Mwanaume mwenye uwezo wa kuzalisha anahitaji kuwa na mbegu zisizopungua milioni 20, chochote chini ya hapa kinaweza kuwa sababu ya kutokutungisha ujauzito.

Ikitokea umegundulika kuwa na mbegu chache, ni nyepesi sana na hazina nguvu za kukimbia vya kutosha basi dawa hii itaweza kukusaidia kuongeza uwingi wa mbegu zako bila kuingia gharama kubwa sana ….

Visababishi vya mbegu kuwa chache:

Kuna vitu vingi vinavyoweza kusababisha tatizo la mbegu chache na ugumba kwa ujumla kwa wanaume, kwa bahati nzuri vingi ya vitu hivyo tunao uwezo wa kuvidhibiti kwa kupunguza matumizi yake.

Vitu hivyo ni pamoja na:

Vifaa vya kieletroniki – Tafiti zimeonyesha vifaa vingi vya kisasa vya kieletroniki vinasababisha kushuka kwa wingi na ubora wa mbegu kwa wanaume wengi miaka ya sasa kwani mionzi yake hupelekea joto lisilohitajika katika mifuko ya mbegu za kiume.

Vifaa hivi ni pamoja na simu na Kompyuta.

Unashauriwa kutokuweka simu ndani ya mfuko wako wa suruali kwa kipindi kirefu na kutokuweka kompyuta mpakato (laptop) kwenye mapaja yako wakati wote ukiitumia.

Ni mhimu pia kutokutumia masaa mengi kutwa nzima ukiwa kwenye kompyuta.

SimuJanja

Vifaa vya Intaneti visivyotumia waya – Siku hizi tofauti na zamani, kuna teknolojia mpya imeingia ya kuunganisha intaneti kwa kutumia vifaa visivyotumia waya (wireless internet) au kwa lugha nyepesi hujulikana kama Wi-Fi.

Vifaa hivi vinapunguza wingi wa mbegu, uwezo wa mbegu kukimbia na kuharibu muundo asili wa mbegu kwa ujumla (DNA fragmentation).

Wanaume wenye tatizo la uzazi wanashauriwa kutotumia aina hii ya vifaa vya kuunganishia intaneti kwenye kompyuta zao na vile vile kutokuweka simu kwenye mifuko yao ya mbele ya suruali.

wi-fi

Uvutaji wa Sigara – Uvutaji sigara, bangi na bidhaa nyingine za tumbaku huharibu ubora wa mbegu za kiume.

Hilo halihitaji majadiliano. Habari njema ni kuwa madhara yaliyosababishwa na uvutaji sigara yanaweza kurekebishika ikiwa tu utaamua kuacha kuvuta.

Huhitaji dawa kuacha kuvuta sigara, unahitaji kuamua tu kwamba sasa basi na hakuna lisilowezekana kwa mtu mwenye maamuzi na mwenye ndoto za maisha mazuri ya kiafya.

Vingine vya kuviacha ni pamoja na madawa mengine yote ya kulevya.

Viuavijasumu na homoni katika vyakula – Viuavijasumu (pesticides) vinavyotumika katika mazao mbalimbali mashambani miaka ya sasa ni sababu mojawapo ya tatizo la homoni kutokuwa sawa kwa wanaume wengi.

Kwenye bidhaa nyingi za maziwa za viwandani sasa huongezwa homoni kama vile homoni ya estrogeni ambazo hazihitajiki katika mwili wako.

Vyote hivi vina madhara katika afya ya mwanaume.

Mkulima akitia dawa kwenye mboga kuua wadudu

Vyakula vyenye soya – Vyakula vyenye soya ndani yake hasa vile vya viwandani kama vile maziwa ya soya, burger za soya nk si vizuri kwa afya ya uzazi ya mwanaume.

Vinasemwa moja kwa moja kuathiri ubora wa homoni ya testosterone homoni mhimu sana kwa afya ya uzazi wa mwanaume
.
Unywaji pombe – Katika moja ya utafiti kwa wanaume wenye mbegu zenye ubora wa chini, matumizi ya kupitiliza ya unywaji pombe yalionyesha kuhusika na kupungua kwa mbegu za kawaida yaani mbegu nzuri zinazofaa kwa ajili ya uzazi.

Pombe

Matumizi ya vifaa vya plastiki – Wakati kifaa cha plastiki kinapowekewa chakula cha moto hutoa kitu kijulikanacho kama ‘xenohormones’ ambacho huigiza kama ni ‘estrogen’ ndani ya mwili na hivyo kupelekea matatizo kwenye mfumo wa uzazi wa mwanaume.

Joto kupita kiasi (Hyperthermia) – Mifuko ya mbegu za uzazi ya mwanaume inahitaji joto la chini kidogo ya lile joto la mwili kwa ujumla ili mbegu zibaki na afya.

Inasemekana kuwa hii ndiyo moja ya sababu viungo vya uzazi vya mwanaume vipo karibu nje kabisa ya mwili wake.

Joto linajulikana wazi kuharibu ubora wa mbegu na hivyo itakuwa vizuri kuepuka mazingira ambayo yanaweza kusabbaisha joto la moja kwa moja kwenye viungo vya uzazi vya mwanaume ikiwemo kuepuka kuvaa nguo za ndani zinazobana sana.

Mfadhaiko (Stress) – Mfadhaiko au stress unaweza kuleta majanga makubwa katika homoni za mwanaume na kupelekea kushuka kwa uzalishaji wa mbegu za kiume.

Stress inahusika sana na tatizo la ugumba kwa wanaume wengi, na moja ya sababu ya stress hii ni ile hamu yenyewe ya kuwa na mtoto inapokujia kila mara kichwani.

Vile vile mfadhaiko huu unaweza kukupata kutokana na presha kutoka kwa wazazi, ndugu jamaa na marafiki kwamba kwanini huzai.

Hivi vyote ukiviweka kichwani na kuviwaza kila mara ni rahisi kwako kupatwa na tatizo la kupungua kwa mbegu na afya yako ya uzazi kwa ujumla.

Kuwa na amani, mwamini Mungu kwamba siku yako ipo, just relax kila kitu kina muda wake.

Mfadhaiko

Aina ya chakula unachokula – Chanzo kingine cha kuwa na mbegu chache au zisizokuwa na afya ni kutokula chakula sahihi na cha kutosha kila siku.

Kwa afya bora kabisa ya uzazi mwanaume anahitaji vyakula vyenye madini ya zinki (zinc) kwa wingi, selenium, Vitamin E, folic acids, Vitamini B12, Vitamini C na vyakula mbalimbali vinavyoondoa sumu mwilini (antioxidants).

Kujichua (punyeto) – Hili ni janga kubwa miongoni mwa wanaume wengi karibu kote duniani. Tabia hii ukiianza huwa ni vigumu kuiacha na ni rahisi sana kugeuka kuwa teja wa punyeto.

Madhara makubwa ya kujichua ni pamoja na kupungua kwa kasi kwa uwingi wa mbegu kwa mwanaume pia nguvu zake kwa ujumla na hivyo kutokuwa na uwezo wa kumpa mwanamke ujauzito.

Vingine ni pamoja na kuendesha baiskeli masaa mengi, kukosa muda wa mazoezi ya viungo na kutoshiriki tendo la ndoa kwa muda mrefu.

Dawa ya kuongeza mbegu za kiume > Unga wa Mbegu za Maboga

Unga wa Mbegu za Maboga

Unga wa Mbegu za maboga una kiasi kingi cha madini ya Zinki ambayo ni mhimu katika kuundwa au kutengenezwa kwa mbegu za kiume na homoni ya testosterone.

Pia unga wa mbegu za maboga una vitamini B, C, D, E, na K ambazo zote ni vitamini mhimu katika kuongeza wingi wa mbegu za kiume (shahawa).

Pia unga wa mbegu za maboga una kalsiamu, potasiaumu, niacin na phosphorous.

Matumizi: Tumia kijiko kikubwa kimoja cha chakula cha unga wa mbegu za maboga kwenye kikombe kimoja cha juisi ya parachichi au kwenye mtindi na uongeze asali vijiko vikubwa viwili ndani yake.

Tumia dawa hii nusu saa kabla ya chakula cha mchana na jioni kwa siku 60 na kuendelea mpaka umepona.

Unaweza pia kuendelea kutumia dawa hii hata kama huna tatizo la kuwa na mbegu chache

Mambo mengine mhimu ya kuzingatia

*Kula lishe bora

*Acha kutumia vinywaji au vyakula vyenye kaffeina

*Kula ndizi mara nyingi

*Kula zaidi mboga za majani

*Kunywa maji mengi kila siku

*Tumia vyakula vyenye folic asidi kwa wingi

*Kula Mayai ya kienyeji mawili kila siku

Soma hii pia > Dawa ya nguvu za kiume na maumbile madogo

Kama unahitaji unga wa mbegu za maboga niachie tu ujumbe WhatsApp +255714800175.

Naweza pia kukuletea ulipo ndani ya Dar naweza pia kukutumia popote ulipo nje ya Dar

Tafadhali SHARE post hii kwa ajili ya wengine.

Naitwa Fadhili Paulo, ni Tabibu wa Tiba Asili na ni mTanzania.

Ofisi yangu inaitwa Victoria Home Remedy ipo Sigara Yombo Vituka Temeke Dar Es Salaam.

Jiunge na mimi na watu wengine zaidi ya 94000 kwenye ukurasa wangu wa facebook kwa kubonyeza hapa

Imehaririwa mara ya mwisho

Niulize swali nikujibu


4 Comments

James Matovolwa · December 10, 2018 at 11:42 am

somo zuri

    Fadhili Paulo · December 10, 2018 at 5:17 pm

    Nashukuru kusikia hivyo James. Karibu tena

Frank Ntangwa · April 11, 2019 at 9:19 pm

somo zuri sana bro

    Fadhili Paulo · April 21, 2019 at 2:24 am

    Ahsante sana ndugu

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WhatsApp Chat na mimi kwenye WhatsApp