NGUVU ZA KIUME NI NINI?

Nguvu za kiume ni neno linalotumika mara nyingi kumaanisha ‘Uwezo wa mwanaume kufanya tendo la ndoa’. Na inapokuwa tofauti na hivi, tunaita ni ‘kupungua au kukosa nguvu za kiume’.

Kupungukiwa kwa nguvu za kiume hutofautiana toka mtu mmoja hadi mwingine.

Inaweza kuwa ni hali ya kutokuwa na uwezo wa kusimamisha uume, au hali ya kutokuwa na uwezo wa kufika kileleni kwa muda mzuri wa kutosha.

Nguvu za kiume pia siyo idadi ya mabao. Hilo ni mhimu kwanza ulielewe. Unaweza kwenda mabao hata manne na bado ukaonekana huna nguvu za kiume.

Nguvu za kiume ni muda gani umetumia kubaki hapo mchezoni ndiyo jambo la mhimu.

Kama unafika mpaka magoli manne na kila goli unatumia dakika 3 au 4 kufika kileleni basi tunaweza kusema wewe huna nguvu za kiume.

Ila kama utaweza kwenda goli moja tu na likachukua dakika 10 au 15 au 20 hivi na kuendelea hakika tunasema wewe una nguvu za kiume. Tunaamini muda huo umetosha kuweza kumfikisha mwenza wako kileleni.

Tatizo la nguvu za kiume na suluhisho lake

Mwanaume pia utahitaji kujua dalili au ishara za mwanamke anapofika kileleleni.

Bila kujua dalili au ishara za mwanamke anayefika kileleni ni kazi bure.

Kama unahitaji kuzifahamu ishara na dalili za mwanamke anayefika kileleni kipo kitabu chenye maelezo yake kwa kirefu nitumie ujumbe kwenye WhatsApp +255714800175 ili kupata kitabu hicho.

Kumbuka pia tendo la ndoa siyo ugomvi.

Wapo baadhi ya wanaume wanadhani ili umfikishe mwanamke basi unatakiwa umfanye kwa nguvu au kwa fujo sana utadhani ni ugomvi fulani hivi!, mapenzi siyo hivyo.

Ndiyo hutakiwi ufanye kilegelege sana lakini pia huhitaji kufanya kwa nguvu kama vile ni ugomvi!

Tatizo ni hizo video feki mnazotazama mnadhani mapenzi ndiyo huwa hivyo jambo ambalo si kweli.

Kila mwaka wasichana na wanawake wengi hutekwa na watu wasiojulikana sehemu mbalimbali duniani na baadhi yao hufanyiwa vitendo vya kikatili ikiwemo vya kingono na hurekodiwa.

Sasa wewe unapoangalia picha kama hizo unadhani mapenzi ndiyo hufanywa hivyo kumbe si kweli.

Kuna wanaume wakianza kazi hiyo ni kama vile mashine inakoboa mahindi yaani ni ugomvi mwanamke anabaki akiumia tu na kama hajuwi naye anabaki kuumia tu. Hata siku nyingine ukimhitaji atakataa kwa visingizio vingi sababu unamuumiza bila wewe kujua.

Pole pole, kwa nguvu kidogo inapochanganya lakini siyo kwa fujo kama vile ugomvi. Umeipata hiyo?! bila shaka kazi inabaki kuwa kwako!.

Kumbuka mwanaume lazima utafika kileleni hata iweje, hivyo ni jukumu lako kuhakikisha kabla hujawa na uwezo tena wa kuendelea na tendo la ndoa uwe umeona na una uhakika mke wako naye amefika kileleleni.

Hivyo nguvu za kiume siyo idadi ya mabao, ni muda unaotumia kubaki hapo kifuani ndiyo mhimu na si idadi ya mabao.

Pamoja na hayo yote, elimu mhimu ambayo mwanaume anatakiwa kuwa nayo, ni kuwa nguvu za kiume hazipatikani kwa kutumia madawa ya kemikali au mahala pengine; bali zinatokana na vyakula tunavyokula kila siku.

SABABU ZA SISI WANAUME KUISHIWA NGUVU ZA KIUME:

Kuishiwa nguvu za kiume ni jambo la kawaida kwa wanaume wengi.

Ni kushindwa kwa uume kudumu kusimama barabara kwa ajili ya tendo la ndoa, au kuwahi kufika kileleni.

Ni jambo linaloweza kumtokea kila mwanaume bila kujali ni nani.

Linaweza kukutokea mara moja moja kwa mwezi au mara kadhaa kwa mwaka kwani hakuna mwanaume anayeweza kuwa na uwezo wa kuchelewa kufika kileleni kila atakaposhiriki tendo la ndoa mwaka mzima.

Ingawa kama linakutokea kila mara mfulululizo kwa kipindi kirefu basi hapo ni lazima upate msaada wa tiba na ushauri juu ya vyakula na mazoezi.

Tatizo la kupungukiwa nguvu za kiume huongezeka sababu ya umri.

Tafiti mbalimbali zinasema wanaume wa umri kuanzia miaka 61 na kuendelea ndiyo wanapatwa na tatizo hili zaidi kuliko wanaume wenye umri wa miaka 41 Kushuka chini.

Wanaume wenye elimu ndogo juu ya utendaji kazi wa mwili na afya ndio wanaokabiliwa sana na tatizo hili.

Hii ni kutokana na kwamba wengi wao wanakuwa hawaelewi aina ya vyakula vinavyoongeza nguvu za kiume na za mwili kwa ujumla, namna wanavyotakiwa kuishi ili kupunguza janga hilo, wanakunywa pombe na hawajishughulishi na mazoezi ya viungo.

Mazoezi ya viungo hupunguza tatizo la kuishiwa nguvu za kiume kwa asilimia kubwa sana.

Kupungukiwa nguvu za kiume kunaweza pia kuwa kumetokana na mambo ya kihisia (emotional causes).

Vitu vingine vinavyoweza kusababisha kupungua kwa nguvu za kiume ni pamoja na magonjwa kama vile ugonjwa wa Kisukari na Shinikizo la juu la damu.

Asilimia 51 mpaka 61 ya wanaume wanaosumbuliwa na kisukari wanapatwa na tatizo la uume kushindwa kusimama vizuri.

Kadharika wagonjwa wa kiharusi na wale waliotekwa na ulevi nao ni miongoni mwa watu wanaoweza kupatwa kirahisi na tatizo la upungufu wa nguvu za kiume.

Walevi wengi wa pombe kwa mfano wanakabiliwa na tatizo la uzalishaji mchache wa mbegu za kiume (manii).

Wengine wenye hatari ya kupatwa na tatizo la kupungukiwa nguvu za kiume ni pamoja na wanaume wenye shinikizo la juu la damu, wenye matatizo ya tezi, waliowahi kufanya upasuaji katika viungo vya uzazi wakabaki na majeraha, watu wanaotumia dawa zenye kemikali kiholela bila kushauriwa na wataalamu na wale wanaougua maradhi yanayodhoofisha msukumo wa damu kwenda katika mishipa ya uume.

Pamoja na hayo, tatizo la upungufu wa nguvu za kiume linaweza kutibika kwa watu wa rika zote.

Kabla daktari hajaanza kukutibu tatizo la kupungukiwa nguvu za kiume, atataka kujuwa:

1. Umri wako
2. Utendaji wa tendo la ndoa kabla na baada ya kuugua
3. Afya yako kwa ujumla
4. Matatizo katika ndoa ikiwa kuna ugomvi wowote n.k
5. Nini sababu ya wewe kutaka kupona

Kuwa na mtaalamu mzuri ni njia ya kwanza katika kupata uponyaji sahihi.

Ni mhimu wewe kujisikia vizuri na kuwa na imani na daktari wako. Kwa kufanya hivi utakuwa umepiga hatua nzuri kelekea kwenye ufumbuzi wa tatizo lako.

Nini Sababu ya uume kushindwa kusimama?

Kushindwa kwa uume kusimama pia hutambulika kama kuishiwa nguvu za kiume. Ni kitendo cha mtu kushindwa kusimamisha uume au kudumisha usimamaji wa uume kwa muda wa kutosha kufanya tendo la tendo na mwenza wake.

Pamoja na ukweli kuwa mara zote Mwanaume lazima atafika kileleni, hali huweza kuwa tofauti kwa upande wa pili kwani mwanamke anahitaji mwanaume akawie zaidi ili na yeye (mwanamke) aweze kutosheka.

Mkeo hupendelea ukawie na ikiwezekana ukawie zaidi. Kama utakuwa unawahi kumaliza, basi mkeo anakuwa hapati raha kamili.

Hata hivyo tambua pia kuchelewa sana kufika kileleni inaweza kuwa kero kwa mwenza wako. Kwa kawaida wanawake wengi wanaweza kufika kileleni kuanzia dakika ya 8 kwenda juu tangu tendo la ndoa lianze.

Muda mzuri wa kutumia katika kushiriki tendo la ndoa bila kuleta kero zingine ni kati ya dakika 15 mpaka dakika 30 hivi. Ikiwa mwanaume ataendelea bila kufika kileleni hata baada ya dakika 35 au 40 na zaidi basi hiyo sasa ni kero na si tendo la ndoa tena.

Ingawa, kama una tatizo la kuwahi kufika kileleni hauko peke yako. Asilimia 30 hadi 40 ya wanaume wa rika zote wanakabiliwa na tatizo la kuwahi kufika kileleni au kupungukiwa kwa nguvu za kiume.

Hata hivyo kutambuwa tu kwamba wanaume wengine pia wana tatizo kama lako siyo sababu ya wewe kukaa tu bila kutafuta suluhisho la tatizo lako.

Habari njema ni kuwa zipo njia zinazoweza kuleta matokeo mazuri na hatimaye kulimaliza tatizo hili bila madhara mabaya hapo baadaye.

Wakati mwingine uume kushindwa kusimama inaweza kuwa si tatizo, lakiini jambo hilo linapojitokeza kila mara na kwa kipindi kirefu inaweza kuleta msongo wa mawazo kwa mume na hata kwa mke.

Sababu nyingine ambazo zinaweza kupelekea uume usisimame vizuri ni pamoja na matatizo ya mhemko kama;

1. Wasiwasi
2. Hasira
3. Msongo wa mawazo (Stress)
4. Huzuni
5. Hofu na mashaka
6. Kukosa hamu ya tendo la ndoa n.k

Ili uume usimame vizuri ni lazima:

1. Mfumo wako wa neva uwe na afya nzuri inayopelekea mpwito neva (nerve impulses) katika ubongo, uti wa mgongo na uume.

2. Mishipa ya ateri iliyo na afya ya ndani na iliyo karibu na corpora cavernosa

3. Kiwango sahihi cha oksidi nitriki (nitric oxide) ndani ya uume.

Uume kushindwa kusimama vizuri kunaweza kusababishwa pia kama kipengele kimojawapo hapo juu hakifanyi kazi vizuri.

Mambo mengine yanayopelekea kupunguwa kwa nguvu za kiume, uume kushindwa kusimama vizuri na kuwahi kufika kileleni ni pamoja na:

1. Uzee
2. Kisukari
3. Kujichua/Punyeto
4. Uzinzi
5. Kukosa Elimu ya vyakula
6. Kutokujishughulisha na mazoezi
7. Shinikizo la juu la damu
8. Ugonjwa wa moyo
9. Uvutaji sigara/tumbaku
10. Utumiaji uliozidi wa kafeina
11. Kudhurika kwa neva au uti wa mgongo
12. Madawa ya kulevya
13. Kupungua kwa homoni ya testerone
14. Athari kutoka kwa baadhi ya dawa
15. Pombe
16. Kutazama picha za X mara kwa mara
17. Kukaa muda mrefu kwenye kiti

Nguvu za kiume na mzunguko wa damu:

Kitu gani husababisha uume usimame?

Unaweza kujibu ni msisimko. Ni kweli, Jibu lako linaweza kuwa sahihi. Hata hivyo msisimko ni matokeo. Kipo kinachosababisha kutokea huo msisimko. Bila hicho, hakuna msisimko unaoweza kutokea.

Kila mwanaume anatakiwa kujuwa jibu sahihi la swali hili ili atakapopatwa na tatizo atambuwe wapi pa kuanzia na pa kuishia.

Siyo lazima uwe daktari, Elimu ya kutambua mfumo wako wa mwili unavyofanya kazi ni mhimu sana kwa kila mtu na si kwa madaktari pekee kama watu wengi mnavyodhani.

Kutokusoma soma lolote kuhusu miili yetu inavyofanya kazi ndiyo sababu kubwa inayotufanya kuparamia dawa kiholela na hivyo kujikuta tunapata madhara zaidi badala ya kujitibu.

Mzunguko wa damu ndicho kitu kinachofanya uume USIMAME.

Na kabla hujaendelea kusoma tambua jambo moja mhimu; ‘’Asilimia 94 ya damu ni maji’’. Hii ni kusema katika kila lita 10 za damu, lita 9 kati ya hizo 10 ni maji.

Kwa kifupi maji ndiyo kila kitu mwilini, nakushauri upendelee Kunywa maji bila KUSUBIRI KIU.

Mzunguko wa damu unaofanya kazi vizuri kama inavyotakiwa na usio na hitilafu yeyote ni kipengele mhimu sana katika afya ya mwili, mishipa na kusimama kwa uume wako.

Kwanini mzunguko wa damu ni mhimu?

Mzunguko wa damu wenye afya bora husambaza damu ya kutosha katika viungo vyote vya mwili ikijumuisha pia damu iliyo katika mishipa ya uume.

Hivyo, hata kama utagusana na mwanamke hautaweza kufanya lolote ikiwa damu haizunguki katika viungo vyako kama inavyotakiwa.

Mtazame mtu aliyekufa, damu yake haizunguki, je anaweza kufanya lolote? Hata hivyo huo ni mfano mkubwa sana.

Hii ni kusema kuwa, chochote ambacho kinazuia mtiririko wa damu kwenda kwenye uume kinaweza kuzuia kusimama kwa uume.

Kama mishipa ya vena na ateri imeziba, mwili wako hautaweza kusimamisha uume vizuri. Hii ni kutokana na kwamba uume hautapata damu ya kutosha.

Mara nyingi vena zilizoziba kutokana na mzunguko dhaifu wa damu ni sababu ya kushindwa kusimama uume kwa wanaume wengi wenye miaka 60 kwenda juu, wanaume wenye kisukari na pia wanaume wenye hali ya kukauka kwa vijiateri vya ateri, na wenye maradhi ya moyo.

Baadhi ya wanaume wanapatwa na tatizo la kuishiwa nguvu za kiume kama matokeo ya kula vyakula vyenye mafuta mengi ambayo yanaweza kuzuia mtiririko mzuri wa damu kwenye uume. Inashauriwa pia kuepuka vinywaji na vyakula ambavyo husindikwa viwandani.

Katika tendo la ndoa kwa mwanaume, mishipa ya damu ya ateri ina nafasi kubwa sana sababu ya kazi yake ya usafirishaji wa damu kwenda sehemu mbalimbali za mwili, hivyo unashauriwa kujifunza namna ya kutunza ateri za mwili wako ili kuruhusu mtiririko mzuri wa damu mwilini mwako.

Pia ni mhimu sana kuwaona wataalamu wa tiba kuhusu unavyojisikia na jinsi unavyohisi kuwa pengine unaweza kuwa na tatizo katika mishipa yako ya ateri.

Jaribu kujiwekea utaratibu wa kujichunguza afya yako mara kwa mara kama utahisi kunyemelewa na tatizo hili.

Baadhi ya watu hufanya maradhi kuwa sugu kwa sababu ya kuacha kujichunguza mara kwa mara hadi wauguwe, huku ni kukosa kuelewa na kushindwa kujithamini na kujipenda mwenyewe.

Jitibu tatizo la kupungua nguvu za kiume au kuwahi kufika kileleni:

Katika kujitibu tatizo hili jambo la kwanza ni kuelewa ni nini kimesababisha tatizo hilo kwa upande wako.

Dawa ya asili ya kuongeza nguvu za kiume > Unga wa Msamitu

Unga wa msamitu (mtishamba wa porini) ni mzuri sana katika kutibu tatizo la nguvu za kiume na pia unasaidia sana kwa wanaume wenye tatizo la nguvu za kiume hasa lililosababishwa na kujichua au kupiga punyeto kwa muda mrefu kwani unaimarisha sana mishipa ya uume.

Pia unaweza kuutumia hata kama unasumbuliwa na tatizo la kisukari au Shinikizo la juu la damu. Msamitu unao uwezo mkubwa katika kuongeza hamu ya tendo la ndoa kwa wanaume hata wa umri mkubwa.

Msamitu pia unatibu magonjwa yafuatayo bila shida yoyote; pumu, chango la uzazi, kupooza mwili, unaondoa kabisa gesi tumboni na kuongeza nuru ya macho kuona.

Kama utahitaji Unga wa msamitu niachie tu ujumbe kwenye WhatsApp +255714800175

Mambo mengine mhimu ya kuzingatia:

1. Acha mawazo

Mawazo na mfadhaiko huondoa mtiririko mzuri wa damu kwenda kwenye uume na kusababisha nguvu kupungua nguvu za kiume na hata uume wenyewe.

Ikiwa unasumbuliwa na mfadhaiko au stress uangalifu mkubwa unahitajika kabla ya kuamua kutumia dawa yoyote.

Katika hali ya mfadhaiko wa akili utokanao na hali ya kushuka kwa uchumi kwa mfano, wanandoa wanapaswa kuwa ni wenye umoja na kujaliana zaidi, shida ni pale kama mke akili yake ni ndogo kwani badala ya kufunga na kuomba kwa Mungu huenda akaenda kukutangaza kwa majirani!.

Kama una mfadhaiko wa akili (stress) ni vigumu sana wewe kuwa na nguvu za kiume. Hilo haliwezekani. Ili uwe na nguvu za kiume unatakiwa usiwe na mawazo mawazo yoyote. Uwe mtu uliyetulia kimwili, kiakili na kiroho (cool).

Jipekuwe na ujitambuwe ni kitu gani hasa kinakufanya uwe na mawazo mawazo kila mara na ufanye kila uwezalo kukiondoa hicho kinachokuletea stress kwenye maisha yako kila mara.

Stress nyingi kwa wanaume wa KiTanzania zinatokana na ugumu wa maisha, magomvi ya mara kwa mara kwenye mahusiano, magonjwa ambayo hayatibiki nk.

Haijalishi nini chanzo cha mawazo mawazo upande wako, ukiamua hakuna stress isiyo na tiba.

Chimba tu inawezekana. Kuwa bize na mazoezi ya viungo kila siku ni namna nzuri ya kuondoa msongo wa mawazo.

Kama stress yako ni matokeo ya maisha magumu basi jipe moyo pia jipe muda hakuna usiku usio na mchana kuna siku tu utatoka kama hutakata tamaa.

Pigana na upambane mpaka kieleweke kuna siku utaishi maisha bila stress ya umasikini.

Kuwa karibu na Mungu kila mara. Usiache kutafuta msaada wa kimawazo toka kwa wataalamu au watu wengine wenye uzoefu juu ya hali unayopitia.

Pia jikubali na umshukuru Mungu kwa kila jambo.

Hili linaenda sambamba pia na kuhakikisha unapata usingizi wa kutosha muda usiopungua masaa saba mpaka nane kila siku. Bila kupata usingizi wa kutosha au kupata muda wa kutosha wa kupumzika kila siku itakuwa vigumu kwako kuwa na nguvu za kiume

Wakati mwingine unajiona una matatizo sababu hujakutana na wenye matatizo zaidi yako.

Kuwa na moyo wa kuridhika kwa mambo madogo Mungu anayokupa. Hata kuamka salama tu ni baraka tosha unahitaji kushukuru Mungu.

Ridhika na hali na usonge mbele.

2. Fanya mazoezi ya viungo

Zingatia sana umhimu wa mazoezi ya viungo.

Bila kujishughulisha na mazoezi ya viungo kila siku itakuwa ni vigumu sana kwako kupona tatizo la upungufu wa nguvu za kiume.

Kutengeneza mishipa na kupunguza uzito isiwe ndiyo sababu pekee ya kwenda gym.

Kama unahitaji nguvu za kiume na uume wenye afya, unahitaji kujishughulisha na mazoezi ya viungo mara kwa mara ili kusafisha mishipa ya damu na hivyo kuongeza kiasi cha utiririkaji wa damu kwenda kwenye uume.

Kama uzito wako upo juu sana na ni mnene fanya mazoezi ya kukimbia (jogging) kila siku. Kama uzito wako upo sahihi tu kwa mjibu wa urefu wako fanya sana mazoezi ya kuchuchumaa na kusimama (squatting).

3. Shiriki tendo la ndoa mara nyingi

Kuna stori zinasema twiga hakuzaliwa na shingo ndefu namna hii kama anavyoonekana akiwa mkubwa, bali wanasema ile tabia yake ya kupenda kula majani ya juu ya miti ndiyo ikapelekea shingo yake ikarefuka!. Inawezekana kuna ukweli kidogo wa stori hizi

Usinielewe vibaya wala usije ukasema huyu jamaa anahamasisha watu kufanya mapenzi!

Hapana usiwe na haraka hivyo utanielewa tu ninachotaka kusema

Wanasayansi wa masuala ya mapenzi wanasema ikiwa mtu mzima hana msongo wowote wa mawazo (stress), ana afya nzuri tu ya kutosha na anakula vizuri basi anaweza kushiriki tendo la tendo kila baada ya masaa 24.

Angalia na umsome pia mwenza wako pia angalia umri wako, sababu kuna wanawake wengine kwa asili hawapendi kushiriki tendo la ndoa kila mara pia hatuwezi kusema mtu mwenye miaka 50 atakuwa na uwezo wa kushiriki tendo la ndoa kila mara kama mtu wa miaka 18 hadi 40 hivi.

Pia inasemwa kushiriki tendo la ndoa mara 200 kwa mawaka kunaongeza miaka 6 zaidi ya kuishi.

Ni vigumu mtu anakaa mwenzi mzima mwingine miezi miwili mwingine anakaa miezi 6 bila kushiriki tendo la ndoa na utegemee utakuwa na uwezo wa kuchelewa kufika kileleni.

Kama hushiriki tendo la ndoa kuna uwezekano mkubwa ukawa unapiga punyeto kitendo ambacho ni kibaya zaidi kwa afya ya uume wako.

Kwahiyo unaweza kushiriki mara 2 hadi 3 kwa wiki na unaposhiriki tuliza akili na upate muda wa kutosha wa kuandaana kabla ya tendo na siyo haraka haraka tu (mambo ya short time).

Tafadhali SHARE post hii kwa ajili ya wengine.

Naitwa Fadhili Paulo, ni Tabibu wa Tiba Asili na ni mTanzania.

Ofisi yangu inaitwa Victoria Home Remedy ipo Sigara Yombo Vituka Temeke Dar Es Salaam.

Jiunge na mimi na watu wengine zaidi ya 94000 kwenye ukurasa wangu wa facebook kwa kubonyeza hapa

Imehaririwa mara ya mwisho

Niulize swali nikujibu


2 Comments

Silvanus M. Mmeku · May 5, 2019 at 5:15 am

Niko na hii tatizo ya kufika kileleni mora moja tu.Kisha uume hausimame tena kabisa, iko utaweza kunisaidia je?

    Fadhili Paulo · May 20, 2019 at 3:29 am

    Tuwasiliane

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WhatsApp Chat na mimi kwenye WhatsApp