Dawa ya kuongeza mbegu za kiume

Published by Fadhili Paulo on

Kwenye makala hii nitakueleza kwa kina juu ya dawa ya kuongeza mbegu za kiume rahisi na isiyo na gharama yoyote kubwa.

Mwanaume mwenye uwezo wa kuzalisha anahitaji kuwa na mbegu zisizopungua milioni 20, chochote chini ya hapa kinaweza kuwa sababu ya kutokutungisha ujauzito.

Ikitokea umegundulika kuwa na mbegu chache, ni nyepesi sana na hazina nguvu za kukimbia vya kutosha basi dawa hii itaweza kukusaidia kuongeza uwingi wa mbegu zako bila kuingia gharama kubwa sana ….

Visababishi vya mbegu kuwa chache:

Kuna vitu vingi vinavyoweza kusababisha tatizo la mbegu chache na ugumba kwa ujumla kwa wanaume, kwa bahati nzuri vingi ya vitu hivyo tunao uwezo wa kuvidhibiti kwa kupunguza matumizi yake.

Vitu hivyo ni pamoja na:

Vifaa vya kieletroniki – Tafiti zimeonyesha vifaa vingi vya kisasa vya kieletroniki vinasababisha kushuka kwa wingi na ubora wa mbegu kwa wanaume wengi miaka ya sasa kwani mionzi yake hupelekea joto lisilohitajika katika mifuko ya mbegu za kiume.

Vifaa hivi ni pamoja na simu na Kompyuta.

Unashauriwa kutokuweka simu ndani ya mfuko wako wa suruali kwa kipindi kirefu na kutokuweka kompyuta mpakato (laptop) kwenye mapaja yako wakati wote ukiitumia.

Ni mhimu pia kutokutumia masaa mengi kutwa nzima ukiwa kwenye kompyuta.

SimuJanja

Vifaa vya Intaneti visivyotumia waya – Siku hizi tofauti na zamani, kuna teknolojia mpya imeingia ya kuunganisha intaneti kwa kutumia vifaa visivyotumia waya (wireless internet) au kwa lugha nyepesi hujulikana kama Wi-Fi.

Vifaa hivi vinapunguza wingi wa mbegu, uwezo wa mbegu kukimbia na kuharibu muundo asili wa mbegu kwa ujumla (DNA fragmentation).

Wanaume wenye tatizo la uzazi wanashauriwa kutotumia aina hii ya vifaa vya kuunganishia intaneti kwenye kompyuta zao na vile vile kutokuweka simu kwenye mifuko yao ya mbele ya suruali.

wi-fi

Uvutaji wa Sigara – Uvutaji sigara, bangi na bidhaa nyingine za tumbaku huharibu ubora wa mbegu za kiume.

Hilo halihitaji majadiliano. Habari njema ni kuwa madhara yaliyosababishwa na uvutaji sigara yanaweza kurekebishika ikiwa tu utaamua kuacha kuvuta.

Huhitaji dawa kuacha kuvuta sigara, unahitaji kuamua tu kwamba sasa basi na hakuna lisilowezekana kwa mtu mwenye maamuzi na mwenye ndoto za maisha mazuri ya kiafya.

Vingine vya kuviacha ni pamoja na madawa mengine yote ya kulevya.

Viuavijasumu na homoni katika vyakula – Viuavijasumu (pesticides) vinavyotumika katika mazao mbalimbali mashambani miaka ya sasa ni sababu mojawapo ya tatizo la homoni kutokuwa sawa kwa wanaume wengi.

Kwenye bidhaa nyingi za maziwa za viwandani sasa huongezwa homoni kama vile homoni ya estrogeni ambazo hazihitajiki katika mwili wako.

Vyote hivi vina madhara katika afya ya mwanaume.

Mkulima akitia dawa kwenye mboga kuua wadudu

Vyakula vyenye soya – Vyakula vyenye soya ndani yake hasa vile vya viwandani kama vile maziwa ya soya, burger za soya nk si vizuri kwa afya ya uzazi ya mwanaume.

Vinasemwa moja kwa moja kuathiri ubora wa homoni ya testosterone homoni mhimu sana kwa afya ya uzazi wa mwanaume
.
Unywaji pombe – Katika moja ya utafiti kwa wanaume wenye mbegu zenye ubora wa chini, matumizi ya kupitiliza ya unywaji pombe yalionyesha kuhusika na kupungua kwa mbegu za kawaida yaani mbegu nzuri zinazofaa kwa ajili ya uzazi.

Pombe

Matumizi ya vifaa vya plastiki – Wakati kifaa cha plastiki kinapowekewa chakula cha moto hutoa kitu kijulikanacho kama ‘xenohormones’ ambacho huigiza kama ni ‘estrogen’ ndani ya mwili na hivyo kupelekea matatizo kwenye mfumo wa uzazi wa mwanaume.

Joto kupita kiasi (Hyperthermia) – Mifuko ya mbegu za uzazi ya mwanaume inahitaji joto la chini kidogo ya lile joto la mwili kwa ujumla ili mbegu zibaki na afya.

Inasemekana kuwa hii ndiyo moja ya sababu viungo vya uzazi vya mwanaume vipo karibu nje kabisa ya mwili wake.

Joto linajulikana wazi kuharibu ubora wa mbegu na hivyo itakuwa vizuri kuepuka mazingira ambayo yanaweza kusabbaisha joto la moja kwa moja kwenye viungo vya uzazi vya mwanaume ikiwemo kuepuka kuvaa nguo za ndani zinazobana sana.

Mfadhaiko (Stress) – Mfadhaiko au stress unaweza kuleta majanga makubwa katika homoni za mwanaume na kupelekea kushuka kwa uzalishaji wa mbegu za kiume.

Stress inahusika sana na tatizo la ugumba kwa wanaume wengi, na moja ya sababu ya stress hii ni ile hamu yenyewe ya kuwa na mtoto inapokujia kila mara kichwani.

Vile vile mfadhaiko huu unaweza kukupata kutokana na presha kutoka kwa wazazi, ndugu jamaa na marafiki kwamba kwanini huzai.

Hivi vyote ukiviweka kichwani na kuviwaza kila mara ni rahisi kwako kupatwa na tatizo la kupungua kwa mbegu na afya yako ya uzazi kwa ujumla.

Kuwa na amani, mwamini Mungu kwamba siku yako ipo, just relax kila kitu kina muda wake.

Mfadhaiko

Aina ya chakula unachokula – Chanzo kingine cha kuwa na mbegu chache au zisizokuwa na afya ni kutokula chakula sahihi na cha kutosha kila siku.

Kwa afya bora kabisa ya uzazi mwanaume anahitaji vyakula vyenye madini ya zinki (zinc) kwa wingi, selenium, Vitamin E, folic acids, Vitamini B12, Vitamini C na vyakula mbalimbali vinavyoondoa sumu mwilini (antioxidants).

Kujichua (punyeto) – Hili ni janga kubwa miongoni mwa wanaume wengi karibu kote duniani. Tabia hii ukiianza huwa ni vigumu kuiacha na ni rahisi sana kugeuka kuwa teja wa punyeto.

Madhara makubwa ya kujichua ni pamoja na kupungua kwa kasi kwa uwingi wa mbegu kwa mwanaume pia nguvu zake kwa ujumla na hivyo kutokuwa na uwezo wa kumpa mwanamke ujauzito.

Vingine ni pamoja na kuendesha baiskeli masaa mengi, kukosa muda wa mazoezi ya viungo na kutoshiriki tendo la ndoa kwa muda mrefu.

Dawa ya kuongeza mbegu za kiume > MSAMITU PLUS

Msamitu Plus  ina kiasi kingi cha madini ya Zinki ambayo ni mhimu katika kuundwa au kutengenezwa kwa mbegu za kiume na homoni ya testosterone.

Pia msamitu plus ina vitamini B, C, D, E, na K ambazo zote ni vitamini mhimu katika kuongeza wingi wa mbegu za kiume (shahawa).

Pia msamitu plus ina kalsiamu, potasiaumu, niacin na phosphorous.

Hebu tuangalie kwa undani zaidi kwanini dawa hii ni mhimu kwako mwanaume mwenye tatizo la kuwa na mbegu chache au zisizo na sifa za kutungisha ujauzito hapa chini;

1: Msamitu ia kiasi kingi cha magnesium

Moja ya madini ambayo ni mhimu sana ili kuwa na afya bora ya mbegu za mwanaume ni magnesium.

Magnesium ni madini ambayo ni mhimu sana katika kudhibiti msongo wa mawazo na yana uwezo pia wa kudhibiti vizuri sana shinikizo la damu na kuwasaidia wanaume kupata usingizi mzuri.

Kama tujuavyo kuepuka msongo wa mawazo (stress) ni njia moja nzuri sana ya kuwa na mbegu za kiume zenye afya na ubora wa hali ya juu.

2. Msamitu ni chanzo kizuri cha omega-3

Ili kuzalisha mbegu zenye ubora wa hali ya juu wanaume wanahitaji mafuta mazuri yenye Omega 3 ambayo hupatikana pia kwa baadhi ya samaki hasa samaki ajulikanaye kama samoni (salmon kwa kiingereza) ni samaki mkubwa mwenye mnofu mwekundu.

Lakini unafahamu pia kwamba unaweza kupata Omega 3 nzuri zaidi kwa kutumia unga wa mbegu za maboga?.

Omega 3 siyo tu itakusaidia kuzalisha mbegu nzuri bali pia itakusaidia kuziweka sawa homoni zako na kuweka afya nzuri ya mwili wote kwa ujumla.

3. Msamitu ina Madini ya Zinki

Kama tujuavyo madini ya zinki huongeza sana afya ya uzazi hasa kwa wanaume na tunaweza kuyapata madini haya mhimu k.

Kiasi cha kutosha cha madini ya zinki ndiyo kitu mhimu sana ili kuwa na mbegu za kiume zenye afya. Hakika afya ya uzazi ya mwanume itaimarika sana kama atakuwa akitumia vyakula vyenye madini haya.

4. Msamitu Plus inaimarisha afya ya tezi dume

Afya ya tezidume na ubora wa mbegu ni vitu vinavyohusiana moja kwa moja.

Msamitu inasaidia mwanaume kuwa na afya nzuri ya tezidume zake na hivyo kuwa na mbegu nzuri mhimu kwa ajili ya uzazi.

Lipo tatizo la kiafya kwa mwanaume ambapo tezi dume zake moja au zote mbili zinaongezeka ukubwa tofauti na umbile lake la kawaida.

Msamitu inasaidia kuwapa wanaume tezidume zenye afya nzuri, matumizi ya unga wa mbegu za maboga unaweza kumsaidia pia mwanaume mwenye matatizo ya kiafya kwenye kibofu cha mkojo.

5. Msamitu inaongeza pia ujazo wa mbegu za mwanaume

Msamitu siyo kwamba inasaidia tu kuboresha nguvu za kiume kwa wanaume bali pia husaidia kuongeza ujazo (sperm count) wa mbegu hizo na ubora wake.  

Kazi hii hasa huwezeshwa na msamitu kutokana na kuwa na kiasi cha kutosha cha protini, omega 3, zinki, magnesium, na vitamini E ndani yake.

Hivyo ni wazi lazima utaihitaji dawa hii kama wewe ni mwanaume unayejiandaa kupata mtoto.

6. Msamitu inasaida kuongeza kasi ya mbegu za kiume

Mbegu bora za kiume zinahitajika pia ziwe na uwezo wa kusafiri na kukimbia kwa kasi inayohitajika ili kuvifikia via vya uzazi vya mwanamke na yai tayari kwa kurutubishwa.

Bila mbegu kuwa na uwezo huu wa kukimbia ni ngumu kwa mbegu hizo kuogelea, kulifikia na kulirutubisha yai la mwanamke.

Katika kesi kama hii msamitu na madini yake mhimu, protini na vitamini mbalimbali utakusaidia kuboresha spidi au kasi ya kukimbia ya mbegu zako (sperm motility).

7. Msamitu inaongeza ujazo wa mbegu

Ukiacha ubora wa mbegu (quality), wingi wa mbegu (sperm count), na uwezo wake wa kukimbia (sperm motility), wanaume wanahitaji pia kiasi fulani cha mbegu (zisiwe chini ya milioni 20).

Ndiyo kiasi hicho cha wingi wa mbegu ni mhimu na kinahitajika ili kuziwezesha mbegu hizo kuweza kubeba na kusafirisha kirahisi mbegu za uzazi za mwanaume kwenda kwenye via vya uzazi vya mwanamke na kulifikia yai kwa ajili ya utungishaji wa mimba.

Viinilishe vilivyomo kwenye Msamitu vinauwezesha mfumo wa uzazi wa mwanume kutengeneza mbegu za kutosha na zenye ubora unaohitajika ili kutungisha ujauzito.

Msamitu ni mchanganyiko wa mimea na mitishamba mbalimbali ya asili. Ni dawa nzuri sana katika kutibu tatizo la nguvu za kiume na pia inasaidia sana kwa wanaume wenye tatizo la nguvu za kiume hasa lililosababishwa na kujichua au kupiga punyeto kwa muda mrefu kwani inaimarisha sana mishipa ya uume.

Pia unaweza kuitumia hata kama unasumbuliwa na tatizo la kisukari au Shinikizo la juu la damu. Msamitu inao uwezo mkubwa katika kuongeza hamu ya tendo la ndoa kwa wanaume hata wa umri mkubwa.

Vitu vifuatavyo vinafanya Msamitu kuwa dawa bora zaidi ya kuongeza mbegu za kiume mpaka sasa:

8. Msamitu inatibu tatizo la msongo wa mawazo (stress)

Mawazo na mfadhaiko huondoa mtiririko mzuri wa damu mwilini na kusababisha nguvu za mwili kupungua, nguvu za kiume kuwa chini na hata uume wenyewe unaweza kunywea na kuwa mdogo na legelege.

Kama una mfadhaiko wa akili (stress) ni vigumu sana wewe kuwa na nguvu za kiume. Hilo haliwezekani. Ili uwe na nguvu za kiume unatakiwa usiwe na mawazo mawazo yoyote. Uwe mtu uliyetulia kimwili, kiakili na kiroho (cool).

Chanzo namba 1 cha tatizo la nguvu za kiume na kuwahi kufika kileleni kwa wanaume karibu wote ni msongo wa mawazo (stress). Jambo la kushangaza ni kuwa msamitu ni dawa bora ya kuondoa stress nzuri ya asili isiyo na madhara mengine mabaya tofauti na zilivyo dawa zenye kemikali zinazotibu msongo wa mawazo.

Tafiti nyingi zimekuwa zikionyesha kuwa moja ya kisababishi kikubwa cha msongo wa mawazo (stress) ni kukosekana kwa viinilishe mhimu katika chakula.

Kukosekana huku kwa viinilishe mhimu katika chakula kunasababisha usawa usio sawa wa homoni mwilini (hormonal imbalance) jambo linalopelekea kutokea kwa msongo wa mawazo.

Msongo wa mawazo umeendelea kuwa tatizo kubwa kwa watu miaka ya sasa na wengi wao wakipatwa na tatizo la kukosa pia usingizi.

Hata hivyo, tatizo hilo linaweza kutibika kirahisi kwa kuongeza viinilishe sahihi kwenye mwili wako

Kwa bahati nzuri msamitu ina viinilishe vingi kuliko dawa nyingine yoyote ya asili ya kutibu tatizo la nguvu za kiume uliowahi kuitumia au kuisikia ukiwa na viinilishe zaidi ya 120 ndani yake!

Msamitu ina kiasi cha kutosha cha vitamini A, B, C, E, Potasiamu, Kalsiamu, zinki na viinilishe vingine vingi mhimu kwa afya ya mwanaume.

Kwahiyo kama utatumia Msamitu kujitibu tatizo la nguvu za kiume na kuwahi kufika kileleni itakuwa ni vigumu kwako kupata tatizo la msongo wa mawazo.

Magnesiamu madini yapatikanayo kwenye Msamitu ni dawa maarufu ya kutuliza akili (Tranquillizer) na kutibu matatizo kama msongo wa mawazo, sononeko, huzuni, hamaki na matatizo mengine ya mvurugiko wa akili.

9. Msamitu inaongeza kinga ya mwili

Sasa kama kinga yako ya mwili haipo sawa je utapata wapi nguvu za kiume?

Kumbuka, ile hali ya kuonekana umezeeka au mwili wako kuonekana umechoka mara zote huwa kuna uhusiano wa moja kwa moja na kushuka kwa kinga yako ya mwili hali ambayo inauacha mwili wako kushambuliwa kirahisi na vijidudu nyemelezi na magonjwa mbalimbali.

Kama unataka kuwa na nguvu za kiume kila siku basi jifunze namna kinga yako ya mwili inavyoweza kuongezwa na kuimarishwa.

Sasa unaweza kuwa unajiuliza ni nini kinachoifanya dawa hii kuwa kitu cha thamani SANA katika kuimarisha kinga yako ya mwili na hivyo kukuongezea nguvu za kiume, kujikinga na vijidudu nyemelezi, homa na magonjwa mbalimbali?

Kwanza kabisa Msamitu una viinilishe vingi ndani yake ukiwa na zaidi ya viinilishe 120, una vitamini nyingi, madini na viondoa sumu mwilini tofauti tofauti zaidi ya 46!

Vitamini C iliyomo kwenye dawa hii ni kitu mhimu katika kurejesha kinga ya mwili kwa sababu ni vitamini inayofanya kazi ya kuripea seli za mwili na kinga ya mwili. Zaidi sana vitamini C huimarisha ngozi ya mwili, nywele, fizi, macho na kuongeza nguvu ya jumla ya mwili kwa kuyataja machache mazuri ya vitamini C

Vitamini A ni moja ya vitamini zilizomo kwa wingi kwenye Msamitu na ni vitamini mhimu sana katika kuimarisha kinga ya mwili. Vitamini A ni mhimu pia kwa watu wanaosumbuliwa na matatizo kama ya kuharisha, upungufu wa kinga mwilini, surua na malaria.

Vileviele kuna madini ya chuma (Iron) kwenye Msamitu na ni kitu mhimu katika mfumo wa kinga ya mwili ambayo hukuwezesha usipatwe na magonjwa na homa mara kwa mara.

Msamitu inaimarisha usawa wa himoglobini katika damu jambo ambalo matokeo yake ni kuimarika kwa kinga yako ya mwili na msukumo wako wa damu kwenda kwenye uume.

Msamitu inasafisha mwili wako wote, inasafisha ini, figo, moyo, macho, inaimarisha meno, ngozi na nywele.

Wakati unatumia Msamitu itakufanya ujisikie vizuri, ujisikie mpya (fresh) na mwenye nguvu.

Uwezo wa Msamitu kuyaweza yote hayo ni kutokana na kuwa na vitamini, madini mbalimbali na viondowaji sumu vingi ndani yake.

10. Msamitu Plus ina madini na vitamini zote mhimu kwa ajili ya nguvu za kiume

Msamitu ina madini ya Zinki madini ambayo ni mhimu sana linapokuja suala la nguvu za kiume. Pia una protini ya kutosha, protini ni mhimu katika suala zima la nguvu ya mwili

Vitamini nyingine mhimu kwa ajili ya nguvu za kiume zilizomo kwenye Msamitu ni pamoja na vitamini B6, B12, D na E

11. Msamitu inatoa sumu mwilini

Viondoa sumu mwilini ni mhimu sana ili kudhibiti vijidudu nyemelezi kuvamia mwili.

Vijidudu nyemelezi (Free radicals) ni adui mkubwa kwa afya ya uzazi ya mwanaume ikihusisha pia afya ya mbegu zake.

Kutumia vyakula safi vyenye uwezo wa kuondoa sumu mwilini ni njia madhubuti ya kuwa na mbegu bora kwa mwanaume.

Hii ya kuondoa sumu inasaidia pia kuzalisha mbegu zenye ubora wa hali ya juu kabisa.

Chanzo kingine cha kupungua mbegu za kiume miaka ya sasa ni sumu nyingi mwilini sababu ya vilevi na vyakula tunavyokula kila siku. Habari njema ni kuwa hakuna sumu inaweza kubaki salama mbele ya Msamitu.

Kwa hiyo ni vigumu mtu utumie Msamitu halafu bado uwe na mbegu chache.

12. Msamitu inaongeza msukumo wa damu mwilini

Msukumo mzuri wa damu usiozuiliwa kusafiri kwa uhuru wote sehemu mbalimbali za mwili ni mhimu katika kutibu tatizo la nguvu za kiume. Kwa ajili hii watu hushauri kunywa maji na kufanya mazoezi ya viungo kila siku. Jambo la ajabu ni kuwa hiyo kazi ya kuongeza msukumo wa damu sehemu zote za mwili ni kazi inayoweza kufanywa vizuri na Msamitu.

Bado sijaona ni namna gani Msamitu itashindwa kukutibu tatizo lako la kuwa na mbegu chache na kuwahi kufika kileleleni.

Jaribu Msamitu na uniletee mrejesho

Kazi inabaki kuwa kwako tu kuanzia sasa …

Mambo mengine mhimu ya kuzingatia

*Kula lishe bora

*Acha kutumia vinywaji au vyakula vyenye kaffeina

*Kula ndizi mara nyingi

*Kula parachichi mara nyingi

*Kula zaidi mboga za majani

*Kunywa maji mengi kila siku

*Tumia vyakula vyenye folic asidi kwa wingi

*Kula Mayai ya kienyeji mawili kila siku

*Acha vilevi vyote

Kama unahitaji msamitu niachie tu ujumbe WhatsApp +255714800175.

Naweza pia kukuletea ulipo ndani ya Dar bila gharama ya ziada, pia naweza kukutumia popote ulipo nje ya Dar

Tafadhali SHARE post hii kwa ajili ya wengine.


6 Comments

James Matovolwa · 10/12/2018 at 11:42 am

somo zuri

  Fadhili Paulo · 10/12/2018 at 5:17 pm

  Nashukuru kusikia hivyo James. Karibu tena

Frank Ntangwa · 11/04/2019 at 9:19 pm

somo zuri sana bro

  Fadhili Paulo · 21/04/2019 at 2:24 am

  Ahsante sana ndugu

John isack Swehele · 16/10/2020 at 3:51 pm

Tunakupate sasa kwa sisi tuliombali na Dar es Salaam nikiimaanisha namba zako za simu

  Fadhili Paulo · 20/10/2020 at 12:35 pm

  Tuwasiliane WhatsApp +255714800175

Leave a Reply

Avatar placeholder

Your email address will not be published.