Dawa ya chunusi

Published by Fadhili Paulo on

Dawa ya asili inayotibu chunusi

Chunusi ni ugonjwa wa ngozi ambao hujitokeza kama viuvimbe au vipele vidogo vidogo hasa sehemu za uso, kifuani na hata mgongoni.

Vipele hivi hutokea wakati vishimo vya kupitisha jasho katika ngozi vinapozibwa kwa mafuta au seli za ngozi zilizokufa au wadudu yaani bakteria.

Chunusi ndio ugonjwa wa ngozi ambao humwathiri binadamu kwa kiasi kikubwa kwa mfano nchini Marekani pekee huathiri watu zaidi ya milioni 17.

Chunusi huweza kujitokeza katika umri wowote lakini huathiri sana vijana hasa.

Dawa ya asili ya chunusi > Mafuta ya Mbegu za mlonge

Mafuta ya mbegu za mlonge yamekuwa yakisifiwa kama mafuta mapya yenye miujiza ndani yake.

Ni bidhaa mpya kwa hakika.

Yamekuwa yakitumika kwa ajili ya afya na urembo kwa karne na karne.

Mti wa mlonge ambao ndiyo huzalisha mbegu za mlonge zinazotumika kutengeneza mafuta ya mbegu za mlonge hujulikana pia kama ‘Mti wa Miujiza’ na wengine huuita ‘mti wa uzima’ sababu ya faida na matumizi yake mengi yasiyokuwa na mwisho.

Ni chanzo cha viinilishe vingi mhimu kwa ajili ya mwili zaidi ya viinilishe 92 ndani yake.

Karibu kila sehemu ya mti huu inaweza kutumika kama chakula na dawa.

Ni mti ambao umekuwa ukitumika kutibu matatizo ya utapiamlo (matatizo yatokanayo na lishe duni) katika nchi nyingi maskini.

Ni mti ambao umeandikwa mara nyingi zaidi kuliko mti mwingine wowote katika majarida mbalimbali ya kisayansi na madawa duniani kote mpaka sasa.

Kuna aina nyingi za miti jamii ya mlonge zaidi ya aina 13 tofauti, bali mlonge ambao hutumika hasa kama dawa ni mlonge ujulikanao kama ‘moringa oleifera’.

Ni mti wenye asili ya milima ya Himalaya.

Hutumika kama chakula na tiba katika taratibu mbalimbali za tiba za Kihindi (ayurvedic medicine).

Ni mti unaojulikana karibu katika kila pembe ya dunia.

Zaidi ya kutumika kama dawa ya asili, sehemu mbalimbali za mti huu zinatumika pia kwa ajili ya matumizi mbalimbali ikiwemo kutumika kama chanzo cha nishati na kama kilainishi (lubricant) kwenye mashine mbalimbali.

Mafuta ya mbegu za mlonge hujulikana pia kama “ben oil” au “behen oil” sababu yana kiasi kingi cha asidi mafuta behenic.

Sababu ya viondoa sumu (antioxidants) vilivyomo kwenye mafuta haya mafuta ambayo hutumika pia kuhifadhia vitu visiharibike (preservatives), sababu mafuta haya ni mafuta safi, sababu ni mafuta yasiyoharibika kwa muda mrefu mpaka miaka mitano tangu yalipotengenezwa; yanakuwa ndiyo dawa bora zaidi ya kutibu chunusi karibu kwa kila aina ya ngozi.

Ni mafuta yenye viinilishe vingi, yana kiasi kingi cha palmitoleic, asidi oleic na linoleic, yanalainisha ngozi na kuiongezea ngozi vitamini A na C.

Mafuta ya mbegu za Mlonge ndiyo siri kubwa ya urembo ya miaka mingi iliyopita

Katika zama za kale za Warumi, Wagiriki na Wamisri mafuta ya mbegu za mlonge yalitumika kama pafyumu na kama dawa ya ulinzi dhidi ya matatizo mbalimbali ya ngozi. Mafuta haya pia hutumika kuotesha au kukuza nywele.

Katika nchi ya Misri mafuta haya tangu karne na karne yamekuwa yakitumika kama dawa na kama msaada mkubwa kwa kulinda afya za ngozi kwa watu wanaoishi maeneo yenye jangwa.

Mafuta ya mbegu za mlonge yalitumika kama dawa ya kila siku kutibu makunyanzi au tatizo la mikunjo ya ngozi na hiyo ndiyo sababu wafalme wengi wa enzi hizo waliagiza kabla hawajafa kwamba katika makaburi yao wazikwe pia na chupa ya mafuta ya mbegu za mlonge kwa imani kwamba watakapofufuka waendelee pia kutumia mafuta haya.

Dawa ya chunusi

Faida za mafuta ya mlonge kwa ngozi

Mafuta ya Mbegu za Mlonge ni kitu ambacho huongezwa karibu katika kila vipodozi vya viwandani kwa ajili ya ngozi sababu ya uwezo wake wa kuifanya ngozi kuwa ya unyevunyevu, uwezo wake wa kuisafisha ngozi na kama dawa pia ya kulainisha ngozi.

Kwenye bidhaa nyingi za urembo za dukani kama vile shampoo ya nywele, losheni, mafuta ya ngozi, lisptiki, dawa za kuzuia uzee, dawa za kuondoa mikunjo katika ngozi, krimu za uso, sabuni, pafyumu, dawa za kuondoa harufu sehemu mbalimbali za mwili, mafuta ya kuchua (masaji) na bidhaa nyingi za kutibu matatizo mbalimbali ya ngozi za dukani mafuta ya mbegu za mlonge lazima yawemo.

Mafuta ya mbegu za mlonge yanaiingia ngozi mpaka ndani kiurahisi na kuboresha afya na muonekano wa ngozi.

Mafuta haya yana viinilishe bora na mhimu kwa ajili ya ngozi ikiwemo vitamini A ambayo ni mhimu katika uundwaji wa seli za ngozi.

Dawa ya asili inayotibu chunusi

Mafuta haya pia yana vitamini C ambayo husaidia kuondoa mistari na mikunjo katika ngozi, yanaondoa uvimbe na pia ni chanzo kingine kizuri cha vitamini nyingine mhimu kwa ajili ya ngozi Vitamini E.

Kile watu wengi hawafahamu kuhusu chunusi ni kuwa chunusi zina uhusiano wa karibu na ubora wa kinga yako ya mwili. Chunusi wakati mwingine zinaweza kuwa ni ishara ya kushuka kwa kinga yako ya mwili.

Mafuta ya mbegu za mlonge yamethibitika kisayansi kama ni dawa bora ya kuongeza kinga ya mwili

Chunusi pia ni ishara ya uchafu na mafuta katika ngozi.

Mbegu za mlonge hutumika kama dawa ya asili ya kusafisha maji isiyo na madhara, hufanya kazi kama ilivyo dawa ya kusafisha maji ijulikanayo kama Water Guard.

Mafuta ya mbegu za mlonge yanaondoa kila aina ya uchafu na mafuta yaliyozidi ndani ya mwili kama ukiyanywa na huondoa pia uchafu juu ya ngozi unapoyapakaa na hivyo kutumika kama dawa ya kutibu na kuzuia chunusi kwa watu wa rika zote.

Chunusi pia ni ishara ya msongo wa mawazo (stress) tatizo linaloweza kudhibitiwa kirahisi kwa kutumia mafuta ya mbegu za mlonge mara kwa mara.

Kwa mtu mwenye ngozi kavu, mafuta ya mbegu za mlonge :

*Yanalainisha ngozi na kuiacha yenye unyevunyevu muda wote
*Yanalainisha midomo mikavu (dry lips).
*Ni mazuri kwa magonjwa mengi ya ngozi, ngozi kavu, ukurutu, fangasi nk.
*Mafuta ya mbegu za mlonge yanazuia kuzeeka mapema
*Yanairudisha upya ngozi iliyoanza kufifia na kuchoka
*Yana viondoa sumu na husaidia kupigana dhidi ya vijidudu nyemelezi ambavyo vingeweza kusababisha kudhurika kwa ngozi na kupelekea kuundwa kwa mikunjo na michirizi katika ngozi
*Mafuta ya mbegu za mlonge yanasaidia kuponya mikunjo katika ngozi
*Mafuta ya mbegu za mlonge yana homoni itokanayo na mimea ijulikanayo kwa kitaalamu kama ‘cytokinins’ ambayo yenyewe kazi yake hasa ni kuhamasisha ukuwaji wa seli na kuzuia uharibifu wa seli za ngozi.
*Vitamini C ipatikanayo katika mafuta ya mbegu za mlonge husaidia kuweka sawa seli za ngozi, kuondoa mikunjo na kuziripea tishu za ngozi zilizoharibika.
*Kama unasumbuliwa na chunusi haijalishi zimekusumbuwa kwa muda gani, pakaa kila siku mafuta ya mbegu za mlonge kwenye ngozi yako ya mwili mzima na pia kunywa mafuta haya kijiko kidogo kimoja cha chai kutwa mara 1 kwa wiki 3 mpaka 4 na tatizo lako la chunusi litakuwa limeisha.

Unaweza kuendelea kupakaa mafuta haya au hata kuyanywa kila mara kama kinga yako hata unapokuwa huumwi chochote

Kama unahitaji mafuta safi, salama na ambayo hayajachakachuliwa ya mbegu za mlonge niachie ujumbe kwenye WhatsApp +255714800175.

Ni mafuta mazuri kwa tatizo lolote la ngozi ikiwemo chunusi, madoa doa, mikunjo, ngozi kuzeeka mapema, kuondoa makovu, mba, fangasi na kadharika na kadharika

Mambo mhimu ya kuzingatia:

1. Fanya mazoezi ya viungo kwa saa moja kila siku
2. Kunywa maji mengi kila siku
3. Ondoa mfadhaiko (stress)
4. Weka homoni sawa kama hazipo sawa
5. Kuwa msafi wa mwili wote kila mara
6. Usiziguse chunusi au kuzitoboa na mikono yako au na chochote kuepuka makovu yasiyo ya lazima
7. Epuka vyakula vifuatavyo kama unasumbuliwa na chunusi kila mara, navyo ni pamoja na:

a)Vyakula vyenye mafuta sana

b)Vyakula vinavyopikwa katikati ya mafuta mengi

c)Kahawa

d)Chai ya rangie)

e)Pombe na vilevi vingine

f)Chokoleti

g)Popcorn

h)Maziwa

i)Mapera

j)Vyakula vya kwenye makopo

k)Pizza

Kama utahitaji dawa hii kwa ajili ya chunusi niachie ujumbe WhatsApp +255714800175

Yote katika YOTE nitashukuru SANA kama utachukuwa uamuzi wa ku SHARE post hii na rafiki zako wengine.

(Visited 36 times, 1 visits today)

0 Comments

Leave a Reply

Avatar placeholder

Your email address will not be published.

WhatsApp WhatsApp +255714800175