Homoni zina mchango mkubwa katika afya kwa ujumla katika mwili wa mwanamke hasa linapokuja suala la uzazi. Mara nyingi usawa usio sawa wa homoni husababishwa na mabadiliko katika homoni ya ‘estrogen’.

Mabadiliko haya mara nyingi hutokea wakati wa kuvunja ungo, wakati wa hedhi, wakati wa ujauzito na wakati wa ukomo wa hedhi (menopause).

Vitu vingine vinavyopelekea mabadiliko ya homoni ni pamoja na:

 1. Kuongezeka umri,
 2. Lishe duni,
 3. Kutokujishughulisha na mazoezi,
 4. Kupungua kwa ogani ya adreno,
 5. Mfadhaiko au stress,
 6. Kukosa usingizi,
 7. Dawa za uzazi wa mpango,
 8. Sumu na kemikali mbalimbali nk.

Dalili zitakazokuonyesha homoni zako hazipo sawa ni pamoja na:

1. Kuwa na tabia ya hamaki (kukosa utulivu)
2. Uchovu sugu
3. Kuongezeka uzito
4. Kupungua kwa nywele
5. Maumivu ya kichwa ya mara kwa mara
6. Kukosa hamu ya tendo la ndoa
7. Chunusi
8. Kuwa na hamu na vyakula au vinywaji vya viwandani kila mara
9. Kushindwa kushika ujauzito
10. Kutokujisikia vizuri kila mara bila sababu maalumu
11. Kukosa usingizi
12. Hasira zisizo na sababu maalumu nk

Zipo dawa za asili zinazoweza kukusaidia kurekebisha na hatimaye kuweka sawa usawa wa homoni mwilini mwako.

Ni mhimu uonane na daktari kabla kwa uchunguzi, vipimo na ushauri zaidi kabla ya kuamua kutumia dawa hasa kama una matatizo kama ya uvimbe katika kizazi, saratani ya matiti, saratani ya kizazi au una saratani katika mirija ya uzazi.

Dawa ya kuweka sawa homoni > Mafuta ya Mbegu za Uwatu

Dawa ya kuweka sawa homoni
Mafuta ya uwatu

Madaktari wengi wa tiba asili duniani hushauri kutumia uwatu (kwa Kiingereza huitwa ‘fenugreeek’) kwa ajili ya kuongeza maziwa kwa mama anayenyonyesha.

Uwatu hutumika pia kama dawa ya asili ya kuongeza ukubwa wa matiti (natural breast enlargement).

Mafuta ya Mbegu za Uwatu husaidia umeng’enywaji wa sukari mwilini na hivyo kuwa msaada mkubwa kwa watu wanaosumbuliwa na ugonjwa wa kisukari na uzito kupita kiasi (obesity).

Matumizi: Kunywa kijiko kidogo kimoja cha Mafuta ya Mbegu za Uwatu baada ya chakula. Fanya hivi kutwa mara 2 kwa mwezi mmoja mpaka miwili.

Unaweza kuongeza asali kidogo kupata radha. Unaweza kutumia pia ndani ya maziwa ya moto hasa kama huna vidonda vya tumbo au kisukari.

MAMBO YA MHIMU KUZINGATIA:

Pamoja na dawa, zingatia haya yafuatayo kwa matokeo mazuri zaidi:

• Kula parachichi 1 kila siku
• Tumia vyakula asili zaidi kuliko vya kwenye makopo na migahawani (fast foods)
• Tumia vyakula vyenye nyuzinyuzi (fiber) nyingi kwenye chakula chako
• Epuka kahawa, chai ya rangi, soda nyeusi na vinywaji vingine vyote vyenye kafeina ndani yake
• Achana na msongo wa mawazo (stress) na upate usingizi wa kutosha kila siku
• Usitumie dawa za uzazi wa mpango kama unahitaji kuweka sawa homoni zako
• Epuka vilevi vyote
• Kunywa maji mengi kila siku lita 2 hadi 3
• Usitumie vyakula vya moto kwenye vyombo vya plastiki

Kama unahitaji dawa ya kuweka sawa homoni niachie ujumbe WhatsApp +255714800175

Kama una swali au unahitaji ushauri uliza hapo kwenye comment nitakujibu.

Nisaidie ku-SHARE post hii kwa ajili ya rafiki zako wengine

Naitwa Fadhili Paulo, ni Tabibu wa Tiba Asili na ni mTanzania.

Ofisi yangu inaitwa Victoria Home Remedy ipo Sigara Yombo Vituka Temeke Dar Es Salaam.

Jiunge na mimi na watu wengine zaidi ya 94000 kwenye ukurasa wangu wa facebook kwa kubonyeza hapa

Imehaririwa mara ya mwisho

Niulize swali nikujibu


2 Comments

we rest Mosille · December 10, 2018 at 9:55 am

Nina tatizo la hormoneinbalance,utanisaidiaje

  Fadhili Paulo · December 10, 2018 at 5:18 pm

  Pole sana Mpendwa. Tuwasiliane WhatsApp +255714800175

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WhatsApp Chat na mimi kwenye WhatsApp