Bawasiri ni ugonjwa katika njia ya haja kubwa, hujitokeza kama uvimbe au kijinyama ambacho huweza kuonekana hadi nje.

Kwa kiingereza hujuliakana kama haemorrhoids au piles.

Bawasiri inaweza kupelekea upungufu wa damu mwilini. Bawasiri inaweza kutibika ama kwa upasuaji ama kwa matumizi ya dawa mbadala kwa kipindi kirefu wiki hata 6 au hata zaidi kutegemea ilikuwa imejijenga kiasi gani.

Bawasiri ya nje

Bawasiri husababishwa na nini

Hakuna sababu ya moja kwa moja inayojulikana kisayansi kwamba ndiyo husababisha bawasiri, bali mambo yafuatayo yanaweza kupelekea wewe kupatwa na ugonjwa huu:

1. Kufunga choo au kupata choo kigumu kwa muda mrefu
2. Ujauzito – wakati wa ujauzito watu wengine wanaweza kupatwa na bawasiri sababu ya msukumo wa mtoto karibu na sehemu ya kutolea haja kubwa
3. Kushiriki mapenzi kinyume na maumbile
4. Uzee – kadri miaka inavyosogea ndivyo inavyokuwa rahisi kwako kupatwa na ugonjwa huu kwa baadhi ya watu
5. Sababu za kurithi – baadhi ya watu wanaweza kurithi udhaifu wa ukuta huo wa njia haja kubwa ingawa ni asilimia ndogo sana.
6. Kuharisha sana kwa muda mrefu
7. Kutumia vyoo vya kukaa
8. Kunyanyua vyuma vizito
9. Mfadhaiko/stress
10. Uzito na unene kupita kiasi nk

Dalili za Bawasiri

1. Maumivu wakati wa kujisaidia haja kubwa
2. Kinyesi kunuka damu wakati wa kujisaidia
3. Muwasho sehemu ya tundu la haja kubwa
4. Uvimbe au kinyama kujitokeza sehemu ya tundu la haja kubwa
5. Haja kubwa yaweza kujitokea tu muda wowote

MADHARA YA TATIZO LA BAWASIRI

👉kupata upungufu wa damu (anemia)

👉Kupata tatizo la kutokuweza kuhimil choo

👉hupunguza nguvu za kiume na kuondoa hamu ya tendo la ndoa kwa wanawake

👉kuathirika kisaikolojia

👉kukosa moral ya kufanya Kazi kutokana na maumivu makali

Bawasiri ni ugonjwa katika njia ya haja kubwa, hujitokeza kama uvimbe au kijinyama ambacho huweza kuonekana hadi nje. Kwa kiingereza hujuliakana kama haemorrhoids au piles.

Bawasiri inaweza kupelekea upungufu wa damu mwilini. Bawasiri inaweza kutibika ama kwa upasuaji ama kwa matumizi ya dawa mbadala kwa kipindi kirefu wiki 4 hata 6 au hata zaidi kutegemea ilikuwa imejijenga kiasi gani.

Bawasiri ni ugonjwa unaoanzia ndani ya tumbo kwenye mfumo wako wa mmeng’enyo wa chakula. Ukiugua bawasiri ujuwe kuna kitu si sawa ndani ya tumbo lako. Bawasiri ni ishara ya moja kwa moja kwamba kwenye mfumo wako wa mmeng’enyo wa chakula kuna tatizo.

Dawa ya Bawasiri > Unga wa majani ya mlonge na mafuta ya habbat soda

Unga wa majani ya mlonge

Mara nyingi bawasiri inaanza kwa mtu kupata choo kigumu au kufunga choo kabisa kwa siku kadhaa. Ukitumia mlonge utapata choo kizuri na kilaini na siyo rahisi upate tatizo kwenye mfumo wa mmeng’enyo wa chakula kama unatumia mlonge.

Mlonge unaboresha afya yote ya mwili kwa ujumla, unaondoa msongo wa mawazo na kukufanya ujisikie vizuri tena. Mtu yeyote anayesumbuliwa na bawasiri pamoja na dawa zingine mlonge lazima atumie ili kupata uponyaji wa hakika na wa kudumu.

Vitamini B1 (Thiamine) na vitamini B2 zipatikanazo kwenye mlonge husaidia mwili wako kubadili wanga kuwa nguvu ndani ya mwili wako.

Kazi hii ni mhimu katika uundwaji na utengenezaji upya wa seli ndani ya mwili. Vitamini hizi mbili pia zina umhimu mkubwa katika kuweka sawa hisia za njaa. Vitamini B3 na folic asidi (niacin) ni moja ya vitu mhimu kwenye mfumo wa mmeng’enyo wa chakula.

Vitamini hizi zinasaidia katika kuvunjavunja chakula hasa vyakula vya wanga na mafuta kwenye mfumo wa mmeng’enyo wa chakula. This vitamin will aid in efficient breakdown of carbohydrates and fats. Vitamini B6 (Pyridoxine) husaidia kushughurikiwa (kumeng’enywa) kwa protini yote iliyomo kwenye chakula.

Vitamini H (Biotin) husaidia mfumo wa mmeng’enyo wa chakula kwa kuzalisha kolesto, kuishughurikia protini, mafuta na wanga. Baada ya protini kuwa imemeng’enywa, vitamini H husaidia mfumo wa mmeng’enyo wa chakula kwa kuuondolea sumu na taka nyingine zisizohitajika.

Vitamini za kundi B nyingi zinaweza kuongezwa mwilini kwa kutumia vyakula ambavyo havijakobolewa, bidhaa za maziwa ya ng’ombe, maharage, maharage ya kijani na samaki wa baharaini. Kwa mjibu wa utafiti, watu wengi hawapati vitamini hizi kiasi cha kutosha kwenye milo yao kila siku.

Vitamini C inajulikana kwa umhimu wake wa kuweka meno na fizi kuwa vyenye afya zaidi ambavyo kama matokeo yake ni afya bora ya mfumo wa mmeng’enyo wa chakula. Vitamini C inasaidia mfumo wa mmeng’enyo wa chakula kutokana na ukweli kwamba ndiyo vitamini inayohusika na umeng’enywaji wa chuma mwilini.

Ikiwa utajumuisha matunda mengi yenye vitamini C kwenye chakula chako ile nyuzinyuzi (faiba) ndani yake inasaidia kuondoa matatizo mbalimbali kwenye mfumo wa mmeng’enyo wa chakula.

Nyuzinyuzi zinasaidia kuondoa sumu mbalimbali ndani ya mwili.

Mlonge una vitamini C mara 7 ZAIDI YA ILE INAYOPATIKANA KATIKA MACHUNGWA!

Vitamini D husaidia kujenga meno imara ambayo ni mhimu katika mfumo wa mmeng’enyo wa chakula. Tafiti zinaonyesha kuwa upungufu wa vitamini D unaweza kupelekea mtu kupata saratani ya utumbo mpana.

Unaweza kupata vitanini D kwa wingi kwa kutumia zaidi mlonge.

Vitamini na viinilishe vingine unavyopata toka kwenye mlo kamili ni mhimu kwa ajili ya mfumo wako wa mmeng’enyo wa chakula. Unapokula kiasi kingi cha wanga na mafuta mfumo wako wa mmeng’enyo wa chakula unazidiwa kazi na hautaweza kuwa na afya nzuri.

Unahitaji chakula chenye vitamini nyingi za kutosha ambazo ni mhimu kwa afya ya mwili.

Kwa kuongezea mlonge una lundo la vitamini kundi B kuliko mti au mmea mwingine wowote unaoufahamu.

Mlonge una vitamini B, B1, B2, B3, B5, B6, B12, D, E, K, folic acid, Kalsiamu (mlonge una Kalsiamu mara 17 zaidi ya ile ya maziwa ya ng’ombe), madini ya shaba, potasiamu, magnesia, kromiamu na vitamini, na madini madogo madogo mengine mengi mhimu kwa ajili ya kuimarisha kinga ya mwili.

Mlonge pia una zile amino asidi mhimu 9 za kwenye protini.

Elewa tu kwamba mti huu wa maajabu mti wa mlonge na majani yake mti ambao hujulikana pia kama mti wa uzima una viinilishe bora na mhimu zaidi kwa ajili ya kuongeza kinga ya mwili ambavyo siyo rahisi kuvielezea vyote kimoja baada ya kingine

Kutibu bawasiri tumia unga wa majani ya mlonge kijiko kidogo kimoja cha chai kwa mwezi mmoja mpaka miwili ndani ya juisi ya matunda (hasa juisi ya parachichi) au katika uji au kwenye mtindi kutwa mara moja.

Kwanini watu wengi hawaponi bawasiri? :

Dawa peke yake haziwezi kukuletea maajabu yoyote, unaweza kupona lakini kama hutabadili vifuatavyo ugonjwa utaendelea kujirudia kwako na pengine hata kupona itakuwa shida.

Bawasiri huwa haiponi haraka, walau dozi yake isiwe chini ya mwezi mmoja na ukizingatia yafuatayo kwa kipindi kirefu basi kupona ni lazima.

WaTanzania wengi wanaugua bawasiri kutokana na sababu kuu mbili, moja wanakula ugali wa sembe badala ya ugali wa dona, pili hawanywi maji ya kutosha kila siku na wengine hawanywi maji mpaka wasikie kiu.

Ili upone bawasiri moja kwa moja kwa urahisi zaidi zingatia yafuatayo kila siku:

  1. Kula vyakula vingi vyenye nyuzinyuzi (fiber) kila siku (Machungwa, ndizi, parachichi, karoti, viazi vitamu, tufaa (apple), maharage, ugali wa dona, broccoli, mapeazi, komamanga, maboga, njegere nk)
  2. Kunywa maji mengi kila siku ili kusafisha mwili na kuepuka kufunga choo
  3. Kula sana mboga majani na matunda
    Kula vyakula ambavyo havijakobolewa
  4. Epuka mapenzi kinyume na maumbile
  5. Usitumie choo cha kukaa
  6. Usikae kwenye kiti masaa mengi
  7. Kula chakula ukiwa umesimama na ukimaliza kula tembea tembea dakika 20 ndipo ukae
  8. Fanya mazoezi ya kuchuchumaa na kukaa mara 1 kila siku (squatting).

Pia kwa matokeo mazuri zaidi kama tayari bawasiri imeshadumu kwa muda mrefu ni vizuri ukitumia unga wa majani ya mlonge sambamba na mafuta ya habbat soda na mafuta ya nyonyo. Vyote ninavyo kama utahitaji.

Kama utahitaji unga wa majani ya mlonge na habbat soda niachie tu ujumbe WhatsApp +255714800175

Naweza pia kukuletea ulipo kama utataka BURE ndani ya Dar, Natuma pia popote ulipo nje ya Dar.

Kama una ushuhuda wowote kuhusiana na unga wa majani ya mlonge ningefurahi kama utaniandikia hapo chini kwenye comment

Tafadhari SHARE post hii kwa ajili ya wengine

Naitwa Fadhili Paulo, ni Tabibu wa Tiba Asili na ni mTanzania.

Ofisi yangu inaitwa Victoria Home Remedy ipo Sigara Yombo Vituka Temeke Dar Es Salaam.

Jiunge na mimi na watu wengine zaidi ya 94000 kwenye ukurasa wangu wa facebook kwa kubonyeza hapa

Imehaririwa mara ya mwisho

Niulize swali nikujibu

Categories: Bawasiri

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WhatsApp Chat na mimi kwenye WhatsApp