Dawa ya asili ya kuongeza hamu ya tendo la ndoa kwa mwanamke

Published by Fadhili Paulo on

awa ya asili ya kuongeza hamu ya tendo la ndoa

Dawa ya asili ya kuongeza hamu ya tendo la ndoa kwa mwanamke

Hili ni tatizo ambalo nimekuwa nikiulizwa mara nyingi sana na wanawake wengi kwa muda sasa na mwanzoni nilikuwa nalichukulia poa lakini kadri siku zinavyoenda naendelea kuona wengi zaidi wakizidi kunitafuta kwa ajili hii.

Wapo ambao wameshakuja hata kuniona kwa macho kwa ajili ya tatizo hili. Kweli unaweza ukadhani ni utani lakini ni tatizo linalozidi kuongezeka katika jamii yetu miaka ya sasa.

Na tatizo linakuwa baya zaidi kama linatokea ndani ya ndoa, kwani sababu hasa ya ndoa ni hiyo, kama ni kupika mwanaume anaweza kula hotelini au hata kujipikia mwenyewe kama ni kufua siku hizi kuna mashine za kufulia zinazotumia umeme nk nk

Na kama kuna jambo linaweza kuharibu ndoa yako taratibu bila wewe mwanamke kujua basi ni kumnyima haki ya ndoa mwenza wako kwa kisingizio cha eti huna hamu ya kushiriki tendo la ndoa!

Hili linapokutokea jaribu kufanya kila uwezalo ili uweze kurudi kwenye hali yako kama mwanzo.

Ni jambo la kawaida kabisa kumkuta mwanaume akinunua dawa ya kuongeza nguvu au hamu ya kushiriki tendo la ndoa lakini ni kinyume kwa wanawake.

Hata hivyo kuna ongezeko kubwa la kina mama wanaopungukiwa na hamu ya kutaka kushiriki tendo la ndoa na wengine wanalichukulia ni jambo la kawaida jambo ambalo ni hatari kwa mahusiano yako na mwenza wako.

Kama una umri wa miaka 45 kushuka chini na unapatwa na tatizo hili, somo hili lina msaada mkubwa kwako katika kukabiliana na tatizo la kukosa hamu ya kutaka kushiriki tendo la ndoa.

Endelea kusoma …

Dawa ya asili ya kuongeza hamu ya tendo la ndoa kwa mwanamke


Sababu za mwanamke kukosa hamu ya tendo la ndoa na suluhisho Lake

Sababu za mwanamke kukosa hamu ya kushiriki tendo la ndoa:

1. Ugomvi kwenye mahusiano

Kugombana kila mara na mwenza wako ndiyo namna rahisi kabisa inayoweza kuua hamu yako ya kutaka kushiriki tendo la ndoa.

Unapokuwa na hasira au umechukizwa na mwenza wako basi tendo la ndoa ndilo jambo la mwisho kabisa linaweza kukujia kichwani mwako.

Kuepuka hili jitahidi kupunguza ugomvi kwenye mahusiano yako na kama tayari yapo basi muwaone washauri wa ndoa yenu au hata viongozi wa dini na mfikie muafaka wa tofauti zenu.

Mheshimu mwenza wako na usimchukulie poa.

Lolote unaloona linasababisha ugomvi kati yenu jaribu kuliweka mbali kama unataka kusonga mbele katika huo uhusiano wenu.

2. Mfadhaiko wa akili (stress)

Haijalishi nini chanzo cha stress yako.

Mfadhaiko wowote wa akili unaweza kupelekea mwanamke kupungukiwa hamu yake ya kutaka kushiriki tendo la ndoa kwa haraka zaidi.

Mfadhaiko wa kama mbona sipati ujauzito, maisha magumu, kusimamishwa kazi ghafla nk vyote hivi vinaweza kukupunguzia hamu ya kutaka kushiriki tendo la ndoa haraka sana.

Mfadhaiko wa akili pia unaweza kukupelekea ukajihisi kuchoka sana jambo ambalo hupelekea kukosa hamu ya tendo kirahisi zaidi.

Tafuta namna ya kuondokana na hii mifadhaiko haraka bila kuathiri afya yako ya mapenzi.

Hakuna lisilo na suluhisho, jitahidi pia usikae na tatizo lako peke yako, ongea na watu utapata tu majawabu ya yanayokusibu.

3. Pombe na uvutaji sigara

Pombe na hata sigara vyote vinasemwa hupunguza hamu yako ya kutaka kushiriki tendo la ndoa kadri unavyoendelea kuvitumia kwa muda mrefu.

Wakati kiasi kidogo cha pombe kinaweza kisiwe kibaya sana lakini kinapozidi lazima kitaleta madhara katika jambo hili.

Wakati upande wa sigara haijalishi ni kiasi gani unatumia ili kubaki na afya yako nzuri ya mapenzi unashauriwa uache tu sasa hivi.

Kuongea ni rahisi kuliko kutenda si ndiyo?

Unahitaji kujua kwanini unapenda kuvuta na ubadili sababu hiyo na kitu kingine kizuri.

Mfano kama unavuta sababu unajisikia mpweke basi jaribu kwenda kwenye viwanja vya michezo na ujumuike na watu wengine.

Pamoja na hayo hakuna lisilowezekana kama ukiamua.

4. Dawa za uzazi wa mpango

Dawa za uzazi wa mpango zinasemwa huwa zinashusha usawa wa homoni mhimu kwa mwanamke ijulikanayo kama ‘testosterone’ kwenye mwili wako na mwisho wa siku hamu yako ya kushiriki tendo la ndoa lazima itashuka.

Ongea na daktari wako kama unahisi matumizi ya dawa za uzazi wa mpango yanaweza kuwa yanahusika na kushuka kwako kwa hamu ya tendo la ndoa kuona namna nyingine mbadala nzuri ya kukusaidia kupanga uzazi wako.

5. Ufanisi mdogo wa mwanaume

Kama mwanaume ataendelea kutokumridhisha mwenza wake kwa muda mrefu mfululizo hili linaweza kupelekea mwanamke husika kupungukiwa hamu yake ya kutaka kushiriki tendo la ndoa.

Hili likitokea mwanamke uwe na akili sana juu ya namna ya kumwambia hilo mwenza wako lasivyo unaweza kuharibu kila kitu bila kujua.

Usimwambie mwenza wako eti huna nguvu au huwezi kazi hivi macho kwa macho.

Kuna namna ya kuwasilisha jambo hilo kwa mwenza wako kwa namna ambayo haiwezi kumumiza.

Ni vizuri pia umjulishe hilo kwani kukaa kimya pia kutaleta madhara makubwa zaidi kwa uhusiano wenu lakini tumia akili unapomjulisha.

6. Historia mbaya ya mapenzi siku za nyuma

Historia mbaya kuhusu mapenzi siku za nyuma inaweza kupelekea mwanamke akapoteza hamu ya kushiriki tendo la ndoa.

Wanawake ambao wamewahi kubakwa siku za nyuma, wamewahi kutendwa vibaya na wapenzi wao au kufanyiwa vitendo vyovyote vibaya kuhusu mapenzi siku za nyuma wanaweza kupoteza hamu ya kushiriki tendo la ndoa kirahisi zaidi.

Kutibu hili unahitaji kuonana na daktari mtaalamu wa saikolojia kwa msaada zaidi na tatizo lako litaisha.

7. Kujiona siyo mrembo vya kutosha

Siku hizi wanawake wanahangaika kuongeza makalio au hata matiti yao ili tu waonekane ni warembo zaidi.

Kutokujiona wewe ni mrembo vya kutosha kunaweza kukupelekea ukaishiwa hamu ya kutaka kushiriki tendo la ndoa.

Unatakiwa tu ujikubali kama ulivyo kama vile ulivyoumbwa na Mungu. Kila mwanaume ana sababu zake za kukupenda, wanaume wengine wanavutiwa tu na jinsi ulivyo na ubongo mzuri na akili yenye utulivu na siyo sura yako wala makalio yako.

Isitoshe hizo ni sababu za muda tu, utazeeka unadhani utaendelea kubaki hivyo miaka yote?

Hivyo jikubali na amini yupo mtu anakupenda hivyo jinsi ulivyo.

Hakuna jambo baya kama kujidharau mwenyewe binafsi, wewe endelea kuwa kama ulivyo yupo mtu kwa ajili yako.

8. Baadhi ya magonjwa

Magonjwa kama Kisukari, Shinikizo la juu la damu, magonjwa ya moyo, vidonda vya tumbo, maumivu wakati wa tendo la ndoa na kansa yanaweza kupelekea mwanamke akapoteza hamu ya tendo la ndoa.

Magonjwa haya pia yanaweza kupelekea kubadilikabadilika kwa homoni za kike.

Hivyo ikiwa umebainika na magonjwa haya ni mhimu upate matibabu yake kwanza ili uweze kurudi katika hali yako ya kawaida.

9. Ujauzito na kunyonyesha

Homoni huwa zinabadilikabadilika wakati wa ujauzito na wakati wa kunyonyesha, Jambo hili linaweza kuathiri hitaji lako la kutaka kushiriki tendo la ndoa.

Ujauzito unaweza kukufanya ujisikie umechoka sana na kukupelekea usijisikie hamu ya kutaka kushiriki tendo la ndoa.

Punguza baadhi ya kazi ukiwa mjamzito na umfikirie zaidi mwenza wako.

Ukiwa unanyonyesha pia ni vizuri ukiwa na wasaidizi kwa ajili ya baadhi ya kazi zako ili kukupunguzia uchovu.

10. Uzee

Wakati mwanamke anafikia ukomo wa hedhi kwenye miaka 40 hivi homoni ijulikanayo kama ‘estrogen’ hushuka chini kwa kiasi kikubwa sana.

Kushuka kwa homoni hii pamoja na mambo mengine pia husababisha uke kuwa mkavu muda mwingi jambo linaloweza kupelekea maumivu wakati wa tendo la ndoa na hivyo kushuka kwa hamu moja kwa moja.

Unaweza kuwa unapakaa mafuta ya asili ya nazi au jeli ya aloe vera freshi ili kupunguza madhara haya yaletwayo na umri.

Wapo wanawake ambao kwa asili wao huwa na kiasi kidogo cha hamu cha kutaka kushiriki tendo la ndoa, lakini inapokutokea hamu hiyo inashuka ghafla na kwa kiasi kikubwa ni mhimu kutafuta ushauri wa kitaalamu ili kukabiliana na hali hiyo.

Soma hii pia > Dalili za mimba

Dawa ya asili ya kuongeza hamu ya tendo la ndoa kwa mwanamke > ROSEMERIA

Rosemeria ni dawa iliyo katika mfumo wa maji ya asili imeandaliwa maalumu kwa ajili ya kuamsha ari ya kushiriki tendo la ndoa kwa wanawake.

Inachofanya hasa hii dawa:

*Inaweka sawa homoni inayohusika na mambo ya msongo wa mawazo na uzazi homoni iitwayo testosterone na hivyo kuweka sawa mvurugiko wa hisia anaoupata mwanamke anapotaka kushiriki tendo la ndoa

*Inasaidia kuondoa tatizo la kukosa usingizi

*Inaongeza joto la mwili kwa ujumla

*Inasafisha mwili wote kwa ujumla na kuongeza msukumo wa damu

*Kwa asili inasaidia kuchoma mafuta yaliyozidi mwilini na hivyo kukupunguzia uzito uliozidi

*Inasaidia kupunguza utegemezi wa vilevi kama sigara, pombe na madawa mengine ya kulevya kama matokeo yake chanya ya kuondoa sumu na taka mbalimbali mwilini

*Inahamasisha hali ya matamanio ya tendo la ndoa yanayoelekea kufa hata kwa mwanamke mwenye umri mkubwa

*Ni formula moja yenye mchanganyiko wa mitishamba maalumu ya asili yenye uwezo wa kuamsha msukumo wa damu na kuongeza hali ya utulivu wa nafsi na akili kwa mwanamke

Vitu vya kuviepuka:

Kama una tatizo hili la kukosa hamu ya kushiriki tendo la ndoa ili kupata uponyaji kwa haraka ukiacha kutumia dawa epuka pia vitu hivi vifuatavyo:

1. Vyakula vinavyopikwa katikati ya mafuta mengi
2. Vyakula vya kwenye maboksi (vya dukani)
3. Vyakula vyenye sodiamu kwa wingi
4. Sukari
5. Chai ya rangi na kahawa
6. Kaffeina
7. Pombe
8. Sigara
9. Madawa ya kulevya
10. Popcorn

Je wewe ni mwanamke na umeishiwa hamu ya tendo la ndoa?

Ikiwa utahitaji Rosemeria, niachie ujumbe WhatsApp +255714800175

Rosemaria inagharimu 55000 (elfu 55).

Ofisi yangu inaitwa Tumaini Herbal Life, ipo Kibugumo Mji Mwema Kigamboni Dar Es Salaam

Tafadhali SHARE POST HII kwa ajili ya uwapendao.

(Visited 14,097 times, 1 visits today)

0 Comments

Leave a Reply

Avatar placeholder

Your email address will not be published.

WhatsApp WhatsApp +255714800175