Kuna watu hudhani ukiwa mnene au mwenye uzito mkubwa ndiyo kuwa na afya na ndiyo maana wengine wakikonda basi huchanganyikiwa kabisa.

Lakini uzito au unene uliozidi ni ugonjwa tena ugonjwa mubaya kabisa ambao unapaswa kuwa makini nao sana kwani ni chanzo cha magonjwa mengine mengi mwilini.

Kila mmoja anapaswa kuwa na uzito unaomstahili kulingana na urefu wake.

Tafiti zinaonesha watu wenye uzito kupita kiasi wana uwezakano mkubwa wa kupatwa na magonjwa mengine hatari kwa kiwango kikubwa zaidi tofauti na watu wembamba.

Magonjwa hatari unayoweza kupata kutokana na uzito wako kuwa mkubwa ni pamoja na yafuatayo:

1. Magonjwa ya moyo.
2. Shinikizo la juu la damu 
3. Kiharusi (Stroke)
4. Kisukari aina ya pili 
5. Baadhi ya aina za saratani
6. Ugumba
7. Msongo wa mawazo (Stress)
8. Matatizo ya mifupa
9. Maumivu ya mgongo
10. Kuishiwa nguvu za tendo la ndoa (kwa wanaume)

Jinsi Mlonge unavyotumika kupunguza uzito na unene

1. Mlonge huuongezea nguvu mfumo wa mmeng’enyo wa chakula

Nitaelezea uhusiano uliopo kati ya mfumo wako wa mmeng’enyo wa chakula na kuongezeka au kupungua kwa uzito wako. Mmeng’enyo wa chakula ni mfumo wa mwili unaotumika kutengeneza nguvu kwa kukichanganya chakula na oskijeni katika seli kwenye sehemu ya seli ijulikanayo kwa kitaalamu kama ‘mitochondrion’.

Muda wote mwili wako unafanya kazi ya kumeng’enya chakula hata unapokuwa usingizini.

Unaongezeka uzito wakati unapokula chakula zaidi na mfumo wa mmeng’enyo unapofanya kazi chini ya kiwango.

Baadhi ya watu wanaonekana kuwa na mfumo wa mmeng’enyo wa chakula wenye kasi zaidi na hivyo wanasaga chakula kwa haraka zaidi na hivyo wanaepuka kuongezeka uzito kirahisi kuliko wale wengine wenye mfumo wa mmeng’enyo wa chakula wa taratibu.

Kwahiyo utaweza tu kupunguza uzito ikiwa mfumo wako wa mmeng’enyo wa chakula unafanya kazi zaidi kuzidi kiasi cha chakula unachokula.

Hivyo ili uzito wako upunguwe inakulazimu ufanye mambo mawili ambayo ni ama unakula chakula kichache au ule chakula kingi huku ukifanya bidii kuchoma chakula zaidi kwa kuushughulisha mwili zaidi (mazoezi ya viungo).

Hilo linaweza kuwa rahisi si ndiyo ndugu msomaji?

Mti wa miujiza (miracle tree) ambao ni mti wa mlonge una kiasi kizuri cha mafuta mazuri yajulikanayo kama Omega-3 fatty acids ambayo kazi yake hasa kuuongezea kasi mfumo wa mmeng’enyo wa chakula ndani ya mwili.

Hii ndiyo utawasikia watu wakisema wanajisikia kuwa na nguvu nyingi wanapokuwa wanatumia mlonge.

Maana iliyopo hapa ni kwamba miili yao ipo kwenye kiwango cha juu kwenye umeng’enyaji wa chakula na hivyo kama matokeo yake wanapata kupungua uzito kirahisi zaidi.

Omega 3 husaidia huongeza msukumo wa damu kwenye mishipa wakati wa mazoezi na kusaidia kuhamasisha vimeng’enya vinavyohusika kuhamisha na kuweka mafuta katika sehemu yatakapoweza kutumika kutengeneza nguvu.

Umeona?

2. Mlonge huondoa hisia za njaa

Njia nyingine mlonge utakufanya upunguwe uzito ni kwa kukufanya ule chakula kichache kwakuwa mlonge utakufanya ujisikie umeshiba (unajiona upo full) kwa masaa mengi baada ya kuwa umeutumia na hivyo unakuwa huna njaa kubwa kama siku nyingine.

Na habari njema ni kuwa pamoja na kukuacha huna hamu ya kula bado unakuachia pia viinilishe vya kutosha ambavyo mwili wako unavihitaji kwa siku nzima. Mlonge una viinilishe vingi kuliko mti mwingine wowote chini ya jua ukiwa na viinilishe zaidi ya 92 ndani yake!

Mlonge una vitamini nyingi, madini, asidi amino, viondoa sumu tofauti tofauti 46 nk

Mwili wako utakuwa umepewa yote unayohitaji kwa kuwa umetumia mlonge hata kama unakula chakula kichache au husikii njaa ni sawa sababu yote unayohitaji kwa ajili ya afya unakuwa umepata tayari katika mlonge hasa ukitumia unga wa majani yake pia.

Hivyo siyo kwamba unakuwa umefunga, la hasha, hii inakufanya uepuke kula hovyo hovyo au kila mara hivyo mlonge unakufanya ubaki na adabu ukiheshimu mwili wako dhidi ya kula kila mara.

Hivyo mlonge unapunguza njaa, unakufanya ujisikie umeshiba muda mrefu na hivyo moja kwa moja utakula chakula kichache.

Hiyo ni njia nyingine mlonge unavyoweza kukusaidia kupunguza uzito na unene kupita kiasi.

3. Mlonge una kiasi kingi cha nyuzi nyuzi (faiba)

Kwa mjibu wa wikipedia, gramu 100 za unga wa mlonge zina nyuzi nyuzi gramu 3.2. Hivyo matumizi ya mara kwa mara ya mlonge yanakupa wewe kiasi unachohitaji cha nyuzi nyuzi ambacho mwisho wake hukusaidia kupunguza uzito

Kwa kawaida unahitaji gramu 38 za nyuzi nyuzi wa siku ili kusaidia kuwa na uzito ulio sawa.

Kile kinachokufanya ujisikie umeshiba kwa muda mrefu baada ya kutumia mlonge ni hii kuwa na nyuzi nyuzi ndani yake (fiber).

Ikiwa unatumia mbegu kupunguza unaruhisiwa kutumia zikiwa na ganda lake la nje ila kama unatumia kwa ajili ya magonjwa mengine zaidi ya kupunguza uzito basi umenye ganda la nje kabla ya kuzitumia.

4. Mlonge husaidia kuondoa sumu mwilini

Kuna mitishamba, vyakula na mbinu nyingi za kuondoa sumu ambazo zinasaidia vizuri tu kazi hii ya kuondoa sumu mwilini.

Nini sababu hasa ya kutaka kutoa sumu mwilini? Jibu ni kuwa inasaidia kuufanya mwili wako mpya tena na kwa sababu hiyo uzito unapata kupungua pia

Programu nyingi zinazotumika katika kuondoa sumu na hivyo kupunguza uzito haraka mara nyingi huondoa tu maji yaliyozidi mwilini huku ukiachwa na mafuta mwilini kwa sehemu kubwa labda mpaka kwa wiki kadhaa baadaye.

Hivyo usianze program za kupunguza sumu kwa lengo la kupunguza hasa uzito bali kama njia ya kuanza njia mpya ya kuishi yenye afya zaidi yaani kula zaidi matunda, samaki na matunda za maboga huku ukipunguza sana kula nyama

Mlonge hasa mbegu zake zinasaidia sana katika kazi ya kutoa sumu na kusafisha mwili wote kwa ujumla na hivyo kukuruhusu wewe upate viinilishe vyote mhimu kutoka katika chakula unachokula na hivyo kukusaidia wewe kupungua uzito katika huo mlolongo

Tumia na haitachukua muda mrefu kuona matokeo yake katika kuweka sawa uzito wa mwili wako.

Usitumie Mlonge hasa mbegu zake mfululizo kwa zaidi ya miezi mitatu hasa kama unatumia kila siku.

Kwa ajili hii ya kupunguza uzito ni vizuri zaidi kama utatumia mbegu zake kwa matokeo ya uhakika zaidi. Zinaweza kukuletea kuharisha kwa siku 2 au 3 za mwanzo ukianza kutumia lakini hiyo hali baaaye hutulia hivyo usishangae likikutokea hilo.

Namna ya kutumia mbegu za mlonge:

Pata unga wa mbegu za mlonge na utumie kijiko kidogo kimoja cha chai ndani ya juisi ya matunda uliyotengeneza mwenyewe nyumbani kikombe kimoja kutwa mara 1. Unaweza kuchanganya pia katika uji au hata mtindi.

*Mhimu: Mama mjamzito asitumie mbegu za mlonge

Mambo mhimu ya kufanya unapokuwa una tatizo la uzito au unene kupita kiasi:

1. Hakikisha unakunywa maji kila nusu saa kabla ya kula chakula
2. Fanya mazoezi hasa mazoezi ya kutembea kwa miguu mwendo kasi lisaa limoja mara 2 kwa siku kwa mwezi 1 mpaka miwili
3. Punguza vyakula vyenye wanga
4. Punguza vyakula vinavyopikwa katikati ya mafuta mengi kama vile zinavyopikwa chipsi au maandazi
5. Acha kabisa soda na juisi za viwandani
6. Usikae kwenye kiti au usikae tu kwa masaa mengi katika siku
7. Unaweza kufunga mara moja moja katika wiki

Kama unahitaji unga wa mbegu za mlonge tuwasiliane WhatsApp +255714800175

Tafadhari share post hii kwa ajili ya wengine

Naitwa Fadhili Paulo, ni Tabibu wa Tiba Asili na ni mTanzania.

Ofisi yangu inaitwa Victoria Home Remedy ipo Sigara Yombo Vituka Temeke Dar Es Salaam.

Jiunge na mimi na watu wengine zaidi ya 94000 kwenye ukurasa wangu wa facebook kwa kubonyeza hapa

(Visited 819 times, 1 visits today)

Last Updated on


2 Comments

Alex musotsi · December 12, 2018 at 4:22 am

How much and how can I get it.

    Fadhili Paulo · December 20, 2018 at 5:13 am

    Kama unahitaji unga wa mbegu za mlonge tuwasiliane WhatsApp +255714800175, Napatikana Victoria Home Remedy, ipo Buza Sigara Temeke Dar Es Salaam.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WhatsApp Chat na mimi kwenye WhatsApp