Dawa ya kupevusha mayai ya uzazi

Published by Fadhili Paulo on

Dawa ya kupevusha mayai ya uzazi

Kama mwanamke, afya nzuri ya mayai ya uzazi ni mhimu kwa ajili ya kuwa na mzunguko mzuri wa hedhi na kuwa na uwezo wa kushika ujauzito.

Je ni dawa gani nzuri ya asili kwa ajili ya kuongeza afya ya mayai yako ya uzazi? Makala hii inajadili hilo kwa kina.

Endelea kusoma ….

Pamoja na dawa, bado kutakuwa na mabadiliko utakayotakiwa kuyafanya hasa upande wa vyakula ili kuongeza uwezekano wa tatizo lako kuisha kwa haraka na kwa uhakika na hivyo kuongeza uwezekano wa wewe kupata ujauzito.

Hapo kabla iliaminika kwamba wanawake huzaliwa na mayai yote ya uzazi na kwamba mwili hauendelei kuyazalisha mengine.

Miaka ya karibuni imegundulika katika tafiti mbalimbali kwamba seli ndani ya ovari za mwanamke zinaendelea kuzalisha mayai mengine mapya katika mzunguko wa miaka ya uzazi.

Umri unabaki kitu mhimu sababu ingawa mwili wako unaendelea kuzalisha mayai mapya bado mji wako wa uzazi utaendelea kuwa na mazingira yasiyo rafiki kwa afya bora ya mayai kadri umri wako unavyozidi kuongezeka

Kama umekuwa ukiambiwa uwezekano wako wa kupata ujauzito ni mdogo sababu mayai yako yamezeeka basi hilo lisikutishe sababu bado mwili wako unaendelea kuzalisha mayai mengine mapya kila mara na hivyo bado kuna tumaini kwako.

Ni mhimu kula mlo sahihi na kufanya mabadiliko chanya ya kitabia ili kuvutia upevukaji mzuri wa mayai yako.

Inachukua siku 90 mpaka yai liwe limezalishwa na kuundwa tayari kwa kurutubishwa.

Hii ndiyo sababu hatua zozote utakazochukua kuimarisha afya na kukomaa kwa mayai yako lazima zidumu kwa muda mrefu si chini ya miezi mitatu mpaka uone matokeo chanya na mazuri.

Wakati mayai yako yanajiandaa kwa ajili ya kurutubishwa yanaweza kuathiriwa ubora wake na mambo mengi yanayohusiana na hali ya afya yako ya sasa.

SABABU ZA KUTOPEVUKA KWA MAYAI YA UZAZI:

Mara nyingi mayai kutopevuka husababishwa na mabadiliko katika homoni ya ‘estrogen’.

Mabadiliko haya mara nyingi hutokea wakati wa kuvunja ungo, wakati wa hedhi, wakati wa ujauzito na wakati wa ukomo wa hedhi (menopause).

Vitu vingine vinavyopelekea mayai kutopevuka ni pamoja na

  1. Kuongezeka umri
  2. Lishe duni
  3. Kutokujishughulisha na mazoezi
  4. Kupungua kwa ogani ya adreno
  5. Mfadhaiko (stress)
  6. Kukosa usingizi
  7. Dawa za uzazi wa mpango
  8. Sumu na kemikali mbalimbali mwilini nk

Hapa nimekuandikia na kukuelezea dawa ya asili unayoweza kuitumia ili kuboresha afya ya mayai yako na hivyo yapevuke vizuri tayari kwa kurutubishwa.

Dawa ya asili inayopevusha mayai ya uzazi > Uzazi Mjarabu

Hii ni dawa ya asili kwa ajili ya kuimarisha afya ya mayai yako.

Mchanganyiko wa dawa hii una madini tofauti tofauti mhimu 31 na viinilishe vingine mhimu kwa ajili ya mwili zaidi ya 60.

Ni dawa inayotumika kutibu maradhi mbalimbali mwilini ikiwemo kuongeza afya ya mayai ya uzazi.

Uzazi Mjarabu huongeza huimarisha afya ya mayai ya uzazi kwa mwanamke.

Uzazi Mjarabu ni dawa ya asili yenye mchanganyiko wa mitishamba na mimea mbalimbali ya asili.

Ni dawa ya asili yenye uwezo wa kutibu matatizo mbalimbali yanayosababisha ugumba kwa pamoja.

Inasaidia kuweka sawa homoni, kuondoa uvimbe kwenye kizazi, kupevusha mayai, kuzuia ujauzito usiharibike, kuzibua mirija, kutibu maambukizi kwenye kizazi, kutoa sumu mwilini, kuleta ute wa uzazi na mengine mengi kwa pamoja.

Dawa hii ina viinilishe, madini na vitamini zote mhimu kama ifuatavyo;

Uzazi mjarabu ina:

1. Vitamini B6

Kazi kubwa ya vitamini B6 ni kusaidia mimba kukaa sawa na salama wiki mbili za mwanzo tangu ujauzito utungwe (Luteal phase).

Hiki ni kipindi cha maandalizi cha kipindi kingine kijacho katika safari ya ujauzito na ni lazima mazingira yawe ya afya katika mji wa uzazi wa mwanamke ili kweli ujauzito uendelee kukua.

Hivyo siku hizi 14 za mwanzo vitamini B6 ni ya mhimu ili ujauzito ubaki na afya.

Kama huna hii vitamini vya kutosha basi hizi siku 14 hazitafika na ndani ya siku 7 au 10 ujauzito utakutoka.

2. Vitamini B12

Vitamini B12 ni vitamini mhimu sababu husaidia kuweka sawa homoni. Kama matokeo yake inakusaidia kupata siku zako vizuri na kama siku zako zinaenda vizuri basi ni rahisi pia kwako kupata ujauzito wenye utulivu na afya bora ya mtoto.

Vitamini hii ni mhimu pia kwa baba kwani husaidia kumpa mwanaume mbegu nyingi na zenye ubora wa kutungisha mimba.

3. Vitamini C

Vitamini C imekuwa ikihusishwa na uzazi kwakuwa inasaidia kuweka sawa homoni na kukupa mzunguko mzuri wa hedhi vitu ambavyo ni mhimu ili uwe na afya ya kuweza kupata ujauzito.

Hii ni vitamini mhimu kwa kinamama ambao wamekuwa wakitumia dawa za uzazi wa mpango kwa kipindi kirefu. Husaidia mji wa uzazi uwe tayari na sawa kwa ajili ya kutunga ujauzito.

Vitamini hii inaisapoti homoni ya ujazi ijulikanayo kama ‘progesterone’ katika mwili na kuimarisha kuta za mji wa uzazi baada ya mimba kutungwa.  

4. Vitamini D

Upungufu wa Vitamini D umekuwa ukihusishwa na ugumba moja kwa moja.

Tafiti zinaonyesha upungufu wa vitamini D unaathiri tishu au ogani za uzazi za mwanamke kwamba ogani hizo haziwezi kufanya kazi kwa ufanisi na kuleta matokeo chanya.

Vitamini D pia ina umhimu mkubwa katika kukua kwa seli na ufanyaji kazi wake. Tafiti zinaonyesha wanawake wenye vitamini D ya kutosha wanakuwa na mji wa uzazi mzuri na wenye afya.

5. Vitamini E

Bila Vitamini E ni vigumu kupata ujauzito. Hii ni vitamini mhimu katika kulinda afya ya seli zetu na hufanya kazi ya kuondoa sumu mwilini na hivyo kuzilinda seli zisidhurike kirahisi.

Hii inajumuisha seli za mayai ya uzazi, kuta zinazozunguka yai zimetengenezwa kwa vitamini E.

Vitamini E pia husaidia kuweka sawa mbegu za mwanaume kwa kuongeza wingi na ubora wake kwa ajili ya uzazi.

6. Madini ya Folate

Kuwa na kiasi cha kutosha cha madini haya ni jambo la mhimu ikiwa unahangaika kupata ujauzito. Madini haya ni mhimu ili kuzuia ujauzito usitoke.

Ni mhimu mwili uwe na madini haya mapema wakati wowote unapojiandaa kushika ujauzito.

Ukisubiri mpaka upate ujauzito ndiyo uanze kutafuta haya madini tayari utakuwa umeshachelewa.

7. Madini ya chuma

Madini ya chuma yana uhusiano wa moja kwa moja na uzazi. Yanahitajika ili kuzizalisha homoni mbili mhimu za uzazi ambazo ni estrogen na progesterone, ambazo ni homoni mhimu kwa utungaji wa kawaida wa ujauzito.

Tafiti zinaonyesha wanawake wenye kiasi kidogo cha madini haya mwilini mwao wanapata wakati mgumu katika kushika ujauzito.

Mara tu upatapo ujauzito madini ya chuma ni ya mhimu sana ili kuwa na ujauzito wenye afya kipindi chote cha miezi 9.

8. Omega-3 na Omega-6

Haya hujulikana kama mafuta mazuri (good fats). Kumbuka siyo kila mafuta ni mabaya kwa mwili wako, yapo mafuta mazuri na ambayo yanahitajika na mwili wako ili kuwa na afya bora.

Omega-3 na Omega-6 husaidia kuweka sawa homoni zako na kuzifanya zifanye kazi kwa usahihi jambo linalohamasisha uhakika wa kuwa na uwezo wa kutunga kwa mimba na kuwezesha damu kusambaa vizuri kwenye ogani za uzazi.

9. Madini ya Selenium

Selenium ni madini madogo ambayo hufanya kazi kama kiondoa sumu mwilini na hivyo kuimarisha ubora wa seli zetu.

Pia ni madini mhimu kwa ajili ya uundwaji wa mayai na hudhibiti kazi za tezi ya thyroid, tezi ambayo ni mhimu kwa uzalishwaji na uwekaji sawa wa homoni.  

10. Madini ya Zinki

Madini ya zinki ni mhimu kwa pande zote mbili kwa mwanamke na mwanaume. Kwa wanawake zinki husaidia uzalishwaji wa mayai na kuyaweka mayai yenye afya na kuweka sawa homoni.

Upungufu wa madini ya zinki pia unahusishwa na mimba kuharibika katika wiki za mwanzo mwanzo tangu kutungwa kwake.

Hivyo kama umekuwa na bahati ya kupata ujauzito halafu haichukuwi muda zinatoka kuna uwezekano mkubwa una kiasi kidogo cha madini ya zinki kwenye mwili wako.

VITU HIVI USIVITUMIE ILI KUBORESHA AFYA YAKO YA MAYAI:

1. Vyakula vya viwandani
2. Mafuta yatokanayo na wanyama
3. Soda
4. Kaffeina – chai ya rangi, kahawa
5. Vilevi
6. Sukari

Kama utahitaji dawa hii kwa ajili ya kupevusha mayai ya uzazi niachie tu ujumbe WhatsApp +255714800175

Kama utanunua kutoka kwangu nitakuwa karibu na wewe kila siku mpaka nione umefanikiwa kutibu tatizo lako.

Napatikana live WhatsApp nyakati zote za mchana kila siku.

Jiunge na mimi na watu wengine zaidi ya 94000 kwenye ukurasa wangu wa facebook kwa kubonyeza hapa

Fadhili Paulo

Fadhili Paulo

Naitwa Fadhili Paulo, ni Tabibu wa Tiba asili. Ninayo ofisi yangu binafsi Jijini Dar Es Salaam. lakini nafanya pia kazi kwa njia ya mtandao. Ofisi yangu inaitwa TUMAINI HERBAL LIFE, Ipo Kibugumo Mji Mwema Kigamboni Kama unahitaji kuonana na mimi uso kwa uso weka miadi (appointment) kupitia WhatsApp +255714800175

0 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published.

WhatsApp WhatsApp +255714800175