Dawa ya kupunguza unene

Dawa ya asili ya kupunguza uzito, unene na kitambi

Dawa ya asili ya kupunguza uzito, unene na kitambi

Kuna watu hudhani ukiwa mnene au mwenye uzito mkubwa ndiyo kuwa na afya na ndiyo maana wengine wakikonda basi huchanganyikiwa kabisa.

Lakini uzito au unene uliozidi ni ugonjwa tena ugonjwa mubaya kabisa ambao unapaswa kuwa makini nao sana kwani ni chanzo cha magonjwa mengine mengi mwilini.

Kila mmoja anapaswa kuwa na uzito unaomstahili kulingana na urefu wake.

Tafiti zinaonesha watu wenye uzito kupita kiasi wana uwezakano mkubwa wa kupatwa na magonjwa mengine hatari kwa kiwango kikubwa zaidi tofauti na watu wembamba.

Magonjwa hatari unayoweza kupata kutokana na uzito wako kuwa mkubwa ni pamoja na yafuatayo:

1. Magonjwa ya moyo.
2. Shinikizo la juu la damu 
3. Kiharusi (Stroke)
4. Kisukari aina ya pili 
5. Baadhi ya aina za saratani
6. Ugumba
7. Msongo wa mawazo (Stress)
8. Matatizo ya mifupa
9. Maumivu ya mgongo
10. Kuishiwa nguvu za tendo la ndoa (kwa wanaume)

Nini hupelekea kuongezeka kwa uzito mwilini au kuwa mnene?

Uzito uliopitiliza hutokana na kuongezeka kwa nishati mwilini, vyakula tunavyo kula kila siku hutengeneza nishati ambayo  hutumika katika shughuli mbalimbali za mwili.

Kwahiyo uzito kupitiliza au unene hutegemeana na kiwango cha nishati ambacho hupatikana katika vyakula na vinywaji ambavyo tumekula na kiasi kinacho tumiwa na mwili.

Kwahiyo ili usiwe na uzito mkubwa wala mdogo ni lazima kiwango cha nishati kinachoingia mwilini kilingane na mahitaji ya mwili wako hivyo basi uzito mkubwa hutokana na kula kiwango kikubwa cha nishati ikiwa matumizi ya nishati hiyo mwilini ni kidogo.

Zifuatazo ni sababu zinazopelekea kuwa na uzito mkubwa au unene nazo ni.

1. Msongo wa mawazo.      

Katika hali ya kawaida  msongo wa mawazo huathiri au huvuruga mfumo wa vichocheo vya mwili ivyo kupelekea kuvurugika kwa utendaji kazi wa mwili.

Kichocheo cha cortisol hufanya kazi ya kuweka uwiano sawa wa nishati mwilini, hivyo Kuvurugika kwa kichocheo hiki hufanya mtu ahisi njaa muda wote jambo ambalo litapelekea kula zaidi na nishati kuhifadhiwa mwilini kwa wingi jambo ambalo hupelekea uzito kuongezeka.

2. Kukosa usingizi.

Kukosa usingizi huongeza athari ya mtu  kuwa na uzito mkubwa, kwasababu usingizi husababisha kuwa na ulinganisho au uwiano kati ya vichocheo ambavyo vinamfanya mtu ahisi njaa na vile ambavyo vina mfanya mtu asihisi njaa.

Vichocheo ambavyo humfanya mtu ahisi njaa huitwa Ghrelin navichocheo ambavyo humfanya mtu asihisi njaa huitwa Leptin.

Kwaiyo kukosa usingizi husababisha kuvurugika kwa uwiano mzuri uliopo katika vichocheo ivyo kusababisha kupanda kwa kichocheo(ghrelin) ambacho kinamfanya mtu ahisi njaa na kushuka kwa uzalishwaji wa kichocheo (leptin)  ambacho humfanya mtu asihisi njaa hali hii hupelekea mtu ale zaidi na kusababisha nishati kuhifadhiwa kwa kiwango kikubwa na matokeo yake ni kuongezeka uzito.

Pia kutokana na kuongezeka kwa uhitaji wa chakula mwilini hupelekea kuathirika kwa utendaji kazi wa kichocheo (insulin) hali hii humfanya mtu  awe katika hatari ya kuugua ugonjwa wa kisukari ambao hutokana na jinsi mtu anavyo ishi maisha ya kila siku.

3. Kutokufanya mazoezi.       

Ili uwe na afya bora mazoezi ni muhimu kwasababu husaidia kutoa taka mwili,huimarisha viungo vya mwili, huongeza kiwango cha msukumo wa damu, vile vile husaidia kupunguza uzito au unene.

Kutokufanya mazoezi huufanya mwili kushindwa kutumia nishati inayopatikana katika chakula ulichokula jambo ambalo husababisha kuwepo kwa uwingi wa nishati mwilini nahivyo kupelekea nishati iyo ihifadhiwe kama mafuta mwilini jambo ambalo litapelekea uzito kuongezeka.

4. Unywaji wa pombe na ulaji wa vyakula vya viwandani.                    

Kuna makampuni mengi sana siku hizi ambayo hutengeneza vyakula na vinywaji katika viwanda vyao.Makampuni haya hutumia gharama kubwa kufanya matangazo ya bidhaa zao.

Kutokana na ushawishi mkubwa wa matangazo yao na bei nafuu ya bidhaa zao watu wengi hujikuta wanatunia bidhaa za makampuni kuachana na zile za kuandaa wenyewe.

Vyakukula na vinywaji hivi vimetengeneza kwa kiwango kikubwa cha nishati.

Pindi mtu anavyo tumia bidhaa hizi kwa wingi husababisha nishati kubwa iendelelee hifadhiwa mwilini wakati matumizi ya mwili ni madogo matokeo yake uzito huongezeka.

5. Kutokuzingatia lishe sahihi.              

Wakati mwingine unaweza kuongeza uzito kwasababu ya kutokula mlo sahihi,na kwa kiwango ambacho siyo sahihi na wakati ambao siyo sahihi.

Baadhi ya watu uzito wao huongezeka japo wanakula kiwango kidogo cha chakula lakini wapo wengine hubaki na uzito ule ule japo wanakula mlo anbao ni sawa.

Hii inaweza kuoanishwa na kiwango tofauti  cha shughuli za kikemikali mwilini au aina ya chakula ambacho mtu anakula na haina mahusiano na kiwango cha chakula ambacho mtu anakula isipo kuwa ni ubora wa chakula chenyewe hii humaanisha unaweza ukala chakula kidogo ukaongezeka uzito na mwingine akala chakula kile kile na akaongezeka uzito.

6. Matumizi ya madawa.                        

Dawa zimetengenezwa kwa kutumia kemikali.

Tunatumia dawa kwa lengo la kutibu au kupata suluhu ya ugonjwa ambao unakusumbua.

Dawa hizi huleta matokeo tofauti pamoja na kutibu tatizo ambalo lina kusumbua.

Mbali na kutibu tatizo ambalo linakusumbua dawa hizi huleta maudhi madogo madogo na mahudhi hayo hutofautiana kati ya dawa na dawa na mtu na mtu na hii ni kutokana na vile tumeumbwa.

Baadhi ya dawa mfano dawa za kisukari , dawa za kutuliza mihemuko (ant depressant) mbali na kushusha sukari dawa hizi husababisha kuongezeka kwa uzito.

7. Ulaji wa vyakula vya wanga na sukari kwa wingi.       

Ulaji wa vyakula hivi kwa wingi huchochea deli za kuhifadhi mafuta ziendelee kuhifadhi mafuta zaidi na matokeo yake in kuwa mnene au kuwa na uzito mkubwa.

8. Urithi.    

Unene au uzito mkubwa unaweza ukarithiwa kutoka kwa moja kati ya wazazi na hii ni kutokana na tafiti ambazo zmefanywa.

Pia endapo mama mjamzito atakula sana au hatokula sana hupelekea kubadilika kwa DNA ya mtoto na kusababisha athari katika utumiaji wa mafuta mwilini kwa baadae.

Dawa ya asili ya kupunguza uzito, unene na kitambi > Banaba Mix

Banaba Mix ni dawa nzuri ya asili inayoondoa uzito, unene na kitambi kwa pamoja bila kukuachia madhara mengine mabaya.

Na inafanya kazi hizo kwa namna zifuatazo:

1. Banaba Mix huuongezea nguvu mfumo wa mmeng’enyo wa chakula

Nitaelezea uhusiano uliopo kati ya mfumo wako wa mmeng’enyo wa chakula na kuongezeka au kupungua kwa uzito wako.

Mmeng’enyo wa chakula ni mfumo wa mwili unaotumika kutengeneza nguvu kwa kukichanganya chakula na oskijeni katika seli kwenye sehemu ya seli ijulikanayo kwa kitaalamu kama ‘mitochondrion’.

Muda wote mwili wako unafanya kazi ya kumeng’enya chakula hata unapokuwa usingizini.

Unaongezeka uzito wakati unapokula chakula zaidi na mfumo wa mmeng’enyo unapofanya kazi chini ya kiwango.

Baadhi ya watu wanaonekana kuwa na mfumo wa mmeng’enyo wa chakula wenye kasi zaidi na hivyo wanasaga chakula kwa haraka zaidi na hivyo wanaepuka kuongezeka uzito kirahisi kuliko wale wengine wenye mfumo wa mmeng’enyo wa chakula wa taratibu.

Kwahiyo utaweza tu kupunguza uzito ikiwa mfumo wako wa mmeng’enyo wa chakula unafanya kazi zaidi kuzidi kiasi cha chakula unachokula.

Hivyo ili uzito wako upunguwe inakulazimu ufanye mambo mawili ambayo ni ama unakula chakula kichache au ule chakula kingi huku ukifanya bidii kuchoma chakula zaidi kwa kuushughulisha mwili zaidi (mazoezi ya viungo).

Hilo linaweza kuwa rahisi si ndiyo ndugu msomaji?

Banaba Mix ina kiasi kizuri cha mafuta mazuri yajulikanayo kama Omega-3 fatty acids ambayo kazi yake hasa ni kuuongezea kasi mfumo wa mmeng’enyo wa chakula ndani ya mwili.

Hii ndiyo sababu utawasikia watu wakisema wanajisikia kuwa na nguvu nyingi wanapokuwa wametumia dawa hii.

Maana iliyopo hapa ni kwamba miili yao ipo kwenye kiwango cha juu kwenye umeng’enyaji wa chakula na hivyo kama matokeo yake wanapata kupungua uzito kirahisi zaidi.

Omega 3 husaidia huongeza msukumo wa damu kwenye mishipa wakati wa mazoezi na kusaidia kuhamasisha vimeng’enya vinavyohusika kuhamisha na kuweka mafuta katika sehemu yatakapoweza kutumika kutengeneza nguvu.

Umeona?

2. Banaba Mix huondoa hisia za njaa

Njia nyingine Banaba Mix itakufanya upunguwe uzito ni kwa kukufanya ule chakula kichache kwakuwa dawa hii itakufanya ujisikie umeshiba (unajiona upo full) kwa masaa mengi baada ya kuwa umeitumia na hivyo unakuwa huna njaa kubwa kama siku nyingine.

Na habari njema ni kuwa pamoja na kukuacha huna hamu ya kula bado unakuachia pia viinilishe vya kutosha ambavyo mwili wako unavihitaji kwa siku nzima.

Banaba Mix ina viinilishe vingi mhimu kwa ajili ya mwili ndani yake!

Mwili wako utakuwa umepewa yote unayohitaji kwa kuwa umetumia Banaba Mix hata kama unakula chakula kichache au husikii njaa ni sawa sababu yote unayohitaji kwa ajili ya afya unakuwa umepata tayari katika dawa hii.

Hivyo siyo kwamba unakuwa umefunga, la hasha, hii inakufanya uepuke kula hovyo hovyo au kila mara hivyo Banaba Mix inakufanya ubaki na adabu ukiheshimu mwili wako dhidi ya kula kila mara.

Hivyo Banaba Mix inapunguza njaa, inakufanya ujisikie umeshiba muda mrefu na hivyo moja kwa moja utakula chakula kichache.

Hiyo ni njia nyingine Banaba Mix inavyoweza kukusaidia kupunguza uzito na unene kupita kiasi.

3. Banaba Mix ina kiasi kingi cha nyuzi nyuzi (faiba)

Banaba Mix ina nyuzi nyuzi nyingi ndani yake.

Hivyo kuitumia dawa hii kupunguza uzito kunakupa wewe kiasi unachohitaji cha nyuzi nyuzi ambacho mwisho wake hukusaidia kupunguza uzito

Kwa kawaida unahitaji gramu 38 za nyuzi nyuzi wa siku ili kusaidia kuwa na uzito ulio sawa.

Kile kinachokufanya ujisikie umeshiba kwa muda mrefu baada ya kutumia dawa hii ni hii kuwa na nyuzi nyuzi ndani yake (fiber).

4. Banaba Mix husaidia kuondoa sumu mwilini

Kuna mitishamba, vyakula na mbinu nyingi za kuondoa sumu ambazo zinasaidia vizuri tu kazi hii ya kuondoa sumu mwilini.

Nini sababu hasa ya kutaka kutoa sumu mwilini?

Jibu ni kuwa inasaidia kuufanya mwili wako kuwa mpya tena na kwa sababu hiyo uzito unapata kupungua pia

Programu nyingi zinazotumika katika kuondoa sumu na hivyo kupunguza uzito haraka mara nyingi huondoa tu maji yaliyozidi mwilini huku ukiachwa na mafuta mwilini kwa sehemu kubwa labda mpaka kwa wiki kadhaa baadaye.

Hivyo usianze program za kupunguza sumu kwa lengo la kupunguza hasa uzito bali kama njia ya kuanza njia mpya ya kuishi yenye afya zaidi yaani kula zaidi matunda, samaki na matunda za maboga huku ukipunguza sana kula nyama

Banaba Mix inasaidia sana katika kazi ya kutoa sumu na kusafisha mwili wote kwa ujumla na hivyo kukuruhusu wewe upate viinilishe vyote mhimu kutoka katika chakula unachokula na hivyo kukusaidia wewe kupungua uzito katika huo mlolongo

Tumia na haitachukua muda mrefu kuona matokeo yake katika kuweka sawa uzito wa mwili wako.

Dawa hii haitumiki kwa mama mjamzito na yeyote mwenye shinikizo la chini la damu.

Dawa ya kupunguza unene

.

Mambo mhimu ya kufanya unapokuwa una tatizo la uzito au unene kupita kiasi:

1. Hakikisha unakunywa maji kila nusu saa kabla ya kula chakula
2. Fanya mazoezi hasa mazoezi ya kutembea kwa miguu mwendo kasi lisaa limoja mara 2 kwa siku kwa mwezi 1 mpaka miwili
3. Punguza vyakula vyenye wanga
4. Punguza vyakula vinavyopikwa katikati ya mafuta mengi kama vile zinavyopikwa chipsi au maandazi
5. Acha kabisa soda na juisi za viwandani
6. Usikae kwenye kiti au usikae tu chini kwa masaa mengi katika siku
7. Unaweza kufunga mara moja moja katika wiki

Kama unahitaji Banaba Mix kwa ajili ya kupunguza uzito, unene au kitambi niachie ujumbe WhatsApp +255714800175.

Banaba Mix inatibu pia Kisukari, Shinikizo la juu la damu, inaweka sawa kolesto na ni msaada mzuri kwa kuimarisha afya ya moyo.

Unataka kujuwa ikiwa una uzito sawa au uliozidi?

Tumia kikokotoo cha BMI (BMI calculator) hiki hapa chini kwa kufuata hatua hizi:

a)Bonyeza Nataka Kupima Uzito 

b)Kisha andika urefu wako katika sentimita na uzito katika kilogramu

c)Mwisho bonyeza KOKOTOA

Itakuambia kama una uzito sawa au umezidi au una uzito pungufu.

Pima uzito hapa

require
require require

Your BMI is......

BMIClassification
less than 18.5:Underweight
18.5 - 24.9:Normal weight
25 - 29.9:Overweight
30 - 34.9:Class I Obese
35 - 39.9:Class II Obese
40 upwards:Class III Obese

.

Mjulishe rafiki yako kwenye twitter naye asome post hii kwa kubonyeza ujumbe ufuatao:

Dawa ya asili ya kupunguza uzito, unene na kitambi Click To Tweet

Tafadhari share post hii kwa ajili ya wengine

Fadhili Paulo
Imesomwa mara 2,842

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *