Dawa ya asili ya kuzuia mimba kuharibika

Published by Fadhili Paulo on

Mimba kuharibika ni tukio linalowatokea wanawake na mamalia wengine wa kike kutokana na shida mbalimbali katika ukuaji wa mimba tumboni mwa mama.

Ni tukio tofauti na utoaji mimba ambalo linasababishwa na binadamu kwa makusudi.

Matukio yote mawili kwa kawaida yanaleta matatizo mbalimbali kwa mama.
Kuharibika kwa kijusi au kiinitete pengine kunatokana na mfadhaiko wa kiajali au sababu za kimaumbile.

Mimba nyingi huharibika kutokana na kutonakiliwa kisahihi kwa kromosomu; pia huweza kuharibika kutokana na mazingira.

Mimba inayotamatika kabla ya wiki ya 37 katika kipindi cha ujauzito husababisha uzaaji wa mtoto hai na hujulikana kama kuzaliwa mapema au njiti.

Kijusi akifa akiwa ndani ya chupa ya uzazi baada ya wiki ya 22, au wakati wa kujifungua, kwa kawaida hujulikana kama mzaliwa-mfu au si-riziki.

Kuzaa mapema na uzazimfu kwa jumla hauchukuliwi kama kuharibika mimba ingawa matumizi ya maneno haya wakati mwingine huingiliana.

Kati ya asilimia 10 na 50 ya mimba hutamatishwa kwa njia zinazoweza kubainishwa kimatibabu, kutegemea umri na afya ya mwanamke mjamzito.

Mimba nyingi huharibika katika hatua za mapema sana za ujauzito, kiasi kwamba mwanamke hafahamu kwamba alikuwa mjamzito.

Utafiti mmoja uliofanywa kupima homoni za kutoa yai na ujauzito uligundua kuwa asilimia 61.9 ya uhamili ulipotezwa kabla ya wiki ya 12, na asilimia 91.7 ya kuhabirika huko kulitokea bila kuonyesha dalili kabla, na bila ya fahamu ya mwanamke aliyekuwa mjamzito.

Hatari ya kutoka mimba ghafla hupungua kwa kiasi kikubwa baada ya wiki 10 kutoka kipindi cha mwisho cha hedhi.

Nini husababisha mimba kuharibika?

Kisababishi kikuu cha mimba kuharibika katika miezi mitatu ya kwanza huwa ni pamoja na;

*Matatizo ya kromosomu ya kiinitete / kijusi, hali ambayo husababisha angalau asilimia 50 ya kutoka kwa mimba mapema.
*Magonjwa ya mishipa (lupus),
*Kisukari
*Matatizo ya kihomoni
*Maambukizi kama vile U.T.I 
*Matatizo ya chupa ya uzazi.
*Magonjwa ya figo
*Miali (radiation)
*Magonjwa ya moyo
*Baadhi ya dawa za kutibu magonjwa kama vile dawa ya kutibu chunusi iitwayo ‘accutane’
*Lishe duni sana
*Uvutaji sigara au tumbaku
*Utumiaji wa madawa ya kulevya na pombe
*Inaweza pia kusababishwa na kiwewe kinachotokana na ajali.

Pia umri mkubwa wa mama na historia ya mimba zilizotangulia kuharibika ni sababu mbili kuu zinazohusishwa kwa sana na mimba kuharibika ghafla.

Tafiti zinazoonyesha hatari ya mimba kuharibika huwa ni asilia 12 hadi 15 katika umri wa miaka 20 na kuongezeka hadi asilimia 25 kuanzia umri wa miaka 40.

Hakuna ushahidi wa moja kwa moja kwamba mfadhaiko yaani stress au tendo la ndoa vinaweza kupelekea kuharibika kwa ujauzito.

Wakati mwingine ikiwa mama atapata matibabu kwa magonjwa sugu yanayomsumbua kunaongeza uwezekano mkubwa wa ujauzito kutokuharibika.

Dalili za mimba kuharibika

*Kuvuja damu
*Mikakamao ya mishipa
*Maumivu yasiyo ya kawaida
*Homa

Ikiwa wewe ni mjamzito na unatokewa na dalili hizo hapo juu unashauriwa kwenda kumuona daktari haraka.

Ikiwa unahitaji dawa ya Asili ya kuzuia mimba kuharibika bonyeza hapa.

(Visited 4,057 times, 1 visits today)

1 Comment

Anonymous · 08/09/2021 at 2:20 pm

Kaka habari samahani naomba unisaidie kitu hapa..Mimi nlikutana na Mr siku ya 12 -15
Baada ya period..baada ya siku sita nkianza kuhis dalili za mimba…alafu tumbo likiwa linauma chin ya kitovu chakushangaza baada ya week mbili nmeingia period…Hali hyo imewai tokea miez kadhaa ya nyuma nlikutana na Mr kwenye siku zangu za hatar nlijua nna mimba lakin nkapata hedhi baada ya week mbil kupita kwenye Ile tarehe nlotakiwa kuingia…Sasa sijui shida Nini?

Leave a Reply

Avatar placeholder

Your email address will not be published.

WhatsApp WhatsApp +255714800175