini inayofanya kazi ya kuripea seli za mwili na kinga ya mwili. Zaidi sana vitamini C huimarisha ngozi ya mwili, nywele, fizi, macho na kuongeza nguvu ya jumla ya mwili kwa kuyataja machache mazuri ya vitamini C

Changanya matunda yote na mboga za majani zote bado viinilishe vyake kwa pamoja haviwezi kuvifikia vile vilivyomo kwenye unga wa mlonge!

Ni kusema mtu aliyekula matunda na mboga za majani zote bado hatakuwa na afya bora kama yule atakayetumia mlonge tu.

Maajabu yanaendelea …

Vitamini A ni moja ya vitamini zinazotajwa kuwa mhimu sana katika kuimarisha kinga ya mwili. Vitamini A ni mhimu kwa watu wanaosumbuliwa na matatizo kama ya kuharisha, upungufu wa kinga mwilini, surua na malaria.

Ukiwaambia watu una upungufu wa vitamini A au macho yako hayaoni vizuri mara zote watakuambia pendelea kula karoti, si ndiyo? Kile ulikuwa hufahamu ni kuwa unga wa MLONGE UNA VITAMINI A MARA 4 ZAIDI YA ILE ILIYOMO KWENYE KAROTI!

Vileviele madini ya chuma (Iron) ni kitu mhimu katika mfumo wa kinga ya mwili ambayo hukuwezesha usipatwe na magonjwa na homa mara kwa mara.

Ukiishiwa madini ya chuma mara nyingi utashauriwa ule sana spinachi. Habari njema kwako ni kuwa unga wa majani ya mlonge UNA MADINI YA CHUMA MARA 25 ZAIDI YA ILE ILIYOMO KWENYE SPINACHI.

Unasemaje ndugu msomaji mpaka hapo! Una swali?

Pia mlonge una beta-carotene.

Unga wa majani ya mlonge ni dawa ya asili inayoongeza kinga ya mwili ambayo hakuna dawa nyingie yoyote ya kuifananisha nayo chini ya jua.

Unga wa majani ya Mlonge unaimarisha usawa wa himoglobini katika damu jambo ambalo matokeo yake ni kuimarika kwa kinga yako ya mwili.

Kwa kuongezea unga wa majani ya mlonge una lundo la vitamini kundi B kuliko mti au mmea mwingine wowote unaoufahamu. Mlonge una vitamini B, B1, B2, B3, B5, B6, B12, D, E, K, folic acid, Kalsiamu (mlonge una Kalsiamu mara 17 zaidi ya ile ya maziwa ya ng’ombe), madini ya shaba, potasiamu, magnesia, kromiamu na vitamini, na madini madogo madogo mengine mengi mhimu kwa ajili ya kuimarisha kinga ya mwili.

Elewa tu kwamba mti huu wa maajabu mti wa mlonge na majani yake mti ambao hujulikana pia kama mti wa uzima una viinilishe bora na mhimu zaidi kwa ajili ya kuongeza kinga ya mwili ambavyo siyo rahisi kuvielezea vyote kimoja baada ya kingine

Kwahiyo, kama unasumbuliwa na homa za mara kwa mara au unataka tu kuiweka kinga yako katika ubora wake wa juu kabisa, katika kipindi chochote cha mwaka, basi hakikisha nyumbani kwako hakukosekani unga wa majani ya mlonge kwa ajili yako, watoto wako na wale uwapendao

Mlonge unasafisha mwili wako wote, unasafisha ini, figo, moyo, macho, unaimarisha meno, ngozi na nywele.

Wakati unatumia mlonge unakufanya ujisikie vizuri, ujisikie mpya (fresh) na mwenye nguvu. Watu wengi wanaotumia mlonge huwa ni wenye afya nzuri hata kwa muonekano tu hata wanapokuwa na umri mkubwa zaidi ya miaka 90.

Matatizo mengi ya kiafya ni matokeo ya lishe yenye viinilishe duni au hafifu jambo linalopelekea kuwa na kinga ya mwili isiyo na nguvu kupigana na magonjwa mbalimbali.

Unaporekebisha usawa huo usio sawa wa kinga yako ya mwili kwa kutumia mimea mhimu ya asili hutakawia kuona matokeo mazuri kwenye afya yako.

Uwezo wa mti wa mlonge kuyaweza yote hayo ni kutokana na kuwa na vitamini, madini mbalimbali na viondowaji sumu vingi kuliko mmea mwingine wowote.

Wagonjwa wengi wenye UKIMWI katika sehemu nyingi za afrika magharibi wameripoti kuongezeka kiasi kikubwa cha kinga zao za mwili kiasi cha kutokuhitaji dawa nyingine yoyote ya hospitali baada ya kutumia mlonge.

Hakika kuna siku utakuja kunishukuru kwa maelezo haya ya bure!

Unga wa mlonge unaweza kuhifadhiwa kwa miezi kadhaa bila kupoteza ubora na faida zake za kiafya.

Faida za mlonge zimeandikwa na majarida ya afya na lishe kadhaa duniani.

Kile ulikuwa hujuwi ni kuwa viwanda na makampuni mengi ya dawa za hospitalini yamekuwa yakitumia virutubishi vilivyomo kwenye mti huu kutengenezea madawa kwa ajili ya binadamu na wanyama.

Dawa ya asili inayoongeza kinga ya mwili

Unga wa majani ya Mlonge

Unga wa majani ya Mlonge pia una zile amino asidi mhimu 9 za kwenye protini. Nitazitaja hizo amino asidi zote hapa chini na kazi zake:

 • Threonine – Hii ni Amino asidi inayoimarisha mfumo wa mmeng’enyo wa chakula na kuzuia mafuta yasijiunde katika ini. Husaidia pia umeng’enyaji wa chakula.
 • Isoleucine – Ni Amino asidi mhimu kwa ajili ya afya ya ubongo na husaidia kuupa mwili nguvu ya asili.
 • Leucine – Hufanya kazi pamoja na isoleucine ili kuongeza nguvu mwilini.
 • Phenylalanine – Husaidia mawasiliano baina ya seli za ubongo, pia husaidia kupunguza hisia za njaa, huongeza uwezo wa utambuzi na ndiyo amino asidi inayosaidia kuongeza uwezo wa ubongo kutunza kumbukumbu.
 • Tryptophan – Huusaidia mfumo wako wa kinga ya mwili, huondoa msongo wa mawazo (stress/depression) na kuondoa tatizo la kukosa usingizi. Amino asidi hii hupunguza uwezekano wa mtu kupatwa na shambulio la moyo na kupunguza kolesto mbaya mwilini.
 • Lysine – Husaidia umeng’enywaji wa kalsiamu katika mifupa, husaidia antibodies na kuzuia kukua kwa seli za virusi.
 • Methionine – Huupa mwili sulphur, husaidia kupunguza kolesto mbaya. Huimarisha afya ya ini, figo na kusaidia pia kutunza afya ya ngozi, nywele na kucha.
 • Valine – Husaidia akili kuwa ya utulivu.

Kuna amino asidi nyingine kadhaa katika unga wa majani ya mlonge ambazo siyo za mhimu sana lakini bado zinahitajika ili kuwa na afya bora.

Nazo ni pamoja na histidine, alanine, glutamic acid, arginine, cysteine, proline, aspartic acid, glycine, serine na tyrosine.

Hii ni orodha ya viinilishe 126 vinavyopatikana kwenye unga wa majani ya mlonge na ukumbuke ni mimi tu ndiyo nimeweza kuvitaja viinilishe hivi vyote kwa majina:

1.iron 64.Pentena
2.copper 65.2-Hexenal
3.sodium 66.Heptenal
4.calcium 67.2,4-Heptadienal
5.magnesium Alcohols
6.phosphorus 68.2-Pentenol
7.potassium 69.3,3-Dimethyl-Cyclohexanol
8.sulfur 70.Benzyl alcohol
9.manganese Ketones
10.zinc 71.Methyl heptenone
11.selenium 72. 2-Hexen-4-olide
Vitamins 2-Acetyl pyrrole
12.vitamin B1 (thiamin) 74.Dihydroactinidolide
13.vitamin E Terpenoids
14.Vitamin B1 75.alpha-Himachalene
15.Vitamin B6 76.(E)-Geranyl acetone
16.Vitamin B7 >77.Ti(E)-beta-Ionone
17.Vitamin D Acids
18.Vitamin K 78.Acetic acid
19.vitamin B2 (riboflavin) 79.Pentanoic acid
20.vitamin B3 (niacin) 80.Hexanoic acid
21.Vitamin C 81.Octadecanoic acid
Amino acids 82.Hexadecanoic acid
22.aspartic acid 83. erythrobic acid
23.glutamic acid 84.citric acid
24.serine Others
25.glycine 85.meChlorophyll
26.threonine 86.meDihydrozeatin
27.alanine 87.Zeatin
28.valine 88.Carbohydrates
29.leucine 89.fibers
30.isoleucine Alkaloids
31.histidine 90.Moringine
32.lysine 91.Strophantidin
33.arginine 92.4-(α-l-rhamnosyloxy)
34.phenylalanine 93.benzyl isothiocyanate
35.tryptophan 94.4-(4’-O-acetyl-α-l-rhamnosyloxy)
36.cystine 95.benzyl isothioyanate
37.proline Flavonoids
38.tyrosine 96.Catechin
39.methionine 97 (β-d-glucopyranosyl-1)
40.cysteine 98.benzyl thiocarboxamide
41.phenylalanine 99.Epicatechin
42.choline 100.4-O-(α-l-rhamnosyloxy)
Fats 101.benzyl glucosinolate
43.Myristic 102.Quercetin
44.Palmitic 103.4-benzylglucosinolate
45.Palmitoleic 104.Kaempferol
46.Stearic 105.Niazimicin
47.Oleic 106.4-(α-l-rhamnosyloxy)
48.Linoleic 107.benzyl acetonitrile (niazirin)
49.Linolenic 108.O-ethyl-4-(α-l-rhamnosyloxy)
50.Arachidic 109.benzyl carmate
51.Eicosenoic Phenolic
52.Behenic 110.Gallic acid
53.Lignoceric 111.Glycerol-1-1-(9-octadecanoate)
Sterols 112.p-Coumaric acid
54.Cholesterol 113.3-O-(6’-O-oleoyl-β-d-glucopyranosyl)-β-sitosterol
55.Brassicasterol 114.Ferulic acid
56.24-methylenecholesterol 115.β-sitosterol-3-O-β-d-glucopyranoside
57.Campesterol 116.Caffeic acid
58.Stigmasterol 117.3-Hydroxy-4-(α-l-rhamnopyranosyloxy)
59.Ergostadienol 118.benzyl glucosinolate
60.Clerosterol 119.Protocatechuic acid
61.Stigmastanol 120.4-(2/3/4′-O-acetyl-α-l-rhamnopyranosyloxy)
62.β-sitosterol 121.benzyl glucosinolate
63.venasterol 122.Cinnamic acid
123.Glucosinalbin
124.Ellagic acid
125.Glucoraphanin
126.Glucoiberin

Hii ni orodha ya viondoa sumu (antioxidants) 46 na zaidi vipatikanavyo katika unga wa majani ya mlonge:

Antioxidants (9, 11, 12, 13, 14, 15)

 1. β-carotene
 2. calcium
 3. potassium
 4. quercetin
 5. chlorogenic acid
 6. hydroxyanisole (BHA)
 7. butylated hydroxytoluene (BHT)
 8. tertiary-butylhydroquinones
 9. propyl gallate
 10. vitamin E (tocopherols)
 11. ascorbic acid (vitamin C)
 12. glucose oxidase
 13. reduced glutathione
 14. citric acid
 15. polyphospages
 16. aminopolycarboxylic acids
 17. vanillin
 18. moringine
 19. strophantidin
 20. 4-(α-l-rhamnosyloxy)
 21. benzyl isothiocyanate
 22. 4-(4’-O-acetyl-α-l-rhamnosyloxy)
 23. benzyl isothioyanate
 24. catechin
 25. 4-(β-d-glucopyranosyl-1→4-α-l-rhamnopyranosyloxy)
 26. benzyl thiocarboxamide
 27. epicatechin
 28. 4-O-(α-l-rhamnosyloxy)
 29. benzyl glucosinolate
 30. 4-(α-l-rhamnopyranosyloxy)-benzylglucosinolate
 31. Kaempferol
 32. Niazimicin
 33. 4-(α-l-rhamnosyloxy)
 34. benzyl acetonitrile (niazirin)
 35. O-ethyl-4-(α-l-rhamnosyloxy)
 36. benzyl carmate
 37. Gallic acid
 38. Glycerol-1-1-(9-octadecanoate)
 39. p-Coumaric acid
 40. 3-O-(6’-O-oleoyl-β-d-glucopyranosyl)-β-sitosterol
 41. Ferulic acid
 42. β-sitosterol-3-O-β-d-glucopyranoside
 43. Caffeic acid
 44. 3-Hydroxy-4-(α-l-rhamnopyranosyloxy)
 45. benzyl glucosinolate
 46. Protocatechuic acid
 47. 4-(2/3/4′-O-acetyl-α-l-rhamnopyranosyloxy)
 48. benzyl glucosinolate
 49. cinnamic acid
 50. glucosinalbin
 51. ellagic acid
 52. glucoraphanin
 53. glucoiber

Hii ndiyo sababu waNigeria waliuita mlonge kwa jina la utani kama “Nebedaya”, ambalo maana yake ni mti USIOKUFA!

Usisahau pia kunywa maji ya kutosha kila siku, kufanya mazoezi ya viungo na kuwa na afya njema kiroho ili kuwa na kinga imara ya mwili wako.

*Usitumie dawa hii bila uangallizi wa karibu wa Tabibu.

Kama unahitaji unga wa majani ya mlonge kwa ajili ya kuimarisha kinga ya mwili niachie ujumbe WhatsApp +255714800175

Kama upo Dar Es Salaam mimi naweza pia kukueletea popote ulipo bila gharama ya nauli.

Kama upo mkoani, tafuta ndugu au rafiki yako aliyoko Dar halafu mtumie yeye hela nitampa mlonge na atakutumia yeye mwenyewe huyo ndugu yako au rafiki yako.

Unga wangu wa majani ya mlonge ni mzuri na naweza kusema pasipo na hofu kuwa huwezi kupata sehemu nyingine wenye ubora unaokaribia na wangu. Ninauandaa kwa umakini mkubwa ili ubaki na viinilishe vyake na ni wa kijani kweli kweli.

Uwe makini na yafuatayo kuhusu mlonge;

 1. Siyo kila mlonge ni dawa. Kuna aina 13 tofauti za mlonge na ni mlonge mmoja tu ndiyo hutumika kama dawa nao hujulikana kwa kiingereza kama ‘Moringa oleifera’. Aina nyingine 12 zote zilizobaki za milonge haitumiki kama dawa.
 2. Ili mlonge ufae kama dawa lazima uvunwe asubuhi tu mapema na uanikwe ndani ya nyumba au sehemu yoyote yenye kivuli kwa siku 4 mpaka 5. Mlonge hauanikwi juani.
 3. Ni lazima uwe una rangi ya kijani kweli kweli ndipo unakuwa na viinilishe vyake vyote vya kutosha. Tofauti na hapo kuna uwezekano mlonge huo ulianikwa juani na haufai tena kutumika kama dawa.

Hivyo nunua mlonge toka kwa mtu unayemfahamu ambaye una uhakika naye na anajishughulisha hasa na mambo ya tiba asili. Usinunuwe tu popote, jali afya yako.

Wakati unaendelea kutumia mlonge hakikisha unabaki kwenye chombo na umefungwa vizuri bila kupitisha hewa wakati wote wa matumizi. Usiuache kwenye chombo cha wazi.

Kama una ushuhuda wowote kuhusiana na unga wa majani ya mlonge kuongeza KINGA YA MWILI ningefurahi kama utaniandikia hapo chini kwenye comment

Vitu vinavyoharibu na kushusha kinga ya mwili

1. Msongo wa mawazo (stress)
2. Vilevi vyote
3. Lishe duni (chakula kichache)
4. Kutokufanya mazoezi ya viungo
5. Kutumia dawa za kupunguza maumivu kila mara bila ushauri wa kitaalamu

Na ukinunua dawa hii kutoka kwangu na siyo sehemu nyingine utapata faida hizi nne zifuatazo:

 1. Utakuwa rafiki yangu
 2. Nitahakikisha tatizo lako linaisha na halijirudii tena
 3. Nitakupa maelezo zaidi kuhusu matumizi kulingana na umri na uzito wako
 4. Nitawajibika kwa lolote linaloweza kukutokea wakati unaendelea kutumia dawa
 5. Napatikana WhatsApp nyakati zote za mchana na unaweza kuchat na mimi mwenyewe mubashara (live) toka popote ulipo.

Kama una swali zaidi niulize hapo chini kwenye comment

Mjulishe rafiki yako kwenye twitter naye asome post hii kwa kubonyeza ujumbe ufuatao:

(Visited 167 times, 1 visits today)

0 Comments

Leave a Reply

Avatar placeholder

Your email address will not be published.

WhatsApp WhatsApp +255714800175