Nywele inawezekana ndiyo kitu cha kwanza hasa linapokuja suala la urembo. Hii inamaanisha nywele zinaangaliwa zaidi na watu kuliko hata nguo, dhahabu au hata viatu.

Nywele ndiyo taji, fahari na kung’aa kwa utukufu wa mwanadamu katika ulinzi na kujiamini.

Nywele zako ni kitu pekee na cha thamani

Hakuna kitu kinavutia zaidi kama kuwa na nywele nzuri za kutosha na zenye afya yake ya asili.

Hata hivyo tatizo la kupotea kwa nywele au upara ni tatizo kubwa linalowapata watu wengi kila pembe ya dunia.

Kuna sababu nyingi zinazoweza kupelekea kupotea kwa nywele kama vile:

a)Sababu za kimazingira,

b)Kuzeeka,

c)Msongo wa mawazo (stress),

d)Kuvuta sigara kupita kiasi,

e)Lishe duni,

f)Homoni kutokuwa sawa,

g) Kurithi

h) Maambukizi kwenye ngozi ya kichwa

i)Matumizi yasiyo sahihi ya vipodozi vya nywele

j)Baadhi ya dawa za hospitali

k)Matatizo katika kinga ya mwili

l)Upungufu wa madini chuma

m)Na magonjwa mengine sugu

Ni jambo la kawaida kupotea nywele 50 mpaka 100 kwa siku lakini unapoanza kupoteza zaidi ya hapo kwa siku ni muda muafaka kwako kuchukua hatua kurudishia kiasi hicho cha nywele kinachopotea.

Leo nimekuletea hapa dawa za asili 2 zinazoweza kuotesha na kuzipa afya upya nywele zako ambazo zimeanza kupotea na hivyo kuondoa huo upara bila gharama sana.

Uvumilivu unahitajika zaidi kwani ni tiba inayochukua muda mrefu kwa kawaida.

Dawa ya kuotesha nywele kwa wenye vipara > Mafuta ya habbat soda na Unga wa Majani ya Mlonge

ili ufanikiwe kwenye zoezi hili la kurudishia nywele kwenye kichwa chako chenye upara utahitaji dawa za aina mbili, moja iwe ya kunywa na nyingine iwe ya kupakaa kichwani moja kwa moja na uzitumie zote kwa pamoja ndipo utakuwa na uhakika na kupata matokeo mazuri.

1. Dawa ya kuotesha nywele kwa wenye vipara ya kunywa > Unga wa majani ya mlonge

Dawa ya kuotesha nywele kwenye upara
Unga wa Majani ya Mlonge

Unga wa majani ya mti wa ajabu wa mlonge una umhimu mkubwa ambao hujawahi kuambiwa na mtu katika kutunza, kukuza na kuweka vema afya ya nywele kwa ujumla.

Unaweza kuniuliza KIVIPI?

Kabla ya yote ngoja tujifunze ni viinilishe vipi, vitamini zipi na madini yapi ambayo ni MHIMU kwa kuotesha, kukuza na kuboresha afya ya nywele kwa ujumla.

Vile vile yakupasa utambuwe kuwa ubora wa afya yako kwa ujumla unaweza kutambulika kwa kuangalia muonekano wa nywele zako tu! Nywele zako zinaonyesha afya yako ilivyo.

Kama mwili wako ni mzima, una viinilishe vyote mhimu na nywele zako zitaonekana kuwa zina furaha pia. Ikiwa kuna shida mahali popote kwenye mwili wako nywele zako zitatuonyesha hilo.

Utumiaji wa kila siku wa vitamini na madini mhimu na asidi amino ni mhimu katika kutunza nywele zetu zibaki na afya na zenye furaha. Baadhi ya vitamini, madini na asidi amino ni mhimu kwa ajili ya uundwaji wa ‘keratin’ ambayo hufahamika kama umeng’enywaji wa nywele ( hair metabolism).

Siri kubwa nyuma ya pazia la ukuwaji wa nywele …

Kwahiyo, kwa ubora kabisa wa kukua kwa nywele, vinyweleo vya nywele lazima viwe na kiasi cha kutosha cha viinilishe na oksijeni katika mfumo wa mwili ili kuotesha na kukuza nywele.

Kumbuka mti huu wa ajabu wa mlonge umebarikiwa kuwa na vitamini na madini kwa wingi kuliko mti au mmea wowote chini ya jua. Mlonge una viinilishe 92 vya madini na vitamini mbalimbali huku ukiwa na viondoa sumu mwilini 46!

Kama tunavyoweza kuona mlonge ni kitu maalumu mno na cha ajabu, una viinilishe vingi mno kwa ajili ya afya ambavyo siyo rahisi kuvieleza vyote katika makala hii lakini nitajaribu kuvigusia baadhi kati ya hivyo mhimu kwa ajili ya nywele.

Mlonge una vitamini C mara 7 zaidi ya ile ya kwenye machungwa, una madini ya chuma mara 25 zaidi ya yale yaliyomo kwenye spinachi na mara 17 zaidi ya kalsiamu zaidi ya ile iliyomo kwenye maziwa na mara 4 zaidi ya vitamini A iliyomo kwenye karoti na vitu vingine vingi.

Vitamini A ndiyo vitamini mhimu zaidi katika kutengeneza afya bora ya tishu na seli mabalimbali katika mwili jambo linalopunguza kupotea au kunyonyoka kwa nywele. Mlonge ni mti tajiri wa vitamini A na utachangia kwa sehemu kubwa katika ukuwaji wa nywele zako.

Madini ya Zinki ambayo yanapatikana kwa wingi katika mlonge yanahamasisha ukuwaji wa nywele na kuimarisha kinga yako ya mwili.

Kiasi cha kutosha cha madini ya zinki na vitamini A pia kunazuia kuzibika kwa tezi mafuta ya nywele katika ngozi ya kichwa. Sababu namba 1 ya watu wengi kusumbuliwa na tatizo la kunyonyoka kwa nywele au upara ni matokeo ya kushuka kwa madini ya zinki mwilini.

Ikiwa una upungufu wa madini ya zinki mwilini kutatokea kupungua au udhaifu katika vinyweleo vya nywele ambavyo vina uhusiano wa moja kwa moja na usanisi na DNA ya nywele, wakati zinki ina ushawishi mkubwa katika uundwaji wa asidi nyukilia.

Kingine mhimu kilichomo kwenye mlonge kinachohusika na afya ya nywele ni uwepo wa viatmini nyingi za kundi B kama B1, B2, B3, B4, B6, B7, B12 ,B14, na B17. Hivyo afya mbovu ya nywele inaweza kutokea ikiwa lishe yako ina upungufu wa kiasi cha kutosha cha vitamini za kundi B hasa hasa vitamini B6 na folic asidi.

Vitamini E ambayo huondoa sumu mwilini ni mojawapo ya kiinilishe mhimu katika mlonge ambacho ni cha lazima katika ukuwaji wa nywele sababu huongeza msukumo wa damu kwenye ngozi ya kichwa.

Kuongezeka kwa msukumo wa damu kwenye ngozi ya kichwa (scalp) kunatengeneza upatikanajai wa viinilishe mhimu kwa ajili ya vinyweleo vya nywele jambo linaloleta afya bora ya nywele na nywele kuwa ndefu.

Kwa kuongezea vitamini C kwenye mlonge inaunda msukumo wa damu katika ngozi ya kichwa na vinyweleo vya nywele.

Madini ya Potasiamu madini mengine mhimu katika mlonge yanazipa nywele zako uwezo wa kuchukua viinilishe katika chakula vinavyohitajika ili kuwa na nywele nzito, nyingi na za kuvutia.

Kwenye mlonge pia kuna kiondoa sumu chenye nguvu sana kijulikanacho kitaalamu kama ‘Zeatin’. Tafiti za wazi zimethibitisha kwamba mlonge una kiasi kingi kisicho cha kawaida cha homoni za mimea zijulikanazo ‘cytokinins’ kama vile zeatin.

Katika kuangalia zaidi katika kemikali hii majaribio mbalimbali yamehitimisha kuwa cytokinins kama zeatin zina kazi kubwa katika kukuzuia usizeeke. Namna hili linatokea ni kuwa Zeatin inachelewesha mgawanyiko wa seli (cell division) na kuondoa sumu mwilini.

Madini, Mlonge na Ukuwaji wa nywele …

Salfa ya asili iliyomo kwenye mlonge ni madini mengine mhimu kwa ukuwaji wa nywele.

Sulfur ya asili ambayo ni tofauti na ile ya kutengenezwa ni kitu kilichopo karibu katika kila vyakula tunavyokula hasa matunda na mboga za majani.

Sulfur inashikilia jina la utani (a.k.a) la ‘madini urembo’ kwa sababu hii. Ndiyo madini yanayokuza nywele, kucha, kung’arisha ngozi na hivyo kukufanya uonekane kijana

Madini mengine yaliyomo kwenye mlonge kama vile manganizi, kalsiamu na shaba yanaweza kuhamasisha kukua na kuripea nywele.

Usisahau pia kupendelea kula vyakula vingi ambavyo havijapikwa (staili ya kachumbali nk). Vyakula vingi vya kwenye migahawa si salama kwa ukuwaji wa nywele zako.

Vyakula feki kama vile vyenye sukari nyingi kupitiliza, vinywaji baridi, keki, utumiaji uliozidi wa nyama nyekundu, nyama ya nguruwe (kitimoto) vinachangia kupotea kwa nywele.

Ili kuotesha au kukuza nywele zako ukitumia unga wa majani ya mlonge anza na kutumia kijiko kidogo kimoja cha chai cha unga wa majani ya mlonge kutwa mara 1 ukitumia kwenye juisi ya matunda uliyotengeneza mwenyewe nyumbani au katika uji au kwenye mtindi au kwenye asali.

Pole pole unaweza kuongeza kiasi mpaka kijiko kikubwa cha chakula kimoja kwa siku kutegemea na afya yako inavyoitika. Wasiliana pia na daktari wako wa karibu kabla ya kuanza kutumia mlonge ikiwa wewe ni mjamzito au una shinikizo la chini la damu.

Mpendwa msomaji, wakati ukiwa bize ukitumia mlonge kukuza nywele zako usisahau pia kutumia mlonge siyo tu kutakusaidia kuwa na nywele nzuri bali pia utakuwa ukiusaidia mwili wako katika kuongeza kinga ya mwili, kusafisha damu yako, kudhibiti uzito wako, kuweka sawa sukari katika mwili wako, kuongeza nguvu za mwili na faida nyingine nyingi za kiafya bila idadi

Unga wangu wa majani ya mlonge ni mzuri na naweza kusema pasipo na hofu kuwa huwezi kupata sehemu nyingine wenye ubora unaokaribia na wangu. Ninauandaa kwa umakini mkubwa ili ubaki na viinilishe vyake na ni wa kijani kweli kweli

2. Dawa ya kuotesha nywele kwa wenye vipara > Mafuta ya habbat soda

Dawa asili za kuotesha nywele
Mafuta ya Habbat Soda kwa ajili ya Kuotesha Nywele

Moja ya matumizi makubwa ya mafuta haya ni kuotesha nywele.

Bidhaa nyingi sokoni zinazotumika kwa ajili ya kuotesha nywele zinaacha madhara makubwa zaidi kwa mtumiaji kuliko faida zake.

Kwahiyo kwa wale wenye tatizo la upala, nywele zisizokuwa na kwa wale ambao nywele zao hazina afya mnashauriwa kuchagua mafuta haya kwa matatizo haya yote.

Ingawa haieleweki ni kwa namna gani mafuta haya yanakuza nywele lakini wanasayansi wanaamini haya yanaweza kuwa ni matokeo ya uwezo wake mkubwa wa kuondoa sumu na protini nyingi ndani yake.

Matumizi:

  1. Dawa ya Unga > Kunywa kijiko kidogo kimoja cha chai kutwa mara 2 nusu saa kabla ya chakula cha asubuhi na cha usiku kwenye kikombe kimoja cha juisi ya matunda au katika uji au kwenye mtindi.
  2. Dawa ya kupakaa > Sugulia kipande cha limao fresh eneo ambalo nywele zimenyonyoka na kisha pakaa kijiko kikubwa kimoja cha mafuta ya habbat soda ya nywele na uache kama dakika 15 hadi 20, unaweza kuacha hivyo hivyo au ujisafishe na maji safi, unaweza kufanya kutwa mara 1 au 2 kwa muda wa mwezi mmoja hadi miwili.

Unahitaji dozi hii kwa ajili ya kuotesha nywele? niachie ujumbe WhatsApp +255714800175.

Kama upo Dar na unahitaji uletewe ulipo niachie ujumbe WhatsApp +255714800175 na natuma pia mikoani.

Tafadhari SHARE post hii kwa ajili ya wengine

Naitwa Fadhili Paulo, ni Tabibu wa Tiba Asili na ni mTanzania.

Ofisi yangu inaitwa Victoria Home Remedy ipo Sigara Yombo Vituka Temeke Dar Es Salaam.

Jiunge na mimi na watu wengine zaidi ya 94000 kwenye ukurasa wangu wa facebook kwa kubonyeza hapa

Imehaririwa mara ya mwisho

Niulize swali nikujibu


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WhatsApp Chat na mimi kwenye WhatsApp