Dawa ya kupata ute wa mimba

Published by Fadhili Paulo on

Dawa ya kupata ute wa mimba

Ute wa uzazi anaoupata mwanamke pale anapokuwa katika kipindi cha upevushaji mayai ndiyo unaosaidia mbegu za kiume ziweze kusafiri hadi katika yai lililopevuka katika mrija wa uzazi.

Kwa kawaida ute wa uzazi ni mwepesi na unavutika au unakuwa na mnato.

Matatizo ya uzazi yanayomfanya mwanamke asipate ujauzito husababishwa na kasoro katika uzalishaji wa mbegu za kiume na matatizo katika ute wa uzazi.

Tunategemea mwanamke yeyote aliye kamili katika uzazi hupevusha mayai na dalili ya upevushaji huu wa mayai ni kuwa anatokwa na ute wa uzazi.

Aina za Ute

1. Ute ukiwa mkavu au unanata

aina ya ute kama huu hauruhusu mbegu za kiume kusafiri na kuingia katika kizazi cha mwanamke hivyo mimba haiwezi kutungwa hapa.

Huu ute huwepo mwanamke akiwa hayupo katika kipindi cha joto au kipindi ambacho yai yake bado halijapevuka.

2. Ute ukiwa na rangi ya krimu

hapo mwanamke anakaribia kuingia katika kipindi cha joto pia yai linakaribia kupevuka bado hawezi kupata mimba.

3. Ute ukiwa maji maji au na unyevunyevu

huu unaweza kusafirisha mbegu ya mwanaume hadi kizazi cha mwanamke na kama imebaki siku mbili au tatu yai kupevuka ukifanya tendo la ndoa hapa kuna uwezo utashika mimba kwa sababu yai likipevuka litakutana na mbegu ya mwanaume ndani ya kizazi kuna uwezo mimba itatungwa.

Mwanamke hupata hisia za kufanya mapenzi lakini siyo sana

4. Ute ukiwa na rangi nyeupe kama yai bichi

ute ukiwa katika hali hii ndiyo mzuri kabisaa kwa kusafirisha mbegu za kiume.

Pia hapa mwanamke ameshafika katika kipindi cha joto hapa tendo la ndoa likifanyika mimba inapatikana kwa asilimia zote kama hakuna vizuizi kutoka kwa Mungu muumba na vizuizi vingine vya afya vinavyozuia mimba kutunga.

Hapa hisia za mwanamke za kufanya tendo la ndoa huwa juu sana na hutamani kufanya mapenzi kila mara especially yai likikaribia kushuka na likishuka.

Ni muhimu sana mwanamke aangalie ute (vaginal mucus) katika kuzifahamu siku zake za kuweza kushika mimba na kutoshika mimba kuliko kutumia calendar ya damu ya mwezi.

Siku za ute ni siku 30 kinyume na siku za damu ya mwezi na pia ni muhimu sana mwanamke kushika ule ute kila siku kwa mkono wake kuangalia rangi na utelezi na harufu.

UTE WA UZAZI USIO WA KAWAIDA

JINSI TATIZO LINAVYOTOKEA

Kupata ute wa uzazi usio wa kawaida kwa mwanamke humfanya awe mgumba, ute wa uzazi unapokuwa na tatizo husababisha mbegu za kiume zishindwe kupenya humo na kuogelea kwenda kurutubisha yai lililo tayari.

Pia ute wenye matatizo huua au kuziharibu mbegu za kiume, hata mwanaume atoe mbegu zenye ubora namna gani kama pale ukeni ute una matatizo basi zitauawa au kukosa ubora wa kwenda mbele zaidi.

Tunapoongelea ute wa uzazi kwa kawaida ute huu tunauweka katika makundi makuu matatu, kwanza ni ute mzito, ute huu baada ya muda mfupi hubadilika kuwa mwepesi na mwembamba huku ukivutika kwa lengo la kuwezesha mbegu za kiume zisafiri humo, mwisho ute wa uzazi unarudi kuwa mzito.

Ute wa uzazi unapokuwa mwepesi na kuvutika unaashiria uwepo wa kiwango cha kutosha cha vichocheo vya Estradiol katika mzunguko mzima wa mfumo wa hedhi wa mwanamke.

Hapa tunategemea vichocheo hivi vya Estradiol kuwa vizuri hasa katika kipindi cha uzalishaji mayai kiitwacho Follicular Phase .

Mwanamke mwenye ute wa uzazi usio wa kawaida yaani anakuwa na ute mzito tu daima, hana historia ya kupata ute mwepesi na wa kuvutika tunasema anapevusha mayai lakini hatoi ute wa uzazi hivyo kuna matatizo katika utoaji wa ute wa uzazi tatizo ambalo kitaalamu linaitwa Abnormal Cervical Mucus.

Kwa hiyo mwanamke anaweza kuwa na tatizo hili la kutokupata ute wa uzazi wenye sifa katika kipindi chote cha umri wake wa kuzaa na hata wakati wa Ovulation au upevushaji wa mayai.

Ute huu mzito ukeni husababisha kuua au kuziharibu mbegu za kiume na wakati mwingine hutoa nafasi kwa bakteria na fangasi kujipenyeza humo na kumfanya mwanamke asumbuliwe na tatizao la muwasho wa mara kwa mara ukeni, kutoa harufu mbaya au ute huo kubadilika rangi na kuwa njano.

Tatizo linaweza kuendelea na kuathiri mlango wa kizazi hivyo mwanamke anapata ugonjwa uitwao Cervicitis.

Wakati mwingine ute huu usio wa kawaida unaweza kutengeneza mazingira ya kinga ukeni ambapo kila mbegu ya kiume inapofika ukeni inauawa.

Ute huu ukigunduliwa mwanamke hutibiwa na kupona na kupata ujauzito, itakuwa ngumu endapo mwanamke huyu atakuwa na maambukizi sugu ukeni au mdomo wa kizazi utabana kutokana na matibabu ya saratani ya shingo ya kizazi.

Tatizo hili hutubika na kuisha kabisa

Kama umekuwa ukitafuta ujauzito kwa kipindi kirefu bila mafanikio na unahitaji dawa nzuri ya asili ya uhakika isiyo na gharama kubwa ya kukusaidia kupata ute wa mimba niachie tu ujumbe WhatsApp +255714800175. Maelezo yake zaidi unaweza kuyasoma kwa kubonyeza hapa.

Share na wengine uwapendao.


4 Comments

Anonymous · 11/10/2021 at 7:31 pm

Na mtu hambae hapati kabisa ute was uzazi shida no nn

    Fadhili Paulo · 13/10/2021 at 3:02 pm

    Ni vizuri kufika hospitali kwa uchunguzi na vipimo zaidi

Comfort kimilike · 03/03/2022 at 8:49 am

Habari,,,me nimezaa watoto wawili na nimeharibu mimba moja kwa sasa sipati tena mimba shida nini Nina o negative na ute wa mimba pia siuoni

    Fadhili Paulo · 10/03/2022 at 11:04 am

    Tuwasiliane kwenye WhatsApp +255714800175

Leave a Reply

Avatar placeholder

Your email address will not be published.

WhatsApp WhatsApp +255714800175