Siku za kuwa mwezini kwa kawaida kwa mwanamke huwa ni kati ya siku 3 mpaka 7.

Hata hivyo hutokea kwa baadhi ya wanawake hasa wale wenye umri mkubwa wanapata hedhi kwa siku nyingi zaidi ya siku 7 na huambatana na kupata damu nzito na yenye mabonge mabonge sambamba na maumivu makali.

Tatizo hili kitaalamu hujulikana kama ‘Menorrhagia’, na ni tatizo ambalo mara nyingi hutokana na homoni kutokuwa sawa, uvimbe kwenye kizazi, maambukizi kwenye kizazi, matumizi ya baadhi ya dawa za uzazi wa mpango nk

Ikiwa unahitaji kufahamu namna ya kutibu tatizo hili la hedhi isiyoisha basi endelea kusoma makala hii kwani ina jibu la tatizo lako.

Nini husababisha kupata hedhi isiyoisha?

Sababu ya kupata hedhi isiyoisha au inayojirudia mara 2 au 3 ndani ya mwezi hutofautiana toka mwanamke mmoja hadi mwingine.

Ikiwa unatokewa na tatizo hili ni mhimu kuonana na daktari mapema kwa uchunguzi na msaada zaidi.

Sababu za tatizo hili ni pamoja na hizi zifuatazo:

1. Homoni kutokuwa sawa
2. Uvimbe kwenye kizazi
3. Ujauzito kutoka
4. Mimba kutunga nje ya kizazi
5. Baadhi ya saratani (saratani ya shingo ya kizazi)
6. Matatizo kwenye mirija ya mayai ya uzazi

Dawa zinazotibu tatizo la hedhi isiyoisha

Ninakutaka utumie dawa hizi tatu kwa pamoja kwa maana moja utatumia asubuhi, nyingine mchana na nyingine jioni kwa kipindi chote unachosumbuliwa na tatizo hili mpaka utakapokuwa umepona.

1. Unga wa Mbegu za Mharadali

Wanawake hujisikia vibaya au kuumwa kabisa wakati wakiwa kwenye siku zao sababu ya kiasi kingi cha usawa wa homoni ya estrogen na homoni kutokuwa sawa.

Mbegu za Mharadali zina kiasi kingi cha omeaga 3 ambayo husaidia kuweka sawa mzunguko na homoni.

Asubuhi ukiamka chukua kijiko kikubwa kimoja cha unga wa mbegu za mharadali na uchanganye na maji ya uvuguvugu au kwenye kikombe kimoja cha maziwa ya moto na unywe.

Hii ni moja ya dawa rahisi nay a uhakika ya kutibu tatizo la damu isiyoisha au kuokwa na damu nyingi na yenye mabonge mabonge ukiwa kwenye siku zako.

2. Unga wa Mbegu za Uwatu

Mbegu za uwatu ni moja ya dawa nyingine za asili ambazo hutumika kuweka sawa homoni hasa homoni ya estrogeni

Ni dawa nzuri pia kutumiwa na wamama ambao wamefika ukomo wa siku zao. Ni moja ya dawa nzuri za asili za kutibu tatizo la damu isiyokoma.

Chukua unga wa mbegu za uwatu kijiko kidogo kimoja cha chai na uchanganye na maji ya uvuguvugu au kwenye maziwa ya moto nusu saa kabla ya chakula cha mchana.

3. Siki ya Tufaa

Vivimbe kwenye kizazi au kwenye mirija ya mayai (PCOS) vinaweza kusababisha kuvurugika kwa homoni na ni moja ya sababu ya kupata tatizo la hedhi isiyoisha

Tafiti zimeonyesha kuwa matumizi ya siki ya tufaa kuwa na matokeo mazuri kwa wanawake wenye vivimbe kwenye kiazi na katika mirija ya uzazi na amabao pia wanapata hedhi isiyoisha au inayojirudiarudia.

Wanawake wanaotumia siki ya tufaa wanaripoti kuongezeka uwezo wao wa kushika ujauzito, kupata mzunguko wa hedhi mzuri na kutopata maumivu wakati wakiwa kwenye siku zao.

Kunywa kijiko kikubwa kimoja cha siki ya tufaa ndani ya maji glasi moja nusu saa kabla ya chakula cha usiku.

Pendelea vyakula vifuatavyo ili kurahisisha matibabu yako:

1. Kula zaidi vyakula vyenye madini ya chuma

Madini ya chuma ni viinilishe mhimu mwili unavihitaji. Kutokwa na damu nyingi au isiyoisha wakati wa hedhi hupelekea kupungua kwa madini ya chuma mwilini na kukusababishia damu kupungua mwilini

Kula zaidi spinachi, karoti, maharage, samaki wa baharini, zabibu kavu, brokoli nk

2. Kula zaidi vyakula vyenye madini ya Magnesium

Kula zaidi ndizi, mtindi na unga wa mbegu za maboga. Kumbuka kuzidisha sana vyakula vyenye madini ya magnesium huleta tatizo la kuharisha hivyo usizidishe.

3. Kula zaidi vyakula vyenye Omega-3

Wanawake wanaopata tatizo la hedhi isiyoishawanapaswa kuongeza ulaji wa vyakula vyenye omega 3.

Omega 3 huhamasisha uzalishwaji wa homoni zenye umhimu na faida zaidi mwilini

Uongezekaji wa uzalishwaji wa homoni mbaya (bad prostaglandings) huchangia kiasi kikubwa kupata hedhi yenye damu nyingi na isiyoisha

Uongezekaji wa uzalishwaji wa homoni nzuri hupunguza damu kuganda kusiko kwa kawaida na kuondoa tatizo la damu ya hedhi isiyoisha.

Omega 3 hupatikana kwa wingi kwenye samaki wa baharini, nazi, mayai, mbegu za maboga nk

4. Kula zaidi papai

Papai lina kimeng’enya kijulikanacho kama ‘papain’ amabacho huidhibiti homoni ya progesterone ambayo hutumika kuandaa mji wa uzazi kwa ajili ya kushika na kuutunza ujauzito.

Kula papai kila siku kunasaidia kulainisha misuli ya tumbo na kuweka sawa kukazika na kutanuka kwa mji wa uzazi jambo ambalo hudhibiti utokaji wa damu ukiwa kwenye siku zako.

5. Kunywa chai ifuatayo kila siku asubuhi

Tumia chai iliyoandaliwa kutokana na kijiko kidogo kimoja kimoja cha unga cha dawa zifuatazo; tangawizi, unga wa majani ya mlonge, mdalasini na kotimiri (parsley) bila kuongeza majani ya chai na utumie asali badala ya sukari kwenye chai hii kwa matokeo mazuri zaidi.

Muunganiko wa chai hii huufanya mwili kuwa na joto na hivyo kupunguza maumivu wakati wa siku zako, kusaidia kukata damu isiyoisha, kuongeza kinga ya mwili na kuweka sawa homoni.

Mambo mengine mhimu ya kuzingatia ili kupona tatizo hili:

• Pata muda wa kutosha wa kupumzika
• Kula vyakula vyenye afya na vya asili zaidi
• Usitumia chai ya rangi, kahawa na soda yoyote au kinywaji kingine chochote chenye kaffeina
• Punguza kidogo chumvi kwenye chakula
• Usitumie vidonge au dawa yoyote ya hospitali ya kuondoa maumivu
• Onana na daktari mara tu upatapo tatizo hili kwa uchunguzi na msaada zaidi

Ikiwa utahitaji dawa hizi niachie ujumbe WhatsApp +255714800175

Share post hii na jamaa zako wengine uwapendao

Naitwa Fadhili Paulo, ni Tabibu wa Tiba Asili na ni mTanzania.

Ofisi yangu inaitwa Victoria Home Remedy ipo Sigara Yombo Vituka Temeke Dar Es Salaam.

Jiunge na mimi na watu wengine zaidi ya 94000 kwenye ukurasa wangu wa facebook kwa kubonyeza hapa

Imehaririwa mara ya mwisho

Niulize swali nikujibu


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WhatsApp Chat na mimi kwenye WhatsApp