Kumbuka, ile hali ya kuonekana umezeeka au mwili wako kuonekana umechoka mara zote huwa kuna uhusiano wa moja kwa moja na kushuka kwa kinga yako ya mwili hali ambayo inauacha mwili wako kushambuliwa kirahisi na vijidudu nyemelezi na magonjwa mbalimbali.

Kama unataka kuishi vizuri kila siku basi jifunze namna kinga yako ya mwili inavyoweza kuongezwa kila siku kadri unavyoendelea kuishi.

Dawa ya Kuongeza Kinga ya Mwili > Unga na majani mabichi ya mti wa Mlonge

Mti wa Mlonge

Ili kuongeza na kuimarisha Kinga yako ya mwili utahitaji utumie dawa mbili kwa pamoja, ya kwanza ni majani fresh ya mti wa mlonge na ya pili ni unga wa majani ya mti huu huu mmoja, mlonge. Nitakueleza faida ya kila dawa katika hizi mbili.

Endelea kusoma …

Sasa unaweza kuwa unajiuliza ni nini kinachoufanya mti wa mlonge mti huu wa ajabu kuwa kitu cha thamani SANA katika kuimarisha kinga yako ya mwili na hivyo kujikinga na vijidudu nyemelezi, homa na magonjwa mbalimbali?

Kwanza kabisa mlonge umebarikiwa kuwa na viinilishe vingi zaidi kuliko mti mwingine wowote chini ya jua ukiwa na viinilishe 92 ndani yake, una vitamini nyingi, madini na viondoa sumu mwilini tofauti tofauti 46!

Huu ndiyo ukweli wa kustaajabisha wa mti huu unaoleta afya na maisha.

Kwahiyo nipe nafasi nikueleze kiundani kidogo kuhusu hivi viinilishe katika mti wa mlonge vinavyoufanya kuwa silaha kubwa katika vita yako ya kulinda kinga ya mwili wako na utaona ni kwanini habari hii uisomayo ni dhahabu katika maisha yako.

  1. Majani Mabichi ya Mlonge (Fresh Moringa leaves)
Majani Fresh ya Mlonge
Majani Fresh ya Mlonge

Watu wengi ukiwaambia kinga yangu inashuka lazima hawaataacha kukushauri upendelee kula machungwa, si ndiyo? Hili siyo jipya kwako. Habari mpya kwako ni kuwa majani mabichi (fresh moringa leaves) ya mti wa mlonge yana vitamini C mara 7 ZAIDI YA ILE INAYOPATIKANA KATIKA MACHUNGWA!

Na hivyo mlonge unabaki kuwa ndicho kitu pekee chenye nguvu ya kuondoa sumu mwilini kuwahi kutokea katika historia. Kwakuwa Vitamini C  iliyomo kwenye majani mabichi ya mti wa mlonge ni moja ya viondoa sumu vyenye nguvu zaidi na zaidi ni kuwa ni kiondoa sumu kinachotokana na mti wa asili.

Vitamini C kama wote tujuavyo ni kitu mhimu katika kurejesha kinga ya mwili kwa sababu ni vitamini inayofanya kazi ya kuripea seli za mwili na kinga ya mwili. Zaidi sana vitamini C huimarisha ngozi ya mwili, nywele, fizi, macho na kuongeza nguvu ya jumla ya mwili kwa kuyataja machache mazuri ya vitamini C

Kumbuka nguvu unayoipata kupitia vitamini C hii iliyomo kwenye majani mabichi ya mlonge ni nguvu ya asili ambayo inatokana na majani ya mti wa asili. Ni nguvu yenye ubora zaidi tofauti na ile inayotokana na asali au sukari au mafuta.

Vitamini C husaidia umeng’enywaji wa protini na madini ya chuma. Vitamini C husaidia mwili kuweza kuchukua na kuyatumia kwa kiwango cha juu madini ya chuma kutoka katika vyakula tunavyokula.

Vitamini C husaidia vidonda kupona upesi.

Vitamini C kwenye mti wa Mlonge inapatikana kwa wingi kwenye majani yake yakiwa bado mabichi, yakiwa fresh yaani yawe yametoka moja kwa moja kwenye mti na kuliwa hivyo hivyo. Yasipite masaa matatu tangu umechuma haya majani uwe tayari umeyatumia. Kwahiyo utalazimika kuupanda huu mti nyumbani kwako

Vitamini C ni dawa mhimu katika kuzuia na kutibu saratani mbalimbali.

Tafiti zinaonyesha vitamini C inao uwezo wa kumuua bakteria anayesababisha ugonjwa wa kifua kikuu (TB), Bakteria ambaye ni mbishi kufa kwa kutumia  dawa za kawaida. Soma utafiti huu wa mwaka 2013 hapa utafiti uliohitimisha kuwa kumuongezea mgonjwa kifua kikuu vitamini C kunapelekea kupona haraka kwa ugonjwa huu.

Watu wenye vitamini C ya kutosha wanaaminika kuwa na uwezo mkubwa wa kuhimili magonjwa mbali mbali nyemelezi na kuishi miaka mingi bila kuugua.

Watu hawa wanahitaji vitamini C kwa wingi zaidi kuliko wengine nao ni pamoja na wavuta sigara, watu wasiokula aina nyingi tofauti  za vyakula katika siku, watu wenye matatizo katika mmeng’enyo wa chakula na magonjwa sugu.

Vitamini C ni vitamini ambayo humeng’enywa na mwili kwa kutumia maji (water soluble vitamin).

Mwili hauna uwezo wa kuitengeneza hii vitamini C. Kuna baadhi za vitamini mwili wenyewe unaweza kuzitengeneza lakini siyo vitamini C. Hivyo lazima kila siku uhakikishe unaingiza mwilini mwako vitamini C ya kutosha ili kubaki na kinga nzuri ya mwili na afya bora.

Mwili hauna uwezo wa kuihifadhi Vitamini C. Ni kuwa mwili unaihitaji hii vitamini C kila siku ili kutengeneza kinga ya mwili, lakini mwili ukishaitumia hii vitamini hauwezi kuihifadhi kwa ajili ya kesho tena kama vile unavyoweza kuhifadhi vitamini zingine na hata mafuta.

Hivyo ni vitamini ambayo unapaswa kuhakikisha unakuwa nayo nyumbani kila siku kwa ajili ya matumizi ya kila siku.

Wazungu wenyewe wana mboga mboga kadhaa ambazo wanakula pasipo kupikwa kabisa, yaani zinaliwa mbichi mara nyingi kama kachumbari na hii inawahakikishia afya bora na ndiyo sababu wanaishi miaka mingi

Tafuta kwenye google mboga inaitwa ‘rocket’ au ruccola kwa kitaliano au bonyeza hapa

Ukiacha kula majani fresh moja kwa moja unaweza pia kutengeza juisi yake, angalia video hapa chini;

2. Unga wa Majani ya Mlonge (Moringa leaves powder)

Vitamini A ni moja ya vitamini zinazotajwa kuwa mhimu sana katika kuimarisha kinga ya mwili. Vitamini A ni mhimu kwa watu wanaosumbuliwa na matatizo kama ya kuharisha, upungufu wa kinga mwilini, surua na malaria.

Ukiwaambia watu una upungufu wa vitamini A au macho yako hayaoni vizuri mara zote watakuambia pendelea kula karoti, si ndiyo? Kile ulikuwa hufahamu ni kuwa UNGA WA MAJANI YA MLONGE UNA VITAMINI A MARA 4 ZAIDI YA ILE ILIYOMO KWENYE KAROTI!

Vileviele madini ya chuma (Iron) ni kitu mhimu katika mfumo wa kinga ya mwili ambayo hukuwezesha usipatwe na magonjwa na homa mara kwa mara.

Ukiishiwa madini ya chuma mara nyingi utashauriwa ule sana spinachi. Habari njema kwako ni kuwa unga wa majani ya mlonge UNA MADINI YA CHUMA MARA 25 ZAIDI YA ILE ILIYOMO KWENYE SPINACHI. Unasemaje ndugu msomaji mpaka hapo! Una swali? Pia mlonge una beta-carotene.

Mlonge unaimarisha usawa wa himoglobini katika damu jambo ambalo matokeo yake ni kuimarika kwa kinga yako ya mwili.

Kwa kuongezea mlonge una lundo la vitamini kundi B kuliko mti au mmea mwingine wowote unaoufahamu. Mlonge una vitamini B, B1, B2, B3, B5, B6, B12, D, E, K, folic acid, Kalsiamu (unga wa majani ya mlonge una Kalsiamu mara 17 zaidi ya ile ya maziwa ya ng’ombe), madini ya shaba, potasiamu, magnesia, kromiamu na vitamini, na madini madogo madogo mengine mengi mhimu kwa ajili ya kuimarisha kinga ya mwili.

Mlonge unaondoa msongo wa mawazo (stress). Unga wa majani ya mlonge una kiasi cha kutosha cha vitamini A, B , E, Potasiamu, Kalsiamu na viinilishe vingine vingi.

Kwahiyo kama utaweka mazoea ya kutumia mlonge kila siku itakuwa ni vigumu kwako kupata tatizo la msongo wa mawazo huku ukipata faida nyingine nyingi za mti huu wa ajabu

Kiasi kingi cha madini ya magnesiamu kwenye mlonge ni mhimu kutibu matatizo ya mifupa kwa wamama wanaofika ukomo wa siku zao (miaka 40 hivi kwenda juu).

Magnesiamu madini yapatikanayo kwenye mlonge ni dawa maarufu ya kutuliza akili (Tranquillizer) na kutibu matatizo kama msongo wa mawazo, sononeko, huzuni, hamaki na matatizo mengine ya mvurugiko wa akili.

Msongo wa mawazo yaani stress ni chanzo cha magonjwa mengi mwilini zaidi ya magonjwa 50 na unahusika moja kwa moja katika kushusha kinga ya mwili.

Changanya matunda yote na mboga za majani zote bado viinilishe vyake kwa pamoja haviwezi kuvifikia vile vilivyomo kwenye mlonge! Ni kusema mtu aliyekula matunda na mboga za majani zote bado hatakuwa na afya bora kama yule atakayetumia mlonge tu.

Maajabu yanaendelea …

Kijiko kidogo kimoja cha chai cha unga wa majani ya mlonge kinakutosha kwa siku ukitumia kwenye juisi ya matunda uliyotengeneza mwenyewe nyumbani au katika uji au kwenye supu au kwenye mchuzi nk nk

Mlonge pia una zile amino asidi mhimu 9 za kwenye protini. Elewa tu kwamba mti huu wa maajabu mti wa mlonge na majani yake mti ambao hujulikana pia kama mti wa uzima una viinilishe bora na mhimu zaidi kwa ajili ya kuongeza kinga ya mwili ambavyo siyo rahisi kuvielezea vyote kimoja baada ya kingine

Kwahiyo, kama unasumbuliwa na homa za mara kwa mara au unataka tu kuiweka kinga yako katika ubora wake wa juu kabisa, katika kipindi chochote cha mwaka, basi hakikisha nyumbani kwako hakukosekani unga wa majani ya mlonge kwa ajili yako, watoto wako na wale uwapendao

Mlonge unasafisha mwili wako wote, unasafisha ini, figo, moyo, macho, unaimarisha meno, ngozi na nywele.

Wakati unatumia mlonge unakufanya ujisikie vizuri, ujisikie mpya (fresh) na mwenye nguvu. Watu wengi wanaotumia mlonge huwa ni wenye afya nzuri hata kwa muonekano tu hata wanapokuwa na umri mkubwa zaidi ya miaka 90.

Matatizo mengi ya kiafya ni matokeo ya lishe yenye viinilishe duni au hafifu jambo linalopelekea kuwa na kinga ya mwili isiyo na nguvu kupigana na magonjwa mbalimbali.

Unaporekebisha usawa huo usio sawa wa kinga yako ya mwili kwa kutumia mimea mhimu ya asili hutakawia kuona matokeo mazuri kwenye afya yako.

Uwezo wa mti wa mlonge kuyaweza yote hayo ni kutokana na kuwa na vitamini, madini mbalimbali na viondowaji sumu vingi kuliko mmea mwingine wowote.

Wagonjwa wengi wenye UKIMWI katika sehemu nyingi za afrika magharibi wameripoti kuongezeka kiasi kikubwa cha kinga zao za mwili kiasi cha kutokuhitaji dawa baada ya kutumia mlonge.

Hakika kuna siku utakuja kunishukuru kwa maelezo haya ya bure!

Ili kutengeneza na kuitumia hii ARV ya asili unahitaji:

1.Majani mabichi ya Mlonge

Majani Fresh ya Mlonge
Majani Fresh ya Mlonge

Kula Majani mabichi ya mti wa mlonge ujazo wa kiganja cha mkono wako.

Kata matawi kadhaa kutoka katika mti wa mlonge na uyasafishe kwenye maji yanayotililika.

Kisha chambua kupata majani yake bila fimbo na uchanganye na kachumbari na ule na chakula kingine chochote kama ni ugali na nyama au na samaki aua kama ni mwanaume wa Dar unaweza kula na chipsi au ndizi na mishikaki.

Unaweza pia kuchanganya kwenye mboga yoyote ya majani iliyoiva na kupoa kabisa ikiwa tayari kwenye bakuli. Kumbuka hii vitamini C kwenye majani mabichi ya mlonge haihitaji moto wala jua.

Jinsi ya kuongeza kinga ya mwili
Majani Freshi ya Mlonge

Inatakiwa majani yatumiwe mara tu baada ya kuyakata toka kwenye mti

Kula hivi kutwa mara 1 kila siku wakati wa chakula cha mchana.

Kama utazidisha Vitamini C mwilini unaweza kutokewa na kuharisha na tumbo kuvurugika.

Hata hivyo kuharisha mara 2 au hata 3 kwa siku siyo jambo baya kwa siku 2 au 3 ila kama inakutokea mfululizo kama wiki hivi basi utashauriwa kupunguza au kuacha kutumia dawa hii kwa siku 2 kisha utaendelea siku zinazofuata

Mwanaume mtu mzima anatakiwa kupata mg 90 za vitamini C kila siku. Wakati wanawake watu wazima wanaweza kutumia mg 75 za vitamini C kila siku.

Mwanamke mjamzito anahitaji vitamini C mg 85 kila siku na mg 120 kila siku wakati ananyonyesha.

Mtu mzima anaruhusiwa kutumia mpaka mg 2000 za vitamini C kwa siku.

2. Unga wa Majani ya Mlonge

Unga wa Majani ya Mlonge
Unga wa Majani ya Mlonge

Tumia unga wa majani ya mlonge kijiko kidogo kimoja cha chai kutwa mara 1 kwenye kikombe kimoja cha ama juisi ya matunda uliyotengeneza mwenyewe nyumbani au katika uji au katika mtindi au kwenye supu au kwenye maharage nk. Tumia nusu saa kabla ya chakula cha usiku kila siku.

Wasiliana pia na daktari wako wa karibu kabla ya kuanza kutumia mlonge ikiwa wewe ni mjamzito au una shinikizo la chini la damu.

Hii ndiyo sababu waNigeria waliuita mlonge kwa jina la utani kama “Nebedaya”, ambalo maana yake ni mti USIOKUFA!

Usisahau pia kunywa maji ya kutosha kila siku, kufanya mazoezi ya viungo na kupata muda wa kutosha wa kupumzika.

Kama utahitaji majani mabichi ya mlonge na unga wa majani ya mlonge na upo Dar niachie tu ujumbe WhatsApp +255714800175. Unga wa majani ya mlonge naweza kukutumia popote ulipo nje ya Dar

Kama upo Dar na una duka lolote la kawaida na unapenda kuwauzia wateja wako au watu wengine majani fresh ya mlonge naweza kuwa nakuletea asubuhi mapema kila siku dukani kwako, nitafute WhatsApp +255714800175.

Unga wangu wa majani ya mlonge ni mzuri na naweza kusema pasipo na hofu kuwa huwezi kupata sehemu nyingine wenye ubora unaokaribia na wangu. Ninauandaa kwa umakini mkubwa ili ubaki na viinilishe vyake na ni wa kijani kweli kweli

Kama una ushuhuda wowote kuhusiana na majani fresh na unga wa majani ya mlonge kuongeza KINGA YA MWILI ningefurahi kama utaniandikia hapo chini kwenye comment

Tafadhari SHARE post hii kwa ajili ya wengine

Naitwa Fadhili Paulo, ni Tabibu wa Tiba Asili na ni mTanzania.

Ofisi yangu inaitwa Victoria Home Remedy ipo Sigara Yombo Vituka Temeke Dar Es Salaam.

Jiunge na mimi na watu wengine zaidi ya 94000 kwenye ukurasa wangu wa facebook kwa kubonyeza hapa

Imehaririwa mara ya mwisho

Niulize swali nikujibu


7 Comments

Balthazar William Rwenyagira · January 17, 2019 at 10:33 am

Nimesoma, nami kama Afisa Kilimo Mkuu mstaafu naafikiana na maelezo yako. Mimi tayari ninayo miti ya mironge niliyopanda mwaka jana. Inatoa mbegu. Hebu elezea pia matumizi, na faida ya mbegu. Aksante kwa elimu hiyo.

leokadia · January 19, 2019 at 6:12 pm

Nakupendaga sana kaka umenisaidiaga. Sana

Lameck Mgani · January 20, 2019 at 11:53 am

Dawa za asili

Obeid · January 20, 2019 at 10:05 pm

Nimeipenda hio dawa

Costa ruheta · January 21, 2019 at 8:05 am

Thank you for all.

Masoud · May 8, 2019 at 4:15 am

Mungu akupe Ulinzi na daraja kubwa duniani na kesho akhera, siku zote huwa naamini…UKILA VYAKULA VYA ASILI, UNAKUWA WA ASILI, ukila vyakula fake vya madukani, UNAKUWA FAKE PIA, ukweli utajulikana na walimwengu wataacha kuwa watumwa na kugeuzwa BIASHARA kununua dawa za kizungu, na kuwa WATEJA WA HOSPITALI ZAO. Shukrani sana FADHILI PAUL

    Fadhili Paulo · May 20, 2019 at 3:28 am

    Amina, Tubarikiwe wote

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WhatsApp Chat na mimi kwenye WhatsApp