Mafuta ya mbegu za mwarobaini ni dawa ya chunusi, fangasi, upele na miwasho, upele na ukurutu wa aina yoyote na matatizo karibu yote ya ngozi.

Kama hujawahi kuisikia hii dawa kongwe ya mafuta ya mbegu za mwarobaini, basi ni wakati muafaka sasa upate kufahamu habari zake hasa kwa matatizo ya ngozi

Mwarobaini ni mti wenye asili ya India hujulikana pia kama Indian lilac, Azadirachta Indica, au ‘Neemba’ na umekuwa ukitumika katika tiba asili za kihindi (Ayurvedic medicine) zaidi ya miaka 5000 iliyopita.

Kwa kawaida mti huu unapatikana karibu katika kila nyumba huko India.

Unasadikika kutibu magonjwa mbalimbali 40 hasa majani yake, huku mbegu zake ndiyo hutumika kutengeneza mafuta ambayo ni dawa kwa matatizo mbalimbali ya ngozi.

Ukishaota unao uwezo wa kuendelea kudumu kwa zadi ya miaka 200.

Ni kiungo mhimu kwenye bidhaa nyingi kama losheni, dawa za kuulia wadudu, sherehe za kidini na mengine mengi.

Taarifa zisizo rasmi zinasema majani ya mti huu ukiyachemsha katika maji na kuyaoga mara kwa mara husaidia kuondoa mikosi na nuksi mbalimbali.

Mwarobaini una viinilishe mhimu kwa ajili ya mwili zaidi ya 100 na una uwezo mkubwa wa kutibu maradhi zaidi ya 40. Hujulikana pia kama mti wa uzima.

Moja ya vitu vilivyomo kwenye mafuta haya ni pamoja na vitamini E, nimbidin na nimbin, carotenoids, linoleic acid, oleic acid, vitamini C, quercetin na kingine kilichomo kwa wingi ndani yake ni ‘azadirachtin’ ambayo ni moja kati ya kiungo asili cha kuua na kufukuza wadudu chenye nguvu zaidi.

Kama unasumbuliwa na fangasi kwenye ngozi, vipele, chunusi na matatizo mengine kwenye ngozi usitafute dawa nyingine zaidi ya mafuta ya mbegu za mwarobani

Mafuta ya mbegu za mwarobaini yanatibu fangasi, mba, chunusi na ukurutu wa aina yoyote na matatizo karibu yote ya ngozi

Unaweza pia kuwapakaa watoto

Mafuta ya mbegu za Mwarobaini

1. HUTIBU MBA KICHWANI

Mafuta ya mwarobaini ni kitu kinachoongezwa karibu katika shampoo zote unazozifahamu.

Kupakaa mafuta ya mwarobaini kichwani husaidia kuondoa mba sababu ni dawaa dhidi ya bakteria na fangasi wanaoleta mba.

Mafuta haya pia yanasaidia kuweka sawa usawa wa pH katika ngozi ya kichwa usawa ambao ni mhimu katika kudhibti mba.

2. HUTIBU CHUNUSI

Fangasi

Chunusi ni ugonjwa wa ngozi ambao hujitokeza kama viuvimbe au vipele vidogo vidogo hasa sehemu za uso, kifuani na hata mgongoni.

Vipele hivi hutokea wakati vishimo vya kupitisha jasho katika ngozi vinapozibwa kwa mafuta au seli za ngozi zilizokufa au wadudu yaani bakteria.

Kwa lugha ya kidaktari chunusi huitwa Acne Vulgaris. Chunusi ndio ugonjwa wa ngozi ambao humwathiri binadamu kwa kiasi kikubwa kwa mfano nchini Marekani pekee huathiri watu zaidi ya milioni 17 kila mwaka.

Chunusi huweza kujitokeza katika umri wowote lakini huathiri sana vijana hasa wakati wa balehe (adolescents) kati ya miaka 15 mpaka 26 hivi.

Ni kweli usiopingika kuwa kwa kupakaa mafuta ya mbegu za mwarobaini ni jambo zuri zaidi kwa kutibu chunusi kuliko kutumia losheni na vipodozi vingine vya kizungu ambavyo huweza kuwa na madhara mabaya kwa ngozi ya mtumiaji.

Mafuta ya mbegu za mwarobaini yanawazuia bakteria wanaoleta chunusi wakati huo huo yanasaidia kuondoa madoa na vivimbe kwenye ngozi.

Vitamini E iliyomo kwenye mafuta haya husaidia kutibu na kuripea ngozi iliyodhurika na miale ya jua huku ikiondoa chunusi na makovu yatokanayo na chunusi.

3. Hutibu maambukizi ya fangasi

Watu wengi hawajisikii vizuri unapokuja wakati wa kuzungumza juu ya fangasi kutokana na namna ugonjwa wenyewe unavyochukuliwa na jamii.

Hii inatokea sababu mara nyingi ugonjwa huu hutokea sehemu ambazo ni aibu kuzizungumzia au kuzionyesha hadharani.

Fangasi mara nyingi inawapata zaidi watu wanaoishi kwenye maeneno ya joto kuliko wale wanaoishi maeneno ya baridi kutokana na vimelea vya ugonjwa wenyewe kushamiri zaidi sehemu za joto.

Pamoja na hayo yote fangasi ni ugonjwa wa kawaida ambao unaweza kumpata mtu yeyote, mimi mwenyewe nimewahi kupatwa na fangasi sehemu za siri na zilinisumbuwa sana.

Takwimu zinadai katika kila watu watano mmoja kati yao anapatwa na maradhi haya.

Hapo awali fangasi walikuwa wanahesabika kama ni aina mojawapo ya mimea lakini baadaye sayansi imekuja kugunduwa kuwa fangasi hawana sifa za kuwekwa katika kundi la mimea.

Kuna fangasi wa aina nyingi lakini tunaweza kuwaweka kwenye makundi makubwa mawili ambao ni fangasi wanaoleta madhara ya kwenye ngozi na fangasi ambao maisha yao yote wanaishi kwenye ngozi wakiitegemea hiyo tu ili waweze kuishi.

Vimelea hivi vya fangasi vinavyokaa kwenye ngozi vimegawanyika tena katika sehemu kuu mbili, kundi la kwanza ni wale wanaojulikana kwa kitaalamu kama dermatophytes au dematofaiti kwa kiswahili na hamira au yeast kwa kiingereza

Kwahiyo kama ulikuwa hufahamu, basi leo fahamu kuwa hamira yaani hamira ile inayotumika wakati wa kupika maandazi na hata mikate ni fangasi.

Fangasi huishi kwenye ngozi kwakuwa hutegemea protini inayopatikana kwenye ngozi iitwayo keratini (keratin).

Vimelea vya fangasi huathiri ngozi moja kwa moja kwa kuvamia na kutafuna keratini ambayo ni protini muhimu ya ngozi ikiwa inatengeneza sehemu kubwa ya ngozi, kucha na nywele.

Mafuta ya mbegu za mwarobaini ni dawa yenye nguvu ya kutibu fangasi ya kwenye ngozi, fangasi ya kwenye kucha na fangasi ya kwenye miguu.

Tafiti zimethibitisha kwa kufanya mafuta ya mbegu za mwarobaini kuwa ndiyo mafuta yako ya kupakaa kila siku utakuwa una kinga ya kutosha dhidi ya fangasi wa aina yoyote.

Fangasi na miwasho yoyote sehemu yoyote ya mwili itaacha yenyewe bila kupenda mara tu uanzapo kupakaa mafuta haya.

Ikiwa kwa upande wako fangasi wanakutokea kama matokeo ya kinga ya mwili kushuka basi tuwasiliane uweze kupata mafuta ya mwarobaini sambamba na dawa ya kuimarisha kinga yako ya mwili na kudhibiti pia fangasi ya kwenye damu.

4. Huzuia kuzeeka mapema

Kuondoa mikunjo kwenye ngozi
Mafuta ya Mbegu za Mwarobaini

Ngozi ikipigwa na miale ya jua kwa miaka mingi inaweza kudhurika na kukupelekea kuonekana una umri mkubwa au mzee wakati wewe bado ni kijana.

Miale ya jua inaweza kupenyeza kwenye ngozi na kuharibu muonekano wake hivyo uonekane kama wewe ni mtu mzima sana kumbe bado ni kijana.

Siyo hayo tu, miale ya mwanga wa jua hurundika pia juu ya ngozi yako vijidudu nyemelezi ambavyo mwisho wa siku vinaweza kukuletea saratani ya ngozi.

Hata kama unavaa nguo kufunika mwili wote, unapakaa losheni maalumu kuzuia jua lisipige moja kwa moja kwenye ngozi yako au unavaa miwani maalumu kuzuia hii miale ya jua, bado hivyo vyote havilizuii jua kujipenyeza kwenye ngozi yako na kuleta madhara.

Mafuta ya mbegu za mwarobaini yana kinga ya asili dhidi ya saratani ya ngozi, yanapunguza makali ya miale ya jua kudhuru ngozi yako huku yakizuia aleji yoyote ya ngozi.

Utafiti wa mwaka 2011 uliofanywa na chuo kikuu cha Kwame Nkrumah ulihitimisha kuwa mafuta ya mbegu za mwarobaini huhamasisha uzalishwaji wa ‘collagen’ juu ya ngozi ambayo inahusika na kuzuia ngozi isionekane imezeeka.

Wanasayansi katika chuo hiki walihitimisha kuwa vitamini E iliyomo kwenye mafuta ya mbegu za mwarobaini inafanya kazi kama muondoa vijidudu nyemelezi kwenye ngozi, inahamasisha uundwaji wa ngozi laini, husaidia kuondoa makovu ya zamani na kuhamasisha uponyaji wa ngozi kwa madhara yoyote iliyonayo.

5. Mafuta mazuri kwa wenye ngozi kavu

Mafuta kwa watu wenye ngozi kavu
Mbegu za Mwarobaini

Mafuta ya mbegu za mwarobaini yanayo vitamini mhimu kwa ngozi, vitamini E pia yana asidi mafuta mhimu sana na tafiti zinasema sababu ya hii vitamini na hizi asidi mafuta mhimu mafuta haya yanapenyeza kwenye ngozi na kuifanya yenye unyevunyevu na hivyo kukuondolea tatizo la kuwa na ngozi kavu ndani ya dakika kadhaa tu tangu ujipake.

Kwenye losheni nyingi za viwandani kwa ajili ya watu wenye ngozi kavu mafuta ya mbegu za mwarobaini huongezwa ndani yake wakati wa kutengeneza hizo losheni.

Sasa huhitaji tena losheni ya dukani bali kitu cha asili kwa asilimia 100 ambayo ni mafuta ya mbegu za mwarobaini kwa tatizo lako la ngozi kavu.

Mafuta haya ni kondishina ya ngozi ya asili, ni msaada kwa watu wanaoosha ngozi zao mara kwa mara na kuwa na ngozi kavu.

Mafuta haya yanajenga ukuta juu ya ngozi na kuifanya ionekane laini, yenye unyevunyevu na muonekano wake wa asili.

6. Hufukuza chawa kichwani

Hakuna kitu kinaudhi kuwa nacho kama chawa.

Mafuta ya mbegu za Mwarobaini yana kiua wadudu WOTE warukao na watambaao cha asili kijulikanacho kama ‘azadirachtin’.

Dawa nyingi za viwandani za kuua chawa ndani yake huongezwa pia mafuta ya mbegu za mwarobaini kwa kuwa yana sifa ya kipekee ya asili ya kuua wadudu lakini shida ni kuwa dawa hizo zina kemikali nyingine ambazo zinaweza kuwa na madhara mengine mabaya kwenye ngozi ya kichwa na mwili kwa ujumla.

Chawa kwa kawaida hawawezi kuishi karibu na harufu ya mafuta ya mbegu za mwarobaini.  

Chawa wanaichukia harufu ya mbegu za mwarobaini na unapopakaa tu haya mafuta iwe kichwani au mwilini basi chawa hawana namna nyingine zaidi ya kukuacha na kuondoka kwenda mbali na wewe.

Hii ndiyo dawa pekee ya asili ya kuua na kuwafukuza chawa kichwani, kwenye nguo zako na mwilini ya uhakika itakayowakimbiza chawa maishani mwako milele.

Kama utahitaji tuwasiliane WhatsApp +255714800175

Soma pia hii > Dawa ya saratani ya tezidume

SHARE post hii kwa ajili ya wengine uwapendao

Imesomwa mara 350

Imehaririwa


Niulize swali hapo kwenye comment nikujibu
WhatsApp Chat na mimi kwenye WhatsApp