Dawa ya asili inayotibu tatizo la kukojoa kitandani

DAWA YA ASILI INAYOTIBU TATIZO LA KUKOJOA KITANDANI

Kukojoa kitandani ni tatizo la kawaida miongoni mwa watoto wadogo wakati mwingine wapo hata watu wazima wanaokabiliwa na tatizo hili.

Ni kitendo cha kutokujitakia cha kutoa mkojo ukiwa usingizini kitandani.

Ni jambo linalohuzunisha sana hasa linapomtokea mtu mzima, hata hivyo ni jambo la kawaida kwa watoto wadogo mpaka miaka 6.

Watu wazima au watoto huwa hawafanyi kitendo hiki kwa kujipendea au sababu ni wavivu, hapana, hili ni tatizo linaloweza kusababishwa na matatizo yafuatayo:

  1. Kuwa na kibofu kidogo cha mkojo
  2. Kuchelewa kukua au kukomaa kwa kibofu cha mkojo
  3. Uzalishwaji uliozidi wa mkojo
  4. U.T.I ( yutiai)
  5. Mfadhaiko (stress)
  6. Kufunga choo kwa muda mrefu au kupata choo kigumu kwa kipindi kirefu
  7. Usawa usiosawa wa homoni
  8. Ammonia kuzidi kwenye kibofu cha mkojo

Unapokuwa ni mtu wa shughuli nyingi sana kila siku au mtoto anapokuwa bize sana na michezo kila siku unapata usingizi mzito sana hivyo ubongo wako unakuwa haupati ishara za kutosha za kibofu cha mkojo kujaa.

Pia katika baadhi ya watu wazima au watoto tatizo la kukojoa kitandani huweza kuwa ni jambo la kurithi toka kwa wazazi wao.

Kadri mtoto anavyokuwa mkubwa ndivyo na tatizo la kukojoa kitandani linavyopungua.

Wakati mwingine hili linaweza kuendelea hata ukubwani na hivyo kuwa shida kwa mtoto mwenyewe, wazazi wake na jamii inayomzunguka kwa ujumla.

Unaweza kumsaidia mwanao au mtu mzima mwingine yoyote aache kukojoa kitandani kwa kutumia dawa hii ya asili ya kuacha kukojoa kitandani.

Dawa ya asili inayotibu tatizo la kukojoa kitandani – Mwilumbala

Dawa ya asili inayotibu tatizo la kukojoa kitandani 1
Dawa ya Asili ya kuacha kukojoa kitandani

Kukojoa kitandani hutokea wakati kibofu cha mkojo kinazalisha ‘hydrogen’ na ‘nitrogen‘ kwa pamoja na kuunda ammonia.

Ammonia ni sumu katika mwili wa binadamu.

Wakati ubongo unapopata ujumbe kutoka kwenye kibofu cha mkojo, ubongo hukufanya uote kwamba upo chooni na hatimaye unakojoa ukiwa usingizini.

Huku upo usingizi bado utaona wazi upo chooni sababu ya hiyo ammonia ambayo ni kama sumu au taka mwili.

Kwahiyo sababu ya mtu kukojoa kitandani ni matokeo ya kuundwa kwa ammonia kwenye kibofu cha mkojo na ammonia hii inaondolewa kirahisi mwilini kwa kunywa dawa hii ndani ya siku 30.

Ni dawa rahisi zaidi kwa mtu mzima au mtoto anayekojoa kitandani.

Dawa hii huufanya mwili kuwa wa moto moto.

Husaidia kuweka sawa usawa wa asidi na alkaline mwilini (body’s Ph) na hivyo kupunguza asidi iliyozidi katika mwili kitu ambacho kinaweza kuwa ni moja ya sababu za tatizo la kukojoa kitandani.

Mwilumbala husaidia kuondoa sumu mbalimbali mwilini pia hutibu tatizo la kufunga choo vitu vingine ambavyo husababisha tatizo la kukojoa kitandani.

Dawa hii pia ni nzuri kwa wale wenye tatizo la kukojoa kitandani kama matokeo ya  U.T.I (yutiai).

U.T.I ni tatizo ambalo kwa namna moja au nyingine linapokuwa sugu linaweza kupelekea tatizo la kukojoa kitandani.

Mambo ya mhimu kuzingatia ili ufanikiwe na dawa hii:

• Wasiwasi na mfadhaiko (stress) huweza kuongeza ukubwa wa tatizo. Hivyo badala ya kumkalipia au kumdhalilisha kila siku mwathirika wa tatizo hili, muonyeshe upendo na uwe tayari kumsaidia polepole mpaka anapona tofauti na hapo tegemea tatizo kutokuisha kwa haraka.

• Jenga mazoea ya kwenda kukojoa kabla ya kwenda kulala kila siku

• Hakikisha kuna taa au mwanga wa kutosha njia ya kuelekea chooni, wakati mwingine mtu akiona giza anaweza kuogopa kwenda chooni hasa kama choo kipo mbali na anapolala hasa kwenye nyumba zetu hizi za uswahilini.

• Kama ni mtu mzima jipongeze mwenyewe. Kama ni mtoto mpe zawadi yoyote ndogo kila siku anapofanikiwa kuamka salama bila kukojoa kitandani. Hii inaongeza nguvu na moyo zaidi wa kudhibiti zaidi tatizo.

• Dhibiti matumizi ya juisi hasa juisi zenye sukari nyingi na za dukani nyakati za jioni

• Epuka vinywaji vyenye kaffeina kama vile chai ya rangi, kahawa, soda, energy drinks zote na vingine vyote vyenye kaffeina ikiwemo chokoleti mpaka hapo utakapokuwa umepona

• Tibu tatizo la kufunga choo au kupata choo kigumu kila mara.

• Tumia karatasi linalozuia maji kupenya kwenye godoro moja kwa moja ili
kupunguza harufu mbaya chumbani na usumbufu usio wa lazima.

• Weka alamu muda ule unaona mara nyingi mtoto ndiyo hujikojolea, weka saa yenye kengele (alarm) muda huo ili aweze kushtuka kabla na aende chooni.

Tatizo la kukojoa kitandani si tatizo linaloweza kutibika kwa haraka haraka ndani ya siku 2 au 3. Kuwa mvumilivu na mpole, walau jaribu tiba kwa mwezi mmoja mpaka miwili mfululizo na usikate tamaa haraka.

Kama unahitaji dawa hii ya kutibu tatizo la kukojoa kitandani niachie tu ujumbe WhatsApp +255714800175

Pokea dondoo nyingine za afya kama hii kupitia facebook BURE. Jiunge na mimi na watu wengine zaidi ya 100,000 kwenye ukurasa wangu. Ili kujiunga PENDA (like) ukurasa wangu kwa kubonyeza hapa .

Tafadhali SHARE post hii kwa ajili ya wengine uwapendao.

Imesomwa mara 1,213

Fadhili Paulo

Naitwa Fadhili Paulo, ni Tabibu wa Tiba asili. Ofisi yangu inaitwa Victoria Home Remedy Ipo Sigara Yombo Vituka Temeke Dar Es Salaam. Kama unahitaji kuonana na mimi uso kwa uso weka miadi (appointment) kupitia WhatsApp +255714800175. Pia kama una semina au kongamano lolote na unahitaji mzungumzaji hasa kwa upande wa afya hususani tiba asili, tuwasiliane napatikana.

0 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WhatsApp +255714800175