Dawa ya fangasi, mba, chunusi, upele na ngozi kavu

Published by Fadhili Paulo on

DAWA YA FANGASI, MBA, CHUNUSI, UPELE NA NGOZI KAVU

Kama hujawahi kuisikia hii dawa kongwe ya mafuta ya mbegu za mwarobaini, basi ni wakati muafaka sasa upate kufahamu habari zake hasa kwa matatizo ya ngozi

Mwarobaini ni mti wenye asili ya India hujulikana pia kama Indian lilac, Azadirachta Indica, au ‘Neemba’ na umekuwa ukitumika katika tiba asili za kihindi (Ayurvedic medicine) zaidi ya miaka 5000 iliyopita.

Kwa kawaida mti huu unapatikana karibu katika kila nyumba huko India.

Unasadikika kutibu magonjwa mbalimbali 40 hasa majani yake, huku mbegu zake ndiyo hutumika kutengeneza mafuta ambayo ni dawa kwa matatizo mbalimbali ya ngozi.

Ukishaota unao uwezo wa kuendelea kudumu kwa zadi ya miaka 200.

Ni kiungo mhimu kwenye bidhaa nyingi kama losheni, dawa za kuulia wadudu, sherehe za kidini na mengine mengi. Taarifa zisizo rasmi zinasema majani ya mti huu ukiyachemsha katika maji na kuyaoga mara kwa mara husaidia kuondoa mikosi na nuksi mbalimbali.

Mwarobaini una viinilishe mhimu kwa ajili ya mwili zaidi ya 100 na una uwezo mkubwa wa kutibu maradhi zaidi ya 40. Hujulikana pia kama mti wa uzima.

Moja ya vitu vilivyomo kwenye mafuta haya ni pamoja na vitamini E, nimbidin na nimbin, carotenoids, linoleic acid, oleic acid, vitamini C, quercetin na kingine kilichomo kwa wingi ndani yake ni ‘azadirachtin’ ambayo ni moja kati ya kiungo asili cha kuua na kufukuza wadudu chenye nguvu zaidi.

Kama unasumbuliwa na fangasi kwenye ngozi, vipele, chunusi na matatizo mengine kwenye ngozi usitafute dawa nyingine zaidi ya mafuta ya mbegu za mwarobani

Mafuta ya mbegu za mwarobaini yanatibu fangasi, mba, chunusi na ukurutu wa aina yoyote na matatizo karibu yote ya ngozi

Unaweza pia kuwapakaa watoto

Mafuta ya Mbegu za Mwarobaini

1. HUTIBU MBA KICHWANI

Mafuta ya mwarobaini ni kitu kinachoongezwa karibu katika shampoo zote unazozifahamu. Kupakaa mafuta ya mwarobaini kichwani husaidia kuondoa mba sababu ni dawaa dhidi ya bakteria na fangasi wanaoleta mba.

Mafuta haya pia yanasaidia kuweka sawa usawa wa pH katika ngozi ya kichwa usawa ambao ni mhimu katika kudhibti mba.

2. HUTIBU CHUNUSI

Ni kweli usiopingika kuwa kwa kupakaa mafuta ya mbegu za mwarobaini ni jambo zuri zaidi kwa kutibu chunusi kuliko kutumia losheni na vipodozi vingine vya kizungu ambavyo huweza kuwa na madhara mabaya kwa ngozi ya mtumiaji.

Mafuta ya mbegu za mwarobaini yanawazuia bakteria wanaoleta chunusi wakati huo huo yanasaidia kuondoa madoa na vivimbe kwenye ngozi.

Vitamini E iliyomo kwenye mafuta haya husaidia kutibu na kuripea ngozi iliyodhurika na miale ya jua huku ikiondoa chunusi na makovu yatokanayo na chunusi.

3. Hutibu maambukizi ya fangasi

Watu wengi hawajisikii vizuri unapokuja wakati wa kuzungumza juu ya fangasi kutokana na namna ugonjwa wenyewe unavyochukuliwa na jamii. Hii inatokea sababu mara nyingi ugonjwa huu hutokea sehemu ambazo ni aibu kuzizungumzia au kuzionyesha hadharani.

Fangasi mara nyingi inawapata zaidi watu wanaoishi kwenye maeneno ya joto kuliko wale wanaoishi maeneno ya baridi kutokana na vimelea vya ugonjwa wenyewe kushamiri zaidi sehemu za joto.

Pamoja na hayo yote fangasi ni ugonjwa wa kawaida ambao unaweza kumpata mtu yeyote, mimi mwenyewe nimewahi kupatwa na fangasi sehemu za siri na zilinisumbuwa sana. Takwimu zinadai katika kila watu watano mmoja kati yao anapatwa na maradhi haya katika safari yake ya kuishi kwa hapa Tanzania.

Hapo awali fangasi walikuwa wanahesabika kama ni aina mojawapo ya mimea lakini baadaye sayansi imekuja kugunduwa kuwa fangasi hawana sifa za kuwekwa katika kundi la mimea.

Kuna fangasi wa aina nyingi lakini tunaweza kuwaweka kwenye makundi makubwa mawili ambao ni fangasi wanaoleta madhara ya kwenye ngozi na fangasi ambao maisha yao yote wanaishi kwenye ngozi wakiitegemea hiyo tu ili waweze kuishi.

Vimelea hivi vya fangasi vinavyokaa kwenye ngozi vimegawanyika tena katika sehemu kuu mbili, kundi la kwanza ni wale wanaojulikana kwa kitaalamu kama dermatophytes au dematofaiti kwa kiswahili na hamira au yeast kwa kiingereza

Kwahiyo kama ulikuwa hufahamu, basi leo fahamu kuwa hamira yaani hamira ile inayotumika wakati wa kupika maandazi na hata mikate ni fangasi. Fangasi huishi kwenye ngozi kwakuwa hutegemea protini inayopatikana kwenye ngozi ambayo huitwa keratini (keratin).

Keratini ni protini ya muhimu sana katika ngozi na inatengeneza asilimia kubwa ya ngozi, kucha na nywele ambako kama umeshagundua mpaka sasa ni sehemu ambazo fangasi hupenda sana kushambulia kuliko sehemu nyingine za mwili.

Kwahiyo utagundua kuwa sababu kubwa ya waTanzania wengi kuugua fangasi ni hii protini ya kwenye ngozi ijulikanayo kama keratini, joto na uwepo wa hali ya unyevu unyevu katika maeneno mengi hasa ukanda wa pwani.

Kwa hali ya kawaida, fangasi wa aina hii huwa hawana madhara makubwa, wao huweka makazi yao tu kwenye ngozi bila kusababisha hali yoyote ya madhara kwenye ngozi. Madhara ya vimelea hivi huonekana baada ya idadi kubwa ya vimelea hivi kuongezeka kwenye eneo dogo moja la ngozi.

Fangasi ni ugonjwa unaoambukiza kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine ikiwa watu hao watashirikiana mavazi na vifaa vingine vya usafi wa mwili.

Madhara ya Fangasi katika ngozi

Vimelea vya fangasi huathiri ngozi moja kwa moja kwa kuvamia na kutafuna keratini ambayo ni protini muhimu ya ngozi ikiwa inatengeneza sehemu kubwa ya ngozi, kucha na nywele.

Mafuta ya mbegu za mwarobaini ni dawa yenye nguvu ya kutibu fangasi ya kwenye ngozi, fangasi ya kwenye kucha na fangasi ya kwenye miguu.

Tafiti zimethibitisha kwa kufanya mafuta ya mbegu za mwarobaini kuwa ndiyo mafuta yako ya kupakaa kila siku utakuwa una kinga ya kutosha dhidi ya fangasi wa aina yoyote.

Fangasi na miwasho yoyote sehemu yoyote ya mwili itaacha yenyewe bila kupenda mara tu uanzapo kupakaa mafuta haya.

Ikiwa kwa upande wako fangasi wanakutokea kama matokeo ya kinga ya mwili kushuka basi tuwasiliane uweze kupata mafuta ya mwarobaini sambamba na dawa ya kuimarisha kinga yako ya mwili na kudhibiti pia fangasi ya kwenye damu.

4. Huzuia kuzeeka mapema

Ngozi ikipigwa na miale ya jua kwa miaka mingi inaweza kudhurika na kukupelekea kuonekana una umri mkubwa au mzee wakati wewe bado ni kijana.

Miale ya jua inaweza kupenyeza kwenye ngozi na kuharibu muonekano wake hivyo uonekane kama wewe ni mtu mzima sana kumbe bado ni kijana.

Siyo hayo tu, miale ya mwanga wa jua hurundika pia juu ya ngozi yako vijidudu nyemelezi ambavyo mwisho wa siku vinaweza kukuletea saratani ya ngozi.

Hata kama unavaa nguo kufunika mwili wote, unapakaa losheni maalumu kuzuia jua lisipige moja kwa moja kwenye ngozi yako au unavaa miwani maalumu kuzuia hii miale ya jua, bado hivyo vyote havilizuii jua kujipenyeza kwenye ngozi yako na kuleta madhara.

Mafuta ya mbegu za mwarobaini yana kinga ya asili dhidi ya saratani ya ngozi, yanapunguza makali ya miale ya jua kudhuru ngozi yako huku yakizuia aleji yoyote ya ngozi.

Utafiti wa mwaka 2011 uliofanywa na chuo kikuu cha Kwame Nkrumah ulihitimisha kuwa mafuta ya mbegu za mwarobaini huhamasisha uzalishwaji wa ‘collagen’ juu ya ngozi ambayo inahusika na kuzuia ngozi isionekane imezeeka.

Wanasayansi katika chuo hiki walihitimisha kuwa vitamini E iliyomo kwenye mafuta ya mbegu za mwarobaini inafanya kazi kama muondoa vijidudu nyemelezi kwenye ngozi, inahamasisha uundwaji wa ngozi laini, husaidia kuondoa makovu ya zamani na kuhamasisha uponyaji wa ngozi kwa madhara yoyote iliyonayo.

5. Mafuta mazuri kwa wenye ngozi kavu

Mafuta ya mbegu za mwarobaini yanayo vitamini mhimu kwa ngozi, vitamini E pia yana asidi mafuta mhimu sana na tafiti zinasema sababu ya hii vitamini na hizi asidi mafuta mhimu mafuta haya yanapenyeza kwenye ngozi na kuifanya yenye unyevunyevu na hivyo kukuondolea tatizo la kuwa na ngozi kavu ndani ya dakika kadhaa tu tangu ujipake.

Kwenye losheni nyingi za viwandani kwa ajili ya watu wenye ngozi kavu mafuta ya mbegu za mwarobaini huongezwa ndani yake wakati wa kutengeneza hizo losheni.

Sasa huhitaji tena losheni ya dukani bali kitu cha asili kwa asilimia 100 ambayo ni mafuta ya mbegu za mwarobaini kwa tatizo lako la ngozi kavu.

Mafuta haya ni kondishina ya ngozi ya asili, ni msaada kwa watu wanaoosha ngozi zao mara kwa mara na kuwa na ngozi kavu.

Mafuta haya yanajenga ukuta juu ya ngozi na kuifanya ionekane laini, yenye unyevunyevu na muonekano wake wa asili.

,Mbegu za Mwarobaini

Kama utahitaji dawa hii kwa ajili ya chunusi au fangasi tuwasiliane WhatsApp +255714800175. Natuma pia popote ulipo nje ya Dar.

Naitwa Fadhili Paulo ni Tabibu wa Tiba Asili, Ofisi yangu inaitwa VICTORIA HOME REMEDY ipo Sigara Yombo Vituka Temeke Dar Es Salaam karibu na ofisi ya Tanesco ya Yombo.

Kama utashea ujumbe huu na rafiki zako wengine uchukuwe kama ulivyo usibadili chochote.

SHARE post hii kwa ajili ya wengine uwapendao

Fadhili Paulo

Fadhili Paulo

Naitwa Fadhili Paulo, ni Tabibu wa Tiba asili. Ninayo ofisi yangu binafsi Jijini Dar Es Salaam. lakini nafanya pia kazi kwa njia ya mtandao. Ofisi yangu inaitwa TUMAINI HERBAL LIFE, Ipo Kibugumo Mji Mwema Kigamboni Kama unahitaji kuonana na mimi uso kwa uso weka miadi (appointment) kupitia WhatsApp +255714800175

0 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published.

WhatsApp WhatsApp +255714800175