Dawa ya kutoa sumu mwilini

Published by Fadhili Paulo on

jinsi ya kutoa sumu mwilini

Dawa ya kutoa sumu mwilini

SUMU ni kitu chochote ambacho kinaweza kuingia mwilini na kusababisha mifumo ya mwili ishindwe kufanya kazi ipasavyo.

Unafikiria kuwa una afya njema, lakini haujisikii vyema. Unapuuza, unaona ni vitu vidogo vidogo.

Hivyo, haushughuliki kwenda hospitali au kwa wataalamu wa afya kwa ajili ya uchunguzi na matibabu.

Hatimaye tatizo linakuwa kubwa. Unafika hospitali unaambiwa una saratani, unapata mshtuko mkubwa! Unaambiwa chanzo cha ugonjwa hakifahamiki, ila unaelezwa chakula na mtindo wa maisha kwa ujumla ni sababu kubwa.

Hii ina maana kuna uwezekano umeingiza sumu nyingi mwilini. Kinga ni bora kuliko tiba. Kama ungeelewa mapema, ungejikinga na saratani.

Sizungumzii sumu za kung’atwa na nyoka, wala sizungumzii sumu zinazohitaji matibabu ya dharura.

Nazungumzia sumu ambazo zinatuua pole pole na kimya kimya bila ya sisi kujua wala kutambua chochote. Nazungumzia sumu ambazo kila kuchapo tuko kwenye mlango wa daktari.

Kila kuchapo afya zetu hizidi kuzorota zaidi. Hizi ni sumu ambazo ziko kwenye vyakula vyetu.

Ni sumu tunazozivuta katika hewa kila siku kutokana na mioshi ya magari, viwanda n.k.

Sumu ambazo zinaweza kutokana na madawa mbalimbali tunayojitibia afya zetu, sumu zinazotokana na vipodozi mbalimbali tunavyotumia kila siku kwa ajili ya urembo na kupendeza.

Tunapata sumu mwilini kwa sababu lazima tuvute hewa, hata kwa sekunde kadhaa tusipopata hewa ya oksijeni tunakufa.

Lakini tunavuta hewa iliyochafuliwa na mioshi ya viwanda na magari ambayo imetamalaki kila kona.

Hivyo lazima tufe polepole na kimya kimya!

Tunapata sumu mwilini kwa sababu lazima tule na tunywe. Lakini kwa bahati mbaya, vyakula vingi tunavyokula siyo salama, vimesheheni kemikali.

Tunapata sumu kwa sababu lazima tujipodoe, lazima tujipambe tupambike, na lazima tung’are tupendeze.

Kwa bahati mbaya sana, vipodozi vingi vimekuwa siyo vipodozi, ni vipopozi. Vimejaa kemikali ambazo huleta madhara mengi ya kiafya.

Tunapongeza mamlaka ya chakula na dawa, TFDA, kwa kuviteketeza baadhi ya vipodozi na kutoa orodha ya vipodozi visivyofaa, lakini hata hivyo juhudi kubwa lazima ifanyike.

Ishara zitakazokuonyesha mwili wako una sumu nyingi:

 • Uchovu sugu
 • Maumivu ya maungio
 • Msongamano puani
 • Kuumwa kichwa kila mara
 • Tumbo kujaa gesi
 • Kufunga choo au kupata choo kigumu
 • Kukosa utulivu
 • Matatizo mbalimbali ya ngozi ikiwemo chunusi
 • Pumzi mbaya
 • Mzunguko wa hedhi usio sawa
 • Kuishiwa nguvu
 • Kushindwa kupungua uzito
 • Kupenda kula kula kila mara
 • Kupatwa na ganzi sehemu mbalimbali mwilini

Kinachosababisha mwili kuwa na sumu au taka taka

Mwili unaweza kupatwa na sumu au takataka zisizohitajika na mwili kwa namna mbili, ama kupitia mazingira tunayoishi (viwanda, migodi nk) au kupitia vyakula na vinywaji ambavyo tunatumia kila siku.

Sumu au taka pia zinaweza kuingia mwilini kupitia dawa mbalimbali hasa za kizungu tunazotumia kujitibia magonjwa mbalimbali.

Mwili huzalisha hizi sumu au takataka (free radicals) kila mara kunapofanyika mmeng’enyo wa chakula mwilini mwako.

1. Kutokula matunda na mboga za majani

Matunda na mboga za majani ni vitu viwili mhimu sana ili kusafisha mwili wako na kukukinga dhidi ya sumu na taka taka mbalimbali.

Kama huna tabia ya kula matunda na mboga za majani kila siku ni wazi mwili wako utatengeneza sumu za kutosha.

2. Kula vyakula vya viwandani

Kama unataka kuepuka sumu au takataka nyingine kirahisi kuingia katika mwili wako basi pendelea zaidi kula vyakula vya asili vinavyopikwa nyumbani kuliko kula vya kwenye makopo au vya dukani au vya kwenye migahawa (fast foods).

3. Kutokunywa maji mengi kila siku

Sababu kubwa ya watu wengi kutengeneza sumu au taka mwilini mwao ni kutokunywa maji mengi kila siku. Maji ni uhai, bila kunywa maji mengi kila siku ni sawa na kwenda dukani bila hela mfukoni.

Haijalishi upo mazingira gani kama ni ya baridi au ni ya joto ni LAZIMA UNYWE MAJI YA KUTOSHA KILA SIKU IENDAYO KWA MUNGU.

Unahitaji maji glasi 8 mpaka 10 kila siku. Watu wengi wanahangaika namna ya kuondoa sumu kusafisha miili yao bila kujua kuwa maji pekee ya kunywa yanatosha kwa kazi hiyo.

Kumbuka asilimia 94 ya damu yako ni maji, asilimia 85 za ubongo wako ni maji, hivyo kama huna mazoea ya kupenda kunywa maji kila siku ni rahisi mwili wako kutengeneza sumu. .

4. Vinywaji vyenye kaffeina

Kama tayari imethibitika una sumu au takataka nyingi mwilini nakushauri uache kunywa chai ya rangi na kahawa.

Badala yake hamia kutumia chai yenye tangawizi au mdalasini au mchaichai.

Chai ya rangi na kahawa vina kaffeina ambayo kwanza huyasukuma maji nje ya mwili kwa haraka na kuuacha mwili bila kuwa na maji ya kutosha kwa ajili ya kazi zake.

Kaffeina pia ni madawa ya kulevya kundi la madawa yanayosisimua mwili (stimulants drugs).

5. Kutopata usingizi wa kutosha kila siku

Moja ya vitu vinaweza kukupelekea kuwa na sumu mwilini au takataka nyingi ni pamoja na kutokulala muda wa kutosha kila siku. Usingizi haukopwi na huwezi kuwa na ufanisi katika kazi zako kama hupati usingizi wa kutosha kila siku.

Usingizi siyo jambo la starehe tu, ni sehemu mhimu sana katika afya yako ya kila siku.

Bila kupata usingizi wa kutosha unaweza kuwa karibu na matatizo kama kuongezeka uzito, kushuka kwa kinga ya mwili na nguvu zako za mwili kwa ujumla zinaweza kushuka.

Unapopata muda wa kutosha wa kulala masaa 7 mpaka 8 kwa siku unaupa mwili wako nafasi ya kutosha ya kupumzika na kujiripea upya na hivyo ndivyo sumu na takataka nyingine zinavyoweza kukutoka kirahisi.

Ingia kulala mapema walau saa tatu usiku ingia kulala siyo unakaa unaangalia tamthiliya au mpira mpaka saa sita za usiku!

6. Mazingira tunayoishi

Kuna mazingira yanajulikana wazi kuwa ni vyanzo vya sumu mwilini. Maeneo ya migodi ya madini, maeneo yenye viwanda vingi, maduka yanayouza dawa za kilimo nk

Maeneo haya yanafaa kukaa mbali na makazi ya binadamu kwa usalama wa afya zetu.

7. Vyakula vilivyokobolewa

Ili kuwa na mwili msafi kabisa epuka kula mkate mweupe, sukari na vyakula vinavyopikwa katikati ya mafuta mengi kama vile chipsi, maandazi na vingine vyote vinavyochomwa katikati ya mafuta mengi.

Mkate upo mkate mweusi (brown bread), sukari ipo asali mbichi, vyakula vinavyopikwa katikati ya mafuta mengi unaweza kuamua kuwa unavioka (bake) au uvichemshe (boiling). Uchaguzi ni wako.

8. Mfadhaiko (stress)

Kile tayari unajuwa ni kuwa mfadhaiko au stress ni jambo baya kwa afya yako. Kile unatakiwa kujua kuanzia sasa ni kuwa ili kubaki na afya bora kabisa yenye TBS basi ukae mbali na stress.

Kama utaruhusu stress kutawala maisha yako basi ujuwe mwili wako hauwezi kufanya kazi zake vizuri ikiwemo ya kuondoa taka au sumu mbalimbali mwilini.

Stress peke yake inaweza kupelekea magonjwa mbalimbali mwilini zaidi ya 50. Unapokuwa na mfadhaiko mwili wako hauwezi kutoa taka nje kirahisi na kinga yako ya mwili inashuka matokeo yake unakuwa karibu na magonjwa mengine mengi.

Watu wengine wenye uelewa mdogo wakiwa na stress hukimbilia kutumia vilevi wakidhani zitapungua kumbe ndiyo wanazidi kuongeza tatizo bila kujua.

9. Dawa za kizungu

Dawa nyingi za hospitali huwa zina matokeo chanya (positive) na matokeo hasi (negative) pia ambayo ndiyo matokeo mabaya.

Kama unalazimika kutumia antibiotic kila mara au unameza dawa za kuondoa maumivu kila mara unaweza kuwa unaongeza sumu na taka mwilini bila kujua na bila sababu yoyote ya lazima.

Kuepuka hilo jaribu kutumia mitishamba au mimea ya asili kwa baadhi ya magonjwa ambayo si lazima uende hospitali. Siyo mafua tu mtu ameenda kuchoma sindano!

10. Vilevi

Moja ya vitu vinavyoweza kuleta sumu au taka mwilini moja kwa moja ni vilevi. Vilevi kama pombe, madawa ya kulevya, sigara, bangi na vinginevyo ni vitu vinavyopelekea mwili kuwa na taka moja kwa moja.

Namna pekee ya kuondoa sumu kutokana na vilevi ni kuviacha hivyo vilevi, ndiyo kuviacha.

Usitegemee asubuhi utumie dawa kuondoa sumu mwilini halafu jioni ukanywe pombe au ukavute sigara utegemee tu ile dawa uliyotumia asubuhi kwamba itafanya kazi, hapana unajidanganya, dawa ni kuacha vilevi moja kwa moja.

Vingine vya kuacha kama tayari imegundulika una sumu nyingi mwilini ni pamoja na vinywaji baridi vyote, juisi zote za dukani, chai ya rangi na kahawa.

Dawa ya kutoa sumu mwilini

Dawa ya kutoa sumu mwilini

.

Dawa ya kutoa sumu mwili > Unga wa majani ya mlonge.

Unga wa majani ya mlonge ndiyo dawa pekee ya asili ya uhakika ya kuondoa sumu mwilini.

Mti wa mlonge umekuwa ukijulikana kama mti wa miujuza (miracle tree) kutokana na kuwa na uwezo mkubwa wa kutibu maradhi mengi mbalimbali mwilini kuanzia kwenye kufunga choo mpaka kwenye saratani.

Kwa sababu hiyo Mlonge unakuja kuwa msaada mkubwa kwenye ogani yetu kubwa kuliko zote katika kazi za kusafisha mwilini ambayo ni INI.

Kwa kawaida Ini letu ndiyo ogani inayohusika na utoaji sumu na taka mbalimbali mwilini.

Ini huchuja kila kinachouingia mwili ili kuchambua na kuondoa vitu visivyohitajika na mwili yaani sumu na taka mbalimbali.

Ini lipo kwenye mawasiliano wakati wote na ogani zingine za mwili hasa zile zinazohusika na umeng’enyaji wa chakula.

Ini zuri lenye afya husaidia kuweka sawa mzunguko na mgawanyo wa damu mwilini.

Ini huihifadhi damu ili kwamba liweze kuupa mwili damu mpya na safi yenye afya wakati mwili unapokuwa umepatwa na majeraha na kuripea au kuziondoa seli za damu zilizodhurika ambazo zinapita kupitia Ini.

Ini ndiyo linahusika na kuganda kwa damu kazi ambayo ni mhimu sana inayosaidia miili yetu kujitibu tunapopatwa na majeraha.

Ini husaidia pia kuondoa damu sukari iliyozidi katika damu na kufanya kazi kwa karibu na kongosho kwa kudhibiti matendo na kazi za insulin.

Ini huzalisha nyongo ambayo kisha huhifadhiwa katika kibofu nyongo (gall bladder). Nyongo husaidia mmeng’enyo wa chakula na uondoaji wa sumu au taka mwilini.

Mlonge unalisaidia ini katika kazi zake

Yote katika yote Ini ni ogani mhimu sana kwa kazi za mwili kwa ujumla. Jambo lolote linaloathiri utendaji kazi wa Ini linaweza kusababisha shida nyingi mwilini ikiwemo matatizo kwenye mfumo wa mmeng’enyo wa chakula, homoni, kudumaa kwa ubongo na hata kudhuru afya yako ya akili kwa pamoja.

Kwa bahati nzuri mlonge unaweza kulirudishia Ini afya yake na hivyo kuliwezesha kufany akazi kwa kiwango chake cha juu kabisa katika kuondoa sumu na taka mbalimbali mwilini kwa njia 3 zifuatazo:

1. Mlonge unapunguza uharibifu uliojitokeza katika ini

Tafiti mbalimbali zimeonyesha kuwa mlonge unasaidia kutibu na kuzuia madhara katika Ini.

Tafiti kadhaa zimeonyesha mlonge kuwa na uwezo wa kupunguza madhara ambayo tayari yamejitokeza katika Ini.

Mlonge unao uwezo wa kuzuia Ini dhidi ya ugonjwa wa Ini (hepatitis) na tafiti zinahitimisha kwa pamoja kuwa unga wa majani ya mlonge husaidia pia kuzuia uharibifu katika Ini.

2. Mlonge Unavirudisha Vimeng’enya vya ini

Mlonge unasaidia kuvirudisha vimeng’enya (enzymes) kwenye Ini lililodhurika.

Ini ni ogani katika mwili inayohusika na kusafisha damu, uzalishaji wa nyongo, kumeng’enya mafuta na umeng’enywaji wa jumla wa viinilishe katika vyakula tunavyokula.

Kazi hizo zote za Ini zinawezekana kwa msaada wa vimeng’enya vyake. Inapotokea Ini lina uchovu au limezidiwa na wingi wa kazi vimeng’enya vyake vyaweza kupungua na hivyo kulifanya Ini kutokuwa na msaada wowote katika kazi ya kutoa sumu na taka mwilini.

Mlonge unasaidia kuvirudisha vimeng’enya (enzymes) vyote kwenye Ini katika hali yake ya kawaida na kufanya kazi kama vinavyopaswa kuwa vinafanya katika ini zuri lenye afya.

3. Mlonge unasaidia kuondoa msongo wa mawazo (stress)

Nimeandika pale juu kwamba moja ya vitu vinavyosababisha sumu au taka taka mwilini ni msongo wa mawazo yaani stress.

Tafiti nyingi zimekuwa zikionyesha kuwa moja ya kisababishi kikubwa cha msongo wa mawazo (stress) ni kukosekana kwa viinilishe mhimu katika chakula.

Kukosekana huku kwa viinilishe mhimu katika chakula kunasababisha usawa usio sawa wa homoni mwilini (hormonal imbalance) jambo linalopelekea kutokea kwa msongo wa mawazo.

Msongo wa mawazo umeendelea kuwa tatizo kubwa kwa watu miaka ya sasa na wengi wao wakipatwa na tatizo la kukosa pia usingizi.

Hata hivyo, tatizo hilo linaweza kutibika kirahisi kwa kuongeza viinilishe sahihi kwenye mwili wako

Kwa bahati nzuri unga wa majani ya mlonge una viinilishe vingi kuliko mmea au mtishamba wowote chini ya jua ukiwa na viinilishe 92 ndani yake!

Unga wa majani ya mlonge una kiasi cha kutosha cha vitamini A, B, C, E, Potasiamu, Kalsiamu na viinilishe vingine vingi.

Kwahiyo kama utaweka mazoea ya kutumia mlonge kila siku itakuwa ni vigumu kwako kupata tatizo la msongo wa mawazo huku ukipata faida nyingine nyingi za mti huu wa ajabu

Kiasi kingi cha madini ya magnesiamu kwenye mlonge ni mhimu kutibu matatizo ya mifupa kwa wamama wanaofika ukomo wa siku zao (miaka 40 hivi kwenda juu).

Magnesiamu madini yapatikanayo kwenye mlonge ni dawa maarufu ya kutuliza akili (Tranquillizer) na kutibu matatizo kama msongo wa mawazo, sononeko, huzuni, hamaki na matatizo mengine ya mvurugiko wa akili.

Hii ni orodha ya viondoa sumu (antioxidants) 46 na zaidi vipatikanavyo katika mlonge:

Antioxidants (9, 11, 12, 13, 14, 15)

 1. β-carotene
 2. calcium
 3. potassium
 4. quercetin
 5. chlorogenic acid
 6. hydroxyanisole (BHA)
 7. butylated hydroxytoluene (BHT)
 8. tertiary-butylhydroquinones
 9. propyl gallate
 10. vitamin E (tocopherols)
 11. ascorbic acid (vitamin C)
 12. glucose oxidase
 13. reduced glutathione
 14. citric acid
 15. polyphospages
 16. aminopolycarboxylic acids
 17. vanillin
 18. moringine
 19. strophantidin
 20. 4-(α-l-rhamnosyloxy)
 21. benzyl isothiocyanate
 22. 4-(4’-O-acetyl-α-l-rhamnosyloxy)
 23. benzyl isothioyanate
 24. catechin
 25. 4-(β-d-glucopyranosyl-1→4-α-l-rhamnopyranosyloxy)
 26. benzyl thiocarboxamide
 27. epicatechin
 28. 4-O-(α-l-rhamnosyloxy)
 29. benzyl glucosinolate
 30. 4-(α-l-rhamnopyranosyloxy)-benzylglucosinolate
 31. Kaempferol
 32. Niazimicin
 33. 4-(α-l-rhamnosyloxy)
 34. benzyl acetonitrile (niazirin)
 35. O-ethyl-4-(α-l-rhamnosyloxy)
 36. benzyl carmate
 37. Gallic acid
 38. Glycerol-1-1-(9-octadecanoate)
 39. p-Coumaric acid
 40. 3-O-(6’-O-oleoyl-β-d-glucopyranosyl)-β-sitosterol
 41. Ferulic acid
 42. β-sitosterol-3-O-β-d-glucopyranoside
 43. Caffeic acid
 44. 3-Hydroxy-4-(α-l-rhamnopyranosyloxy)
 45. benzyl glucosinolate
 46. Protocatechuic acid
 47. 4-(2/3/4′-O-acetyl-α-l-rhamnopyranosyloxy)
 48. benzyl glucosinolate
 49. cinnamic acid
 50. glucosinalbin
 51. ellagic acid
 52. glucoraphanin
 53. glucoiber

Mlonge unasafisha mwili wako wote, unasafisha ini, figo, moyo, macho, unaimarisha meno, ngozi na nywele.

Mlonge una Kalsiamu mara 17 zaidi ya ile ya maziwa ya ng’ombe. Mlonge UNA MADINI YA CHUMA MARA 25 ZAIDI YA ILE ILIYOMO KWENYE SPINACHI

Changanya matunda yote na mboga za majani zote bado viinilishe vyake kwa pamoja haviwezi kuvifikia vile vilivyomo kwenye mlonge!

Ni kusema mtu aliyekula matunda na mboga za majani zote bado hatakuwa na afya bora kama yule atakayetumia mlonge tu.

Kwahiyo tunaweza kuhitimisha kuwa unga wa majani ya mlonge ni dawa nzuri na ya uhakika kwa kuondoa sumu mwilini na kulinda afya ya INI kwa ujumla.

*Usitumie dawa hii bila uangallizi wa karibu wa Tabibu.

Kama unahitaji unga wa majani ya mlonge kwa ajili ya kutoa sumu mwilini niachie ujumbe WhatsApp +255714800175

Unga wangu wa majani ya mlonge ni mzuri na naweza kusema pasipo na hofu kuwa huwezi kupata sehemu nyingine wenye ubora unaokaribia na wangu. Ninauandaa kwa umakini mkubwa ili ubaki na viinilishe vyake na ni wa kijani kweli kweli.

Uwe makini na yafuatayo kuhusu mlonge;

 1. Siyo kila mlonge ni dawa. Kuna aina 13 tofauti za mlonge na ni mlonge mmoja tu ndiyo hutumika kama dawa nao hujulikana kwa kiingereza kama ‘Moringa oleifera’. Aina nyingine 12 zote zilizobaki za milonge haitumiki kama dawa.
 2. Ili mlonge ufae kama dawa lazima uvunwe asubuhi tu mapema na uanikwe ndani ya nyumba au sehemu yoyote yenye kivuli kwa siku 4 mpaka 5. Mlonge hauanikwi juani.
 3. Ni lazima uwe una rangi ya kijani kweli kweli ndipo unakuwa na viinilishe vyake vyote vya kutosha. Tofauti na hapo kuna uwezekano mlonge huo ulianikwa juani na haufai tena kutumika kama dawa.

Hivyo nunua mlonge toka kwa mtu unayemfahamu ambaye una uhakika naye na anajishughulisha hasa na mambo ya tiba asili. Usinunuwe tu popote, jali afya yako.

Wakati unaendelea kutumia mlonge hakikisha unabaki kwenye chombo na umefungwa vizuri bila kupitisha hewa wakati wote wa matumizi. Usiuache kwenye chombo cha wazi.

Na ukinunua dawa hii kutoka kwangu na siyo sehemu nyingine utapata faida hizi nne zifuatazo:

 1. Utakuwa rafiki yangu
 2. Nitahakikisha tatizo lako linaisha na halijirudii tena
 3. Nitakupa maelezo zaidi kuhusu matumizi kulingana na umri na uzito wako
 4. Nitawajibika kwa lolote linaloweza kukutokea wakati unaendelea kutumia dawa
 5. Napatikana WhatsApp nyakati zote za mchana na unaweza kuchat na mimi mwenyewe mubashara (live) toka popote ulipo huhitaji kuonana na sekretari au msaidizi wangu kwanza.

Mjulishe rafiki yako kwenye twitter naye asome post hii kwa kubonyeza ujumbe ufuatao:

Dawa ya kutoa sumu mwilini Click To Tweet

Tafadhali SHARE post hii kwa ajili ya wengine uwapendao.

Fadhili Paulo
Imesomwa mara 2,589

Fadhili Paulo

Naitwa Fadhili Paulo, ni Tabibu wa Tiba asili. Ofisi yangu inaitwa TUMAINI ALL NATURAL STORE, ipo Mwanagati Kitunda Ilala Dar Es Salaam. Kama unahitaji kuonana na mimi uso kwa uso weka miadi (appointment) kwa kubonyeza HAPA Pia napenda kukujulisha kuwa sina wakala au tawi mahali popote duniani.

10 Comments

Zawadi Yakotuu · 02/25/2020 at 8:35 am

Najaribu kukutafuta kwenye laini zako sikupati,nahitaji huo unga wa mlonge mwili wangu sumu tupu za hedex.

  Fadhili Paulo · 02/26/2020 at 6:18 am

  Kama unahitaji unga wa majani ya mlonge niachie ujumbe WhatsApp +255714800175

  Fadhili Paulo · 02/26/2020 at 6:18 am

  Sijaandika popote kwamba nipigie simu

Tulizo Owen · 02/29/2020 at 6:43 am

Naomba Kujua kama mbegu za mlonge zinafanya kazi Sawa na majani yake mlonge

  Fadhili Paulo · 02/29/2020 at 6:47 am

  Hapana hazifanyi kazi sawa

julius · 03/29/2020 at 10:35 am

nataka kupunguza kitambi nipe formula

  Fadhili Paulo · 03/30/2020 at 2:58 am

  Bonyeza HAPA

Arnold Ngwira · 10/17/2020 at 9:39 pm

Habari, mm naishi Tabora nilikwenda Mwanza kuna duka moja linauza unga wa mizizi ya mlonge, nayo mizizi hiyo inatibu Kama ilivyo majani?

  Fadhili Paulo · 10/20/2020 at 12:35 pm

  Bila shaka hukununua kwangu, ningekushauri umuulize huyo aliyekuuzia bidhaa maswali haya maana ulimlipa kabisa hela

Arnold Ngwira · 10/17/2020 at 9:42 pm

Unga wa mizizi ya mlonge Ina kazi gani?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WhatsApp WhatsApp +255714800175